Subscribe:

Monday, November 30, 2009

Tumekuwa Watu Wa Ovyo Ovyo!




Sanamu hiyo ya mzee anayepiga ngoma inayotoa maji ( sasa haitoi) nimeiona tangu nikiwa chini ya miaka mitano kiumri. Iko kwenye bustani ya Mnazi Mmoja wilyani Ilala. Nilipita mahali hapo jioni ya leo, pamenikumbusha utotoni. Ndio, ni enzi hizo ambapo wazazi wetu walikuja mahali hapo kupumzika nyakati za jioni na sisi watoto wao. Leo mahali hapo pamefungwa, watu wa Darisalama hawaruhusiwi kuingia hapo kujipumzisha. Muhusika hapo ameniambia wakiwaruhusu watu, basi huchafua eneo hilo hata kwa haja ndogo na kubwa! Kuna choo cha public mahali hapo, lakini ni cha kulipia.

Kwanini tunashindwa kuwa na taratibu zitakazorudisha utamaduni wa watu kujipumzisha bustanini kama ilivyo kwa jirani zetu wa Kenya pale Nairobi? Nahofia kuna watoto wa kizazi cha sasa ambao hawaelewi hata bustani ya kupumzikia ina maana gani kwao. Jamani, nahofia hata baadhi ya viongozi wakiwamo baadhi ya waheshimiwa madiwani wa jiji hawaelewi umuhimu wa bustani. Ndio, maana kuna kiroja kimetokea mjini na hakuna anayelalamika au kuandika gazetini. Pale viwanja vya Mnazi Mmoja siku hizi wanakodisha kwa ajili ya shughuli za harusi binafsi! Ndio, kwenye bustani ya umma.
Kuna wajanja wamejitengenezea kamradi kao.

Watu wa Darisalama lazima waamke na kukataa ujinga huu. Itakumbukwa miaka ya 90 enzi za Meya Kitwana Kondo kuna mfanyabiashara kwa jina la Baghdad alipewa ruhusa na jiji ajenge jengo la ghrofa la biashara katika bustani hiyo na chini kuwe na maduka yanayozunguka bustani. Basi, mfanyabiashara yule akazungushia mabati bustani ile tayari kwa ujenzi. Watu wa Darisalama walikataa ujinga ule, wakagawana mabati yale. Baadae Serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ikapiga 'stop' ujenzi huo. Walichopigania watu wa Darisalama wakati ule ilikuwa ni haki yao ya kutumia viwanja hivyo kwa mapumziko. Kinachotokea sasa hakina tofauti sana na cha miaka ile ya 90. Viwanja vya umma vilivyotengwa kama bustani ya kupumzikia kwa umma vinabinaifsishwa kiholela. Kamwe, watu wa Darisalama na Watanzania kwa ujumla hatutakubali kuchungulia kwenye matundu ya ukuta , harusi na shughuli binafsi kwenye viwanja vya umma, tena vya kupumzikia. Wahusika wabadili utaratibu huu wa sasa, wavirudishe viwanja hivi vya umma vya kupumzikia kwa wenye navyo, wananchi. Kumbi za kufanyia sherehe binafsi ziko tele mjini!
Reactions::

Utalii Wa Ndani



Mikumi National Park, Jumamosi ya juzi.
Reactions::

Soko Mjinga



Kisutu, leo alasiri.
Reactions::

Mtaa Wa Livingstone



Kariakoo, leo jioni.
Reactions::

Mnazi Mmoja



Leo saa kumi na mbili jioni.
Reactions::

Walikuja Kwa Mafungu, Wameondoka Kwa Mafungu !



Wageni kutoka Sweden, wameondoka jana asubuhi. Wamefurahia sana ziara yao ya juma moja.
Reactions::

I & I !



Kigamboni, Jumapili wiki iliyopita.
Reactions::

Maelezo Mafupi



Bw. Jacob Diaz, Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo Ya Wananchi cha Anaotoglo Cha Dar es Salaam, akitoa maelezo kuhusiana na chuo hicho na shughuli zake kwa ujumbe kutoka Sweden uliotembelea chuo hicho juma la jana. Chuo hicho kinatoa mafunzo kwa vijana wenye ulemavu ikiwamo wenye mtindio wa ubongo.
Reactions::

Wanafunzi Darasani: Anaoutoglo FDC




Mnazi Mmoja Dar, juma la jana.
Reactions::

FaceHook!


facebook t-shirts zinapatikana kwa slogan mbalimbali....wahi yako mapema!!

