Thursday, June 30, 2011
Muungano Wa Afrika Waishutumu Ufaransa
| Reactions:: |
Balozi Wa Ireland Atembelea Maonesho Ya Sabasaba
| Balozi wa Ireland nchini Lorcam Fullam akiweka saini kitabu cha wageni leo mchana katika Jengo la NDC, alipotembelea jengo hilo. |
| Reactions:: |
Mengi Atembelea Sabasaba
| Reactions:: |
Wakala Wa Vipimo Watoa Somo
| Reactions:: |
Nape Atembelea Mwananchi Na Global Publishers
| Nape akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers katika chumba cha habari cha Global. Wengine ni Mrisho, Ndauka, Sixtus na Ally. |
| Nape akiwa katika ofisi za Global Publishers.Kushoto ni Abdallah Mrisho Wengine kutoka kulia ni, Sixtus Mapunda, Maloto,Ndauka na Mhariri kiongozi wa michezo wa Global Saleh Ally. |
| Reactions:: |
JK Yuko Malabo, Equatorial Guinea
1. Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na baadhi ya marais wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU wakimpongeza Rais mstaafu wa Brazil Lula Da Silva kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa nchi za AU uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sipopo,jijini Malabo,Equatorial Guinea leo asubuhi.Hotuba hiyo ya kusisimua ilitilia mkazo kwa nchi za Afrika kushirikiana ili kujiletea maendeleo na kuepuka misaada yenye masharti inayolididimiza bara la Afrika katika lindi la umaskini.
2.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Malabo, Equatorial Guinea(Picha: Freddy Maro)
| Reactions:: |
Ngoma Za Asili Zipo, Zina Hadhi Na Nafasi Kubwa; Lasema BASATA
| Reactions:: |
Maonesho Ya Kimataifa Ya Biashara(Sabasaba); Tembelea Wizara Ya Fedha Na Uchumi Uelimike
| Mapokezi utakutana na Da' Mary na Dada Ingiaheri Mduma ambaye ni aAfisa uhusiano na Msemaji Mkuu wa Wizra ya Fedha na Uchumi, hapo utafaidi ukarimu wa hali ya juu na maelekezo muhimu. |
| Mtaalamu wa Uchumi, Idara ya Bajeti, Adamu Msumule akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea Jengo la Wizara hiyo jana. |
| Wananchi Mbali mbali wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakaz wakarimu wawIWizara ya Fedha na uchumi. Picha zote na Victor Makinda |
| Reactions:: |
Mo Blog Inahujumiwa
TAARIFA YA MO BLOG KWA WADAU
MO BLOG INAPENDA KUWAFAHAMISHA WADAU NA WASOMAJI WA BLOG HII KUWA TUMESIKITISHWA
NA KUHUZUNISHWA NA TABIA INAYOENDELEA YA KUHUJUMIWA NA WAPINZANI WASIOPENDA
MAENDELEO YETU KWA SABABU ZAO BINAFSI.
KWA MUDA MREFU TUMEKUWA KATIKA HARAKATI NA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA
TUNAWAHABARISHA, ELIMISHA NA KUJADILIANA NA WADAU MBALIMBALI WA BLOG HII BILA KUINGIA
UHURU WA WENGINE WALA KUKOSOA WENGINE, KWANI MAENDELEO YA KWELI YANATOKANA NA
KUJIAMINI.
KWA MANTIKI HII TUNAOWAMBA RADHI WADAU WETU KWA KUTOKUWEPO HEWANI KWA SAA
KADHAA LAKINI SASA MO BLOG IMERUDI NA ITAENDELEA KUWALETEA HABARI NA BURUDANI
MBALIMBALI NANYI MSISITE KUTUSHAURI NA KUTUONGOZA KWA MAWAZO YA KUJENGA.
IKIWA NI MARA KWA MARA TATIZO HILI LA KUPOTEA NA KUPOTEZA KAZI ZETU KUTOKEA KATIKA BLOG
YETU ,TUNAJIULIZA NI WAPI TUNAKOSEA AU KUHARIBU KATIKA UHABARISHAJI WETU WA HABARI NA
MATUKIO ,AU KUFANYA HIVI NI MAKOSA..?!!!
