Subscribe:

Thursday, March 31, 2011

'Makamanda' Wamesafisha Kikaango!




Kama baba kwenye nyumba unafurahi unapoona chakula ulichomwandalia mkeo na wanao kimeliwa kikaisha. Ina maana wamekipenda. Leo nimeiandalia familia yangu uyoga na tambi. Kinachoonekana kikaangoni ni uyoga niliouchanganya na sosi niliyoiandaa kwa kuchanganya unga wa ngano kidogo, maziwa na buljong.

Mmenisema kuwa nimekaanga kitunguu maji na uyoga kwa wakati mmoja. Niliwatega kuona kama kuna mabingwa kweli wa upishi. Lengo langu  lilikuwa ni kupunguza maji ya kitunguu na uyoga kwa wakati mmoja. Kisha nikakatakata tena vitunguu na kuendelea na kukaanga. Ni staili yangu.

Naam. Wengi mmefaulu mtihani, zero ni tatu tu!
Na si mnaona, 'makamanda' wangu wamekwangua kikaango!
Reactions::

Makamu Wa Rais Asaini Kitabu Cha Kumbukumbu Ubalozi Wa Japani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakati alipokwenda kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Japan Upanga jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu kutokana na maafa makubwa yaliyotokana na Sunami Nchini Japan hivi karibuni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu kufuatia maafa makubwa yaliyotokana na Sunami Nchini Japan hivi karibuni, wakati alipokwenda katika Ofisi za Ubalozi huo Upanga jijini Dar es salaam leo.(Picha: Amour  Nassor-VPO)
Reactions::

Kiwanja Kinauzwa

Mimi naitwa Mr Amon, nimepata matatizo ya kuishiwa pesa ya ada, na sina mtu wa kunilipia ili nimalizie course yangu ya India term iliyobakia.

Hivyo sasa ninaomba kwa heshima na taadhima uniwekee/Miniwekee tangazo kwenye Blog yako/zenu ili nipate wadau upesi waweze kununua ili niondoke kwenda India kumalizia course yangu iliyobakia.

Kiwanja kiko: Tegeta Salasala

Kipimo: Metre 80 urefu X Metre 35 upana

Bei: Makubaliano

Nime-attach picha za kiwanja.

Please sihitaji madalali nahitaji wanunuzi tu .


Contacts: 0652-692024 Mr. Amon

0715-341004 Mrs. Lydia
Reactions::

Kesho Ni Siku Ya Maadhimisho Ya Upandaji Miti Kitaifa

Kesho ni siku ya kitaifa ya kupanda miti ambapo maadhimisho haya kwa mwaka huu yatafanyika katika ngazi za mikoa yote Tanzania.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Maimuna Tarishi. Maadhimisho ya mwaka huu ni ya kipekee kwa kuwa ni mwaka ambao umetangazwa na Umoja wa Mataifa kama Mwaka wa Kimataifa wa Misitu pia ni mwaka ambao Tanzania inaadhimisha miaka 50 ya uhuru.
”Tukumbuke pia kuwa huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Hivyo, tutaadhimisha siku hii kwa kutathmini tulikotoka, tulipo na tunapokwenda kuhusiana na hali ya misitu”, imefafanua taarifa hiyo.

 Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kila mtanzania anatakiwa atathmini athari anazopata kutokana na ufyekaji na uharibifu  wa misitu ili aamue kwa dhati kuihifadhi  misitu kwa ajili ya kuwanufaisha watu wa kizazi hiki na vizazi vijavyo.

Bi. Tarishi amesema, kila familia haina budi kuanzisha bustani ndogo yenye miche inayolingana na idadi ya wanafamilina ambayo ni rahisi kuitunza miche hiyo kwa kutumia maji yanayopatikana nyumbani.
Katibu Mkuu huyo anafafanua kuwa, njia nyingine ya kuongeza kiwango cha upandaji miti ni kupanda mbegu moja kwa moja ardhini kwa baadhi ya miti hasa katika mikoa iliyoko katika nyanda za juu hapa nchini kama Tanga na Iringa.

“Wakati mwingine siyo lazima miche yote inayopandwa itoke bustanini. Njia nyingine ya kustawisha miti ni kutumia miche inayojiotea yenyewe ardhini kama maotea. Miche hiyo inapandwa katika sehemu zilizokusudiwa ikiwa bado midogo. Njia hii inatumika hasa kwenye sehemu zenye mvua nyingi na udongo tifutifu,” amebainisha Bi. Tarishi.
Katika taarifa yake, Bi. Tarishi anasema, aina nyingine ya kustawisha misitu ni kutenga na kulinda eneo kutokana na uharibifu wa kimazingira ili mbegu ziote zenyewe (natural regeneration), njia hii imefanikisha shughuli za kustawisha misitu na malisho ya mifugo mkoani Shinyanga.

“Wananchi wa Shinyanga wanatumia utaalam wao wa jadi unaojulikana kwa jina la Ngitili wa kutenga maeneo na kuyapumzisha ili mbegu zijiotee zenyewe, matokeo yake mkoa huu umeongeza zaidi ya hekta 500,000 za ardhi ambayo ilikuwa imeharibika kabisa hapo awali,” Bi. Tarishi anasema.

