Subscribe:

Saturday, April 30, 2011

Vipaji Vingi Vyajitokeza Serengeti Filamu Jijini Arusha

Muigiza ji Hemed akiigiza na  mmoja wa waigizaji chipukizi waliojitokeza wakati wa kutafuta vipaji, katika Mwendelezo wa Dahabu na  Serengeti Fiesta Filamu  uliyofanyika leo kwenye klabu ya Mawingu jijini Arusha, mchakato huo ulianzia mkoani Mwanza, ambapo ulifanyika  kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kupatikana kwa wasanii chipukizi lukuki ambao wanatakiwa kuendelezwa katika tasnia ya filam nchini.

Dada huyu anaonekana ni mtu mzima lakini naye ameamua kujitokeza na kuonyesha uwezo wake, katika kutafuta nafasi wakati wa  mchakato kutafuta vipaji vya uigizaji wa Serengeti Fiesta Filamu, uliofanyika leo kwenye klabu ya Mawingu jijini Arusha na kukutanisha vijana wengi wa jiji hilo.

Hapa wigizaji Hemed ambaye pia ni mwanamuziki akiigiza kwa umakini na Merry mmoja wa waigizaji chipukizi waliojitokeza katika mchakato wa Serengeti Fiesta Filamu, msanii huyo chipukizi ameeleza wazi kwamba anamkubali sana mwigizaji Aunt Ezekiel, kutokana na uwezo wake awapo kazini kwani amekuwa ni mvaa uhalisia halisi wa eneo ambalo analiwakilisha katika uigizaji wake.  (Fullshangweblog)
Reactions::

Je, Ni Wanawake Wanaopenda Zaidi Harusi Za Kifahari?



Kwanini?

Jana niliingiza picha hiyo chini na kuanzisha mada juu ya harusi. Pichani chini ni harusi simple kabisa niliyoikuta kijijini Chala, Nkasi, Sumbawanga. Wanaume wengi kwenye ukurasa wangu wa facebook wametokea kuipenda sana harusi hiyo ukilinganisha na wanawake. Je, hii inamaanisha wanawake wengi wanapenda harusi za kifahari? Kama jibu ni ' Ndio', basi, kwanini?
Reactions::

Haya, Warembo Hawa!


Kushoto ni Da' Maria, Mwalimu, Iringa International School na kulia ni Da' Gil, Mwenyekiti, Bodi Ya Uongozi, Iringa International School.
Reactions::

MshikeMshike!

Jumamosi Ya Michezo, Iringa International School, leo asubuhi.
Reactions::

' Kamanda' Wangu Huyu!

Iringa International School, leo asubuhi.
Reactions::

The Royal Wedding Invitation!

Above: A Royal kiss

Yesterday the world has witnessed one of the biggest wedding ceremonies after a long time. It

was estimated about 2 billion people viewed the event through their television sets around the

world; the wedding between the future King of the UK, Prince William and Kate Middleton. It’s

no exaggeration to say that almost every corner of Britain was engulfed by Prince William-Kate

wedding ecstasy. Everyone seemed happy. Great Britain became ‘real’ great. Some argued it was

truly one of those once in a lifetime opportunities.

Almost 2,000 people were invited to the big/main event, at Westminster Abbey. Our country,

Tanzania, was represented by our ambassador to London. He was one of dignitaries who came

into the fold via commonwealth links.

A few people couldn’t be that ‘lucky’. The two most recently Great Britain PMs, Tony Blair and

Gordon Brown of Labour party were not invited while Baroness Margret Thatcher and Sir John

Major, the former PMs via Conservative party were-because ‘they are not Knights of the Garter’.

Fair enough.

Then there was an ‘omission’ of the Syrian ambassador’s name to London, Dr Sami Khiyami. At

first, his name was on the list of those ‘lucky’ but he was later ‘summoned’ to the Foreign Office

and he was told, ‘he can no longer attend the Royal wedding’ due to his government’s excessive

use of force against demonstrators. They (Britain) termed it ‘unacceptable’.

