Subscribe:

Wednesday, March 31, 2010

JK Aweka Jiwe La Msingi



Rais Jakaya Mrisho Kikwete(wanne kushoto) na Balozi wa China nchini Bwana Liu Xinsheng(watatu kushoto) wakiweka udongo katika jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa Taasisi ya tiba ya moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH leo asubuhi.Wengine katika picha ni Waziri wa Afya Profesa David Mwakyusa(watano kushoto) na kuli ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bwana Adolar Mapunda, wapili kushoto ni kiongozi wa ujumbe wa Jamhuri ya watu wa China Bwana Sun Liang (Picha:Freddy Maro)
Reactions::

TANGAZO LA MSIBA

BOSCO SAFARI MOSHA WA GLASGOW SCOTLAND.
ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MDOGO ABOUD NDESAMOKE MSOKE,
KILICHOTOKEA HUKO DAR-ES-SALAAM TANZANIA.
JANA MCHANA, MIPANGO YA MAZISHI YANAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA.
HABARI HIZI ZIWAFIKIE UKOO WA MOSHA WA MAREKANI, FAMILIA YA DR MOSHA WA
SAVANA-LA -MAR,JAMAICA, UKOO WA MOSHA POPOTE PALE WALIPO, NAOMBA UNITUNDIKIE KWENYE BLOG
YETU INAYOSOMWA POPOTE ULIMWENGUNI. NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI.
AKSANTE
Reactions::

Michuzi Aendeleza Libeneke Ughaibuni



Ankal akiwa katika ofisi za Quality Machinery and Truck Commercial Ltd ya mji wa kusoma ambako alikutana wakurugenzi wake Mohamed Hijja (aliyekaa) na Athumani Mloka (kuume). Shoto ni mdau Gardol. hawa wadau ni mabingwa wa kusafirisha aina yoyote ya magari makubwa na matrekta na magreda na hata meli na treni popote duniani. wanapatikana katika email ya qmtcommercial@bconnect.com
na namba ya simu ya chap chap ni +441 1895 98614
Reactions::

Wapi Hapa; Kanda Za Nyanda Za Juu Kusini?

Reactions::

Usafiri Huu!



Nyololo, Mafinga, hivi karibuni.
Reactions::

Born Again Pagan - 'Sir' George Kahama Ni Utani Tu!




Hiyo ya Kahama ni ya utani, kama ilivyo kwa Charles Njonjo (m-Kenya wa kwanza kuwa Mshauri Mkuu wa Sheria).

Kidogo inavalishwa ya kilemba cha kuwa "knighted" (lakini kwa utani tu).

Charles Njonjo alipenda sana u-British, kiasi cha wengi kumtania "Sir".

Na huku kwetu, pia, kulikuwa na huyo George Clement Kahama. Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa amkipenda sana kumtania Kahama, kama "Sir George"!

Kwa kutaja baadhi tu, Sir Tito Winyi wa Toro (Omukama wa Toro) Sir Edward Muteesa II (Kabaka wa Buganda), ma-Bohara Sir Yusufali Jivanjee na Sir Tayebali Karimjee Jivanjee Tanganyika) na Sayyid Sir Jamshid bin Abdullah Al Said (Sultan wa Zanzibar) ni sawa na "knighthoods” za Waingereza.

BAP
Reactions::

Tuesday, March 30, 2010

Wamechagua Kutuwakilisha Umoja Wa Mataifa



Kila mwaka wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mataifa mbalimbali, hukusanyika na kuunda Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (Model United Nations) Baraza hili ambalo ni la kuigiza lakini linalozingatia na kufuata sheria na taratibu zote za uendeleshaji wa Baraza Kuu halisia, huwapa fursa wanafunzi hao kuvaa viatu vya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa.


Kupitia Baraza lao, wanafunzi hao huendesha mijadala katika Nyanja mbalimbali kama vile masuala ya uchumi, mabadiliko ya tabia nchi, malengo ya maendeleo ya millennia, nafasi ya nchi zinazoendelea, ulinzi na usalama n.k. wanafunzi hawa hujenga hoja na kuzitetea hoja hizo katika mijadala hiyo kuligana ‘interest’ ya nchi wanayoiwakilisha.


