Subscribe:

Thursday, September 30, 2010

Viongozi Wa Chadema Walipokutana Na Viongozi Wa Dini




1.ASKOFU Tomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati (kushoto), akizungumza na mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willibroad Slaa, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni Dar es Salaam, baada ya ujumbe wa Kamati ya viongozi wa dini nchini akiwemo askofu Laizer, kufanya mazungumzo na viongozi wa CHADEMA jana, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia mustakabali utakaowezesha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kufanyika kwa amani na kutozusha rabsha baada ya matokeo, kwa kuzingatia mambo kadhaa ikiwemo vyama shiriki kukubali matokeo baada ya uchaguzi. Kulia ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na wa tatu ni mgombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama hicho, John Myika.

2.Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (katikati) akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum wakati mgombea huyo alipokutana na viongozi mbalimbali wa dini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mgombea mwenza, Said Mzee Said (jachieblog)
Reactions::

Jeshi La Polisi Laboresha Vifaa





1. Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha akimtunukia Cheo Mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo uafisa wa Polisi PC Happines Temu wakati wahitimu hao walipotunukiwa vyeti vya kumaliza mafunzo hayo leo kwenye Chuo cha maafisa wa polisi (Dar es salaam Police Academy) yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Wahitimu hao pia walionyesha uwezo wao wa kukabiliana na wahalifu wakati zinapotokea ghasia katika maeneo mbalimbali ya nchi na kuonyesha uwezo mkubwa katika kutumia vifaa mbalimbali ambavyo ni vya kisasa kabisa Hongera Serikali kwa kuboresha vitendea kazi kwa jeshi hilo ambalo lina kazi kubwa ya kuhakikisha raia wote wanaishi kwa amani nchini ikiwa ni pamoja na kuwaongezea mbinu mpya askari kitu kitakachowaongezea ufanisi wawapo kazini.

2.Wahitimu wa mafunzo hayo wakipita kwa gwarede la Heshima mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha hayupo pichani.

3.Magari Maalum papya yatakayokuwa yakitumiwa na jeshi la polisi Kikosi maalum cha kutuliza fujo FFU likionyesha uwezo wake wa kuzuia ghasia kwa kurusha maji leo mbele ya wageni na waalikwa mbalimbali.
Reactions::

Mkono Wa Heri.. Vodacom Miss Tanzania.. Rudi Na Ushindi





1.Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akimsisitizia jambo Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel wakati alipokuwa akiondoka kweda Nchini China kwa ajili ya kushiriki shindano la Dunia Miss World 2010. Kushoto ni Ibrahimu Kaude Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania.

2.Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania akimuaga Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo wakati mrembo huyo alipokuwa akiondoka kuelekea nchini China ambako atawakilisha nchi kwenye Shindano la Miss World 2010 litakalofanyika Oktoba 31 jijini Sanya.

3.Romana Mpangala ambaye ni bibi yake Vodacom Miss Tanzania Genevive Emanuel akimuaga mjukuu wake kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere wakati mnyange huyo alipokuwa akisubiri kupanda ndege kuelekea nchini China kwa ajili ya kushiriki shindano la Miss World 2010, katikati ni mama yake Maria Mpangala. (Picha:Mdau)
Reactions::

Balozi Peter kallaghe kuongea na Watanzania Birmingham




Kaka Mjengwa,,Tubandikie Hiyo...
Kaka naomba utuwekee hili tangangazo la Mh. Balozi kuzungumza na Watanzania wa Birmingham na vitongoji vya siku ya jumamosi 02/10/2010 kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11. address ipo kwenye hiyo flyer nimekutumia.
Naomba uwasisitize Wabongo watakaokuwa wanakuja kuzingatia sana muda.

Asante kwa kazi yako njema kaka.

Jackson M
Katibu TA-Birmingham / Mjumbe TA-Taifa
Reactions::

Mdau Kaanzisha Mjadala Huru: .. Tumjadili Dr Willbroad Slaa...



Zikiwa zimebaki takribani siku 30 kabla ya kupiga kura octoba 31 nimeona ni vema kuanzisha mjadala huu huru ambao kimsingi hauna lengo la kuegamia upande wowote na kwa mgombea yoyote wa chama chochote. Lengo ni kupata maoni toka sehemu mbali mbali kutoka kwa wadau wetu katika dhana ile ile ya kubadilishana mawazo kwa lengo la kuelimisha;.....Dr Wilbroad Slaa.... Ni mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Mdau toa maoni yako ikijumuisha matarajio yako juu ya Dr Slaa na CHADEMA ikiwa Dr Slaa akashinda kinyang'anyiro katika uchaguzi wa urais wa jamuhuri ya muungano nini unatarajia toka kwa Dr Slaa na CHADEMA?
Imeletwa kwako na mdau wa Mjengwablog..
Reactions::

Maji,,,,Na Ujumbe Wa Matarajio...



