Subscribe:

Sunday, January 31, 2010

Siri Ya Mafanikio Ya Egypt


SIRI YA MAFAANIKIO YA SOKA KATIKA TIMU YA TAIFA YA MISRI.
Kwanza twamshukuru Mungu na pili pongezi nyingi sana kaka kwa kutupa nafasi wadau wako wa Globu hii ya Jamii kusema japo bado hatujakabidhiwa rasmini peni na makaratasi katika Maofisi Makubwa katika kuhakikisha mambo yanaenda sawa Nchini Kwetu Tanzania tunaileta kwenu wadau Wenzetu kama Hoja ambayo tunaomba ichangiwe na kwa wale ambao wana nafasi Fulani ya kuweza wafika wahusika wa kutekeleza haya tutakayosema wachukue nafasi ya kuwaeleza ili tuzidi kuliendeleza libeneke letu la Tanzania Daima kila kitu kinawezekana.hasa katika swala …Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

ILO Yaimwagia Sifa Tanzania


Na Mwandishi Maalum, Davos, Uswisi

Shirika la Kazi Duniani (ILO) limesema kuwa Tanzania ni mfano mzuri wa nchi yenye uongozi bora na imara, hali iliyoiwezesha nchi hiyo kutoyumbishwa kupita kiasi na msukosuko wa karibuni wa uchumi duniani. Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Jerry Muro Ni Mshtuko Mkubwa



Taarifa za kukamatwa kwake na kuwekwa ndani zimetapakaa kama moto wa porini. Hapa Iringa ni gumzo la mitaani. Itakumbukwa majuma kadhaa yaliyopita alikuja na ripoti iliyobainisha rushwa miongoni mwa askari wa Usalama Barabarani hapa Iringa. Kumi na mmoja walipoteza ajira zao. Inaaminika mmoja wao alimpoteza mkewe kutokana na mke huyo kukata roho kwa mshtuko wa yaliyompata mumewe. Kama Jerry Muro atatiwa hatiani, basi, atakuwa sio tu amekifedhesha chombo anachokitumikia, bali pia atakuwa ameifedhehesha sekta ya habari hapa nchini.
Reactions::

JK Na Waziri Mkuu Wa Vietnam


President Jakaya Mrisho Kikwete(right) in conmversation with Vietnam Prime Minister Nguyen Tan Dung(centre) and the chairman of the New Delhi Television Roy Prannoy(left) who was also the moderator during the debate on Global Food Security held at Davos Congress Hall yesterday evening(Photos: Freddy Maro)
Reactions::

JK Alitumia Vema Jukwaa La Davos



Mbali ya mambo mengine, Rais Jakaya Kikwete ameainisha nguzo kuu sita za kuleta maendeleo Afrika. Ametaja nguzo kuu sita ambazo amesema kuwa zikitekelezwa ipasavyo zitaharakisha kasi ya maendeleo ya Bara la Afrika. (Photo: Freddy Maro)
Reactions::

JK Aongea Davos, Switzerland


President Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a debate on improving agriculture production to boost food Security during the World Economic forum in Davos yesterday.On the left is Ellen Kullman Chairperson and CEO of of the US based DuPont company and on the right is Microsoft Founder and Chairman Bill Gates.
Reactions::

JK Na Bill Gates


President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the the Microsoft founder and Chaiman of the Bill and Melinda Gates Foundation, Bill Gates shortly after participating in a debate on improving Food Security held in at Davos Congress Hall, yesterday afternoon.(Photos: Freddy Maro)
Reactions::

" Your Exellency Mr President..."



President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with World Trade Organisation WTO Director General Pascal Lammy at Davos Congress hall in Davos yesterday evening during the last session of the World Economi Forum held in Davos Switzerland(Photo: Freddy Maro).
Reactions::

Born Again Pagan: Kwanini Tunakwenda Shule? Jibu...



Tunakwenda shule ili kupata njia bora za kurahisisha (kwa vitendo na matokeo yake) katika kukidhi matakwa ya mahitaji ya lazima (basic needs) maishani, kuliko wanyama: zaidi ya kulinda miili yetu kwa chakula na maji, mavazi na mahali pa kulala! Kwani wanyama nao wana uwezo huo.