Bi. Tarishi amewapongeza wananchi wanaostawisha miche ya miti bila kutegemea ile inayostawishwa katika bustani za serikali, kwa sasa asilimia 70 ya miche ya miti yote inayopandwa inatokana na juhudi za wananchi wenyewe.

Maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupanda Miti yalifanyika kwa mara ya kwanza tarehe Mosi Januari mwaka 2001 kutokana na Waraka wa Waziri Mkuu Namba 1 wa mwaka 2000 uliomtaka kila mwananchi kupanda miti kwa manufaa yake na mwaka jana Siku ya Taifa ya Kupanda Miti iliadhimishwa kitaifa Aprili Mosi mkoani Shinyanga.
(Imeandikwa na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
Reactions::

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
 

          WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Ali Mohamed Shein amemteua Othman Masoud Othman kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kuanzi leo tarehe 31/03/2011.                                                      Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema kwamba Rais Dk Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa nafasi za Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na kumteua Omar Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo, Othman Masaoud Othman alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar(DPP) ambaye alianza kushika wadhifa huo tangu mwaka 2003.
  Rais Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Rais Dk Shein amemteua Omar  Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Makungu alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
  Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 94(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. uteuzi huo umeanza tangu tarehe 30/03/2011.
 
Imetolewa na:-
 Idara ya Habari(MAELEZO)
Reactions::

Truck For Sale

Brothers and sisters, Mercedes Benz tank for sell. Make 1992, Model 911in good condition. It can be seen in Dar Es Salaam, contact through phone number 0784/15 041 540.
Regards,

Reactions::

Enyi Mabingwa Wa Mapishi; Nawapa Mtihani!


 Iringa alhamisi  jioni. Nshatoka kibaruani. Niko jikoni naandaa mlo wa jioni kwa mke na ' makamanda' wangu. Kikaangoni nimeshaweka uyoga mbichi wa leo leo. Nimekata pia kitunguu maji ( vinne). Nimetia chumvi robo kijiko ( cha chai)Nimeanza kuvikaanga vyote kwenye mafuta ya alizeti. Vijiko viwili ( vya chakula)

Baada ya dakika kadhaa n'taweka nyanya maji na pilipili shamba. Nna vingine nimefikiria, lakini nataka niwashirikishe enyi mabingwa wa mapishi kwa kuwatupia swali; Je, baada ya hapo vipi vije kikaangoni? Na je, mmeshayaona mapungufu ya kimapishi mpaka hapo nilipofikia? Kama ndio, myataje.

Na hapa ndio tutakapowajua mabingwa wa mapishi, kama wapo.... Kazi kwenu!
Reactions::

Marlaw{bongo} featuring Jua Cali {genge}Perfoming live on same stage Easter Sunday!! You are on your holidays so theres no excuse, come down to the most famous Easter Party bank holiday W,kend on 24th Sun April @ Face club rg1 7je Reading.Entry £15 Deejays Richie Dee, Fugga Flex & guest Playing the BEST in Afro Beat, R’n’B Old Skul and Bashment till 6am... Get down early to make sure you don’t miss out!
Reactions::

JK Akutana Na Waziri Mkuu Wa Zimbabwe



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(Picha:Freddy Maro)
Reactions::

Matokeo Ya Utafiti Wa Tiba Ya Babu Wa Loliondo

Kwa niaba ya Bongo Promotions tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wale wote walioshiriki katika survey tuliyoitangaza siku ya jumatatu (28.03.11). Lengo la kufanya huu utafiti mdogo ni kuangalia mitizamo ya wananchi kuhusu tiba ya babu Loliondo. 

Tumepata maoni  mengi sana kutoka kwa watu zaidi ya 180. Takwimu zinaonyesha wengi wamependekeza kwamba taratibu za kitaalam zifanyike kuthibitisha kama dawa inatibu, wengine  wanasema kuwa hili ni suala la imani zaidi. Wapo walio fedheheshwa na juhudi za vingozi kutokuwa za kuridhisha katika kufuatilia suala hili na badala yake wao kuwa ni miongoni wa wanaojitokeza kwenda kupata kikombe. Unaweza kupata maelezo zaidi na report kamili ya hii tafiti ndogo kupitia link hiyo hapo chini. 

Tunashukuru kwa ushirikiano wako
BONGO PROMOTIONS Team
Reactions::

Mbunge Wa Chadema Atoa Msaada Wa Gari La Kubebea Wagonjwa Lenye Thamani Ya Shilingi 32 Milion


Mbunge wa jimbo la Ilemela (CHADEMA) Mheshimiwa Highnes Kiwia amekabidhi gari la kubebea wagonjwa aina ya Nissan Patrol lenye thamani ya shs.millioni 32  katika Zahanati ya Karume, iliyopo katika kata ya Bugogwa wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
   Katika kampeni za uchaguzi mwaka jana, aliwahaidi wananchi katika jimbo lake kuwa atawasaidia gari la kubeba wagonjwa ambalo litawasaidia wananchi kuwasafirisha hadi katika hospitali nyingine na baadhi yao kuwatoa majumbani kwao hadi katika zahanati hiyo ahadi ambayo ameitekeleza ndani ya siku 90 kama alivyoahidi.                                                                                                                                                                                                                                                                                                  Mhe.Kiwia ametoa ahadi nyingine kuwajengea wananchi wa kata ya Bugogwa, kituo cha polisi na kumuagiza Diwani wa Kata ya Bugogwa, Swila Dede Swila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo, kata ya Bugogwa kusimamia ujenzi wa kituo hicho ambacho kitaanza kujengwa muda wowote kuanzia sasa na ujenzi wake kukamilika ndani ya siku 90.    
(Habari na Picha:Mdau wa Mwanza)                                                                                                                                                                                               
Reactions::

