Subscribe:

Monday, January 31, 2011

Miili Ya Vichanga Kumi Yaokotwa Dar



Miili ya vichanga 10 vilivyokutwa vimetupwa katika jalala kwenye nyumba moja iliyo jirani na makaburi ya Mwananyamala, na wanawake watatu wako mikononi mwa polisi kusaidia uchunguzi wa tukio hili la aina yake ambalo Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Afande Charles Kenyela amethibitisha.

Pia Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Jordan Rugimbana naye amethibitisha tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi ofisini kwake kesho saa sita kamili mchana. Pichani juu ni sehemu ya miili ya vichanga hao ambayo haikuweza kuoneshwa yote kwa sababu za kimaadili


Michuziblog
Reactions::

Nitafika Tu.....


Manispaa ya Morogoro hivi karibuni.
Reactions::

Maandamano Yazidi Nchini Misri


Waandamanaji wamepuuza amri ya serikali

Maelfu ya watu wameendelea na maandamano katika mji mkuu wa Misri, Cairo, huku maandamano hayo yakiingia siku ya saba.

Maelfu ya watu wameendelea na maandamano katika mji mkuu wa Misri, Cairo, huku maandamano hayo yakiingia siku ya saba.

Kundi la kwanza la raia wa Marekani wanasafirishwa leo kutoka Cairo kupelekwa nchini Cyprus, katika mwanzo wa mpango ulioanzishwa na Marekani.

Uchina, Japan na Australia pia zimetuma ndege kuwachukua raia wao huku kukiwa na taarifa kwamba mamia ya raia wa kigeni wamekwama kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Cairo.

New Zealand imesema huenda ikatumia usafiri wa kijeshi kuwahamisha raia wake kutoka Misri.

Nchi nyingi duniani zimewatahadharisha raia wao dhidi ya kusafiri kwenda Misri.
(BBC Swahili)
Reactions::

Balozi Mwanaidi Maajar Afanya Mkutano Wa Kwanz Na Watanzania Waishio Nchini Marekani





1.Mh.Balozi(kati) akisiliza mjadala wa kuchagua kamati itakayounda katiba mpya ya Jumuiya ya Watanzania DMV,kutoka kulia ni Prof.Julius Nyang'oro.Alu Kalala Nyang'oro,Mh.Balozi,Dr.Mkama na Asia Dachi.

4. Mh.Balozi(wa pili toka kulia)kwa pamoja wakipata picha ya ukumbusho na Kanumba(the Great-kulia),Mzee Yusuf Kalala(kati) Aunt Sharifa Kalala na Baba mweye nyumba wake Salma.
Reactions::

FFU Watumika Kusafisha Mji Shinyanga



HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga imeendesha operesheni ‘Safisha Mji’ kwa kumwaga vyakula vya mama lishe, kuzoa viatu madukani na
kukamata baiskeli za wananchi zilizokuwa zimeegeshwa nje ya maduka na masoko vikidaiwa kuwa ni uchafu, ikisaidiwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Mbali ya tukio, pia wakazi wa manispaa hiyo wameshangazwa na kitendo cha kutumika kwa FFU waliokuwa na bunduki, mabomu ya kutoa machozi na simu za upepo (radiocall) mikononi badala ya askari mgambo wa manispaa kama ilivyokawaida na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.
Chanzo:Gazeti Majira)
Reactions::

Visura Waanza Kambi Mwanza.



1.Pichani kati Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania (BTA), Juliana Urio,akizumgumza na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusina kuanza kambi wa warembo wa shindano la Kisura wa Tanzania 20110.kushoto ni Meneja masoko wa SBC,Bwa.George Michael,Afisa Mipango Ujana wa FHI Bwa.Aziz Itaka,Mwisho kabisa ni Meneja Masoko wa ATCL,Bwa. Musyangi Kajeri

2.WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini mapmea jana katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.


WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini mapmea jana katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.

Mchakato wa kuwapata wasichana
hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.

Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),

Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).

Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records
Reactions::

Magufuli Atembelea Mradi Wa Ujenzi Wa Babarabara Ya Jet Lumo




1. Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli akionyesha orodha ya majina ya watu watakaolipwa babada ya kuvunjiwanyumba zao kupisha ujenzi wabarabara ya jet Lumo wilayani Temeke

2.Baadhi ya wananchi wa eneo la jet-lumo wilaya ya temeke wakimsikiliza Dr.

3.Eneo la ujenzi wa barabara ya jet lumo.



(Picha:Mwanakombo Juma)
Reactions::

Neno La Leo: Dowans; Kuku Anayekimbia Na Panzi Mdomoni!



Ndugu Zangu,


HUTOKEA, kuku akimdaka panzi mdomoni, basi, ukimwandama ukimpigia kelele. Kuku huyo atakimbia na panzi wake mdomoni . Mara ile atakapoona umesitisha kumfukuza , na kelele pia. Basi, kuku huyo, taratibu ataanza kumla panzi wake.



Lakini, kama utaendelea kumwandama na kumpigia kelele, hutokea, kwa kuku anayekimbia na panzi mdomoni, kumtema panzi ili kuandamwa huko kwishe.


Dowans ni kama kuku na panzi wake mdomoni. Alishamdaka, kabla hajaanza kumla, Watanzania tumeamka na kuanza kumwandama Dowans huku tukimpigia kelele.



Kuku Dowans ameonyesha dalili za kuweweseka. Tukiongeza kupiga kelele, basi, upo uwezekano wa Dowans kumtema panzi.


Naam. Tuendelee tu kupiga kelele za ’ HATULIPI!, HATULIPI! ’- NON SI PAGA! Kwa Kiitalia. Yumkini panzi aliyemdomoni mwa Dowans anaweza kutemwa! Itakuwa nafuu kwetu. Na Hilo Ni Neno La Leo.



Maggid
Iringa,
Jumatatu, Januari 31, 2011
mjengwa
Reactions::

Lady Jay Dee Europa Tour ( RATIBA)



These are the booked dates for Lady JAY DEE”s european Tour

1. 21/04 BERGEN NORWAY ( CHIKU ALLY )
2. 22/04 OSLO NORWAY ( HASSAN NGANZO )
3. 23/04 AMSTERDAM HOLLAND ( EDDIE BUKENYA )
4. 24/04 ESSEN GERMAN ( NASHE MVUNGI )
5. 29/04 ZURICH SWISS (Dalla Silk )
6. 30/04 STOCKHOLM SWEDEN ( FREDY NICE )
She’s only doing two weekends. NO MORE BOOKINGS NEEDED.



Hassan Ngazo.
Reactions::

Sunday, January 30, 2011

Vipanya Vingine Vichokozi!

Reactions::

Dunia Ya Waarabu I-Karibu Nasi!



