Subscribe:

Thursday, December 31, 2009

HERI YA MWAKA MPYA WA 2010!



Wanakijiji Wenzangu,

KWA mara nyingine tena, natuma salamu zangu hizi za kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya wa 2010 nikiwa hapa Bagamoyo. Tofauti na mwaka unaomalizika, salamu zangu za Mwaka Mpya wa 2010 nazituma katika hali ya huzuni. Watanzania, katika siku hii ya mwisho ya mwaka, tumeondokewa na mtu muhimu sana katika historia yetu, Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Atabaki kuwa kiongozi wa kupigiwa mfano, aliishi kama alivyohubiri. Historia ya nchi haitaandikwa ikakamilika bila kutajwa kwa mchango wa Mzee Kawawa. Vivyo hivyo, historia ya TANU na CCM haitaandikwa na kukamilika bila kutajwa kwa mchango wa Mzee Kawawa. Hata historia ya filamu na mpira wa miguu katika nchi hii haitaandikwa na kukamilika bila kutajwa kwa mchango wa Mzee Kawawa. Atakumbukwa daima.

Vinginevyo, mwaka unaoisha umekuwa wa matukio mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.Kijiji chetu hiki kimebaki kuwa chachu ya mijadala yenye kulenga kwenye kulinda maslahi mapana ya nchi yetu.
Mijadala mingi humu kijijini imekuwa yenye siha. Kwa baadhi yetu imekuwa ni darasa tosha la kujichotea maarifa mbalimbali. Na tuendelee kukifanya kijiji hiki kuwa chachu ya mijadala hata mwaka ujao wa 2010.

Nawatakia Heri Na Fanaka Kwa Mwaka wa 2010.

Maggid,

Bagamoyo. ( Pichani ni Bagamoyo jioni hii)
Reactions::

Kumbukumbu Ya Simba Wa Vita Katika Picha: Marehemu Mzee Wetu Rashid Mfaume Kawawa




Taarifa za kifo chake zimewashtua wengi. Zimesambaa kwa haraka na kuwa gumzo mitaani. Wengi wanaisubiri kwa hamu usiku huu, hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Katika salamu zake za mwaka mpya, Rais Kikwete anatarajiwa mbali ya mambo mengine, kuanza kwa kumzungumzia marehemu Rashid Kawawa, mchango wake kwa taifa na hata jinsi Rais Jakaya Kikwete mwenyewe alivyokuzwa kisiasa na mwanasiasa huyo mkongwe, marehemu Rashid Mfaume Kawawa.
Reactions::

Kumbukumbu Ya Marehemu Mzee Kawawa Katika Picha





Reactions::

Simba Wa Vita Hatunaye Tena: Mzee Rashid Mfaume Kawawa Amefariki Dunia



Imethibitishwa asubuhi hii. Historia ya Tanganyika na Tanzania haiwezi ikaandikwa na kukamilika bila kutaja jina la Rashid Kawawa na mchango wake. Historia ya TANU na CCM haiwezi ikaandikwa na kukamilika bila kutaja jina la Rashid Kawawa. Amefanya mengi kwa nchi hii, atakumbukwa daima. Binafsi nikiwa mtoto naikumbuka kauli yake mara ile aliposhiriki jitihada za kumsaka simba mla watu kule Tunduru. Kawawa alisema; " Nchi ya Ujamaa na Kujitegemea haiwezi kusumbuliwa na simba!". Mwenyezi Mungu Amlaze Mzee wetu Kawawa mahali pema peponi, Amen.
Reactions::

Wednesday, December 30, 2009

Mzee Rashid Kawawa Mgonjwa



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jioni(Picha: Freddy Maro) TUNAMTAKIA KILA LA HERI APONE HARAKA.
Reactions::

Semina Ya Biashara

HABARI! NINA KUKARIBISHA KATIKA SEMINA YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ITAKAYOFANYIKA IKWETA HOTEL ARUSHA MJINI SIKU YA JUMAMOSI SAA 9 MCHANA. KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0719 886 193