Wadau Wajadili Rasimu Ya Sera Ya Utawala Bora Afrika Mashariki

Naibu Waziri wa ushirikiano wa Afrika mashariki Mhe. Adballah Sadalla akitoa hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya utawala bora ya jumuiya ya Afrika mashariki  uliofanyika jana jijini Dar es salaam

Wadau mbalimbali waiohudhuria katika mkutano wa rasimu ya sera ya utawala bora ya jumuiya ya Afrika mashariki (Picha:Fullshangweblog)
Reactions::

Bondia Francis Cheka Kupambana Na Marcus Upshaw Wa Marekani

Bondia wa ngumi Francis Cheka nchini Tanzania (kulia) akiongea
na waandishi wa habari jijini leo kuhusu pambano lake na Bondia
Marcus Upshaw wa Marekani litakalofanyika Mei 1,2011 katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee. Pambano hilo limedhaminiwa na
AURORA GROUP OF COMPANIES (T) LTD. Pichani kushoto ni
Afisa Uhusiano wa Makampuni ya AURORA Shomari Kimbau.

Afisa Uhusiano wa Makampuni ya AURORA Tanzania (AURORA
GROUP OF COMPANIES (T) LTD) Shomari Kimbau (kulia)
akiongea na waandishi wa habari jijini leo kuhusu mambo
mbalimbali yanayohusu mpambano wa ngumi kati ya Bondia Francis
Cheka (TANZANIA) na Bondia Marcus Upshaw wa Marekani
utakaofanyika Mei,1,2011 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
(kushoto) ni Afisa Habari kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Anna
Nkinda. (Picha:Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Reactions::

Na Vijana CCM Nao Ni Wazee! ( Makala, RAIA MWEMA)


Na Maggid Mjengwa,

"HAYO malumbano ni ya kwao, sisi hatuyajui, wala hatutaki kuyajua. Tunashughulika na kutekeleza Ilani tu… maneno maneno kama hayo hayatuhusu”, anasema John Chiligati, Katibu Mwenezi wa CCM.


Simba anapozeeka na kukaribia kufa huanza kupoteza uwezo wa kuona, kunusa na hata kusikia. Lakini, kuna moja ambalo simba ana hakika nalo, kuwa ameacha simba watoto. Kizazi cha simba kitaendelea.


Chiligati anasema hayajui yanayotokea ndani ya UVCCM na malumbano yanayoendelea. Hapa kuna mawili; kama ni kweli hayajui ni tatizo, na kama anayajua na kuamua kutingisha mabega na kujifanya hayaoni wala kuyasikia ni tatizo kubwa zaidi. Kwa vile, Umoja wa Vijana wa Chama ni moja ya viungo muhimu kwenye mwili wa chama.


Maana, katika maisha haya ya kisiasa, vijana ndio nguzo na uhai wa chama chochote kiwacho. Inakuwaje basi, chama kinachozeeka kinapozungukwa na ’vijana wazee’? Uhai wa chama hicho utakuwa hatarini.


Si na juzi hapa, vijana wa CCM walikutana kule Dodoma. Tunaambiwa kuwa vijana wamewasha moto ndani ya chama chao. Nilijua, kuwa kwenye ukumbi ule wa White House walipokutana vijana wa CCM alikuwamo Mzee Kingunge Ngombale- Mwiru.


Ukimwondoa Mwalimu , nikiri, kuwa Mzee Kingunge ni mmoja wa Watanzania walionifanya niipende siasa na aliyechangia tangu utotoni mwangu, katika kujenga misingi yangu ya kiitikadi kwenye Ujamaa na Kujitegemea. Hakika, Kingunge Ngombale- Mwiru ni hazina ya kiitikadi, si tu kwa CCM, bali kwa Taifa.


Naam. Mkutano ule wa vijana ulipokwisha kule Dodoma nikamwuliza mjumbe mmoja aliyekuwamo mkutanoni; ” E bwana we, nimesikia Mzee Kingunge mmechagua kuwa Kamanda wenu wa vijana Kitaifa, amesemaje kwenye hotuba yake ya shukrani?


Nikaambiwa, ilianzia kwenye salamu. Kingunge aliposalimia; ”Kidumu Chama Cha Mapinduzi!” akaitikiwa; ” Kidumu Chama Tawala! ” Ikasikika ’ ajua’, kutoka kwa Mzee Kingunge. Akaawambia; mmekosea kwenye kuitikia salamu. Hamtakiwi kujibu ”Kidumu Chama Tawala!” Jibuni “Kidumu!”


