Subscribe:

Friday, December 31, 2010

Tajiri Nambari Moja Duniani Atua Arusha Kimyakimya



TAJIRI namba moja duniani, Bw. Mukesh Ambani (53) (pichani) raia wa India amewasili nchini jana alfajiri kimyakimya kwa safari ya
kitalii.
Tajiri huyo aliwasili jana saa 10.15 alifajiri Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na ndege nne binafsi akifuatana na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 50.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mmoja wa waratibu wa safari hiyo hapa nchini, Bw. Godfrey Famandes zimeeleza kuwa lengo la safari yake ni kutembelea hifadhi za taifa, hususan Hifadhi ya Serengeti.

Bw. Ambani kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kimataifa ndiye tajiri namba moja akimiliki dola za Marekani bilioni 63.2 (zaidi ya sh. trilioni 90), akifuatiwa na Carlos Slim Helu kutoka Mexico mwenye dola za Kimarekani bilioni 62.2993 na Mmarekani William Bill Gates akifuatia kwa karibu akimiliki dola za Marekani bilioni 62.29.

Katika kundi hilo dogo la matajiri watano duniani nafasi ya nne inashikiliwa na Warren Buffett kutoka Mexico ambaye anamiliki dola 55.9 na kufuatiwa na Lakshmi Mittal wa India mwenye kitita cha dola bilioni 50.9.Akizungumza na njia ya simu jana, Bw. Famendes ambaye ni Mkuu wa Oparesheni wa Kampuni ya Gapco Tanzania ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo na mwenyeji wa
tajiri huyo, alikiri kuwasili kwa tajiri huyo na kusita kuzungumzia safari hiyo zaidi.
Safari yenyewe ni ya binafsi zaidi, hivyo sina cha kukueleza zaidi ya kukuthibitishia kuwa ni kweli amewasili…sina uhakika na idadi ya wafanyabiashara aliofuatana nao,� alisema Bw. Famendes kwa njia ya simu.

Habari zaidi kuhusiana na safari hiyo zimeeleza kuwa tajiri huyo pamoja na wenzake wamewasili Hifadhi ya Serengeti, ambayo ina hadhi ya urithi wa dunia, na tayari jana walifanya mzunguko wa kwanza wa kutembelea hifadhi hiyo na kujionea maajabu ya dunia ya hifadhi hiyo.
Kuja kwa mfanyabiashara huyo na wenzake na fahari kubwa kwa Tanzania, kwani ni kielelezo kuwa tayari dunia imeanza kujua vivutio tulivyo navyo, nchini na umuhimu wake duniani, alisema mmoja wa wakurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) huku akisizitiza kuwa hana habari lakini akiahidi kufuatilia ujio huo.

Bw. Ambani alizaliwa Aprili 19 mwaka 1957, huko Aden (Colony of Eden) sasa Yemen akiwa na uraia wa India. Kwa sasa anaishi Antilia, Mumbai Maharashtra na mke wake Nita Ambani, wakiwa na watoto watatu, Akash, Anant na Isha

Alisoma Chuo Kikuu cha Mumbai na baadaye Stanford, Uingereza. Kwa sasa ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reliance Industries chini ya Ambani Group of Campanies.
(Chanzo:Gazeti Majira)
Reactions::

Vodacom Babati Half Marathon zafana



1.Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume kwa kilometre 21 Vodacom babati half Marathon ndugu Fabian Joseph akipokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi mh. Claudio Bitegeko Regional Admistrative Secretary wa mkoa wa Manyara.

2.Washiriki wa mashindano ya Vodacom babati half marathon wakiwa tayari kwa kuanza mashindano katika ofisi za Manyara internet café.
(Michuziblog)
Reactions::

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA IRINGA!



Ndugu Zangu,

Naandika nikiwa Iringa.
Ndio, tunaumaliza mwaka huu na mjadala wa Katiba mpya. Nami, katika siku hii ya mwisho wa mwaka, nimeona umuhimu wa kuzungumzia suala hili lililo ndani ya wakati.

Mapema kabisa nataka niweke wazi , kuwa lililo muhimu kabisa katika mjadala wowote uwao ni kujiuliza; nini shabaha na malengo yetu? Nionavyo, shabaha na leo letu liwe kudumisha Umoja wetu wa Kitaifa, amani na utulivu tulio nao. Kama swali ni je, Katiba yetu ya sasa, na kwa wakati uliopo, inakidhi matakwa ya shabaha na malengo yetu kama taifa? Jibu langu ni HAPANA. Na ndio maana naunga mkono juhudi za kufanya marekebisho makubwa ya Katiba yetu.

Na katika hili hatuna sababu za kugombania fito ilihali nyumba tunayojenga ni moja na ni yetu sote.
Ieleweke, kuwa madai ya Watanzania kupata Katiba mpya ni madai muhimu na ya kihistoria. Kuna wanaojidanganya, wakidhani, kuwa madai haya yanatokana na ‘ Njama za mabeberu!’. Hizi ni propaganda za miaka ya 70, zimepitwa na wakati.

Ni busara kutambua, kuwa wakati umebadilika. Mtanzania wa mwaka 1977 si Mtanzania wa mwaka 2010. Hoja hii ya Katiba si kama nzi anayetua na kuruka. Hoja ya Katiba kwa sasa inaongozwa na kundi kubwa la vijana wanaotaka mabadiliko. Hawa si nzi wanaotua na kuruka, ni siafu wanaokuja kwa kuongezeka idadi yao.

Na madai ya marekebisho ya Katiba si madai mapya. Si madai ya chama au kikundi kidogo cha ’wapinzani’ wasioitakia mema nchi hii. Ni madai ya msingi ya Watanzania, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kidini, rangi na makabila.

Kama ni shauri mahakamani, basi, lilishafunguliwa. Kinachofanyika sasa ni mwendelezo wa shauri. Ndio, tunapongia mwaka 2011, madai ya Katiba mpya yatatimiza miaka 20. Yalianza tangu mwaka 1991.

Ndio, si wengi, miongoni mwa vijana wa sasa, wenye kumbukumbu ya ukweli huu. Tayari mwaka 1991 vuguvugu la kudai vyama vingi na Katiba mpya lilishaanza. Ndio, wakati huo madai makubwa yalikuwa mawili; vyama vingi na Marekebisho ya Katiba. Kuna mnaokumbuka ’ KAMAKA’- Kamati ya Marekebisho ya katiba iliyondwa na wanaharakati. Hayo yalikuwa ni madai ya Watanzania ndani ya mfumo wa chama kimoja.

Marehemu Chifu Abdalah Fundikira aliongoza Kamati iliyoundwa, si na Serikali, bali wanaharakati, kuratibu mchakato wa kudai vyama vingi na Katiba mpya. Hata wakati huo Mzee Mwinyi, kama Rais,

Aliweka ‘ mkwara’, kuwa madai hayo yasiendeshwe na watu au makundi ya watu bila kibali cha Serikali. Presha ya madai ilipoongezeka, tunakumbuka, kuwa Mzee Mwinyi aliweza kusoma alama za nyakati. Aliongea pale Chuo Kikuu Mlimani na kuweka bayana dhamira ya Serikali ya kuunda ‘ Tume ya Nyalali’ . Tume hiyo ilizunguka nchi nzima kuwauliza Watanzania kama wanataka kuendelea na Chama kimoja au Vyama vingi.

