Subscribe:

Sunday, February 28, 2010

Uhuru Wa Wasichana: " E Bwana Uliye Mbinguni....


.... Tunaomba uwape wasichana wetu uhuru na nguvu ya kufanya maamuzi juu ya miili yao, Amen."
Reactions::

Macho Hayana Pazia!

Reactions::

Yanga, Ah, Bahati Mbaya!

Imeyaaga mashindano ya klabu bingwa barani Afrika kwa kufungwa 1-0 na Wakongo.
Pamoja na kufungwa, Yanga wamejitahidi sana.
Reactions::

Wanahabari Wadau Wa Deutsche Welle



Hawra Shamte na Ramadhan Tua
Reactions::

Saturday, February 27, 2010

JK Audhuria Mazishi Ya Mwakawago Na Pia Arobaini Ya Marehemu Mzee Kawawa




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika ibada ya arobaini ya marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa iliyofanyika nyumbani kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo mchana.Kulia ni mtoto wa Marehemu Vita Kawawa na kushoto ni Shekhe wa Mkoa wa Dar Es salaam Alhaj Musa.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Seif Shariff Hamad wakati wa mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia Marehemu Balozi Daudi Mwakawago yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni.Katikati ni Rais Mstaafu Awamu ya Tatu Benjamin Wiliam Mkapa.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Balozi Daudi Mwakawago wakati wa mazishi ya Mwanasiasa huyo mkongwe yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni(Picha Zote: Freddy Maro)
Reactions::

Mazungumzo Kabla Ya Mazungumzo



Mbele kushoto ni Ute Schaeffer, Mkuu wa Idara ya Afrika Na Mashariki ya Kati Redio Deutsche Welle, Tido Muhando, Mkurugenzi ( TBC) Ananilea Nkya , Mkurugenzi TAMWA na Andrea Schmidt, Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Deutsche Welle.
Reactions::

Ananilea Na Andrea



Ananilea Nkya, Mkrugenzi wa TAMWA na Andrea Schmidt, Mkuu wa Idhaa Ya Kiswahili Redio ya Deutsche Welle katika ufunguzi wa ' DW Punkt' pale Goethe Institut.
Reactions::

Maulid Njema!



Leo ni Maulid. Nawatakia Maulid Njema yenye amani na upendo.
Maggid
Reactions::

USIKU WA MAVAZI( STYLE AND SWAGG NITE) HOUSTON TX @ CLUB SAFARI



MARCH 6 STYLE N SWAGGA ALL LADIES GET UR BEST OUTFIT N WIN $200 FIRST PLACE $100 SECOND PLACE $50 THIRD PLACE
@CLUB SAFARI
SPECIAL LIVE PERFORMANCE FROM LBT(BONGO FINEST).
AB(BLACK SENSATION).
GIE MANIE(TZ FINEST)
Reactions::

Yanga Kufunga kazi Leo

Reactions::

Ban Ki Moon Amwomboleza Balozi Daudi Mwakawago



BAN KI MOON AMWOMBOLEZA BALOZI DAUDI MWAKAWAGO

Na Mwandishi Maalum


Umoja wa Mataifa - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema ,amepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kufariki kwa aliyewahi kuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, nchini Sierra Leone, Balozi Daudi Ngalautwa Mwakawago.

Ban Ki Moon ameyasema hayo katika salamu zake za rambirambi ambazo amemtumia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe kufuatia kifo cha Balozi Mstaafu Daudi Mwakawago.

Katika salamu zake , Katibu Mkuu , amemuelezea Balozi Mwakawago kama mtumishi na kiongozi aliyetoa mchango mkubwa sana katika mchakato wa kutafuta maridhiano nchini Sierra Leone.

Aidha Ban Ki Moon anasema, Balozi Mwakawago wakati wa uhai wake aliyatekeleza majukumu yake kwa umakini na uhodari mkubwa. Na kwamba aliitumikia nchi yake Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jumuia ya Kimataifa kwa heshima kubwa.

