Subscribe:

Monday, February 28, 2011

Night University!




Diploma Course In Adult And Continuing Education at WAMO, Morogoro this night.
Reactions::

Maelekezo Ya Mwalimu!




WAMO, Morogoro, leo jioni.
Reactions::

Kozi Imepamba Moto!









Diploma In Adult And Continuing Education, WAMO, Morogoro, leo.
Reactions::

Group Nr 4!



Diploma Course In Adult And Continuing Education, WAMO, Morogoro, leo mchana.
Reactions::

CHADEMA Yawasha Moto Shinyanga


Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga.
Reactions::

Watano Wafa Kwa Ajali Dodoma


WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 34 kujeruhiwa katika ajali ilihoyahusisha magari mawili ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Kahama na Dar-Es-Salaam na jingine Itigi –Dodoma.

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa sita mchana eneo la Mbwanga karibu na mizani ya Tanroad ,nje kidogo ya mji wa Dodoma ilihusisha basi la kampuni Ally`s lenye namba T312 AUU lililokuwa likitokea Kahama kuelekea Dar-Es-Salaam ambapo liligongana na gari aina ya Coaster leny namba T896BGH ambalo lilikuwa likitokea Dodoma kuelekea Itigi wilayani Manyoni .

Kwa mujibu wa miongoni wa majeruhi wa ajali hiyo,chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa basi dogo ambaye alitaka kulipita gari jingine huku akiwa katika mwendo mkali.

Walisema alipokuwa akitaka kulipita gari jingine huku akiwa katika mwendo mkali,ghafla alikutana na gari jingine hivyo akaamua kukatisha barabara jambo ambalo lilisababisha dereva wa basi kubwa(ally`s) kujikuta ameligonga basi dogo ubavuni.
Reactions::

Yanga Yarejea Kileleni.


Timu ya Yanga ya Dar es Salaam imerejea kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochhezwa uwanja wa Jamuhuri mjini Morogoro jioni ya leo.
Reactions::

Pinda Awatembelea Waathirika Wa Mabomu Gongolamboto



Waziri mkuu Mizengo Pinda amewatembelea waathirika wa mabomu gongolamboto na kuziagiza mamlaka zinazohusika na misaada kuhakikisha kuwa misaada hiyo inawafikia walengwa na sio vinginevyo.
Reactions::

Watanzania London Wachangia Maafa Gongolamboto




1.Abuu Faraji akipewa mkono wa asante.

2.Fredy Macha alikuwapo kuchangia

3.Ali Hamini na rafiki yake wakikabidhi mchango.
Reactions::

Sitta Azidi Kuwakuna Wasomi, *Wasema aliongoza bunge kwa maslahi ya taifa




WASOMI wa vyuo vikuu Kanda ya Kaskazini, wameeleza kuridhishwa na utendaji wa aliyekuwa
Spika wa Bunge la Tisa, Bw. Samueli Sitta kutokana na kuendesha mijadala mbalimbali kwa maslahi ya taifa.

Wasomi hao kutoka vyuo vikuu vya Mwenge, Tengeru, Mount Meru, KCMC College, Chuo Kikuu cha Stephano Moshi (SMMUCo) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS), wameyasema hayo katika mdahalo wa kujadili katiba mpya.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Bw. Clemence Mbogo kutoka MUCCoBS, alisema katiba ya sasa haioneshi kuwalinda viongozi wanaoweka maslahi ya taifa mbele kama alivyokuwa Bw. Sitta.

Alisema Bw. Sitta ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa spika wa bunge aliweka utaifa mbele na siyo maslahi bianfsi au vyama vya siasa kama wanavyofanya baadhi ya viongozi kwa sasa.

Katiba yetu ya sasa imekaa kimya, haioneshi namna gani itawatetea viongozi wanaoweka maslahi ya taifa mbele na hii inasababisha wenye mamlaka kuwaondoa nani asiyejua Sitta alifanya kazi kwa maslahi ya taifa� alihoji.

Kuhusu madaraka ya rais wasomi hao walisema katiba ya sasa inampa rais madaraka makubwa ya kuteua mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya bila ukomo.