Despite being a slap on the wrist, I would say, that was ‘okay’ course of action to express the

feeling(s), based on the fact that the UK government is perceived to be one of the ‘frontiers’

of democracy, rule of law and human rights in the world. It should be remembered that, these

Syrian demonstrators are peaceful demonstrators. They have asked for ‘basic changes’ after

being ‘humiliated’ for a long, long time. The level of nepotism is highest in the country. The

political power is held by a small elite.

But there’s a paradox that entangles the whole issue here! Despite the use of overwhelming force

against peaceful demonstrators, the name of the Crown Prince of Bahrain was on the list. Of

course, he pulled out at the weekend so not to overshadow the event.

The question that many would like to have an answer to it is what’s the difference between Syria

and Bahrain? In both cases innocent people are being killed brutally and remorselessly, so why

one rule to Syria and another one to the like of Bahrain?

We all want to live in a peaceful world to cherish the ‘beauty’ of this world and use the

potential God has given us to betterment our lives.

so called ‘superpowers’ stop what I call ‘double standard’. It’ has been a chronic disease

among ‘superpowers’.

a.k.a:Jua Kali
Reactions::

Olimpiki Maalumu Wanaomba Msaada Wa Tiketi 5 Za Wachezaji Kwenda Ugiriki

       Mkurugenzi wa Olimpik Maalumu Frank Macha.                                                                                                                                      Wachezaji wenye ulemavu wa akili  11 wamechaguliwa kushiriki mashindano ya riadhaa ya DUNIA nchini UGIRIKI ambayo yamepangwa kufanyika JUNE mwaka huu.        
Mkurugenzi wa Olimpiki Maalumu ameseama kuwa  mpaka sasa wamepata tiketi sita tu  kati ya tiketi kumi na moja zinazohitajika kufanikisha safari ya wachezaji hao. Bado tiketi tano kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo ,hivyo Mkurugenzi huyo anawaomba watu wenye uwezo wa kuwasaidia wachezaji hao wajitokeze kutoa msaada wa vifaa vya michezo nguo kwa ajili ya safari pamoja na tiketi ili kufanikisha safari ya wachezaji hao wenye ulemavu wa akili.

Amesema iwapo watashindwa kupatiwa msaada huo watapeleka wachezaji wachache tu ,wachezaji hao mpaka sasa wanaendelea na mazoezi  nje ya kambi kabla ya kuondoka nchini kwenda Ugiliki kwenye mashindano hayo ya Dunia June mwaka huu.
                           
Reactions::

DVD Ya 'Super D Boxing Coach' Kupatikana Kesho PTA

Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D (kushoto) akitoa
maelekezo yaliyomo katika DVD yake ya mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa
wadau wa mchezo huo kutoka kulia ni Saidi Chaku, Amri Masare, Zainabu
Kiliware, Edson Joer na Antoni Ruta Dar es salaam leo ambapo VIDEO CD
hazo zitapatikana kwenye mapambano yote ya ngumi nchini,
Reactions::

Wauzaji Nyota SBC Wazawadiwa

Avinash mmoja kati ya wakurugenzi wa kampuni ya  SBC wazalishaji wa vinywaji baridi vya Pepsi akielezea jambo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo katika ukumbi wa New Africa jana usiku wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa wauzaji nyota wa bidhaa za Pepsi kutoka kanda zote za Tanzania.

Ansgar Mnywele ambaye ni  Accounts Development Representative (ADR) kutoka kiwanda cha Pepsi Mbeya akipokea cheti cha utambulisho wa uuzaji nyota wa bidhaa za Pepsi jana jioni katika Hoteli ya New Afrika


Vedast Mgalla  Teritory Development Manager (TDM) kutoka kiwanda cha Mbeya akipokea cheti cha utambulisho wa uuzaji nyota( Sales Star) wa Bidhaa za Pepsi.