Lakini binadamu ni zaidi ya mnyama. Ndio maana kajiundia mazingira mengine (supestructures)juu ya familia, kwa mifano, dini na shule ili kuboresha wajibu wa familia katika kutafuta na kukidhi “basic needs”.

Tunakwenda shule kujenga “our totality”, ya kusaidiana katika kuondokana na unyonge wa kutoishi maisha. Hiki ni chakula ya ubongo (akili): habari, maarifa uelewaji na hekima ya kuishi katika jamii, zaidi ya ubinafsi wetu.

BAP
Reactions::

Utabiri Wangu Kwa Egypt Uko Pale Pale!



Niliwatabiria Egypt ushindi dhidi ya Algeria ndani ya dakika tisini, ikawa hivyo. Nikatabiri kuwa Egypt watawafunga Ghana kwa zaidi ya goli moja ndandi ya dakika 90 na hivyo kuchukua Kombe la Afrika. Mechi yenyewe ni leo, utabiri wangu upo pale pale!
Matokeo ya Man United na Arsenal leo yatakuwa ni ya Man United kuadhirika! Na leo jioni Simba watawatafuna bila huruma Wa-Toto Wa Dar Young Africans wanaoishi Mwanza!
Reactions::

Profesa Mbele Amekuja Na Changamoto!




Bei $13.00

Ships in 3–5 business days

Kitabu hiki ni mkusanyiko wa insha nilizoandika mwaka 2009 na kuzichapisha katika gazeti la KWANZA JAMII. Vile vile kuna mahojiano niliyofanyiwa na blogu ya Bongo Celebrity, mwaka 2008. Kwa ujumla, yaliyomo ni mawazo kuhusu masuala mbali mbali ya uchumi, siasa, jamii, na utamaduni yanayoihusu Tanzania na dunia kwa ujumla.

Mtembelee; http://josephmbele.blogspot.com
Reactions::

Mkalifya: Mchungu Lakini Mtamu!




Jana mchana nilikuwa kijijini Kalenga, Iringa. Huko nilikaribishwa ugali na mboga ya mkalifya. Ni mboga ya majani, chungu lakini tamu!
Reactions::

Kalenga Umefika Hapa!




Ndipo ilipokuwa ngome ya Chifu Mkwawa wa Wahehe. Pichani ni jana Jumamosi.
Reactions::

Spika Wa Bunge Wa Enzi Za Mwalimu!



Chifu Adam Sapi Mkwawa. Mjukuu wa Chifu Mkwawa wa Wahehe.
Reactions::

Makumbusho Ya Chifu Mkwawa



Jana nilitembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa wa Wahehe pale kijijini Kalenga. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Chifu Mkwawa na jinsi alivyokuwa kiongozi mahiri na mweledi wa masuala ya kijeshi. Aliongoza jeshi lilotumia mbinu zilizowashangaza majemedari wa Kijerumani ikiwamo kutumia inteligensia ya kijeshi. Nina picha na simulizi zaidi kutoka Kalenga. Nitaziingiza.
Reactions::

Nina Hoja: Watumishi Wa Serikali Wasio Na Namba Za Jeshi Wapelekwe Makambi Ya JKT!



Pamoja na hatua ya Serikali kutaka kurudisha utaratibu wa vijana kupitia JKT, ili kurudisha nidhamu ya utendaji Serikalini ikiwamo uzalendo, kuna haja ya kufanyika utaratibu wa kuwapeleka watumishi wa Serikali wasio na namba za jeshi kwenye makambi ya JKT. Huko waende wakatumikie taifa kwa kipindi cha siku arobaini na tano ( mwezi mmoja na nusu ). Watumishi watakaokacha kwenda makambini ( kama si wagonjwa au walemavu) wapoteze sifa za kuwa watumishi wa Serikali au wasipandishwe vyeo. Mwezi mmoja kambini uwe wa kupiga kwata na wiki mbili za kuitumikia jamii kwa kwenda kuishi na kufanya kazi za kujitolea na wanajamii vijijini. Kuna faida nyingi katika hilo, Serikali itaokoa fedha nyingi kwa kuwa na nguvu kazi yenye uzalendo na isiyoona lazima ya kutanguliza masuala ya posho mbele na badala yake kuona, kuwa katika utendaji wao wa kazi, Cha KWANZA ni Jamii. Pichani ni Marehemu Rashid Mfaume Kawawa ( Simba wa Vita) katikati, Abdu Jumbe ( Alikuwa Rais wa Zanzibar) wa kwanza kushoto na aliyekuwa Spika wa Bunge, Chifu Adam Sapi Mkwawa. Hawa walipitia mafunzo ya muda mfupi ya JKT kambi ya Ruvu wakitokea Serikalini, huo ndio msingi wa hoja yangu.
Reactions::