Itakumbukwa, Chifu Fundikira alipata kutamka; kuwa huko ni kupoteza muda na fedha za wananchi. Itakumbukwa pia, Mabere Marando alikuwa Katibu wa Kamati ile ya wanaharakati ya kuratibu mchakato wa madai ya kuwepo na vyama vingi na marekebisho ya Katiba. Marando alipata kutamka na kunukuliwa na Daily News, April, 12, 1991; “ We have a bad political system because our Constitution embraces political discrimination. What we want is that all of us should shout out that our Constitution is bad.” ( Mabere Marando, Daily News, April 12, 1991)

Ndio, Marando aliyasema hayo katika Semina ya kwanza ya Kamati ya kuratibu mchakato wa madai ya vyama vingi na Katiba mpya iliyoongozwa na Chifu Fundikira. Semina hiyo iliudhuriwa na watu wapatao 800 kwa mujibu wa taarifa ya Daily News la April 12, 1991.

Na akina Chifu Fundikira waliandamwa sana. Kwa mujibu wa Daily News la April 26, 1991, Mbunge wa Shinyanga, Ndugu Paulo Makolo alimshambulia Fundikira kwa kusema kuwa , katika hilo la kuwa na vyama vingi na katiba mpya , Chifu Fundikira hawasilishi mawazo ya Wasukuma na Wanyamwezi wenzake; “ This is not a Wanyamwezi and Wasukuma movement. It is the selfish interests of Fundikira and his ten colleagues. Our people are not after parties. They want food, water, education and health care.” ( Paulo Makolo, MP, Shinyanga, Daily News, April 26, 1991). Mwenyezi Mungu umrehemu Chifu Abdalah Fundikira.

Na hili nalirudia, kuwa, enyi Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yenu, msikae mkafikiri, kuwa madai ya kupata Katiba mpya ni kazi nyepesi. Ni kazi ngumu sana, hata kama mnaowataka wawasaidie kupata Katiba hiyo ni Waafrika wenzenu na si wakoloni.


Ilivyo Afrika, kwanza mtaletewa na walio kwenye mamlaka, ’Katiba mpya’ iliyofanyiwa marekebisho madogo kwa maana katiba iliyoongezewa viraka. Haitawapitisha kwenye chaguzi kwa salama. Kuna kuandamana na hata raia kupoteza maisha. Kuna akina Ocampo wa Mahakama za Kimataifa watakaokuja kuwanyofoa wahusika wa vurugu zitakazozua mauaji ya raia.


Kisha itakuja Katiba mpya. Ni njia mbaya na ya kusikitisha, lakini inaepukika, kama kuna utashi wa kisiasa. Ndiyo, Afrika kudai Katiba mpya yaweza kuwa ni kazi ngumu kuliko kudai uhuru kutoka kwa mkoloni.


Wahenga walinena; "Kazi ngumu ianze!" Si kupiga domo tu, akina Chifu Fundikira wameonyesha mfano. Na nani ajuaye, kwa vile madai ya Katiba mpya ni madai ya haki, kama sauti za wenye kudai zitakuwa nyingi, upo, uwezekano wa kufanyika kwa marekebisho makubwa ya Katiba ndani ya miaka mitano ijayo. Na hapa ielekewe, Katiba iliyofanyiwa mabadiliko makubwa nayo ni Katiba mpya, na ndiyo yenye kuhitajika kwa sasa. Ndiyo, kuipata ni kazi ngumu. Kufanikisha kuipata ni kuianza kazi hiyo, sasa.

HERI YA MWAKA MPYA KWENU NYOTE!
Maggid
Iringa
Desemba 31, 2010.
Reactions::

Swali Langu La Kufunga Mwaka.....



Je, Uhuru = Hakuna Upinzani? Jibu NDIYO/HAPANA( Fikiri kwa bidii, jibu na jadili, ukipenda)

HERI YA MWAKA MPYA!

Maggid
Iringa.
Reactions::

Kama Nchi, Tumefanya Kosa Kubwa Sana ( Makala, Raia Mwema)



Na Maggid Mjengwa,



UKITAKA kumjua Mwafrika, basi, mwangalie siku anapohama. Ndivyo tulivyo. Hata kwenye uongozi, ni hivyo hivyo. Mwangalie kiongozi wa Afrika anapoingia na anapotoka kwenye madaraka.


Ndiyo,; hana tofauti sana na Mswahili anayehama kutoka
Reactions::

Nauza Samaki.....


.....wapo wa shilingi 500 na 700. Mjini Morogoro.(Picha:Mdau)
Reactions::

Wakimbizi Wa Ivory Coast Kusaidiwa


Wakimbizi wa Ivory Coast katika kituo cha Msalaba Mwekundu

Mashirika ya misaada ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu yameanzisha wito wa kuchangisha dola milioni moja kusaidia nchi zinazopakana na Ivory Coast ili kusaidia watu wanaokimbia msukosuko wa kisiasa nchini humo.

Liberia inajiandaa kupokea wakimbizi wapatao laki moja kutoka Ivory Coast.

Mapema, balozi mpya wa Ivory Coast katika Umoja wa Mataifa, alionya kuwa nchi hiyo inakaribia kuingia katika mauaji ya kimbari.

Balozi Yusufu Bamba, aliyeteuliwa na mtu anayedhaniwa kuwa mshindi na jumuiya ya kimataifa Alassane Ouattara, aliomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati suala hilo.

Rais aliyekuwa akitetea kiti chake Laurent Gbagbo amegoma kuachia madaraka.

Zaidi ya watu mia moja na sabini wamekufa katika ghasia tangu kufanyika kwa uchaguzi mwezi uliopita.
(BBC Swahili)
Reactions::
Reactions::

Thursday, December 30, 2010

Maamuzi Mengine Ni Magumu......


.... Lakini Ni Lazima Yafikiwe, Na Busara Itangulizwe. Hapa Najiuliza; Nisubiri Wavuke, Au Nipite Halafu Nao Wavuke? Mikumi National Park.
Reactions::

Polisi Mwanza Wanusuru Uvamizi Wa Bank


Jeshi la polisi mkoani Mwanza linafanikiwa kuwanasa watu wanne waliokuwa katika mpango wakufanya uvamizi katika benki ya BOA iliyopo mtaa wa Kaluta jijini hapa.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Simon Sirro amesema kuwa mara baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasiri wake kuwa kuna watu wamejipanga kuvamia benki hiyo, waliweka mtego na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Donard Charles (28) mfanyakazi wa zamani wa benki hiyo aliyetimuliwa kazi.

Baada ya kuhojiwa na maafisa wa polisi, Charles alikiri kuhusika na mpango huo wa uvamizi na kusema kuwa kabla ya kukamatwa, yeye pamoja na wenzake wengine watatu walipanga uvamizi huo ufanyike mnamo tarehe 21 disemba 2010.

Ndani ya maelezo yake mtuhumiwa huyo amesimulia kuwa mara baada ya kufukuzwa kazi alifanya mpango wa kutafuta watu wengine watatu ili apate kushirikiana nao katika mpango huo haramu ambao nao tayari wamekwisha kamatwa.