Ndugu Zangu,

MOTO unazidi kuwaka Cairo, unasambaa pia. Tumeona picha za askari wale vijana wakitabasamu na kupeana mikono na wananchi. Ni ukweli, wengi wa wanajeshi hao wamekuwa recruited ( kuingizwa jeshini) wakitokea kwenye familia za kimasikini.
Kwa wanajeshi hawa, wana uelewa mkubwa wa wanachokipigania watu wa Misri. Ni suala la wakati tu kabla wanajeshi kuchukua uamuzi wa jumla wa kusimama upande wa umma. Na hilo likitokea, basi, mwisho wa zama za Hosni Mubarak utakuwa umeharakishwa, kwa nguvu ya umma ukisaidiwa na jeshi.
Maana, hata Hosni Mubarak akifanikiwa kuning’inia madarakani, bado, siku zake zitakuwa zikihesabika. Hosni Mubarak hana support ya umma, hivyo basi, hana uhalali wa kuendelea kuongoza dola kubwa na kongwe ya Egypt.
Watawala Afrika wana cha kujifunza?
Katika Afrika, mtawala atakayepuuzia moto unaowaka katika Dunia ya Waarabu ama ni mgonjwa au ni mjinga tu . Ni ukweli, kuwa Dunia ya Waarabu i-karibu nasi sana. Ni mwendo wa saa tano tu kwa ndege kutoka Dar es Salaam, Nairobi au Kampala kabla ya kutua Egypt, Tunisia, Yemen au Algeria. Ndio, ni umbali mfupi sana kabla ya aliye kwenye ndege kuanza kuuona moshi wa moto unaotokana na moto uliowashwa na umma unaotaka mabadiliko.
Ni dhahiri, kuwa yanayotokea kwenye Dunia ya Waarabu yana athari kubwa kwa ‘ Dunia Ya Waafrika’. Kihistoria na Kiutamaduni, Waafrika tuna mengi yanayotufanya tuwe karibu na Waarabu. Yaliyokuwa yakitokea Ulaya Mashariki miaka ile ya 80, ingawa yalisaidia kuleta mabadiliko pia barani Afrika, lakini, bado, yalitokea mbali na Afrika.
Lakini, harakati za vijana wa Kiarabu kuleta mabadiliko na hata kufanikiwa katika harakati zao, yana kila uwezekano wa kuwatia hamasa vijana wa Kiafrika katika nchi zao. Ikumbukwe, mengi wanayopigania vijana wa Kiarabu yanafanana na ya wenzao wa Afrika. Inahusu ukandamizaji, mgawanyo wa rasilimali wa haki na kukua kwa demokrasia ili kuchangie ustawi wa mataifa yao. Kupelekee kupata ajira na kuongeza vipato vyao. Kwa vijana hawa, kukua kwa uchumi wa nchi zao hakuna maana kama hali za watu wa kawaida zinakuwa ngumu kila kukicha na huku pengo la walio na wasio nacho likikua kwa kasi ya kutisha.
Kwa viongozi Afrika busara ni mapema kupunguza nywele zao kabla ya kulazimishwa kutia maji na kunyolewa vipara! Inahusu mabadiliko makubwa ya Katiba za nchi zetu ambazo bado zina ukakasi wa enzi za ‘ Chama Kushika Hatamu Zote’. Dunia Imebadilika.
Maggid
Iringa,
Jumapili, Januari 30, 2011
Reactions::

Maandamano Yaendelea Misri





Maandamano dhidi ya serikali, yameendelea kwa siku ya tano mfululizo mjini Cairo.Amri ya kutotoka nje ilitangazwa jana usiku katika miji ya Cairo, Alexandria na Suez, baada ya mapambano makali baina ya polisi na waandamanaji

Hata hivyo, maandamano yameendelea, na jeshi linashika zamu barabarani.

Waandamanaji hasa wamekuwa wakipiga kelele kuwa serikali sio halali, na pia rais Mubarak.

Ni wazi kuwa ahadi aliyotoa rais, kubadili baraza lake la mawaziri na kuleta mabadiliko, hayatoshelezi wananchi.

Wanataraji kuwa, wanaweza kumtoa kiongozi, kama ilivyotokea Tunisia.

Wengi wanasema, baada ya kuishi chini ya sheria ya dharura, inayozuia mkusanyiko wa watu hadharani, sasa wamepata moyo kumiminika barabarani, kutokana na yale yaliyotokea Tunisia.

Watu hawakupata kuonesha nguvu kama hii.

Rais Mubarak amehakikisha kuwa mataifa rafiki ya magharibi yaone kuwa tishio linatoka kwa kundi kubwa la upinzani, la Muslim Brotherhood.

Chama hicho kimepigwa marufuku, na awali kililaumiwa kwa makosa, kuwa kilihusika na maandamano.

Wanaharakati wa kisiasa, wanataka watu wapya wasiohusika na serikali, waruhusiwe kuwania uongozi.

Mohammed El Baradei, aliyewahi kuwa mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Atomiki, ametokeza kuwa kiongozi maarufu wa upinzani.

Lakini wengine wanamtaka Katibu Mkuu wa Jumuiya Nchi za Kiarabu, Jenerali Amr Moussa.
BBC Swahili.
Reactions::

Yahusu Matokeo Ya Kidato Cha Nne Shule Za Kata

Reactions::

Rafiki Zangu Hawa.............


..........Tulisoma wote darasa moja Shule ya msingi.

Mdau wa Mjengwablog, Victor Makinda(Katikati) akiwa na rafiki zake Richard (kushoto) na Mendrad (Kulia) Kijijini Ichonde Wilayani kilombero hivi karibuni.
Reactions::

Mazishi Ya Mwalimu Mzee



Familia ya Mbaruku Mzee wa Reading-United Kingdom na Mzee Mwalimu wa London (UK), wanasikitika kuwatangazia msiba wa Baba yao mzazi Mwalimu Mzee
kilichotokea tarehe 28/01/2011 -Tanzania.
Marehemu ni baba : Mbaruku na Mzee wakazi wa Reading UK
Habari za msiba huu ziwafikie watanzania wote waishio Reading na sehemu zingine za UK na ndugu wote, jamaa na marafiki popote walipo.Mfiwa anatakiwa kusafiri na kama ilivyo desturi yetu ,basi fikisha mchango wako ili aweze kusafiri.
Mazishi yatafanyika Kesho TAREHE 30/01/2011 - Saa Saba Mchana - Huko nyumbani kwake MBAGALA - DAR ES SALAAM, TANZANIA
TEL: +44 7799435327 - UK
+255716826127 - Tanzania
ADDRESS: 2 Appleshaw Court , School Rd ,READING. RG31 5AL
Reactions::

Wafanyakazi UN Wamuaga Mwenzao Omary Mjenga







Wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Wamuaga mwenzao Ndugu Omary Mjenga, ambaye ameteuliwa kuwa Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi na Huduma- UNOPS, FreeTown, Sierra Leone
Reactions::

IBADA READING

KARIBUNI NYOTE KWENYE IBADA YA KUWAFARIJI WAFIWA

FAMILIA YA MUBARUKU MZEE WA READING INACHUKUA FURSA YA KUWAKARIBISHA WATANZANIA POPOTE PALE LEO JIONI KUANZIA SAA KUMI NA MOJA NA NUSU ,KWENYE IBADA FUPI YA KUWAFARIJI WAFIWA ,MUBARUKU MZAZI WAKE MAUTI ILIMKUTA SIKU YA IJUMAA, HUDUMA YA IBADA ITAFANYWA KWENYE ADDRESS IFUATAYO
ADDRESS: 2 Appleshaw Court , School Rd ,READING. RG31 5AL
TEL: +44 7799435327 - UK

--


Director Of Communication
CCM Branch -Reading ,
Berkshire .
United Kingdom
Reactions::

Saturday, January 29, 2011

Balozi Mwanaidi Maajar Awaalika Friends Of Tanzani Ubalozini Washington






1.Mh.Balozi wa Tanzania nchin Marekani Hon.Mwanaidi Sinare Maajar alipokua akiongea na kuwapongeza Friends of Tanzania kwa kazi yao nzuri ya kujitolea na kuijali Tanzania na kuwaasa wasichoke waendelee na moyo huo.

2.Mh.Balozi Mwanaidi Maajar(kushoto) akizungumuza mawili matatu na Ed Kneedler(kati) na Lynn Kneedler Friends of Tanzania.

3.Mh.Balozi wakipata picha ya pamoja na Emmanuel Muganda

4.Kutoka kulia ni Emmanuel Muganda,Afisa Ubalozi Masanja,Denns Warner,John Hatch,Afisa Ubalozi Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi Asia Dachi,Shante na Candy Warner.
Reactions::

UVCCM Iringa Yawapongeza Wanafunzi Walifaulu Vizuri




1.Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa mjini Ibrahim Ngwada akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Ipogolo baada ya kutembelea shule hiyo leo kukabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi waliofanya vizuri mwaka jana,UVCCM ipo katika maandalizi ya sherehe ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika Feb.5 mwaka huu

2. Viongozi wa UV CCM wakisalimia wanafunzi wa shule ya msingi Mtwivila mjini
Iringa.
(Francisgodwin)
Reactions::
Reactions::

Mgambo v/s Muuza Madafu


Mgambo wa Manspaa ya Ilala wakiwa wamemkamata muuza madafu aliyekuwa akifanya biashara kinyume na taratibu barabara ya Msimbazi jijini Dar es salaam. (Picha:Burudanblog)
Reactions::

Tamko

Utangulizi

Oktoba 31, 2010 Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu ambapo wananchi walipata fursa ya kumchagua Rais, wabunge pamoja na madiwani. Katika uchaguzi huo, Watanzania kwa ujumla wao walikichagua Chama cha Mapinduzi, CCM, kuongoza tena nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Hata hivyo, wakati wananchi wakiamini kwamba wanaongozwa na watu waliowapigia kura, matukio yanayoendelea hivi sasa yanaashiria serikali kutelekeza majukumu yake na kuwaacha maaskofu wakielekeza nchi wanakotaka.