Wakizungumzia suala hilo, Bw. Godfrey Banza, Bw. Antony Lyimo na Paul Momba walisema katiba haioneshi idadi kamili ya mawaziri wanaopaswa kuteuliwa jambo ambalo husababisha rais kuteua idadi itakayompendeza yeye bila kujali gharama kwa taifa.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi, Bw. Japhary Michael aliwabeza baadhi ya watu wanaopinga wanasiasa kuzungumzia katiba kwani siasa ndiyo mhimili pekee ambao kila jambo nchini hupitia kwao.

Aidha meya huyo alibeza kauli za baadhi ya viongozi wa CCM wanaotaka Watanzania wasizungumzie katiba kwa madai hawaifahamu kwani mahitaji ya katiba mpya kwa sasa yanatokana na katiba iliyopo kutofahamika na asilimia kubwa ya Watanzania.

Akifungua mdahalo huo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dkt. Norman Sigalla aliwataka wasomi kuwa makini katika kufafanua katiba inayohitajika kwani mtazamo wa ubovu wa katiba iliyopo sasa huenda ukaonekana hivyo kutokana na uongozi uliopo madarakani.

Katiba inaweza kuwa nzuri au mbaya kutokana na uongozi uliopo madarakani lakini pia viongozi wasipokuwa na uhusiano mzuri na wananchi wao huweza kuleta hali ya kutaka mabadiliko,� alisema.

Awali waandaaji wa mdahalo huo, Waziri wa Elimu wa Serikali ya Wanafunzi MUCCoBS, Bw. Zawadi Kalist na Naibu wake, Bw. Amani Laizer walisema mdahalo huo umelenga kutoa muongozo sahihi kwa jamii kuhusu mabadiliko ya katiba badala ya kuvutwa na ushabiki wa kisiasa.
(Chanzo: Gazeti Majira)
Reactions::

CHADEMA Yazuru Kaburi La Baba Wa Taifa Butiama





1.Mama Maria Nyerere(kulia)akitete jambo na katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa wakati viongozi wa chama hicho na baadhi ya wabunge walipomtemhbele nyumbani kwake jana Butiama

2.Mbunge wa jimbo la kawe(Chadema)Halima Mdee akiweka shada la maua katika kaburi la baba wa taifa mwalimu julius Nyerere wakati viongozi wa chadema na baadhi ya wabunge wa chama hicho walipomtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama
Jana.

3.Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)nas mbunge wa hai Freeman Mbowe akitoa Salaam za chama hicho kwa familia ya mwalimu nyerere wakati viongozi wa Chadema na Wabunge wa chama hicho walipomtembelea Mama Maria Nyerere(katikati) nyumbani kwake butiama jana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa.
(
Picha Zote: Joseph Senga)
Reactions::

Nishati Ya Kuni....


......Barabara ya Isamilo jijini Mwanza hivi karibuni.
Reactions::

Jaribio La Mapinduzi Lazimwa Congo




Habari kutoka Kinshasa zinaeleza kuwa watu saba wameuawa baada ya kufanya jaribio la kumpindua Rais Joseph Kabila katika makazi yake.

Watu hao waliuawa na walinzi wa Rais Kabila, kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo.

Mwandishi wetu Lubunga Bya'Ombe akiwa Kinshasa amethibitisha kumetokea taarifa hizo. Hata hivyo watu waliohusika bado hawajajulikana.

Taarifa zaidi tutawaletea kadri zitakavyokuwa zikipatikana.
BBC Swahili.
Reactions::

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Rais Mazingira Atembelewa Na Balozi Wa Iran Nchini



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akisalimiana na Balozi wa Iran Nchini Tanzania Bw M. Movahhedi Ghomi wakati alipofika Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Kujadili Maandalizi ya Mkutano wa Mkataba wa Kuhifadhi aradhi Oevu utakaofanyika Nchini Iran.(Picha:Ali Meja)
Reactions::

UN Yamwekea Vikwazo Gaddafi



Balaza la usalama.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura - na kupita bila kupingwa - ya kuuwekea vikwazo utawala wa Muammar Gaddafi kutokana na hatua yake ya kutaka kuzima maandamano.

Baraza hilo limeunga mkono kuweka vikwazo vya silaha na kupiga tanji amana, huku wakifikisha suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo wa Libya aondoke madarakani na kuondoka nchini humo.
Serikali ya mpito

Hata hivyo bado anadhibiti mji wa Tripoli, lakini upande wa mashariki wa nchi unashikiliwa na waadamanaji.

Majadiliano ya kuunda serikali ya mpito ya wanaompinga Gaddafi inaarifiwa yanafanyika.

