Tuesday, May 31, 2011
Tanzania Yaadhimisha Siku Ya Kupinga Matumizi Ya Tumbaku
| Reactions:: |
Yaliyojiri Kikao Cha Baraza La Madiwani Temeke;Shilingi bil. 2.5 Zatumika Ulipa Fidia Wakazi Wa Gezaulole
![]() |
| Mstahiki Meya wa wilaya ya Temeke (kulia) Maabad Hoja akiingia katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za manispaa ya Temeke kwa ajili ya kuanza kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo. |
![]() |
| Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Eng.Gaston Gasama akijibu maswali ya madiwani wa wilaya hiyo wakati wa kikao cha baraza la madiwanikilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke. Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Maabad Hoja. |
![]() |
| Madiwani wa wilaya ya Temeke wakiwa katika kikao chao leo kinachofanyika kila baada ya miezi katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke. (Picha: Anna Nkinda - Maelezo) Shilingi bilioni 2.5 zimetumika kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi 313 kati ya 427 kwenye mradi wa upimaji viwanja Gezaulole wilayani Temeke. Hayo yamesemwa leo na ofisa mipango miji wa manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo wakati akitoa taarifa ya maendeo ya mradi huo katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo. “Zoezi hili linaendelea vizuri hadi kufikia jana tumeshalipa fidia ya shilingi bilioni 2.5 kati ya shilingi bilioni 2.8 zinazotakiwa kulipwa fidia kwa wananchi hao ambao ni sawa na asilimia 79,” alisema Kagimbo. Aliendelea kusema kuwa maradi huo ambao ni wa awamu ya kwanza unajumla ya viwanja zaidi ya 700 na tayari zoezi la uchukuaji fomu limeshakamilika jana ambapo urudishwaji wake mwisho ni ijumaa ya tarehe 3 mwezi wa sita mwaka huu. Kagimbo alifafanua kuwa mradi wa awamu ya pili uko katika mchakato na tayari fedha za fidia za kuwalipa wananchi zimeshatengwa ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni sita. Alisema, “Kabla ya kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunatarajia kupima viwanja zaidi ya 4000 katika eneo la Gezaulole na mara baada ya kukamilika kwa zoezi hili tutawajulisha wananchi ili waweze kutuma maombi kwajili ya kupatiwa viwanja.” Mradi huu ulianza mwaka 2007 lakini ulisimama kutokana na ufinyu wa bajeti kwa ajili ya upimaji na ulipaji wa fidia kwa wananchi hivi sasa mradi huo unaendelea baada ya manispaa hiyo kupata fedha za mkopo kutoka Benki ya Rasilimali (TIB) na wizara ya Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi. (Imeandikwa na Anna Nkinda-MAELEZO) |
| Reactions:: |
CAG, PPRA Wasaini Hati Ya Mkataba Wa Makubaliano Ya Mashirikiano Ya Ukaguzi
| Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovic Outoh (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa PPRA (CEO-PPRA) Dr. Ramadhan Mlinga (kushoto) Mei 31,2011 jijini Dar es Slaam wakisaini hati ya mkataba wa makubaliano ya mashirikiano ya ukaguzi katika sekta za umma kwa maboresho zaidi |
| Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovic Outoh (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa PPRA Dr, Ramadhan Mlinga (kushoto mwenye miwani) Mei 31,2011 jijini Dar es Slaam wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano wa ukaguzi katika sekta za umma nchini |
| Picha ya pamoja baina uongozi wa ofisi ya CAG na PPRA. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO). |
| Reactions:: |
Mbunge Abood Asisitiza Umuhimu Wa VICOBA Kwa Uchumi Wa Jamii
| Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa benki ya wananchi vijijini (VIKOBA) ya Ngoto A kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoroeneo la Masika, wa pili kutoka kushoto ni Diwni wa kata hiyo Mohamed Lukwele. (Picha:Juma Mtanda) MBUNGE wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood ametoa wito kwa benki za wananchi vijijini (VIKOBA) kuongeza juhudi za kuingiza wanachama wengi kwani vikundi hivyo vimekuwa suluhisho la kutatua matatizo mbalimbali katika jamii ya vikundi hivyo mkoani hapa. Akizungumza katika uzinduzi wa kikundi cha Ngoto A kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro Abood alisema kuwa benki za wananchi vijijini zikisimamiwa vizuri na viongozi pamoja na kuongeza idadi kubwa ya wananchama suala ya umakisini kwa mwanancham moja moja wa vikundi hivyo litapungua kwa jiasi kikubwa. Abood alisema kuwa ipo haja kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro kujiunga na vikundi mbalimbali vilivyopo katika kata zote 29 za Manispaa hiyo kwani utafiti umeonyesha kusaidia wanachama wake na jamii inayozunguka katika matatizo mbalimbali. “nimetembelea vikundi hivi karibu vikundi 15 vya Manispaa yetu na kuelezwa kuwa malengo makubwa ni kusaidiana katika matatizo ya kijamii ikiwemo msiba, ulipaji wa ada ya wanafunzi shuleni, kutoa ajira kwa vijana sasa malengo ya vikundi hivi ni mazuri” alisema Abood. Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Ngoto A, Salum Ally alisema kuwa kikundi hicho kina aina tatu za uchangiaji ikiwemo mfuko wa maendeleo wa jamii, hisa na kutoa mikopo kwa wanachama ambapo mwanakikundi hurejesha fedha katika kikundi kwa liba ya 5% ya fedha anazokopo. Mwenyekiti huyo alisema kuwa kikundi hicho kina jumla ya wanachama 33 wanaume wakiwa 14 na wanawake 19. Katika Manispaa ya Morogoro ina jumla ya benki za wananchi vijijini 220 (VIKOBA) katika kata zake 29 na inakadiriwa kuwa na wananchama zaidi ya 500. (Imeandikwa na Juma Mtanda) |
| Reactions:: |
Oxfam: Bei Za Vyakula Kuwaumiza Maskini
![]() |
Ongezeko la bei za vyakula litawaathiri watu maskini zaidi ambao tayari wanahangaika kununua chakula cha kutosha, wakitaka mabadiliko makubwa kwa mfumo mzima wa chakula duniani, Shirika la Oxfam limeonya. Inakadiriwa kuwa mpaka mwaka 2030 bei ya wastani ya mazao muhimu itapanda kwa asilimia 120 hadi 180, kwa mujibu wa makadirio ya wahisani.Huu ni mwendelezo wa hali ambayo tayari imeshuhudiwa ya kupanda kwa bei za vyakula mara mbili katika kipindi cha miaka 20. Nusu ya ongezeko lijalo la bei za vyakula litakuwa ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, Oxfam limetabiri. Limetoa wito kwa viongozi wa dunia kupitia upya mfumo wa masoko ya vyakula na kuwekeza fedha zaidi katika mfuko wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani. "Mfumo wa vyakula lazima upitiwe upya iwapo tunataka kukabiliana na changamoto zinazooongezeka za hali ya hewa, ongezeko la bei za vyakula na upungufu wa ardhi ya kutosha, maji na nishati” alisema Barbara Stoking, Afisa Mtendaji wa Oxfam. Bei za vyakula tayari zilishapanda zaidi ya mara mbili tangu 1990, kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), na Oxfam linatabiri kuwa hali hii itaendelea kuongezeka kwa miaka 20 ijayo. Katika taarifa yake, Oxfam linasema makadirio yanaonyesha kuwa idadi ya watu duniani itafikia bilioni tisa ifikapo mwaka 2050 lakini wastani wa mazao ya kilimo ulishapungua kwa karibu nusu tangu mwaka 1990.BBC |
| Reactions:: |
Washindi Wa 'TUSKER Million 500 Kwa Mashabiki' Wakabidhiwa Zawadi
![]() |
| Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Caroline Ndungu wa pili kutoka kushoto akimkabidhi Robert Zablon ambaye ni mshindi wa milioni moja katika shindano la Tusker Milioni 500 kwa mashabiki mfano wa cheki yenye tamani ya shilingi milioni moja katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Tusker Rittah Mchaki na kulia ni Mkurugenzi wa Utawala Eric Adadevoh.Jumla ya washindi1883 wameshinda zawadi katika shindano hilo linaloendelea mpaka mwezi julai kati yao washindi 1625 wa shilingi 10,000 kila mmoja , 188 wameshinda shilingi 50,000 kila mmoja , washindi 53 wameshinda shilingi 100,000 kila mmoja na washindi 17 wameshinda shilingi milioni 1,000,000 kila mmoja |
![]() |
| Washindi wa shilingi milioni moja katika shindano la Tusker Milioni 500 kwa mashabiki pamoja na viongozi wa kampuni ya bia ya Serengeti kutoka kulia ni Robert Zabrlon, Mkurugenzi wa Utawala (SBL) Eric Adadevoh Simon Jacob, Caroline Ndungu Mkurugenzi wa Masoko (SBL) Othamn Seif na Meneja wa kinywaji cha Tusker Rittah Mchaki .(Fullsahangweblog) |
| Reactions:: |
Mstahiki Meya Dar es Salaam: Hii Ni Aibu Yako, Ni Aibu Yetu!
Dar es Salaam ilikuwa kijiji enzi zile za Mzizima. Sasa ni Jiji. Picha hii ni ya mchana wa leo. Haya pichani yako barazani mwako Mstahiki Meya, tena eneo lenyewe ni Masaki, je, kule Tandale mambo yakoje? Kipande hiki cha barabara kinachoelekea Slip Way na hotel ya Double Tree hakizidi mita mia tatu. Hilo ni eneo muhimu kiuchumi ikiwamo makusanyo ya kodi. Kila uchao kinazidi kuwa kero na hatari kwa waendesha magari kuvamiwa na vibaka hususan giza linapoingia. Maana, mashimo hayo ni sharti uendeshe kwa mwendo wa kinyonga.
Mstahiki Meya Wa Jiji; Naahidi nitakuwa nakukumbusha juu ya kipande hiki cha barabara kwa picha mpaka pale litakapopata sura nyingine.
| Reactions:: |
Wenye Wivu Wajinyonge; Msamvu Kwa Bi Mkora!...