Kupitia mijadala hiyo, wanafunzi hao hujaribu kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa, kwa kuandaa rasimu za maazimio na

kuzijadilia rasimu hizo na hatimaye kuzipitisha iwe kwa kuipigia kura au kwa kuipitisha kwa kauli moja.

Na ili kufanikisha mijadala ya baraza hilo, wanafunzi hao hufanya utafiti wa nchi zile wanazotaka kuziwakilisha katika baraza hilo pamoja na mada na ajenda mbalimbali.




MAELEZO YA PICHA


Pichani ni wanafuzi kutoka mataifa mbalimbali ambao waliichagua Tanzania kama nchi wanayoiwakilisha katika Baraza hilo. Na ili waifanye kazi hiyo vema, wanafunzi hao waliutembelea Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ili kujifunza na kupata uelewa zaidi kuhusu historia ya Tanzania, matatizo, mafanikio , changamoto, na namna gani Tanzania inavyoutumia Umoja Mataifa kusukuma ajenda zake mbalimbali. Aliyevaa suti nyekundu ni Afisa Ubalozi Bi Joyce Kafanabo ambaye alitoa maelezo na kujibu maswali mbalimbali ya wanafunzi hao, kwa niaba ya Balozi.
Reactions::

" E Bwana, Tutakula Wapi Pasaka?"




Na ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, `` E nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.'' Wakamwuliza, ``Tukaandae wapi?''Yesu akawajibu, ``Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni huyo huyo mpaka kwenye nyumba atakayoingia. Kisha mwambieni mwenye nyumba; Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani. Chumba kilicho na fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.''

Basi, wakaenda wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Hivyo, wakaandaa chakula cha Pasaka.Wakati ulipofika Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Kisha akawaambia ``Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.'' Hapo Yesu akapokea kikombe cha divai, akashukuru akisema, ``Chukueni mnywe wote. Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.'' Alitamka Yesu.( Wanazuoni mnaweza kunikosoa pale nilipokosea katika kukariri hayo)

Pichani juu nikishiriki kunywa uji wa saa nne pamoja na wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Ikwiriri mwezi Machi mwaka jana.
Reactions::

Mubelwa Bandio: "Sote Twaiandikia Jamii"

Amani, Heshima na Upendo kwenu.
Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo.
Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo.
Nafurahi kuwasiliana na kila mmoja wetu kuweza kuwaza changamoto zilizo mbele yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii na kisha tujiulize kama tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu. Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (http://kamalaluta.blogspot.com/2009/07/swali-kwa-wenye-blogu.html) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blog zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (http://udadisi.blogspot.com/2009/08/blogu-zinachochea-au-zinafifisha.html). Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.
Lakini kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ambalo ni JAMII. Awekaye picha anataka kuionesha jamii alichokiona, ahabarishaye anataka kuihabarisha jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye biashara anataka jamii ijue ilipo huduma. Afunzaye mapishi, mitandao, mavwazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.
Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.
Lakini je, mwaka huu ambao unamaliza robo yake ya kwanza wiki hii unaonekana kuwa hatua gani kwetu? Tumeshuhudia KUTHAMINIKA KWA KAZI ZA BLOGGERS kwa aina mbalimbali.
Tuliona wenzetu wakitunukiwa vyeti vya kuthamini kazi zao, tumesikia wengine (kupitia utambulisho wa blog zao) wamepata nafasi ya kushiriki vipindi vya idhaa za kimataifa kufanya uchambuzi wa habari. Hivi juzi tumemuona Kaka Michuzi akishiriki Diaspora huko London kwa nafasi yake kama blogger. Hizi ni chachu kwetu kuwa kuna kuonekana mchango wa kile tufanyacho na pia kuna kukua kwa ueleweka wa kazi zetu.
Ninalowaza ni VIPI TUNAWEZA KUWEKA NGUVU NA JITIHADA ZETU PAMOJA KUWEZA KUITUMIKIA VEMA JAMII?
Mafanikio ya blogger mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA na tunalostahili kufanya ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo.

Tunapoianza robo ya pii ya mwaka 2010, tuangalie nyuma na kujiuliza, robo ya mwaka inakatika....Tumesonga mbele ama nyuma??
Na hii iwe CHANGAMOTO YETU sote

Baraka kwenu nyote

http://www.changamotoyetu.blogspot.com
Reactions::

Bongo Kila Kitu Kinawezekana......