Saturday, January 30, 2010

Bi. Mkora: Kiberenge Mara Kuwahi, Mara Kuchelewa Kufika Au Kuzimika!


Samahani sana kaka yangu uliyeuliza swali, naomba nikujibu swali lako uwanjani ili watu wengi wapate kunufaika, maana hilo tatizo unalolisema watu wengi wanalo na wanaona ni hali ya kawaida. Lakini hali hii ina madhara makubwa katika suala zima la mahusiano. Hebu fikiria ingekuwa ndio wewe kila linapofanyika hilo tendo ama mwenzio kishamaliza haraka au inamchukua muda wee mpaka unaona toba! hii karaha itaisha lini, ungelifanyaje? Huo ndio mwanzo wa mtu kutafuta spea tairi/kucheat/ au kuwa na mahusiano ya pembeni. Sisemi kuwa wote wanaokumbwa na hali hiyo wenza wao wanatafuta faraja pembeni, hapana, msije mkatoana ngeu huko mkasema aah Bi Mkora kasema, na kwa vile yeye ni Kungwi basi ni kweli. Maana yake ni hivi ikiwa mtu anakuwa na kiu kila siku iko siku akikuta kisima cha maji baridi na matamu atakunywa! Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Wanafunzi Wa Kibasila Waandamana Dar-es-Salaam


Askai Polisi wakitoa jiwe kubwa lililotegwa na wanafunzi wa Kibasila ili magari yasipite

Wanafunzi wa Kibasila wakiwasaidia wenzao na kuwapepea baada ya kuzirai kutokana na ,mabomu ya machozi na kipigo kutoka kwa askari.

Wanafunzi wakiwasaidian wenzqao kwa kuwapepea.

Wanafunzi wakitoa msaada kwa wenzao baada ya kipigo.

Wanafunzi wa Kibasila wakiwapeleka wenzao waliozidiwa hospitali.

POLISI wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kibasila waliokuwa wamefunga barabara ya Mandela na Chang’ombe kwa kutumia mawe makubwa yaliyokuwa kandokando ya barabara hizo.

Kikosi hicho chenye askari 11 walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutokana na wanafunzi hao zaidi ya 200 wa Sekondari hiyo kupinga hatua ya kugongwa kwa mwananafunzi mwenzao Emmanuel Mapande.

Tukio hilo limettokea leo majira ya saa 3:30 asubuhi, kwenye makutano ya barabara hizo zilizopo karibu na kituo cha Polisi cha Chan’gombe.

Tanzania Daima lilikuweko kwenye eneo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya askari kufuatiwa kugongwa mwanafunzi hiyo na basi la abiria aina ya Toyota Coaster ambalo lilitoweka baada ya kufanyika kwa tukio hilo, hata hivyo namba zake badi hajizafahamika bado.

Tanzania Daima lilishuhudia kiongozi wa askari hao akiwaamrisha askari kutumia mabomu zaidi kwa wanafunzi hao kutokana na kukaidi kuondoka eneo la barabara huku wakizuia magari kuendelea na safari, mengine kuvunjwa vioo.

“Tutumia mabomu ya machozi wanafunzi hawa wanakaidi amri ya Polisi, basi na sisi tunatumia nguvu kuwaondoa” alisema Kiongozi huyo.