Dumu Shilingi500, Nzega jana mchana.
Reactions::

JK Akiwa Mjini Nzega Jana....







1. Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr Jakaya Kikwete akimnadi mgombea ubunge jimbo la Nzega kwa tiketi ya Chama hicho Dr Hamis Kingwangwala jana mchana katika viwanja vya Samora mjini Nzega.
2. Watu waliohudhuria katika mkutano huo wa kampeni mjini Nzega jan.
Picha nyingine ni mjini Nzega jana katika uwanja wa Samora kabla na baada ya mkutano wa kampeni za CCM.(Picha:Mdau, Nzega)
Reactions::

Swali Kwa Bi Mkora: Mwenzangu Anapenda Mara Nyingi Kwa Wiki, Nifanyeje?


Bi Mkora,
Nina shida, Nashindwa kuwauliza rafiki zangu, nimeona nikuulize kwa kutambua mchango wako kwa wengine. Mimi ni mwanamama, miaka yangu inakaribia 34. Nina mtoto mmoja. Shida yangu ni hamu ya kufanya tendo la ndoa. Sina, au labda niseme imepungua.
Mwenzangu anataka ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Tumepata Ugeni Kutoka HakiElimu




Jana kibaruani kwetu hapa Iringa tumepata ugeni kutoka taasisi ya HakiElimu. Mgeni wetu alikuwa Margareth Paul kutoka Idara ya Ushiriki wa Jamii. Katika mazungumzo yetu tumeainisha maeneo ambayo tunaweza kushirikiana baina ya jumuiya yetu; Karibu Tanzania Association na HakiElimu. Karibu Tanzania Association (KTA) inafanya kazi na programu tatu; Maktaba za Jamii, Kuwasaidia na kuendelea na masomo akina mama waliokatishwa masomo yao kutokana na uja uzito na Mafunzo ya Kujiendeleza kwa njia ya masafa kwa walimu na wakufunzi wa Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ofisi zetu ziko Akiba House, Chumba Namba 221, Iringa Mjini. ( Picha ya juu ni Margareth ( kushoto), Devota wa KTA na mimi, jana asubuhi.)
Reactions::

Na Da' Gil Yupo!



Iringa, wiki endi ya jana.
Reactions::

Mama Na Mwana


Makambako, hivi karibuni.
Reactions::

Kwa Wenye Kublogu!

Mazingatio kwa mablogger juu ya libeneke

Siku za hivi karibuni tumeshuhudia kila mtu akija na blog yake,mlundikano wa blog umezagaa kila kona ya .com,kila mmoja ana malengo yake binafsi,wapo waliokuja na blog kama njia ya kujitangaza,kuna waliokuja kwa ajili ya kutafuta umaarufu,wengine kwa kuwa mtu fulani ana blog nami lazima niwe nayo,kuna waliokuja kwa ajili ya kusaidia jamii(kama AfroIT Blog) na kuna walioamua kuja na blog kwa ajili ya kutengeneza pesa. Hivyo madhumuni ya blog ni mengi ambapo hutegemeana na mwana bklog mwenyewe.


Hivyo basi ushindani unakuwa mkubwa mno,kumbuka mazingira ya ushindani siku hizi yanazidi kuwa magumu hivyo unahitajika kuumiza kichwa ili kuibuka kidedea kwenye uwanja wa wanablog.


Kuwa na blog bila ufahamu au maarifa yake kwa undani kuna uwezekano mkubwa sana usifikie lengo lako,ingawa niwengi wetu inatuwia ugumu kupima ufikiwaji wa malengo zaidi ya kuangalia figure ya takwimu za watembeleaji ambazo kwa upande mmoja au mwingine zinaweza kuwa na mapotezo makubwa.

Hapo zamani kuna watu walisema,ukitaka kumnyima kitu mwafrika basi kiweke kwenye maandishi(kitabu),ila kwa dunia ya leo hii,kila kitu kipo kwenye maandishi tena kwa urahisi zaidi vilevile hii imani imepotea kwakuwa tumekuwa na mapenzi makubwa na kusoma vitabu,hii ni kwakuwa kama unataka kufahamu mambo mengi ni lazima uwe msomaji mzuri ma wada na vitabu mbalimbali huku ukijumuika na wataalam ambao watakusaidia kuweza kufikia lengo.Sisi kama nchi tunazoendelea bado tunahitaji kujifunza na kujua mengi zaidi kila kukicha.

Hivyo basi nimeambatanisha kitabu ambacho naamini kitakuwa na msaada mkubwa kwa wanablog wa kitanzania ambapo utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza blog inayolipa na kufanikiwa. Yote haya na mengine meengi yanapatikanika bure ndani ya AfroIT Downloads.
Download kitabu hiki nenda AfroIT Downloads au link ya chini
http://download.afroit.com/?p=1166
Reactions::

Picha Hii Ya Mwanakombo Jumaa Imenivutia!