KWA KIFUPI MOBLOG INATEMBELEWA NA WATU 20,000 KWA SIKU NA HILI LINATUPA NGUVU
NA KUFAHAMU KUWA WADAU WETU WANARIDHISHWA NA KUPENDEZWA NA HABARI ZA KITAIFA,
KIMATAIFA, BIASHARA, MICHEZO, BURUDANI NA INTERVIEWS ZA WATU MAARUFU WANAOJULIKANA
NA WALE PIA WENYE VIPAJI WASIOJULIKANA.
WADAU HILI NI KOSA…???
KWA MASIKITIKO MAKUBWA TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA KAZI ZOTE ZA MWAKA HUU 2011
ZILIZOPENDWA NANYI WADAU NA NYINGINE ZIKITOKANA NA MCHANGO WA NINYI WADAU NA
WASOMAJI ZIMEPOTEA KWA LUGHA NYINGINE (ZIMEFUTWA/ZIMEPOTEZWA) KWA SABABU AMBAZO
ZINATUTIA SHAKA NA KUTUPA HISIA KUWA NI ZA KIPINZANI.
TUSINGEPENDA KUSEMA MENGI NA WALA KUTAJANA MAJINA ILI KWA WEMA KABISA NA HEKIMA
TUNAPENDA KUSISITIZA KUWA UPINZANI WA KUHARIBIANA SI MZURI NA HAUJENGI WALA KULETA
MAFANIKIO KWANI MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
HAIPENDEZI KUONGEA HAYA YOTE HAPA ILA YAKIZIDI NI AFUENI YA MOYO NI KUONGEA NA KUSEMA
WAZI TUMECHOKA KUHUJUMIWA.
ASANTE KAKA MAKWAIYA KWA MSAADA WAKO, MKUBWA MICHUZI TUNAKUSHUKURU BILA
KUMSAHAU MZEE WA FULL SHANGWE NA WENGINE KWA MISAADA MBALIMBALI NA USHAURI
MLIOTUPA KWETU.
WADAU WA MOBLOG TUKO PAMOJA NATUTAENDELEA KULIJENGA TAIFA LETU KWA AMANI, UPENDO
NA MATUMAINI.
TUNAWAPENDA, TUNAWATHAMINI, TUNAWAHESHIMU NA TUTAFANYA KAZI PAMOJA NA TUTAFIKA
PALE TUNAPOKUSUDIA.
MUNGU IBARIKI MO BLOG NA WADAU WAKE WOTE.
Endelea kuperuzi MO BLOG www.mohammeddewji.com/blog

Oscar Salathiel Kambona; Upande Wa Pili Wa Shilingi ( 2)
-Ziara mbili za ughaibuni zilizovunja urafiki wa Nyerere na Kambona
Na Maggid Mjengwa,
KUNA wakati nilimsikia Ahmad Rashid akitoa hoja bungeni. Wakati huo mbunge huyo wa CUF alikuwa kiongozi wa upinzani bungeni. Ahmad Rashid aliomba kambi ya upinzani bungeni ibadilishwe jina na badala yake iitwe kambi ya ushindani bungeni. Ni kwa vile neno ‘upinzani’ linatafsiriwa vibaya na wananchi. Spika Samwel Sitta alisimama na kutamka; “ Mtaendelea kuitwa hivyo hivyo kambi ya upinzani, kwa vile nyinyi ni watu wa kupingapinga tu!”
Na maneno haya ya Samwel Sitta yanatokana na historia yetu. Maana, haya ni makosa ya kihistoria yaliyofanywa na waliojenga msingi wa taifa letu. Na ndio tunayoyaona hata katika mfarakano wa miaka hamsini iliyopita kati ya Julius Nyerere na Oscar Kambona.
Na mara ile, mwaka 1965, TANU ilipoaachana na mfumo wa vyama vingi na kuasisi mfumo wa Chama kimoja Kambona alipata kutamka; ” Kwanini tupige marufuku ya vyama vingine vya siasa wakati tunajua wananchi walio wengi wanaipigia kura TANU?” Kambona akaongeza kusema; ” Bila shaka, umaarufu wa TANU utabaki kwa muda mrefu, lakini, je, pale umaarufu wa TANU utakapopungua, ina maana tuwe madikteta?” Alihoji Kambona.