Wali wa nazi kidogo, mchicha wa chukuchuku kidogo, kachumbari kidogo, tango, embe la Matombo, na harage pia. Wenye wivu wajinyonge!
| Reactions:: |
CUF Kuandamana Kupinga Mauaji Ya Kila Kona
![]() |
| CHAMA Cha Wananchi Cuf (CUF) kinaandaa maandamano makubwa kupinga mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi kila kona ya nchi ya kuwauwa raia wasio na hatia yakiwemo mauaji yaliyotokea Jimbo la Urambo kata ya Usinge mkoani Tabora. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Katibu wa CUF Bw.Julius Mtatiro alisema matukio hayo ambayo yamekuwa yakijitokeza kila mara yanadhihirisha namna serikali ilivyo dhaifu kwa sababu kila mamlaka inafanya vile inavyotaka. Pia alisema matukio ya namna hiyo kwa wananchi wasio na hatia kuuwawa,kunyanyaswa, kukamatwa na kubambikiziwa kesi ...soma zaidi http://www.kwanzajamii.com |
| Reactions:: |
Banda La TA Reading Latingisha Ndani Ya Reading Carnival
![]() |
| Dello Akifanya makamuzi ya kuku wa kuchoma |
![]() |
| Mh Naibu Balozi akiwa na wadau wa Reading wakati wa Carnival |
![]() |
| Umati ulikuwa wa kutisha |
![]() |
| Wadau wa reading wakila pozi ndani ya banda na TA Reading wakiwa na Berry Black. Kwa mara ya kwanza TA Reading ikishirikiana na TANZ UK waliandaa banda la kitanzania kwa kupika chakula cha Kitanzania na kuuza kwa wadau mbalimbali waliojitokeza kutembelea banda la TA ikiwa ni mojawapo ya mradi wa kuchangia mfuko wa TA Reading. Mgeni rasmi alikuwa Mh Naibu Balozi wa Tanzania Uingereza Chabaka Kilumanga alieambatana na Afisa wa Ubalozini Amosi Msanjila. Kwa ujumla banda ka kitanzania lilitia fora kuliko mabanda yote mengine ya mataifa mbalimbali. Asanteni URBAN PULSE CREATIVE |
| Reactions:: |
Tunachota Maji....
TPHA PRESS RELEASE IN RESPONSE TO TOBACCO ADVERTISEMENTS
![]() |
| A PRESS RELEASE BY THE TANZANIA PUBLIC HEALTH ASSOCIATION IN RESPONSE TO THE BREACH OF THE TOBACCO PRODUCT CONTROL ACT (2003) AND THE WORLD HEALTH CONVENTION ON TOBACCO CONTROL Currently more than 4 million people die globally per year, because of illnesses related to tobacco use, and projections show a threatening increase in tobacco related deaths by the end of the first quarter of the 21st century. It is important to note that, 70% of the projected 10 million "tobacco associated deaths" in 2020 shall occur in the developing world, where the number of deaths due to communicable and other non-communicable diseases is already the highest. Illnesses related to tobacco use, include but are not limited to: the cancers of the respiratory and digestive tracts, hypertensive conditions, diabetes and reproductive disorders. The World Health Organization has proactively established the Framework Convention on Tobacco Control (FCTC) to bring about awareness of the many tobacco hazards, by involving world nations to address tobacco control among major priorities in global health. The FCTC contains guidelines and requirements for the implementation of the most cost-effective tobacco control measures. Key provisions that parties to the FCTC (i.e. countries that have ratified the convention) are required to implement include: a) a comprehensive ban on tobacco advertising, sponsorship and promotion within five years of ratification, b) strong health warnings on tobacco packaging that cover at least 30% (and ideally 50%) of the principal display areas within three years, c) protection with immediate effect of everyone from secondhand smoke in all indoor workplaces, public places and in public transportation, and d) to introduce strong measures to reduce the smuggling of tobacco products. Almost simultaneously with this WHO initiative, Tanzania enacted its first National Tobacco Control law (The Tobacco Product Control Act, TPRA 2003), and in April 2007 ratified FCTC. In this aspect Tanzania Government showed the best intention of giving the highest regard to the health of its citizenry. Similar to FCTC, TPRA (2003) Part IV Section 26 prohibits tobacco advertising, sponsorship and promotion, and among other things the Act also prohibits Tobacco companies to mislead the public on tobacco hazards. However, it is extremely disappointing to note that the tobacco control law passed in 2003, is not being enforced across the country, primarily due to the absence of or inadequate directives and guidelines for its implementation. Tobacco advertising continues to feature prominently at all strategic public areas and in news papers. In this context, recently in breach of FCTC and TPRA (2003) Tobacco Company named