
Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (aliyeketi kushoto) na Marehemu Abeid Amani Karume (aliyeketi kulia) pamoja na Mashahidi kwenye utiaji saini makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika kuiunda Tanzania
Leo tarehe ya ishirini na sita ya mwezi wa Aprili mwaka elfu mbili na kumi (26 Aprili 2010), tumeadhimisha miaka arobaini na sita (46) tangu Waasisi wa Mataifa haya mawili yaani, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa iliyokuwa Tanganyika na hayati Abeid Amani Karume wa iliyokuwa Zanzibar, wakiri mbele ya kadamnasi kuwa nchi mbili hizi sasa zimeungana na kuunda Jamhuri ya Tanzania na hivyo kuwaunganisha wananchi hawa kuwa Taifa moja.
Maadhimisho ya sherehe hizo yalijumuisha pia vikundi vya burudani, na kama kawaida mara baada ya shughuli ya makundi mbalimbali ya Jeshi kukamilisha shughuli zao, Halaiki ya Vijana ilikuwa kivutio kikubwa.
Kwa sisi tuliofuatilia kwa njia ya redio, tulifaidi kusikia ujumbe wa Mrisho Mpoto, Nyimbo za Ngoma na nyimbo za Vijana wa Halaiki 'Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote' na mwingine mpya ambao jina lake rasmi sijalifahamu, lakini wasema, 'Ni furaha kuzaliwa Tanzania', ukipenda kusikiliza haya yote, tafadhali bofya linki hiyo -->
http://bit.ly/8X3QMS
Subi|