Subscribe:

Saturday, July 31, 2010

Dk Slaa ,Chadema Wang'ara Mwanza




1.Mwenyekiti wa CHADEMA akiwatambulisha wakazi mjini Mwanza.

2.Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando, ambaye alijunga na chama hicho hivi karibuni akitokea chama cha NCCR Mageuzi, akiwahutubia wakazi wa jiji la Mwanza, katika mkutano wa hadhara wa kuomba kudhaminiwa, aliuofanyika kwenye Uwanja wa Furahisha jana.*(Hakingowiblog)
Reactions::

Kura Za Maoni Visiwani Zanzibar Leo.



Wakazi wa Zanzibar leo wanapiga Kura ya Maoni kuhusu kuwepo ama kutowepo kwa Serikali ya Mseto . Mjengwablog inawatakia kila la kheri wakazi wa visiwa hivyo katika kufanikisha zoezi hili muhimu la kihistoria ambalo kimsingi litaamua hatma muhimu sana ya mustakabari wa kisiasa visiwani humo.(Mdau: Victor Makinda)
Reactions::

Uhaba Wa Maji Mvomero






Wanafunzi wa shule ya msingi ya Manza, tarafa ya Mlali, wilayani Mvomero wakisomba maji kutoka umbali wa kilomita moja kutoka shuleni hapo. Wanafunzi hao walisema kuwa maji hayo yalikuwa ni kwa ajili ya matumizi binafsi ya mmoja wa walimu wao.(Globalblog)
Reactions::

Basi La Najimunisa Lililoua 17 Jana.



Ajali mbaya iliyotokea jana majira ya saa 6 mchana wilayani Kahama kwa kuhusisha basi la Super Najimunisa lililokuwa linatoka Bukoba kwenda jijini Dar Es Salaam na kugongana uso kwa uso lori aina ya fuso. Watu 17 walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.
Reactions::

Corporate Golf Day 2010



Asalam Alaykum..

Hii ni kuwataarifu kuwa, ile Press conference iliyokuwa ifanyike leo,
imeahirishwa hadi Alhamisi tarehe 5 mwezi wa nane, saa nane mchana
pale Dar es Salaam Gymkhana Club.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokea,


Wote mnakaribishwa tarehe 5/08/2010 saa nane mchana, Gymkhana Club.....

Shukran
Reactions::

SINGLE CD IMESHATUA: JAKAYA KIKWETE 2010




Singo CD "Jakaya Kikwete 2010" kutoka kwao "Ngoma Africa Band"
IMESHATUA NCHINI KWA KISHINDO NA NGUVU ZAIDI !!!

PATA KOPI YA CD KWA KWA ANKAL MICHUZI

Hayawi !Hayawi ! Yamekuwa hile CD inayozungumziwa na washabiki wengi kila kona duniani
Sasa imeshatua nchini ,CD hiyo yenye jina "JAKAYA KIKWETE 2010" Kutoka kwao
"The Ngoma Africa Band" yenye maskani yake uko Ujerumani,Sasa unaweza kupata kopi za CD
hiyo kwa ANKAL Muhidin Issa Michuzi aka Mzee wa Libeneke,kwa simu 0754271266 wa blog ya
ya kimataifa ya jamii.
Pia kwa yeyote yule anayetaka atumiwe mp 3 au kuweka nyimbo hizo katika mlio wa Simu za viganjani
tafadhali usisite kuwasiliana na Ankal Michuzi kwa simu namba 0754271266 CD hiyo yenye mziki mtamu
unaosindikiza ujumbe muhimu kwa watanzania zaidi ya milioni 40 sasa CD hiyo ipo nchini na unaweza kupata kopi yake kwa kupiga katika sherehe ,mitaani,katika biashara yako,ndani ya mabasi,harusini,sokoni n.k
hili upate raha na ujumbe uliomo katika CD "Jakaya Kikwete 2010" utunzi wake Ebrahim Makunja aka
kamanda Ras Makunja wa FFU wa Ngoma Africa Band.
pia Jumamosi ya 31-07-2010 saa 4 hasubui Ras Makunja atahojiwa na radio Free Africa ya mwanza
tafadhali tega sikio.
Reactions::

Friday, July 30, 2010

Hapa Nabahatisha Kitoweo!