Da' Safina mwimbaji wa Bendi ya Kalunde alitoa burudanui kabambe iliyowaburudisha wafanyakazi wa Pepsi na wageni waalikwa.

Wadau wa Pepsi wakisereebuka

Timu ya mauzo na baadhi ya viongozi wa kampuni ya SBC Tanzania katika picha ya pamoja baada ya kutolewa tuzo za wauzaji nyota wa bidhaa za Pepsi. Picha zote:Mjengwablog)
Reactions::

Andrew Chenge

Haya...... kazi kwenu wadau mnaoweza kusoma/kutafsiri picha.
Reactions::

Friday, April 29, 2011

Wafanyakazi Wa Idara Ya Habari Maelezo Wamuaga Clement Mshana


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana (kushoto) akikabidhiwa zawadi iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Afisa Habari Mwandamizi Bi. Anna Itenda (kulia)wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi leo jijini Dar es salaam , Bw. Clement Mshana ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) .
 

 


Wafanyakazi wa Idara ya Habari(MAELEZO) wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Clement Mshana(katikati) mara baada ya hafla fupi ya kumuaga rasmi leo jijini Dar es salaam.
Reactions::

TBL Yachangia Maandalizi Ya Mwanza Heroes

Meneja wa mauzo wa kampuni ya bia Tanzania TBL tawi la Mwanza bw. Maliki Sitaki akikabidhi fedha taslimu shilingi milioni 1.5 kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro kama sehemu ya mchango wa kampuni yake kusaidia maandalizi ya awali kwa timu ya mkoa wa Mwanza (Mwanza Herous) itakayoshiriki michuano ya ligi ya Taifa inayotaraji kuanza kutimua vumbi may 7/2011.(Picha:Mdau Mwanza)
Reactions::

Wawili Wafa Katika Ghasia Kampala

Watu wasiopungua wawili wameuawa huko Kampala, mji mkuu wa Uganda katika ghasia za kupinga unyanyasaji anaofanyiwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.
Bofya Video ya ghasia Kampala
Majeshi ya usalama yalifyatua risasi za moto na za mpira pamoja na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.
Bw Besigye alilazimika kutibiwa baada ya kunyunyizwa gesi ya kutoa machozi ndani ya gari yake kabla ya kuburuzwa kuingia kwenye karandinga la polisi alipokamatwa siku ya Alhamisi.
Hiyo ilikuwa mara ya nne mwezi huu kukamatwa kutokana na kushiriki kwake "maandamano ya kutembea kwenda kazini" kupinga kupanda kwa gharama za maisha.
Rais Yoweri Museveni amesema kampeni hiyo ya kutembea kwenda kazi inafanyika kinyume cha sheria.
Baada ya kukamatwa kwake, Dr Besigye alifunguliwa mashtaka ya uchochezi lakini akaachiliwa kutokana na sababu za kiafya mpaka tarehe 2 Mei.
Kulikuwa na taarifa kuwa kiongozi huyo wa upinzani alikataliwa kutoka nje ya nchi, ingawa hatimaye aliruhusiwa kuondoka kwenda Nairobi kutibiwa.
Reactions::

Historical Royal Wedding, Prince William And Kate



Today.
Reactions::

Achana Na ' Royal Wedding' In Europe ', Hii Ni ' Rural Wedding' In Africa!


Harusi hii ' simpo' kabisa niliikuta kijijini Chala, Nkasi, Sumbawanga mwaka 2008. Bwana na Bibi harusi walikwenda kanisani kwa miguu. Baada ya ndoa kufungwa taratibu wakarudi nyumbani kwa miguu. Ndugu, jamaa na marafiki walijumuika kwa furaha kubwa. Je, hapo pichani mnaweza kumwona Bi Harusi? Naam. Sumbawanga kuna mambo!
Reactions::

Wabunge Wapya Wamvaa Katibu Wa Bunge


Spika Makinda

Katibu wa Bunge Thomas Kashilila

Joseph Mbilinyi, mmoja wa wabunge vijana wapya kutoka kambi ya upinzani                                         BAADHI ya wabunge vijana wa vyama vya upinzani wamelaani kauli iliyotolewa na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah na kueleza kuwa wao ni vinara wa
sheria na kanuni kuliko hata Spika wa Bunge, Bi. Anna Makinda.

