Tangu asubuhi mpaka jioni hii. Nilibanwa sana na majukumu kiasi cha kuchelewa kuingiza comments zenu. Ni nyingi, zinaelimisha, zisome.
poleni kwa usumbufu.
Maggid
Tuesday, November 30, 2010
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akutana na wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini
african night in michigan saturday december 11, 2010

Come and enjoy the Night with Full of Flavors.
Old School, New Joint, Bongo Flavor, Rumba and other African Hits.
DJ. MENDRAD and other Michiana DJs will drop the hits, come and have funny.
Venue: Honeys Night Club/Cowboy Saloon
405 N. 2nd St
Niles, MI 49120
Date: December 11, 2010(Sat)
Cover Charge: $ 5:00
Time: 10:00 till LATE
NB: Age, must be over 21 to enter.
| Reactions:: |
Polisi Yaruhusu Mikutano Ya Chadema

SIKU moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kulilalamikia Jeshi la Polisi juu ya kutoa amri ya kuzuia mikutano yake ya hadhara na ile ya kuwapokea wabunge wa
chama hicho maeneo mbalimbali nchini, jeshi hilo limeondoa rasmi zuio hilo.
Jeshi hilo limesema kuwa limeondoa rasmi zuio hilo kuanzia jana baada ya 'uchaguzi kumalizika rasmi juzi' kwa mujibu wa taratibu za ndani za usimamizi wa shughuli ya uchaguzi, ambazo walikuwa wamejiwekea, ambazo hazikuwa zikimlenga mtu wala chama chochote cha siasa.
Jana CHADEMA kilikaririwa na vyombo vya habari kikisema kuwa vitendo hivyo vya polisi vilikuwa vinashiria hatari kwa demokrasia nchini, kuvunja haki za kikatiba na za kisheria za wananchi, huku vikiwa ni dalili ya nchi kupelekwa katika 'dola ya kipolisi,' kama vile ilivyokuwa katika nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini wakati wa utawala wa makaburu na Kenya wakati wa utawala wa Rais wa Pili, Daniel Arap Moi.
Vyombo vya habari vilimnukuu Mkurugenzi wa Haki, Sheria na Katiba wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu akisema kuwa chama hicho hakitakuwa tayari kunyamazia hatua hiyo, kwani ingeweza kuwa mwendelezo wa kuminya haki ya watu kujumuika na kujadili mustakabli wa nchi yao, kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Akizungumza na Majira jana kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Kamishna wa Polisi Clodwig Mtweve alisema kuwa uzuiaji huo wa maandamano na mikusanyiko ya kuwapokea wabunge na mikutano mingine ya kawaida ya hadhara, ilikuwa sehemu ya utaratibu wa jeshi hilo wakati na baada ya uchaguzi.
Bw. Mtweve alisema kuwa uzuiaji huo haukumlenga mtu yeyote wala chama chochote kile cha siasa, bali ulikuwa ukizingatia hali halisi ya nchi baada ya uchaguzi, ambapo "serikali ilikuwa haijaundwa wala mawaziri hawajateuliwa," hivyo wameondoa rasmi amri hiyo jana.
"Kusema ukweli nimeshaongea na vyombo vya habari vingi leo juu ya suala hilo na nimeshatoa ufafanuzi. Tulichokuwa tumezuia ni maandamano na kupongezana si mikutano...unajua baada ya bunge kumalizika kulitolewa maombi mbalimbali ya maandamano watu wakitaka kuwapokea wabunge wao.
"Lakini unajua maandamano ni kitu kingine na mikutano ni kitu kingine, kila kimoja kina utaratibu wake, mapema ilikuwa imetolewa amri ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi kusimamia mambo yote hayo ya maandamano na mikutano...lakini amri hiyo sasa imeondolewa rasmi leo (jana) baada ya uchaguzi kuisha rasmi jana (juzi)," alisema Bw. Mtweve na kuongeza;
"Kwa mujibu wa utaratibu tuliokuwa tumejiwekea ndani ya jeshi, uchaguzi umemalizika jana (jana)...ma-OCD walipewa maelekezo ya kutoruhusu masuala ya maandamano kwani yale hayaangalii tu kitendo chako cha mwisho, bali yanahusisha taasisi nyingi na masuala ya usalama wa mali za watu, suala hilo halikumlenga mtu wala chama cha siasa...
"Hata hivyo, tulijaribu kuhoji kama ni suala la kupongezana kwani ni lazima watu wapongezane kwa kukusanyika uwanjani, wangeweza kufanya hata hotelini au ukumbini mahali," alisema.
Bw. Mtweve aliongeza kusema kuwa haikuwa vizuri baada ya uchaguzi kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara kwani nchi ilikuwa imetoka katika uchaguzi, huku 'mambo yakiwa hayajakaa sawa', serikali ikiwa haijaundwa na mawaziri hawajateuliwa.
Majira lilipotaka kujua kama jeshi hilo lilikuwa na wasiwasi zaidi na maandamano na mapokezi ya wabunge kwa nini lilizuia hata mikutano ya hadhara kama vile huko Segerea, Dar es Salaam, Bw. Mtweve alisema kuwa hiyo ilikuwa ni kwa mujibu wa "operetion order" (amri ya utendaji).
