Subscribe:

Wednesday, June 30, 2010

Baadhi Ya Washiriki; Mr & Miss East Africa In UK


B



Adyam


Barbara
Reactions::

Kona Kali Za Ihovi...



Zinahitaji umakini, ingawa barabarani lolote laweza kutokea. Pichani ni jioni hii kwenye moja ya kona kali za Ihovi barabara ya Dar- Tunduma nilikutana na lori lililopinduka likiwa limesheheni mafuta ya kupikia. Nimewasili salama Iringa leo usiku nikitokea Dar nilikokuwa kikazi kwa saa 48 zilizopita( Siku mbili).
Reactions::

Nilishuhudia England Ikiangamia Nikiwa Chalinze!



Juzi hapa. Na tatizo la England ni England yenyewe, basi!
Reactions::

Haya Twende!



Kitonga hii, juzi mchana.
Reactions::

Siku Hizi Nasafiri Na Kamba.....



... Jeans na raba miguuni badala ya mukasini. Maana, uzoefu ni mwalimu mzuri. Kwa msafiri unayajua ya unakotoka, ya unakokwenda huyajui. Unaweza kuhitaji kuvutwa, kuvuta au ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Magodoro.....



Magodoro ya sufi moja Tsh 14000. Msamvu Morogoro.
Reactions::

Vodacom Yatoa Msaada Wa Vyandarua Iramba



Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi moja kati ya vyandarua 1,300, Esta Aron akiwa na mwanae mwenye umri wa miezi 6 Peter William ambaye ni mmoja wa Wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya akina mama katika hospitali ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi Singida. Mfuko huo ulitoa msaada wa jumla ya Vyandarua 1,300 katika mkoa (fullshangweblog)
Reactions::

Matunda...



Maeneo ya Masika, Manispaa ya Morogoro leo jioni.
Reactions::

Mji Kasoro Bahari



Mji Kasoro Bahari, Morogoro leo jioni.
Reactions::

Serikali Yaongeza Muda Wa Kusajili Simu Za Mkononi




1. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msollla
2. Moja ya kituo cha kujasili namba za simu za mkononi kilichopo katika manispaa ya Morogoro kinavyoonekana jioni hii.

Serikali imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani hadi Julai 15.
Reactions::

Raila Odinga Afanyiwa Upasuaji



Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amefanyiwa upasuaji wa ubongo baada ya kubainika kuwa kulikuwepo na shinikizo kubwa la damu kichani. Daktari wa waziri mkuu huyo Oluoch Olunya amethibitisha kuwa Odinga amefanyiwa upasuaji huo. Taarifa zaidi zinazsema kuwa Odinga anaendelea vizuri isipokuwa anakabiliwa na uchovu mwilini hali itakayomlazimu kulazwa kwa siku tano zijazo ili kuendelea kuwa chini ya uangalizi wa Madaktari.
www.bbcswahili.com
Reactions::

Ajali Ya Ndege Yaua Wawili Tanga.




Sehemu ya ndege iliyopata ajali baada ya kutua barabarani kwa dharura na kugonga basi la watalii ambalo linaonekana juu kushoto likiwa limeanguka. Ajali hiyo ilitokea jana katika barabara ya Segera Tanga ambapo Marubani wote wawili waliokuwapo kwenye ndege hiyo walipoteza maisha. ( Michuziblog)
Reactions::
UWEZESHWAJI WA WABUNGE

NA MWANDISHI MAALU New York.
Imeeleza kuwa, licha ya wabunge na taasisi za kijamii, kuwa na fursa na nafasi ya kushiriki katika ufuatilia wa upangaji na utekelezaji wa bajeti ya taifa, sera zinazohusiana na masuala ya fedha na misaada ya kimaendeleo kutoka kwa wahisani, imebainika uwezo wa vyombo hivyo kutimiza wajibu huo kikamilifu bado ni mdogo.

Waziri wa fedha na Uchumi, Bw. Mstafa Mkulo ameyasema hayo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York. Wakati wa majadiliano ya kisera kuhusu uwajibikaji na uwazi katika ushirikiano wa kimaendeleo; namna gani serikali zinaweza kujenga ushiriano ulio sawa kati yake na taasisi nyingine. Mjadala huo umefanyika ukiwa ni sehemu ya mkutano wa kilele wa Kamati ya Baraza Juu la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii. (ECOSOC).
Mkulo anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, anasema “ ushiriki wenye nguvu wa wabunge na taasisi za kijamii katika masuala yahusuyo fedha ni jambo la muhimu sana kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi, lakini ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uwajibikaji na uwazi. Lakini uzoefu unaonyesha kuna udhaifu kwa upande wa wabunge na taasisi za kijamii.