Na kinyume chake!
Reactions::

Mgambo Wa Vita!



Nyololo, Iringa
Reactions::

Kuuliza Si Ujinga: Mzee Wetu Sir George Kahama



Habari ya leo Kaka Maggid,
nilikuwa natafuta sana hii habari kuhusu mzee wetu Sir George Kahama...nadhani wewe waweza kunisaidia. Ninapenda kujua ni lini Mzee Kahama alipata hiyo title ya Sir... na lifanya kitu gani hadi kupata..pia nadhani ni mtanzania pekee mwenye cheo cha '' SIR''.
Nitashukuru sana kwa maelezo yako

Nikutakie kazi njema na siku njema pia.

dennis
Reactions::

Mjumbe Hauawi: Uonevu

( Naiwasilisha kama ilivyowasilishwa)


habari yako kaka mjengwa.naitwa bw.zawadi masoud. ni fundi simu hapa kahama.hivi karibuni nimeponea chupuchupu kupewa kesi ya kubaka.mpaka hivi naandika hii email kama siamini vile kama nimeponea katika tundu la sindano.

mwaka mmoja ulio pita alikuja mteja mmoja ofisini kwangu akitaka afungiwe kioo kwenye sim yake iliyo imevunja koo.scleen.nilimpa galama za kumfungia kioo kingine ambayo ni 30 000. na baada ya kumaliza kufunga kioo alidai pesa hana kwa muda ule mpaka kesho ndo angekuja kulipia kisha tumpe simu yake.tokea siku hiyo huyo mama akawa hafiki tena hapo ofisini kwangu,na nikionana nae mtaani ananiahidi kwamba atakuja lakini wapi mpaka hii juzi ambapo kaja na kuzua mambo ya ajabu.

mida kati ya saa 11 na 12 jioni alikuja na kuomba simu yake nami nikampa anakuomba pesa.alichosema nikuwa pesa hana pengine tumpe simu pesa ataleta,kitu ambacho nilipinga kutokana na kuwa nje ya makubaliano.hata hivyo huyu mama alikuwa kama amekuja kwa jambo moja tu,kucukua simu yake bila malipo.kwani alidai tutoe kioo chetu tumpe simu yake.pamoja na kumwambia kwamba takuwa ametufanyisha kazi mala mbili yaani kujenga kisha kubomoa,hilo hakulijali nami ili nilazimu kutoa kioo changu kuepusha kelele.

kumbe kitendo hicho tu ndio ikawa chanzo cha matatizo juu yangu.

kifupi huyo mama ilifikia hatua ya kupiga simu polisi akidai kafungiwa ndani ya ofisi yangu huku tukijaribu kumbaka polisi walikuja na kutukamata mpaka kituo cha polisi ambapo mipango waliifanya haraka haraka ili tupelekwe mahakamani
hata hivyo ocd wilaya alibaini kuwa tulipakaziwa.
kaka mjengwa nimeandika kwa ufupi sana ila kama itakuwa ni habari nzuri naweza nikaiandika vizuri kisha ukalewa namna gani polisi walivyo shilikiana na huyo mama kutuaibisha.pamoja na matusi mbali mbali ya tuliyo tukanwa.na jinsi gani tulinusulika

nina ushahidi wa maandishi kutoka kwa huyo mama na ushahidi wa kukamatwa kwangu
mbaya zaidi huyu mama anajitapa kwamba mme wake ni polisi kitu kinacho nipa hofu asije mme wake akatupa kesi mbaya zaidi ya kubaka.

namba zangu ni 0754 056019, 0783 056019, 0658 056019,

Nashuru kwa kunisoma.
Reactions::

Monday, March 29, 2010

" Ndugu Mjengwa Isome Vizuri Historia Ya Uganda!"