Kamanda amewataja watu hao wanaoshikiliwa kuwa ni Henry Juma Salehe (32) ambaye ni shoe shine jijini Mwanza, Emanuel Masamilo (27) anayejihusisha na udalali pamoja na Wachu Kaloboka mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga ambaye ndiye mwenye siraha ambayo ilikuwa itumike kutekeleza uvamizi huo.
Reactions::

Wakamatwa Wakinadi Nyeti Za Baba Yao


IGP Mwema.

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limewakamata ndugu wawili wakitafuta soko la viungo vya binadamu walivyotarajia kupita kwa kumuua baba yao mzazi.Vijana hao walikamatwa wakitafuta soko hilo kwa mfanyabiashara maarufu wa mafuta katika
manispaa ya Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 6:00 usiku katika eneo la Msamala mjini hapa, kwenye ofisi ya kampuni moja ambayo inajishughulisha na uuzaji wa mafuta na usafirishaji wa abiria.

Alisema kuwa watu wawili ambao ni Mohamed Mohamed (25) na Hashim Yasin (25) wote wakazi wa Kijiji cha Hanga Monasteri wilayani Namtumbo, walifika kwenye ofisi hiyo na kumkuta mkurugenzi wa kampuni na kumueleza kuwa wana viungo vya binadamu ambavyo wanataka kumuuzia.

Baada ya mazungumzo, watu hao walikubaliana kuwa viungo hivyo ni sehemu za siri za baba yao, ambazo zingeuzwa kwa sh. milioni sita na za kaka yao kwa sh. milioni tatu.

Baada ya makubaliano hayo, mkurugenzi huyo aliwasiliana na polisi ambao waliweka mtego na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao.

Kamanda Kamuhanda alisema kuwa watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi kuhusiana na madai hayo walikiri na kuwa walikuwa na mpango wa kwenda Tunduru kuwaua baba yao na kaka yao ili wafanikiwe kuchukua viungo hivyo na kuviuza kwa mfanyabishara huyo.
(Chanzo:Gazeti Majira)
Reactions::

Membe Aelekea Nchini Brazil leo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), ameondoka nchini leo tarehe 30 Desemba 2010 kwenda Brazil kumwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye sherehe za kumwapisha, Rais Mteule wa Brazil, Bibi Dilma Rousseff zitakazofanyika mjini Brasilia tarehe 1 Januari 2011.

Wakati wa sherehe hizo, Mhe. Membe atawasilisha salaam maalum kwa Mhe. Dilma Rousseff kutoka kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete.

Aidha katika ziara hiyo, Mhe. Membe atapata fursa ya kufuatilia makubaliano mbalimbali ya ushirikiano yaliyofikiwa baina ya Tanzania na Serikali ya Brazil wakati wa ziara yake aliyoifanya nchini humo mwezi Septemba, 2010.

Makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara hiyo ni pamoja na Brazil kuisaidia Tanzania katika sekta ya kilimo, kuendeleza mradi wa kufua umeme katika Bonde la Mto Rufiji (Stigler’s Gorge), uzalishaji nishati mbadala ya umeme kwa kutumia mimea, miundombinu viwanda na biashara.

Mhe. Membe atarejea nchini tarehe 3 Januari, 2011.

IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 DESEMBA 2010


Reactions::

Candid Scope Anaendeleza Mjadala: Je, Ni Kweli Watu Weusi Tuna Akili Ndogo?





Nlilipokuwa nasoma darasa moja ambalo Instructor na wanafunzi wote ni wazungu isipokuwa mie mweusi peke yangu katika moja ya mataifa makubwa siku ya kwanza nikaona kama ni kiinimacho ukitilia maanani kuwa wao lugha ni yao ya kuzaliwa na mie ulimi mzito kidogo tokana na kimatumbi changu. Utundu wao ndio... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Mapacha Walioungana Wamaliza La Saba


Mapacha wawili walioungana kiwiliwili,Maria Mwakikuti(kushoto)na Consolata Mwakikuti(kulia) wakipata chakula pamoja wakati wa hafla ya kuwapongeza kwa kufaulu mtihani wa Darasa la Saba iliyofanyika katika Hospitali ya Misheni Ikonda Makete
. (Picha: Frank Leonard)
Reactions::

Mboga,,,,


......Manispaa ya Morogoro hivi karibuni. (Picha: Mdau)
Reactions::

Anaitwaje Huyu?



Kwa Kiswahili na kilugha cha kwenu?
Reactions::

Vuai Nahodha Atunuku Vyeti Na Zawadi





Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha (suti nyeusi ) leo jijini Dar es Salaam akikagua Gwaride la Jeshi la Polisi wakati wa Hafla ya kutunuku vyeti na zawadi kwa utendaji uliotukuka kwa askari wa vyeo mbalimbali na raia walioshiriki kufanikisha utendaji wa kazi za Polisi nchini. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Reactions::

" Pokea Laki Tano Hizi!"


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha (suti nyeusi) akimkabidhi cheti na shilingi laki tano kwa mdau mkereketwa wa mambo ya ulinzi na amani Mohamed Majid (kulia) katikahafla fupi leo jijini Dar es salaam.
Reactions::

Maonyesho Ya Doria



Baadhi ya askari Polisi wakionyesha mfano wa matumizi ya Doria kwa baiskeli leo jijini Dar es Salaam ambazo baskeli 100 zimetolewa na Kampuni ya Home Shopping Centre kwa jeshi la Polisi. Sherehe ya makabidhiano yamefanyika jijini leo wakati wa hafla ya kutunuku vyeti na zawadi kwa utendaji uliotukuka kwa askari wa vyeo mbalimbali na raia walioshiriki kufanikisha utendaji wa kazi za Polisi nchini. Picha na Mwanakombo Jumaa -MAELEZO.
Reactions::

Ngeleja Abeza Msimamo wa TUCTA



WAZIRI wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja amekejeli tishio la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), kutaka kuandamana kupinga ongezeko la bei ya umeme na kueleza kuwa Watanzania si wajinga kuburuzwa na watu wenye
maslahi binafsi.

Alisema kiwango cha juu kilichoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (UWURA) ni sh. 28 kwa kila uniti moja katika matumizi ya kawaida, kiasi ambacho kwa mujibu wa Bw. Ngeleja si kikubwa kama inavyotafsiriwa na TUCTA na baadhi ya watu.

Kwa kiwango hicho, mteja wa TANESCO alikuwa anatumia uniti 100 za umeme kwa mwezi, kuanzia Jumapili atalazimika kutoa sh 2,800 zaidi ya bei aliyokuwa anatoa awali.

"Nilichoelewa ni kuwa TUCTA walikurupuka kutoa kauli bila kujua ukweli wa kiwango gani kilichoidhinishwa, kilichoongezeka kwa kila uniti ni sh. tano, sh. tisa, sh. 11 na kiwango cha juu kabisa ni sh. 28, kutegemea na aina ya matumizi.

“Hivi ni nani akipewa sh. 28 anaweza kununua chochote kwa dunia ya leo, wasidhani Watanzania ni wajinga wanaweza kuburuzwa tu na fikra binafsi za watu kujitafutia umaarufu hapana tutafute ukweli jamani," alihoji Bw. Ngeleja.