Itakumbukwa kwamba awali kabla ya uchaguzi mkuu maaskofu walikuwa wametoa Ilani yao ya uchaguzi bila kueleza kipi chama chao kitakachosimamia na kutekeleza Ilani hiyo. Baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala, CCM, walishabikia Ilani hiyo na kuwatetea maaskofu. Kwa hakika taarifa za vyombo vya habari zilifahamisha kwamba baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya serikali walishiriki katika kuandaa Ilani hiyo.

Ilipofika wakati wa kampeni hadi kuingia siku ya kupiga kura, ilikuwa imedhihiri kipi kilikuwa chama cha maaskofu ambacho walitarajia kitekeleze Ilani yao. Haikuwa tena jambo la siri kwani walisimama wazi wazi kuwaelekeza waumini wao wampigie nani kura. Na katika juhudi zao za kutaka wafuasi wao wawaelewe vizuri, maaskofu walithubutu hata kuweka kando mafundisho ya Biblia yao juu ya masuala ya uzinzi wakawahimiza waumini kumpigia kura mtu wanayemtaka bila kujali kwamba anakabiliwa na kashfa ya kupora mke wa mtu. Waliwaambia wasihangaike na maisha binafsi ya ndoa ya mgombea.

Hata hivyo, matokeo ya kura yalitoa majibu kwamba Watanzania walikuwa wameikataa Ilani ya Maaskofu.

Waislamu tumelazimika kukutana na kutoa tamko hili kwa sababu matukio yanayotokea hivi sasa yanaonesha kuwa wale ambao Watanzania walikataa kuwapa uongozi na Ilani yao iliyoandaliwa na maaskofu, ndio sasa wanaielekeza nchi pa kwenda huku viongozi wa CCM na serikali wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kunyenyekea kwa maaskofu hao.

Tumeona na tumemsikia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda akihangaika kuwapigia magoti na kuwaomba radhi maaskofu kule Sumbawanga. Tumesikia jinsi viongozi wanaojaribu kuwaambia maaskofu kwamba kama wanataka kuingia katika siasa wavue majoho na vyeo vyao vya kikanisa kama Padiri mwenzao waliyekuwa wakimpigania kuingia Ikulu, wanavyokemewa na kutakiwa wawaombe radhi maaskofu hao.


Lililo baya zaidi maaskofu walioshindwa kuwashawishi wananchi waipokee na kukubali Ilani yao, wamekuja na kampeni za kuchochea uasi kwa serikali iliyopo madarakani. Lakini pamoja na hali hiyo, viongozi wa CCM na serikali wamebaki wanagwaya. Hakuna aliyeweza kupata ujasiri wa kukemea hali hii. Kinyume chake Waziri Mkuu na Mzee John Samwel Malecela wanahangaika huku na kule wakiwapigia magoti maaskofu hao na kuwakemea wanaothubutu kuwakosoa.

Hali kama hii ni hatari kwa usalama na utulivu wa nchi. Ni hali ya kuchochea udini na kuweka ombwe la uongozi wa kisiasa ambao utazua balaa. Waislamu hatuwezi kukubali hali hii. Kwa hiyo, ama CCM na serikali vitekeleze wajibu wao wa kuongoza au kama wanaona hawawezi, basi waseme rasmi ili Maaskofu na wengine wenye Ilani zao za uchaguzi waingie tena ulingoni kuomba ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi kuliko kuishi katika hiki kiini macho ambapo maaskofu na mawakala wao ndani ya serikali wameachwa waikokote nchi wanakotaka.

Kiini cha Hali hii ya Kisiasa

Hali hii ya kisiasa tunayoishuhudia leo nchini mwetu ni matunda ya mbegu liliyopandwa na kupaliliwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Wakoloni walikuwa na kanuni yao waliyoiita divide et impero yaani wagawe ili uwatawale. Huko Rwanda wakoloni waliwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila. Watusi ambao ni watawala wapewe elimu ya juu na wafundishwe kwa Kifaransa, na Wahutu ambao ni watawaliwa wapewe elimu duni na wafundishwe kwa Kiswahili. Ubaguzi huo wa kuwagawa raia wa nchi moja ulipandikiza sumu iliyokuja kusababisha Wanyarwanda kuuana.

Hapa kwetu wakoloni walitugawa kwa misingi ya dini. Kabla ya uhuru wa Tanganyika, wakoloni kwa kushirikiana na makanisa waliwaona Waislamu kama ni mahasimu wao kidini na kisiasa. Na kwa sababu hiyo serikali za kikoloni zikaweka mikakati maalum ya kuwakandamiza Waislamu katika maeneo matatu: kwanza kuwawekea vikwazo katika kutangaza dini yao ili wasiongezeke; pili kuwabana katika elimu na ili kuhakikisha kuwa Waislamu wanabanwa, jukumu la kuwaelimisha Waafrika likawekwa mikononi mwa makanisa na kazi ya serikali ni kuzigharimia tu shule hizo. Lengo likiwa ni kuwabatiza Waislamu wachache watakaoruhusiwa kusoma, na tatu kuwabana katika ajira serikalini kwa sababu makanisa yote yalisisitiza kuwa kuwaajiri Waislamu serikalini ni kusaidia kuenea kwa Uislamu..

Kwa kuwa ubaguzi huo haukuwa na kificho chochote, Waislamu wengi walijitokeza kupambana na ukoloni kwa matarajio kuwa serikali huru itaondosha chuki na uadui huo dhidi ya Waislamu. Lakini msiba mkuu wa taifa hili ni kwamba kinyume chake, baada ya uhuru msimamo ukawa ni ule ule wa kuwaona Waislamu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na mikakati ya kuwabana Waislamu katika maeneo yale matatu ikaimarishwa zaidi wakati wa utawala wa Nyerere. Kuanzia 1957 mkakati uliopangwa na Kanisa Katoliki ukawa ni kuhakikisha kuwa nafasi zote muhimu za uongozi na serikali zinashikwa na wao. [Taz. Confidential Diary – Tanganyika, March-April 1957, uk. 3-4 Maryknoll Central Archives, New York ]. Na ni mkakati huu ndio ambao Mwalimu Nyerere aliokuwa akimhakikishia Askofu Rweyemamu mwaka 1970 kuwa anatumia mamlaka yake kama Rais na kama kiongozi wa TANU kuhakikisha kuwa anatoa upendeleo maalum kwa Wakristo ili wasimamie sera za Chama. Na kwamba amemteua padiri katika nafasi nyeti ya Chama si kwa sababu anajua siasa bali kwa sababu ni Mkristo safi. Lakini Nyerere huyo huyo akisimama hadharani alijidai kukemea udini. Na kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuliimarisha kanisa na kuwadhoofisha Waislamu, leo Kanisa lake limo katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni Mtakatifu!

Dr. Sivalon anaarifu katika kitabu chake kuwa mara baada ya uhuru Kanisa katoliki liliwahamasisha Wakristo wote na hasa watendaji wa serikali juu ya hatari ya Ukomunisti na Uislamu na walikusanya nguvu zao zote katika kukabiliana na maadui hao.

Matokeo ya Hujuma Hizo

Matokeo ya hujuma hizo za kichinichini ni kwamba katika sura ya nje na katika propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na kisiwa cha amani. Lakini uhalisia wa mambo ni kuwa Tanzania ni nchi yenye jamii kubwa mbili. Jamii ya Wakristo wanaopewa msaada, upendeleo, ulinzi na heshima, na jamii ya Waislamu ambao wanachukiwa, kudharauliwa na kudhoofishwa na serikali kabla na baada ya Uhuru. Ifuatayo ni mifano michache tu ya baadhi ya hujuma hizo baada ya Uhuru.