Leo nimevua samaki, japo ni dagaa, wametosha kikaango. Na sheria za Sweden eti wanasema samaki ukimvua samaki na akiwa mdogo umrudishe majini. Mi nimevunja sheria hii, maana kwetu Tanzania samaki wadogo wa kutosha kikaango ni dagaa hao. Kuwarudisha majini ni kufuru. Rizki ikitoka majini hairudi majini!
Reactions::

Macho Hayana Pazia, Na Huku Ndio Kusafisha Macho!



Stockholm City, jana alhamisi.
Reactions::

Maestro Dekula ' Vumbi' Kahanga In Stockholm!



Tanzania imepata kuwa na wachawi wa gitaa la Solo; marehemu Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, Ndala Kasheba, Said Mabela.... Ndio, Maestro Dekula ‘ Vumbi’ Kahanga ( Pichani) ni mmoja wa wachawi hao. Jana nilipata bahati ya kuwa nawe kwa zaidi ya nusu siku. Alinipokea Central Station. Akanipa lunch ya nguvu kwenye restaurant moja ya hapo hapo Central Station. Kisha... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

jaji eliamani mbise afariki dunia



Marehemu Jaji Eliamani Mbise wa tatu toka kushoto mstari wa nyuma,nyuma ya Rais Kikwete katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa July 31,2009.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Eliamani Mbise amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msajili wa Mahakama ya Rufani Francis Mutungi imesema Jaji Mbise amefariki majira ya saa nne na nusu tarehe 29/7/2010 .
Taarifa hiyo imesemakuwa taratibu za mipango ya Mazishi ambayo yatafanyika Arusha itatolewa baadae baada ya utawala kuwasiliana na ndugu wa marehemu.

Aidha Bwana Mutungi amesema msiba umewekwa kwa muda nyumbani alipokuwa akiishi marehemu Mikocheni kwenye nyumba za viongozi wa Serikali.

Marehemu Mbise alikuwa akifanya kazi katika kituo cha kazi cha Mahakama kuu ya Tanzania .
Reactions::

Dr Slaa....Ang'ara Arusha.




Mgombea wa urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, akiwahutubia maelefu ya wakazi wa jijini Arusha, ambao walijitokeza kumdhamini katika Uwanja wa NMC jana. (Picha: Joseph Senga).
Reactions::

People Welcome PCCB Drive To Nab Corrupt Politicians



Several residents in Dar es Salaam, Arusha and Kilimanjaro regions have expressed their support to the officers of the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) for their current efforts to curb corrupt practices during the general elections process....read more...http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Thursday, July 29, 2010

JK Aapisha Manaibu Katibu Wakuu.



JK katika picha ya pamoja ya Manaibu Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali baada ya kuwaapisha leo Ikuku jijini Dar. (Picha:Mwanakombo Jumaa wa MAELEZO)
Reactions::

TBL yaipiga tafu TASWA FC



Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milion 4.8 kwa Mwenyekiti wa TASWA FC,Majuto Omary kwa ajili ya mashindao ya Bonanza huko mkoani Arusha.katikati ni Afisa Uhusiano wa TBL,Lilian Erasmus
Reactions::

Mbuyu...



Unakadiriwa kufikisha miaka mia tano. Upo maeneo ya Kaole mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Reactions::

Women Living with HIV and AIDS have a right to know about Reproductive Health – Dr. Julitta Onabanjo




Dr. Julitta Onabanjo, the United Nations Population Fund (UNFPA) Representative has highlighted the importance of reproductive health information and services for women living with HIV and AIDS.”All women including women living with HIV and AIDS have a right to sexual and reproductive health care including the prevention of HIV infections and the treatment of HIV related illnesses.

Only when women are healthy can they effectively contribute to social and economic development of their communities and the nation”. Dr. Onabanjo commented ahead of an advocacy and training workshop on ‘Reproductive Health and Rights for Women Living with HIV and AIDS (WLHA)’.

The three days workshop, which takes place in Dar es Salaam from 28th -30th July aims at empowering WLHA with capacity in advocating for their reproductive health and reproductive rights.

The organizers of the workshop, National Council of People Living with HIV and AIDS (NACOPHA) sees the workshop as a stepping stone and very crucial at empowering the women since it is fundamental to their well-being and that of their partners and children. NACOPHA also sees this as their contribution to national efforts in integrating sexual and reproductive health and HIV services.

In Tanzania, the HIV prevalence among women is almost 2 per cent higher than men (6.8% vs 4.7%). The Government has initiated a number of programmes on HIV and AIDS care, treatment, support and prevention.