Mustafa Abdel-Jalil, aliyejiuzulu uwaziri wa sheria kwa kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji amesema tume yenye raia na wanajeshi itaandaa uchaguzi katika kipindi cha miezi mitatu, limekaririwa gazeti binafsi Quryna.

Mabalozi wa Libya nchini Marekani na katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono mpango huo, ambao unajadiliwa katika mji wa mashariki unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi.

Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa, wakati utawala wa Kanali Gaddafi ukijitahidi kuzima vuguvugu la mabadiliko lililodumu kwa siku kumi.

Hii ni mara ya pili tu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikisha nchi katika ICC, na ni kwa mara ya kwanza kura kama hiyo kupita bila kupingwa.
Reactions::

IFM Wagoma Leo


Wanafunzi wa chuo cha IFM cha jijini Dar es Salaam, wakiwa wamekusanyika leo asubuhi kwa lengo la kuanzisha mgomo kupinga kitendo cha wanafunzi wenzao kuzuiliwa kufanya mitihani kwa sababu ya kutolipa/kutomaliza ada ya semista ya kwanza.(Picha kwa hisani ya michuziblog)
Reactions::

CHADEMA Wataingia Ikulu Mwaka 2015: Magige Nyerere





FAMILIA ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, imekitabiria Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ushindi wa kishindo wa kuongoza nchi mwaka 2015.
Familia hiyo ya mwasisi wa taifa imesema ukomo wa serikali ya CCM umefika ambapo inaamini Uchaguzi Mkuu wa urais ujao, CHADEMA itaibuka kidedea.

Kauli hiyo ya familia ya Mwalimu Nyerere, ilitolewa leo na mtoto wa tatu wa Baba wa Taifa, Magige Nyerere, akiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa wakati viongozi wa CHADEMA Taifa walipozuru nyumbani kwa mwasisi huyo Butiama, Musoma, mkoani Mara, ambapo waliweka mashada katika kaburi hilo na Mama Maria kuongoza sala.
Alisema anaamini wapigakura mwaka 2015 watakuwa milioni 12 na kati ya hao, CHADEMA itapata kura milioni sita na CCM itaambulia kura milioni nne.
Kwa mujibu wa mwanafamilia huyo wa Baba wa Taifa kwa sasa nchi iko katika joto kubwa la kisiasa.

“Lazima tuseme ule ukweli uchaguzi mkuu uliopita CHADEMA haikuweza kuongoza dola, lakini mwaka 2015 wapigakura watakuwa milioni 12 na milioni sita zitaenda CHADEMA na milioni nne CCM.

“Hali ilivyo sasa, joto la kisiasa hapa nchini liko juu na wananchi wameonekana kufanya mageuzi ya kiuongozi,” alisema Magige Nyerere mbele ya mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere.
Huku akimfananisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na mdogo wake, Makongoro Nyerere, ambaye naye alikuwapo alisema, “Nakiri kuwa mimi ni CCM, lakini nafurahia kazi na siasa yenu…naomba uendelee hivyo na hata ukiwa bungeni kama kiongozi wa upinzani.”

Viongozi hao wa CHADEMA na msafara wao walizuru nyumbani kwa Nyerere majira ya saa 5:55 asubuhi kwa lengo la kumsalimia mjane wa Baba wa Taifa.
Kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alimuomba Mama Maria kukiunga mkono chama hicho na kukiombea mema.
“Mama tumekuja kukusalimia na familia yako…CHADEMA tunaomba mtuombee na mtuunge mkono,” alisema Mbowe kisha Mama Maria kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maelezo hayo.

Akitoa nasaha zake mbele ya kaburi la Nyerere, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema mchakato wa Nyerere kuwa Mtakatifu mwenye kheri bado haujakamilika, hivyo raia wawe na uvumilivu.
Alisema nchi ya Uganda imepiga hatua juu ya mchakato huo, hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.
Kuhusu maandamano ya CHADEMA nchi nzima, Magige Nyerere alisema,” Awali nilipatwa na wasiwasi mkubwa, lakini nimebaini kumbe ni maandamano mazuri; yaendelee.”

Hata hivyo, mtoto huyo wa Baba wa Taifa alisema maandamano hayo ni vema yakaendelea kwa amani, ili kufikisha ujumbe husika katika mamlaka husika.