PRICE:15.000 TSH
COLOR: BLU, BLACK, WHITE AND GREY
SIZE: L, M,S AND FREE SIZE
LOCATION: MAYFAIR PLAZA

HIGH QUALITY

CONTACT: 0784670105 or 784670106

Cheers,

Hugo
Reactions::

Uhuru Day Finland

Reactions::

Mayasa Hamad





Course :
Masters of Arts in Diplomacy, Law and
Global change
Chuo: Coventry University, United Kingdom,
Coventry
Reactions::

Sunday, November 29, 2009

Saturday, November 28, 2009

Nimewasili Tena Dar Salama Alasiri Hii

Nimeianza safari yangu kutoka Iringa alfajiri ya leo nikiwa na wageni kutoka Sweden. Dar ni ile ile, joto kali lakini Eid El Hajj imeifanya iwe tulivu hususan barabarani, hakuna msongamano wa magari. Nina picha kadhaa za njiani, nikipata muda nitaziingiza usiku huu au kesho alfajiri, inategemea na mtandao pia!
Reactions::

Eid El Hajj Njema!



Leo ni Eid El Hajj. Natawakia Waislamu na msio Waislamu, Eid El Hajj yenye furaha, amani na upendo.
Maggid
Reactions::

Maarifa Ni Nini?



Ni kile kilichobaki katika kumbukumbu zako baada ya kusahau vyote ulivyotafuna kichwani kwako. Je, wanazuoni na msio wanazuoni maarifa kwenu ni nini?
Reactions::

Heshima Mbele Kwa Mnyama Wa Taifa



Ukimgonga huyu .....
Reactions::

Friday, November 27, 2009

Porini Hutakiwi Kujipeleka Mbele Mbele!




Unaweza kuwa wa kwanza kudakwa na mamba au mnyama mwingine wa hatari. Na ukiwa nyuma sana ya wenzako, unaweza kunyofolewa na mamba au mnyama mwingine wa hatari. Chunga sana pia sehemu zilizo karibu na maji wakati wa jua kali, husogelewa na wanyama wengi. Unatakiwa kuwa makini muda wote, na ndio maana ya kulipa pori heshima yake.
Reactions::

Mkao Wa Kuwinda!




Jamaa si tu ana kucha kali, ana mawe pia! Simba wa Mikumi. Jumatano asubuhi tuliwaona kwa karibu wakiwa watatu na katika mkao wa kuwinda.
Reactions::

..... Filamu Inaendelea!






Simba Wa Mikumi
Reactions::

Tafuta Tofauti!

Reactions::

Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania



Kushoto ni Bw. Stellan Arvidsson wa Shirika la Misaada la nchini Sweden ( SIDA) na Bw. Reuben wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.
Reactions::

Mazungumzo Ya Kikazi



Kati ya uongozi wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania na ujumbe kutoka Chuo Kikuu Cha Linkoping. Mazungumzo hayo ya saa moja na nusu yalifanyika siku ya Jumanne ya juma hili. Pichani: Kutoka kushoto ni Profesa Bisanda, Dr. Mushi, Dr. Cornelia Muganda, Kiki, Stellan, Johan na Eva Marie.
Reactions::

Profesa Bisanda



Deputy Vice Chancellor ( Academics) Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania
Reactions::

Mwalimu Wangu Nilipokuwa Linkoping University



Sweden, enzi hizo. Anaitwa Johan A. Shahada yangu ya Ualimu niliipatia Chuo Kikuu Cha Linkoping cha nchini Sweden.
Reactions::

Hata Mbuyu Ulianza Kama Mchicha!



Dr. Asha Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Reactions::

Athumani Mauya



Mkuu wa Idara inayohusika na mafunzo ya masafa ( Distance Education) Taasisi ya Elimu Ya Watu Wazima Dar akiongea na wageni kutoka Chuo Kikuu cha Linkoping ofisini kwake hivi karibuni.
Reactions::

Hapo Vipi?



