Mwenyekiti wa klabu ya simba Ismail Aden Rage amelitaka gazeti la mwanasport kumuamba radhi ndani ya siku kumi na nne kutoka na gazeti hilo kuandika makala ambayo si yakweli kweli juu yake yenye kumtuhumu mambo mbali mbali ya kiutendaji katika timu hiyo kwa nafasi yake aya uenyekiti. (Mdau)
Tuesday, August 31, 2010
Rage Achimba 'Mkwara' Gazeti Mwanasport'
Mwenyekiti wa klabu ya simba Ismail Aden Rage amelitaka gazeti la mwanasport kumuamba radhi ndani ya siku kumi na nne kutoka na gazeti hilo kuandika makala ambayo si yakweli kweli juu yake yenye kumtuhumu mambo mbali mbali ya kiutendaji katika timu hiyo kwa nafasi yake aya uenyekiti. (Mdau)
Karume Katika Ufunguzi Wa Mkutano Wa Kujadili Ugaidi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Augustino Ramadhani. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
| Reactions:: |
Hakuna Aliyefukiwa na Kifusi Machimbo Dhahabu Geita....
1.Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akipata maelezo ya uvumi wa kufukiwa kwa wachimbaji wadogo zaidi ya 70 katika machimbo ya dhahabu ya Nyakagwe kutoka wa Ofisa madini mkazi wa wilaya ya Geira Donald Mremi.
2. Greda la kampuni ya GGM ambao ni wamiliki wa mgodi wa Geita wakifanya zoezi la ufukuaji katika machimbo yasiyo rasmi ya Nyakagwe baada ya kusikika madai ya kufukiwa kwa zaidi ya wachimbaji wadogo 70,hata hivyo hakuna mwili hata mmoja uliopatikana.(Michuziblog)
| Reactions:: |
Kocha Mpya Netball.....
Kaimu katibu mkuu wa CHANETA Rose Mkisi.
Kocha mpya wa timu ya taifa ya netiboli anatarajia kutua nchini kesho saa sita mchana tayari kwa zoezi zito lz kukinoa kikosi cha taifa cha timu hiyo kilichopo kambini mjini Kibaha. Timu hiyo inajiaandaa kwa mashindano ya kimatifa yaliyotarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini mwezi ujayo.(Mdau)
| Reactions:: |
Pingamizi La Uchaguzi Dhidi Ya JK...Tendwa Alonga
Dr Slaa Amnadi Mnyika Ubungo


1.Mgomea Urais kwa tiketi ya CHADEMA,Dr. Willblod Slaa akimnadi kwa wapenzi na wakereketwa wa chama hicho mgombea ubunge jimbo la Ubungo, John Mnyika katika uzinduzi wa kampeni Jimboni Ubungo. Dr Slaa amemuhakikishia Mnyika kuwa atakuwa nae bega kwa bega kuhakikisha kwa pamoja wanashindi katika uchaguzi mkuuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi octoba.
2.Wasanii wa muziki wa Bongo Freva wakiongonzwa na mgombea Ubunge wa jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II (SUGU) wakitoa burudani katika ufunguzi wa kampeni za Mnyika Kimara Suca jijini Dar es Salaam.
| Reactions:: |
Bado Niko Njombe, Mtandao Ni Afadhali Ya Jana!
... Na Njombe kibaridi bado kipo. Hata hivyo, naona wanafunzi wangu wamejitahidi kupost picha na maelezo ingawa picha nyingine nimeona haina title. Hata miye sijui ilihusu nini! Taratibu tutafika, hata Roma haikujengwa kwa mwaka mmoja. Mtandao ukitulia nami nitarudi tena kuongeza nguvu.
Siku Njema.
Maggid
Siku Njema.
Maggid
| Reactions:: |
Waumini Wamlalamikia Askofu Jimbo La Rulenge