Although the number of new HIV infections are still high in Tanzania (almost 200,000 annually), there have been successes in improving care and treatment services for People Living with HIV and AIDS (PLHIV). This calls for a greater emphasis on addressing the reproductive health needs of PLHIV, especially women who form the majority and currently accessing care and treatment services.

Dr. Chilanga Asmani, UNFPA’s HIV and AIDS Programme Officer comments that a number of guidelines exist that address the specific sexual and reproductive health needs of women living with HIV and AIDS. “All women have the same rights concerning their reproductive desires and their sexuality, but WLHA require additional care and counseling during their reproductive life”. HIV infection accelerates the natural history of some reproductive illnesses, increases the severity of others and can affect the ability to become pregnant or the outcome of the pregnancy.

In 2009 an inter-agency guideline titled ‘Advancing the sexual and reproductive health and human rights of People Living With HIV (PLHIV)’ was released and different national HIV and AIDS guidelines, plans and strategies also address the importance of supporting PLHIV to access SRH services and information. These global and national guidelines will be used during the NACOPHA workshop.

NACOPHA is funded and works closely with UNFPA and other UN agencies under the UN Joint Programme on Support to the National HIV and AIDS Response. NACOPHA is a Non Governmental Organization which was established in 2003 with the purpose of bringing together people living with HIV/AIDS for the purpose of increasing participation and improving their lobbying capacity in their responsibility towards waging war against HIV/AIDS in Tanzania.

For more information about HIV & AIDS
contact
Dr. Chillanga Asmani:
Asmani@unfpa.org;

Information about UNFPA
contact
Sawiche Wamunza:
wamunza@unfpa.org;

Further information about NACOPHA
contact
Deogratius Peter:
nacopha@yahoo.com
Reactions::

Enzi Za Biashara Ya Watumwa.



Eneo hili ndipo mahali ambapo watumwa walikuwa wanafungwa minyoro wakati wanasubiri kusafirishwa. Ni pembeni tu ya Bandari ya Bagamoyo.
Reactions::

Mamba Hao.....






Maeneo ya Kaole Bagamoyo. Mamba hawa ni Kivutio kikubwa cha Utalii katika eneo hili.
1.Mamba huishi miaka zaidi ya 150.

2.Mamba mkubwa hula kilo 28.

3 Mamba hula mara moja kwa wiki na ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki mbili bila kula

4.Mamba hana ulimi, humeza tu bila kutafuna

5.Mamba huvuta hewa nchi kavu na kuihifadhi na anaweza kuzama majini zaidi ya masaa matatu.

5. Hutaga mayai zaidi ya 70, mayai hayo hutaga kwenye mchanga. Kuenguliwa kwa mayai ya mamba huchua zaidi ya siku 60 na hutengemea sana joto la mwanga wa jua.

Pichani chini ni mamba mwenye umri wa miaka 60 na anakadiriwa kufikia uzito wa kilogram 340.
(Picha:Victor Makinda)
Reactions::

Turkish Airlines Ndio Yenyewe: Bei Nafuu, Huduma Bomba!




1. Huduma zao ndani na nje ya ndege ni za kiwango cha kuzidi hata baadhi ya mashirika makubwa ya ndege tuliyoyazoea. Hii ni pamoja na menu murua kabisa.

2. Ndege niliyopanda imeruka kwa wakati kutoka Dar na imeruka kwa wakati kutoka Instabul na kufika Stockholm kwa wakati. Inaonyesha jamaa wako makini katika kuzingatia muda. Hata takwimu zao kimataifa zinaonyesha hivyo.

3. Kusafiri na Turkish Airlines hakuchoshi. Abiria unaondoka Dar saa ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Instanbul



Uturuki, picha ya kutoka angani.
Reactions::

Wednesday, July 28, 2010

Uppsala



Leo jioni.
Reactions::

" Kilimo Kwanza, Sweden!"



Per akiwa kwenye trekta lake kuelekea shambani. Nimeshatoa mchango wangu kwenye shughuli yake ya shamba. Kesho naelekea Stockholm. Nimekuwa na wakati mzuri nyumbani na shambani kwa Per. Wakati mwingine ni vizuri kwa afya ya mwili na akili kufanya kazi za mikono.
Reactions::

Chai Masala, Uppsala



Leo jioni nilikaribishwa chai masala nyumbani kwa rafiki zangu, Anna-Karin, Hussein na binti yao Miriam. Wanaishi mji wa Uppsala. Nilipata wakati mzuri na nilifurahi kufika Uppsala. Ahsante sana Anna-Karin, Miriam na Hussein.
Reactions::

Injinia Ajitolea Kujenga Daraja

AN "engineer" from Langa township near Cape Town is the darling of the community after he built a pay-bridge over a canal - allowing an easy crossing to many areas previously difficult to access.