(1) Mwaka 1963 katika Barua ya Kichungaji, Kanisa Katoliki lilisema Waislamu walikuwa wanajenga umoja na mshikamano miongoni mwao, jambo ambalo ni “hatari kubwa kwa hatima ya Wakristo wetu” na Sivalon anabainisha kuwa Wakristo walimwomba Nyerere awasaidie kuvuruga umoja huo wa Waislamu. Ndio sababu ya Nyerere kutumia dola kuiparaganya EAMWS. Kwa kuwa Waislamu ni jamii inayotakiwa kuwa dhalili, hawatakiwi kuwa na umoja. Ndio maana tangu wakati wa Nyerere hadi leo, uchaguzi wa viongozi wa Waislamu husimamiwa na vyombo vya dola. Nia ikiwa ni kutokuwapa Waislamu uhuru wa kuwachagua viongozi wao. Katika taifa moja haki hiyo ni ya Wakristo peke yao. Sote ni mashahidi kuwa mwaka 1994 serikali ilimwagiza Naibu Waziri Mkuu Mh. Augustino L. Mrema kuhakikisha kuwa Bakwata inapitisha katiba mpya inayotakiwa na serikali. Na Maaskofu wakachangia gharama. Waislamu ni maadui kidini na kisiasa, lazima wadhibitiwe.

(2) Mwaka 1992 Serikali ya Tanzania ilitiliana saini Makubaliano ya Itifaki rasmi na Makanisa ya TEC na CCT. Kwa mujibu wa makubaliano hayo ambayo yalitiwa saini na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye wakati huo alikuwa Mh. Edward Lowasa serikali imewajibishwa pamoja na mambo mengine, kutenga nafasi za masomo kwenye vyuo vyake vya Ualimu mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wanaopangwa kufundisha katika shule za Kanisa; pia kutoa ruzuku ya kuendeshea taasisi za Makanisa. Kuanzia 1992 hadi leo serikali imetoa mabilioni ya kodi za wananchi kwa Makanisa. Katika kipindi chote hicho Waislamu wamepinga ubaguzi huo. Lakini kwa kuwa lengo ni kuwaimarisha Wakristo ambao ni jamii inayotakiwa kupewa nguvu zaidi dhidi ya jamii ya Waislamu ambao wanatizamwa kama maadui, serikali imeyapuuza malalamiko ya Waislamu. Lakini propaganda zinaendelea kuwa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na ni kisiwa cha amani.

(3) Waislamu wameiomba serikali kujiunga na OIC kama njia mojawapo itakayowezesha nchi yetu kupata misaada itakayotumika kuinua hali za Waislamu ambao wameachwa nyuma sana katika elimu na uchumi. Makanisa yote kwa kauli moja yamepinga kwa nguvu zao zote pendekezo hilo. Sababu ya kupinga kwao ni kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanadhoofishwa katika kila hali, na ni makosa makubwa kuwaimarisha kiuchumi au kielimu maadui hao. Serikali ilipofanya utafiti wake wa kina ikajiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote. Na Mh. Bernard Membe alitamka hilo Bungeni. Mara akaitwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Cardinali Pengo na kukumbushwa mkakati wa kuwadhoofisha Waislamu. Msimamo wa serikali ukabadilika. Lakini propaganda za kuwazuga Waislamu zinasema Watanzania wote ni kitu kimoja na nchi hii haina ubaguzi!

(4) Kwa kuwa tangu wakati wa ukoloni hadi leo mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanaminywa kadiri iwezekanavyo katika nafasi za uongozi na ajira, ndio maana hadi leo, miaka 50 baada ya Uhuru Waislamu ni wachache sana katika nafasi zote za uongozi na ajira katika sehemu muhimu serikalini na katika vyombo muhimu vya maamuzi. Kisingizio kinachotolewa ni kuwa Waislamu hawataki kusoma. Lakini ukitazama orodha ya Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa na sifa zao, utaona dhahiri kuwa wapo Waislamu wengi wenye sifa bora zaidi ambao wangestahili kuwa ma-DC. Waislamu hawateuliwi kwa sababu mkakati uliopo ni kuwatenga Waislamu na ikiwezekana kuwaondosha kabisa katika sehemu muhimu za uongozi, kwa sababu kama wao hawajui ukweli ni kwamba hawatakiwi kushika nafasi zozote muhimu za uongozi au ajira. Ndio maana asilimia 75 ya Ma-DC wote ni Wakristo na karibu wasimamizi wote wa Uchaguzi katika wilaya ni Wakristo. Wabunge asilimia 75 pia ni Wakristo, na hali ni hiyo hiyo katika Vitengo vya serikali na Mashirika ya umma. Ndio maana hakuonekani tatizo lolote pale taasisi yote inapokuwa na Wakristo watupu. Na kelele nyingi maadui wa serikali na Kanisa wanapopewa nafasi hata kama wana uwezo kiasi gani. Katika sura ya nje Tanzania ni taifa moja, katika uhalisia wake ni kuna mataifa mawili, moja nyonge na jingine lenye nguvu.

(5) Kwa kuwa Waislamu wanahesabiwa kuwa ni maadui, ule mkakati uliowekwa na wakoloni wa kuwawekea vikwazo Waislamu katika kutangaza dini yao unaendelea hadi leo. Ipo mifano mingi sana ya Waislamu kukamatwa, kutiwa ndani na kunyanyaswa na vyombo vya dola kwa sababu tu ya kulingania hadharani dini yao. Kwa kuwa Waislamu ni maadui, basi ni muhimu kuhakikisha kuwa hawaongezeki. Wakristo wanayo haki ya kuitisha mkutano wa hadhara na kutangaza kuwa Yesu ni Mungu. Wao ni jamii inayostahiki ulinzi wa dola. Lakini pindi Mwislamu atakaposema hadharani kuwa Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi siyo Yesu mwana wa Mariamu atakuwa amekashifu dini ya dola na atakamatwa na kubughudhiwa. Lakini kipropaganda, Tanzania ni nchi moja na inafuata katiba moja. Lakini uhalisia ni tofauti.

(6) Msimamo wa serikali na makanisa kuhusiana na mauaji ya Waislamu katika msikiti wa Mwembechai ni kielelezo kingine cha ukweli kuwa Tanzania ni mkusanyiko wa jamii mbili zenye haki na hadhi tofauti katika taifa moja. Kwa kushinikizwa na Maaskofu serikali iliwauwa Waislamu watatu Mwembechai pasi na hatia yoyote. Waislamu waliiomba Mahakama, Bunge na hata Rais aunde Tume ya uchunguzi. Mihimili yote ya dola ilikataa. Kiongozi wa Kanisa Katoliki akenda mbali zaidi. Akahalalisha mauaji hayo. Kwa sababu waliouliwa ni wale maadui kutoka ile jamii nyoge isiyotakiwa kustawi. Lakini alipouliwa mbwa “Imigresheni” mwaka huo huo wa 1998, Jaji Mkuu wa wakati huo Mh. Francis Nyalali aliamuru uchunguzi wa kuuliwa mbwa huyo na hakimu akaadhibiwa. Jaji Mkuu alichukua uamuzi huo bila kuombwa na mtu. Lakini wale waliowauwa Waislamu walipongezwa na kupandishwa vyeo. Uhasama wa serikali na makanisa dhidi ya jamii ya Waislamu ni wa kiwango cha kutisha. Msimamo ukawa huo huo walipouliwa Waislamu Unguja na Pemba 2001 kwa kuandamana kudai Katiba Mpya. Lakini kipropaganda tunaambiwa Watanzania wote wanahaki sawa.