Amri hiyo iliwafanya askari wenye silaha hizo kurusha mabomu hadi kwenye eneo la shule ya sekondari hiyo, huku wanafunzi hao wakijibu mashambulizi kwa kuwarushia mawe kwa askari hao.

Hata hivyo walionekana wanafunzi hao wakitokwa na machozi kutokana na madhara ya mabomu hayo na wengine ambao idadi yao haijafahamika mara moja wamekimbizwa kwenye hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi.

Walikimbizwa hospitali ni;Agatha Kivuvyro, Yusta Herman, Fani Abdul, Kuruthum Athanas, Jackline Gades na Mary Richard.

Wengine ni pamoja na Janeth Kagoa, Anet Kiyogoa na Mary Shao wote wa kidato cha nne na tano.

Baadhi ya wanafunzi waliiambia Tanzania Daima kuwa, mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, aligongwa majira ya asubuhi wakati akivuka barabara akitokea shuleni.

“Amegongwa wakati akitoka maeneo ya shule kuelekea nje, hata hivyo ilikuwa ni makusidi ya dereva kwani yeye (dereva), anafahamu kuwa barabara hii inatengenezwa kwa sasa” alidai mwanafunzi huyo ambaye hakitaka kujata jina lake.

Wakizungumza leo wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliziomba mamlaka zinazohusika kuweka taa za kuongozea magari ili kupunguza ajali katika eneo hilo ambalo pia ni maarufu kama "machinjioni"
Chanzo: Issa Michuzi)
Reactions::

Gari La Ukweli Linauzwa


kaka naomba unitangazie kwenye libeneke.
Nauza gari Toyota RAV4 GX ya mwaka 2002.

Mileage: 59000
Colour: Silver
Body Type: Station Wagon (5 Doors)
CC: 2000
Transmission: Automatic
Engine Type; VVTi
Fuel: Petrol
Duty Paid

Other specifications including CD Player, Sunroof, Alarm, Airbag, Alloy wheels, etc. It is in excellent condition.

Kama mtu atahitaji kuiona anaweza kuwasiliana nami kwa simu namba

0732 202083
Bei ni kuanzia Tshs 22,000,000.

Makubaliano yanakaribishwa.

Hiyo picha ilipigwa UK few days kabla ya kusafirishwa kuja Dar.

Thank you.
Reactions::

Yanga Kulipa Kisqasi Kwa Majimaji?


Timu ya soka ya Yanga leo kukipiga na timu ya majimaji kutoka Songea( Wanalizombe) ikiwa ni mechi ya Marudiano baada ya Yanga kufungwa kwa bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza.Mechi hiyo inategemewa kufanyika katika uwanja wa Uhuru.
Reactions::

Kuelekea serikali Ya mseto Zanzibar

Reactions::

Red Carpet Affair In Houston Today


MOO FLAVA DJS & SAFARI ENTERTAINMENT

IN COLLABORATION WITH
CLEAR VYBZ PRODUCTION

WANAWAKARIBISHA WADAU WOTE WA HOUSTON TO THE ALL AFRICANS RED CARPET & CAR SHOW" ITAKAYOFANYIKA OUTSIDE SAFARI CLUB IN HOUSTON TX, SAT, 30th JAN 2010 (leo) KUANZIA SAA NNE MPAKA TANO USIKU(10PM TO 11PM).

WADAU WOTE MNAOMBWA KUHUDHURIA TUKIO HILO LA KIHISTORIA KUTOKEA HAPA HOUSTON, LIKIFUATIWA NA HOUSTON BEST AFRICAN DJ CONTEST NDANI YA CLUB SAFARI.

RED CARPET & CAR SHOW HIYO ITAJUMUISHA VIDEO NA PHOTO SHOOT KUANZIA UNAVYOINGIA NA GARI KWENYE VIWANJA VYA SAFARI CLUB , UNAVYOTOKA NDANI YA GARI MPAKA SEHEMU MAALUMU YA KUPIGIA PICHA.