Asante mwenyekiti kwa kazi nzuri uifanyayo hasa kutuelimisha kwa njia ya Blog, nasema hongera sana mkuu! Hivi karibuni nilikuwa ngara mkoani kagera kufanya utafiti kwenye masuala yangu ya shule, lakini ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
| Reactions:: |
Monday, August 30, 2010
Marais Waliostaafu Kwa Amani Wajadili Amani Dar,
1. Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi (katikati) akiongea na washiriki wa mkutano wa marais wastaafu wa Afrika waliostaafu madaraka kwa njia ya amani leo jijini Dar es salaam. Kushoto balozi Charles Stith ambaye pia ni mkurugenzi wa kuhifadhi kumbukumbu za marais wa Afrika.
2.Sehemu ya washiriki wa mkutano huo
| Reactions:: |
Tunazindua Ilani, Tutaanza Kampeni Baada Ya Ramadhani

Mgombea urais kwa Chama cha NCCR Mageuzi, Mh. Hashim Rungwe akionyesha ilani ya uchaguzi ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho jana jijini Dar.
Mwenyekiti wa chama hicho taifa James Mbatia alisema chama chake kitazindua kampeni zake kitaifa Septemba 11 baada ya mfungo wa Ramadhani ili kutowakwaza Waislam ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu.(michuziblog)
| Reactions:: |
JK 'Alivyofunika' Mbeya
Niko Njombe Na Mtandao Sina!
Tangu jana Jumapili niko Njombe. Modem yangu imegoma. Hapa naandika nikiwa kwenye mtandao wa kuazima. Ndio kwanza na mimi nimeitembelea mjengwablog tangu niondoke Iringa jana. Nashukuru wanafunzi wangu watatu wa enzi za Kwanza Jamii ni mahodari wa kupost picha za matukio ingawa captions zao inabidi wakati mwingine niingie nizibadilishe. Vinginevyo, sote tunajifunza na tuna mapungufu yetu. Hakuna aliye mtimilifu.
Poleni kwa usumbufu wowote kama umejitokeza.
Maggid
Njombe.
Poleni kwa usumbufu wowote kama umejitokeza.
Maggid
Njombe.
| Reactions:: |
Sunday, August 29, 2010
Haya Ndio Maisha Ya Kila Siku Ya Akina Mama Vijijini
Castro Claims Osama Bin Laden Is CIA Agent


Fidel Castro has said Osama bin Laden is in the pay of the CIA and was summoned up whenever George W Bush needed to scare the world.
"Any time Bush would stir up fear and make a big speech, bin Laden would appear threatening people with a story about what he was going to do," Mr Castro said.
"Bush never lacked for bin Laden's support. He was a subordinate.".(Sky News)
| Reactions:: |
Msiba Washington DC MaryLand

Andrew Pesa Igala. amefariki Huko Washington DC Maryland . Juzi tarehe 26 aug 2010, Sasa hivi tunaomba Michango ya hali na Mali kwa ajili ya kufikisha $10.000 Ambazo ni gharama za kusafirisha mwili kuja Tanzania. Kwa habari zaidi wasiliana na MR Prosper Sugai Tell +819022308435 Ngoya Willy +81 9072187118 kwa USA wawasiliane na Mr. Mziray Tell no+12162350138 michango ya haraka Inatakiwa kwa ajili ya kufanikisha kufikisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwa mazishi, wapendwa katika jina la mungu tufanikishe msiba huu kwa kuchangia gharama za kusafirisha mwili wa marehemu mungu awabariki wote.
| Reactions:: |
JK Agombewa Sumbawanga,,,