Ndugu Mjengwa,
Samahani kuchukua muda wa kutoa ufafanuzi wa kipengere kidogo katika habari yako au makala juu ya demokrasia. Ninakuomba uisome vizuri historia ya Uganda na baada ya hapo toa tathimini ya viongozi waliotangulia. Kwa kifupi, Waingereza waliacha uhuru wa Uganda kwa kabila moja tu nalo ni 'Baganda' (sawa kwa Z'bwe yaani chini ya Smith) na mfalme wao ndio aliyekuwa rais. Hivyo basi, Obote aliteuliwa na mfalme kuwa waziri mkuu. Kama ilivyokuwa kwa Tanganyika na Zimbabwe, mawaziri wakuu yaani Nyerere, na Mugabe waliondoa mfumo wa waziri mkuu kama mtendeji mkuu wa serikari na badala yake 'ceremonial president' ndio akachukua rungu. Na hili liko wazi, Uganda kama nchi haikuwa na mfumo wa kifalme ispokuwa kabila moja tu yaani Wa-baganda. Ikiwa Obote alilewa madaraka basi nitashawishika pia kuwa Nyerere na Mugabe nao walilewa madaraka (nafahamu suala la Mugabe ni exception). Ikiwa ndivyo basi wengi walilewa madaraka. La msingi ni kwamba ni katika utawala wa Obote (awamu ya kwanza) juhudi za kujenga misingi ya utaifa zilifanyika yaani kuondoa dhana kwamba Uganda si 'baganda' tu na makabila mengine ni kama vivuli. Ni katika kipindi cha Obote ndipo unapoweza kuona maendeleo yote ya Uganda ya leo, yaani ujenzi wa hospitali kuu ya Mulago, chuo cka Makerere, barabara za lami toka Malaba hadi Gulu, mbarara, na bandari ndipo ulipofanyika. Kumbuka misaada kutoka kwa wafadhili hadi 1985 ilikuwa ni $6 bilioni tu. Je unataka kumlinganisha Obote na Musevelini ambaye aliharibu barabara kwa kupitisha magari ya kivita, na leo hii kuzikarabati barabara alizoharibu ndio tuite maendeleo? Je zaidi ya taasisi alizoacha Obote nini zaidi kilichoongezeka? Kumbuka kutoka 1985 hadi leo Uganda imepokea misaada ya kiasi cha $22 billion kutoka nje na bado hakuna kinachoonekana. Katika kutimiza miaka 23 ya NRM mwaka 2009, chama hicho kiorodhesha mafanikio nane (8) tu! Je ni kweli ndani ya miaka 23 ni hayo tu! Vurugu zote zinazotokea Uganda ni kutokana na kwamba misingi ya utaifa aliyotaka kuijenga Obote haikufanikiwa au ilivurugwa na kabila moja. Kumbuka palikuwa na shule nzuri za serikali kipindi cha Obote ambazo hazikuwa Kampala tu, bali Lango, Arua, Soroti, hadi Jinja. Leo hii chini ya Museverini elimu nzuri ipo Kampala tu. Na ndio maana vijana wetu toka Tanzania wanaishia katika shule za Kampala na vitongoji vyake. Mfano ni kwamba katika matokeo ya kidato cha sita ya kitaifa, wanafunzi waliofanya mitihani na kupata alama 3A's (A,A,A), 90 walitoka kwenye wilaya tatu za Kampala na labda 6 sehemu nyingine za nchi. Ukikutana na kizazi cha Obote (walioshuhudia) utawala wake watakuambia kwamba wao ni kizazi cha 'nationalist' kwa maana maana walikuwa wakisoma kila pembe ya nchi na kwamba wanao marafiki kila kona pasipo suala ya ukabila kuweka mbele.
Nitakuja suala la Iddi Amini, naye singependa historia imu-hukumu vibaya. Tatizo la huyo bwana ni kwamba licha ya kuwa na mipango mizuri, hakuwa na fedha za kutekeleza maana wafadhili walimpa kisogo. Mfano mzuri ni kuwa master plan ya jiji la Kampala ilichorwa kipindi chake, na leo hii miaka kadhaa kupita kuna barabara imejengwa inaitwa 'northern bypass', architect wake ni Idd Amin! Lakini bado vile vile imechukuwa miaka 10 kuijenga (5-7kms) na gharama zake mara kumi ya ilivyopangwa. Ninatamani angalau barabara hiyo ingepewa jina lake maadam bado haijafunguliwa rasmi.