The 8m wooden bridge provides Langa residents with an easy route - for 50 cents - to the Bonteheuwel clinic, Vanguard Mall in Athlone and N2 - and is manned daily from 8am to 6pm by owner-creator Sebenzile Mazembele.
Hundreds of people cross the bridge each day, but some do not have to pay because of the high level of unemployment, he says.
Mazembele says he makes about R50 a day during the week and about R60 at weekends.
Sowetan visited the bridge yesterday morning and witnessed scores of people, some from Khayelitsha, crossing the bridge to visit their relatives in the Langa community.
Some were happy to pay while others pleaded poverty.
"When I started building it people thought I was mad. I was working alone, knee-deep in dirty water in the canal. I knew one day they would appreciate this," Mazembela says.
"I noted that people were struggling to access many areas since the other bridge built by the government is far from the community.
"I want to help people. I want us to help each other. I also want to put bread on the table.
"Some people can't pay me. I just pray for them to get jobs so that they are able to pay one day.
Source: http://www.sowetanlive.co.za/news/2010/07/28/the-bridge-man
Reactions::

Polisi Yafafanua Kifo Cha PC Suzani.



Jeshi la Polisi nchini limesema kifo cha askari Polisi WP.7338 PC Suzana kilichotokea katika kituo cha Polisi Tarime tarehe 4/7/2010 kilitokana na tukio la askari huyo kujipiga risasi kifuani
Reactions::

Vodacom Yazindua Vocha Ya Shilingi Mia Tatu.




Mteja wa simu za mkononi wa Vodacom Tanzania Erick Kabelege(kulia)akiangalia salio lake aliloingiza mara baada ya kupewa laini ya simu iliyosajiliwa na vocha mpya ya shilingi 300“JITI TATU”ya kampuni hiyo na mfanyakazi wa kampuni hiyo Sharifa Maggid(kushoto)Vocha hiyo imezinduliwa leo na kugawiwa bure maeneo mbalimbali jijini Dares salaam,katikati Emmanuel Mwasaga. (Michuziblog)
Reactions::

SHUKRAN: HAJRA KASSU ALOO



Familia ya Kikeke na Kassu Aloo , inatoa shukrani za dhati kwa ndugu,
jamaa, marafiki na majirani kwa misaada yao ya kiroho, hali na mali wakati
wa kumuuguza, kifo na hatimaye mazishi ya mpendwa Mama yetu, HAJRA
KASSU ALOO ambaye alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe
24.06.2010 sawa na mwezi 11 Rajabu na kuzikwa tarehe 27.06.2010 sawa na
mwezi 14 Rajabu Kenya makaburi ya Pasua, Moshi.
Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Madaktari wa Emergency MNH Dk
Alwyn Mziray, Dk Faith Ringo, Dk Henry Joseph na Dk Mpoki wa ICU MNH
na wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili ICU na Madaktari wa Regency ,KCMC,
Mtakatifu Joseph ya Moshi, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF) na watumishi wote wa Mfuko , Uongozi na
wafanyakazi wote wa BBC idhaa ya Kiswahili, J Ray McDermott, Jumuiya ya
Watanzania waishio Houston Texas na Kikundi cha akina mama cha Tumaini
Jema cha Matete Kimara Bucha.
Kwa kuwa sio rahisi kumshukuru kila mmoja peke yake, tunaomba mzipokee
shukrani zetu kwa namna ya pekee na Mwenyezi Mungu awajaalie kila la
kheri kwa upendo wenu.
Khityma (AROBAINI) itafanyika nyumbani kwa marehemu Hajra Kassu siku
ya Jumamosi tarehe 31.07. 2010 (Mwezi 19 Shabani) Uwanja wa sabasaba,
Moshi mjini kuanzia saa 4 asubuhi.
Karibuni sana.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati
Wana Familia ya Kikeke na Kassu Aloo
INNA LILAH WA INNA ILLAHI RAJIUUN
Reactions::

Kesho Nitakuwa Mitaa Ya Kati Stockholm!



