Subscribe:

Sunday, October 31, 2010

Dr Slaa Apiga Kura Karatu



Reactions::

Ratiba Ya Kumuaga Syllersaid Mziray



Tunaomba utuwekee hii ratiba ya kuaga mwili wa marehemu Syllersaid Mziray, "Super Coach" kwa ajili ya mazishi yake yanayotarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar.

Taratibu hizi zitaanzia Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Kinondoni Biafra kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Tutashukuru sana.

4.00 – 05.00 Kuwasili Waombolezaji

05.00 – 5.30 Viongozi, Wageni Waalikwa wa CKHT kuchukua nafasi zao.

05.30 – 6.00 Nyimbo za Maombolezo.

06.00 – 07.00 Kuwasili Mwili na Ndugu wa Marehemu.

07.00 – 07.15 Wimbo wa CKHT kupigwa.

07.15 -08.15 Misa/Sala.

08.15 – 08.20 Maelezo ya Wizara ya Michezo, Mwakilishi wa Wizara.

08.20 – 08.25 Maelezo ya TFF, Mwakilishi wa TFF.

08.25 – 08.30 Maelezo ya Simba Sport Club , Mwakilishi wa Simba.

08.30 – 08.25 Wasifu wa Marehemu CKHT .

08.35 – 08.40 Maelezo ya mwisho ya MMC VC.

08.40 – 08.45 Shukrani ya Familia,Mhusika wa Familia,

08.45 – 09.45 Kuaga mwili wa Marehemu.

10.00 – 10.05 Wimbo wa Chuo.

10.05 Kuelekea Makaburini Kinondoni
Reactions::

Leo Nimepiga Kura Nyalumbu



Ni Kata ya Nyalumbu, Kilolo, Iringa. Niliongozana na wana wangu. Hali ilikuwa ni ya utulivu mkubwa. Kituo changu kilikuwa na waliojiandikisha 394. Kubwa kabisa lililonigusa ni pale Mama mtu mzima aliyehitaji msaada wangu ili aweze kupiga kura. Hakujua kusoma na kuandika. Aliulizwa kama anahitaji msaada wa mtu anaye...mwamini. Alinigeukia, akaniambia; " Mwanangu njoo unisaidie". Alikuwa akiangalia picha na rangi. Kazi yangu ikawa kumsomea na kumtilia tiki. Sitasahau, na naliona jukumu lililo mbele yetu.
Reactions::

' Matatizo Ni Kipimo Cha Akili!'




Utaratibu ukishapiga kura unatakiwa usimame mita mia moja toka kituo cha kupigia kura. Mimi na wanangu tuliamua kutembea kwa miguu kilomita moja kwenye mitaa ya kata ya Nyalumbu. Tumekutana na kuongea na jamaa kadhaa tuliofahamiana tangu huko nyuma. Tulikuwa na wakati mzuri sana pamoja.Kata ya Nyalumbu, Kilolo, Iringa, ni Kata yangu ya Uchaguzi. Mimi na familia yangu tuliishi kata hii kwa mwaka mmoja, 2004. Hapo kuna Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi pia.
Reactions::

Uliona Wapi Mmasai Anamkimbia Ng'ombe? " Utakoma Mwaka Huu!"

Reactions::

Usalama......



Maeneo mengi ya Tanzania leo yameripotiwa kuwa na hali nzuri ya usalama. Ulinzi umeimarishwa. Hatutaraji 'TOFAUTI' hata baaada ya matokeo ya kura kutangazwa katika vituo mbali mbali vya kupigia kura. MUNGU IBARIKI TANZANIA
Reactions::

Ajuza Mwenye Umri Wa Miaka 120 Apiga Kura Iringa





Bibi Kizee anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 120, Adelphina kayombo akisubiri kusaidiwa kupiga kura katika kituo cha Kihesa chekechea mjini Iringa leo

Bibi Adelphina Kayombo akisaidiwa na mtoto wake wa mwisho Ade mgohamwende (kushoto) mwingine ni mjukuu wake Esta Mahagama.
(Picha: Mdau Francis)
Reactions::

Waziri Mkuu Pinda, Mama Pinda Wapiga Kura




1.Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga kura kwenye kituo cha uchaguzi kijijini kwake, Kibaoni Katavi mapema leo.