Wakazi wa mjini Sumbawanga licha ya kujitokeza kwa maelfu kumlaki na kumsikiliza mgombea urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Kikwete,walijikuta wakiwa katika purukushani kugombea kupata fursa ya kusalimiana kwa kushukana mikono na Rais Kikwete. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani wakazi wa mjini sumbawanga walivyokuwa wamejawa na shauku ya kumwona Rais wao mpendwa na mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM.(Picha: Mdau, Sumbawanga)
| Reactions:: |
Tutazame Kusini......
Zitto Alipozindua Kampeni Kijijini Mkongoro
1.Mgombea ubunge jimbo la Kigoma kaskazini Zitto kabwe akivalishwa vazi la jadi la kabila la waha na kutawazwa kuwa mwami (Mtemi) wakati wa uzinduzi wa kampeni zake za kuwania tena nafasi hiyo zilizofanyika katika kijiji cha mkongoro.
2. Mgombea ubunge jimbo la Kigoma kaskazini Zitto kabwe akihutubia mkutano wa hadhara ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampeni zake za kuwania tena nafasi hiyo zilizofanyika katika kijiji cha Mkongoro.(Picha:Mdau Kigoma)
| Reactions:: |
Mama Salma Kikwete Ziarani Dodoma.
1.Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT mkoa Dodoma Fatma Tawfiq alipowasili katika uwanja wa ndege Mkoa wa Dodoma jana.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. James Msekela. (michuziblog)
2.Kikundi cha ngoma ya asili cha wakina mama mkoani Dodoma kikitumbuiza mbele ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kushoto) alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Dodoma katika muendelezo wa ziara zake za kuwahamasisha wanawake wa UWT kuhusu Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
| Reactions:: |
Saturday, August 28, 2010
JK Atinga Mpanda



1. Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja muda mfupi baada ya mgombea huyo kuwasili katika uwanja wa michezo wa mjini Mpanda ambapo alihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni jana mchana.
2. Baadhi ya wakazi wa mji wa Mpanda wakimkaribisha kwa mabango mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete jana mchana.(Picha: Freddy Maro)
| Reactions:: |
CHADEMA Wazindua Ilani, Kampeni.





1.Mwenyeki wa CHADEMA,Freeman Mbowe akimkabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho mgombea Urais wa chama kwa tiketi ya chama hicho Mh Willbrod Slaa leo jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar mara baada ya kuizindua.
2.Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akisalimiana na Mgombea Ubunge jimbo la Ubungo kwa chama kwa tiketi ya CHADEMA,John Mnyika mara baada ya kuwasili viwanjani vya Jangwani huku akilakiwa na shangwe za wananchi waliokuwa wamefika viwanjani hapo jioni ya leo.
3.Aliyekuwa mbunge wa Maswa na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,na baadae kuhamia CHADEMA,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi leo jioni wakati CHADEMA hicho ikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
4.Wananchi wakionesha kuunga mkono baadhi ya mambo yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho leo jioni katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.
5.Baadhi ya Watu wakiwa juu ya mti huku wakisikiliza mambo kadha wa kadha yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi wa juu wa chama cha CHADEMA wakati wa uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho jioni ya leo katika viwanja vya Jangwani.(Jiachieblog)
| Reactions:: |
JK Atua Kigoma..... Maelfu Wajitokeza Kumsikilza.
Chagueni Viongozi Kutoka CCM......
Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na Maendeleo (WAMA) ,Mama Salma Kikwete, akiongea na wanachama wa UWT jana Wilayani Mafia katika ziara ya siku moja aliyoifanya wialayani humo kuwahamasisha wanacham wa umoja wa nawake Tanzania kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao. (Picha:Mwanakombo Jumaaa Maelezo Dar es salaam)
| Reactions:: |
Kivuko Kipya
Kivuko kipya MV Pangani cha mto Pangani hapa kikisubiri abiria katika feri ya njini Pangani ili kuwavusha upande wa pili unaoitwa Mwera eneo la mto huo lilinishangaza kidogo kwani mpana sana na ukiangalia utaona kama maji ya mto Pangani na na maji ya Mkondo wa Bahari ya Hindi yanakinzana sana hasa wakati mawimbi ya bahari ya yanapokuja kupiga ufukweni ni eneo zuri la utalii kama litaendelezwa vizuri na Serikali hasa uboreshaji wa miondombinu ya barabara kwani barabara hiyo ya Pangani pia inaweza kukufikisha mjini Bagamoyo kwa kupitia katika hifadhi ya Saadani ukitokea Mkoani Tanga. (Fullshangwe)
| Reactions:: |
Bi Mkora: Kinachochangia Mwenzako Asijishughulishe Kitandani..