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@


KARIBU KWENYE FURSA YA BIASHARA
JE wewe ni mwajiriwa au sio mwajiriwa nani tegemezi wa KIPATO chako?
JE unayo familia na wewe ndiyo kiungo chakuendesha familia?
JE una watoto,ndugu na marafiki wanaokutegemea?Ikitokea bahati mbaya ukawa kilema wa maisha au Mungu amekuchukua, JE familia yako na watoto wako watalipwa na ofisi yako maisha yao yote?
JE, ungependa uwaache wapo kwenye shida nakuomba misaada kwa marafiki zako?
JE wewe ni mmoja kati ya watu wanaosumbuliwa na KIPATO? Au unafikiria kuwa na NYUMBA NZURI, GARI ZURI, AMANI, au KUSOMESHA WATOTO?
JE unafahamu kuwa watu wengi wanamaisha duni kwa sababu tu hawana MTAZAMO sahihi wa maisha?
JE unafahamu familia ngapi ambazo zinaishi kwa taabu sababu tu kiungo cha familia hiyo ambacho kilikuwa chanzo cha mkate wa siku Mungu amekipumzisha mahali pema peponi?
JE una ndoto(Malengo) yoyote mwaka huu? Imekamilika au ipo mbali kukamilika? Umepanga chakufanya?
Umefika wakati wakabadili mfumo(mawazo mgando) wetu wakufikiri na tutumie muda wetu kwa manufaa yetu wenyewe.
Karibu kwenye semina ya Bure itakayokupa fursa nyingine mbadala kwa kutumia muda wako wa ziada uweze kufikisha malengo yako uliyojipangia.

MAHALI: DSM, ELITE CITY BUILDING 2nd Floor. ARUSHA ,BLUE ROCK HOUSE MKABALA NA GOLDEN ROSE,MWANZA PPF PLAZA SECOND FLOOR .DODOMA UKUMBI WA VETA,MBEYA FOREST HILL HOTEL ,IRINGA –KIHESA KICHANGANI STUDENT CENTRE
MUDA: SAA 9:00 ALASIRI
SIKU: JUMAMOSI NA JUMAPILI
KWA WAKAZI WA ARUSHA WIKI HII TUPO IKWETA HOTEL KARIBU SANA
Mawasiliano:- 0719 886 193

JACKIE
Reactions::

" Nakwenda Kupima Afya Yangu"




Jana nilikutana na jamaa yangu hapa Dar Es Salaam. Aliniuliza niendapo, nikamjibu; " Nakwenda kupima afya yangu". Niliona jinsi alivyoshtuka kusikia kauli yangu ile. Kuna vitu alikuwa anafikiri na kujiuliza kichwani mwake. Kwa bahati mbaya Watanzania hatuna mazoea ya kupima afya zetu. Mtu akitamka anakwenda ' kupima afya yake' na kama asiposema kuwa anajisikia malaria, basi, kuna watakaodhani mengine. Binafsi nimejiwekea utaratibu wa kupima afya yangu mara mbili kwa mwaka; mwisho wa mwaka ( kama sasa) na katikati ya mwaka.

Mwili wa binadamu ni kama gari, unahitaji kufanyiwa ' service'. Utamkuta mtu yuko tayari kugharamia service ya gari lake mara sita kwa mwaka lakini hayuko tayari kugharamia ' medical check up' ya mwili wake mpaka augue. Kwangu mie ni heri nitembelee baiskeli na kuwa na senti za kupima afya yangu kuliko kutembelea gari la kifahari huku nikiwa na afya mbovu.