Nimepata kukumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Na wanadamu hatupaswi kuwa vipofu wa historia yetu wenyewe. Kuifumbia macho historia yako ni kujiandalia njia ya kutumbukia korongoni, kwa kujitakia. Tunapoadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika tuna lazima ya kuipitia na kuitafakari historia yetu. Kwa macho makavu na maangavu, tuangalie nyuma tulikotoka. Tuangalie tulipo sasa. Ndio, tufanye hivyo ili tuutafute mwelekeo mwema wa nchi yetu hata kwa miaka mingine hamsini ijayo.
Tuna maswali mengi ya kujiuliza, moja kuu ni hili; Je, ni nchi ya namna gani tutayotaka kuijenga na hata kuvirithisha vizazi vijavyo? Kwa maneno mengine; ni jamii gani tunayotaka kuijenga? Sisi wa ’ Kizazi Cha Azimio’ tulikuwa wadogo sana katika miaka kumi ya mwanzo ya uhuru na hata utekelezaji wa Azimio la Arusha. Nimezaliwa Ilala, Dar es Salaam, Machi 11, 1966.
Ndio, kuna mema mengi tuliyoyaona, lakini, tukitafakari sasa, kuna mabaya mengi pia tuliyoyashuhudia. Tuna wajibu wa kusimulia mema na mabaya hayo kwa manufaa ya Watanzania wa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Kati ya kumbukumbu zangu mbaya za wakati huo ni jinsi tulivyowaona wazazi wetu wakiishi kwa hofu. Waliogopa kushutumu mamlaka hadharani na kwa sauti. Waliishutumu Serikali na hata kiongozi mkuu wa nchi kwa kunong’ona. Wazazi wetu walimwogopa hata mjumbe wa nyumba kumi.
Ni ukweli, kuwa kwa wakati ule, Serikali na chama tawala havikuwa na uvumilivu wa sauti za upinzani.
Na siku zote, mamlaka bila upinzani huzaa kiburi na majigambo. Huzaa hali ya kutokujali na kukosa usikivu. Taratibu, huzaa hali ya kujisikia u-bwana mkubwa. Hali hii ikiachwa ikaendelea, basi, husababisha madhara makubwa kwa nchi. Huleta hasara kubwa kwa nchi, kiuchumi na kijamii.
Juma la jana nilimalizia kwa kuandika, kuwa makala haya ni jaribio la kuvunja ukimya wa juu ya nini kilitokea takribani miaka hamsini iliyopita. Ni mmoja tu wa mfano , wa jinsi umma ulivyofichwa ukweli wa juu ya nini hasa kilitokea kikasababisha mfarakano wa waliopata kuwa viongozi wa mstari wa mbele kwenye harakati za kuanzishwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika; Julius Kambarage Nyerere na Oscar Salathiel Kambona.
Kuna aliyesoma makala yangu ya juma la jana na kuniuliza; ” Maggid, hivi wewe huogopi?” Ni kweli, kama ningeandika haya mwaka 1976 nilipokuwa mtoto wa umri wa miaka kumi tu, basi, vyombo vya dola vingenishukia mithili ya mwewe anayekishukia kifaranga cha kuku. Sio tu mimi ningeswekwa rumande ya watoto, bali hata mama na baba yangu wangetikiswa na dola kwa ’ dhambi’ ya kumzaa mtoto mwenye fikra za ’ kipinzanipinzani ’ na ’ kihainihaini’. Mtoto ’ anayepingapinga’ tu!
Na hapa ndipo kwenye moja ya mapungufu makubwa ya waliojenga msingi wa taifa letu; kuchukia wenye kufikiri tofauti na watawala. Na zaidi kuwachukia wenye ’ akili’ ya kufikiri na kuutumia vema welewa wao- hostility towards execelency. Si tunajua, kuwa utotoni tulisikia kuna maadui wa nchi wa aina mbili; maadui wa nje na wa ndani. Wapinzani ama wenye kufikiri tofauti ndimo walimowekwa wanaoitwa ’maadui wa ndani!’
Niseme tu, mfulilizo wa makala haya ni moja ya makala zangu muhimu tangu nianze kushika kalamu na kuandika makala magazetini. Na naandika nikiwa sina hata chembe ya hofu. Ni kwa sababu moja kuu; kuwa yanahusu historia yetu na mustakabali wa nchi yetu. Sote tuna wajibu wa kuandika historia yetu.