Wakiwa wilayani Tarime jana Mbowe alimtaka Rais Kikwete kuacha mara moja kuwajaza hofu Watanzania juu ya kuwepo mipasuko ya kidini. Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa kabla ya mkutano, alihoji sababu ya Rais Kikwete kushindwa kuwakamata na kuwasweka ndani wanaoleta chokochoko za kidini.
Reactions::

Ujumbe Umefika!

Reactions::

Imejaa!

Reactions::

Sunday, February 27, 2011

Leo Yamenikuta Milima Ya Kitonga!



Niliondoka nikiwa peke yangu kutoka Iringa Mjini kuelekea Morogoro kunako saa tisa alasiri. Pale kwenye milima ya Kitonga nililazimika kufunga breki kwa nguvu kumruhusu dereva aliyekuwa akiovateki kizembe kutoka upande mwingine. Kilichotokea, kwa vile miteremko ya Kitonga ni mikali, brake plates zangu zikapata moto na kuanza kufuka moshi. Bahati niligundua hitilafu hiyo kwa haraka na kusimama mara moja.

Baada ya nusu saa hivi kila kitu kikapoa. Nikaendelea na safari yangu. Nimefika salama Morogoro usiku huu kuwahi programu ya mafunzo itakayoanza kesho pale kituo cha mafunzo cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima maarufu kama WAMO. Nitashiriki kama mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya kozi ya masafa iliyozinduliwa majuzi kule Dar es Salaam.
Reactions::

Vodacom Foundation Yatoa Msaada Wa Mradi Wa Kuku



Mkurugenzi mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akiwakabidhi vifaranga vya kuku watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Rafiki Child Care Home kilichopo Mererani wilaya Simanjiro mkoani Manyara,Mfuko huo umetoa msaada wa jengo la kufugia kuku vyote vikiwa na thamani ya Milioni 15.
Reactions::

TAKUKURU Yazidi Kumkalia Kooni Mwakalebela.



1.Dr Edward Hosea
2. Fredrick Mwakalebela


SIKU moja baada ya mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa kumwachia huru aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Frederick Mwakalebela katika shitaka lake la rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa mjini,taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa imekusudia kuendelea na kesi hiyo.

Akizungumza na mtandao huu wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ mwanasheria wa TAKUKURU mkoani Iringa Ntime Mizizi alisema kuwa maamuzi ya mahakama hiyo chini ya hakimu Festo Lwila ameyakubali na kuwa mapungufu yaliyokuwemo awali katika kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2010 taasisi hiyo inayafanyia kazi na kufungua kesi yenye maelekezo ya mahakama.

Alisema kuwa maamuzi ya mahakama katika kesi hii ya Mwakalebela yameonekana ni mazuri na yenye maelekezo ya kina zaidi kuliko ilivyo kuwa kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin Joseph Mungai ambao mahakama haikwenda kiundani zaidi kama ilivyo katika maamuzi madogo ya kesi ya Mwakalebela.

Hata hivyo alisema kuwa kesho jumatatu kutakuwa na majibu sahihi dhidi ya uamuzi wa takukuru katika kuendelea na kesi hiyo ama lah.

“Nakuomba unitafute jumatatu nitakuwa na majibu sahihi ….japo maandalizi ya s
hitaka jipya yatakuwa yamefanyika” alisema mwanasheria huyo wa Takukuru
Reactions::

Bongo Fleva FC Yaichapa Bongo Move FC 2-0





1. Washabiki waliofurika uwanjani.2. Bongo Movie FC
3.Bongo Fleva FC


Timu ya Bongo Fleva FC jana iliibuka mshindi dhidi ya timu ya Bongo move FC kwa magoli 2-0 katika mechi iliyochezwa ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukusanya fedha ili kuwasaidia waathirika wa Mabomu Gongolamboto. Pia walikuwepo wasanii mbali mbali katika kutoa burudani.
Reactions::

Wataalam Wa Takwimu Waijia Juu Takwimu!