Alisisitiza kuwa kuanzia jana utaratibu wa kuomba na kukubaliwa mikutano ya hadhara na maandamano unarudi kama kawaida chini ya makamanda wa polisi wa wilaya.
Wakati huo huo, CHADEMA kimepongeza hatua ya kuondoa amri hiyo na kusema kuwa ni jambo zuri lakini halizuii kusudio lake la kufikisha hoja yake bungeni juu ya uvunjifu wa Sheria ya Haki, Mamlaka na Kinga ya Bunge ya mwaka 1988, kikisema kuwa polisi hawana ruhusa ya kuzuia mikutano ya wabunge "pale serikali inapokuwa haipo."
Akipongeza hatua hiyo, Mkurugenzi wa Haki, Sheria na Katiba wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu alisema "Kama wameiondoa basi ni jambo zuri sana...ni kitendo kizuri lakini hakituzuii kwenda kuhoji bungeni kwa nini wabunge wetu walizuia kufanya kazi...kufanya mikutano.
"Hakuna sheria yoyote inayowaruhusu polisi kuvunja au kukiuka sheria ya haki, mamlaka na kinga ya bunge ikiwa serikali haipo au mawaziri hawajateuliwa," alisema Bw. Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni.(Gazeti Majira)
| Reactions:: |
Kandoro Ayapa Somo Makampuni Binafsi Ya Ulinzi
1. Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro.
2. Baadhi ya washiriki katika semina ya PPF na waajiri iliyofanyika katika Hotel ya Lakairo jijini Mwanza
MKUU wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ameyashukia baaadhi ya makampuni binafsi ya ulinzi mkoani Mwanza kutokana na tabia yao ya kutowasilisha michango ya waajili wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kuitaka mifuko hiyo kuyachukulia hatua kali ili iwe fundisho kwao.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza amesema kuwa kwa siku amekuwa akipokea wastani wa malalamiko 10 toka kwa walinzi wa makampuni binafsi wakilalamikia kufukuzwa kazi na waajili wao kushindwa kuwalipa mafao yao ambayo walikatwa kwa mujibu wa sheria .
| Reactions:: |
Gurumu Atoka ICU
Mwanamuziki wa siku nyingi Mzee Makasy akimjulia hali mwanamuziki mwenzie Maalimu Muhindini Gurumo (KAMANDA) aliyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili,Uncle Gurumo yupo wodi ya Mwaisera namba 1 kwa sasa baada ya kutoka katika chumba cha wagojwa wenye uangalizi maalumu (ICU). Kunradhi kwa picha haionekani vizuri.Picha na mdau Rajab Mhamila.
Globu ya Jamii inamtakia Kamanda Gurumo nafuu ya haraka na inatoa wito kwa wapenzi wa muziki kujitokeza kumsaidia mzee wetu huyu ambaye ni mmoja wa wanamuziki wachache waliosalia wakiendeleza fani kwa weledi wa hali ya juu huku ukikuza vipaji vipya kwa wakati huo huo.
Mwanamuziki wa siku nyingi Mzee Makasy akimjulia hali mwanamuziki mwenzie Maalimu Muhindini Gurumo (KAMANDA) aliyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili,Uncle Gurumo yupo wodi ya Mwaisera namba 1 kwa sasa baada ya kutoka katika chumba cha wagojwa wenye uangalizi maalumu (ICU). Kunradhi kwa picha haionekani vizuri.Picha na mdau Rajab Mhamila.
Globu ya Jamii inamtakia Kamanda Gurumo nafuu ya haraka na inatoa wito kwa wapenzi wa muziki kujitokeza kumsaidia mzee wetu huyu ambaye ni mmoja wa wanamuziki wachache waliosalia wakiendeleza fani kwa weledi wa hali ya juu huku ukikuza vipaji vipya kwa wakati huo huo.
| Reactions:: |
' Udhalilishaji Wa Kimpira!'
Blogu Ya Mkandawile
Kwanza naomba nianze kwa kukupa pole sana na majukumu ya kila siku hasa katika kuendeleza ulimwengu wa habari,pili naomba sana unisaidie kunitangazie kablog kangu,bado ni kapya hivyo mchango wa mawazo na pia ushauri ni mhimu sana kutoka kwa wadau lakini pia kwenu nyie mlio wazoefu katika maswala ya blogs.Natanguliza shukrani zangu kwako.http://raymondmkandawile.blogspot.com
| Reactions:: |
Poleni Kwa Usumbufu: Simulizi Ya Mwamwindi Natembea Nayo Mfukoni!

... Kuchezwa kwa mechi kubwa, 'El Classico' kati ya Barcelona na Real Madrid jana usiku, basi, nikalazimika kuifuatilia mpaka saa saba za usiku. Na usiku wa manane ukaingia. Simulizi ya Mwamwindi inahitaji kutulia. Alfajiri hii kuna kilichojitokeza kikazi. Nikitulia alfajiri ya kesho nitaendelea nacho. Msitie shaka, simulizi natembea nayo mfukoni! Poleni kwa usumbufu. ( Pichani ni eneo la Isimani, yalikokuwa mashamba ya akina Said Mwamwindi na wenzake)
| Reactions:: |
Monday, November 29, 2010
Michuzi Awapa Somo Wasanii
Michuzi akiwaonyesha wadau wa Jukwaa la Sanaa jinsi ya kuweka video kwenye U-Tube
Ankal Michuzi (Issa Michuzi) ambaye ni mmoja wa waasisi wa mitandao ya habari ya jamii (blogs) hapa nchini amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani.