Maana, kwa mujibu wa maelezo ya Mzee Kingunge, CCM haiwezi kuwa chama tawala siku zote. Na kuna maeneo ya nchi hii kwa sasa ambapo CCM si chama tawala. Akawauliza vijana wale; “ Sasa ina maana mkifika huko mtaacha kujibu salamu ya Kidumu Chama Cha Mapinduzi!?


Mpaka hapo Kingunge amedhihirisha jambo moja muhimu, kuwa umri uko wa namna mbili. Kuna umri wa miaka na umri wa kifikra. Ndiyo, kuna wanaozeeka kifikra hata kama bado ni vijana. Na kuna wazee ambao kifikra bado ni vijana sana pamoja na umri wao mkubwa. Kingunge katika hilo alionekana kuwa kijana zaidi. Ameonyesha kwenda na wakati kuliko vijana wale.


Na nikaambiwa, kuna mahali mjumbe mmoja mkutanoni alitoa hoja ya umri wa mwana-CCM kuhesabiwa kuwa kijana uongezwe. Katika kujadili lile, Mzee Kingunge akasema, ”Hakuna tatizo katika mtu kuleta hoja yake, lakini kuhusu hili la mipaka ya umri wa kijana muangalie hata katika nchi nyingine wenzenu wanafanyaje.” Mzee Kingunge akawa ameua hoja ile ya kijinga kwa kutumia busara zaidi.


Na hili la vijana wa vyama na umri linahitaji makala yake, inakuja. Haiwezekani katika dunia hii ya sasa mtu mwenye miaka 40 na zaidi bado anang’ang’ania ndani ya jumuiya ya vijana ya chama chake.
Mtu mzima huyo anafanya nini ndani ya jumuiya ya vijana?


Hebu fikiri, hivi leo kijana wa miaka 20 akiwa mtundu anaweza kupata mtoto wake wa kwanza, na mtoto wa kijana huyo akiwa mtundu, naye anaweza kupata mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 20. Sasa basi, hapo mzazi mwenye miaka 40 atakuwa na mjukuu, ataitwa babu.


Yumkini, kwenye jumuiya zetu hizi za vyama kukawa na wanaoitwa babu. Ndiyo, wana wajukuu. Hawa walistahili kuwa kwenye Jumuiya za Wazazi au Wanawake za vyama vyao. Nimeahidi, kuwa hili la vijana na umri nitaliandiakia makala yake.


Turudi kwenye mkutano ule wa vijana wa CCM. Nimeambiwa, kuwa Mzee Makamba aliwekwa kiti moto. Kuna waliomshutumu kuwa kachangia CCM kupoteza majimbo. Niseme, kuwa Mzee Makamba wanamwonea bure. Alipaswa kupongezwa badala ya kukaangwa.


Hivi nani katika CCM hiyo asiyejua kuwa karibu wajumbe wote wa Sektretariati ya chama hicho walikuwa majimboni kupigania ubunge. Pale Lumumba alibaki Makamba. Labda Makamba hakuona jimbo la kwenda kupigania, ndilo kosa lake? Makamba ni kama ’fan-belt’- mkanda wa pangaboi kwenye injini ya gari yenye matatizo. Injini ya CCM ina matatizo. Na hayakuanza Awamu hii ya Kikwete.


Malumbano haya na mlolongo huu wa matamko ya vijana wa CCM kila Mkoa hayatakisaidia chama chao kwa sasa. Bila kufahamu, vijana wa CCM, badala ya kumsaidia Mwenyekiti wao, wanamdhoofisha katika kutekeleza majukumu yake ya kichama na Kiserikali, tena kwa kasi. Na tatizo nilimeshalisema, kuwa vijana nao ni ’ wazee’.


Kuna wanaojipanga kwa 2015. Kuna wanaojipanga kuwania U-NEC mwakani. Kuna wanaovizia U-DC na vyeo vingine. Vijana- Wazee wa sasa wamekaa kimaslahi zaidi, si ya chama, bali ya kimakundi na zaidi yao binafsi.


Kikwete anasemwa kuwa mpweke kisiasa, tumeanza kuelewa. Uchaguzi uliopita ukawa mtihani mgumu kwa Kikwete na chama chake. Na katika vita ya uchaguzi wa kisiasa Sektariati ya chama ndiyo ’ War Room’- Chumba cha Vita.



Unafanyaje wakati Mwenyekiti wa chama yuko vitani anapigania Urais na wajumbe wa Sekretariati ya chama nao wanapigania majimbo yao? CCM wana bahati. Idadi ya majimbo waliyopoteza ingekuwa kubwa zaidi kama wapinzani wao wangejipanga vema.


Na siasa ni mchezo wa makosa, si wa bahati. Ndiyo, ni kama kandanda. Wanaokosea ni wale wasemao; ’ Footbal is a game of chance’- Kwamba kandanda ni mchezo wa bahati. Hapana, kandanda ni mchezo wa makosa. Ushindi unapatikana kutokana na makosa ya timu pinzani. Yaweza kuwa makosa ya kimkakati au ya mchezaji mmoja mmoja.


Kuna kosa CCM wamelifanya na wanaendelea kulifanya; CCM imeanza kupoteza sifa muhimu ya mwanasiasa na chama cha siasa. Kuwa karibu, kuyasikiliza, kuyaelewa na kuyafanyia kazi matatizo ya watu wa kawaida walio wengi.