VINYWAJI LAINI(SOFT DRINKS) NA VITAFUNWA (MISHIKAKI AND OTHER SNACKS) VITAKUWEPO WAKATI WOTE WA TUKIO HILO HAPO NJE BILA KUSAHAU LIVE OUT DOOR DJ ATAKUWA AKIENDELEA KUTUMBUIZA. PIA UKIPENDA UNAWEZA KURUHUSU VIDEO CAMERA NDANI YA GARI YAKO KUONYESHA UNIQUE FEATURES OF UR CAR (OPTIONAL).

AGAIN TUKIO HILO LITADUMU KWA SAA MOJA TU(10PM TO 11P) NA BAADA YA HAPO PARTY ITAHAMIA NDANI YA CLUB SAFARI KWA AJILI YA HOUSTON BEST AFRICAN DJ CONTEST NA PARTY MPAKA ASUBUHI.

ZAWADI KWA 'THE MOST SEXY OUTFIT(LADIES) THE MOST GENTLEMAN OUTFIT(MEN) & THE MOST GOOD LOOKING COUPLE ZITATOLEWA IKIWA NI PAMOJA NA FREE ENTRANCE TO THE DJ CONTEST. TUNARUDIA TENA 'RED CARPET & CAR SHOW NI BURE KWA WOOOOTE!!

HIVYO MWAMBIE JIRANI NA RAFIKI
YAKO ASIKOSE! KARIBUNI WOOTE!!

SPONSORED BY CLEAR VYBZ STUDIOS & PRODUCTION
Reactions::

Mlango Wa Pili Wa Maarifa: Episteme, Kwanini Tunakwenda Shule?



Nikiwa Mwanza hivi karibuni nilimwona mtoto huyo aliyelala na kushika tama kila asubuhi niliyokuwa nikifanya jogging. Nilipokwenda nikikimbia, nilimpita akiwa bado hajaamka, na niliporudi kukimbia nilimpita akiwa hajaamka. Kwake ilikuwa ni mapema mno, saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Lakini picha ya mtoto huyo inatukumbusha changamoto za kijamii zinazotukabili. Huko nyuma niliainisha mlango wa kwanza ambao mwanadamu anautumia katika kupata maarifa; Fronesis, ni neno la Kigiriki likiwa na maana ya maarifa yatokanayo na uzoefu.
Picha ya mtoto huyo wa mitaani inatupelekea kwenda kuufungua mlango wa pili wa maarifa; episteme, ( Epistemolojia) nalo ni neno la Kigiriki likiwa na maana ya maarifa tuyapatao kutokana na elimu ya darasani, shuleni. Na tujiulize basi; kwanini tunakwenda shule? Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Kalikwendwa Coach: Kuna Mliokwea Basi Hili!



Mwanza. Na bila shaka lina simulizi zake.
Reactions::

Kuna Mliosoma Hapa!

Reactions::

Wapi Hapa Katika Mwanza City?


Kwa mnaoijua Mwanza City.
Reactions::

Fundi Simu



Mwanza
Reactions::

Friday, January 29, 2010

Mwulize Bi. Mkora: Kiberenge Changu Mara Kinawahi, Mara Kinachelewa Kuondoka, Nifanyeje?



Submitted on 2010/01/29 at 4:28am
Bi. Mkora unasitahili pongezi kwa mafundisho yako na kuwaweka watu katika hali ya kujiamini hasa kutujenga kisaikolojia.Ila nina swali moja nataka niulize.Mimi nina tatizo la kumaliza haraka niwapo kwenye yale mambo yetu na sometimes nachelewa hii inatokana na nini ukizingatia nakua sina mawazo kabisa na kisaikolojia niko vizuri.Kama unaweza kunijibu through mail yangu ntafurahi sana
J. Sinzokabwila.
Reactions::

Bi. Mkora: Mawazo Hupunguza Nguvu Za Kiume, Kwa Mwanamke Hamu Ya Kufanya Sex!