Maegesho ya gari la Meya wa Jiji la Dar es Salaam
Reactions::

Je, Ni Vibaya Kwa Mwanammke Kumtongoza Mwanamme?

deselectBloggerImageGracefully();} catch(e) {}" href="http://2.bp.blogspot.com/_1fXMXYztr0w/Sw-zuiD-MNI/AAAAAAAAVTs/VEP2ORSjHjo/s1600/1.jpg">

Je, ni vibaya kwa mwanammke kumtongoza mwanamme?
- Katika mila na tamaduni zetu inachukuliwa si uanauke kwa mwanammke kuwa wa kwanza kuchukua hatua ya kumtongoza mwanamme. Na mwanamme anadhani anatarajiwa ( dhana potofu) kuwa awe ‘ simba wa kumrarua’ mwanamke. Inakuwaje basi, pale mwananmke anapomtamani mwanamme kimapenzi na mwanamme asielewe kwa haraka kama amependwa? Ni vibaya kwa mwanamke kuanza kumtongoza mwanamme? Fuatili pia mada hii kwenye; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Profesa Mbele: Utamaduni Na Utandawazi



Tangu mwaka jana, nimekuwa naendesha warsha hapa Tanzania kuhusu utamaduni na utandawazi. Mwaka jana nilifanya hivyo Arusha, na mwaka huu nimeendesha warsha Tanga na Dar es Salaam. Warsha hizi zimehudhuriwa na watu kutoka Tanzania, Kenya, Cameroon, Uingereza, Sweden, na Marekani. Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Saundi Traki!

salam kaka

Pole na pilika na hongera kwa kazi nzuri unaoifanya.

Kwa niaba ya timu nzima ya £ovely Gamble tunapenda kuwaletea habari njema kuwa soundtrack ya movie £ovely gamble starring Steve kanumba iko tayari na inapatikana kwenye hii link chini.Movie itakuwa tayari soon. Wadau kaeni mkao wa kula

http://www.youtube.com/watch?v=A2qD_7G8a4o

Naomba msaada wako kuiweka kwenye blog yako.

Asante sana na Mungu akubariki.


Frank Eyembe
CEO Urban Pulse Media
Reactions::

Mambo Ya Viriyala Haya!


Reactions::

Mapacha Wanne

Reactions::

Sweet Easy

Reactions::

Thursday, November 26, 2009

Elimu ya Kijijini




Mara kwa mara nakumbuka elimu niliyopata kijijini, kabla ya kuanza shule. Wengi wetu tulipitia njia hiyo. Ni elimu gani hiyo? Tangu utotoni, tulipata maelekezo kutoka kwa wazazi kuhusu mambo mbali mbali, kufuatana na umri, kuanzia namna ya kuvaa hadi namna ya kula kwa adabu na kuwasalimia watu.
Baadaye wavulana tulijifunza kuchunga mbuzi na ng’ombe, na kutandika nyasi kwenye zizi la ng’ommbe, na kukamua maziwa. Wasichana walifundishwa kazi za jikoni na kulea watoto..Soma zaidi http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Kilimanjaro Stars Yakabidhiwa Bendera


Naibu waziri wa Ulinzi, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia) akikunjua bendera ya taifa kabla ya kumkabidhi nahodha wa timu ya taifa ya bara 'Kilimanjaro stars;, Salum Sued( pili shoto) wakati wa kuiaga timu hiyo leo ofisi za TFF tayari kwa kushiriki michuano ya chalenji Kenya kuanzia Nov.28. shoto ni kocha Marcio Maximo, Makamu wa Rais wa TFF Mh. Nyamlani na katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela
Reactions::

Kipa Mpya wa Taifa Stars Anayecheza Msumbiji


Huyu ndiye kipa mpya wa timu ya taifa ya bara a.k.a Kilimanjaro Stars Mohamed Mwalami anayechezea klabu ya Ferroviaro ya Maputo, Msumbiji. Anachukua nafasi ya kipa Shaaban Dihile ambaye ametemwa. Kipa mwingine ni Shaaban Kado wa Mtibwa Sugar. Kwa habari kamili ya kikosi kinachoondoka asubuhi hii kuelekea Kenya kwenye michuano ya Chalenji inayoanza Jumamosi.
Reactions::

MOTO WATEKETEZA MTAA IGUNGA.




Janga kubwa la moto limeukumba moja kati ya mitaa maarufu na wenye wakaazi wengi mjini hapa, {Mtaa wa Line Polisi}, karibu kabisa na kituo cha polisi cha wilaya na kuteketeza nyumba zaidi ya tatu na kuua mtu mmoja mtaani hapa hivi karibuni.
Wakielezea tukio hilo..soma zaidi http//www.kwanzajamii.com
Reactions::