2.Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akipiga kura kwenye kituo cha Uchaguzi kijijini Kibaoni Katavi mapema leo. (Picha:Ofisi ya WAziri Mkuu).
Reactions::

Mzee Elvis A. Musiba Hatunaye



ALIYEKUWA MWENYEKITI WA TCCIA TANZANANIA A MZEE ELVIS MUSIBA AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO . HABARI ZA MIPANGO YA MAZISHI ZITATOLEWA MARA TU BAADA YA KUPATIKANA. KWA WALE WALIOKO LONDON BASI MNAKARIBISHWA KWA BINTI YAKE ANAYEITWA LISA MUSIBA
ADDRESS
6 MANTON RD
ENFIELD MIDDLE SEX
LONDON
EN3 6XZ
07949737185
Reactions::
Reactions::

Yaliyojiri Wakati Wa Kampeni.



Hii imekaaje?
Reactions::

Dr Bilal Piga Kura Kiembe Samaki Zanzibar




1.Mgombe mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitumbukiza karatasi ya kupigia kura Kiembe Samaki mjini Zanzibar mapema leo asubuhi

2.Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika chumba cha kupigia kura katika kituo cha Kiembe Samaki mjini Zanzibar leo.( Picha:Muhidin Sufiani)
Reactions::

Dr Salim Apiga Kura



Dr Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipiga kura leo jijini Dar es salaam. Dkt Salim aliwasili katika Eneo la Soko la Samaki Msasani saa 12.50 Asubuhi na kufanikiwa kupiga kura katika Kituo B 3 cha Soko la Samaki Msasani saa 1.30 Asubuhi. (Picha:Vicent Tiganya)
Reactions::

JK, Mama Salma Wapiga Kura




Mgombea wa urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akipiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Msoga, kata ya Msoga,Chalinze leo asubuhi.

Picha ya chini ni mke wake Mama Salma Kikwete.
Reactions::

Kumekucha! Foleni Ya Kupiga Kura, Iringa Mjini



Pichani ni leo asubuhi. Kituo cha kupigia kura kilicho kwenye kituo cga zimamoto, Iringa Mjini. ( Ahsante ya picha: Francis Godwin)
Reactions::

Mgombea Urais Juani, Mlinzi Kivulini!



Kuga Mziray, mgombea urais kwa tiketi ya PPT- MAENDELEO. Nilimkuta hivi karibuni pale Makambako mjini akimwaga sera huku mlinzi wake akifuatilia kila hatua yake. Na dereva wake kajipumzisha ndani ya gari kama anavyoonekana.
Reactions::

CUF Wafunga Kampeni Zao Kwa Kishindo




Morogoro na Dar, jana.
Reactions::

Mjengwablog Inawatakia Uchaguzi Mwema



Wenye Amani Na Utulivu. Mungu Ibariki Tanzania. Pichani , Mwalimu Julius Nyerere akiwa kwenye foleni ya kupiga kura enzi hizo.( Picha ya Maktaba)
Reactions::

Kule Jamii Forums Maneno Hayeshi!



Ndugu Zangu,

Kule Jamii Forums maneno hayeshi. Jana niliingiza makala yangu. ( Balozi Joy Mukanyanga; alichokiona, Watanzania hatukukiona). Basi, ikaanzia hapo. Mjadala ulienda vema, lakini wako wengine kama huyu;

Quote Originally Posted by chanai View Post
Hii makala ni ya kuwasifia mafisadi. Hakuna lolote la maana

Chanai,

Jibu hili ni kwako na wengine pia.

Nafahamu, kuwa kuna baadhi humu hawanifahamu, lakini wanajaribu kuandika kama vile wananifahamu. Ni tatizo lao.
Nimeandika ... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Mdau Norway: " Pongezi Mjengwablog!"