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa leo Jumatatu,Michuzi ambaye blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com imepata umaarufu mkubwa kutokana na kutembelewa na watu wengi aliweka wazi kwamba,blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.
Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.
Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.
Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.
Katika kuonesha kwamba, teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa. (janejohnblog)
| Reactions:: |
Waziri Mkuu Wa Kenya Alaani Mashoga

Waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga amesema nchi hiyo haipo tayari kuwatambua wapenzi wa jinsia moja.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la bunge mjini Nairobi, Bw Odinga alisema suala la wapenzi wa jinsia moja lilitumiwa kama propaganda kupinga katiba mpya.
Waziri Mkuu huyo amesisitiza katiba mpya ya Kenya haikubali kuwepo wapenzi wa jinsia moja. Na amependekeza wapenzi hao wa jinsia moja wakamatwe na polisi endapo watajitokeza hadharani.
Lakini kauli hiyo imepingwa na David Kuria, mwanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja.
Bw Kuria ameiambia BBC kuwa kauli hiyo itaathiri kampeni zao za kutetea haki sawa za huduma ya afya kwa watu hao, hasa kuhusu suala la kudhibiti maambukizi ya Ukimwi.(BBC swahili)
| Reactions:: |
Spika makinda ziarani namibia
Mhe. Anne Makinda (Mb)Spika wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC-PF (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Essau Chiviya , wakati wa kikao cha Kamati Tendaji mjini Swakompmund, Namibia tarehe 29/12/2010 baada ya kupitia agenda na maandalizi ya Mkutano wa 28 wa SADC-PF utakaofunguliwa na Rais wa Namibia Mhe, Hifikepunye Pohamba.
| Reactions:: |
Nyaraka Hizi Hapa ... Karibu Uendelee...
........Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. John Chiligati (kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali za kutendea kazi Waziri mwenye dhamana hiyo Mh. Prof. Anna Tibaijuka. Makabidhiano hayo yalifanyika mara baada ya Mh. Tibaijuka kuingia ofisini jana tangu aapishwe. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara Mh. Patrick Rutabanzibwa.
| Reactions:: |
JK Akutana Na Baraza Lake
Wasomi Wameisaliti Nchi: Askofu Cheyo
ASKOFU Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania mhashamu Alinikisa Cheyo amesema kuwa kuwa chanzo cha ufisadi na uhujumu mkubwa nchini ni wasomi walioamua kuisaliti nchi baada yakusomeshwa kwa kodi za watanzania.
Askofu Cheyo aliyaseama hayo wakati wa mhafali ya tatu Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji kinachomilikiwa na kanisa hilo jijini Mbeya, Katika hatua nyingine Askofu Cheyo aliwaasa wahitimu wa shahada na stashahada katika chuo hicho kutofuata mkumbo wa wasomi wengi ambao alidai wamewaibia Watanzania kwa kuwasaliti.
Askofu Cheyo alisema kuwa wasomi ndio wenye nafasi ya kuzuia mianya ya rushwa kwa kutoa elimu waliyojifunza sanjali na kupiga vita vitendo vya kifisadi, ambavyo alisema vimeifikisha nchi mahali pa kuweka matabaka ya walio nacho na wasio nacho.(Gazeti Majira)
| Reactions:: |
Polisi Yapiga 'Stop' Mikutano ya Chadema Nchi Nchini.


Jeshi la polisi limezuia mikutano ya Chadema iliyopangwa kufanyika nchi nzima.Akizungumza na wanahabari juzi katika ofisi za Makao makuu ya chama Kinondoni jijin Dar es Salaa, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu (MB) alilalamikia hatua ya polisi kupiga marufuku mikutano yao nchi nzima.
| Reactions:: |
Je, Kwanini Mwamwindi Alimpiga Risasi Kleruu? Nimefanya Mahojiano Na Mtoto Wa Mwamwindi (2)

Kleruu akamwuliza Mzee kwa ukali, ” Mbona mnafanya kazi leo siku ya Krismasi?”. Baba akamwomba Kleruu waende wakuzungumze nyumbani. Akamwambia mdogo wangu Mohammed aendelee kulima. Mzee akatangulia mbele, nyuma anamfuatia Kleruu. Kabla ya kufika kwenye nyumba yake wakayapita makaburi. Kleruu akamtamkia baba mzee Mwamwindi; ” Hapa ndipo unapozika mirija yako?” Alitamka hivyo huku akimtomasa tomasa mzee na kifimbo alichoshika mkononi.