Hata kama maradhi huja bila taarifa, lakini kuna umuhimu wa kupima afya zetu japo mara moja kwa mwaka. Tusisubiri tuugue kwanza. Afya njema ni muhimu kwa ufanisi wa mipango yetu pia. Nimeshapanga, kuwa ndani ya nusu ya mwaka ujao, 2010, mbali ya mambo mengine, nitakimbia mbio za Dar Vodacom Half Marathon, ni kilomita 30. Itakuwa ni kwa mara ya tatu mfululizo. Nitaendesha baiskeli pia, kutoka Iringa hadi Dodoma. Ni kilomita 290. Yote hayo yanaihusu afya yangu, ni vema nikajua ' hali ya afya yangu' ninapojiandaa kuingia mwaka mpya. Januari 8 nimepata muda na daktari kuangalia hali ya afya ya meno yangu, hilo pia ni eneo muhimu. Mara nyingi tunasahau kuangalia afya za meno yetu mpaka pale yanapomomonyoka.

Pichani ni leo asubuhi, baada ya kukimbia kilomita saba maeneo ya ufukwe wa Oysterbay, Dar es Salaam. Nawatakia maandalizi mema ya kuingia mwaka mpya wa 2010.
Reactions::

Mafuriko Yafunika Morogoro(Kilosa)



Reactions::

Vita Ya Udini bado Unaitesa Nigeria


Watu 39 wameuawa wengi wao wakiwa ni watoto wa kati ya miaka 9 hadi 15 katika mapigano yanayoendelea kati ya kikundi cha kiislam na jeshi nchini Nigeria.
Reactions::

Muungwana Ni Vitendo Si Maneno Matupu



BAADA ya wakazi kata ya Ilula kupata shida kubwa katika huduma ya maji safi mbunge wa jimbo la Kilolo ambaye pia ni waziri wa mawasiliano sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla amelazimika kushika jembe na kushirikiana na wananchi wa Ilula kuchimba mtaro wa maji huku akimcharukia meneja wa mamlaka ya maji wa mji mdogo wa Ilula kuwa kama atashindwa kuthamini nguvu za wananchi kwa kukamilisha mradi wa maji ndani ya siku 18 kuanzia leo atawajibishwa .
Chanzo(Francis Godwin)
Reactions::

Mafuriko Yazuia Safari Ya Treni


Shirika la Reli la Tanzania (TRL)jana lilisitisha safari zake kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Dodoma na baadhi ya mikoa ya jirani.
Reactions::

Karibu Mikumi National Park!


Reactions::

...Jongoo Mpenda Watu....



.. Na Watu Hawamupendi Jongoo!
Mwendo wa jongooo poleple
Mwendo wa libata upande upande
Mwendo wa kinyonga kusuasua
Mwendo wa konokono....

Mwanammke muzuri hakosi kasoro ( Remmy Ongala)

PS: Na mwanamume muzuri?
Na mwendo wa kuku?
Reactions::

Hii Mnaitaje Kwa Kilugha Cha Kwenu?

Reactions::

Tuesday, December 29, 2009

China Habari Nyingine!

Mjengwa,

Naomba urushi hii habari, China leo hii wamemuua jamaa aliyejaribu kupitisha heroin ndani ya nchi, kwa kumpiga risasi moja tu, kwenye kichwa, Je sisi watanzania should we start doing the same ? au kwa upande mwengine vile vile China wanaua watu wabadhirifu wa mali ya umma, ie. Mafisadi, nk.. Je kwetu sisi hii adhabu si ingetufaa kwa kweli hususan kwa wale ambao wameiba over a billion should deserve this I guess,

Naomba unirushie tuiongelee kwa undani zaidi, VIPI HII ADHABU ITATUFAA AT LEAST KWA WABADHIRIFU WA MALI YA UMMA, KAMA WATAONEKANA WITH NO DOUBT WAMEFANYA HIVYO...KWANI WENGI TUNAATHIRIKA NA HILI SWALA.