Alisema TANESCO iliomba ongezeko hilo kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji na kwamba mara ya mwisho bei hizo ziliongezwa Januari 2008.

"Serikali kwa maana ya TANESCO inatambua uwezo wa wateja wake ndio maana inajitadi kubeba sehemu kubwa ya gharama za umeme, ukiangalia tangu mwaka 2008 bei ya vitu ikiwemo mitambo imepanda kwa kiasi kikubwa," alisema Waziri Ngeleja.

Tanesco ilikuwa imeomba ongezeko la asilimia 34.6 lakini EWURA baada ya kusikiliza hoja za wadau ikapitisha asilimia 18.5.Wakati huo huo TANESCO imetoa taarifa inayoonesha mchanganuo wa ongezeko la bei mpya ya umeme kwa watumiaji kulingana na matumizi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kundi la watumiaji wadogo majumbani (D1) itapanda kwa sh. 11 kwa uniti moja hivyo kuwa sh. 60 kwa uniti badala ya sh.49 za awali.

Kundi la watumiaji wa kawaida (T1) ambao ndio wamepanda zaidi watalipa sh 157 kwa uniti moja kutoka sh. 129 za awali, sawa na ongezeko la sh. 28 kwa uniti moja.

Taarifa hiyo ya TANESCO imetaja kundi la mahitaji ya juu ya msongo mdogo (T2) kuwa na ongezeko la sh. tisa kwa kila hivyo na kufikia bei ya 94 kutoka sh. 85 za awali.Kundi la mahitaji ya juu ya msongo mkubwa (T3/T3a) ongezeko ni sh. tano kwa uniti, hivyo kupanda kutoka sh. 79 ya awali hadi sh. 84.

Kundi la mwisho linalohusu Tanzania visiwani (T5/T3b) ongezeko ni sh. nane kwa uniti moja hivyo gharama zitapanda kutoka sh. 75 hadi 83 kwa kila uniti moja.Wiki iliyopita Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Nicholas Mgaya, aliitaka Serikali kufuta uamuzi wa kupanda kwa bei ya umeme na kutishia kuandaa maandamano ya amani nchi nzima kupinga hoja hiyo.

Bw. Mgaya alisema Kamati ya Utendaji ya TUCTA ilifikia maamuzi hayo kwa maelezo kuwa ongezeko hilo ni kubwa na haliendani na hali ya Mtanzania na hivyo litazidisha ugumu wa maisha kwa wafanyakazi na Watanzania kwa ujumla.

(Chanzo:Gazeti Majira)
Reactions::

CUF Wapewa Pole Na Kupongezwa


Maandamano Ya Cuf juzi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Zanzibar For Democracy (U.K.) inachukua nafasi hii ili kuwapa pole na kuwafariji wanachama wa CUF na wananchi waliojeruhiwa na kukamatwa katika maandamano ya kuwasilisha rasimu ya katiba mpya; Wakati huo huo Jumuiya inawapongeza sana viongozi na
wanachama wa CUF na wananchi waliojitolea kushiriki katika maandamano hayo na kufanikiwa kuiwasilisha rasimu hiyo.
Hatua hiyo waliyoichukua inathibitisha uelewa wao wa kiwango cha juu wa mapungufu yaliyomo katika Katiba iliyopo sasa ambayo haikidhi matakwa ya wananchi wengi wa Tanzania.
Tunaamini kuwa rasimu hiyo ni kielelezo halisi cha matakwa ya wananchi walio wengi na itakidhi kabisa hoja zote za kikatiba na kisheria ambazo kwa muda wote zimekuwa ni miongoni mwa matatizo ya msingi yanayoidhoofisha demokrasia nchini.
Tunataraji kuwa hatua iliyochukuliwa na wananchi hao itakuwa ni changa moto muhimu sana kwa viongozi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ngazi zote na kila mmoja wao ataikubali na kuitafsiri kuwa ni kichocheo cha kufungua kwa upana zaidi milango ya siasa za uwazi na kuwa ni dira kamili ya demokrasia iliyokamilika.
Tunaziomba taasisi zote za kiserikali na zile ambazo si za kiserikali kuunga mkono rasimu hiyo ili nchi yetu iweze kupata katiba mpya na tuachane na tabia ya kutia viraka kwani kufanya hivyo ni kuongeza matatizo badala ya kuyatatua.
Aidha, tunawasifu sana wale wote walioiandika rasimu hiyo, kwani wao wameonyesha na kuthibitisha kwa vitendo namna wanavyoipenda na kuitakia mema nchi yetu. Tunawaomba wananchi wote waiunge mkono rasimu hiyo ili tuondokane na migogoro na mivutano inayokwamisha maendeleo.

Ahsante.
(Abdulla A. Abdulla),
KATIBU,
ZANZIBAR FOR DEMOCRACY(U.K.)
Reactions::

Chenge Ahukumiwa Faini Ya Laki 7.


Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu wa Serikali ya
awamu ya tatu Andrew Chenge, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela
au faini ya Sh 700,000 na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ambapo
aliwasilisha faini hiyo mara baada ya hukumu hiyo kutolewa leo
asubuhi.

Akitoa hukumu hiyo jana Hakimu Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi
hiyo Kwey Rusema alisema uamuzi huo wa Mahakama unafuatia kukamilika
kwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote mbili katika kesi
hiyo iliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi minane.

Akisoma ushahidi wa awali Rusema alisema Chenge anashitakiwa kwa
makosa manne yakiwamo kuendesha gari bila uangalifu, kusababisha vifo
vya wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine na Victoria Geogre,
kuendesha gari kwa uzembe na kuharibu pikipiki aina ya bajaj pamoja na
kuendesha gari lilikuwa na bima iliyokwisha muda wake.

Katika ushahidi wa awali Chenge aliukana na upande wa mashitaka ambapo
waliitwa mashahidi sita kati yao wanne walikuwa Askari Polisi akiwamo
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Fortunatus Musilimu.

Ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulidai tarehe 26 Machi 2009 majira
ya usiku wa manane Chenge akiwa katika matembezi yake binafsi alikuwa
anaendesha gari lake aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili
T512ACE kwenye barabara ya Haille Selasie Oysterbay jijini Dar es
Salaam aligonga bajaj na kusababisha ajali iliyosababisha vifo vya
wanawake wawili.

Maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo kuhusu kuendesha gari kwa uzembe
na kuharibu bajaj Chenge aliyakana na kwa madai kuwa alikuwa katika
mwendo wa kawaida kati ya kilo mita 30 hadi 50 na kudai kuwa dereva wa
bajaj alimfuata upande wake kwani yeye alikuwa upande wa kulia zaidi.

Hukumu hiyo ambayo ilitakiwa kusomwa Desemba 16, mwaka huu,
iliahirishwa baada ya Hakimu kukubali ombi la Wakili wa Chenge
aliyeomba kuahirishwa kwa hukumu hiyo kwa kuwa mteja wake alipata
udhuru.

Mponda alidai kuwa mshitakiwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa
kuwa alisafiri kwenda Mwanza kwenye msiba na kuiomba Mahakama
kuahirisha hukumu hiyo.