Akabainisha kuwa udhaifu huo ndio unaolazimisha kuwapo kwa hitajio la kuzijengea uwezo zaidi taasisi hizo ili kuhakikisha kwamba ushiriki wao katika mijadala ya kitaifa na kimataifa kuhusu ubora wa misaada ya maendeleo unakuwa na tija.
Akisisitiza haja hiyo ya taaisi hizo kujengewa uwezo zaidi, Mkulo anasema, sera zinazohusu fedha na hasa zile zinazohusu misaada ya wafadhili ni ngumu na zenye vipengere vingi, ambavyo anasema vinahitaji mshiriki awe uwezo na upeo wa kutosha wa siyo tu wa kuvijadili bali pia kivielewa na kuwa na mbinu za kufuatilia.
Wanajopo wengine katika majadiliano huo walikuwa ni Bi. Irene Freudenshuss-Reichal kutoka serikali ya Austria, Michael Anderson kutoka serikali ya Uingereza na Bi. Ingrid Srinath kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya CIVICUS.

Mkulo ambaye aliainisha hatua mbalimbali ambazo zimefanywa na serikali lipokuja suala la uwazi na uwajibikaji, amewaeleza washiriki wa mjadala huo, kwamba kwa kiasi kikubwa Tanzania imefanikiwa kuwa na uhusiano endelevu na wenye kuridhisha kati yake na wadau wa maendeleo.
“ kwa kujiwekea sera, mipango na mikakati mbalimbali ambayo tumeshirikiana na wadau wetu wa maendeleo, wabunge na taasisi za kijamii, Tanzania imeweza kuongeza kiwango cha umiliki wa ajenda zake za maendeleo, kupanua wigo wa majadiliano kati yake na wafadhili , na wadau wengine. Na kwamba kiwango cha uwazi na uwajibikiaji kimeongezea katika uandaaji na utekelezaji wa bajeti ya taifa na sera zinazohusiana na masuala ya fedha na misaada kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa” anasema mkulo.

Hata hivyo anaeleza kuwa , dhana hiyo ya uwazi na wajibikaji bado inaelemea zaidi upande mmoja yaani upande ule unaopokea misaada ( serikali) kuliko upande wa pili yaani wafadhili.
“Suala hili la uwajibikaji kwa kweli kwa wafadhili bado halijawa na uzito wa kutosha. Mara kwa mara sisi nchi tunao pokea misaada ndio tunaolazimishwa kuwa wawazi na kuwajibika. Hii si haki kwa sababu inakwenda na kinyume na Tamko la Paris la mwaka 2008 linalo sisitiza uwajibikaji wa pamoja”.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Uchumi, anasema kuwa ujenzi wa ushirikiano endelevu na wenye tija kati ya serikali na wadau wengine, ni jambo linalohitaji kuaminiana, kujituma, uwazi katika majadiliano na kwamba litachukua muda mrefu.

Aidha anasema ili hilo liweze kutekelezeka, uwajibikaji wa kisiasa kati ya mfadhili na mfadhiliwa ni jambo la muhimu sana.Kwa sababu ndiko kutakako pelekea uwajibikaji wa pamoja kwa lengo la kuimarisha misingi ya uwajibikaji katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Wakati wa majadala huo, baadhi ya wazungumzaji pamoja na kukubaliana na hoja ya uwezeshwaji zaidi wa wabunge na taasisi za kijamii hasa katika mataifa yanayoendelea, walitaka pia uwezeshaji huo ushuke mpaka kwenye vyombo vya habari, kwa kile walichosema kwamba nao ni wadau muhimu katika kufuatilia utendaji wa serikali.

Wengine waliainisha kwamba, linapokuja suala ya uwazi na uwajibikaji, basi lisiishie kwa serikali na wadau wa maendeleo, bali uwazi na uwajibikiaji huo uwepo pia kwa taasisi nyingine zikiwamo Bunge na vyama visivyo vya kiserikali.
Reactions::

Mkulo Ziarani New York






1.WAZIRI WA MUSTAFA MKULO FEDHA AKICHANGIA MJADALA KISERA KUHUSU WAJIBIKAJI NA UWAZI KATIKA USHIRIKIANO WA MAENDELEO; NAMNA YA KUJENGA USHIRIKIANO ULIO SAWA MIONGONI MWA WADAU MBALIMBALI. MJADALA HUO UMEFANYIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK.