Jambo hilo lilizidi kumkasirisha marehemu mzee. Akafika nyumbani kwake. Mlangoni alisimama mke wake mdogo. Inaonekana mzee alishafanya uamuzi. Jana yake alikwenda kuwinda. Hakupata mnyama. Bunduki yake moja aia ya riffle kati ya bunduki zake mbili ilikuwa bado ina risasi. Akamwambia mke wake mdogo huku Kleruu akiwa anasikia;
” Kanichukulie bunduki yangu”…… Endelea…
“ Je, aliposikia hayo Dr Kleruu alifanyaje?”
” Nadhani alipigwa na butwaa. Hakuamini kama baba angefikia hatua hiyo”
”Na ilikuwaje basi Mwamwindi alipoletewa bunduki?”
” Ilienda haraka, Mzee Mwamwindi akainua bunduki yake. Tayari ilikuwa loaded na risasa tangu jana yake alipotoka kuwinda. Kleruu aliinua mikono yote miwili kama mtu anayesalimu amri. Mwamwindi akampiga risasi ya kwapani. Kleruu akabaki hai. Akapiga risasi nyingine. Ikamwua pale pale.” Anasimulia Mzee Amani Mwamwindi.
Kinafuatia kimya. Anainama, namwona usoni, kuwa huzuni imemjia. Bila shaka, ni kitendo kile cha baba yake kumpiga risasi na kumwua Dr Kleruu ndicho kilichoashiria mwanzo wa ukurasa mgumu katika familia ya Mwamwindi , Isimani na pengine Iringa kwa ujumla.
Nafikiria kumwuliza swali lifuatalo; Risasi ya pili ya Mzee Mwamwindi ilimpiga Dr Kleruu katika sehemu gani ya mwili? Nasitisha swali hilo. Litasubiri mara nyingine. Mzee Amani Mwamwindi anaendelea kunisimulia;
” Mdogo wangu Mohammed akiwa shambani alisikia mlio wa bunduki. Alidhani kuwa baba amepigwa risasi. Alikimbia kurudi nyumbani. Na pale ilipowekwa kumbukumbu ya Kleruu nyuma yake ndio ilipokuwa nyumba ya mzee. Hivyo, pale ulipowekwa mnara ni mbele ya nyumba. Kwa sasa nyumba hiyo haipo.
Alipofika nyumbani, Mohammed akamkuta baba amesimama, na Kleruu amelala chini, amekufa. Mzee alichukua kofia ya pama ya Kleruu, akaivaa. Akaingiza mkono mifukoni mwa Kleruu, akachukua funguo za gari la Kleruu. Mzee alimwambia mdogo wangu amsaidie kumwinua Dr Kleruu. Mzee alimshika miguuni na mdogo wangu Mohammed alimshika kwenye mikono. Wakamwingiza kwenye buti la gari.
Baba akaendesha mwenyewe gari lile la Mkuu wa Mkoa Kleruu, Peogeot Injection, rangi ya bluu likiwa linapepea bendera ya taifa. Aliendesha kuelekea mjini Iringa. Njiani kuna walioshangaa kumwona Mwamwindi akiendesha gari la Mkuu wa Mkoa huku akiwa kichwani amevalia pama la Kleruu.
Mzee alipoingia mjini Iringa breki ya kwanza ilikuwa hapa tulipo, nyumbani kwangu Mlandege. Kama nilivyosema, wakati huo nilikuwa kijana wa miaka 21. Nilishakuwa na mji wangu, nilijenga kibanda changu hapa tulipo. Nilifanya kazi kama karani wa Ushirika. Siku ile ya tukio nami nilikwenda kwenye shamba langu Ifunda.
Basi, Mzee alipofika hapa nyumbani akaambiwa kuwa nimekwenda shamba Ifunda. Alisikitika sana.” Anasema Mzee Mwamwindi huku naye bado akionyesha huzuni machoni. Miaka 40 baada ya tukio.
Alipotoka hapa alipita nyumbani kwake pale Mshindo, na baadae akasimama kwa binamu yake. Ile nyumba ya njano nyuma ya benki ya CRDB, si unaijua?” Ananiuliza.
” Ndiyo” Namjibu.
” Pale alikuwa anakaa binamu yake na baba. Basi, alipofika pale akakutana n abinamu yake. Binamu yake yule alishangaa kumwona mzee akiwa na damu kwenye nguo zake. Akashangaa pia kumwona akiwa na gari la Kleruu lenye bendera ya taifa ikipepea. Akamwuliza nini kimetokea? Mzee hakuweza kuongea akaeleweka. Alitamka; ” Nimeenda kwa Amani ( Mimi) nimeambiwa kaenda shambani kwake Ifunda”. Alionekana kuchanganyikiwa.
Akaingia kwenye gari. Akaendesha moja kwa moja hadi Kituo cha polisi. Akamkuta polisi kijana. Akashuka, akamwambia; ” Njoo chukua mzigo wako”. Akaweka chini pia kofia ya pama ya Kleruu.
Polisi alipofungua buti ya gari akashangaa kuona mzigo wenyewe ni mwili wa Mkuu wa Mkoa, Dr Kleruu. Mzee akawa amejisalimisha.