Kwa mara ya kwanza, Chenge alifikishwa mahakamani hapo Machi 28, 2009
akikabiliwa na mashitaka matatu likiwamo la kuendesha gari kwa uzembe
na kusababisha vifo vya wanawake wawili, kuharibu pikipiki ya matairi
matatu pamoja na kuendesha gari lisilokuwa na stika ya bima.

Katika ushahidi wake mahakamani hapo, Chenge ambaye ni Mbunge wa
Bariadi Magharibi, alidai kuwa shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka,
Fortunatus Musilimu, ana ugomvi naye.

Chenge alidai shahidi huyo ambaye aliwahi kutoa ushahidi kuwa mabaki
ya ubongo wa marehemu yalikutwa kwenye gari la Chenge na kuwa
aliwasilisha bima batili, kuwa ni mwongo na ana ugomvi naye.

Ilidaiwa kuwa Machi 27, mwaka jana katika Barabara ya Haile Selassie
Oysterbay, Chenge akiendesha gari aina ya Toyota Hilux Pick Up lenye
namba za usajili T512 ACE, aliigonga pikipiki ya matairi matatu
(bajaj) yenye namba T736 AXC na kusababisha vifo vya Beatrice
Costantino na Vick George.
Reactions::

Wednesday, December 29, 2010

Nyumbani Ni Nyumbani!




Mwanablogu mahiri, John Bukuku amekumbuka kwao, kijijini Lwezi, Mbozi, Mbeya. Mtembelee; http://fullshangwe.blogspot.com
Reactions::

Wanapandana Au Wanafanya Mapenzi?



Kamera yangu iliwanasa mwaka mmoja uliopita. Simba wa Mikumi.
Reactions::

Siku Ya Krismas Alionekana!



Simba, a.k.a Mzee Wa Masharubu, Mikumi National Park.
Reactions::

Kibarua Changu Kinaota Nyasi Keshokutwa



Desemba 31, 2010. Miaka miwili ya nyongeza imekwenda mbio. Nilipenda sana kazi niliyoifanya. Nimekutana na watu wengi, nimejifunza mengi. Siku za baadae kuna nitakayopenda kuyafanya, kwa mfano; kurudi darasani na kushika chaki; kufundisha. Nitapenda kujikita kwenye masuala ya uandishi na picha. Nimependa sana mambo ya uandishi na picha tangu nikiwa mtoto. Nitapenda pia kujishughulisha na kilimo ingawa vyetu ni Vi-jishamba! Nitapenda pia kusoma zaidi.Na mengineyo. Salaam zangu za Mwaka mpya zinakuja.
Reactions::

Hukumu Ya Chenge: Faini Ya Vi-Ji- Senti!



Mahakama ya Kinondoni imemwamuru Andrew Chenge kulipa faini ya shilingi laki saba kwa kosa la kugonga na kuua. Labda faini ngumu kwa Chenge ni kulipa senti thelathini!
Reactions::

Born Again Pagan: Richmond/Dowans; Matokeo Ya Unyonge Wa Mtanzania



BAP: U-Nyanga’u Kupitia Wakala – Sakata la Richmond
©Born Again Pagan, New York, 2009-03-07

———————————————

Mwishoni mwa mwaka jana, gazeti moja nchini liliandika habari zenye kichwa, “Giza Nene”
kuhusu sakata la kampuni moja “bandia” ya Amerika ya kufua umeme wa dharura nchini
Tanzania. Wote tunaijua kampuni hii. Na mmojawapo wa wakurugenzi wake, Naeem
Mohamme, sasa kafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusema uwongo na ufisadi!

Wengi wetu bado tumo katika “giza nene” la sakata la Richmond kwa kutoelewa
tunazungumzia kampuni zipi! Sijui ni makosa ya vyombo vya habari. Tusomapo au
tusikilizapo habari kuhusu sakata hili, yaonekana kuwa kuna kampuni sita zinazotajwa tajwa
(mbali na kampuni mbili za Dowans (Afrika Kusini na Tanzania):

Richmond Development Co. (RDC); Richmond Development Corporation (RDEVCO);
Richmond Development, LLC.; LLC.; Richmond Tanzania Limited; na Richmond
Development (Tanzania), Ltd.

Kwahiyo, kabla ya kuelewa “giza nene” lililotangazwa na gazeti hilo, ingekuwa vizuri
tusaidiane kuliondoa. Tubakie na kampuni mbili za awali. Nionavyo, kuna kampuni mbili tu.
Moja, ni kampuni tanzu ya utata ya Richmond Development Company of Houston (RDEVCO)
iliyojidai kusajiliwa huko Houston, Texas, na kampuni-toto ya Richmond Development
Company Tanzania, Ltd. iliyosajiliwa nchini Tanzania, pia kwa utata. Wakati mwingine
yaandikwa kama Richmond Development Company (Tanzania), Ltd. Hii ina maana kuwa ni
“extension” ya kampuni tanzu ya huko Houston!

Kampuni iliyosajiliwa huko Houston, Amerika, ilijulikana kwanza kama Richmond
Development Corporation (RDC). Lakini sasa yajulikana kama Richmond Development
Company of Houston (RDEVCO). Kampuni hii iliundwa na mmoja wa familia ya Gire ya huko
Houston, Mohamed S. Gire. Hao akina Gire ni Wahindi wa kutokea Tanzania!

Akina Gire hao Bwana Mohamed S. Gire (Alim Gire) wana kampuni ya ki-familia yenye
kuchapisha na kurudufu “nyaraka” ijulikanayo kwa jina la Richmond Printing Company.
Bwana Mohamed S. Gire (Alim Gire) ni Chief Executive Officer). Wengine ni ndugu zake:
Samad Gire (Vice President, Business Development), Javeed Gire (Manager), Zahoor Gire
(Vice President Finance), na Imad Gire (Vice President Operations). Dada zao wawili
wanaishi nchini Uingereza, ambako baba yao alikwenda kuishi, kama mfanyabiashara.
Anwani: Richmond Printing L.L.C. ni 5825 Schumacher Lane, Houston, Texas 77057.

Kampuni zote mbili, Richmond Printing Company na Richmond Development Company
of Houston (RDEVCO), zinatumia fax moja: (713) 952-0932-5825. Hii ina maana kuwa
kampuni hizi mbili zinatumia, pengine, jengo moja.

Tovuti ya mwanzo ya Richmond Development Corporation ilionyesha historia ya habari za
Gire kuhama Chicago kwenda Houston kuanzisha kampuni ya kurudufu nyaraka (“copying
centre”) iitwayo, Richmond Printing Company, mwaka 1985. Pia kulikuwa na habari nyingi
za michango ya Bwana Mohamed S. Gire ya takrima na kutunisha mfuko wa kampeni za
Democratic Party (“political campaigns contributions”) kwa House of Representatives.
Inaonekana kuwa....Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Tuesday, December 28, 2010

Bashir atakubali matokeo ya Sudan Kusini.


Rais Bashir wa Sudan
Rais wa Sudan Omar al Bashir amesema atakubali uamuzi wowote ambao Sudan Kusini itaufanya katika kura ya maoni ya uhuru wa eneo hilo mwezi wa Januari mwakani.
Rais Bashir amesema Sudan Kaskazini itatoa msaada wowote utakaohitajika kwa Kusini, kama wataaamua kujitenga au la.