(7) Rais wa Marekani George W. Bush alipotangaza Vita vya Msalaba dhidi ya Waislamu mwaka 2001, serikali ya Tanzania ikapata uhalali zaidi wa kuzidi kuwakandamiza Waislamu. Serikali ikawa radhi kuvunja Katiba ya nchi kwa kupitisha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2002 ili zipatikane fursa zaidi za kuwanyoongesha Waislamu. Waislamu waliipinga sheria hiyo kwa nguvu zao zote, lakini kwa kuwa wao ni jamii inayotakiwa kupigwa vita hawakusikilizwa. Bunge ambalo nalo lina Wakristo wengi likaipitisha haraka sheria hiyo. Naam, tangu imepitishwa hadi leo, sheria hiyo imetumika kuwadhuru Waislamu wasiokuwa na hatia yoyote, na kufunga taasisi zilizokuwa zikiwasaidia Waislamu. Misaada ni haki ya Wakristo, siyo Waislamu. Pamoja na madhila yote hayo Waislamu wanatakiwa waendelee kuamini kuwa Tanzania ni nchi moja inayojali raia wake wote.

(8) Wakati serikali ikidai kuwa Tanzania ni taifa ambalo raia wote wana haki sawa, lakini serikali hiyo hiyo kwa makusudi kabisa inafanya jitihada za waziwazi za kuwahamasisha Wakristo wawaone Watanzania ambao ni Waislamu kuwa ni maadui zao na maadui wa taifa lao. Januari 2001 Waziri Mkuu Mh. Frederick Sumaye alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa serikali inazo taarifa kuwa kundi la magaidi waliopata mafunzo nchi za nje limerejea nchini na magaidi hao wanapanga kuilipua hospitali ya Muhimbili. Kufuatia kauli hiyo wafanyakazi watatu wa Muhimbili ambao ni Waislamu akiwemo Profesa wa Micro-Biology walitiwa mbaroni. Japo baadaye waliachiwa kwani hawakuwa na hatia yoyote, lengo la serikali la kupandikiza sumu ya chuki lilikuwa limetimia. Tarehe 24 Agosti 2001 Waislamu walifanya maandamano kupinga kufungwa kwa Dibagula kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali kupitia jeshi la polisi likawatangazia wananchi wote kuwa Waislamu wamepanga kuyalipua makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba 2001. Na serikali ikawahakikishia Wakristo kuwa itaweka maaskari wa kuwalinda na hiyo shari ya Waislamu. Lengo la uzushi huu ni kuwachochea Wakristo wawachukie Waislamu na hivyo waunge mkono hatua za serikali za kuwapa kipondo. Hivi sasa huo umekuwa ni mchezo wa kawaida. Kila baada ya muda fulani serikali kwa kpitia jeshi la polisi hutoa taarifa za kuonesha kuwa kuna mpango wa shambulio la kigaidi. Na watuhumiwa siku zote ni Waislamu. Serikali na makanisa yanawachukia Waislamu kiasi cha kuwa tayari kushirikiana na wasiokuwa Watanzania katika kuwahujumu Waislamu. Ni dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, Maaskofu wakipata kisingizio chochote watakuwa tayari kuwauwa Waislamu kama walivyoshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda.

(9) Papa John Paul II alipoitembelea Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki lilimkabidhi Ripoti yenye anwani: Activities of the Church in Tanzania. Katika ripoti yake hiyo Kanisa Katoliki limetaja kuwapo kwa Tume ya Majeshi ya Kivita [ Commission of Armed Forces ] ndani ya Kanisa hilo. Tangu wakati huo hadi leo Waislamu wameitaka serikali iwaondoshe hofu kwa kuweka wazi kazi za Tume hiyo ya Majeshi ya Kivita ndani ya Kanisa. Serikali haijajibu na wala haijashughulisha na taarifa nzito kama hizo. Hatujui kama Tume hiyo ya Majeshi ya kivita inafanya kazi ndani ya Jeshi la Wananchi au nje ya jeshi hilo. Lakini kwa muktadha wa hali ya uhasama wa serikali na hasa wa Maaskofu dhidi ya Waislamu wanaowahesabu kuwa ni maadui zao, si vigumu kukisia kwa nini Kanisa Katoliki limeunda Tume ya Majeshi ya Kivita. Lakini serikali ambayo haishughulishwi kabisa na Tume ya Majeshi ya Kivita ya Wakatoliki imekuwa na tabia ya kuwakamata na kuwatia ndani Waislamu kwa kesi za kuwabambikia zisizokuwa na kichwa wala miguu. Lakini propaganda zinasema Tanzania ni nchi moja yenye katiba inayolinda haki za watu wote. Mwenye macho haambiwi tazama.

Dalili ya Mvua ni Mawingu

Alipokuwa akitoa mada yake juu ya “Mifumo ya Viashiria vya Migogoro” katika Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ulioandaliwa na REDET mwaka 2003, Mh. Bernard L. Membe alisema kwamba migogoro mingi duniani na hasa vita vya wenyewe kwa wenyewe vina dalili na viashiria vyake. Akasema miongoni mwa dalili kubwa kuwa nchi karibu itaingia katika machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kutokea kwa mgawanyiko au kutokea kutoelewana kwa viongozi ndani ya chama au serikali tawala.

Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri wakipingana hadharani juu ya maamuzi waliyoyafanya wenyewe. Lakini pia katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia pia mgongano wa waziwazi kati ya wabunge wa CCM na Chama chao. Na wote hao hawachoki kujisifu kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere. Lakini mwaka 1993, Nyerere katika Kitabu chake Tanzania! Tanzania! Aliandika na tunanukuu:

Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hoja ya hadhi ya Bunge. Ni nani huyu anayefanya kazi hii? Ni haki kabisa ya vyama vya upinzani kujaribu kugombanisha Wabunge wa chama kinachotawala na chama chao. Lakini viongozi wa chama kinachotawala pamoja na Serikali yenyewe wanapojaribu kufanya mambo ambayo yatagombanisha Wabunge wa CCM na chama chao, tuna haki ya kuwauliza viongozi hao wanafanya kazi hii kwa niaba ya nani, na chama chao ni chama gani? [uk. 41]

Pamoja na kuyajua yote hayo hivi sasa kuna msuguano ulio dhahiri kabisa baina ya Wabunge wa CCM na Chama chao.

Kiashiria kingine alichokitaja Mh. Membe ni kwa serikali kushindwa kuyashughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi yanayoelekezwa serikalini.

Maazimio ya Waislamu

Kwa kuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ilipofikia hivi sasa, Waislamu tumefikia maamuzi yafuatayo:

(1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa mfano wa kuigwa.

Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana kama Waislamu.

(2) Kwa kuwa kila wanachosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia.

(3) Kwa kuwa tangu ukoloni hadi leo Waislamu wanahesabiwa na serikali na Maaskofu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na wasiostahiki haki sawa na wengine, na kwa kuwa Waislamu wameazimia kutokukubali tena kudhulumiwa na kuonewa kwa namna yoyote ile iwayo, ni wazi kuwa hakuwezi kuwa na katiba itakayoweza kulinda haki za madhalimu na wadhulumiwa kwa wakati mmoja. Ingawa kwa propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja, lakini kiuhalisia ni nchi yenye jamii mbili zenye hadhi na haki tofauti kabisa. Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi. Mwalimu Nyerere alipigania kwa nguvu zake zote Nigeria igawanywe ili Wakatoliki ambao walikuwa wanadhulumiwa Nigeria wajitenge na waruhusiwe kuishi katika nchi ya Biafra. Na katika kijitabu alichokiandika 1966 Nyerere alisema madai ya kuhifadhi umoja wa kitaifa wa Nigeria hayana maana yoyote pale ambapo baadhi ya raia wa taifa hilo wanadhulumiwa. Ushahidi wa dhulma za Waislamu upo wazi. Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC bila ya kuwakera Maaskofu. Ni wajibu wetu kulifikisha hili kwa Waislamu wenzetu nchi nzima ili lijadiliwe zaidi kabla halijafikishwa rasmi

(4) Kwa kuwa hakuwezi kuwa na amani ya kweli bila ya haki, na kwa kuwa amani ya Tanzania inashikiliwa na Waislamu walioruhusu dhulma hiyo, Waislamu tunayo dhima kubwa kwa kustawi kwa Mfumo Kristo ambao sasa hapana shaka yoyote unalisambaratisha Taifa. Lakini kama alivyosema Nyerere, anayedhulumiwa ni mtu anayeteseka. Asipopambana na huyo dhalimu, yeye ataendelea kuteseka wakati dhalimu anastarehe kwa amani. Akiamua kupambana, wote yeye na dhalimu watateseka. Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.