Vile vile wameahidi katika bunge la bajeti watatoa hoja bungeni na kumtaka katibu huyo kufuta na kuomba radhi kwa kauli yake ya kuwaita wabunge mbumbumbu wa sheria na kanuni.


Dkt. Kashililah akizungumza na vyombo vya habari juzi, alisema kuwa vitendo vya fujo na kutoleana maneno ya kejeli baina ya wabunge wakiwamo ndani ya bunge, ni matokeo ya kuwepo kwa wabunge wengi wapya na wasiojua vema sheria na kanuni za bunge.


Wabunge hao walisema kuwa kauli ya Katibu wa Bunge imewadhalilisha wao, bunge na wananchi kwani amedharau wananchi kwa kuwa wamechagua wawakilishi mbumbumbu wa sheria na kanuni.


Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Bw. Ezekia Wenje alisema kuwa katika bunge la mwezi wa sita atapeleka hoja bungeni ya kumtaka Katibu huyo wa Bunge kuomba radhi na kufuta kauli yake hiyo.


"Kutuambia wabunge ni mbumbumbu ni madharau makubwa sana na utovu wa nidhamu. Zile kanuni si dictionary wala biblia, huhitaji mwezi mzima kujifunza, ni ndani ya wiki moja tu umeshajifunza kwani ni kajitabu kadogo sana," alisema.


Kwa mujibu wa Bw. Wenje, wabunge vijana hawakubali kuburuzwa bungeni na wanakuja juu pale wanapoona kanuni zinavunjwa kwa manufaa ya kundi fulani.


"Wakiona wamebanwa kwenye vifungu, wanaamua tu kutengua kanuni, sisi hatutakubali na hatutanyamazishwa, tutaendelea kusema," alisema.


Mbunge wa Mihambwe (NCCR-Mageuzi), Bw. Felex Mkosamali alisema kuwa kwa upande wake amesoma sheria na kanuni na kufauli vizuri masomo hayo, hivyo anao uwezo mkubwa na upeo wa masomo hayo.


"Mtu kama mimi ni mwanasheria nimeenda darasani na maprofesa wamenipa A kwenye masomo hayo, sasa anataka hawa maprofesa kutuambia hawana akili?


"Spika tunajua si mwanasheria na ndiyo maana mbunge anapotoa hoja anamkatisha kabla hajamaliza. Tunaijua sheria na kanuni kuliko huyo spika anayemtetea," alisema Bw. Mkosamali wakati akizungumza na gazeti hili jana.


Aliongeza kuwa kauli ya Bw. Kashillilah imewadhalilisha na kusisitiza kuwa, kwa kuwa kipimo cha kwenda shule ni vyeti, hivyo alimtaka Spika kutoa vyeti vyake alivyosomea masomo hayo ili vilinganishwe na vya kwake.


"Wametudhalilisha sana, nia yao wanataka kutunyamazisha tukiwa bungeni...mwezi wa sita tunakwenda kuwasha moto ndani ya bunge," alisema.


Mbunge mwingine wa NCCR-Mageuzi wa jimbo la Kigoma Kusini, Bw. David Kafulila, hali kadhalika alilaani kauli hiyo na kusema kuwa fujo ndani ya bunge hazisababishwi na wabunge vijana tu, kwani wapo wazee wa siku nyingi ambao wamekuwa vinara wa fujo ikiwa ni pamoja na kutojua kanuni na sheria.