Hii ni nchi yetu. Hatuna sababu za kuionea aibu historia yetu, badala yake, tujivunie, kuwa tuna historia. Na ni unyonge na utumwa kusubiri wasomi kutoka Marekani na Ulaya waje kutafiti na kutuandikia historia yetu. Historia yako isimulie mwenyewe. Hivyo basi, tuna wajibu wa kuifanya kazi hiyo. historia itusaidie kutukumbusha machungu na furaha ya tuliyoyapitia kama taifa. Si kwa kuandika tu, hata kwa kusimulia machache tuliyoyashuhudia.
Niliahidi kuchambua zaidi juu ya marafiki hawa watatu; Kambona, Nyerere na Kawawa. Nitafanya hivyo sasa.
Naam. Julius na Oscar walikuwa viongozi vijana sana katika Tanganyika huru ya wakati huo. Ikumbukwe, wakati tukipata uhuru, Nyerere alikuwa na miaka 39 na Oscar alikuwa na miaka 36. Hawa walikuwa ni vijana waliokabidhiwa dhamana kubwa ya kuingoza nchi kubwa ya Tanganyika. Naamini, walikuwa ni wenye dhamira njema kwa taifa hili; Julius, Oscar, Rashid na wenzao wengine katika TANU.
Ukweli unabaki, kuwa Oscar Kambona hakuikimbia nchi yake kwa kashfa ya kuiba fedha ya Serikali au ufisadi mwingine. Na kwa utafiti mdogo tu niliofanya, nilichobaini, ni ukweli kuwa marafiki hawa wawili; Oscar na Julius walikuwa na mgongano wa tofauti ya kimaono ya kisiasa yaliyoathiri hata urafiki wao.
Maana, haiyumkini Kambona aliyeaminiwa na Nyerere akaja kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa TANU, akawa Waziri wa kwanza wa Elimu wa Tanganyika huru, akaja kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na hata kwa wakati mmoja kushika wizara mbili; Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Nje. Kwamba, aje tena baadae kutuhumiwa uhaini na hata kushukiwa uraia wake.
Ndio, kwangu mimi, ya Kambona na Nyerere ilihusu zaidi mgongano wa tofauti za kimaono ya kisiasa . Na ukiingia kwa undani kwenye maandiko na simulizi utaupata ushahidi wa haya. Na kwa hakika, ili siasa ya nchi istawi, basi, inahitaji uwepo wa migongano ya kifikra. Hivyo basi, siasa ni migongano ya kifikra yenye kuhitaji majadiliano endelevu.
Tunaona, kuwa migongano ya kifikra kati ya Oscar na Julius ilianza kuonekana dhahiri katika ziara mbili walizozifanya kwa pamoja katika mataifa mawili tofauti. Ziara ya Marekani mwaka 1963 na ziara ya Uchina mwaka 1965. Na hapo katikati kuna jambo lililoopelekea uwepo wa mahusiano ya mashaka kati ya Julius na Oscar. Ni uasi wa jeshi wa Janauri 20, 1964.
Uasi ule ulipelekea Nyerere na Kawawa waende mafichoni, inasimuliwa walijihifadhi eneo la Kigamboni. Mjini alibaki Oscar Kambona aliyeshiriki kikamilifu kuwatuliza wanajeshi wale. Kimsingi, katika kipindi kile cha maasi, Kambona, kama angetaka, alikuwa na fursa ya kutwaa mamlaka ya nchi akisaidiwa na jeshi. Inasemwa, kuwa akiwa Waziri wa Ulinzi, Kambona alikubalika sana jeshini.
Baada ya ziara ya Marekani akiwa na Oscar Kambona mwaka 1963 ambako Rais John Kennedy alimsifia sana Nyerere kwa kuonyesha uwezo wa kiungozi , miaka miwili baadae, mwaka 1965, Nyerere na msafara wake akiwamo Oscar Kambona walikwenda China kwa mara ya kwanza na kulakiwa na Mwenyekiti Mao Tse Tung. Nyerere akiwa kwenye gari la wazi na mwenyeji wake Mao , alishangiliwa na Wachina wapatao milioni moja waliojipanga barabarani.
Pale Ilala tulikoishi, nakumbuka nikiwa na umri wa miaka sita tu, usiku mmoja pale viwanja vya shule ya msingi Boma tuliangalia sinema ya ziara ya Julius Nyerere Uchina . Nyerere aliiona China na alivutiwa sana. ” What we have seen in China is relevant to us”. Nimemsikia Nyerere akiongea hayo kwenye kipande cha filamu ya zamani kilichopo mtandaoni . ” Ana maana, walichokiona China kinaweza kikafanyika kwetu. Na Julius alianza kwa kubadilisha hata staili yake ya mavazi, yakafanana na ya Mwenyekiti Mao, na wengine katika TANU wakamwiga.