Na kuna wakati Benjamin Mkapa aliwaambia wazi wana CCM wenzake kule Dodoma, kuwa kihistoria, TANU na CCM imekuwa kimbilio la wanyonge. Mkapa akabainisha, kuwa CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara. Hili ni kosa la kisiasa.


Yaweza kuwa kazi bure kwa CCM kuwaparamia CHADEMA. Hakuna anayewasomba wananchi kwa malori kwenda kwenye maandamano na mikutano ya CHADEMA. Mpinzani mkubwa wa CCM kwa sasa ni wananchi, umma. CCM ijitathimini, basi.


Na nilipata kuandika, kuwa kama Chama Cha Mapinduzi kina nia ya kupunguza kupotea kwa imani ya umma kwa chama hicho, basi, kutahitajika, si tu kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya muundo wa Serikali na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, bali kufanyika kwa mabadiliko makubwa yenye kishindo.


Kuna watakaopuuza, lakini, kuna ukweli, kuwa tuhuma za ufisadi zimekipaka na zinaendelea kukipaka matope mno CCM. Kwenye macho ya umma, chama hicho kimechafuliwa na tuhuma hizo za ufisadi. Kuna wana CCM leo wanajiuliza kama wavae sare za chama au la wapitapo mitaani. Maana, kuna Watanzania walioanza kuchukia rangi za chama hicho. Wanazihusisha na ufisadi.


Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yawe ni fundisho kwa chama tawala. Kama CCM inataka kubaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi, kuwa na uhalali wa kubaki madarakani, basi, ina lazima ya kujipambanua kwa vitendo kutoka kwenye yote makubwa yenye kuhusiana na ufisadi na maovu mengine. Ibaki kuwa kimbilio la wanyonge. Isifike mahali, chama kikajikuta katikati ya mgogoro na umma. Hilo laweza kuharakisha mazishi ya chama yasiyo na kisomo.

Maggid
Reactions::

Naibu Waziri Wa Mawasiliano, Sayansi Na Teknolojia Atembelea Zantel

Ofisa Mkuu wa Tekenolojia Kampuni ya Zantel Bw. Moncef Mettiji wa pili (kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya mawasiliano ya Kampuni hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw. Charles Kitwanga alipotembelea kampuni hiyo Dar es salaam jana. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu Ali Bin Jarsh na kushoto ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Norman Moyo.(Picha:Rajabu Mhamila)
Reactions::
Reactions::

Michezo Ya Watoto Hawa...

.....Ina faida nyingi kuliko hasara.(Picha ya mtandao)
Reactions::

Mzee Wa Upako Aibuka Akimfagilia JK

MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema kuwa wanaompinga, Rais Jakaya Kikwete katika utawala
wake wapo katika ushindani lakini hawatashinda katika vita hiyo.  

Akizungumza na mwandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kile alichokiita Afya ya Amani, Umoja, Upendo na Uvumilivu, Mchungaji Lisekelo alisema kuwa ili nchi iwe na afya inahitaji matunzo na si kelele za kulaumiana.


Alisema kulaumiana kumeshika kasi tangu Rais Kikwete ashike madaraka kwa miaka mitano lakini mazuri aliyoyafanya hayasemwi bali mabaya ndiyo yanayozungumzwa hata kama yamejificha. ...soma zaidi..
http://www.kwanzajamii.com

Reactions::

Wednesday, March 30, 2011

Babu; " We Obama, Ukinipa Dola Feki Utakuwa Umekunywa Juisi!"


... Hii bei ya kikombe imepangwa na Mungu, Kikwete mia tano na Obama dola moja, hata kama baba yako alitoka Kenya!
Reactions::

Serikali Mkoani Mwanza Yajipanga Usafiri Salama Kwenda Kwa Babu Loliondo.; Mwingine Aibuka Na Kikombe Wilayani Magu

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro akizungumza leo katika kikao cha wadau wa usafiri wa kwenda kwa Babu Loliondo.

Wadau wa usafiri wakiwa katika kikao hicho                                                                                                       Katika kudhibiti usalama, hali mbaya ya huduma za afya, malazi, chakula, maji na huduma nyingine kwa mahitaji ya mwanadamu Serikali mkoani mwanza kupitia kamati yake ya ulinzi na usalama leo imetoa taarifa kwa vyombo vya habari jinsi ilivyo jipanga kuhakikisha watu wake wanaosafiri kuelekea kijiji cha Samunge wilaya ya Ngorongoro kupata tiba wanapata tiba bila usumbufu na hatimaye kurejea kwa usalama.                                                                                                                                            Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema kuwa katika kipindi cha tiba ya babu wa Loliondo ofisi yake imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ikiwa ni pamoja na watu kuachwa njiani bila msaada wowote, kutofikishwa kwa mchungaji kupata tiba kutokana na ubovu wa vyombo vya usafiri na baadhi ya watu kupoteza ndugu zao bila taarifa.             
                                                Kupitia sababu hizo na nyingine nyingi za kiusalama na kepuka mfumuko wa bei ya vyakula kijijini na nauli kwa vyombo vya usafiri Kamati yake imekuja na utaratibu mpya utakaofuatwa na watu wote ili kupunguza kadhia iliyopo na msongamano huo.                                                                                                  Aidha Bwana Abbas Kandoro amesema kuwa serikali imeamua kuunda vituo vya kanda vilivyopewa majukumu ya