Alisema alichotakiwa kusema Katibu wa Bunge ni kuwataja wale wasiojua kanuni na sheria lakini anaposema wabunge wapya hawazijui, ni kuwadhalilisha wao na bunge lenyewe.


Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi. Ester Bulaya naye alipinga kauli ya Katibu huyo wa Bunge kuwa tatizo si kutozijua kanuni, bali wengi wa wabunge wanashindwa kutawala jazba zao na baadhi wana uchanga wa kisiasa.


Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa wabunge kuendelea kujifunza taratibu za bunge ili waweze kutoa hoja za msingi huku wakizuia jazba zao.
Reactions::

Vodacom Wadhamini Tena Vodacom Miss Tanzania 2011

Mratibu wa mashindano ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akifafanua jambo katika semina ya waandishi wa Habari inayofanyika katika hoteli ya Paradise jijini Dar es Salaam, semina hiyo inahusu masuala ya ushiriki wa mashindano la kumpata mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2011 ambapo kwa mara nyingine tena Vodacom wamejitokeza kudhamini mashindano hayo mwaka huu kuanzia ngazi ya vitongoji.

 Waandishi wa Habari wakiwa katika Semina hiyo inayoendelea katika hoteli ya Paradise jijini Dar es Salaam. (Picha:Mjengwablog)
Reactions::

Tukutane Daispora DC Mwezi Wa Kumi

Watanzania: Seattle, WA  na  Portland, OR

Kwa niaba ya Mwenyekiti  TANZASEATTLE nawakumbusha kuwa sherehe zetu za Muungano ni Jumamosi
hii tar. 30/4/2011 katika ukumbi wa Eritrean Association Hall (1528 Valentine
Place South, Seattle, WA, 98144). Sherehe zitaanza saa kumi jioni.

Kiingilio ni dola 15 (utapata chakula, utaburudika kwa fashion show, utapata
burudani ya ngoma, utacheza muziki mpaka majogoo). Vinywaji vitauzwa ukumbini (maji na soda ni dola moja moja, bia dola 3). Tutapokea cash au check tu.

Niwakumbushe tu kuwa Fashion show itaongozwa na dada ASIA IDOROUS- KHAMSIN
kutoka Taxes, Ngoma na  Mr. Kedmon Mapana (Jiandae kucheza ngoma, usisahau khanga za kujifunga) , Muziki na DJ Dully).

Tafadhali usikose, alika jamaa  na marafiki (wageni wote watalipa kiingilio kama
kawaida)
=================   NJOO TUSELEBUKE
Reactions::

Zara Tours Wadhamini Wengine Tuzo Za Wanamichezo Bora Wa 2010

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinatangaza kuwa kampuni ya utalii iitwayo Zara Tours Limited ya mkoani Arusha imejitosa kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2010.

Zara Tours itadhamini tuzo hizo kwa kumpa ziara ya siku tano atakayeibuka Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2010 kutembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti kwa nia ya kutangaza utalii hapa nchini.

TASWA inamshukuru Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Zainab Ansell kwa udhamini huo, ambapo mshindi huyo akiwa huko yeye pamoja na mtu mwingine atakayeamua kuambatana naye watapata huduma zote za watu mashuhuri.

Pia mshindi ataambatana na mwandishi wa habari mmoja.

Udhamini huo sasa umeongeza zawadi atakazopata mshindi, ambaye pia atapewa gari aina ya Toyota Cresta GX 100 kutoka kwa wadhamini Kampuni ya Bia ya Serengeti na Dekoda kutoka MultiChoice Tanzania.

Pia
atalala kwa siku moja hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam.

Pia naomba kutoa ufafanuzi kuwa TASWA inatafuta wanamichezo bora wa mwaka 2010 na si wa mwaka 2011 kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

Tayari orodha ya vyama ambavyo wanamichezo wake watapewa tuzo tumeshaitangaza na wengi wa wanamichezo hao wanatokana na mapendekezo ya vyama vyao ukiacha michezo michache ikiwemo soka.