Kuhusu suala la Wa-baganda kumiminika barabarani baada ya Amini kuchukua madaraka, ni kwamba walidhani kwamba angelikuwa ni kibaraka wa kabila moja yaani 'Baganda'. Ukweli ni kwamba alianza kwa kufanya hivyo na mifano ni mingi, kwanza, alifanikisha kuurejesha mwili wa mfalme wa Buganda kutoka Uingereza. Hiyo ilimpa 'credit' kubwa sana. Pili, alipokwenda Canada kwenye mkutano, Iddi Amini akiwa si m-baganda, na kutokana na elimu yake kuwa sio kubwa ya kuweza kujieleza kwa ufasaha kwa lugha ya kiingereza, badala yake alizungumza 'ki-baganda'. Baada ya hapo ikawa kama kumkaribisha twiga kwenye kibanda ili apunge mvua, mwisho wake ni kukuondoa mwenye kibanda. Yaliyo mtokea Amini, ndio yanayomtokea Museverini sasa, maana naye aliingizwa madarakani kwa 'backing' ya wa-baganda wakidhani kwamba atabaki kuwa ni kibaraka wao. La hasha! mambo hayajaenda hivyo. Lakini tofauti kubwa kati ya Obote, Amini na Museverini, hakuna mtu zaidi ya Obote ambaye alijaribu kutaka kujenga misingi ya utaifa. Sasa hivi kinachotekea ni kuigawa Uganda kutokana na makabila. Na hii ni kuanzia na kuwa na waziri karibu kila kabila, na kila kabila kuwa na wilaya yake, kila kabila kuwa mfalme wao hata yale makabila ambayo hayajawahi kuwa na mfalme yanashauriwa yafanya hivyo, . Pia, ushawishi wa vikabila vidogo kujitoa kuwa chini ya himaya kubwa kama ya wa-baganda ambapo kihistoria imekuwa hivyo.
Ninaweza kuandika mengi lakini la msingi, aliyelewa madaraka ni nani kati ya hao watatu Obote, Amini na Museverini? Kumbuka Museverini ameomba 'ngwe' nyingine tena ya uraisi.
Tuendelee kubadilishana mawazo.
Mnyalu
Reactions::

JK Apokea Misaada Kutoka China






MAELEZO YA PICHA

1. Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete mipira ya soka na vifaa vingine ikiwemo baiskeli,pikipiki, chupa za maji na mshine za kushonea nguo kama mchango wake kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro.

2. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepanda katika pikipiki aliyokabidhiwa na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xingshen kama seshemu ya msaada wa China kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Misaada mingine iliyokabidhiwa katika hafla hiyo ni pamoja na baiskeli, chupa za maji na mashine za kushonea nguo.

3. Balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete moja ya baiskeli alizozitoa kama msaada wa sekta mbalimbali za maendeleo nchini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

4. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro(Picha: Freddy Maro)
Reactions::

Dada Yangu Huyu, Na Mwenye Dada Hakosi Shemeji!



Mwajuma Mjengwa, Rujewa.

" Mwenye dada, hakosi shemeji eh,
Unataka kumuoa mwenyewe?" ( Mbaraka Mwinshehe Mwaruka)
Reactions::

Maasai Ladies



Rujewa, hivi karibuni.
Reactions::

Stendi Kuu Ya Mabasi



Rujewa, Mbarali, Mbeya.
Reactions::

Kliniki Ya Simu!



Makambako, hivi karibuni.
Reactions::

Photo Studio



Makambako, hivi karibuni.
Reactions::

Tumekuwa Watu Wa Ovyo; Hatuna Ya Keshokutwa Wala Mtondogoo!



Na Maggid Mjengwa,

SIKU ile dikteta Idi Amin alipoingia madarakani kule Uganda, Kampala iliwaka moto kwa furaha za wakazi wa mji huo.

Kuna simulizi za kweli za Waganda waliochukua funguo za gari zao na kutoka majumbani wakiendesha magari kuelekea katikati ya jiji la Kampala. Walifanya hivyo bila hata kuvaa nguo. Naam. Walikwenda uchi. Ni uchi wa furaha na matumaini mapya!

Amin (mwanajeshi) alimwondoa madarakani Rais Obote aliyeingizwa madarakani na Waganda. Ni Waganda hao hao waliofurahia kuondolewa kwa Obote madarakani. Soma zaidi; http://www.raiamwema.co.tz
Reactions::

Haya Tuanze...