MFANO, hivi nikikwambia NAILIPA TANZANIA TAX ISIYOPUNGUA MILIONI 50 ZA KITANZANIA KWA MWAKA, KWENYE BIASHARA YANGU NDOGO TU, HALI YA KUWA MAHITAJIO YANGU YA KULA NI YA KUJIBANIA, KWA KUTEGEMEA KWAMBA PESA HIYO ITAMSAIDIA MTANZANIA MWENZANGU, HOSPITAL, BARABARA MOJA, NA UIMARISHAJI WA NYANJA NYENGINE ZA KIMAENDELEO KWA KWELI INANIFANYA NILIE NA NITOKWE NA MACHOZI.

KWA HIYO SERIKALI KUPIGANA NA VITA HIVI VYA UBADHIRIFU, KUUAWAWA KWA MBADHIRIFU, NI PERFECT SOLUTION.

KWA HABARI ZAIDI JUU YA CHINA YA EXECUTION YA HUYU MTU SOMA HAPA...

http://news.bbc.co.uk/2/hi/uk_news/8433285.stm
Reactions::

Huyu Ni Samaki Au Binadamu Mwenzetu?


Wadau huyu samaki wa ajabu alionekana akiwa amekufa kule Malaysia baada ya tsunami. Mwangalie samaki huyu kwa makini utaona kuwa ana mbavu, mikono na kichwa kama binadamu. Je huyu ni samaki mtu(mermaid)?. Wadau toeni maoni yenu kuhusu kiumbe hiki cha ajabu.Chanzo(Maajabu ya kweli)
Reactions::

Wanaklijiji Wa Igowole Wavamia Ofisi Za Kijiji


Habari za uhakika zilizotua katika mtandao kutoka kijiji cha Igowole wilaya ya Mufindi mkoani Iringa zinadai kuwa kundi la wananchi wakiwa na silaha mbali mbali za kijadi asubuhi hii wamevamia ofisi za serikali ya kijiji hicho na kuwateka viongozi wa kijiji kwa madai kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuvunja milango yao usiku na kuwataka walipe michango ya maendeleo ya elimu,pichani ni kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa ACP Evalist Mangalla
Reactions::

Yanga Yatwa Ubingwa Wa Tusker


Mshambuliaji machachari wa Yanga Mrisho Ngasa akiwa katika harakati za ushindi siku ya fainali ya kombe la Tusker kati ya Yanga ya Tanzania na Sofapaka ya Kenya. Yanga ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Sofapaka bao 2-1. Bao za yanga zilifungwa dakika tano za mwisho ikitokea nyuma baada ya kufungwa bao moja na sofapaka. Bao la kwanza la yanga lilifungwa na mkongwe Boniface Ambani na lile la ushindi lilifungwa na Mrisho Ngasa.
Reactions::

Monday, December 28, 2009

Tangazo La Msiba

TANGAZO LA MSIBA

Shule ya Msingi Rwamlimi iliyopo Musoma Mjini inasikitika kutangaza kifo cha Mwalimu mwenzao Mwl Dalphone Lameck kilichotokea katika hospitali ya Bugando tar 28/12/09.Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Rwamlimi –Musoma.Marehemu ameacha Mke na watoto

Marehemu Mwl Lameck katika uhai wake alishika nyadhifa tofauti hasa ualimu mkuu katika shule zifuatazo za msingi Nyakato, Nyasho, Rwamlimi zilizopo Musoma Mjini.

Habari ziwafikie ndugu wa marehemu popote pale walipo,Walimu wote waliowahi kufundisha nae ,wanafunzi wote waliofundishwa nae wakatika wa uhai wake,Majirani na marafiki wote pale Rwamlimi Musoma bila kuwa sahau washiri wote wa kanisa la wasabato Rwamlimi na Nyakato

Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe-Amen
Reactions::

Sherehe Za Kuukarisha Mwaka Japani

Sherehe za kuukaribisha Mwaka Mpya 2010 Tokyo

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) inapenda kuchukuwa fursa hii kuwatangazia Watanzania wote wa Kanto na maeneo ya jirani na wale watakaokuwa wanatembelea Kanto wakati huu wa kipindi hiki cha Mwaka mpya kuwa kutakuwa na sherehe kabambe ya kuukaribisha mwaka mpya (2010). Sherehe hizi zitafanyika huko Mkoani Kanagawa. Maelezo kamili ya shughuli hiyo ni kama ifuatavyo:-