“Wakati tunapotafakari utumishi wa kutukuka wa marehemu Balozi Daudi Mwakawago kwa nchi yake na kwa Jumuia ya Kimataifa , tuna kila sababu ya kuwa na shukrani, si kwaajili ya yale aliyoifanyika nchi yake lakini pia kwa aliyoufanyia Umoja wa Mataifa. Kuondoka kwake kumeacha pengo kwa familia yake na halikadhalika kwa wale wote waliomfahamu. Tafadhali pokea salamu zangu za rambirambi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Familia ya Marehemu Balozi Daudi Ngalautwa Mwakawago”.
Reactions::

Tafuta Visivyo Vya Kawaida Katika Picha 3 Za Kariakoo





Zote tatu nimezipiga Kariakoo, Alhamisi ya juzi majira ya saa kumi na moja jioni.
Reactions::

Hapa Zilibaki Sekunde Tu!




Mikumi, saa kumi na mbili na nusu alfajiri, Februari 20. Nikiwa peke yangu ndani ya gari nilisogea umbali wa mita tano kutoka alipo simba dume huyo pichani. Nikachukua kamera na kuanza kumpiga picha. Mara nikamwona simba aliyejawa na hasira. Alinitolea macho makali ( picha ya kwanza juu). Sekunde iliyofuata akanifokea. Mikono ilinitetemeka na picha hiyo ya pili ika-shake. Maamuzi yangu yakawa ya sekunde pia. Nikafunga kioo huku nikiondoa gari mahali hapo kwa haraka. Wataalamu wameniambia, kile ambacho kingeweza kufuata katika sekunde zilizofuatia ( kama ningebaki mahali pale). Ni kwa simba yule kunirukia kwa hasira, maana nilikuwa karibu nae mno. Kioo cha gari kilichofungwa kisingesaidia. Duniani kuna mengi ya kujifunza.
Reactions::

Obama Na Nanihii, Kariakoo!

Reactions::

Kila La Heri Dar Young Africans!



Fuateni nyayo za Simba. Mwaka 1979 Mufulira walituchapa 4-0 Dar. Tulipokwenda Lusaka tukawafunga 5-0 mbele ya KK ( Rais Keneth Kaunda) wao. Mpira una miujiza yake. Inawezekana kwa Yanga kufanya miujiza Kinshasa leo Jumamosi. Kuna simba tunaofurahia pia Yanga ikishinda. Huwa tunatoka kwenye boksi la utani.
Reactions::

Tungependa JK Atukabidhi Kombe La Ubingwa Mwaka Huu!



Kapuya ni Simba mwenzetu, hainogi! Hakika mwaka huu ni raha tupu, kuanzia Mchafukoge, Msimbazi hadi kwenye tawi la wanaSimba wa Igoma Mwanza. Na Yanga hawaishiwi maneno, kama kawaida ya watani zetu!
Reactions::

JK Aifariji Familia Ya Marehemu Balozi Daudi Mwakawago




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia marehemu Balozi Daudi Mwakawago nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu.





Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi.Daisy Mwakawago mjane wa Marehemu Balozi Daudi Mwakawago aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam.Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam.Rais alikwenda nyumbani kwa marehemu kuifariji familia yake.Marehemu ameacha mjane na watoto watatu Lulu Mwakawago,Kie Mwakawago na Mtage Mwakawago (Picha: Freddy Maro)
Reactions::

Friday, February 26, 2010

Simba Kujipima Ubavu Na Zesco Kesho


Wachezaji wa simba Musa Hassani Mgosi na Jabir Aziz wakishangilia mojawapo ya mabao msimu huu.
Baada ya juzi kutoka sare ya 1-1 na African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara, Simba itashuka uwanjani kesho kucheza na Zesco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba na Zesco zote zinajiandaa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Simba itaanza kwa kucheza na mshindi kati ya Lengthen ya Zimbabwe na AS Adema ya Madagascar.
Reactions::