Kutoka kushoto mstari wa mbele ni....
Reactions::

Fally Ipupa- Amsterdam!





FALLY IPUPA- AMSTERDAM

FOR THE FIRST TIME THE CHAMPION OF LOVE WILL GIVE A LIVE CONCERT IN HOLLAND THIS SPRING 10/04/10 TELL UR FRIENDS AND COLLEAGUES COME IN BIG NUMBERS AND CELEBRATE WITH THIS MOST TALENTED AFRICAN ARTIST OF OUR TIME THE ONLY ONE WHO DID A DUET WITH *OLIVIA G UNIT * AND HE WILL DANCE WITH U ALL NITE LONG..COME ONE COME ALL.. DONT FORGET DRESS TO IMPRESS AND BELEAVE ME..HE WILL BRING MORE SUN WITH HIM.. IF YOU WANT TO BELEAVE visit: www.fally-ipupaa2bm.blogspot.com or www.congomikili.com and www.decosmukoko.skyblog.com
Reactions::

Sunday, March 28, 2010

JK Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ikulu





Maelezo ya Picha:

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akingoza kikao cha Kamati kuu ya CCM Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine katika picha ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume, Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba, Makamu wa CCM Bara Pius Msekwa, Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi,Rais mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa na Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha.

2. Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM wakiwa katika kikao Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi Chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete

(Photos: Freddy Maro).
Reactions::

Kitendawili Cha Daraja La Kijiji Chetu!



Ukitokea Rujewa unavuka daraja hili ndipo unaingia kwenye kijiji cha asili yangu, kijiji cha Nyeregete. Ni umbali wa kilomita nane kutoka Rujewa kuelekea hifadhi ya Ruaha kwenye bonde la Usangu. Daraja hilo limejengwa kwa nguvu za wanakijiji. Wamekata na kubeba magogo ya kupanga darajani. Wanakijiji walishangaa sana kusikia ripoti ya wilaya inayosema winchi ilitumika kubeba magogo hayo. Naam. Ni wajanja wachache waliotumia hila kujipatia fedha.
Kisa hiki kinanikumbusha simulizi ya kweli kutoka Malawi. Kwenye moja ya vijiji vya Malawi, usiku mmoja raia alisikia ripoti ikisomwa na Waziri Bungeni kuwa barabara inayopita kijijini hapo imeshajengwa kwa kiwango cha lami, na kwamba kuna madaraja mawili pia yamejengwa.

Raia yule wa Malawi alishangaa sana. Asubuhi ilipofika akafunga safari kwenda Lilongwe lilikokaa Bunge hilo. Huko akataka kuwaambia ukweli waheshimiwa Wabunge wale; kuwa barabara na madaraja anayosema Mheshimiwa Waziri kuwa yamejengwa ni ya katika barabara ile inayopita kijijini kwake au barabara nyingine? Kisa kile kilipelekea Waziri mhusika kupoteza kibarua chake. Kuna ya kujifunza hapa.
Reactions::

Issa Michuzi Azungumza Uingereza






BACKGROUND

Since Jon Barger put online what is considered to be the first blog (known as weblog by then) in 1995, millions of blogs have been created. Today, it is estimated that over 100 million blogs are created every day. As of December 2007, Technorati was tracking more than 112,000,000 blogs.

Even though it took a bit longer for Tanzanians to embark on the social media networking scene, such as blogging, when it finally did, the results were impressive. Today, there are over 200 active blogs written for Tanzania or by people who, in one way or another, refer themselves as Tanzanians.

It is fair to estimate that at least 10 to 20 blogs or online forums are created every week by Tanzanians with the purpose of sharing information, news and personal thoughts on different issues affecting or occurring in Tanzania or by Tanzanians wherever they could be in the globe. Read On: http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

JK Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi Wa Machinjio Ya Kisasa, Ruvu





MAELEZO YA PICHA:

1. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi ili kuzindua rasmi ujenzi wa machinjio ya kisasa huko Ruvu, mkoa wa Pwani jana asubuhi.Kulia ni Waziri wa mifugo na Uvuvi Dr.John Pombe Magufuli, watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi za Taifa Salum Shamte na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani.