WABILLAHI TAWFIQ

Reactions::

Magufuli Atembelewa Na Balozi Wa Umoja Wa Ulaya




1.Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli akizungmza na Balozi wa Umoja wa Ulaya(European Union)Tim Clarke(kushoto) alipomtembelea waziri Magufuli Ofisini Kwake Jijini Dar es Salaam na kuzungumza mambo mbalimbali ya miradi ya barabara inayoghramiwa na jumuiya ya Ulaya(EU)husuni maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mandela

2. Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli akizungumza na Balozi wa israel kwa nchi za afrika mashariki ambaye pia ofisi yake ipo nchini nairobi Jacob Keidar(kushoto)alpomtembelea Waziri Magufuli OFisini Kwake Jijini Dar es Salam na kuzungumza maswala mbalimbali hususani israel kujenga nyumba za bei nafuu nchin Tanzania kwa gharama nafuu kwa wafanya kazi wa serikali pamoja na Taasisi.Picha na Kitengo Cha Habari na Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi
Reactions::

Tume Ya Kudhibiti Dawa Za Kulevya Yakabidhi Vifaa Kwa Asasi Ya Happy Root


Tume katika majukumu yake kisheria ni kuziwezesha Asasi zinazojihusisha na kupunguza matumizi kwa waathirika wa dawa za kulevya.

Asasi ya Happy Roots, ni asasi ambayo tumekuwa tukifanya nayo kazi kwa muda mrefu sasa, Happy Roots inafanya kazi kitaifa na ina tawi lake Geita mkoani Mwanza na makao makuu yake yapo Mbezi Beach wilaya ya Kinondoni hapa Dar es salaam.

Happy Roots wanafanya kazi kwa kuzunguka maeneo mbalimbali hasa mashuleni ili kuelimisha jamii juu ya athari za dawa za kulevya, kwa kuwa huwa wanazunguka sehemu mbalimbali, katika viwanja vya michezo na kwa wajumbe wa nyumba kumikumi kwa kutumia vifaa na zana duni kuelimisha jamii, waliomba wawezeshwe TV moja (Samsung 29”), Deki ya DVD (Sumsung) moja Deki VHS (LG) moja pamoja na Generator moja. Ili viweze kuwasaidia katika katika kazi zao. Tume kwa kuona umuhimu imewanunulia vifaa hivyo. Vifaa hivyo vina thamani ya Tsh. 2,796,600/=.

Natumaini vifaa hivyo vitawasaidia katika kutimiza majukumu yenu ya kila siku.
Reactions::

Msuya: Kuna Uwezekano CCM Kung'olewa




WAZIRI Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Bw. Cleopa Msuya amesema kwa jinsi vuguvugu la kisiasa lilivyo kwa sasa nchini, si ajabu chama kingine
tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua hatamu za kuongoza serikali.

Mbali na hilo, Bw. Msuya (80) amesema ni wazi kama hatua za dhati hazitachukuliwa kuweka mfumo mzuri wa kutatua matatizo ya wananchi, hususan vijana, hali kama iliyotokea nchini Tunisia na katika nchi nyingine za Misri, Algeria na Ivory Coast, inaweza kutokea Tanzania.

Lakini ameonesha matumaini kuwa mjadala wa katiba mpya ambao Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeuridhia, utasaidia hali kama hiyo isitokee kwani baadhi ya mifumo inayoweza kuepusha itajadiliwa kwa kina na hata kuwekwa katika katiba, kwa manufaa ya Watanzania.

Kwa mujibu wa Bw. Msuya, katika mjadala unaonedelea nchini juu ya katiba mpya, ni vyema ikafikiriwa kama kuna haja ya kuendelea kuwa na bunge moja, huku yeye akipendekeza kuwapo wa mabunge mawili, kama ilivyo nchini Uingereza.

Mzee Msuya aliyasema hayo juzi, alipofanya mahojiano maalum na magazeti ya Kampuni ya Business Times Ltd, inayochapisha Majira, Business Times, Dar Leo na Spoti Starehe, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Akionekana kufurahishwa na namna Watanzania wengi wanavyoonesha utayari wa kutafuta maisha, alisema hiyo ni changamoto kwa serikali kwani inao wajibu wa kuonesha njia sahihi na kuweka mazingira bora ya wananchi wake kutumia fursa nyingi zilizopo.

Pamoja na kuisifia serikali katika baadhi ya maeneo, huku akionesha imani kuwa inaweza kurekebisha ili kulikwamua taifa hasa kwa kutumia fursa anuai ambazo Tanzania imebarikiwa kuwa nazo, Bw. Msuya alionekana kushangazwa na kusuasua kwa ushughulikiaji wa mambo muhimu kiasi cha kuzua minong'ono kwamba 'kuna mkono wa mtu hapo.'

Maendeleo yatokane na vipaumbele

Mzee Msuya alisema kuwa Tanzania ina kila kitu kinachoweza kuifanya nchi yoyote kuendelea kiuchumi, akisema "kwa mfano kwa nini tusiwe Qatar ya Afika Mashariki kwa kuzalisha gesi na kuweza kuuza gesi yetu ya asili kwa majirani. Mwalimu alisema kupanga ni kuchagua."

Akifafanua suala la umuhimu wa vipaumbele katika kuiwezesha nchi kuendelea, Bw. Msuya alisema kuwa haiwezekani maendeleo kupatikana kwa kufanya kila kitu kwa wakati mmoja.

"Unajua masuala ya maendeleo you need (unahitaji) kupanga, Mwalimu (Nyerere) alikuwa akisema kupanga ni kuchagua...ukijaribu kufanya kila kitu kwa wakati mmoja huwezi, lazima uwe na specific (malengo) target on some issues. Nitawapatia mfano...

"Kuna wakati baada ya uhuru serikali iliamua kutumia fursa za kiuchumi kwa majirani zetu, ndani ya muda fulani tukaamua kujenga reli ya TAZARA kwenda Zambia kwa msaada wa Wachina, tukajenga barabara ya lami kwenda huko mikoa ya kusini na tukajenga bomba la mafuta, TAZAMA, ilikuwa ni mipango ndani ya muda fulani, mnaacha mengine mna-concetrate.

"You have to select priorities (lazima uwe na vipaumbele). Imekuwa ikiniuma sana mimi, lakini ni changamoto, maana sasa tunazo raslimali zaidi kuliko tulivyokuwa wakati ule, tunao watu, lakini results (matunda) hayaonekani, sisi sio landrocked kama walivyo baadhi ya majirani zetu, sisi si nusu jangwa kama kama Kenya kwa mfano.

Huku akinukuu maneno ya Balozi wa Ujerumani, Bw. Guido Hertz, ambaye aliwahi kuhojiwa na gazeti moja nchini na kuonesha mshangao juu ya umaskini uliokithiri wa Watanzania pamoja na utajiri wa raslimali zilizopo, akisema "ni vigumu kuelewa wala kuielezea hali hii," Mzee Msuya aliongeza;

"Tuna kila kitu kinachohitajika...kuna haja ya kujitazama upya, tuna raslimali za kila aina zikiwemo za asili, are we putting them on the best use (tunazitumia inavyostahili ?)...tuna gesi ya asili, tuna akiba ya kutosha ya dhahabu, utalii pia...kuna hili ka kilimo kwanza, serikali imeshatamka ingawa kwa kuchelewa kidogo.

"Lakini nalo hatujalianza vizuri (la kilimo kwanza) kwa sababu hiyo hiyo ya kutopanga na kukosa vipaumbele...viwanda ni muhimu, suala la umeme ni critical (tatizo sugu) sasa lakini kuna possibilities (uwezekano) wa kugeuza coal (makaa ya mawe), umeme wa upepo na ule wa Rufiji ambao unazidi hata mahitaji yetu," alisema na kuongeza.