Siku: 3/1/2010 (Jumapili)

Muda: Kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo

Kiingilio: Yeni 1500 (utapata kinywaji kimoja)

Ukumbi: Amore Club uliopo ghorofa ya pili ya jengo la Grande Hon Asugi, Hon Asugi, Nakacho-2-13-13, ilipofanyikia sherehe ya Uwataja2008 (Karibu na ukumbi wa mama Mperu). Dakika 5 toka kituo cha train cha Hon Asugi (Odakyu line)

Muziki: DJ mkongwe, DJ Zee atakupatia miziki ya aina mbalimbali kuanzia zile za kizazi cha zamani (enzi za mababu zetu) mpaka za kizazi cha kipya, hip hop, taarab, nk.

Kwa ufafanuzi na maelekezo ya ziada tafadhali wasiliana na wanakamati wa kamati ya uhamasishaji na Starehe:

Bw Pembe: 080-3458-8786

Bi Angela: 080-3397-0339

Bi Upendo: 080-1326-9700

Bi Mariam: 090-4422-8555

Bw Ntale: 080-4149-1257

Tunawaomba watanzania pamoja na marafiki zao wa mataifa mengine kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha shughuli hii. Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.

Ahsante

Kamati ya Uhamasishaji na Starehe

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani
Reactions::

Mikumi Wana Breakfast Iliyokamilika!




Na kuna vingi vingine.
Reactions::

Sunday, December 27, 2009

HONGERA DAR YOUNG AFRICANS!



Mmeingia fainali kwa hila na mmechukua kombe kwa hila!
Tukiacha utani, Yanga leo wametandaza soka ya kisasa. Bila shaka haya ni matunda ya kocha mpya. Ni changamoto kwetu Simba. Halafu goli la pili alilofunga yule mtoto ( lugha ya soka)Mrisho Ngassa ni la kiwango cha dunia ( World Class). Sijui ni kitu gani kinachomkwamisha Ngassa asichezee klabu cha nje?
Turudi kwenye utani, Yanga hamjazoea kushinda mechi kubwa za kimataifa, tumeona ushamba wenu, eti, mnasema kesho mtafunga barabara za mji kusherehekea ushindi. Hata Mtibwa walibeba Kombe hilo mwaka jana, hatukusikia hayo! Simba tumecheza mechi kubwa Afrika, tumewafunga Zamalek na hata El Ahly lakini hatujawahi kufikiri kufunga barabara! Naam. Watani zetu tunawajua.
Reactions::

Kinondoni Namanga



Leo mchana.
Reactions::

Abrakadabra Kutoka Nigeria!



Zamani ilikuwa Mganga kutoka Sumbawanga au Tanga ndiye aliyekimbiliwa, siku hizi sio tu filamu za KiNigeria, hata waganga wa KiNigeria wako juu! Naam. Wabongo wanajaribu kucheza filamu za KiNigeria kwa maana ya kuiga, na mganga kutoka Mtwara naye anajiita Mnigeria. Tangazo analiweka Oysterbay ofisi yake iko Tandale kwa Mtogole. Hapo hakuna cha uganga bali ni Abrakadabra, neno la wajanja.
Reactions::

SofaPaka Ndio Hawa!



Niliwakuta pale Best Bite Namanga leo wakipata chai ya saa nne. Niliongea na baadhi ya wachezaji wa SofaPaka. Pichani ni wawili kati yao.
Reactions::

Timu Hii!



Del Piero, Ahmed Amasha, Kaseja na Nsajigwa!
Reactions::

Nyati Huyu!



Mbele ya banda nililoishi, Mikumi.
Reactions::

Kila La Heri Dar Young Africans!