Bashir alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Al-Jazira katikati mwa Sudan.

Alisema serikali ya Sudan itawasaidia watu wa Kusini kuijenga nchi yao, kwa vile inataka taifa hilo liweze kujiendesha bila matatizo.

Rais Bashir mapemwa mwezi wa Desemba alisema sehemu ya kaskazini mwa Sudan, ambapo kuna Waislamu wengi, itaimarisha sheria za Kiislamu ama sharia, baada ya kura ya maoni.
Reactions::

Mwanasheria Mkuu Apinga Katiba Mpya



WAKATI Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika akiwasilisha hoja binafsi ya mabadiliko ya katiba mpya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema amesema kuwa haiwezekani kuandikwa upya na badala yake
kinachowezekana ni kuifanyia marekebisho iliyopo.

Hatua hizo mbili katika mjadala wa katiba mpya unaoendelea kupamba moto kila kukicha zilifikia katika sehemu na nyakati tofauti jana, ambapo Bw. Mnyika alikuwa anawasilisha nia yake hiyo kwenye ofisi za bunge na Jaji Werema akizungumza na waandishi wa habari, ikuru, baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande.

Katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, Bw. Mnyika aliwasilisha nia ya kutoa hoja binafsi katika Mkutano wa Bunge utakaoanza Februari 8, 2011 kuhusu kuanzishwa kwa mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Bw. Mnyika aliwasilisha nia hiyo jana katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es Salaam katika Ofisi ya Katibu wa Bunge na kupokewa na Mkurugenzi wa Idara ya Taarifa, Bw. Eliakim Mrema kwa niaba ya katibu aliyekuwa likizo.

"Nimepokea taarifa hii, sisi kama taasisi, na kwa bahati mbaya au nzuri katibu yupo likizo hivyo naipokea mimi kwa niaba yake," alisema Bw. Mrema.
Kabla ya kuwasilisha taarifa hiyo, Bw. Mnyika alizungumza na waandishi wa habari katika moja ya kumbi za ofisi hiyo, na kudai kuwa, ameona upungufu mkubwa katika maeneo zaidi ya 90 katika katiba, na hivyo kuomba mawazo zaidi ya wananchi juu ya matatizo hayo na mapendekezo yao ya nini kifanyike.

"Katiba inayotumika hii leo ni ya mwaka 1977, tangu kipindi hicho kuna mabadiliko mengi yameshatokea kama ya kiuchumi, kiteknolojia; pili uundwaji wa katiba hiyo haukuwashirikisha wananchi; tatu katiba hii inakabiliwa na changamoto nyingi, mfano suala la Muungano na Tume ya Uchaguzi," alisema.

Alisema katiba ya sasa sio ya kufanyiwa marekebesho tena, bali kubadilishwa kabisa, kwani huwezi kuweka viraka katika upungufu mkubwa namna ile.

Alisema upungufu hayo yamegawanyika katika misingi mikuu mitatu, ikiwa ni pamoja na kasoro za ibara mbalimbali za katiba, zinazominya demokrasia na kunyonya haki za wengine ikiwemo mamlaka makubwa ya rais aliyopewa.

"Mapungufu mengine ni katika uchaguzi, Tume ya Uchaguzi kutokuwa huru pamoja na mfumo wa utendaji kwa ujumla, matokeo ya urais kutopingwa mahakamani, pamoja na mfumo wote wa uchaguzi kwa ujumla.

"Muingiliano wa mamlaka pamoja na taasisi za uwajibikaji mfano Tume ya maadili, TAKUKURU na kufanya vyombo hivyo kutokuwa huru," alidai.
Alisema kuwa msingi wa hayo yote ni katiba mpya, na kudai kuwa mapungufu mengine makubwa katika katiba ni pamoja na kuwa na baadhi ya mambo ambayo hayatumiki kabisa tangu yawekwe.

"Mfano kwenye katiba kuna sehemu inasema kutakuwa na chombo cha mamlaka ya katiba na hakijawahi kufanya kazi hata siku moja, kwani chombo hicho kilikuwa ni kwa ajili ya kushughulikia muungano tu.

Sasa huwezi kuwa na katiba yenye mashimo mengi kiasi hicho, suluhisho ni katiba mpya," alidai.

Bw. Mnyika aliwashangaa wote wanaokusanya maoni kwa wananchi ya kuuliza kama wanataka katiba mpya au la, kuwa kufanya hivyo ni makosa kwani wananchi tayari wameshaonesha kuwa wanataka katiba mpya, kinachotakiwa ni utekelezaji, na maoni yawe wakati wa kupitisha katiba mpya.

Alisema kuwa hoja yake anayotarajia kuwasilisha bungeni, rasimu yake itakuwa wazi wiki ya kwanza Januari, 2011 na wananchi wanaruhusiwa kuongeza na kutoa mawazo juu ya rasimu hiyo ya hoja.

"Kabla sijapeleka hoja bungeni nitaitoa hadharani ili kila mtu atoe maoni yake, ili nitakapoipeleka bungeni yasiwe ni mawazo yangu bali yenye mchango wa wananchi," aliongeza.

Alidai kuwa baada ya kuweka hadharani rasimu hiyo ya hoja, wananchi wanaweza kuchangia kupitia ofisi yake ya ubunge iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam; au kwa barua pepe ; au kwa simu namba 0783 552010; au kwa sanduku la barua, S.L.P 62066 Dar es Salaam.

"Na wiki ya pili ya Januari, 2011 nitafanya mkutano wa wazi Ubungo kukusanya mawazo ya jumla. Na nimefanya hivyo kutokana na unyeti wa suala lenyewe ili nitakapoiwasilisha bungeni iwe ni hoja yenye uzito, yenye mawazo ya wengi na si Mnyika pekee," alisema.

Aliongeza kuwa mfumo huo wa kuwasilisha hoja alioutumia ni wa pekee kidogo, kwani yupo bungeni kuwakilisha wananchi, na hivyo ameona ni bora kuwasilisha hoja za wananchi na si yake binafsi kama wafanyavyo wabunge wengi.

Kwa upande wake Jaji Werema ambaye ndiye mshauri mkuu wa Serikali katika masuala ya kisheria aliweka msimamo wake huo jana katika viwanja vya Ukulu, Dar es Salaam katika hafla ya kuapushwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othuman Chande.

Kurekebisha na kuondoa mambo mengine ni ruksa lakini sio kuandika katiba mpya...tutafanya haya kulingana na mapendekezo au matakwa ya Watanzania hivyo hili halina tatizo litafanyika, alisema Jaji Werema.

Alisema kuwa haitakuwa vyema kama Watanzania watatofautiana kutokana na suala hili kwa kuwa linajadilika na linaweza kutekelezwa kwa manufaa ya wananchi na katika hili kila mmoja anatakiwa kusikilizwa kwa kuwa anao uhuru wa kusema na yuko sahihi.

Kutokana na hali hiyo, alitumia mwanya huo pia kuwaasa wanahabari kutokuwa wachochezi katika suala hili bali watumie kalamu zao vyema kuelimisha wananchi umuhimu wa katiba.