Niliporudi nyumbani kutoka Ifunda nikazikuta habari hizo mbaya. Nikaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Mzee pale Mshindo. Nikawakuta akina mama wanalia. Ilikuwa ni kilio. Hiyo bado ilikuwa ni Jumamosi, siku ya Krismasi. Nikauliza; kuna aliyekwenda kumwona baba pale polisi? Jibu likawa hapana. Nikaenda moja kwa moja polisi ili nikamwone baba na nimsikie kauli yake.
Nilipofika polisi nikaanza kujieleza kwa askari polisi kuomba ruhusa ya kuongea na Mzee. Wakati nikifanya hivyo mzee nae alisikia sauti yangu. Akatamka; ” Mwanangu huyo, mruhusu niongee nae”. Nikaongea na Mzee.
( Jamani nayaandika haya alfajiri sana. Ningependa niendelee, lakini nisitishe hapa kwa asubuhi hii. Nitaendelea kusimulia usiku wa leo au kesho alfajiri, maana Jumatatu imeingia hapa Iringa. Ngoja nikawachemshie uji wana wangu kabla hawajaenda shule!)
| Reactions:: |
Mzozo Umekwisha Zimbabwe - Zuma



Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema amesaidia kumaliza mvutano kati ya viongozi mahasimu wa Zimbabwe, baada ya kufanya ziara mjini Harare siku ya Ijumaa.
Bw Zuma amesema mzozo kati ya Rais Robert Mugabe na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai umemalizika, baada ya saa nne za majadiliano.
Lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaonya kuwa mazungumzo haya huenda yasilete matokeo ya mara moja.
Mzozo kati ya viongozi hao ni dalili ya kudorora zaidi kwa uhusiano kati ya mahasimu hao wa muda mrefu.
"Wamekubaliana kuwa kulikuwa na matatizo ya mawasiliano kati yao, na tumetatua hilo, kwa hiyo wameamua kuendelea kukutana," amesema Rais Zuma.
Bw Zuma, Bw Mugabe na Bw Tsvangirai walionekana katika hali ya utulivu kwenye mkutano na waandishi wa habari, huku baadaye wakitabasamu na kupeana mikono.
Kiongozi huyo wa Afrika Kusini aliwasili siku moja baada ya Bw Tsvangirai kumpeleka mahakamani Bw Mugabe kuhusiana na uteuzi wa wakuu wa mikoa.
Bw Tsvangirai amesema alitakiwa ashauriwe kwanza kabla ya uteuzi kufanyika, chini ya makubaliano ya kugawana madaraka, ambayo yalimpa uwaziri mkuu. Washirika wa Bw Mugabe wametupilia mbali madai hayo.
"Kwa ma mtazamo wangu, na kwa unyenyekevu, hii iko wazi kabisa. Chochote kitakachoamuliwa na Rais ni lazima na mimi nihusishwe kama Waziri Mkuu, lazima kwanza na mimi nikubali," amesema Bw Tsvangirai katika nyaraka za mahakamani, limeripoti shirika la habari la AFP.
Mwandishi wa BBC mjini Harare Brian Hungwe, amesema viongozi wote wawili wamekuwa wakizidi kuushutumiana juu ya kutofanikiwa kwa makubaliano ya kugawana madaraka, huku kila mmoja akitaka uchaguzi wa mapema ufanyike.
Mwezi uliopita Bw Mugabe alisema mkataba wa makubaliano ya serikali ya kugawana madaraka yasiongezwe muda, wakati muda wake utakapokwisha mwezi Februari.
Makubaliano ya kuuda serikali ya kugawana madaraka yalifikiwa baada ya uchumi wa Zimbabwe kuporomoka kufuatia uchaguzi uliozua utata mwaka 2008.
Sehemu muhimu ya makubaliano hayo ilikuwa kuandika muswada wa katiba mpya.
Lakini mchakato wa kukubaliana kuhusu katiba mpya umesimamishwa kufuatia taarifa za mara kwa mara za kuwepo kwa ghasia za kisiasa.
Siku ya Alhamisi, Waziri wa Fedha Tendai Biti aliwaambia waandishi wa habari kuwa Zimbabwe ina fedha za kuandaa uchaguzi mwakani.
"Tumeandaa fedha za uchaguzi, na za kura ya maoni pia," Bw Biti aliwaambia waandishi wa habari baada ya kuwasilisha bajeti ya mwaka 2011.
(BBC Swahili)
| Reactions:: |
Watanzania Waishio Ujerumani waanzisha Umoja wao


1.Umoja wa watanzania Ujerumani ukiwa katika picha ya pamoja na Mhe Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani,Mh. Ahmada Ngemera. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja huo. Na kulia Ni Mhe Katibu wa Umoja huo.
2.Viongozi wa muda wa umoja wa watanzania Ujerumani. kushoto Mhe Katibu wa Umoja Bi Tulalumba Mloge wa pili kushoto, Mwenyekiti wa Umoja Bw Mfundo Peter Mfundo, katikati Mhe Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh. Ahmada Ngemera, Anayefuata ni Makamo M/Kiti Xavier Komba Na mwisho kulia Ni Muweka Hazina Bi Nashe Mvungi.
| Reactions:: |
Sunday, November 28, 2010
Nyumba Ya Marehemu Said Mwamwindi
Wasio Wavutaji Hufa kwa Kuvuta Sigara


Utafiti mpya uliofanywa na shirika la afya duniani WHO unaonyesha kuwa watu 600,00 wasio wavutaji sigara hufariki kila mwaka kutokana na kuvuta moshi unotokana na kukaa karibu na watu wanaovuta sigara.