Nimeziona hizo kungu hapo, nimecheka, nikasema mwanawane watu wasije kwenda kununua kungu Kisutu wakala, wakaenda kutest zali, au wakaenda kupopoa kungu kwenye mikungu huko mitaani watu wakawashangaa. Nakumbuka siku moja tukiwa safari za porini kutafuta mitishamba, nilimwambia kaka mmoja kuhusu kanga, basi tulipofika kimji kinachofuata mwenzangu akateremka akaenda sokoni kuulizia kungu manga, basi wacha watu wa sokoni wamshangae, kwa sababu wanununzi wakuu ni wanawake. Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Mume Mwema Hutoka Wapi?



Tumesikia tungo, "Mke Mwema Hutoka Kwa Bwana" Sawa, mume mwema hutoka wapi? Enyi wajuzi wa mambo, akina Bi.Mkora, Mrisho Mpoto na wengine mtusaidie kupata jibu!
Reactions::

Bi. Mkora Tujuze: Kisirani Chapungua Kwa Kufyoza Bibo, Kula Kungu, Muhogo Wa Kuchoma Au Kutafuna Zambarau? Kuna Faida Nyingine?



Picha hiyo niliipiga mitaa ya Kisutu Kisutu hivi karibuni.
Reactions::

Jiandae Na Kitabu!


Reactions::

Mambo Ya Pasaka Amsterdam

Reactions::

Hawa Ndio Mafarao Wa Egypt



Kaka Jamaa wamefurahi sana kwa kuwafunga jamaa wenzao 4-0 siri ya mafaanikio ya huyu Mmisri kupiga soka kama hivi naona itakuwa vyema sana baada ya kuchukua kombe tuieleze japo kwa ufupi ili nasi timu yetu ya Bongo ifike Japo Kombe la Dunia miaka Ijao.
Ahsante Mdau Cairo
Ijumaa Njema.
Reactions::

Thursday, January 28, 2010

Wajumbe Wenzangu Mpira Umewapitia Pembeni!



Leo jioni nilishiriki kikao cha Bodi ya Uongozi wa Iringa International School. Wajumbe wote kasoro mimi mpira umewapitia pembeni. Kikao kiliisha saa moja na nusu na kufika nyumbani ni half ya pili ya mechi ya Ghana na Nigeria. Nilishindwa kujenga hoja kikaoni ya kumaliza kikao mapema ili tuwahi kuangalia game, nani angenielewa?
Reactions::

Naitabiria Egypt Ushindi




Ndani ya dakika 90 za mchezo dhidi ya Algeria. Kwanini, Egypt ndio timu pekee kwa sasa yenye kikosi chenye wachezaji wenye kujiamini zaidi wawapo uwanjani. Matambiko ya Waarabu wa Misri ya kutoa kafara ng'ombe au mbuzi ( kama inavyoonekana pichani) huwatia imani zaidi wachezaji wao. ( Kisaikolojia). Wana uwezo wa kupachika mabao. Natabiri pia ushindi wa Misri dhidi ya Ghana katika mechi ya fainali. Ghana watafungwa mabao zaidi ya moja ndani ya dakika 90. Ni utabiri tu!
Reactions::

HATIMAYE NIMEFANIKIWA KUREKEBISHA HITILAFU!

Nina furaha kuwajulisha kuwa hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika saa takribani 72 zilizopita hatimaye nimeipatia ufumbuzi dakika chache zilizopita. Hakika, nimejifunza mengi katika kujaribu kutafuta ufumbuzi huo. Ningeshindwa leo ningelazimika kuomba msaada wa wataalamu.
Ahsanteni sana kwa kuwa wavumilivu.
Maggid
Reactions::

Mdau: " Mjengwa Wewe Ni Nani?"

Juzi hapa niliulizwa swali hilo ( hapo chini) na mwenzetu mmoja. Nilijibu kwa utani; " Uliza Swali Lingine!". Wengine hupata tabu kupambanua la utani na lisilo la utani. Nitaweka msisitizo maana swali la mdau yule ni swali zuri na gumu. Maana hata miye hujiuliza; " Mimi ni nani?