Tobacco Republic Holding Co. Limited, was advertising Silver Leaf cigarette brand through some popular local newspapers. The firm uses misleading messages like “HIGH QUALITY CIGARETTE REDUCES DANGER TO YOUR HEALTH”, and is actually looking for agents to paddle its products. This message contravenes both international and national laws; it is not only a lie presenting misleading information, but has the intention of fooling people into buying and using hazardous product which will slowly destroy healthy Tanzanians with tobacco related illness. In essence, this is an insult to Tanzanian public, the Tanzania Government and the World Health Organization, who all together, are aware that tobacco in all its forms, regardless of the “advertised” quality, usually attractively packaged, is very dangerous to human health in the long run. With regard to this issue, The Tanzania Public Health Association (TPHA) first of all calls upon the Tanzanian public to be aware of a hidden agenda of that Tobacco Company that wants to entice people to its dangerous products; please be wise to ignore the advertisements and save your health and lives. The company totally ignores our national laws and international laws, and should be taken to task for doing so. Secondly, TPHA calls upon the Government of Tanzania, through the Ministry of Social Welfare and the law enforcement agents, to take urgent and necessary measures to hold this company accountable, and that all forms of tobacco advertisement should be banned, and the culprit be sued for contravening the country’s laws. Thirdly, the Association calls upon all public health activists to join hands, and assist the government to ensure that such abuses of business and trade ethics cease immediately, and are not repeated within the boundaries of this country. We should all protect our youth from these glamorous advertisements packaged with deadly lies and misinformation. Tobacco products are hazardous to health, tobacco kills!! |
| Reactions:: |
Monday, May 30, 2011
Wachina Wachaingia Riadha Milioni Tano
| JUMUIYA ya wafanyabiashara wa Kichina waishio Tanzania imetoa hundi ya sh .milioni tano kwa ajili ya kuchangia mashindano ya riadha ya Afrika Mashariki na Kati. Hundi hiyo ilikabidhiwa leo na Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Wu Quansheng kwa Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania , Suleiman Nyambui na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Henry Lihaya katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dares Salaam. Akikabidhi hundi hiyo Quansheng alisema mbali na kutoa mchango katika sekta ya michezo pia wataendelea kuchangia kwenye shughuli mbalimbali. Akizungumzia kuhusu mashindano hayo ambayo yataanza Juni 3,mwaka huu, Lihaya alitoa wito kwa watu mbalimbali kuendelea kutoa michango yao kwa kuwa misaada bado inahitajika. Kwa upande wake, Nyambui alisema maandalizi ya mashindano yanaendelea vizuri ,ambapo tayari vifaa vya kisasa vitavyotumika vimeshafungwa. Alitoa wito kwa wannachi kushiriki kwa wingi katika mashindano hayo ambayo ni bure. Aliongeza kuwa mashindano hayo yanaanza saa 2.00 asubuhi, siku ya Ijumaa wiki hii na kumalizika Jumamosi. Nyambui alisema aliitaja bajeti ya mashindano hayo kuwa ni sh. milioni 113, ambapo hadi sasa Shirika la Fedha Duniani(IMF) limetoa sh. milioni 20 na kampuni moja kutoka Arusha imetoa sh. 1.5na wadau wengine wameahidi kutoa maji ya kunywa. Jumla ya nchi 10 zinatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo.IMEANDIKWA NA MAGRETH KINABO – MAELEZO |
| Reactions:: |
Watoto Elfu 35 Wamekimbia Abyei
![]() |
| Shirika la kimataifa la kuwasaidia watoto, Save The Children, linasema kuwa watoto elfu-35 nchini Sudan wamelazimika kukimbia makwao kwa sababu ya mapigano katika eneo la mzozo la Abyei. |
Abyei inaaniwa na Sudan Kusini na Kaskazini, na sasa inakaliwa na jeshi la Sudan Kaskazini.
Wakati huo-huo, Sudan Kusini inajitayarisha kujitenga na kaskazini mwezi wa July.
Fujo katika jimbo la Abyei zimezidi tangu mapigano yalipoanza mapema mwezi huu.
Save The Children inasema karibu wakaazi wote wa mji wa Abyei wamehama makwao, huku kukiwa na ripoti za mapigano, makaazi kuchomwa moto na uporaji.
Shirika hilo linakisia kuwa watoto 35-elfu wamekimbia na wengi wamepoteana na wazee wao.
Save The Children inasema iko tayari kusaidia lakini mapigano yanayoendelea yanazuwia msaada kufika katika maeneo yaliyoathirika.
Mwezi wa Januari watu wa Sudan Kusini walipiga kura kwa wingi kuamua kujitenga na Sudan Kaskazini.