-Ukaguzi wa magari ambapo malori na magari ya wazi yamepigwa marufuku kuelekea Samunge.
-Utoaji wa namba za magari kwa kila kanda kuwa na rangi yake maalum, Kanda ya ziwa - Nyekundu, Kanda ya Kaskazini - Njano na Kanda ya Kati - Kijani.
-Ukaguzi wa wasafiri kutoka nje ya nchi
-Utoaji wa leseni za muda/ vibali maalum
-Kuangalia wagonjwa mahututi
-Kutolewa kwa matibabu ya dharura
-Usalama wa vituo na
-Kupanga muda wa kuondoka


Amezitaja kanda tatu zilizoundwa za uthibiti wa usafirishaji wa abiria kuelekea Loliondo ambazo ni Kanda ya ziwa vituo vikiwa Musoma , Bunda, Mugumu na Loliondo/ Wasso,huku njia ya Ndabaga ikipigwa marufuku, Kanda ya Kaskazini ambayo itahusisha mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar na nchi jirani huku vituo vilichoainishwa vikitajwa kuwa ni Arusha mjini – viwanja vya NMC, LKanda nyingine iliyotajwa ni Kanda ya Kati ikihusisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Manyara na Nyanda za juu kusini nacho kituo kikiainishwa kuwa ni babati.

Taarifa hiyo imewataja wasimamizi wakuu wa kanda kwa utawala kuwa watakuwa Wakuu wa mikoa ile hali utekelezaji utasimamiwa na RPC, RIO, RMO, JWTZ, TAKUKURU, RSO, SUMATRA, TRA na TANROADS.

Wakati huo huo taarifa kutoka kijiji cha Bulima katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza zinasema kuwa kikombe kingine kimeibuliwa na mtu anayejiita SHANGAZI (Marieta Charles) ambaye ameibuka akitoa tiba ya dawa ya miti shamba yakunywa vikombe viwili kwa gharama ya shilingi 1000.

Serikali ilisitisha safari kwenda kijijini Samunge kwa muda wa wiki moja kuanzia jumamosi ya tarehe 26/03/2011 hadi tarehe 01/04/2011 kwa magari yote hii ikiwa ni pamoja na magari ya serikali na viongozi wa aina zote, usafiri kwa njia ya ndege na Helkopta, sababu kuu zikitajwa kuwa ni hali tete za Afya, mazingira na huduma muhimu.oliondo na Mto wa Mbu. (Habari na Picha:Mdau wa Mwanza)                

Reactions::

Japan Yaimwagia Zanzibar Bilioni 54 Kutekeleza Miradi Ya Umeme


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Japan zimetiliana saini kutekeleza mradi mkubwa wa usambazaji umeme katika Kisiwa cha Unguja utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 54
Akitia saini mkataba wa msaada wa mradi huo leo Mjini Zanzibar, Balozi wa Japan hapa nchini, Hiroshi Nakagawa alisema pamoja na matatizo yaliyoikumba nchi yake, lakini bado kuna umuhimu wa kuisadia Zanzibar.
“Watu wengi hapa Zanzibar wanasumbuka kwa ukosefu wa umeme wa uhakika, bila shaka mradi huu utasaidia kupunguza mzigo kwa Shirika la umeme” Alisema Balozi Nakagawa.
  Mradi huo ambao una lengo la kuboresha kituo cha kupokelea umeme Mtoni Unguja, ujenzi wa vituo vidogo vya umememe kwa njia tatu za Kv 33 yenye urefu wa Km 80.
Alisema mradi huo unaosimamiwa kwa pamoja na Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani Kampuni ya VISCAS ya Japan ndio iliyopewa kazi ya ukandarasi kuweka waya kuanzia Fumba.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha uchumi na mipango ya maendeleo, Khamis Mussa alisema Serikali itachangia shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi mradi utakapopita.Alisema mradi huo utasaidia mradi mkubwa wa umeme chini ya bahari kutoka Ras Kiromoni  hadi Fumba unaofadhiliwa na Shirika la Changamoto za Milenia, hivyo mradi huo utasambaza umeme katika maeneo mengine ya Unguja.
Awali, Mwakilishi wa Shirika la misaada la Japan(JICA), Yukihide Katsuta alisema anaamini mradi huo unasubiriwa kwa hamu na wananchi wa Zanzibar hasa wakati huu ambao kuna matatizo ya upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Yukihide alisema Japan imekuwa ikilisaidia Shirika la Umeme Zanzibar(ZECO) katika mambo mbalimbali hivyo, anaamini mradi huo utakuwa chachu ya kukuza uchumi.
(Imeandikwa na Fatuma Mzee_MAELEZO Zanzibar)
 

Reactions::

JK Akutana Na Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa Wa Haki Za Binadamu


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Bibi.Navanethem Pillay wakati alipomtembelea na kufanya mazungumzo naye leo asubuhi.(Picha:Freddy Maro)
Reactions::