Ni nini kilitokea kwenye Mkutano wa TANU wa Januari, mwaka 1967 na kabla ya hapo. Mkutano uliopelekea kumalizika kabisa kwa urafiki wa Nyerere na Kambona. Fuatilia toleo lijalo.

Wednesday, June 29, 2011
Janga La Mgao Wa Umeme; Makamba Amkingia Kifua Ngeleja
| Reactions:: |
Mwanamke Wa kwanza Kuongoza IMF
| Reactions:: |
Madaktari Na Wauguzi Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Bidii Ili Kuokoa Maisha Ya Wagonjwa; Asema Mama Salma
| Reactions:: |
Nape Azidi 'Kukanyaga Mafuta' CCM
1. MAMIA ya wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mtwara 28/6.2011
2. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akijadiliana jambo na Mbunge wa Lindi mjini, Hasnain Mohammed Murj wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mtwara 28/6/2011
3. Aliyekuwa mwanachama wa CUF na mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita, Mohamed Chiungulumana akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipotangaza kurejea CCM kwenye mkutano uliofanyika 28/6/2011 mjini Mtwara. Jumla ya wanachama 154 wa CUF walijiunga na CCM katika mkutano huo.Kuhsoto ni Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma. Picha zote: Bashir Nkoromo
| Reactions:: |
" Shangazi Hujambo?"
Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akizungumza na mtoto Fatma Mohammed, alipomkuta kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kijiji cha Mpapura Mtwara vijijini. Picha: Bashir Nkoromo.
| Reactions:: |
Wazee Wanafuatilia Mkutano Wa Nape
Wazee wa Kijiji cha Mpapura, Mtwara Vijijini, Abdurahmani Dadi (70) na Dadi Hamis (65) wakifuatilia kwa makini , Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho 28/6/2011. Picha: Bashir Nkoromo.
| Reactions:: |
EASTERN AND SOUTHERN AFRICA CARGO LIMITED- UK
We are an import/export company based in the United Kingdom with global dealings. We offer specific services to suit each individual client.
Whether you require a single service or an annual requirement,ESAC LTD will treat you with care, consideration and most of all the best solution for your requirements. We pride ourselves in our service and welcome any job regardless of size.
ESAC LTD is proud to announce this service for those who wish to send urgent consignments or smaller items,Quick goods to East Africa and many other destinations.
*OUR AIRFREIGHT SERVICES ARE WORLWIDE £2.70 PER KILO £38.00 Customs Entry Fees. Our minimum weight is 100KG.
We ship all types of cargo to Africa at subdued rates, i.e. containers, trucks, cars, machines etc. we also sell used vehicles & machinery from UK.
RORO
Saloon & 4X4 TO DAR OR MOMBASA
TRUCKS from $81.50 per cubic metre
TRUCKS from $81.50 per cubic metre
CONTAINER
20ft CONTAINER TO DAR
40ft CONTAINER TO MOMBASA
40ft CONTAINER TO DAR, TANGA & ZANZIBAR
Bill of Lading will be processed in 3-5 working days if you pay full amount ;"GAURANTEE"
Also we provide the service to West frica, please ring us to get a quotation.
Note: For our customers who are outside UK, but would like to buy fromUK, we can buy to match your specifications weather is cars, trucks, machinery, hospital equipments and other goods, please do not hesitate to contact us. We will buy and ship your good/s timely and as per your requirements.
At Eastern and Southern Africa Cargo LTD, we aim to: -
* Put the Customer First *
*Like many other international business our price may vary due exchange rates and currency fluctuation*
* Provide High Quality Service*
--
--
Regards,
CEO: Bernard Chisumo
Eastern & Southern Africa Cargo Limited (ESAC)
(Exporters & Importers )
Tel No: +44 783 369 2695, +44 0148 221 4949 (North England - HQ)
Tel No: + 44 118 954 5890, +44 79000 43224 (South England office)
132 Victor Street, HULL, HU9 2EY- East Yorkshire
REG NO:07609023. VAT NO:113 999 585

Tuesday, June 28, 2011
Mama Salma Kikwete Yuko Comoro
1- Mke wa Rais mama Salma Kikwete(nguo nyekundu) akipata ufafanuzi wa vifaa mbalimbali vya kutengenezea simu katika moja ya darasa la kituo cha mafunzo EMDAD kilichopo mjini Moroni nchini Comoro, June 28/2011.