Mjengwa nianze kwa kukushukuru kwanza kwa kuwa makini na kwa kuwa mtu wa watu!!! Nimekuwa nafuatilia kampeini za uchaguzi nchini mwetu toka zimeanza kupitia blog za nchini mwetu ikiwemo ya kwako!! Wewe ni jasiri na unaweza kazi ya kuhabarisha jamii!! Umeweza kutangaza habari za vyama vyote bila woga wala ubaguzi!! Nasema ufanikiwe zaidi na Mungu akusaidie katika harakati zako za kila siku!!! Kesho watanzania wanafanya maamuzi makubwa saana ya mustakabari wa maisha yetu na watu wetu!! Wasisite kufanya kile ambacho ni bora kwao !! wanaweza kufanya maamuzi yatakayopunguza na hata kumaliza shida walizonazo watanzania kwa kipi kirefu!!! Tumezipokea salamu za Dr . Slaa na ujumbe umefika kwa wote!!! Mjengwa nakutakia kila la kheri na uzidi kuwa hivi katika nyanja zote!! Kosoa panapohitajika na sifia panapohitajika pia kama ambavyo umekuwa unafanya!! Uchaguzi mwema Tanzanaia na fanyeni maamuzi ya mabadiliko kwa maisha ya watanzania wote!!

Mjengwa blog yako imekuwa ikituhabarisha vizuri hapa ughaibuni na kupata taarifa za pande zote!!! Sasa tunaweza kufahamu Tanzania ina sura gani na watanzania wanafikiria nini!!

Tanzania yenye utajiri mkubwa na watu makini Maendeleo yanawezekana!!!

UCHAGUZI MWEMA NA WENYE AMANI!!!

MUNGU ASAIDIE HAKI ITENDEKE!!

Morato; Norway!!

JIBU:

Morato,

Ahsante sana. Inatia moyo. Tutaendelea kufanya kazi iliyo njema. Kwenye mapungufu, wewe na wengine msisite kutukosoa.
Maggid
( Picha hiyo nimeipiga jana mchana hapa Iringa. Mwanamke na ndizi zake kichwani, mchana wa jua kali sana. Ndizi tatu shilingi mia mbili.)
Reactions::

Ramani Ya Kura Hii Hapa!



Chanzo: The Citizen
Reactions::

CHADEMA Wahitimisha Kampeni Kwa Kishindo





Mbeya Mjini, jana Jumamosi. ( Ahsante ya picha: Francis Godwin)
Reactions::

Iringa Mjini Kama Florida!





Kumekuwa na hamasa kubwa ya kisiasa hapa Iringa. Hamasa ambayo sijapata kuishuhudia tangu nifike Iringa mwaka 2004. Mwaka huu ushindani wa kisiasa ni mkali sana jimbo la Iringa Mjini. Kuna Mama Monica Mbega (CCM), Mch. Peter Msigwa ( CHADEMA) na Mama Mariam Mwakingwe ( NCCR).

Hata hivyo, mchuano mkali ni kati ya CCM na CHADEMA. Kura za Mama Mwakingwe zinaweza pia kuamua mshindi. Ukiongea na watu wa CCM wanasema ushindi ni wao. Ukiongea na watu wa CHADEMA, nao vile vile, wanadai safari hii wanaibuka kidedea. Lakini, nimetembelea vijiwe mbalimbali hapa Iringa. Ukiwauliza watu wa vijiweni, wao wanasema; mwaka huu ngoma nzito!

Naam. Na leo ndio siku yenyewe ya kupiga kura. Muda mfupi ujao nitaelekea kwenye kata yangu ya uchaguzi. Kata ya Nyalumbu, Ilula, Kilolo. Nawatakia nyote, uchaguzi mwema uliojaa amani na utulivu. ( Ahsante ya picha: Francis Godwin)
Reactions::

CCM Wamaliza Kwa Kishindo Jangwani





Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010
Reactions::

SHUKRANI KUTOKA FAMILIA YA MAREHEMU MCHUNGAJI NYITAMBE



Familia ya Marehemu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe tuishio Uingereza na Tanzania, kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Jumuiya ya watanzania Reading na Slough ,Kanisa La wasabato (Angaza SDA Church -Reading), Madhehebu yote ya kidini hapa UK ,vyama vyote vya kisiasa,Waganga wote kutoka Mkoa wa Mara ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na pia bila kusahau blog zote zilizo shiriki kutoa taarifa(Hakingowi,Issa Michuzi,Majid Mjengwa ,TZUK,Watanzaniaoslo,Musoma -tanzania ,wavuti n.k) , kwa kufanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu baba yetu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe ambaye alifariki Kutokana na ajali ya gari tarehe 3/October /2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 9 /October/2010 kijijini kwake Kirongwe Tarime MkoaniMara.

Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani,ndugu,jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali ambayo imewezesha familia ya marehemu walioko Uingereza kuweza kuwahi mazishi .


Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee, tunasema tu kwamba Asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilisaidia katika mipango na mikakati yote ya kuuhifadhi mwili wa Marehemu hadi kuzika.

Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia mibaraka katika shughuli zenu za kila siku.Tumeambatanisha picha za ajali .

Sisi tulimpenda sana Marehemu Nyitambe lakini

Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,

Jina la Bwana lihimidiwe.

Asanteni sana





Amen



Blog:www.musoma-tanzania.blogspot.com
Reactions::

Saturday, October 30, 2010

Reactions::

CCM Yamaliza Kampeni Jangwani





1. Mgombea urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dr Jakaya Kikwete akisalimiana na mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni hii.

2.Dr Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

3.Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika katika viwanja Jangwani kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM iliyofanyika jioni hii.
Reactions::

Dr Slaa Atuma Salamu



Ndugu wana JamiiForums, Mtandao wa IssaMichuzi, wana FaceBook na mitandao mingine na Watanzania wenzangu wote kwa ujumla mtakaosoma ujumbe huu, Salaam toka Mbeya Vijijini, ndio tumeanza mikutano midogo ya kufunga kazi asubuhi hii na tutahitimisha baadaye.

Ninashukuru sana kwa maneno ya heri kwa siku yangu ya kuzaliwa hapo jana na ningekuwa sina shukrani kama ningeacha ipite bila kusema asante kwa maneno mema mliyonipatia humu na kwenye facebook na hata waliopata nafasi kwa njia ya simu. Ninawashukuru vile vile kwa mashauri mbalimbali, na pia kwa sala na dua zenu.

Ninashukuru sana na ninaona fahari kuwa ni mwanachama mwenzenu.

Kampeni zote zinaisha leo na kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu kama mnavyofahamu. Kwa upande wangu nimetembelea karibu maeneo yote ya nchi yetu kubwa, nimekutana na watu mbalimbali na nimeona mengi. Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimena mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

Ninaelewa vizuri zaidi sasa kupitia mang’amuzi binafsi hali ya Taifa letu ilivyo na ya kwamba ni lazima tubadili mwendo na huko tunakokwenda maana tutafika mahali ambapo tutashindwa hata kujiuliza tulifikaje. Watu makini hawawezi kuendelea na njia ambayo wanajua wamepotea. Kuendelea kung’ang’ania kwenda wakati mnajua mmeshapotea ni kutukuza kiburi cha kujiona. Taifa letu limepotea njia na hata kama tukijitahidi kwa nyimbo na masimulizi mbalimbali kuhalalisha huko tunakokwenda bado tutakuwa tumepotea.

Ni kwa sababu hiyo nilipoombwa kugombea Urais nilitambua uzito wa mzigo huu mkubwa kwani utahusiana moja kwa moja na kubadilisha mwelekeo wa taifa letu na kuanza kutengeneza pale palihorabiwa, kuinua kilichoanguka na kumwagilia kilichoanza kunyauka. Hili linahitaji mawazo mapya, uthubutu wa kiuongozi na mtazamo mpya wa nini Taifa letu linahitaji. Ndugu zangu, Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ili tuweze kujipa sisi wenyewe na watoto wetu nafasi ya kuweza kufanikiwa huko mbeleni.

Mabadiliko haya siyo mabadiliko ya mapambo yaani kuhamimisha maua na vitambaa sebuleni wakati nyumba inanuka na nichafu. Wote mliosikiliza au kumwangalia mgombea mwenzangu jana ni wazi hana ahadi ya mabadiliko yoyote makubwa isipokuwa mwendelezo wa yale yale yaliyotufikisha hapa. Ni kutokana na hilo natambua kuwa kura ya kesho siyo kura ya kawaida; siyo kura kama ya 2005 au ya miaka kabla yake.

Kura ya kesho ni kura ya kuchagua kuendelea na vile tulivyo kwa miaka mitano ijayo au kubadilika ili tuanze upya kwa njia sahihi na kwenda ambako sote tunakujua tunataka kwenda. Ninaamini tunachohitaji ni mabadiliko yatakayoanzisha mwamko wa kuanza kulijenga upya taifa letu. Hili ndilo lililonifanya nikubali pale Chama changu kiliponiomba ninyanyue bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huu katika nafasi ya Urais.