Lakini kwa vile wanajeshi wa Sudan Kaskazini wameingia katika eneo la mpaka hilo la Abyei, taharuki imezuka tena katika nchi ambayo imekuwa ikijaribu kujikwamua kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo kadha.BBC
| Reactions:: |
Zanzibar Inahitaji Dola za Kimarekani milioni 123 Kumaliza Tatizo La Maji
![]() |
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inahitaji kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 123 kuweza kumaliza tatizo la maji safi na salama kwa Mikoa ya Unguja na Pemba. Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Shariff Hamad ameuambia ujumbe wa viongozi wa Jumuiya ya Madhehebu ya Khoja Shia Ithinashir kwamba tatizo la maji safi na salama linafanyiwa kazi na kwa sasa zinahitajika fedha hizo kuweza kukamilisha miradi ya maji. “Kama mnavyofahamu Zanzibar kuna tatizo la maji, Serikali haijakunja mikono, mipango mbalimbali inafanywa kukabili tatizo hilo” Alisema Maalim Seif. Maalim Seif amesema ikiwa fedha hizo zitapatikana basi matatizo yanayowakabili wananchi wa Visiwa vya Zanzibar kukosa maji safi na salama litakuwa historia hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kuwa na subira. Akizungumzia suala la umasikini,Makamu huyo wa kwanza wa Rais amesema Serikali imedhamiria kuwakwamua wananchi wake katika dimbwi la umasikini kwa kubuni mipango mbalimbali yenye tija kwa umma. Maalim Seif amesema kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na hali ya umasikini, lakini pamoja na hali hiyo, bado kuna matumaini ya kupunguza kwa kiasi kikubwa hali hiyo chini ya mpango mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini(MKUZA) Sekta kadhaa zimetajwa chini ya mikakati ya kupunguza umasikini katika Visiwa vya Zanzibar huku kiwango cha elimu kikitarajiwa kuimarishwa sanjari na ukuzaji wa Sayansi na Teknolojia. Makamu huyo wa kwanza wa Rais, amesema masuala ya afya ya jamii yamekuwa wakipewa kipaumbele ili kujenga jamii yenye afya bora ambayo itashiriki katika uzalishaji mali. Alisema kwa kuwa na watu wenye afya bora kunasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wan chi kwani muda mwingi utatumika katika uzalishaji mali na sio kwenye matibabu, hivyo aliwahakikishia msimamo wa Serikali kuimarisha sekta ya afya Zanzibar. Maalim Seif amepongeza uamuzi wa Jumuiya hiyo kujenga kituo cha afya ambacho kinatumika na wananchi wote ambacho kinazingatia zaidi utoaji huduma kwa njia isiyo ya kibiashara. (Habari:Maelezo Zanzibar) |
| Reactions:: |
Kumbukumbu
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari; Mtemi Milambo Festival Julai 8-10,Tabora
![]() |
TAMASHA la ngoma za utamaduni na maonyesho ya biashara la Mtemi Milambo linatarajiwa kurindima kuanzia Julai 8 hadi 10 kwenye Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa taasisi ya Chief Promotions ambao ndio waandaaji,Amon Mkoga, alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuenzi na kuuendeleza utamaduni wa Kitanzania, hususani makabila makubwa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga na Mwanza, ambao ni Wanyamwezi na Wasukuma. Mkoga alisema pia michezo na maonyesho ya bidhaa zenye asili ya Kitanzania pia vitakuwepo,kama vile mchezo wa bao na kurusha mishale. Alisema, Ijumaa ya Julai 8 shughuli itaanza saa 4:00 asubuhi hadi 12:00 jioni na kuendelea kwa muda huo huo hadi Jumapili Julai 10. Mkurugenzi huyo alizitaja baadhi ya ngoma zitakazokuwemo wakati wa tamasha hilo kuwa ni pamoja na Manyanga, Maswezi, Uyeye, Bagalu, Bagika, Bazuba, Radu na nyinginezo. Naye Meneja wa Bia ya Balimi, ambao ni kati ya wadhamini wa tamasha hilo,Bi Edith Bebwa, alisema wameamua kujitosa kudhamini tamasha hilo kwa mara ya pili ili kuwaenzi wateja wa bia hiyo ambayo ni mahususi kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa. “Ngoma hizi za Wasukuma na Wanyamwezi huchezwa sana wakati wa mavuno, hivyo kwa kuwa Balimi ni bia ya mkulima tumeona tuungane kusherehea pamoja wakati wa mavuno huku tukienzi utamaduni wa Kitanzania,” alisema Bebwa. Mgeni rasmi katika Tamasha hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Abeid Mwinyimusa. Kauli mbiu ya Tamasha hili mwaka huu ni KUSHOKE KUKAYA yaani turudi nyumbani tafsiri ya Kiswahili toka kinyamwezi. Mbali ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi, wadhamini wengine ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ubalozi wa Switzerland ,Kalunde General Supplies, UNESCO na Fly 540(Shirika la ndege),Geita Goldmines, Magic Fm, Channel Ten na TBC. Aksanteni kwa kunisikiliza na karibuni Tabora. Amon Mkoga Mkurugenzi Mtendaji Chief Promotions P.O.Box 78566 Simu: 0755 638 004/0655 638 004 Barua Pepe:dramontz2002@yahoo.com Tovuti:www.chiefpromotions.or.tz Dar es Salaam Tanzania |
| Reactions:: |
Benki Ya NBC Yachangia Mbio Za Mwenge Shilingi Milioni 5
| Mshauri wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi. Robi Matiko-Simba (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Bw. Evans Balama ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki hiyo kwa ajili ya mbio za Mwenge wa Uhuru katika makabidhiano yaliyofanyika Mbeya hivi karibuni. Wengine pichani kushoto ni Meneja wa NBC Kanda ya Nyanda za Juu, Bw. Ramadhani Lesso, Meneja wa benki hiyoTawi la Mbeya, Bw. Salema Kileo (wa pili kulia) na Bw. Lazaro Mwankenja, mmoja wa waratibu wa mbio hizo. |
| Reactions:: |
Baraza La Wafanyakazi Wa Wizara Ya Habari, Vijana, Michezo Na Utamaduni Lafanyika
| Waziri wa Habari , Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akiongea na viongozi na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa Baraza hilo jijini Dar es Salaam na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na kuepuka migogoro mahala pa kazi. Kutoka ni Naibu Waziri Dkt. Fenella Mukangara na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Seith Kamuhanda (kulia) |