Ni vyema kalamu zenu mkazitumia vizuri kwa kuwa zikitumika vibaya zina madhara makubwa...zinaweza zikanyonga mtu, zinaweza kuleta machafuko, hivyo katika hili acheni ushabiki na muweke mbele maslahi ya Watanzania,� alisema Jaji Werema.

Akijibu swali kuhusu suala hilo kubebwa na wanasiasa, alisema kuwa kila jambo ni lazima liwe na mbebaji, hivyo hata katika suala la katiba ni lazima awepo mbebaji wa aina yoyote kwa kuwa matokeo yake ni matakwa ya Watanzania wote.

Tusivilaumu vyama vya siasa kwa sababu mambo yote hayo ni siasa na hili la katiba lingeweza kubebwa na mtu yoyote awe Profesa, mbunge, mwananchi au mtu yoyote,� alisema.

Akizungumzia uteuzi wa Jaji Mkuu, Jaji Werema alisema kuwa ni mtu mtulivu mwenye uwezo wa kuwaunganisha majaji wote mahali pa kazi lakini pia ni mtu mwenye uzoefu na anayeifahamu vyema sheria hivyo kuteuliwa kwake kutasaidia kuimarisha mhimili huo.

Naye Jaji Mkuu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kula kiapo cha uaminifu, alisema kuwa ni wajibu wake kuhakikisha wananchi wanapata haki zao mapema na kuondoa malalamiko ya ucheleweshaji wa kesi.Changamoto zipo na hazijaanza na mimi lakini nitajitahidi kuhakikisha tunakuwa imara kwa kuwa na mahakimu wa kutosha na wenye ujuzi na sifa za kutosha ili waweze kukidhi mahitaji au matarajio ya wananchi.

Kwa upande wa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan, aliwaomba wananchi kuendelea kuheshimu mahakama na maamuzi yanayotolewa katika kila jambo hivyo kuachana na utamaduni wa kuchukua sheria mkononi.
( Chanzo:Gazeti Majira)
Reactions::

Singida Kuzalisha Umeme Wa Upepo



Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Power Pool East Africa, Machwa Kagoswe akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu juu ya eneo la kuzalishia umeme wa upepo mkoani Singida . Serikali imeingia Ubia kupitia Shiriaka la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni binafsi ya Power Pool East Aftrica ili kuzalisha umeme huo kuanzia mwakani.

Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) limeingia ubia na kampuni ya Power Pool East Africa wa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida utakaogharimu takribani ya Sh Bilioni 180.

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu alisema tayari makubaliano yamesainiwa na shirika la NDC kwa niaba ya serikali itakuwa ikimiliki asilimia 51 za hisa na nyingine zitakuwa za mwekezaji binafsi.

Nyalandu alisema kwa mradi huo ambao utakuwa wa gharama nafuu katika uzalishaji utaingizwa katika gridi ya taifa na kwa kuanzia zitazalishwa megawati 50 na baadae zitaongezwa kulingana na uwezo wa wabia hao.

“Tokea kuanza kufungwa kwa mitambo itachukua takribani miezi 15 ili umeme uingie katika gridi na hii itakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme kwa sasa” alisema Nyalandu.

Mkurugenzi wa Viwanda vikubwa wa NDC, Alley Mwakibolwa alieleza kuwa kwa ujenzi wa mitambo hiyo ya kutumia upepo kutasaidia kuzalisha umeme ampema kwani mitambo ya aina hiyo huchukua muda mfupi kuwekwa ikilinganishwa na ya maji ama ya gesi.

Tutajitahidi mradi huu uende kwa kasi kubwa kwani kwa kuanzia tutazalisha megawati 50 na baadae tutaongeza 50 ili kuoingia katika gridi ya taifa" alisema.

Aidha katikaeneo hilo ambalo liko ukingoni kwa bonde la ufa, upepo ni mkakli kiasi cha kufanya miti karibu yote kulalia upande mmoja na upeo huende kwa kasi ya hadi mita 21 kwa sekunde.
Reactions::

Neno La Leo: Utamjua Mwafrika Anapohama!



Na Maggid Mjengwa,


UKITAKA kumjua Mwafrika, basi, mwangalie siku anapohama. Ndivyo tulivyo. Hata kwenye uongozi, ni hivyo hivyo. Mwangalie kiongozi wa Afrika anapoingia na anapotoka kwenye madaraka.


Ndio, hana tofauti sana na Mswahili anayehama kutoka Mwananyamala kwenda Magomeni. Mswahili wa Mwananyamala, hata kama atahakikishiswa, kuwa anakohamia Magomeni vyumba vyote vina taa za balbu na pazia za madirishani na milangoni, bado, Mswahili huyu atahakikisha, kabla ya kuhama, anang’oa balbu na pazia zote kutoka nyumba anayohama. Mpangaji mpya atakayekuja atajua mwenyewe! Huyo ndio Mwafrika, ingawa si wote, hata ukimchanja kwenye damu yake, utakuta chembe chembe za ushamba uliochanganyika na hila.


Hakika, hizo ni hulka za Mwafrika, hata azaliwe na kukulia Ulaya au Marekani. Si tumesikia majuzi, Waziri aliyepoteza ubunge alihakikisha anahamisha mpaka pazia kutoka kwenye ofisi ya mbunge jimboni kwake. Naambiwa, kuwa Waziri huyo kakulia Marekani. Kumbe, kukulia Marekani hakumwondolei Mwafrika hulka zake! Na hilo Ni Neno La Leo.


( Hii ni sehemu ya makala yangu ( Raia Mwema) ikichapwa, kesho Jumatano.)



Maggid
Iringa
Desemba 28, 2010. ( Picha hiyo ya jamaa wanaohama niliipiga Kinondoni Msufini, miaka hiyoo)
Reactions::

Je, Unataka Kuisoma Katiba?



Tembelea....
Reactions::

Monday, December 27, 2010

JK Amwapisha Jaji Mkuu Mpya






Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Pichani Jaji Mohamed Chande Othman akila kiapo mbele ya Rais huku Jaji Mkuu mstaafu Augostino Ramadhani(kulia) akishuhudia.Katikati ni Kaibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo(Picha: Freddy Maro)
Reactions::

'Mwenye Dowans Atajwe kabla Ya Kulipwa' : Wananchi





SAKATA la malipo ya sh. bilioni 185 kwa Kampuni ya DOWANS iliyorithi mikoba ya kampuni hewa ya Richmond imezidi kuchafua hali ya hewa baada ya wananchi kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumtaja hadharani mmiliki wa kampuni hiyo
kabla ya kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wananchi hao wamesema wanasikitishwa na kauli ya serikali kukubali kuheshimu sheria kulipa Dowans fedha hizo wakati mmiliki wake hajulikani hadi sasa.

�Tunataka serikali, hasa Rais Kikwete, atuonyeshe mmiliki wa Dowans, ajitokeze hadharani mbele ya vyombo vya habari tumfahamu. Haiwezekani nchi ikashindwa kesi na hewa, maana hadi leo hatujui mmiliki wa Dowans ni nani.