"Kinachotakiwa ni vipaumbele...sasa tuna raslimali watu ambazo zina ujuzi, maarifa na mafunzo. Suala la infrastructure (miundombinu)...ingawa serikali imejitahidi katika hili kwa kujenga barabara nyingi, lakini kuna tatizo la usafiri wa reli. Kuna kila haja ya kushughulikia reli ya kati, TAZARA na reli ya Tanga.

"Tujenge hizo ili mizigo kutoka bandarini isafirishwe, nasikia sasa wanajenga bandari sijui wapi, nyingine ya nchi kavu hapa...suala si kujenga bandari za nchi kavu, muhimu ni kujenga reli ili tuweze kuzifikia nchi jirani...ni changamoto ya kuanza kwa kutumia fursa zote hizo.

"Mimi nafurahi sana siku hizi unawaona Watanzania wanahangaika huku na huko, kila ukipita...hata hii ya machinga ni namna gani wananchi wanajitahidi, tunapaswa kuiona hiyo kama changamoto si laana, maana yake ni kuwa wananchi wako tayari kwa mabadiliko ya haraka, serikali inapaswa kusaidia hapo.

"Tufufue miundombinu yetu, hasa reli, spirit (ari) ya ujenzi wa barabara iliyopo sasa iendelezwe...concetrate on few key issues (kujikita katika mambo machache ya msingi) lazima tujue hilo...lazima tujue tunaondoka vipi kwenda mbele baada ya miaka 50 ya uhuru," alisema Bw. Msuya, ambaye pamoja na umri wa miaka 80 bado anaonekana kuwa na nguvu.

Akijibu swali juu ya ukuaji wa uchumi kitakwimu na kuongezeka kwa umaskini miongoni mwa wananchi walio wengi, alisema pamoja na kuwa serikali haiwezi kuwawekea watu fedha mfukoni, isipokuwa mpaka wanapojishughulisha kwa ajili ya kujipatia kipato, serikali inapaswa kuweka mazingira maridhawa ya shughuli hizo.

Alisema ni watu wachache wanaoweza kupata ajira rasmi za ofisini katika sekta ya umma na binafsi, kwani wengi wa Watanzania wanapata ajira katika kilimo, lakini tatizo limekuwa ni bei ndogo.

"Katika kilimo watu wetu wanajishughulisha kweli, lakini tatizo limekuwa ni bei ndogo, ukiulizia tatizo ni nini utakuta ni gharama za usafiri, tunahitaji kwenda kwa kasi...ndiyo maana nikasema masuala ya miundombinu ya uchukuzi ni muhimu.

"Kwa mfano hakuna haja ya soko kuwa Dar es Salaam tu, kila mkulima aje kupata soko hapa, mkulima aliyeko Rukwa anaweza kuuza nje ya nchi Zambia huko," alisema Mzee Msuya.

Akizungumzia juu ya mazingira ya uwekezaji nchini, alisema kuwa ni mazuri lakini kuna kila haja ya kujikita na kuweka kipaumbele katika miundombinu ya reli na bandari na upatikanaji wa umeme wa uhakika na rahisi, sambamba na mawasiliano ya elektroniki, ili kujiongezea uhakika na uwekezaji.

Alisema hata jiografia ya Tanzania ni fursa ya kipekee inayoweza kutumiwa na nchi kunufaika kiuchumi kwani inazungukwa na nchi nane, ambazo nyingine hazina bahari wala ziwa, hivyo kutokuwa na bandari, hali ambayo inazifanya kutegemea nchi jirani kama Tanzania.

"Miaka 30 iliyopita Dubai haikuwa lolote, it was just a small..., lakini wameibadilisha kuwa moja ya miji mikubwa kama Singapore. Miaka 50 ijayo Tanzania inao uwezo kabisa wa kuwa nchi yenye uchumi wa kati, tunaweza kuweka malengo ya kuwa kama Korea Kusini, hata kama hatutawafikia kabisa, lakini tunaweza.

Mjadala wa katiba mpya

Katika suala la katiba mpya, Mzee Msuya alisema kuwa kuna kila haja ya vyombo vya utendaji kazi hasa vile vya kisheria kufanyiwa mabadiliko ili vifanye kazi inavyopaswa.

Pia alisema ni wakati mwafaka katika mjadala wa katiba mpya, Watanzania waanze kufikiria iwapo kuna haja ya kuendelea kuwa na bunge moja, huku yeye akionea mfumo wa mabunge mawili, ndiyo unafaa kwa sasa nchini kutokana na wabunge kupatikana kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii nchini.

"Sasa hata wasomi wanakimbilia kwenye siasa...tunao wabunge wanatokana na NGO sijui wapi huko, hivyo ni vyema watu wakafikiria hilo.
(Chanzo: Gazeti Majira)
Reactions::

Idadi Ya Wagonjwa Wa Ukoma Yapungua


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda.

Serikali imesema hali ya maambukizi na idadi ya wagonjwa wa Ukoma nchini inaendelea kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda wakati akitoa Tamko kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani ambayo kitaifa itafanyika mkoani Lindi.

Amesema idadi ya wagonjwa wa Ukoma imepungua kutoka wagonjwa 35,000 mwaka 1983 hadi kufikia wagonjwa wapatao 2,600 kwa mwaka 2009 huku takwimu za mwaka 2009 zinaonyesha kuwa ,asilimia 11 ya wagonjwa wapya waliogunduliwa tayari walikuwa wamekwishapata ulemavu wa kudumu.

“Wagonjwa wengi wamekuwa wakipata madhara ya ugonjwa wa Ukoma kutokana na kuchelewa kwenda kwenye vituo vya afya kwa uchunguzi na matibabu” Amebainisha.

Ameeleza kuwa takwimu za mwaka 2009 zinaonyesha kuwa hali ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukoma bado ni kubwa katika mikoa ya Lindi wagonjwa 176, Rukwa wagonjwa 376, Dar es salaam wagonjwa 386 na mkoa wa Mtwara ambao una wagonjwa 175.

Amesema kuwa serikali kwa kutambua athari za ugonjwa huo na umuhimu wa kuzuia ulemavu utokanao na ukoma imeweka msisitizo kupitia kauli mbiu ambayo ni “Pambana na Ulemavu Utakanao na Ukoma” ili kuhimiza ushiriki wa jamii nzima katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukoma.

“Ninapenda kuwahimiza wananchi wote kuwa wakiona dalili za ugonjwa wa ukoma ambazo ni baka au mabaka kwenye ngozi yasiyo na hisia ya mguso ambayo huambatana na ganzi kwenye mikono na miguu wawahi kwenye vituo vya tiba kwa ajili ya uchunguzi na kupatiwa matibabu sahihi ya ugonjwa wa ukoma ambayo hutolewa bila malipo”

Dkt. Mponda ameongeza kuwa serikali imekuwa ikiwahudumia waathirika wa ugonjwa wa ukoma ikiwemo kugharimia jozi za viatu maalum 7000 kila mwaka kwa wale walioathiriwa na ukoma bila malipo ili kuzuia athari na kupunguza ulemavu utokanao na kuharibiwa kwa mishipa ya fahamu, huduma za marekebisho ambazo ni pamoja na huduma za upasuaji, viungo bandia, magongo na viti mwendo .

Aidha ametoa wito kwa jamii kutowanyanyapaa wala kuwatenga wagonjwa wa ukoma kutokana na mila potofu na ukosefu wa uelewa kuhusu ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa mtu ambaye yupo kwenye matibabu hata kama ana ulemavu hawezi tena kuambukiza ugonjwa huo na anastahili kuishi katika jamii.

Kwa upande wake Meneja wa Programu ya kupambana na Ugonjwa wa Ukoma nchini Dkt.Said Egwaga amefafanua kuwa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kupambana na ugonjwa huo huku akibainisha kuwa dawa za matibabu kwa ajili ya wagonjwa zinapatikana tofauti na miaka ya nyuma ambapo wagonjwa waliwekwa kwenye kambi maalum.