2.NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI, DKT. SERVACIUS LIKWELILE AKIFUATILIA MAJADILIANO

3.WAZIRI AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAJUMBE MBALIMBALI WA KIKAO CHA KILELE CHA KAMATI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII YA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA( ECOSOC)
Reactions::

Sikinde.....



Hassan Rehani Bichuka na Abdala Hemba, wakifanya vitu vyao katika ukumbi wao wa nyumbani DDC Kariakoo hivi karibuni.
Reactions::
Reactions::

Bao La Hispania Na Mlinzi Wa Gereza Aliyewafungulia Wafungwa!



Na Maggid Mjengwa,

FAINALI Za KOMBE LA DUNIA ina maana ya msimu wa kuamka kwa hisia za utaifa. Jana tulimshuhudia David Villa akipachika bao muhimu sana kwa taifa lake la Hispania. Bao lililowafanya mamilioni ya Wahispania wajawe na furaha kubwa. Na utamu wa bao lile ni ukweli kuwa Hispania waliwafunga na kuwafungasha virago majirani na mahasimu wao wakubwa katika kandanda; Ureno.

Hakika kandanda ina miujiza yake na inaweza kuwafanya watu wapagawe, wawe kama wendawazimu. Kule Hispania miaka ya sabini kuna kisa ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Ajali..








Ajali hii imetokea leo asubuhi majira ya saa 1:10 barabara ya Nyerere maeneo ya Ukonga karibu na Gereza la Uonga jijini Dar es Salaam.(Picha:Victor Makinda)
Reactions::

Friends Of Mafia: TAMKO KUHUSU TAMASHA LA MASHOGA



Sisi kama wenyeji wa kisiwa hichi na wenye nia uchungu na kisiwa hiki
tumesikitishwa na hatua ya baadhi ya wenye mahoteli ya kitalii kwenye
kisiwa hichi pamoja na uongozi mzima wa wilaya (DC) na halmashauri kutoa
kibali kwa kundi la burudani toka Ugiriki kuja kufanya vitendo vya ushoga
kwa kutumia mgongo wa Tamasha la muziki. Pia tumesikitishwa na DC wetu
bwana Mangochie Manzie kukubali kutoa kibali kwa hawa vijana
3,000(revelers) bila kupata ridhaa ya wenyeji wa Kisiwa hichi (Public
consultation). Tungependa ifahamike kuwa sisi kama wenyeji wa Kisiwa hichi
tunakaribisha wageni lakini ni LAZIMA wazingatie na waheshimu mila na
taratibu zetu na moja kati ya hizo mila zetu USHOGA haumo!



Kitendo cha kutaka kuleta vijana hawa mashoga hapa kisiwani kufanya
vitendo vyao kwa siku 14 mfululizo hakikubaliki kimaadili na tunawaunga
mkono wana Mafia na hasa wazazi ambao hawako tayari kuona watoto wao
wakishuhudia vitendo vya kishoga, utumiaji wa madawa ya kulevya ambavyo
ni si mila na desturi yetu kama waTanzania.

Kama mjuavyo Mafia ni kisiwa cha amani na ndio maana kimekuwa kinaongoza
kwa utalii wa scuba diving duniani na tunaendelea kuwakaribisha watalii
ambao wanakuja na kutuheshimu na wanaoelewa umuhimu wa kutunza mazingira
ya kisiwa hichi.

Kisiwa hichi hakina uwezo wala fedha za kuweza kutoa huduma za afya kwa
watu wake iweje leo tamasha hili la mashoga 3,000 ambao itabidi wajisaidie
kwenye mashamba ya watu kwani hakuna public toilets za kuweza kuhimili
kishindo hichi.

Hivi kwa mfano mazingira yashachafuliwa ni sisi watu wa Kisiwa hiki ndio
tutasafisha au halmashauri? je wanazo pesa za kusafisha na kuokota toilet
papers zitakazo achwa na hawa Mashoga kwenye mashamba yetu?

Hospitali zetu hapa zinatia aibu na mbaya zaidi huduma za afya kwa mama
zetu na dada zetu wanapojifungua zipo katika hali duni, hivi kweli
mheshimiwa DC na timu yake wameona kwa sasa tunachohitaji ni hili Tamasha?