| Viongozi na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (Katikati) Naibu waziri Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kutoka kushoto), Katibu mkuu wa wizara Bw. Seith Kamuhanda (wa pili kulia) na Naibu katibu mkuu Bi. Sihaba Nkinga (kushoto). (Picha:Aron Msigwa-MAELEZO) |
| Reactions:: |
Dr Chalse Kimei Mwenyekiti Mpya Wa Bodi Ya Mikopo Ya Serikali Za Mitaa
![]() |
Mheshimiwa Waziri Mkuu amemteua Bwana Charles Kimei ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa. Aidha Waziri Mkuu amemteua Bwana Juma Iddi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo. Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi hiyo ni pamoja na Mh.Didas Masaburi ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Bwana George Lubeleje ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Mpwapwa.Wajumbe wengine ni Bwana Severine Kahitwa ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Bwana Mohamed Mkupete ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Bibi Magreth Nyalile ambaye ni Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha. Pia katika uteuzi huo wapo Mhe.Theresia Msuya ambaye ni Mweneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Mhe.Amir Nondo ambaye ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Uteuzi huo umefanyika kwa Mamlaka aliyopewa Waziri Mkuu chini ya kifungu cha 57(1)-(3) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa sura ya 290 na ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 16/4/2011. (Imeandikwa na Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam) |
| Reactions:: |
FFU Watumia Mabomu Ya Machozi Kutawanya Maandamano Ya Amani Ya Wanafunzi Wa Tosamaganga Sekondari
| HALI ya usalama kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Tosamaganga wilayani Iringa mkoani hapa leo ilikuwa tete baada ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia kulazimika kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya wanafunzi zaidi ya 1000 wa shule hiyo ambao walikuwa katika maandamano ya amani kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya uongozi wa shule hiyo. Pamoja na askari hao kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao kama njia ya kuwazuia wasiandamane bado waandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo wakichukua madai ya wanafunzi hao walizuiwa na polisi hao kuendelea kuchukua habari za wanafunzi hao pasipo kibali cha polisi huku wananchi wa maeneo ya Mseke wakizihama nyumba zao kwa muda na kukimbilia porini kukwepa mabomu hayo. Tukio la mapambano kati ya FFU na wanafunzi hao lilianza majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana kwa polisi kufukuzana na wanafunzi hao kuwarudisha kwa mabomu shuleni pasipo mafanikio baada ya idadi kubwa ya wanafunzi kukimbilia porini na wengi wao kujificha porini na katika nyumba za wenyeji wa maeneo hayo. Kabla ya polisi kufika na kuwatawanya wanafunzi hao waliwaeleza waandishi wa habari kuwa sababu ya wao kufanya mgomo wa kutoingia madarasani na kutaka kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Iringa umetokana na uongozi mbovu wa shule hiyo usiozingatia haki za binadamu. Waliyataka madai hayo yao kuwa ni pamoja na mfumo wa ufundishaji kutofuata taratibu na kanuni za ualimu ,pia ukosefu wa vitendea kazi kama madawati na vitabu , makamu mkuu wa shule hiyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kujinufaisha binafasi badala ya kusaidia kukuza kiwango cha elimu na kuwa amekuwa akidhalilisha wanafunzi kwa kuwapekua simu hadharani hadi kanisani . Waliwataja walimu wengine zaidi ya 6 wakiwemo wa kike (majina tunayo) ambao wamekuwa wakiwadharirisha kwa kuwapekua sehemu za siri hadharani na kupokonya simu zao kwa faida yao . Aidha walidai kuwa chakula wanacholishwa shuleni hapo hakina ubora kama wanaoelezwa wazazi huku wakimtaka mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kutolea ufafanuzi juu ya bajeti inayotengwa shule hiyo kwa ajili ya chakula. Madai mengine ambayo wanafunzi hao wanapinga ni pamoja na ubadhilifu wa mali za shule pamoja na fedha zinazochangwa na wanafunzi hao . Walisema kuwa mfano wamekuwa wakichanga rim mbili kwa mwaka rimu zenye thamani ya shilingi 8500 kila moja ila matokeo yake uongozi wa shule hiyo umekuwa ukiziuza rim hizo kwa wafanyabiashara na kununua rim za shilingi 3500 zisizo na ubora kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi hao. Hata hivyo walipinga matumizi mabaya ya fedha za shule hiyo yanayofanywa na mwasibu na kuwa wana kama wanafunzi wanataka uongozi wa shule hiyo kuweka wazi matumizi ya michango yao mbali mbali ambayo wamekuwa wakichangia . “Tunatoa pia kujua kuhusu Fund ya wasomi waliosoma hapa Tosamaganga inatumikeje na leo tunaiomba wizara ya elimu ,mkuu wa mkoa wa Iringa ,mkuu wa wilaya ,mkurugenzi na afisa elimu kufika shuleni hapa na kuja kusikia kilio chetu wanafunzi” Mwandishi wa habari hizi alishuhudia askari polisi hao wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) wakikabiliana na wanafunzi . Hata hivyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi aligoma kutoa ushirikiano wowote kwa madai kuwa vyombo vya habari vimeripoti sivyo habari za kutekwa magari juu milima ya Kitonga.Mkuu wa shule hiyo hakuweza kupatikana kuzungumzia madai ya wanafunzi hao kutokana na vikao mbali mbali na vyombo vya dola ambavyo vilikuwa vikiendelea shuleni hapo.(Habari na Picha:Francisgodwinblog) |
| Reactions:: |
Mkanganyiko Wa Leo.....