Utafiti huo uliochapishwa siku ya Ijumaa ndio wa kwanza duniani kuangazia hasa madhara ya moshi wa sigara.
Shirika la WHO lilichukua takwimu kutoka karibu kila taifa duniani. Takriban asilimia 40 ya watoto na zaidi ya asilimia 30 ya watu wazima ambao hawavuti sigara huwa wanakabiliana na moshi kutoka kwa wavuta sigara.
Kulingana na utafiti huo watu 600,000 hufariki kila mwaka thuluthi yake wakiwa watoto.
Moshi unaowafikia watu ambao hawavuti sigara unaweza kusababisha maradhi ya moyo, pumu na hata saratani ya mapafu kama tu inavyofanya kwa wavuta sigara.
Tofauti hata hivyo ni kwamba wale wanaofikiwa na huo moshi hawafanyi hivyo kwa uamuzi wao wa kuhatarisha afya yao kwa kutumia tumbaku.
Hofu kubwa kulingana na waliochapisha ripoti hiyo ni athari kwa watoto hata katika mataifa ambayo yana sheria kali dhidi ya uvutaji sigara kwa sababu bado wanaathirika kutokana na watu wanaovuta nyumbani.
Ingawaje ni vigumu kuunda sheria kubana watu kuvuta sigara nyumbani, WHO inakiri kuwa kuna haja ya hatua kuchukuliwa ili kulinda watoto kutokana na madhara ya moshi wa sigara.
| Reactions:: |
Siku Ya Uhuru: Watanzania Japani Kusherehekea
Watanzania wa Japani Kusherehekea Siku ya Uhuru.
Jumuiya ya Watanzania Nchini Japani inapenda kuwakaribisha Watanzania wote
wanaoishi Japani kuhudhuria sherehe ya uhuru.
Mheshimiwa Balozi, Mama Salome Sijaona atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe
hii.
Sherehe hii itafanyika siku ya tarehe 12/12/2010 (Jumapili), kuanzia saa Nane mchana
mpaka saa saa Tatu usiku katika ukumbi wa club ya PPP uliopo karibu station ya
Sagamino (sotetsu line). Ukifika station ya Sagamino tokea SOUTH EXIT. Ni dakika
5 kutokea station. Anuani ya ukumbi ni: Ebina-shi, Higashiwagaya 5-1-15. Kwa
maelezo zaidi ya jinsi ya kufika ukumbini piga namba zifuatazo: 080-1326-9700, 080-
3242-7442.
Tungependa siku hiyo itumike kutukutanisha Watanzania na kuweza kubadirishana
mawazo na kufahamiana ili kuweza kujenga umoja na ushirikiano pia kutafakari
mustakabali wa Taifa letu tangu tupate uhuru. Pamoja na hayo, kutakuwa na uzinduzi
rasmi wa Tovuti ya Jumuiya na kutakuwa mjadala wa mada mbili tatu zitakazotolewa
na watu mbalimbali, bila kusahau muziki wa Kitanzania.
Ili kurahisisha shughuli za maandalizi na hasa makadirio ya chakula na vinywaji,
tafadhali tunaomba wale wote wanaopenda kuhudhuria tafrija hii kuthibitisha kwa
kujiandikisha wao na wale watakaofuatana nao kwa viongozi wafuatao:
1. Upendo Mwimbage: 080- 4002-9700
2. Mariam Yazawa: 090-4422- 8555
3. Gwakisa Muhoka: 080-3242-7442
4. Bagilo Jumbe: 090-1733- 7447
5. Juma Kipya: 080-3414- 4460
6. Amani Paul: 080-4200- 0684
7. Christopher Ntyangiri: 090-9377-3524
8. Asmah Kobayashi: 080-3311-8183
9. Yusuf Mzee wa MAJI: 080-2064-6573
Siku ya mwisho ya kujiandikisha ni tarehe 4/12/2010. Wasiojiandikisha na kuthibitisha
kuhudhuria hawataruhusiwa kuingia ukumbini siku ya tafrija. Pia tunawaomba wale
wote watakaohudhuria kuzingatia muda.
Tafadhali ukipata taarifa hii muhabarishe Mtanzania mwenzako.
Ahsanteni.
Uongozi,
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.
| Reactions:: |
Kwanini Mwamwindi Alimpiga Risasi Dr Kleruu? Nimefanya Mahojiano Na Mtoto Wa Mwamwindi...


Jana Jumamosi jioni nilikuwa na mazungumzo marefu na Bw. Amani Mwamwindi. Mstahiki Meya wa Iringa aliyemaliza muda wake. Huyu ni mwana wa marehemu Saidi Mwamwindi ambaye simulizi juu ya kilichotokea kule Isimani mwaka 1971 tumeifuatilia.