Soka kama tulivyotangaza juzi kwenye mkutano na waandishi wa habari, kwamba kulikuwa na Kamati Maalum iliyoteuliwa ikiongozwa na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na baadhi ya wajumbe wa TASWA kulingana na vigezo ambavyo vipo kwa tuzo hiyo.

Pia ieleweke mshindi upande wa soka si kwamba ndiye moja kwa moja atazawadiwa gari, maana tuzo yetu si ya Mwanasoka Bora wa Mwaka, ila kinachofanyika mshindi wa kila mchezo atashindanishwa na wenzake wa michezo mingine ili kumpata Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2010, ambaye atapewa hilo gari.

Lakini kwa vile kila mchezo una majina matatu, washindi wa kila mchezo nao watapewa zawadi ya fedha taslimu, ambayo tayari imeshatangazwa na watahesabika ni washindi wa mchezo husika mwaka 2010.

Ahsanteni.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
29/04/2011
Reactions::

TAWLA Waunda Jukwaa La Jinsia Kuhusu Katiba

Mwenyekiti wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Maria Kashonda (katikati) akisoma taarifa kwa waandishi wa habari leo Idara ya Habari Maelezo kuhusu jukwaa la kijinsia la katiba, Gender Forum Constitution  Review (GFCR) jukwaa ambalo limeundwa na TAWLA kwa kushirikiana naAsasi zisizo za Kiserikali (NGO's). Akielezea malengo ya kuundwa kwa jukwaa hilo alisema kuwa  lengo ni kutoa msukumo na msisitizo kwa Serikali kushirikisha makundi ya kijinsia  hususani wanawake katika mchakato wa kupatikana  kwa katiba mpya. Wengine ni Magdalena Kamugisha (Kushoto) ambaye ni mweneykiti wa (GFCR) na kulia ni Bi Victoria Mandari.

Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa chama cha wanasheria wanawake TAWLA Bi. Maria Kasonda leo Idara ya Habari Maelezo.(Picha;Mjengwablog)
Reactions::

Usukumani, We Acha Tu!




Msukuma hakuulizi utakula ugali na nini? Anakuuliza utakula sato na nini? Na Msukuma hakuletei sato robo au nusu. Atakupa mzima.
Naam. Nilikuwa Usukumani hivi karibuni. Hakika, kwa watani zangu nili-enjoy sana!
Reactions::

Mkanganyiko Wa Leo

Mdau anakanganywa na tafsiri ya maneno haya, ZAWADI, BAKSHISHI, RUSHWA, SEHEMU YAKO, ZA WATOTO, ZA UBANI, ZA SIKUKUU, ZA SABUNI,ZA USAFIRI.
Kwenu Wadau hususani wataalamu wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili (Picha ya matandaoni)
Reactions::

JK; " Jamani Rostam Mmemwona?......"

Ni wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana. Mjini Igunga katika viwanja vya Sabasaba. Mbele ya maelfu ya wakazi wa Igunga na vitongoji vyake waliofurika katika mkutano  wa kampeni. Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Mrisho Kikwete alisika akimnadi Rostam Azizi mgombea ubunge jimbo la Igunga kwa maneno yafuatayo. "Jamani Rostam mmemwaona......."?   Watu.. Ndiyooooo... (Maelezo na Picha:Victor Makinda)
Reactions::

Shein Awasili Nchini Uturuki

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi Hassan Servat Oktem,Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Uhusiano wa Kisiasa wa Nchi wa Wizara ya mambo ya nje ya Jamhuri ya Uturuki,pamoja na viongozi wengine wa nchi humo,alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ankara Nchini Uturuki,akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika ziara Rasmi kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania,Dr Sander Gurbuz,alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ankara Nchini Uturuki,akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Viongozi wengne wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzi bar,katika ziara Rasmi kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania,Dr Sander Gurbuz,(kushoto) na Balozi Hassan Servat Oktem,Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Uhusiano wa Kisiasa wa Nchi wa Wizara ya mambo ya nje ya Jamhuri ya Uturuki,(kulia) pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya Uturuki jana alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ankara Nchini Uturuki,akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Viongozi wengne wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzi bar,katika ziara Rasmi kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo.
Reactions::