| ..........Kuna wakati ilielezwa kuwa bustani nyingi za mbogamboga wastawishaji hutumia mbolea za chumvi chumvi kukuzia mboga hizo. Wataalamu walieleza madhara yatokanayo na matumizi ya mbolea za chumvi chumvi kukuzia mboga za majani. Moja kati ya madhara yaliyotajwa na wataalamu hao kuwa ni hatari ya watumiaji kupata ugonjwa wa kansa. Sikumbuki ni hatua gani zilifuata baada ya ropoti ile! Binafsi inanikanganya sana, kwenu wadau. (Picha: Victor Makinda) |
| Reactions:: |
JK Afungua Barabara Ya Usagara
| Rais Dr.JakayaMrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Barabara ya Usagara Geita leo asubuhi.Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 90 imejengwa kwa thamani ya zaidi Tshs.78bn/ zilizotolewa na serikali ya Tanzania.Wengine katika picha, Kutoka Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro,Katibu Mkuu Ujenzi Balozi Herbert Mrango,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli, Mbunge wa Misungwi ambaye pia ni naibu Waziri Sayansi na Teknolojia Charles Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu TANROADS injinia Patrick Mfugale(Picha:Freddy Maro) |
| Reactions:: |
Ya Babu Wa Loliondo Na Ushauri Wa Wamarekani
Na Maggid Mjengwa,
INAYODAIWA kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeanza kuonyesha madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu sasa ni mradi, na kwa kweli umeanza kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa.
Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi mabaya, na ni sugu. Ndio, miongoni mwetu kuna wenye kusumbuliwa na maradhi ya unafiki. Nitatoa mfano wa juzi tu; nilikaa na wasomi wawili, tena wana digrii zao. Tukazungumzia ya Babu wa Loliondo.
Mimi na wasomi wale tulikuwa na misimamo ya kufanana, tulipinga upotoshaji unaoendelea katika jamii kuwa Babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapile , anatibu ukimwi, kansa, kisukari na mengineyo. Na kwa vile wote tumekwenda shule, hoja kuu ilikuwa hii; kuwa hadi sasa hakuna hata wagonjwa watatu wa ukimwi waliothibitishwa kitaalamu kuwa wamepona ukimwi kwa dawa ya Babu. Badala yake, kuna wengi wamekufa baada ya kuacha kutumia madawa waliyoelekezwa na madaktari watalaamu waliosomea tiba.
Wakati tukiendelea kuzungumza, mara akatokea mheshimiwa fulani, naye akaingia moja kwa moja kwenye mjadala. Alimtetea Babu na kusisitiza kuwa Babu ni lulu ya taifa, lazima aenziwe. Wasomi wale afadhali wangekaa kimya, hapana, walianza kumuunga mkono mheshimiwa kwa hoja nyepesi.
Hawakuwa wapumbavu, walijifanya tu wapumbavu wakiniacha mimi nikipambana peke yangu kuziponda hoja za mheshimiwa yule. Kwa kiasi fulani, niliogopa kuona hulka hii ya wasomi wetu. Wasomi ambao, kwa unafiki, wanashindwa kutetea na kusimamia katika hoja zao za msingi. Na hii, bila shaka, ni moja ya majibu ya swali la kwa nini Tanzania ni masikini?
Hakika, ya Babu wa Loliondo ni aibu yetu kitaifa. Katika karne hii ya 21 nchi yetu inatumia raslimali zake kufanya promosheni ya ndoto ya Mtanzania mmoja kati ya Watanzania milioni 42! Ndio, tunafanya promosheni ya jambo lisilo na uthibitisho wa kisayansi. Si tunaona, haipiti siku bila kusikia habari za Babu wa Loliondo?
Kwa sasa, tunaweza kabisa kusema, kuwa habari za huduma za Babu wa Loliondo zinatangazwa na kuufikia umma kuliko habari za Wizara yeyote ile katika Serikali ya Awamu ya Nne. Babu wa Loliondo si mchezo bwana, ana ‘maafisa habari wake’ wanaowafunika hata maafisa habari wa Wizara za Serikali.
Na katika mzaha huu wa mambo ya msingi kitaifa, tuna maelfu kwa maelfu ya Watanzania wanaotaabika na hata baadhi kufa kwa kuamini kuwa Loliondo kuna tiba, na iko Loliondo tu! Leo, kuna Watanzania walioweka rehani mavuno yao ya mwaka mzima ili wapate nauli ya kwenda kwa Babu. Si wameambiwa, kuwa hata mawaziri wanapanga foleni ya kwenda kupata kikombe cha Babu!