Pole mdau kwa yanayokukuta,
Kuna vitu vingi vinaweza kuchangia hayo kama walivyokueleza wadau waliotangulia kutokana na uzoefu wao ambao nitawaita masomo. Kungwi Bi Mkora ana
1. Mko kwenye uhusiano wa namna gani? Mke na mume, au bibi na bwana au wa kirafiki? Aina ya uhusiano mlionao mara nyingi huchangia katika namna ambavyo mwanamke atashiriki katika tendo la ndoa. Ikiwa yuko kwenye mahusiano yasio na uhakika wala mwelekeo basi mara nyingi hushiriki kwa hofu na wasi wasi wa kupata mimba nje ya ndoa, na kuogopa kuwa atakapopata hiyo mimba anaweza kuachwa solemba na mtoto wake. Pia anaweza kuwa na hofu ya kukutwa na mwenye mali maana yake sie wanawake huwa hatuamini kuwa mwanaume anaweza kukaa siku zote hizo hana mwenyewe, kwa hiyo wakati mwenzio anajishughulisha wewe kichwa chako kinazunguka kuhusu kufumwa na mwenyewe, au ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
| Reactions:: |
Friday, August 27, 2010
KUMBUKUMBU: Mzee Richard J. Kasella Bantu

Mwezi uliopita 15-07-10 Familia ya Kasella-Bantu tulimpoteza mpendwa Baba yetu mzee Richard J.Kasella-Bantu.
This Saturday 28-8-10 will be our beloved Fathers Arubaini. On behalf of the Kasella-Bantu family we would like to inform family and friends and all of those who knew Mr Richard to come to celebrate his life through prayer. The mass will be held at home in Mbweni from 8:00 am.
Our Father was an intelligent, loving and a wonderful person to know, you have taught us life is precious and should be shared with loved ones. We thank God for his life and the moments we shared. You were a great man to many and a rock to your loving family, you will be deeply missed by your loving wife Florence Kasella, your son's Ray,Roy and Ronald. Your Brothers, sisters, Uncle's, Aunties, Grandchildren, family and Friends.
Lamentations 3:31-33
For men are not cast off by the Lord forever.Though he brings grief, he will show compassion, so great is his unfailing love.For he does not willingly bring affliction or grief to the children of men.
Thank you to all our family and friends and those who have grieved with us and continue to bring the family comfort through prayer.
| Reactions:: |
Katiba Mpya, Kenya Mpya!

Leo Agosti 27, 2010, watu wa Kenya wamefungua ukurasa mpya katika historia ya taifa lao. Ni kwa kusainiwa kwa Katiba mpya itakayolinda maslahi ya Wakenya wa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Hongera sana jirani na watani zetu wa Kenya! ( Pichani ni watoto wakipita katikati ya reli kitongoji cha Kibera, Kenya. Picha hiyo niliipiga mwezi Januari, mwaka 2007)
| Reactions:: |
Niliwahi Kushiriki Mkutano Wa Hadhara Uhuru Park, Nairobi
Born Again Pagan: Gathering At Uhuru Park!

oh, mighty rivers of optimism
from both worlds drawn,
like deer panting for water,
walalahoi common goal-crying
for the world better place;
montage voices reverberating
through the Nairobi cliffs
and permeating its air
against inequality
and social injustice
in the world!
( From Mjengwablog's Archive, Born Again Pagan, 2007)
| Reactions:: |
Tanzani Mwenyeji Mkutano Wa Mahakama Ya Afrika

Ofisa Habari na Mawasiliano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika (African Court on human and people’s Rights) Kamel Grar (kushoto) akifafanua jambo leo jijini Dar es salaam kwa waandishi wa habari wakati wa maandalizi ya mkutano wa 18 wa Mahakama hiyo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Septemba 2010 hadi tarehe 1 Oktoba 2010 nchini Tanzania. Kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama hiyo Dkt . Robert Eno.(Moblog)
| Reactions:: |
JK Na Watoto
Subscribe to:
Posts (Atom)