Wapiganaji Wa Ivory Coast Waelekea Mji Mkuu

Majeshi yanayomtii Bw Ouattara
Majeshi yanayomtii Rais anayeungwa mkono na Umoja wa Mataifa Alassane Ouattara yanaelekea kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Yamoussoukro.
Majeshi yake hivi karibuni yameteka miji kadhaa na kiongozi aliye madarakani Laurent Gbagbo ametaka mapigano yasitishwe.
Bw Gbagbo amekataa kuachia madaraka licha ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa Novemba.
Mwandishi wa BBC alisema Yamoussoukro ni mji mkuu tu kwa jina, lakini kutekwa kwake kutakuwa ni ushindi wenye umuhimu mkubwa kwa majeshi yanayomwuunga mkono Ouattara.
Takriban watu 1,000,000 wamekimbia mapigano- hasa katika mji mkuu Abidjan- na karibu 462 wameuawa tangu Desemba, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Katika mji wa magharibi wa Duekoue, maelfu ya watu wamejihifadhi kwenye kanisa baada ya kukimbia mapigano wiki hii.BBC
Reactions::

Rais Kikwete Atembelea Wizara Ya Maliasili Na Utalii

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na utalii wakati alipofanya ziara yake ya kukazi wizarani hapo jana jioni.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi pamoja wafanyakazi wa Wizara ya maliasili na utalii wakati wa ziara yake ya kikazi Wizarani hapo jana jioni(Picha: Freddy Maro).
Reactions::

VodacomFoundation Yakabidhi Madarasa Mawili Mkoani Tabora

Mkuu wa wilaya ya Urambo    Anna Magowa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili    yaliyojengwa  kwa ajili ya shule ya sekondari ya Kaliua iliyopo Wilaya    ya urambo Mkoani Tabora, anaeshudia ni Meneja wa Vodacom Foundation    Yessaya Mwakifulefule, Madarasa hayo yalijengwa kwa thamani ya shilingi    milioni 30.

Baadhi ya wanafunzi wa shule    ya secondary ya Kaliua iliyopo Wilaya ya urambo Mkoani Tabora wakiwa    wamekaa darasani mara baada ya Meneja wa Vodacom Foundation kuwakabidhi    rasmi madarasa hayo yaliyojengwa na kampuni hiyo kwa thamni ya shilingi    milioni 30.
Reactions::

Loliondo Debate; Majibu Yangu Kwa Mashaka Na Mwilima


Ndugu Mashaka and Ndugu Mwilima,


Greetings,

I noted with great interest what you gentlemen wrote regarding Babu’ s Miracle Cure in Loliondo.

Yes, we may differ in some areas, BUT, with no doubt, we all love our country, thus why spend our pressing time in this Loliondo issue.


Two days ago, the Ministry responsible came up with official statement regarding ‘ Kikombe cha Babu’- Babu’s cup. We now know, that the ‘Single Cup’ administered by Babu is safe, it is harmless. Our Govt told us.


Further laboratory tests will be conducted for the Babu’s Murigariga tree that he claim is able to treat five chronic deseases ; diabetes, cancer, TB, and AIDS.


What MISSED in the Ministry statement is the fact that while Babu’s miracle cure was declared harmless, people were not told to continue with their medicine after taking Babu’s cup. Here is my great worry. As some of us know, there are confirmed reports, that people are dying after taking Babu’s cup simply because they ceased to take their ARV’s or diabetes medicines.


I believe, at this stage, it would be wrong for people to take the “miracle cure” as a substitute for conventional medical treatment administered in official government and private hospitals or our clinics throughout the country.


The today Citizen’s cartoonist, King Kinya tells it all ; a government official throwing away hospital medicines while rushing to Loliondo!


And the media has a role to play, of correctly and professionally informing Wananchi on this issue Why not some media houses do not take the initiative of conducting independent investigation on ‘ Babu’ miracle Cure?

For me, it has been a lot of abrakadabra and no facts. If thousands of sick Tanzanians including politicians have been at Babu’s place , why is it difficult for a single media house to collect medical data and present them to the public? So far, there is none, but plenty of abrakadabra- streets testimonies.


We must , at this stage, until we get laboratory confirmation, make it open, that the Loliondo ‘miracle’ cure can only complement or be given in addition to qualified, specialized medical treatment offered by the hospitals or clinics.

We need to remind the government, to take it’s responsibility, of informing the mass on the above mentioned facts.


Regards,

Maggid

Iringa
Reactions::

Harusi Trade Fair 2011, Mambo Moto Moto

Mustafa Hassanali, briefs journalists about the upcoming event of Harusi Trade Fair 2011 which will be held at Diamond Jubilee starting on 1st to 3rd April this year. Left is Markerting Manager of Mustafa Hassanali, Hamis

PR&MEDIA Manager of Mustafa Hassanali, Mfaume Shaban speaks during the Press Conference as Mustafa Hassanali (centre) and Hamis Omary, Marketing Manager of Mustafa Hassanali listens in Dar es salaam today
Reactions::

Maporomoko Ya Maji Ludewa Yanatumika Kuzalisha Umeme Wa Gharama Nafuu

Maporomoko ya maji katika kijiji cha Mawengi ambayo yanatumika kuzalisha umeme wa gharama nafuu

Mitambo ya kuzalisha umeme katika maporomoko ya maji Ludewa.                                                                                                                                        Baadhi ya vijiji katika Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa vimeanza kuzalisha umeme wake kwa kutumia maporomoko ya maji.  Wateja wanaotumia umeme huo wanalipa bili kwa mwezi shilingi 1,500 tu.(FrancisGodwinblog)
Reactions::

Huyu Ndiye Dada Mage Mtoa 'Kikombe' Wa Mkoani Tabora

Dada Magreth Mutalemwa akiwa kazini ambapo humuombea mgonjwa kabla ya kumpa Kikombe cha dawa!