Pichani: Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kuu ya Taifa ya Takwimu,(NBS) Dkt, Albina Chuwa akihudhuria Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa (UNSD). Mkutano huo uliofanyika kwa siku nne uliwakutanisha Wakurugenzi Wakuu wa Takwimu na Wataalamu wa takwimu kutoka nchi 192 Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Katika Mkutano huo, ajenda iliyoibua mjadala mkali kati ya wataalamu hao na sekretarieti ya Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, ilikuwa ni ile iliyohusu Taarifa ya Maendeleo ya Watu Duniani ya Mwaka 2010. aliyekaa nyuma ni Bi Redegunda Maro, Mkurugenzi wa Idara ya Operesheni za Takwimu kutoka Idara kuu ya Takwimu, Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohamed Hafidhi hayupo pichani.



·

NI YA MWAKA 2010 WASEMA IMAJAA KASORO KIBAO

Na Mwandishi Maalum

New York-Kasoro kadhaa zikiwamo za upotoshaji mkubwa wa takwimu zilizomo
katika Taarifa ya Maendeleo ya Watu Duniani ya Mwaka 2010( Human Development
Report) kumewafanya Wakurugenzi Wakuu wa Takwimu kutoka nchi za Umoja wa
Mataifa kugeuka mbogo na kuzijia juu Taasisi zilizoandaa taarifa hiyo.

Wakuu wa maswala ya takwimu walikutana hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,
wakihudhuria mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya UM ( UNSD). Mkutano
huo wa siku nne, uliomalizika ijumaa, ulijadili ajenda mbalimbali zikiwamo hiyo ya
Taarifa ya Maendeleo ya Watu Duniani ya mwaka 2010.

Kwa ujumla
hali katika
chumba cha mkutano wa Kamisheni hiyo, ilikuwa ya
sintofahamu, huku kila mjumbe aliyechangia taarifa hiyo,
akishindwa kudhibiti
hasira, uchungu na masikitiko ya waziwazi ya kutoridhishwa na namna taarifa hiyo
ilivyoandaliwa huku ikiwa na mapungufu yasiyo yakawaida.

Licha ya kwamba takwimu zilikuwa ama zimekosewa ama zimepotoshwa nchi kadhaa
hazikutokea kabisa kwenye taarifa hiyo.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ulijumuisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara
Kuu ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa, Bw. Mohamed Hafidhi Mtakwimu
Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Bi. Radegunda Maro Mkurugenzi wa Idara ya
Operesheni za Takwimu.

Akichangia mjadala wa Taarifa hiyo, Dkt. Albina Chuwa anasema.“ Serikali yangu
inaungana na wasemaji waliotangulia, kuhusu upotoshwaji mkubwa wa takwimu
zilizoonyeshwa kwenye taarifa hiyo zikiwamo za nchi yangu Tanzania, sijui UNDP
wamezitoa wapi takwimu hizi , sisi kama wenye dhamana na masuala yote yahusuyo
takwimu, hatukushirikishwa ni wazi kwamba UNDP wametumia takwimu ambazo sisi
hatukuziridhia na wala hazina baraka ya ofisi yangu.

1

Akiongea kwa hisia kali, Dkt. Chuwa amesema . “Ni wazi kwamba zoezi zima
la maandalizi ya taarifa hiyo yameishia katika ukiukwaji wa kanuni na taratibu
zilizokubalika kimataifa za uchambuzi na usambazaji wa taarifa za takwimu za nchi
wanachama”.

Akasema kuwa Tanzania ingependa kuona, Kamisheni ya Takwimu ya Umoja
wa Mataifa ( UNSD) ikizifanyia kazi hoja zilitotolewa na nchi wanachama kuhusu
mapungufu yaliyomo katika Taarifa hiyo ambayo ilizinduliwa mwaka uliopita.

Wajumbe wa Kamisheni hiyo wameeleza na kusisitiza kwamba, wakati wanatambua
umuhimu wa Taarifa ya Maendeleo ya Binadamu kama nyenzo muhimu katika
uendeshaji wa mijadala ihusuyo maendeleo ya watu
kitaifa na kimataifa. Lakini
wamelazimika kuelezea masikitiko yao kuhusu vyanzo vya takwimu na mbinu
zilizotumiwa kuaanda taarifa hiyo.

Watakwimu Wakuu kutoka Serikali za Afrika ya Kusini, na Suriname na ambao majina
yao hayakupatikana mara moja. Pamoja na kuelezea masikitiko yao juu ya taarifa
hiyo. Wametaka masikitiko na maelezo yaliyotolewa na wajumbe ya kutoridhishwa
na taarifa hiyo, maelezo na malalamiko hayo yajitokeze kama yalivyoelezwa na
wajumbe katika majumuisho ya mwisho ya mkutano huo.