Pichani tunapata mlo wa jioni tukiwa nje na jua linawaka nyumbani kwa rafiki yangu Per. Pichani hapo ni saa tatu usiku. Jana tulifanya kazi shambani mpaka saa mbili usiku. Katika majira haya ya kiangazi, jua nchini Sweden linazama kunako saa tano usiku! Leo nitaendelea kupiga jalamba kumpa tafu mshkaji shambani kwake. Kesho Alhamisi nitakuwa jijini Stockholm kusafisha macho kabla ya kupanda basi saa kumi jioni kutoka Sthlm kuelekea mji wa Orebro na Karlskuga. Haya basi, kesho nitakuwa mjini Sthlm, kama kuna anayejisikia kuni-join au nim-join kwa kikombe cha chai nitafurahi. Namba yangu ni Comviq 0762 300064, msije mkanilaumu; "Oh ' Mwenyekiti' kaja kimya kimya na kaondoka kimyakimya!".
Reactions::

Gari Hili Linakwenda Kwa Nguvu Ya Gesi



Ni gesi inayotokana na mabaki ya mimea. Analitumia Mkulima Per Eklund kwa shughuli za kusafirisha mazao na hata nyumbani. Bei ya gesi ni nusu ya bei ya diseli. Sweden bei ya diseli lita moja ni shilingi za Kitanzania 1200 na lita moja ya gesi inayotumika kwenye gari hilo pichani ni shilingi za Kitanzania 750.
Reactions::

Mtembelee Mkulima Per Eklund Shambani Kwake!




Chini ni squash, moja ya aina ishirini za mboga mboga zinazopatikana shambani kwa Per pichani kushoto akiwa na jirani yake. Maelezo mafupi kwa king'eng'e kuhusu shamba lake-Alsike Trädgård is situated 5 km from the small town Knivsta. It’s about 15 km to Uppsala and 50 km to Stockholm. We live in a beautiful country area close to the lake Mälaren and the national reservation Morga Hage (good area for recreation and bath).

We grow vegetables on 0,8 ha close to a small lake. We have a big varity of crops and like to experiment with different types of cultivation. Close to our main house lays a small greenhouse for plants in springtime and wine and tomatoes in summertime. It’s closely connected to our chickens (its just 10 of them). Mtembelee shambani kwake; http://alsiketradgard.se
Reactions::

Kisima Cha Maajabu Bagamoyo.




1.Kisima hiki kipo eneo lililojulikana kwa jina la Pumbuji, sasa ni Kaole mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

2.Kilijengwa karne ya 13 kando ya msikiti kwa ajili ya kutawaza waumini wa dini ya kiislam chini ya usimamizi wa Shekhe Alli Bin Jumaa aliyefariki mwaka 1273.

3.Maji ya kisima hiki hayajai wala hayapungui ujazo wake katika majira yote ya mwaka.

4.Maji yake hayana chumvi (ni maji baridi) licha ya kuwapo kando ya Bahari mita chache tu.

5.Watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania hufika mahali hapa kujionea maajabu ya kisima hiki na maajabu mengineyo ya kihistoria yaliyopo eneo hili la kaole mjini Bagamoyo.

Picha ya chini Mdau wenu Victor Makinda.
Nami sikukubali kupitwa nikateka na kunawa maji ya kisima hiki.
Reactions::




Reactions::

Mjini Bagamoyo Jana Mchana.






1.Jengo la Police Mess Bagamoyo jana mchana.
2.Boma la Wajerumani.
3.Jengo la Mwana Mfalme.
4 Pwani ya Bagamoyo jana mchana
5.Nyumba kama hii ni nyingi kweli mjini Bagamoyo.(Picha:Victor Makinda)
Reactions::

Neno La Leo: Ulaya Mgeni Jembe Siku Ya Kwanza!



Jana nilifika Sweden saa tano na nusu asubuhi nikitokea Dar. Mwenyeji wangu alinipokea Uwanja wa ndege. Alikuja na gari yake inayotumia gesi inayotokana na mabaki ya mazao. Gharama ya gesi hiyo ni nusu ya gharama ya diseli. Sweden kuna vituo vya kujazia gesi ya magari.

Gari lake lina nafasi kubwa nyuma. Ni gari analotumia zaidi kubebea mazao yake kupeleka kwa wateja wake. Analitumia pia kwa matumizi ya nyumbani.Nilipofika nyumbani kwake ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Mkutano Wa AU Wamalizika, JK Aagana Na Museveni





1. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda muda mfupi baada ya kumalizika mkutano wa 15 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU uliofanyika Kampala, Uganda.

2. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa 15 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika huko Kampala Uganda.

3. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji jijini Kampala jana mchana. ( Picha: Freddy Maro)
Reactions::