Leo ni fainali ya Kombe la Tusker; Dar Young Africans Vs Sofa Paka. Utabiri wangu uko pale pale. Leo Yanga watapaluliwa na paka! Naam. Watani zetu mnalala mbili kavu. Mjitahidi yasizidi hayo mawili ili mlinde heshima ya taifa. Kila la Heri!
PS: Na matokeo ya jana ni kama nilivyobashiri, Simba tumewafunga Tusker na tumechukua ushindi wa tatu na milioni 20 ingawa mechi ya leo ya fainali ilikuwa ni yetu. ( Pichani ni kijiwe cha watani zangu Yanga pale Soko Kuu, Iringa)- Udumu Utani Wa Simba Na Yanga.
Reactions::

Saturday, December 26, 2009

Hili Ni ' Taifa Kubwa!'



Tangu kuanza kwa msimu huu Simba haijapoteza hata mchezo mmoja ndani ya dakika tisini za mchezo. Yanga wanalijua hilo. Hata mechi tuliyofungwa kwa 'hila' na watani zetu juzi, bao la pili la Yanga lilipatikana nje ya dakiki tisini. Hivyo basi, rekodi ya Simba haijavunjwa. Tunawasubiri Yanga mzunguko wa pili wa ligi, tutalipiza kisasi ndani ya dakika tisini. Uwezo, sababu na nia ya kufanya hivyo tunayo. Na leo tutaingia uwanjani kuwafunga Tusker na kuchukua milioni 20 tunazostahili. Yanga kesho msubiri kipigo cha 2-0 kutoka kwa SofaPaka! Haya Yanga mnasemaje?( Udumu Utani Wa Simba Na Yanga!)
Reactions::

Starter Hii!



Smoked fish, Mikumi.
Reactions::

Kitonga Umefika Hapa!



Juzi asubuhi.
Reactions::

Friday, December 25, 2009

Milima Ya Kitonga Inapendeza!




Ina kona kali si chini ya saba. Ni mahali ambapo dereva anatakiwa awe makini sana hata kama barabarani lolote laweza kutokea. Pichani ni jana asubuhi. Kwa mbali ni basi la Abood njiani kuelekea Dar na abiria waliokuwa wakiwahi Krismasi.
Reactions::

Mikumi Ya Yangayanga!




Ni kijani kijani na hapo chini pia. Vingenevyo, nimekuwa na usiku tulivu wenye sauti za asili, wanyama na ndege. Asubuhi hii nimekaa barazani kwangu nikinywa kikombe cha chai na kuangalia nyati walio mbele ya banda ninaloishi.
Reactions::

Jana Kijani Zilikuwa Nyingi!



Hata banda nililofikia hapo chini lilikuwa na bendera ya kijani!
Reactions::

Thursday, December 24, 2009

Niko Mapumziko Ya Krismasi Mikumi

Ni ile ofa niliyopewa, miye na familia yangu. Naandika usiku huu huku nikisikia sauti za simba wanaounguruma. Mikumi ni mahalli pazuri sana. Ninachosikia kwa sasa ni sauti za wanyama tu.

Tangu nimefika mchana wa leo sijawa na mawasiliano na dunia ya habari. Hata hivyo, kuna mfanyakazi wa hoteli aliyeninong'oneza kuwa Simba wamelala bao 2-1 kwa Yanga. Kwanza nimesikitishwa kwa Simba kufungwa, lakini wakati huo huo nimejikuta nikufurahi matokeo hayo. Naamini ni matokeo mazuri kwa kandanda ya Tanzania. Simba tunawahitaji watani zetu, kama tungewafunga leo, nahofia Yanga wangezidi kukosa mwelekeo, hilo la mwisho halina maslahi kwa Simba na kandanda ya Tanzania. Nimesikia pia refa aliwabeba Yanga kwa kumtoa Haruna Moshi wa Simba kwa kadi nyekundu. Hongera sana watani zetu wa jadi! Nina picha kadhaa za njiani na hapa Mikumi. Nitazitundika kesho.
Reactions::

Mapishi Ya Krisimasi!