“ Ujumbe wangu unasisitiza kwamba hisia zilizoonyeshwa na wajumbe wa mkutano
huu, za kutoridhishwa na taarifa hii, zijitokeze kwenye taarifa ya mwisho ya mkutano
huu kama zilivyotolewa, sisi ni wataalam wa takwimu na si wanadiplomasia hakuna
kupindisha lugha hapa” akasisitiza Mjumbe huyo wa Suriname. Kauli iliyoungwa mkono
na wajumbe wengi.

Wajumbe wameipa miezi mitatu Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, kutoa
taarifa yenye majibu ya hoja zilizotolewa na wajumbe kuhusu kasoro za taatia hiyo.

Aidha katika mambo mengine yaliyolalamikiwa na wajumbe katika taarifa hiyo ni
pamoja kutoridhishwa na matumizi ya takwimu ambazo hazikuwa rasmi na ambazo
zimepatika kutoka vyanzo visivyo rasmi.

2

Kwa sababu hiyo wamesisitiza kuwa pale ambapo takwimu rasmi zinakosekana, basi
matumizi ya takwimu zisizo rasmi razima yapate ridhaa ya nchi husika.

Halikadharika washiriki wa mkutano huo, pia wameelezea masikitiko yao kuhusu
utofauti na upishanaji mkubwa wa taarifa za kitakwimu kati ya Taasisi moja na
nyingine ndani ya Umoja wa Mataifa. Na wakatoa wito wa kutaka kurekebishwa kwa
tofauti hizo haraka.

Vile vile Watakwimu hao wamezitaka taasisi zinazoandaa taarifa hiyo ya maendeleo ya
binadamu duniani, kuwasiliana na wataalamu wa takwimu wa kila nchi kabla ya kutoa
hadharani taarifa hiyo ili kuepusha kujirudia kwa matatizo na makosa yaliyojitokeza
katika taarifa ya mwaka jana.

Taarifa ya Maendeleo ya Watu Duniani huandaliwa na Mfuko wa Maendeleo wa
Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kuzishirikiana na taasisi nyingine za kimataifa na
kwa kufanya kazi kwa karibu na nchi husika kupitia Idara za Takwimu. Lakini katika
hali ya kushangaza, taarifa zinaonyesha kuwa taarifa ya mwaka jana, utaratibu huo
haukuzingatiwa hasa eneo la ushirikishwaji nchi husika.

Wakati huo huo, Tanzania kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu, imetoa taarifa
kwamba, sensa ya idadi ya watu na makazi itafanyika mwakani (2012).

Katika hatua nyingine Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe katika Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa
Mataifa ikiwakilisha Bara la Afrika. Tanzania itakuwa mjumbe wa Kamisheni hiyo kwa
kipindi cha miaka minne kuanzia mwakani 2012.
Reactions::

CHADEMA Waandamana Mara

Reactions::

Waandamanaji Wakaa Tayari Tripoli


Kanali Gaddafi
Watu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli wanajiandaa kwa mapambano zaidi, baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kusema atafungua maghala ya silaha kwa ajili ya wanaomuunga mkono.

Uondoaji wa maelfu ya wafanyakazi wa kigeni unaendelea kwa njia ya anga, bahari na barabara, lakini wengine bado wamekwama.

Marekani imezuia matumizi yoyote ya fedha na amana za Kanali Gaddafi na baadhi ya watu wake wa karibu.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa katika mzozo wa kisiasa wa siku 10.

Siku ya Ijumaa, waandamanaji wanaopinga serikali mjini Tripoli wameshambuliwa kwa nguvu na bunduki.

Shirika la habari la AP limesema, limeelezwa kuwa serikali ya Kanali Gaddafi inawapa silaha raia wanaoiunga mkono ili kuweka vizuizi mjini Tripoli na kuwabana waandamanaji.

Wakazi ambao wamezungumza na AP kwa njia ya simu siku ya Jumamosi, wameripoti kuwa magari ya raia wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi yanafanya doria mitaani.
BBC Swahili.
Reactions::

Neno La Leo: Kiongozi Wa Nchi Haui Watu Wake, Gaddafi Amewaua, Hana Aibu!




Ndugu Zangu,



KIONGOZI wa nchi haui watu wake, Moummar Gaddafi amewaua. Ndio, mchana wa jua kali, na bado anasimama, anadai ni kiongozi wa WaLibya, Gaddafi hana aibu.