Yanga Kusuka Au Kunyoa Kesho


mchezaji machachali wa yanga m, mrisho ngasa aikiwa katika moja wapo ya harakati za uwanjani.
Kesho Yanga itapambana na FC Lupopo katika mechi ya pili ya kombe la klabu bingwa barani Africa ambapo Yanga ili iweze kusonga mbele inahitaji mabao 2-0. Mechi ya kwanza ilifanyika Daresalaam ambapo yanga ililala kwa bao 3-2
Reactions::

Mambo Ya Kipanya

Reactions::

Congo Street



Kariakoo, jana mchana.
Reactions::

Thursday, February 25, 2010

Ni Kweli Kuwa Sheria Ya Kumiliki Silaha Iko Kimya Juu Ya Silaha Za Jadi?


Reactions::

" Hii Imetulia Madam!"




Linea, kutoka Sweden. Kariakoo leo mchana.
Reactions::

JK Kwenye Mkutano Wa TAKUKURU




Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo unaofanyika mjini Mwanza leo asubuhi.





Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia viongozi waandamizi wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo mjini Mwanza leo asubuhi.



Baadhi ya maafisa waandamizi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo mjini Mwanza leo asubuhi katika ukumbi wa Benki Kuu(Picha: Freddy Maro).
Reactions::

Uzoefu Wa Kusisimua!





Karimjee Hall jana usiku. Unapokaa hapo mbele na kuwaangalia watu zaidi ya mia mbili mbele yako kuna ya kutafakari. Namwona Mheshimiwa Jussa Ismail ( CUF), Prince Bagenda na wengine wengi wenye majina makubwa wakiwa tayari kunisikiliza mimi pia, kwa lugha ya KiNgereza. Nilio nao mezani ni ' tembo wa habari'. Ni magwiji.Jenerali Ulimwengu, Tido Mhando, Ananilea Nkya na Ayoub Rioba. Najisemea moyoni, ninacho cha kuongea, ndio maana nimeitwa nikae hapa mbele. Sina cha kuhofia.Walio mbele yangu hawawezi kuwa ni watu hatari kama simba yule wa Mikumi niliyekutana nae uso kwa uso! Naam.Kuna mengi nimejifunza jioni ya jana. Ni uzoefu wa kusisimua.
Reactions::

JK Afungua Mkutano Wa TAKUKURU MWANZA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia viongozi waandamizi wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo mjini Mwanza leo asubuhi. ( Picha: Freddy Maro)
Reactions::

Alikotokea Profesa Born Again Pagan na Wenzake:



Msomaji mpendwa, tumeishaona ya ujumbe mfupi uliotilia mkazo umuhimu kwa wale tuliopata nafasi ya kusomeshwa bure (au kusoma hapo mashuleni kwetu) kuweza kuanzisha alumna kwa shule zetu tulikopitia (msingi, kati na sekondari). Iatubidi tuunde uwezekano wa kuzisaidia, ikiwa ni pamoja na wastaafu wake kujitolea kufundisha, kila watembeleapo shule hizo. Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Umoja Wa Mataifa Wajadili Tishio La Mtandao Wa Uhalifu Kimataifa




Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akishiriki kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kilichokuwa kikijadili tishio la Mtandao wa Uhalifu wa Kimataifa kwa usalama, amani na maendeleo ya Mataifa. ( Picha kwa hisani ya Umoja Wa Mataifa)




Na Mwandishi Maalum

New York-Mtandao wa uhalifu wa kimataifa ambao umeelezwa kwamba sasa ni tishio lililodhahiri kwa maendeleo na usalama wa dunia. Unajijenga kwa kasi kubwa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na meneo ya Afrika ya Magharibi, Kati na Mashariki.

Na kwa sababu ya tishio hilo, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimetakiwa kuongeza kasi ya ushirikiano kwa kubadilishana taarifa mbalimbali zikiwamo za kitelejesia, kuongeza ulinzi mipakani, pamoja na kuimarisha utawala wa sheria na kupiga vita rushwa.