“Miaka ya nyuma hakukuwa na tiba ya ukoma tulikuwa na kambi maalum kwa ajili ya waathirika lakini sasa wagonjwa wa ukoma hawapelekwi tena kwenye kambi isipokuwa hupewa dawa ambazo huzitumia majumbani mwao”

Ameongeza kuwa Wizara kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii imekuwa ikiwaangalia waathirika wa ukoma wakiwemo walemavu kwa kuwapatia misaada ikiwemo ujenzi wa makazi yao na kuwasaidia katika shughuli za kilimo.

Siku ya Ukoma Duniani iliasisiwa takribani miaka 56 iliyopita kwa lengo la kuielimisha jamii kuhusu ugonjwa wa ukoma na huadhimishwa ulimwenguni kote kila jumapili ya mwisho wa mwezi januari kila mwaka.
Imeandikwa na Aron Msigwa-MAELEZO
Reactions::

Egypt Moto Bado Unawaka: Hosni Mubarak Avunja Baraza La Mawaziri



Hatimaye Rais Hosni Mubarak ameongea na watu wake.

Ametamka kuwa amevunja baraza la Mawairi. Lakini yeye atabaki kama Rais. Leo ataunda Serikali mpya itakayotoa suluhu ya matatizo ya WaMisri.
Obama ameongea na Hosni Mubarak na kumtaka atimize aliyoyasema. Na kwamba arudishe mawasiliano ya simu na internet kwa watu wake. Obama katoa tamko pia: " Tuko pamoja na watu wa Misri".

Tafsiri:

Siku za Hosni Mubarak Ikulu huenda zinahesabika. Mwenyewe anapima upepo, na kuna wengine wengi wenye kufanya hivyo.
Egypt na Hosni Mubarak ni mshirika mkubwa wa Marekani. Ni kiungo muhimu cha Marekani na Dunia ya Waarabu.
Marekani inaweka taadhari kubwa. Itataka kuwa na hakika ya nani atachukua nafasi ya Hosni.
Mohamed ElBaradei anaweza kuwa chaguo kubalika kwa Marekani. Lakini, kama akikataliwa na Muslim Brotherhoods wakajikita kuziba hombwe ni nini kitatokea? Kuna maswali yanayotakiwa majibu yake na Marekani.

Na Hosni Mubaraka hajaelewa, kuwa wanachotaka WaMisri wengi kwa sasa sasa si Serikali mpya inayoongozwa na Mubarak. Kwa WaMisri , miaka yake 31 Ikulu imetosha. Na chama chake nacho kimepoteza mvuto.

Ndio, Egypt ni taifa kubwa katika Arab World. Akianguka Hosni Mubarak, basi kuna wengine wengi katika Dunia ya Waarabu, ambao, himaya zao zitaporomoka kama nyumba ya karata. Siku chache zijazo zitaamua mustakabali wa Dunia ya Waarabu na watu wake.

Na Tusubiri tuone.

Maggid
Iringa.
Reactions::

Friday, January 28, 2011

Cairo Kunawaka Moto!




Ndugu Zangu,

JANA niliandika juu ya uwepo wa dalili za Cairo kuwaka moto Ijumaa ya leo mara baada ya swala ya Ijumaa. Na ndivyo ilivyokuwa. Miji ya Cairo, Suez, Alexandria na mingineyo inawaka moto. Waandaamanaji wameingia mitaani kudai mabadiliko. Wanataka Bunge livunjwe, Rais Hosni Mubarak na mwanawe Gamal waondoke Misri. Yale yale ya Tunisia.

Naam. Kuna Mapinduzi yanayoongozwa na vijana kwenye Dunia ya Waarabu. ( The Arab World). Tumeona Tunisia. Kule Yemen moto bado unawaka. Na sasa Egypt. Hali si shwari. Vijana wako mstari wa mbele.

Hosnu Mubarak amemrisha jeshi kuingia mitaani. Wananchi wamewashangilia wanajeshi. Kwamba idadi ya raia waliokufa mpaka sasa haizidi 20 inatoa tafsiri moja; kuwa jeshi huenda limeasi, maana imeripotiwa pia mapigano baina ya wanajeshi na polisi jijini Cairo.

Jengo la Makao makuu ya Chama tawala, PDP liko katika hali ya majivu. Limechomwa moto na waandamani. Kiongozi wa upinzani Mohammed ElBaradei amezuiwa nyumbani kwake baada ya kujaribu kuingia mitaani.
Barack Obama inaripotiwa hajapata mawasiliano na Hosni Mubarak. Kuna tahadhari kutoka Washington. Tamko rasmi la Washington kwa sasa ni " Tuko Pamoja na Misri". Ni dalili kuwa Marekani inaamini zama za Hosni Mubarak zinakaribia ukingoni.

Marekani imeionya Serikali ya Misri isitumie nguvu kukabiliana na waandamanaji. Imetaka pia mawasiliano ya simu na internet yafunguliwe. Kwa sasa yamefungwa.

Hosni Mubarak bado hajajitokeza kuongea na wananchi. Kauli yake inasubiriwa kwa hamu.

Na tusubiri tuone.

Maggid
Iringa.
Reactions::

Mwanamke Au Mwanamme? Kwa nini Unasumbuka Na Swali Hilo?

Leo pale mitaa ya Morogoro mjini nilimwona mtu aliyetaka kujua kijana aliyemwona mtaani ni wa jinsia gani. Ni kwa vile alivyovaa na anavyoonekana. Kwa nini binadamu tunasongwa na swali hili. Si ingetosha kufahamu kuwa uliyemwona ni binadamu mwenzako. Je, nawe husongwa na swali hilo?
Reactions::

Nimeingia Nyumbani Iringa Usiku Huu

Nikitokea Dar. Msamvu, Morogoro nimepita kwa mwendo wa pole. Sikusimama, kuepusha nongwa ya Bi Mkora!
Reactions::

Mandela aruhusiwa kutoka Hospitali



Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela ametolewa hospitali ambapo alikaa kwa siku mbili.

Daktari General Vejaynand Ramlakan alisema Bw Mandela, mwenye umri wa miaka 92, ambaye alikuwa na maradhi mbalimbali yaliyo ya kawaida kwa watu wa umri yake anaendelea uzuri.

Makamu wa Rais Kgalema Motlanthe- akitumia jina lake la ukoo la Bw Mandela-alisema "Madiba anaendelea vizuri."

Siku ya Ijumaa Bw Ramlakan alisema Bw Mandela alipata matatizo ya kupumua, lakini alikuwa akiendelea vizuri na atakuwa anapata matibabu akiwa nyumbani.

Alisafiri kutoka Cape Town hadi Johannesburg siku ya Jumatano kwa kile serikali kilichoita uchunguzi wa "kitaalamu".

Hatua hiyo ilichochea wasiwasi upya juu ya afya dhaifu ya kiongozi huyo.

Marafiki na familia walimtembelea licha ya kuwepo kwa usalama wa hali ya juu siku ya Alhamis.

Afisa mwandamizi wa polisi alisema mfululizo wa magari ulikuwepo nyuma ya eneo la kuingilia katika hospitali ya Milpark mjini Johannesburg, yakijiandaa kumchukua Bw Mandela nyumbani kwake Houghton.

Shujaa huyo wa ukombozi wa Afrika Kusini-anayejulikana miongoni mwa Waafrika Kusini kwa jina lake la ukoo, Madiba- tangu ajiuzulu na masuala ya umma mwaka 2004 ameonekana kuwa dhaifu katika mara chache anazoonekana hadharani.
BBC Swahili.
Reactions::

JK And Other African Leaders At World Economic Forum In Davos



President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete (fourth right) together with some African leaders and Heads of government who are in Davos attending the World Economic forum(WEF)2011.From left, Zimbabwean Prime Morgan Tsvangirai,(left) former UN Secretary General Koffi Annan,(Second left), Ethiopian Prime Minister Meles Zenawi(third left) and South Africa’s President Jacob Zuma. One of the major theme in this year’s WEF is Responding to New realities for improved economic condition(right)(Photo:Freddy Maro).
Reactions::