Obama Aomboleza Maafa Ya Alabama


Mamia ya watu wamefariki baada ya vimbunga vikali kupiga kusini mwa Marekani           
Rais Barack Obama amesema serikali yake itafanya kila juhudi kusaidia wakaazi wa jimbo la Alabama kufuatia athari za dhoruba kali na kimbunga.
Zaidi ya watu 280 wameuawa na uharibifu mkubwa umefanyika katika jimbo hilo la kusini mwa Marekani.
Serikali imetangaza hali ya hatari katika eneo hilo ambako watu wamelazimika kuondoka kwenye makaazi yao.
Maafa na uharibifu pia yametokea katika majimbo ya Tennessee, Mississippi, Georgia na Virginia.
Rais Obama amesema ataelekea Alabama kuugana na familia za walioathirika na makundi yanayotoa misaada ya dharura kwa wakaazi wa eneo hilo.
Shirika la kitaifa la kutabiri hali ya hewa nchini Marekani, limesema eneo hilo la kusini mwa marekani limepigwa na msururu wa vimbunga 300 tangu ijumaa wiki iliopita. Vimbunga venye nguvu zaidi vilipiga jumatano wiki hii.
Kufikia jana zaidi ya watu milioni moja walikuwa hawana huduma za umeme.
Wanajeshi 2,000 wametumwa kusaidia katika harakati za uokozi.BBC
Reactions::

Raia 82 Wa Somalia Wakamatwa Msituni Morogoro

    Kundi la Wasomali likiwa chini ya ulinzi kwenye kituo kiku kikuu cha polis mkoan Morogoro                                                                                                                                                        WATU wapatao 82 raia wa Somalia wamekamatwa jana mchana kwenye msitu wa moja ya vijiji vya Wilaya ya Gairo mkoani hapa wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam kutafuta maisha.

Akizungumza na mtandao huu kwenye kituo kikuu cha  polisi mkoani hapa, askari mmoja wa kikosi cha kutuliza ghasia wilayani Gairo maarufu kwa jina la 'voda fasta'alisema Wasomali hao walikamatwa baada ya polisi kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

"Tumepokea taarifa kutoka kwa raia wema wakitujuza kuwa kuna kundi la wasomali wanakata mbuga katika misitu ya Vijiji vya Gairo hivyo baada ya kuwafuatilia tumewakamata na kuwaleta hapa mkoani," alisema afande huyo aliyekataa kutaja jina lake kwa kuwa sio msemaji mkuu wa jeshi la polisi.

Mwandishi wetu aliwashuhudia Wasomali hao wakishushwa kwenye roli huku wakiwa na matope hali inayoonesha kuwa huenda wana muda mrefu hawajaoga kutokana na kutembea kwa muda mrefu. (Globalpublishers)      
Reactions::

Kwa Wadau Wa Habari Wote

Ndugu,
Salaam katika upendo

Hii ni kuwajulisha kuwa mtandao mkubwa wa habari ujulikanao kama http://thehabari.com umeanzishwa kwa kushirikiana na baadhi ya wanataaluma wa tasnia ya habari nchini Tanzania na baadhi ya wanahabari kutoka Tanzania walioko Los Angeles, Marekani kwa shughuli mbalimbali. Mtandao huu ulianza kazi tangu Novemba mwaka 2010 na sasa unaendelea kuongeza wadau na wachangiaji ili kukidhi malengo ya mtandao.