Korosho na mabibo yake. Tandahimba, Mtwara. Mwaka juzi Tandahimba iliingiza shilingi bilioni 8 kutokana na zao la korosho. Uchumi wa korosho Tandahimba unawezekana. ( Picha: Mwanakombo Jumaa, MAELEZO)
Reactions::

Mama Salma Kikwete Azidi Kuchanja Mbuga



Pichani akikampeni Mtwara Mjini. ( Picha: Mwanakombo Jumaa, MAELEZO)
Reactions::

Vuvuzela Kwa Kwenda Mbele!



Mtwara Mjini. ( Picha: Mwanakombo Jumaa, MAELEZO)
Reactions::

MSIBA COLUMBUS, OH





Mr. Matthew Salukele (Marehemu)
Date of Birth: 22/02/1941
Died: 09/28/2010 @ 4:30 pm at St Ann’s Hospital Columbus Ohio.

Miss Happyness Salukele ( Daughter)
Happyness na David Salukele wanasikitika kuwataarifu habari ya msiba wa mpendwa baba yao,Mzee Matthew Salukele uliotokea leo jumanne Sept 28,2010 saa 10 unusu(4:30pm),St Ann's Hospital.

Tunaomba msaada wenu katika kukamilisha kusafirisha mwili wa marehemu Tanzania,Gharama za kuusafirisha mwili zinafikia $25,000.
Unaweza kusaidia kupitia Chase Bank Acc #917118267 Routing # 044000037.

Msiba upo Add:
1427 hideaway Woods Dr
Westerville OH 43081

Tunatanguliza Shukrani kwa msaada wako wa hali na mali utakaotoa hasa kwa kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa Baba yetu,
Baba Tulikupenda Sana lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi,kimwili hatuko pamoja,kiroho tutakua nawe siku zote mpaka hapo Mwenyezi Mungu atakapo tukutanisha tena,Jina lake lihimidiwe.

For more information Please contact:
David Salukele cell# 614-859-9602
Walter kalosi cell#614-537-1448
Happiness Salukele cell#614-772-5126
Adella Njau cell#614-446-9710
Dorah Njau cell#614-589-5685
Jacqueline Mjengwa Cell# 614-804-5237
Reactions::

Wednesday, September 29, 2010

Hussein Bashe Azua Kizaa Zaa Nzega Leo.. Mamia Waandamana.





1.Wananchi wa Nzega wakimbeba Hussein Bashe.
2. Wananchi wakiwa katika maaandamano
3. Wananchi wa Nzega wakisukuma gari iliyombeba Bashe.

Ni mara baada ya hotuba ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr Jakaya Kikwete ambapo pia alimnadi mgombea ubunge jimbo la Nzega Dr Hamis Kingwangala katika mkutano wa kampeni uliofanyika mchana wa leo katika viwanja vya Samora mjini Nzega, palitokea kizaa zaa kikubwa kutokana na kundi kubwa la wananchi kumzonga aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM ambaye alishinda kura ya maoni na baadae kufuatiwa na jina lake kutorudishwa baada ya mchujo, Kijana Hussein Bashe. Wananchi hao walifanya maandamano makubwa huko wakiimba nyimbo za kusifu Bashe na kumkataa Dr Hamis Kigwangwala ambaye ndiye aliyeteuliwa kuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM. Kigwangwala alishindwa katika kura za maoni na kushika nafasi ya tatu akitanguliwa na Hussein Bashe, na nafasi ya pili kushikwa na aliyekuwa mbunge wa jimboo hilo Lukas Selelii, yeye Kigwanwala akishika nafasi ya tatu na baadae majina hayo yalikatwa na kurejeshwa jina lake. (Picha na maelezo: Mdau aliyekuwepo Nzega)
Reactions::

Vodacom Miss Tanzania Akabidhiwa Bendera




1.Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel akiwa ameshikilia bendera yab Tanzania mara baada ya kukabidhia rasmi leo tayari kwa safari yake ya kuelekea nchini China katika jiji la Sanya ambako shindano la dunia Miss World 2010 linatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini humo. Mrembo huyo ataondoka kesho kwa ndege ya Shirika la ndege la Quatar Airways akipitia Uarabuni, Mongolia na kisha Sanya nchini China.