Umati wa  watu wakiwa kwenye foleni wakisubiri Kikombe cha DADA MAGE.     Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora mjini amejitokeza na kudai alioteshwa kutibu watu na Bikira Maria,mama yake Yesu. Sasa anafanya kazi hiyo na umati mkubwa wa watu unamiminika kupata kikombe nyumbani kwake. (Asante ya Picha:Keronyingiblog)      
Reactions::

Kikombe Cha Dada Mage Wa Tabora; Mkuu Wa Mkoa Tabora, Kamanda Wa Mkoa Wamekipata

Afisa Mwandamizi wa Jeshi la polisi akiombewa kabla ya kupata kikombe cha Dada

Kutoka kushoto ni RPC Barlow, Mkuu wa mkoa Bw Minyimsa na afisa usalama wa wilaya ya Tabora mjini.

Mkuu wa mkoa Abei Mwinyimsa akiwa kwa dada

Gari la kamanda Barlow maeneo ya kwa dada Mage!

Mkuu wa mkoa wa Tabora akisikiliza tiba kwa makini!
  Baada ya kutoka katika kikao cha kamati ya usalama, Mkuu wa mkoa wa Tabora alikwenda Urban quater Uzunguni mkoani mjini Tabora kukutana na Dada Mage ambapo alipata kushuhudia mambo ya ugawaji wa Dozi Ya Kikombe maarufu kama 'Kikombe Cha Dada Mage' yanavyokwenda. Mkuu wa mkoa na kamati yake ya ulinzi na usalama  walijaribu kumshauri Dada Mage ahamie sehemu ya wazi na kubwa lakini dada Mage alikataa ombi hilo akidai kuhama hapo ni kukiuka  maelekezo. Pia mkuu wa mkoa aliangalia uwezekano wa kujengwa vyoo maeneo ya jirani ambapo mita 200 hivi toka kwa dada kuna bara bara ya lami iendayo Urambo na pana nafasi kubwa sana ambayo inaweza ikatumika kujenga vyoo. Urban quarter  Uzunguni ni kiasi cha kilometa 2 hivi toka Tabora mjini! Dada ameahidi kuwa atakuwa anatoa Dozi ya Kikombe mpaka saa  kutoa huduma mpaka saa 12 na mbili na nusu jioni ambapo wagonjwa watatakiwa kuondoka na kurudi kesho asubuhi, Hatua ambayo mesisitizwa kutekelezwa na Afisa usalama wa wilaya Bw Shaban Murumbi! Ujumbe huo wa mkuu wa mkoa wote ulipata Kikombe kwa Dada Mage (Keronyingiblog)
Reactions::

Pinda Katika Ufunguzi Wa Mkutano Wa REPOA

Waziri mkuu Mizengo Pinda akizungumza na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya taasisi ya utafiti kuhusu kuondoa umaskini (REPOA) Profesa Esther Mwakikambo (kushoto) na mkurugenzi mtendeji wa taasisi hiyo Profesa Samweli Wangwe baada ya kufungua mkutano  huo katika hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam leo.
Reactions::

Neno La Leo: Simba Mzee Anapokaribia Kufa....


Ndugu Zangu,


” HAYO malumbano ni ya kwao, sisi hatuyajui, wala hatutaki kuyajua. Tunashughulika na kutekeleza Ilani tu… maneno maneno kama hayo hayatuhusu”. Anasema John Chiligati, Katibu Mwenezi wa CCM.( NIPASHE, Jumapili, Machi 27, 2011)


Simba anapozeeka na kukaribia kufa huanza kupoteza uwezo wa kuona, kunusa na hata kusikia. Lakini, kuna moja ambalo simba ana hakika nalo, kuwa ameacha simba watoto. Kizazi cha simba kitaendelea.


Chiligati anasema hayajui yanayotokea ndani ya UVCCM na malumbano yanayoendelea. Hapa kuna mawili; kama ni kweli hayajui ni tatizo, na kama anayajua na kuamua kutingisha mabega na kujifanya hayaoni wala kuyasikia ni tatizo kubwa zaidi. Kwa vile, Umoja wa Vijana wa Chama ni moja ya viungo muhimu kwenye mwili wa chama.


Maana, katika maisha haya ya kisiasa, vijana ndio nguzo na uhai wa chama chochote kiwacho. Inakuwaje basi, chama kinachozeeka kinapozungukwa na ’vijana wazee’? Uhai wa chama hicho utakuwa hatarini. Na hilo ni Neno La Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu, RAIA MWEMA, leo Jumatano)



Maggid
Iringa
Jumatano, Machi 30, 2011
Reactions::