Bw. Antonio Maria Costa, Mkurugenzi Mtendaji Katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu (UNODC) , ameonya kuwa mtandao wa uhalifu wa kimataifa unaohusisha biashara ya dawa za kulevya, silaha na ugaidi na utekaji nyara ina uwezo mkubwa wa kifedha na matumizi ya teknolojia za kisasa za mawasiliano kiasi kwamba si rahisi kwa nchi moja moja kukabiliana nao.

Alikuwa akiwasilisha taarifa ya ofisi yake mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuhusu mwenendo wa mtandao wa uhalifu wa kimataifa na tishio lake dhidi ya maendeleo, usalama na ustawi wa mataifa.

Akasema njia nyingine ya kudhibiti mitandao hiyo ya uhalifu wa kimataifa ni kupunguza nguvu zao za kifedha kwa kumata na kutaifa mali zao na kuziba mianya ya rushwa na fedha chafu, pamoja na kuzisaidia nchi za Afrika kuimarisha vyombo vyao ya sheria na kujikwamua na umaskini.

Katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, Mkurugenzi Mtendaji huyo ameeleza kwamba, kwa kutumia uwezo wao wa kifedha, wahalifu hao wa kimataifa wameweza kujipenyeza na kuweka mitandao yao hususani katika nchi maskini za Afrika , zenye migororo, zisizokuwa na utawala madhubuti unaozingatia sheria na zenye kukumbatia rushwa.

Akasema kuwa wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya kwa kutumia faida kubwa wanayopata kupitia biashara hiyo, huangalia wapi penye udhaifu na kujipenyeza kwa kutoa rushwa, kuwatumia vijana wasio kuwa na ajira kuleta vurugu na machafuko katika nchi zao na hata kuzipindua serikali halali.

Akionyesha uwezo mkubwa wa kifedha wa mtandao wa biashara ya dawa za kulevya, Bw. Antonio Mario Cost anasema .

“ Bajeti ya matumizi ya kawaida ya ofisi yangu ni asilimia moja ya bajeti ya Umoja wa Mataifa, ambayo nayo ni chini ya asilimia moja ya faida wanayoipata wafanyabiashara wa kimataifa wa dawa za kulevya ambayo ni Dola 320 bilioni kwa mwaka”.

Akatoa mfano mwingine kwa kusema “Mstari mmoja wa mnuso wa Kokeini anaonusa mtumiaji wa kule Ulaya faida yake inanunua risasi 100 za AK-47 kule Afrika Magharibi. Sasa zidisha mara tani 850 za kokeini kwa mwaka utaona ni kama vile kumshindanisha Daudi na Goliath”

Akichangia majadiliano hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema Jumuia ya Kimataifa kupitia Baraza Kuu la Usalama inatakiwa kujipanga upya kwa kubuni mbinu na mikakati ya kukabiliana na tishio hilo.

Akasisitiza Umoja wa Mataifa hauwezi kufumba macho na kujifanya kama vile haioni tishio la uhalifu wa kimataifa dhidi ya usalama na maendeleo.

“Hatuwezi kuzima moto kwa kutumia moto, wahalifu hawa wana mbinu nyingi na za kisasa ambazo hata hatuwezi kushindana nao kama kila nchi itapigana vita hii kivyake vyake. Lazima tukusanye nguvu zetu kama jumuia na tukidhamiria tunaweza” akasisitiza Ban Ki Moon.

Akasisitiza kuwa mataifa hayana njia mbadala zaidi ya kujijengea mazingira ya kuaminiana na kushirikiana kwa sababu kila nchi inaathirika au itaathirika na janga hili.

Mwisho mwa mkutano huo,wajumbe 15 wa Baraza Kuu la Usalama walikubaliana kwamba lazima sasa jumuia ya kimataifa iwajibike kwa pamoja katika kukabiliana na tatizo hilo.
Reactions::

InterMilan Yaibanjua Chelsea Kwa Mabao 2-1


Wachezaji wa Internationale ya Italia wakiwa katika harakatui za ushindi jana usiku
Reactions::

Lyon Yaibana Simba Mbavu.