Kwa kawaida ya Mashoga hawatokaa sehemu moja hapa kisiwani na watataka
kwenda kufanya uchafu wao kwenye fukwe zetu hapa kisiwani, hivi Uongozi wa
Kisiwa hichi utatoa polisi wangapi kwa kila kundi la hawa mashoga kufanya
mambo yao? kwani sidhani kama wananchi watakaa na kushangilia vitendo
hivi vikifanyika hadharani.

Tungependa kuufahamisha umma kuwa hawa waandaji tamasha hili lilipofanyika
kwenye kisiwa cha Skyros, watu walililalamika sana pamoja na kuwa Wagiriki
wana mitizamo ya ku liberali kwenye mambo haya lakini hali ilikuwa mbya
kiasi cha Polisi kuvamia na kusitisha lile Tamasha kwani lilikuwa
linaelekea kuvujinka kwa amani.

Katika kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi je ni kweli
Serikali inataka kuona uvunjikaji wa amani katika kipindi hichi
tunachoelekea kwenye Uchaguzi kwa kukubali hili tamasha la Mashoga?

Je jeshi la polisi linazo resources za kulinda mashoga 3,000 usiku na
mchana kwa siku saba mfulululizo?

Kwa nini Bwana Mike Athanassakis ambaye ndiye mratibu wa hili Tamasha hili
la Mashoga hataki kukutana na viongozi wa Kisiwa hichi na kuwaeleza kwa
kinaga ubaga nia yake?

Maandaji wa Tamasha hili wamesema wamepata ushirikiano wa karibu na
kampuni ya uwindani na utalii inayojiita KARIBUSANA ambayo iko chini ya
Costa Coucoulis,Angela Damas,Chyrista Batou na Mark Evans ambao wanajiita
wahifadhi wa mazingira kwenye tovuti yao lakini wakati huo huo wako tayari
kuhakikisha kuwa mazingira ya kisiwa chetu yanachafuliwa na hawa wageni.

Je Mbunge na DC wa Kisiwa hichi watakuwa wanatekeleza ilani ya chama gani
kulikubali hili Tamasha la Mashoga?

Je wilaya iliyo masikini kuliko zote Tanzania inahitaji Tamasha la muziki
au tunahitaji miradi ya Maendeleo?

Je BASATA na Wizara ya Utalii wameamua ku promote USHOGA Tanzania?

http://www.friendsofmafiaisland.com/

admin@friendsofmafiaisland.com
Reactions::

Miss East Africa In UK



Salam kaka,

Utawala wa Urban Pulse unapenda kuwaletea exclussive behind the scenne kwa wadau wote wa libenekene kuhusu matayarisho na maandalizi ya
Miss & Mr East Africa Uk 2010 yaliyofanyika katika kitongoji cha Edmonton, Ukerewe jumamosi 26.6.10

Fainali ya kuwania Taji la U miss na U mr East Africa UK litafanyika jumamosi 3rd July 2010katika ukumbi wa Central Hall,Westminister, London
wote mnakaribishwa. Bofya chini kuangalia kideo kutoka kwa wahisani URBAN PULSE kuhusianana na Maandalizi

http://www.youtube.com/watch?v=EEBjHhW7NeI

Mdau

`Frank Eyembe

Urban Pulse
Reactions::

KUMBUKUMBU: MPENZI MAMA HAWA BINT HASSAN KINGWELE



MPENZI MAMA HAWA BINT HASSAN KINGWELE
Leo ni miaka 3 toka ulipotuacha baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Unakumbukwa sana na wanao; Baba Hawa . Wajukuu zako Miraji, Mwahija, Zena,
Zawa, Sabi, Ahmed, Salum, Hawa na Nune. Unakumbukwa pia na kitukuu chako Ayyan Kikondo na rafiki zako.
Mungu akulaze mahali pema peponi Amen
Hakika sisi sote kwake in marejeo yetu
Reactions::

KUMBUKUMBU: Striker Abdalah Ally Madenge Kidunyu



STRIKER ABDALLAH ALLY MADENGE KIDUNYU
Leo ni miaka 12 toka ulipotuacha baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Unakumbukwa sana na wanao wanao Miraji, Mwahija, Zena, Hawa, Sabi na Ahmed . Mjukuu
wako Ayyan, Rafiki zako , wachezaji wenzako wa Bot BAY ASHUKURU
KAMPIRA, MWALUSAKO,. KASSIM MUSSA Rafiki zako Abdalah Nuia, Capt Mbuli

Mungu akulaze mahali pema peponi Amen
Hakika sisi sote kwake in marejeo yetu
Reactions::

Tuesday, June 29, 2010

Ujumbe Umefika.." Tusitafutane!"