2. Wataalamu wa ujenzi kutoka Shirika la SUMA JKT wakimpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa machinjio ya kisasa unaofanywa na shirika hilo wakati Rais alipokuwa akikagua ujenzi huo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika machinjio hayo.

3. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr.John Pombe Magufuli(wa pili kushoto),Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange(wanne kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi za Taifa Bwana Salum Shamte(kushoto) muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika machinjio ya kisasa huko Ruvu, Pwani. (Picha zote: Freddy Maro)
Reactions::

Saturday, March 27, 2010

Timu Hii!



Mariam Dodo, Ben Waziri, Ramadhan Ali na Ramadhan Tuwa. Wote ni wa Redio Deutsche Welle. Ben Waziri Amestaafu.
Reactions::

Mjomba Njoo, Daftari Linunuliwe....



Na kipande cha sabuni pia. Pichani ni duka, kijijini Nyeregete nilipokuwa huko hivi karibuni.
Reactions::

Muhongo Wa Makambako Huu!



Fungu shilingi mia tano.
Reactions::

SanSiro!



Makambako
Reactions::

Malangali

Reactions::

Nyororo Hapa!



Iringa
Reactions::

Aliye Juu Usimngoje Chini!

Reactions::

JK Azindua Kitabu Cha Historia Ya Utumishi Serikalini Wa Sir. George Kahama






Maelezo ya Picha:

1. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe ulizingushwa kwenye kitabu kinachohusu historia ya maisha ya utumishi serikalini ya Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama(wapili kushoto), Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi(wanne kushoto) na watano kushoto ni Mwandishi wa kitabu hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Royalty Bwana Joseph kahama.

2.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mezani tayari kwa mauzo kitabu kinachohusu maisha ya Mwanasiasa Mkongwe Sir.George Kahama muda mfupi baada ya kukizindua katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir George Kahama(wapili kushoto) na wanne kushoto ni Joseph Kahama ambaye ni mwandishi wa kitabu hicho.Joseph ni Mtoto wa Mzee Kahama.

3. Joseph Kahama ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu historia ya Maisha ya Utumishi Serikalini ya Mwanasiasa Mkongwe Sir.George Kahama akimkabidhi Mama Maria Nyerere nakala ya kitabu hicho katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua kitabu hicho.

4. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Joseph Kahama(Wanne kushoto) ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu maisha ya mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam jana jioni.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamim Mkapa, Sir Geroge Kahama(wapili kushoto) na kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi(picha zote: Freddy Maro)
Reactions::

Friday, March 26, 2010

Nafasi Ya Kazi Iringa: Accountant

Karibu Tanzania Association inatafuta Mtanzania atakayejaza nafasi ya Mhasibu. Mwombaji awe na shahada ya Uhasibu na uzoefu wa kazi hiyo. Kituo cha kazi ni Iringa: Tuma maombi: kaributz@yahoo.com
Reactions::

Kuna Wanaoishi Kwenye Nusu Kibanda



Ubaruku, Mbarali, Mbeya. Juma la jana.
Reactions::

Thursday, March 25, 2010

Unaporudi Kijiji Chenu Cha Asili...



Kwa desturi zetu Waafrika, kama umerudi kijijini kwenu kwa asili baada ya kupotea kwa muda fulani, basi, kuna kiumbe hai kitakachopoteza uhai wake. Huwezi ukashinda, ukalala na kuamka bila kutafuna nyama japo ya kuku. Pichani ni kijijini kwetu kwa asili, Nyeregete, Mbarali, Mbeya juma la jana.
Reactions::

" Bwana Mdogo Hizi Ndio Taratibu Zetu!"




... Ukiwa safarini kikazi posho ya siku ni shilingi elfu sita na mia tano."
Pichani juu ni kijana Garasiano Muyinga. Tumemwajiri hii leo kama Mratibu wa programu za Karibu Tanzania Association. Ameanza na bahati. Jumapili hii anakwenda Arusha kushiriki Kozi ya siku tatu juu ya masuala ya Uongozi wa Fedha itakayofanyika pale Corridor Hotel. Kozi hiyo imeandaliwa na Shirika la Forum Syd na inashirikisha wadau kutoka NGO's zinazopokea misaada ya Forum Syd au zilizowahi kupokea misaada hiyo.
Reactions::