Mchezaji kiungo wa timu ya Simba, Hilary Echesa (kushoto) akichuana na vicent barnabas wa African Lyon katika mechi ya ligi kuu iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.
AFRICAN Lyon imeungana na Kagera Sugar kutibua rekodi ya Simba ya ushindi wa mechi zote msimu huu baada ya kuibana na kutoka sare ya bao 1-1.

Kwa matokeo hayo, Simba wamezidi kucheleweshewa hafla yao ya ubingwa ambayo ilihitaji ushindi wa mechi mbili pekee kabla ya mechi ya jana.

Katika mchezo huo, Lyon, walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji Robert Ssentongo katika dakika ya 5 baada ya kupata krosi safi ya Hamis Shengo iliyomchanganya kipa Juma Kaseja wa Simba.
katika dakika ya 81, Mgosi aliisawazishia timu yake baada ya kupiga shuti kali lililompita kipa wa Lyon, Ivo Mapunda.
Reactions::

Waziri Wasira Apandishwa Kizimbani


WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira(pichani) leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akidaiwa sh milioni 90 kwa kumdhalilisha na kumsumbua Mkurugenzi wa Kampuni ya Cargo Building, Andrew Ngai mtandao huu umeelezwa kuwa.Zaidi soma ..http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Nimeshiriki Panel Discussions Karimjee Hall



Jana jioni. Nilikuwa ni mmoja wa wazungumzumzaji. Topic ni ' The role of media prior to general election 2010. Kulikuwa na Jenerali Ulimwengu. Tido Mhando, Ananilea Nkya, Ayoub Rioba na mimi. Naam. Nilifurahia sana. Pichani ni Jenerali Ulimwengu na Tido Mhando, muda mfupi kabla ya shughuli yenyewe kuanza. Mjadala ulichukua saa mbili na robo. Uliandaliwa na Redio Ujerumani na Inwent Tanzania.
Reactions::

Watu Walikuwa Wengi!



Karimjee Hall, jana jioni.
Reactions::

Ismail Jussa



Kulia, alikuwa mmoja wa wasikilizaji pale Karimjee Hall jana jioni. Katikati ni Tido Mhando na kushoto ni Ayoub Rioba.
Reactions::

Wednesday, February 24, 2010

Tanzania Kuendelea Kushiriki Ulinzi Wa Amani Umoja Wa Mataifa- Balozi Mahiga




Na Mwandishi Maalum
New York-Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kushiriki operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, licha ya kwamba operesheni hizo hivi sasa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Msisitizo huo umetolewa na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Augustine Mahiga wakati alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Kamati Maalumu inayohusika na Operesheni za Ulinzi wa Amani maarufu kama C-34

Mkutano wa Kamati hiyo unafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na wajumbe wake ni kutoka nchi wanachama wa UN wanaochangia operesheni za ulinzi kwa kutoa wanajeshi na polisi.

Balozi Mahiga amewaeleza wajumbe wa mkutano huo, kwamba Tanzania ambayo ni mgeni katika ushiriki wa operesheni hizo, kwa maana ya kuchangia wanajeshi na polisi, inajiunga katika jukumu hilo katika kipindi ambacho ulinzi wa amani hivi sasa unakabiliwa na changamoto nyingi na kubwa.

Kwa mfano anataja baadhi ya changamoto hizo, kuwa ni kubadilika kwa uasilia wa mwenenzo mzima wa vita kutoka ule wa mapigano kati ya taifa moja na jingine na kuwa vile vinavyopiganwa na makundi yanayohasimiana ndani ya nchi husika tena yakishindana kwa silaha nzito na kali.

“ Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa hivi sasa wanakabiliwa na changamoto tofauti kabisa na zilizo nje ya misingi na majukumu yanayojulikana na ambayo tayari yameainishwa katika mfumo mzima wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa” akasisitiza.