Reactions::

beatrice premsingh ndiye vodacom miss kanda ya kati




Mshindi wa Vodacom Miss Kanda ya Kati Beatrice Premsingh(katikati) mshindi wa pili Willem Etam (kushoto) na Mshindi wa tatu Pili Issa (kulia) na mshindi wa tano Leilah Salvaory wakiwa katika picha pamoja baada shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.(michuziblog)
Reactions::

Kiwanda....





Mashine zinazo onekana pichani zinaundwa hapa hapa katika kiwanda hiki,,,,Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam.
Reactions::

Biashara Ya Chupa Za Plastiki




Kilo moja tsh 20.
Reactions::

Dhamira Nzuri....

Reactions::

Takataka




Temeke.....jijni Dar es Salaam.
Reactions::

Ikiwa Imebaki Siku Moja Kusajili Namba Za Simu.....



Hali ilivyo leo katika vituo mbali mbali vya kusajili namba za simu za mkononi. ( Picha: Victor Makinda)
Reactions::




Banda la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,viwanja vya Sabasaba jana.
Reactions::


Ujumbe huo, maandamano ya Twanga Pepeta kusherehekea miaka 10 ya bendi hivi karibuni.
Reactions::

Maliasili Zetu



Twiga.
Reactions::

" Ndugu Mwenyekiti, Asalaam Aleikum!"



Ndugu Mwenyekiti,

Asalamu aleykum. (kama salamu hii ina mapungufu wadau mniwie radhi)

Kwa mza nikushukuru kwa kutembelea kitunda na kuliona hili la wajasiriamali KUKU.

Huwa nina shangaa na nitaendelea kushangaa kuona jinsi eneo hilo linavyozalisha mayai kwa wingi. Nilikwishawahi kutembelea huko kama Mtanzania wa kawaida tu nikaangalia mabanda (nyumba za kuku)na ufugaji wake kwa ujumla nilifarijika kwa kiasi fulani kwa usalama. Kule nilivyouliza kuhusu usalama wa hawa ndege kuhusu wizi, wenyeji walisema hakuna mtu atakayethubu kuchukua (kuiba) kuku.
Wenyewe wanafahamiana, iwapo utakamatwa ama ndani ya banda au nje ya banda ukinyemelea kuku wa mtu, wewe ni RIP. Kwa hili nawasifu.

tuje katika suala zima la Uchumi-kuku.

Ndugu Mwenyekiti, nitaomba kama hujaondoka huko hebu hesabu Baiskeli zinazotoka huko kila siku zilizobeba mayai. Nadhani kitongoji cha Kitunda kinaweza kuwa namba one Tanzania kwa uzalishaji wa mayai. Sijatembea Tanzania yote lakini Kitunda panatoka maya si kawaida.

Soko.

Nadhani hadi sasa soko nila uhakika kama sijakosea, kwa sababu sijawahi kusikia yai kushuka bei, hata hivyo wafugaji na wachuu wangestahili kujitafutia vitu ambavyo watu wangefika na kujinunulia bidhaa hiyo kwa jumla na hata ikiweekana kwa reja reja.

Nasema hivi kwa sababu, baadhi wanapata ajali kwa kugongwa na magari. Iwapo wangekuwa na kituo kila wilaya TEMEKE, KINONDONI NA ILALA, wangekuwa wanakodi gari na kubeba mzigo wao badala ya BAISKELI
Reactions::

Ushindi Wa Ghana Ulivyoshangiliwa Tottenham!



Salam kaka,

Kwa mara nyingine tunapenda kuwaletea wadau wote wa libeneke yaliojiri hapa ukerewe katika kitongoji jana usiku cha Mji Tottenham kususiana na ushindi wa Ghana.

Washibiki wote wa mpira walikusanyika pamoja na kusherekea ushindi wa Ghana kwa staili ya kipekee.

Haya ndio mambo ya Waghana na wadau wa mataifa mengine wakisheherekea na kurusha nyuki kushangilia ushindi wa timu yas taifa ya Ghana THE BLACKSTARS dhidi ya timu ya Marekani kwa Obama.

Bofya link chini kuangalia video.

http://www.youtube.com/watch?v=Qttrz4vNzhw

Habari ndio hiyo

Mungu Ibariki Africa,

Urban Pulse Production
Reactions::

Monday, June 28, 2010

Uchukuzi...



Baiskeli zikiwa zimepaki kusubiri kupakia mayai, Kitunda jijini Dar. Yai moja kwa bei ya jumla ni tsh 180.
Reactions::