"Pia tunataka hiyo hukumu ipelekwe kwa Jaji Mkuu ili baadaye ilitolewe hadharani kwa vyombo vya habari tujue inasemaje,� alisema Bi. Catherine Maliwa wa Kigogo Dar es Salaam.

Alisema katika historia ya Taifa la Tanzania haijawai kutokea nchi ikashindwa kesi na mtu asiyejulikana na kuonya viongozi wa Serikali wanaohusika kutothubutu kutoa hata senti kulipa Dowans bila wamikiki wake kujulikana na kujitokeza hadharani.

“Jambo linalotusikitisha ni kuwa Richmond ni Kampuni feki na wamiliki wake hawajulikani, iweje Kampuni feki ambaye mmiliki wake hajulikani kuuzwa kwa Dowans, mtalipa pesa mashetani?� alihoji Bi. Maliwa.

Alisema hivi sasa Watanzania wamechoshwa na viongozi wazembe wanaowabebesha mzigo wajane na maskini huku wahusika wakibaki salama na kufurahia maisha ya anasa kwa jasho lao.

Alisema baada ya hatua ya Rais Kikwete kumtangaza mmiliki wa Dowans na mwenye kampuni hiyo kujitokeza hadharani na nakala ya hukumu kukwekwa hadharani kwenye vyombo vya habari wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria suala la kulipa fedha hizo liwe la mwisho.

Mkoani Shinyanya wananchi walisema licha ya Mahakama ya Kimataifa ya kusuluhisha migogoro ya kibiashara (ICC) kuipa ushindi Dowand, utekelezaji hauwezekani hadi mmiliki wake ajulikane kwa Watanzania wote.

Walisema ni ajabu na mshangao kwa shirika la serikali kupelekwa mahakamani na mtu asiyejulikana huku baadhi ya viongozi waandamamizi wakionesha kwa haraka dalili ya kutaka kulipa adhabu hiyo kwa mtu asiyefahamika.

“Umefika wakati kwa Rais Kikwete abebe jukumu la kuwafahamisha rasmi Watanzania mmiliki halisi wa Dowans, itakuwa ni miujiza na aibu kwake kulipa fedha hizo kwa mtu asiyejulikana. Watanzania hatujawa wajinga kiasi hicho, kila mara serikali imekuwa ikieleza wazi kutomfahamu mmiliki wa Dowans,� alisema Bw. Fredy Mmassy.

Wananchi hao walihoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa serikali inaheshimu sheria na kwamba ikibidi haina ujanja zaidi ya kulipa mabilioni hayo kwa Dowans.

Rais atueleze na amtaje huyo mtu, vinginevyo Watanzania hatutokubali fedha hiyo ilipwe, na hata ikilipwa kwa nguvu waelewe iko siku tutaidai kwao, alisisitiza Bw. Mmassy.

Wananchi hao walisema mbali na Rais Kikwete kumtaja mmiliki wa kampuni hiyo pia awaeleze Watanzania mwakilishi wa serikali aliyeiwakilisha TANESCO katika mahakama ya ICC.

Walisema imefika wakati wa serikali kuweka wazi mkataba kati yake na kampuni hewa ya Richmond pamoja na ule wa Dowans ili kila kitu kifahamike na Watanzania wajionee wenyewe ni wapi TANESCO inapotiwa hatiani kabla ya fedha hizo kulipwa.

Katika hatua nyingine wananchi hao walimtaka Rais Kikwete kuangalia upya maamuzi ya TANESCO kupandisha bei ya umeme na kuweka wazi kuwa hali hiyo haiendani na maisha yao duni na umasikini uliokithiri.


Tunaomba Rais Kikwete kama kweli anawathamini Watanzania waliomchagua kwa moyo mmoja basi, azuie ongezeko la bei mpya za umeme, viongozi wetu wameonesha wazi kutokuwa na huruma na watu wao, wanakubali kulipa sh. bilioni 185 na kuongeza bei ya umeme,� alisema Bw. Masunga Jilaba, mkazi wa kitongoji cha Ndembezi mjini Shinyanga.

Hawa wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu hawatoi hata chapa moja mifukoni mwao kwa ajili ya kulipia umeme, uchungu wataupata wapi? Ni Watanzania masikini wanaohangaikia hata mlo wao wa siku ndiyo watapaswa kulipa deni hilo la Dowans kupitia ankara za kila mwezi za matumizi ya umeme,� alisema Bw. Jilaba.

Wananchi hao walisema ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 18.5 ni dalili ya wazi kuwa wateja wa TANESCO ndiyo wanaopaswa kuilipa Dowand na kwamba hilo halihitaji mtu kuwa na elimu ya chuo kikuu kufahamu kuwa kampuni hiyo ni ya mfukoni na kuna watu wanafaidika nayo kwa njia moja au nyingine.

Katika hatua nyingine wanachi hao wamehoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, kwamba wananchi watangulize upendo kudai katiba mpya na kumtaka atafute kwanza upendo na huruma kwa Watanzania.

“Najiuliza ni upendo gani anaounzungumzia, yeye anajua upendo tumeumizwa na mengi ikiwemo mikataba mibovu, kama angejua upendo nchi isingeingia katika mkataba wa aibu wa Richmond wakati akiwa madarakani,� alisema Bi. Maliwa.

Alisema Bw. Lowassa anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwanza ili kuonesha upendo badala ya kujifunika shuka nyeupe wakati ndani kuchafu.

Wakati huo huo serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kusitisha mikataba yote na makampuni ya uzalishaji umeme ikiwemo IPTL na Songas ili fedha zinazotumika kulipa capacity charge zitumike kununulia mitambo itakayomilikiwa na serikali.

Umefika wakati wa serikali kukatisha mikataba mibovu inayowakamua Watanzania katika uzalishaji umeme hata kama ni kulipa fidia basi fidia ilipwe ili fedha zinazolipwa kila siku kwa makampuni hayo zielekezwe katika kununua mitambo yetu sisi wenyewe,

Kwa hii Watanzania tutakuwa radhi hata kama nchi itaingia gizani kwa miezi miwili mfululizo ni bora iwe hivyo, na katika kipindi hicho umeme kidogo unaozalishwa na TANESCO yenyewe uelekezwe katika maeneo nyeti tu ya uzalishaji, ili mradi tu baada ya muda mfupi tuwe na mitambo yetu wenyewe,� alisema Bw. Juma Shukuru.
(Chanzo:Gazeti Majira)
Reactions::
Reactions::

Maelfu Wakimbia Ivory Coast


Ouattara anayetambulika kimataifa kuwa mshindi

Umoja wa Mataifa (UN) umesema takriban watu 14,000 wamekimbia kutoka Ivory Coast na kukimbilia nchi jirani ya Liberia, kufuatia mtafaruku unaotokana na uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita.

Msemaji wa umoja huo ameiambia BBC kuwa UN inajiandaa kupokea wakimbizi 30,000 katika eneo hilo.

Wengi wanaokimbia ni wafuasi wa Alassane Ouattara, ambaye anatambulika kimataifa kama mshindi halali wa urais.
Reactions::

Milima Ya Udzungwa!



Njia ya kuelekea Iringa. Niko nyumbani Iringa.
Reactions::

Krismasi Mysore Ilifana!







Wanafunzi wa Kitanzania, Mysore, India.
Reactions::