Na wakishapata kikombe wanapiga picha ya ukumbusho, au labda ya kisiasa. Asubuhi yake ’maafisa habari’ wa Babu wameshatundika picha ya waziri ukurasa wa kwanza gazetini! Jimboni kwa mheshimiwa wapiga kura wake watamwona au kusikia kuwa Mheshimiwa naye anaumwa kama sisi, na amepata kikombe cha Babu!
Kikombe cha Babu ni abrakadabra, nilipata kuandika hilo. Na Watanzania, baadhi, kwa hiyari yetu, tumekubali kujifanya, wajinga na hivyo kuwapumbaza wengi wengine. Kwanini? Tulitafute jibu kwa kufikiri kwa bidii.
Hebu jiulize; wakati Shirika la Afya Duniani (WHO), ifikapo Juni mwaka huu, litaadhimisha miaka 30 ya mapambano dhidi ya ukimwi, je, Tanzania, kama nchi, tutakuwa na banda la maonyesho likielezea ugunduzi wa tiba ya ukimwi iliyotokana na ndoto ya Babu?!
Labda ndio maana, magazeti yetu ya lugha ya Kiingereza hayafanyi sana promosheni ya tiba ya Babu. Maana, kama habari za Babu zingepewa uzito kama ilivyo kwenye magazeti yetu ya lugha ya Kiswahili, basi, wana jumuiya ya Kimataifa, wakiwamo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, huenda wangeshindwa kuamini wanachokisoma.
Maana, wawakilishi wa mashirika kama PSI na FHI yenye miradi ya kupambana na ukimwi nchini na mengineyo wangejiuliza; nini hasa wanachokifanya katika nchi yetu. Na pengine wameshatafsiriwa tunachooandika juu ya Babu kwa Kiswahili chetu!
Si ajabu basi, Ubalozi wa Marekani umekuja na tamko lake Mei 5 mwaka huu. Wamarekani hawa, kwa kuwaonea huruma Watanzania, wameshauri watu wanaotumia tiba mbadala wasiache kutumia dawa walizopewa na madakatri na vile vile waendelee kujikinga na maambukizi.
Na wakaweka msisitizo kuwa, kuacha kutumia dawa hizo za madaktari watalaamu kunafanya dawa hizo zinapotumiwa tena kushindwa kufanya kazi ipasavyo (drug resistance). Na ajabu ya habari ya tamko lile la Wamarekani ilichapishwa katika gazeti moja tu kwa lugha ya Kiingereza - The Citizen, jina la gazeti hilo lina maana ya Mwananchi; ingawa wananchi wengi hawakupata habari hiyo kwa lugha yao!
Kwa hakika, hatuhitaji kuambiwa na Wamarekani juu ya ukweli huu na wajibu wetu. Huu ni wakati kwa wizara inayohusika kufanya jitihada za dhati kutoa tamko litakaloweka bayana kuwa tiba inayodaiwa kutolewa na Babu bado haijathibitika kitalaamu kama inaponya maradhi sugu kama vile ukimwi, kansa na kisukari.
Wakati utafiti huo ukiendelea, umma ukumbushwe kuwa, dawa zinazotambulika kitalaamu kwa sasa ni zile zinazotolewa na madaktari wetu watalaamu. Kwamba wanaokwenda kwa Babu wana ruhusa ya kufanya hivyo, lakini, kikombe cha Babu kinaweza kunywewa pamoja na dawa za hospitalini.
Tufanye hivyo sasa, na ujumbe huo usambazwe kwa nguvu zote na maafisa wa habari wa wizara husika. Ndio, maofisa habari wa Wizara ya Afya nao washindane na ‘maafisa habari’ wa kujitolea wa Babu wa Loliondo!
Watanzania tunapita kwenye kipindi kigumu sana. Na huu ni wakati wa kutafakari kwa kina. Na nimepata kumwuliza jamaa yangu swali hili; mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani angetamka kuwa, angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.
Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri?
Haya ya kwa ‘Babu wa Loliondo’ ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, unahitaji mwanga.
Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu wakaoteshwa na Mungu juu ya dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndio, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa kiserikali.
Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo; maana, watakuwa wameufanyia utafiti. Nahitimisha.
| Reactions:: |
Kutoa Ni Moyo, Usambe Ni Utajiri; Mwakalebela Ajitolea
Fredrick Mwakalebela akiwa na familia yake Mama mzazi Erica Mwakalebela,Mke wake
Nicelina Mwakalebela,Watoto Vannesa na wilfredy akifanya tukio la utoaji jana Jumapili tarehe 30 May 2011
baada ya kutembelea kwenye ward ya Watoto wenye matatizo ya Saratani-Muhimbili.
Kujitolea ni moyo unaotakiwa kujengwa kuanzia Ngazi ya familia.
Wasalaam
Emmanuel
Image Profession.
Nicelina Mwakalebela,Watoto Vannesa na wilfredy akifanya tukio la utoaji jana Jumapili tarehe 30 May 2011
baada ya kutembelea kwenye ward ya Watoto wenye matatizo ya Saratani-Muhimbili.
Kujitolea ni moyo unaotakiwa kujengwa kuanzia Ngazi ya familia.
Wasalaam
Emmanuel
Image Profession.
| Reactions:: |
Subscribe to:
Posts (Atom)



