Bw. Amani Mwamwindi alikubali kufanya mazungumzo nami hiyo jana nyumbani kwake Mlandege hapa Iringa. Ni simulizi ya kusikitisha, kusisimua na yenye kutoa mafunzo. Inahusu pia maarifa ya uongozi na dhana nzima ya utawala bora. Naandika haya saa saba za usiku Jumapili. Ngoje nikapumzike. Baadae Jumapili ya leo nitaanza kuwasilimua niliyosimuliwa.
Kumekucha. Jumapili saa kumi na mbili asubuhi. Naanza kusimulia nilichosimuliwa;
Nimefika Nyumbani kwa Amani Mwamwindi. Ni majira ya saa kumi na nusu jioni. Ni nyumba ya kawaida sana katikati ya eneo wanaloishi watu wengi, karibu kabisa na soko. Ni kata ya Mlandege.
Nagonga mlango mkuu. Anayenifungulia ni Amani Mwamwindi.
” Karibu Bwana Mjengwa”. Tunafahamiana, tumewahi kukutana kabla. Miguuni hana viatu, amevaa soksi nyeusi.
Ananikaribisha kiti sebuleni. Anaagiza nilitewe kinywani. Naye anakaa kitini. Mazungumzo ya ana kwa ana. Kichwani najiuliza; unaanzaje mahojiano na mtu aliyefiwa baba yake kwa kunyongwa miaka arobaini iliyopita?
”Bw. Mwamwindi, pole sana kwa tukio lile la mwaka 1971. Mimi nimelifuatilia kiasi. Kuna simulizi nyingi mitaani. Nimeanzisha mjadala bloguni. Vijana wengi wanaonyesha kuwa na kiu ya kutaka kujua ukweli hasa wa tukio lile. Kwa vile uko hai, nikaona nikutafute tusikie kutoka kwako.”
Mwamwindi ananiangalia usoni.
” Alaa!” Anatamka. Kisha kinafuata kimya.
Nakumbuka, kuwa nimetoa maelezo ya utangulizi, sijauliza swali.
” Je, ni kweli kuwa Dr Kleruu alikwenda Isimani kwa marehemu mzee Mwamwindi kuhimiza suala la kilimo ndipo akakutana na kifo chake? ” Namwuliza kwa staili ya kurusha mshale bila kulenga hasa ninachotaka kupiga. Namjengea mazingira ya kuogelea katika kile anachokijiua. Na swali hili kwake analiona zuri sana.
” Swali zuri, umeuliza kama Kleruu alikwenda kuhimiza kilimo. Hapo ndipo lilipoanzia tatizo.”
Nakumbuka swali muhimu kabla hajaendelea.
” Mzee Mwamwindi, hivi ulikuwa na umri gani siku hiyo ya tukio?”
” Nilikuwa na miaka 21, na marehemu mzee alikuwa na miaka 42.”
Nauliza tena.
” Tunasoma kuwa ilikuwa siku ya Krismasi. Je, ilikuwa ni Jumapili au siku gani? Na wewe ulikuwapo nyumbani kwa mzee?”
” Ni kweli ilikuwa siku ya Krismasi, Desemba 25, 1971. Ni siku ya Jumamosi” Anajibu Mwamwindi.
” Turudi kwenye tatizo lilipoanzia” Namwomba Mzee Amani Mwamwindi.
” Kulikuwa na tofauti ya kimtazamo. Na ugomvi ulianzia siku ya Alhamisi, Desemba 23 kwenye ukumbi wa welfare pale Mshindo. Kleruu aliwakusasanya wakulima wakubwa wa Isimani. Nataka ujue kuwa Isimani ilikuwa na wakulima wakubwa sana na mmoja wao ni marehemu baba yangu. Mle ukumbini kulitokea malumbano makali sana baina ya wazee wale na mkuu wa mkoa Kleruu.
Wazee hakukubaliana na Kleruu kuwaita pale kuzungumzia kilimo cha eka mbili au tatu wakati wao kila mmoja ukubwa wa shamba ulianzia eka mia mbili. Na tayari walikuwa na ushirika wao. Mimi nikiwa na miaka 21 nilikuwa karani wa chama cha ushirika.
Siku ile Mzee alitoka kwenye mkutano ule na kuja nyumbani kwangu hapa tulipo, Mlandege. Akanieleza juu ya mkutano ule na jinsi walivyokosana kimazungumzo na Kleruu. Akaniambia, kuwa mle mkutanoni alimwambia Kleruu ni vema akawasaidia wale ambao hawajaanza hata kutembea kuliko kuhangaika na watu wenye uwezo wa kutembea na kukimbia. Na baba yangu hakwenda shule.
Kwenye Umoja wao wa wakulima wa Isimani, baba na wenzake walijipanga vema. Walishaanza kuzungumzia haa uwezekano wa kumlipa mwanasheria, hata kama ni wa kutoka Uingereza, aje kuwatetea katika uovu ule wanaotaka kufanyiwa. Hawakukubaliana na utekelezaji wa sera za Ujamaa kwa staili ile aliyotaka Kleruu. Kuingia kwenye ushirika na wengine wakati wao walishaanza zamani. Fikiri, wao walifyeka mashamba yao tangu miaka ya hamsini. Hoja yao ni kuwa mapori yalikuwa hayajaisha kwa wengine kwenda kufyeka na kulima. ” Anazungumza Mzee Mwamwindi. Anaonekana kuwa na mengi sana, na hamu ya kusimulia zaidi. Nabaini pia, kuwa kwake yeye mkuu yule wa mkoa ni Kleruu na hamtaji kama ' Dr Kleruu'. Namwacha aendelee.