Na kuongeza .“ na sisi Tanzania tunaingia katika jukumu hili tukiwa ni wageni, bado tu wapya katika uchangiaji wa wanajeshi na polisi wetu na kwa kweli ushiriki wetu ni mdogo, kwa sasa tupo katika misheni tano tukiwa na idadi ndogo ya walinzi wa amani. Na tunaingia katika kipindi ambacho Umoja wa Mataifa na taasisi zake zimo katika majadiliano ya kina kuhusu changamoto na mwenendo mzima wa operesheni hizi za ulinzi wa Amani” anaeleza Mahiga

Akasema kuwa Tanzania iko tayari kukabiliana na changamoto hizo na kueleza kuwa ni hivi karibuni tu Tanzania imekamilisha zoezi la kupeleka kwa mara ya kwanza Bataliani yenye wanajeshi 875 katika misheni ya kulinda amani huko Darfur nchini Sudan chini ya mwamvuli wa jeshi la mseto la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID).

Balozi Mahiga akatumia fursa hiyo kutoa shukrani za serikali ya Tanzania kwa Umoja wa Mataifa na wahisani wengine waliofanikisha maandalizi ya ushiriki wa Tanzania huko Darfur.

Kundi la mwisho la wanajeshi 600 wa TANZBATT-1 waliondoka nchini kati ya tarehe kumi na moja na kumi na tatu mwezi wa huu wa pili kwenda Darfur ambako wamejiunga na wenzao ma- injinia na maafisa 275 waliokuwa wametangulia kuaanda kambi ya kufikia wanajeshi hao

Pamoja na ushiriki wa Tanzania huko Darfur, Balozi Mahiga pia alibainisha kuwa Tanzania inaendelea na maandalizi ya kupelekea wanajeshi wake 200 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Misheni ya MONUC ambako watakwenda kutoka mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

Katika hatua nyingie, Tanzania imesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa wa kuendelea kuijengea uwezo Umoja wa Afrika, ili umoja huo uweze kujizatiti katika kuzuia machafuko, kuyatafutia ufumbuzi machafuko na ujenzi wa amani.

Akasema kuwa kwa ujumla umoja wa Afrika unaridhishwa na mwenendo wa ushirikiano uliopo kati yake ya Umoja wa Mataifa. Lakini anasema Tanzania inaamini kwamba kuna kila sababu ya kuongeza kasi ya ushirikiano huo, kwa kile alichosema ikiwa Afrika itawezeshwa kukabiliana na migogoro siyo tu itapunguza gharama za operesheni hizo. Lakini pia itapunguza urasimu na mlolongo mrefu wa maandalizi ya misheni za ulinzi.
Reactions::

Easter Conference



Wadau,
Natumaini kabisa hamjambo na Mungu anawasaidia katika mambo yote. Ninaomba mnisaidie kuweka tangazo hili katika blog zenu na Mungu awabariki sana.

Tangazo ni hili hapa na nimetuma pia poster kwa ajili ya kusupport tangazo.

Wadau wote mlioko Marekani mnakaribishwa kwenye semina kubwa ya sikukuu ya Pasaka yenye nguvu za Mungu zenye kuleta mabadiliko maishani iliyoandaliwa na Mchungaji Pastor Abihudi na Catherine Abihudi. Semina hii itafanyika Kansas City, MO.

Wahudumu ni Mchungaji Charles and Catherine Abihudi(Wenyeji), Pastor Kagumba, Emmy Ntwina, Ben Maira(UK) na Dr. Shallua.

Unaweza kujiandikisha kwenye huu mtandao hapa, www.wakati.net/events.htm. Gharama za mkutano ni $50 kwa siku mbili, Ijumaa na Jumamosi. Jumapili mchana semina itakuwa imeisha. Gharama hii ni ya malazi na chakula. Tafadhali jiandikishe kabla ya March 20, 2010.
Address ni
Residence Inn, Marriot
10300 North Ambassador Dr
Kansas City, MO 64153


Kwa maelezo zaidi piga hizi namba hapa
417 423 0591
417 837 9340
417 619 4951

--
Musa H M Shila
Reactions::