Naweza kuwaahidi mengi na kwa maneno matamu ya kila aina. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

Tutawapa nafasi Watanzania hatimaye nao wafurahia matunda ya uhuru wao na vile vile kuweza kuanza kujenga Taifa la kisasa ambalo litakuwa ni tamanio nakinara cha mabadiliko ya kiutawala, kiuchumi na kiutendaji katika Bara letu. Tuna uwezo, tuna sababu na tuko tayari kuwatumikia.

Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Usiuze, usiache kuitumia na pale utakapoitumia itumie kwangu, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wetu wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote tuliyowaahidi tutayatimiza na zaidi.

Msiwe na shaka, hata toka Ikulu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa mitandao hii na kuwapa taarifa mbalimbali moja kwa moja na kujibu maswali mtakayokuwa nayo kuhusu serikali yenu pale inaponipasa mimi kutolea kauli. Asanteni!!

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika
Reactions::

' Super Coach' Mziray Hatunaye Tena



Syllesaid Mziray ( Pichani) amefariki dunia leo alfajiri. Mziray, mpaka kifo chake alikuwa Kocha Msaidizi wa Simba SC. Habari za kifo chake zimepokelewa kwa mshtuko mkubwa na wadau wengi wa soka. Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa kandanda ya Tanzania, ndani na nje ya uwanja.
Reactions::

Mama Kikwete Na Mama Lowassa



Mama Salma Kikwete amehitimishia Arusha ziara za kampeni kwa Chama cha Mapinduzi. Mama Salma amezunguka kila kona ya nchi kusaka kura kwa CCM. ( Picha: Mwanakombo Jumaa, MAELEZO)
Reactions::

" Jamani Tumnyanyue Mwanamke Mwenzetu!"



Mama Salma Kikwete akimnadi Batilda Burian Arusha. ( Picha: Mwanakombo Jumaa, MAELEZO)
Reactions::

CCM Arusha Magharibi



Picha: Mwanakombo Jumaa, Maelezo.
Reactions::

Balozi Joy Mukanyange: Alichokiona Watanzania Hatukukiona



( Makala haya yamechapwa kwenye jarida la Raia Mwema juma hili. Pichani ni Balozi Joy Mukanyange, alikuwa balozi wa Rwanda nchini Tanzania kati ya mwaka 1996-1999. Picha ya Maktaba)


Na Maggid Mjengwa,

UZOEFU ni mwalimu mzuri. Unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.
Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.
Tumefundishwa, kuwa tusicheze na moto. Watanzania tunakwenda kupiga kura Jumapili Oktoba 31, 2010. Tunachokwenda kuamua ni mustakabali wa nchi yetu, taifa letu.
Tunapokwenda kwenye uchaguzi tuyakumbuke maneno ya busara sana kutoka kwa Bi. Joy Mukanyange. Huyu alikuwa Balozi wa zamani wa Rwanda nchini Tanzania.
Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange alituambia Watanzania .... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Wanafunzi California Wajifunza Kuhusu Tanzania




Pichani ni Afisa Ubalozi Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bibi Joyce Kafanabo (mwenye suti nyekudu), akiwa na baadhi ya wanafunzi kutoka shule kadhaa za sekondari za Jimbo la Califonia, Marekani. Wanafunzi hao wakiwa na walimu wao ambao hawapo pichani, waliutembelea Ubalozi wa Tanzania wakiwa katika ziara ya mafunzo ya kujifunza historia ya Tanzania, mila, desturi na tamaduni za Watanzania. Walitaka kujua pia mfumo wa siasa za Tanzania, Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii na pia mfumo wetu wa elimu. Maelezo hayo kwa wanafunzi hao yalitolewa na Bibi Kafanabo kwa niaba ya Mhe. Balozi Ombeni Sefue. Baada ya maelezo ya kina pamoja na maswali na majibu, wanafunzi hao wamevutiwa na kuonyesha hamu kubwa na wamelezea nia yao ya kwenda Tanzania mwakani (2011). ( Picha na Maelezo na Mwandishi Maalum, New York)
Reactions::