A Taste of Tanzania has posted a new item, 'Christmas Recipes / Mapishi ya
Noeli'
I have put together a pdf of simple recipes from Tanzania that many people will
be preparing this weekend back in Tanzania. Traditionaly Pilau is the number one
recipe to think of during the holidays. I wish you a VERY MERRY CHRISTMAS. Click
here to get the pdf.

Nimetayarisha mapishi ya Noeli katika pdf. Kwa sababu [...]
You may view the latest post at
http://tasteoftanzania.com/blog/2009/12/24/christmas-recipes-mapishi-ya-noeli/
You received this e-mail because you asked to be notified when new updates are
posted.
Best regards,
Miriam Rose
miriam@tasteoftanzania.com
Reactions::

Je, Mkukuta Umepunguza Umaskini?


Hapa ni wakazi wa Manzese (Dar)wakipata shida ya maji baada ya bomba lililokuwa likiwapa maji ya bure kufungwa. Sasa jiulize, Kama huduma muhimu kama hiyo ikiwa ni ngumu kupatikana, je, Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza Umaskini (mkukuta) unatusadia?
Reactions::

KAKAKUONA,: Mnyama Mwenye Uwezo Wa Kinabii


KAKAKUONA ni Mnyama nadra kuonekana na binadamu ambaye anasemekana na uwezo wa kutabiri matukio yanayoweza kutokea katika nchi.
Mnyama huyo ana uzito unaokadiriwa kufikia kilo zaidi ya sita na urefu wa futi zaidi ya tatu.
Huenda alipewa jina kaka-kuona kwa sababu ya uwezo wake wa kuona mambo yajayo.
Reactions::

Lionel Messi Atwaa Tuzo Ya Mwanasoka Bora wa Dunia.


Mwanasoka mwenye mvuto kiuchezaji raia wa Algentina anayekipiga Barcelona F.C Lionel Messi ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia katika hafla ya jana Mjini Zurich Uswis, akiwashinda nyota wengine akiwemo Christian Ronaldo, Xavi Hernandes na Andres Iniesta.
Reactions::

Sofapaka Yatinga Fainali Kwa Mkwara Mzito


Timu ya Sofapaka kutoka Kenya imetinga Fainali za kombe la Tusker kwa mkwara mzito baada ya Kuichabanga Tusker ya nchini humo kwa jumla ya mabao 6-0.
Reactions::

Salaam Za Christmas Kutoka Kwa Viriyala

Reactions::

Jengo La Serikali Iringa: Tangu Enzi Za Mjerumani




Ni kumbukumbu ya historia yetu. Ni matumaini yetu hatatokea ' mwendawazimu' akapitisha amri ya jengo hilo kuvunjwa na kujengwa la 'kisasa'. Ukikaa na wazee wa zamani wa Iringa watakuelezea mengi yenye kuhusiana na jengo hilo. Nilipata kusimuliwa na Mzee Nzowa wa hapa Iringa, kuwa enzi za ujana wao walifuatilia mechi za Kombe la Gossege sasa Chalenji za Afrika Mashariki wakiwa nje ya jengo hilo. Mahali hapo palikuwa na ofisi ya posta pia. Ili kupata matokeo, Posta Master alikuwa akiwasiliana na mwenzake wa Dar es Salaam kwa simu ya kukoroga. Basi, kila anapotoka Posta Masta kutoka ofisini kwake watu walijiandaa kusikia kama ametoka na habari yeyote ya matokeo ya mchezo. Wakati mwingine alitoka, alipiga mluzi wake na kuingia ofisini tena bila kusema lolote. Naam. Siku kama hiyo, Posta Masta alikuwa ' Mfalme'. Leo tunafuatilia mechi za Ligi ya Uingereza kutoka kwenye simu zetu za viganjani. Naam. Tumetoka mbali. Merry X-mas!
Reactions::