The Habari.com ni mtandao wa kizalendo unaokuletea habari za kijamii, kisiasa, burudani na teknolojia. Tupo hapa kushirikiana na waTanzania wenzetu popote walipo duniani katika kuelimishana na kufahamishana mustakabali mzima wa nchi yetu. Tumedhamiria kuleta habari kwa uwazi na umakini bila uwoga wala upendeleo wa aina yeyote.
Tuna amini katika falsafa ya habari kuwa habari ni watu na watu wenyewe ndiyo sisi, hivyo basi tushirikiane katika kuendeleza gurudumu la maendeleo katika nchi yetu tuipendayo ya Tanzania.

Ukiwa kama mdau unakaribishwa kutuma, kutoa taarifa, kuchangia ushiriki na hata kutoa maoni yako. Asante kwa kupokea. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi;

Joachim Mushi
Mhariri wa The Habari.com Tanzania
0717030066, 0756944670,
Mail; mushi@thehabari.com
Or tembelea; joemushi.blogspot.com
Reactions::

Msamaria Mwema Anataka Kumsaidia Yohana...


Kaka mjengwa.

Ni matumanini yangu u mzima.

Niliona tangazo la kaka Yohana kwenye blog yako likanigusa baada kusoma.
Nimesha wasiliana na mwenye baskeli hapa ingawa ni baskeli ya used na Ijumaa hii nakwenda kuiona naamini iko kwenye hali nzuri na itamsaidia kaka Yohana.

Mimi ntakuwa nyumbani Tanzania June 3, na nitawasili na ndege ya QATAR. Ningeomba kama kuna njia yeyote ili niweze kupitisha baskeli pale airport bila kutozwa ushuru mkubwa ningeshukuru.

Mdau,
Canada.

Mdau
Reactions::

Mtani Wangu Anapata ' Bakuli' L a Uyoga!



Anaitwa Isike Maganga, mtani na rafiki yangu wa siku nyingi hapa Iringa. Ni Mnyamwezi anayetoka kijiji kimoja na Profesa Ibrahim Lipumba, Ilolangulu, Urambo.
Reactions::

Thursday, April 28, 2011

Sweden Yapongeza Ubunifu Wa Tanzania...


 Photo: Mjengwablog

Speech at the Lauching Ceremony of Diploma in Adult and Continuing Education at the Institute of Adult Education

The Institute of Adult Education in collaboration with Karibu Tanzania Association have developed a Diploma in Adult and Continuing Education through Open and Distance Learning. The programme is planned for capacity building to teachers of Folk Development Colleges and other adult educators on matters related to facilitation/teaching of adults. The programme will be pursued for a minimum of three and maximum of four years to allow participants have sufficient time to accomplish the proposed modules.

Emphasis will b on learning by place emphasis on reason, reflection and practical thinking. Ambassador Lennarth Hjelmåker from the Swedish Embassy attended the launching ceremony of the programme and held a speech in which he emphasized the linkages between the model of Swedish Folk High Schools and Folk Development Colleges in Tanzania. He also stressed the importance of adult education and education for democracy and human rights related to community development. Read the speech; http://www.swedenabroad.com/Page____124239.aspx
Reactions::

Magufuli Azindua Bodi Ya TAMESA


Waziri wa Ujenzi Daktari John Magufuli April 28,2011 akizindua Bodi za Ushauri za Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) na Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) Dar es salaam. Picha zote na Mwnakombo
Jumaa-MAELEZO
Reactions::

Bodi Mpya Ya TAMESA

Imezinduliwa leo na Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli ( Picha: Mwanakombo Jumaa, MAELEZO)
Reactions::

Lady Jay Dee In Stockholm!



The Best Female artist in East Africa Lady Jay Dee has Landed in Stockholm Ready for The Biggest Spring Party in Stockholm SPRING BREAK 2011 which will be on Friday night 29 APRIL...

STOCKHOLM Lets all come together and enjoy the Spring in Style....

GOOD PEOPLE
GOOD MUSIC....

YOUR MOST WELCOME..

Reactions::