” Sasa baada ya ile alhamisi, mzee akashinda Ijumaa. Jumamosi ikawa siku ya Krismasi. Kwa vile wafanyakazi wake wa shambani walikuwa mapumziko ya krismasi. Na yeye ni mwislamu, na alikuwa mchapa kazi kweli, basi, alikwenda shamba lake la jirani akiwa na mdogo wangu, sasa ni marehemu, anaitwa Mohamed. Wakawa wanalima kwa trekta.
Siku hiyo Kleruu, pamoja na kuwa ni Mkristo, aliamua kutokula Krismasi. Alivaa kofia yake ya pama. Inaaminika alibeba pistol yake pia. Kleruu akaendesha mwenyewe gari lake la mkuu wa mkoa aina ya Peugeot Injection, rangi ya bluu. Katika orodha yake, Kleruu alikuwa na watu watatu wa kuwashughulikia miongoni mwa wakulima wale wakubwa wa Isimani. Target nambari moja alikuwa Bw. Rashid Juma wa Nyangólo. Nambari mbili ni marehemu baba. Namba tatu simjui.
Kleruu alipofika Nyang’olo hakumkuta mkulima Rashid Juma. Siku hiyo ya Krismasi Rashidi Juma alipata habari, kuwa kuna ng’ombe wake walipotelea milimani. Alikwenda huko milimani kusaka ng’ombe wake. Hivyo, Kleruu akafunga safari kurudi kwa target namba mbili, baba yangu Mzee Mwamwindi. Ni njia hiyo hiyo, Nyang´'olo iko mbele ya ilipokuwa ngome ya mzee.” Anasema Mwamwindi akionekana kuzama katika simulizi inayomgusa. Nami namsikiliza kwa makini.
”Basi, Kleruu akafika kwa Mzee. Baba akiwa shambani akaliona gari la Kleruu limesimama nje ya mji wake. Kisha akamwona Kleruu akitembea kumfuata shambani. Baba alihisi tu, kuwa Kleruu amekuja na shari.
Kleruu akamwuliza Mzee kwa ukali, ” Mbona mnafanya kazi leo siku ya Krismasi?”. Baba akamwomba Kleruu waende wakuzungumze nyumbani. Akamwambia mdogo wangu Mohammed aendelee kulima. Mzee akatangulia mbele, nyuma anamfuatia Kleruu. Kabla ya kufika kwenye nyumba yake wakayapita makaburi. Kleruu akamtamkia baba mzee Mwamwindi; ” Hapa ndipo unapozika mirija yako?” Alitamka hivyo huku akimtomasa tomasa mzee na kifimbo alichoshika mkononi.
Jambo hilo lilizidi kumkasirisha marehemu mzee. Akafika nyumbani kwake. Mlangoni alisimama mke wake mdogo. Inaonekana mzee alishafanya uamuzi. Jana yake alikwenda kuwinda. Hakupata mnyama. Bunduki yake moja aia ya riffle kati ya bunduki zake mbili ilikuwa bado ina risasi. Akamwambia mke wake mdogo huku Kleruu akiwa anasikia;
” Kanichulie bunduki yangu”…… ( Simulizi hii inaendelea baadae. Jamani, Jumapili leo, nipumzike kidogo!)
| Reactions:: |
Saturday, November 27, 2010
Bunda, Jimbo Katoliki Jipya
Spika Makinda akutana na Balozi Radhia Msuya nchini Afrika kusini akiwa safarini kwenda namibia

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) ( wa pili kushoto) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe. Radhia Msuya (mwenye gauni).Wengine ni maafisa wa Ubalozi pamoja na wasaidizi wa Spika. Spika Makinda alisimama kwa muda nchini Afrika Kusini alipokuwa safarini nchini Namibia kuhudhuria mkutano wa mabunge ya nchi wanachama wa SADC. Balozi Msuya alitumia fursa hiyo kumwandalia Mhe. Spika chakula cha mchana ikiwa ni pamoja na kumpa pongezi kwa kuchaguliwa kwake kushika wadhifa wa uspika wa bunge.
| Reactions:: |
JK Awaapisha Mawaziri Ikulu Leo
1.Mawaziri wakiwa wanasubiri kuapishwa katika vwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
2.Naibu waziri Wizara ya Ujenzi Dr. Harrison Mwakyembe akielekea kula kiapo.
3.Waziri wa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe wakibadilishana Mawazo Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja kabla ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete leo jijini.
4.Rais Jakay Kikwete akimpongeza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka baada ya kuapisha na kumkabidhi zana za kufanyia kazi Ikulu jijini leo Dar es salaam .(Picha:Mwanakombo Jumaa)
4.
| Reactions:: |
Subscribe to:
Posts (Atom)





