Mdau wa pili amenisaidia kujibu na kufananua vema kabisa, si udaku. Namshukuru. Na kwa kujibu bila utani swali la mdau yule ni kwamba; Mimi ni Maggid tu, ' Mgambo Wa Vita!' Sina tepe ( vyeo mabegani). Napenda sana kufanya kazi za kijamii na kwa kushirikiana na wanajamii. Kama tunaamua tujitolee kuchimba mitalo ya mabomba ya maji, na miye nitapenda nikabidhiwe sepetu ( koleo). Kama ni kujitolea kuezeka nyumba, na miye nitaitafuta ngazi, nipande juu nisaidie kuezeka, na hata nikibaki chini, basi nisaidie kupandisha fito za kuezekea. Naamini, kuwa kuongoza si tu kuonyesha njia, bali uwe mfano kwa matendo. Uongozi ni vitendo.


•Date: Tue Jan 26, 04:11:00 PM EAT, Anonymous

Mjengwa tunashindwa kuelewa wadhifa wako katika vyuo vya maendeleo mara unasaidia wazungu kupandisha mizigo kwenye gari kule Njombe, mara uko na wazungu kuwaonyesha mbuga za wanyama kule Mikumi, mara umesafiri kwenda Mwanza lakini ikija kwenye mikutano kama ya Kibaha umekaa kiti cha nyuma katika semina wewe ni nani?

Kama ni mkufunzi wa kawaida wa chuo huwezi kuruhusiwa kusafiri mara kwa mara kama vile na kama ni mkuu wa chuo huwezi kukaa viti vya nyuma namna ile wewe ni kachero wa wizara ya jinsia na watoto nini?


•Date: Tue Jan 26, 08:58:00 PM EAT, Mjengwa

Anony wa 04:1100 PM

Uliza swali lingine!


•Date: Tue Jan 26, 10:55:00 PM EAT, Anonymous

Mimi sidhani kama ni kachero wa wizara ya maendeleo ya jamii, ingawa mwenyewe kakataa kujibu yeye mwenyewe lakini nafikiri ni mdau wa maendeleo ya jamii. kama si hivyo anaweza mwenyewe akapinga ila wangu ni udaku tu!
Reactions::

Tatizo La Kiufundi: Hali Haijawa Shwari ( Latest)

Tatizo bado liko pale pale,picha zinakuwa blocked.
Nitaendelea kushughulikia leo usiku. Nikishindwa kabisa nitawatafuta wataalamu.
Poleni kwa usumbufu.
Maggid
Reactions::

Wednesday, January 27, 2010

Nimeikuta Ajali Mbaya Mazombe Usiku Huu

Usiku huu nikiwa njiani kutoka Dar kuja Iringa nilifika eneo la Mazombe, Kilomita 40 hivi kabla ya kuingia Iringa Mjini, hapo niliikuta ajali mbaya ya lori la mafuta. Cha kushangaza, polisi wa usalama barabarani walionekana kuwa karibu na lori hilo sambamba na wananchi wengine ambao, baadhi yao, walikuwa na magaloni na ndoo walizokuwa wakibebea mafuta ya diseli. Cha hatari hapo, kama ilivyotokea kule Mdaula, Chalinze, miezi kadhaa iliyopita, inaweza kutokea hata mahali pale lilikoanguka lori lile la mafuta pale Mazombe mkabala na nyumba ya Profesa Msolla.
Nilidhani polisi wangehakikisha kuwa wamazungusha uzio ili raia wasisogee katika eneo hilo kwa kuhofia hatari ya kutokea mlipuko wa moto. Lakini ilionekana polisi nao walikuwa katika hali ya ' kuchonga dili' ya kuyapata mafuta yale, kaazi kweli kweli!

Vinginevyo nimerejea Iringa, na usiku huu nitafanya kila niwezalo ili nirekebishe hitilafu inayopelekea nishindwe kuingiza picha, hata kama kukesha nitakesha!
Poleni kwa usumbufu.
Maggid
Reactions::

Norman Wage: "This Has To Stop, Now"

Dear Brothers and sisters,
Tanzania is still one of the most peaceful countries in Africa if not in the world. We have enjoyed peace and tranquility through the years. We have managed to achieve this feat by simply respecting, loving and valuing our own status and that of others.