Anapostahili kusimama Gaddafi sasa si kwenye jengo la Ikulu ya Tripoli, bali Mahakama ya Kimataifa Ya Haki na inayoshughulika na Wahalifu wa Kivita, The Haag.



Baraza la Usalama la Umoja Wa Mataifa jana limepitisha azimio la kumwekea Gaddafi vikwazo vya silaha na kugandisha amali zake. Inasemekana, Gaddafi ana akaunti za mabilioni ya dola za KiMarekani. Kumwekea Gaddafi na familia yake vikwazo ni msaada mkubwa kwa watu wa Libya kwa sasa.


Kosa kubwa kabisa alilofanya Gaddafi kwa WaLibya ni KUWAKANDAMIZA. Ndio, kuwanyima UHURU. Gaddafi aliwafanya WaLibya kama ng’ombe kwenye zizi. Waliotoa sauti kumpinga aliwakamata na ‘kuwachinja’, kimyakimya.



Libya ikawa mali ya Gaddafi na familia yake. Wanaodai haki yao sasa anaowaona kuwa ni majambazi wanaovamia nyumba yake. Kumbe! Jambazi mkubwa kwa WaLibya alikuwa ni Gaddafi na familia yake. WaLibya, kama wenzao wa Tunisia na Misri, wameamka. Hawatalala tena mpaka Gaddafi na familia yake wameondoka madarakani.


Naam. Gaddafi bado anang’ang’ania madarakani. Ameshindwa kusoma alama za nyakati, kabla na sasa. Ninavyofuatilia yanayoendelea Libya na ulimwengu mzima wa WaArabu, naziona kila dalili, za Gaddafi kutomaliza hata wiki moja kutoka sasa akiwa madarakani.


Gaddafi anatumia kila mwanya na hila, kujaribu kuurudisha nyuma mshale wa saa ya mabadiliko. Huko ni sawa na kulizuia wimbi la bahari kwa mikono. Hakika, WaLibya hawastahili tena kuongozwa na mtu kama Gaddafi. Ni Gaddafi huyu wa sasa, amewadhalilisha watu wake mbele ya macho ya walimwengu, anaendelea kufanya hivyo.


Si tumeona Ijumaa jioni , amesimama na kuwaambia WaLibya waendelee kuimba na kucheza! Gaddafi amepoteza mwelekeo na mguso wa hali halisi. Amepitisha viwango vyote vya ulevi wa madaraka, Gaddafi wa sasa anaonekana kama mwehu fulani aliyeshika bunduki na kupita mitaani. Gaddafi anatishia usalama wa WaLibya kwa mamilioni kwa kila siku anayoendelea kuamka akiwa madarakani.


Tushukuru , kuwa Gaddafi hana silaha za kemikali wala nyuklia, maana, Gaddafi wa sasa, katika dakika za mwisho za kupoteza mamlaka, angeweza kufanya maangamizi makubwa kwa WaLibya na dunia. Kisingizio? Njama za Wazayuni, George Bush ( hata kama hayupo madarakani) na Osama bin Laden! Je, kuna namna nyingine ya kumtambua kama binadamu ni mwendawazimu?


Kwa sasa Gaddafi ametengwa na dunia na hata baadhi ya marafiki zake. Huenda Gaddafi yuko tayari kufanya lolote lile kwa sasa, maana, hajui ni wapi salama pa kukimbilia. Hata kwa rafiki yake Mugabe kuna wanaojiandaa kufanya kama ya Tunisia na Misri.


Na kule Saudi Arabia? Haiwezekani. Si ana ugomvi wa siku nyingi na mfalme. Na wala Gaddafi asingepata tabu sana kupata pa kukimbilia, lakini, ugumu anaoupata sasa ni wa kujitakia; kuwaua watu wake. Hata rafiki zake wanapata tabu kumwelewa kwa hilo, maana, wao bado wana chembe za aibu.


Naam. Kiongozi wa nchi haui watu wake, Gaddafi amewaua, hana aibu. Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid
Iringa
Jumapili, Februari 27, 2011
Reactions::

Wallahi Ladhim, Maisha Gani Haya?!

Reactions::

Hunger Banquet!






Greek Club, Iringa, jana jioni. Soma maelezo kwenye picha za chini.
Reactions::