2.Esther Mkwizu ambaye ni Mwenyekiti wa Sekta Binafsi na aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi bendera ya taifa kwa Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel akikabidhi bendera hiyo huku wazazi wa Genevive wakishuhudia kulia ni baba yake Bw. Emmanuel Mpangala na kushoto ni mama yake Mary.(fullshangwe)
Reactions::

Ilani Ya Chadema





ILANI YA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI, OKTOBA 31, 2010
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

kupitia linki ifuatayo(bofya anuani hiyo chini kupata ilani)

http://www.chadema.or.tz/uchaguzi/2010/Ilani%202010-2015.pdf
Reactions::

Mama Salma Kikwete, Tandahimba






Picha ya juu ni kikundi cha Utamaduni. Chini ni akina mama waliofurahi wakati wakimsikiliza Mama Salma Kikwete. ( Picha: Mwanakombo Jumaa)
Reactions::

Mama Salma Kikwete Awanadi Madiwani Mtwara



Pichani ni baadhi ya madiwani hao. ( Picha: Mwanakombo Jumaa, MAELEZO)
Reactions::

Tuesday, September 28, 2010

Talib Hilal






Alipata kuwa mchezaji Simba na timu yetu ya Taifa. Kwa sasa anafundisha soka Oman. Picha hizo juu alipokuwa kwenye mafunzo ya FIFA kwa wakufunzi wa makocha wa soka iliyoandaliwa iliyofanyika Abu Dhabi.( Picha Kwa Hisani ya Talib Hilal)
Reactions::

Neno La Leo: Mwana Wa Gavana Anapotenda Kosa...



Na Maggid Mjengwa,

KUNA kisa cha mwana wa gavana katika Misri ya Kale. Mwana yule alitembea akijivunia cheo cha baba yake. Akajawa kiburi kufikia siku moja kumdhalilisha mwalimu wa shule mtaani huku watu wazima na watoto wengine wakiangalia.
Ndio, mwana yule alimchapa bakora ya matakoni mwalimu yule, hadharani. Mwalimu alifedheheshwa sana, maana hata kosa lake hakulijua. Mwalimu yule akafunga safari ndefu kwenda kuarifu jambo lile kwa mfalme wa nchi . Huko akapokelewa, akaeleza yaliyomsibu.
Mfalme akaamuru... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Ridhiwan Kikwete Sasa Ni Chifu Wa Wanyakyusa




1.Chifu Mwailemale (Ridhiwani Kikwete) akiwa amekalia kigoda baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa.

2.Machifu wa kinyakyusa Ernest Mwailemale (kushoto) na Glasswell Mwakalukwa wakimvisha golole,Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, alipotawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa na kuitwa Chifu Mwailemale juzi katika mkutano wa kampeni za ndani za kuweka mikakati ya kuipatia CCM ushindi wa kishindo,juzi katika Kata ya Ipinda, Kyela.
Reactions::

MO...Ana 'Vituko' .........




1.Baada ya kutoka katika mkutano wa kampeni huko Kisasida jana MOhamed Dewji (MO) njiani alikutana na mama mmoja akipampu maji kwenye kisima ambacho yeye MO alichangia kukichimba kama mbunge. Aliamua kumsaidia mama huyo kupampu maji kisimani hapo.

2.MO akiomba kura kwa mlemavu wa miguu Hamis Issa aliyefika kwenye mkutano wa kampeni katika Kitongoji cha Ng'aida kijiji cha kisaki wakati wa mkutano wake wa kampeni ulofanyika hivi karibuni.
Reactions::

Umoja, Mshikamano Na Undugu Ndio Nguzo Yetu.



Mwenyekiti wa CCM na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tamzania Jakaya Mrisho Kikwete (katikati Maalimu Seif Sharif Hamad katibu mkuu wa CUF na Prof Ibrahim Haruna Lipumba Mwenyekiti wa CUF.
Reactions::

JK Atua Kwa Kishindo Shinyanga...






1.JK akimnadi mgombea ubunge wa Shinyanga mjini Bw. S. Masele
2.JK akiingia uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga
3.Helikopta anayotumia JK ikitua nje ya uwanja wa Kambarage ambapo iliamsha msisimko mkubwa kwa maelfu ya wakaazi wa Shinyanga waliokuwa wakimsubiri kwa hamu jana jioni.
Reactions::

Adha Ya Usafiri....



Kijijini Kwachiga, Wilayani Handeni mkoani Tanga hivi karibuni.(Picha: Mdau:Mtanda)
Reactions::

Nimetunza Kadi Tangu Mwaka 1977....Hii Hapa.....



Mwanachama Mkongwe wa CCM Bi.Fatma Ndugulile akimuonesha Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kadi yake ya uanachama na risiti za malipo ya uanachama tangu mwaka 1977 wakati Bibi huyo alipokutana na Mgombea huyo wa Urais kwa kupitia CCM mjini Shinyanga jana jioni. Dr.Kikwete alimsifu Bibi huyo kwa uaminifu wake kwa CCM na umahiri wake wa kutunza risiti zake za malipo.
Reactions::

Duka La Matunda....



Mombo Mkoani Tanga.
Reactions::