But today, we have buried our brother and a dear friend Swetu Fundikira who was murdered in cold blood in the hands bloodthirsty thugs who by their own ignorance perceived to be above the law. In a clear display of contempt of the law these cowards tried to justify their barbaric actions in the name of Tanzania People Defence Forces.

A soldier is a mere employee of the army and at no given time whatsoever are they entitled to take the law into their own hands. This is not the first time soldiers have behaved in this manner and got away with it. This time we have to stand up against this bullish behaviour and say enough is enough!We ain't going to stand aside and watch these cowards take innocent lives of our brothers and sisters for whatever reasons they may have.

There is not one single reason that can justify what they did to our beloved brother Swetu. For that reason it makes us angry. We are angry because they took a life of an innocent man who was a brother, a son, a neighbour and a lovely friend to most of the people who knew him, myself included.

He was a man of peace, intergrity and love. He did not deserve to die this way. Today we have buried him as a hero but we promise those thugs that we will leave no stone unturned as we fight for justice. We will never rest till justice is done. His death will never be in vain but it will be a defining moment for all the victims who have perished in similar circumstances.

It is also a reminder of how dangerous our peaceful world can be when people like those thugs are given the chance to take advantage of their positions. In strongest words possible we condemn this deliberate and unnecessary killing of our brother.
I urge all Tanzanians to stand up and be counted, stand up against injustice, stand up against victimisation of innocent people, because if we don't the next one will be your father, your mother, your son, your daughter, your friend or even your neighbour. This has to stop now.

Our thoughts are now with the Fundikira family especially his father Mzee Ramadhani Fundikira, his brothers and sisters, Ismail, Mgalula, Mtagwa, Chellu, Nzwala, Mshama Mkalla and the rest of the family memebers.

Rest in peace my brother Swetu and God will bless you.
Yours in deep sorrow
Norman Wage

Reactions::

Tuesday, January 26, 2010

Imejitokeza Hitilafu Ya Kiufundi

Hakuna uwezekano kwa sasa wa kuingiza picha. Nalishughulikia tatizo.
Poleni kwa usumbufu.
Maggid
Reactions::

JK Meets Africare Representatives



President Jakaya Mrisho Kikwete greets Africare Country Representative Sekai Chikowero at State House Dar es Salaam while Africare President Darius Mans(centre) looks on.The two held talks with President Kikwete at State House this morning(Photo: Freddy Maro)
Reactions::

Dhana Ya Matumizi Mabaya Ya Mamlaka: Mchana Hivi, Usiku Je?





Ni pamoja na matumizi ya nguvu kupita kiasi. Ni tatizo linalokua kwa haraka katika jamii yetu kwa sasa. Tumefika mahali, raia mwema unamwogopa polisi au mwanajeshi, iwe mchana au usiku. Unaingiwa na mashaka naye na kujisikia kukosa amani. Kwanini?
Tunaobahatika kutembea maeneo ya nje ya miji tunashuhudia mifano hai kama huo pichani. Pichani raia ndio wanaonekana kufanya kazi ya polisi, wanataka isitumike nguvu pasipo lazima. Kinachoonekana hapo ni udhalilishaji wa polisi kwa raia, lakini hata machoni mwa raia, polisi huyo analidhalilisha jeshi la polisi.
Na tijiulize, kama dereva huyo angekuwa mtu wa hatari, ingewezekana kwa polisi huyo wa usalama barabarani kupanda lori hilo ( picha ya tatu) ili waende wakayamalize kituoni au katikati ya kituo na eneo la tukio? Tutafakari, tujadili.
Reactions::

Dar Es Salaam, Leo Mchana

Reactions::

Kazi Inaendelea...



Katikati ni Mkurugenzi Wa Maendeleo ya Jamii, Bw. Leone B. Msimbe, kushoto ni Bw. George Mangoma, kulia ni Bi. Fatuma Mtalazo. Kikombe changu cha chai ni cha kwanza kushoto! Pichani ni jana asubuhi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Na Watoto.
Reactions::

Dhima Ya Wizara: Maendeleo Ya Jamii, Jinsia Na Watoto

Reactions::

Mheshimiwa Dkt. Asha-Rose Migiro

Reactions::