Picha no 2 na 4. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA mama Salma Kikwete(aliyevaa baibui) akiwa na mke wa Rais wa Comoro mama Hadija Aboubacar Ikililoi Dhoinine (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa waziri wa afya wa Comoro Mwanafuraha Mohammed (wa tatu kutoka kulia) kuhusu mtoto ambaye yuko chini ya uangalizi wa madaktari baada ya kuzaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya El Maarouf mjini Moroni Comoro - June 28/2011.
Picha no 3 - Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiangalia aina ya samaki ambaye amehifadhiwa katika makumbusho ya Taifa mjini Moroni, Comoro. Samaki huyo yuko katika orodha ya samaki wasiotakiwa kuvuliwa nchini humo, (mwenye nguo za kijani) ni mwenyeji wake mke wa Rais wa Comoro mama Hadija Aboubacar Ikililoi Dhoinine - June 28/2011.
| Reactions:: |
Mdau Anauliza; " Mliokulia Enzi Za Mwalimu, Je Haya Ni Ya Kweli?"
Anony wa Jun 28th; 02:10:00 inawezekana ni kweli wachangiaji wengi ni wale wa 1980's and 1990's. Mimi binafsi nimezaliwa 1979 na sijui mengi kuhusu maisha ya wakati wa utawala wa Nyerere. Naomba nikuulize maswali kadhaa kuhusu nyerere ili niweze kufanya utafiti zaidi.
Jee ni kweli kwamba wanafunzi wengi wa shule za dar-es-salaam walikuwa wakikaa sakafuni na wakiuza ubuyu na kalimati za mwalimu?
Jee. ni kweli mlikuwa mkipanga foleni kwa masaa kadhaa mkusubiri gari la ugawaji?
Jee ni kweli mlipigia mswaki jivu na mkaa?
Jee ni kweli mlifua nguo kwa kutumia harita?
Jee ni kweli mlikula ugali wa njano wa mahindi ya kutoma marekani?
Jee ni kweli kwamba watu walikuwa wakivaa midabwada? (au nguo zenye viraka?)
Jee ni kweli ulikuwa ukimtembelea ndugu yako darisalama ni lazima balozi wa nyumba kumi ajulishwe madhumuni ya ujio wako na utakaa siku ngapi?
Jee ni kweli kwamba ulikuwa ukikamatwa na kilo 10 za sukari unakamatwa kwa ulanguzi na uhujumu uchumi?
Jee ni kweli ulikuwa umekaa kijiweni basi unakamatwa na askari wa nguvu kazi na unashitakiwa kwa uzurulaji na uzembe na unapelekwa sehemu yoyote ya nchi?
Jee ni kweli kwamba safari ya kutoka dar-es-salaam kwenda bagamoyo ilichukua kutwa nzima na wengine walisafiri safari hiyo kwa kupanda magari ya mizigo? (lorries)
Jee ni kweli kwamba mlivaa viatu vya matairi ya gari? (katambuga)
Jee ni kweli kwamba Tanzania bara haikuwa na TV station wakati Zaizibar walikuwa nayo?
Jee ni kweli kwamba demokrasia ya wakati huo ilikuwa unachagua rais au kivuli kwa kura ya ndiyo au hapana?
Jee ni kweli wakulima wakubwa walipokonywa mashamba yao na yakafanywa kuwa mashamba ya ushirika?
Jee ni kweli kwamba kila familia(kaya) iliwahi kupewa kadi ya ugawaji ambayo inaamua kwamba unaruhusiwa kununua kilo kadhaa za mchele/sukari/ngano?
Naomba tuu unielimishe katika maswali yangu haya.

Lowassa Katika Viwanja Vya Bunge Leo
Matunda..Mchanganyiko
Serikali Ya Japani Yatoa Msaada Wa Mafuta Ya Kupikia
| Balozi wa Japan Hiroshi Kanagawa akielekeza jambo kwa mwakilishi wa shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) Ronald Simanda wakati wa makabidhiano ya msaada huo. Picha zote na Victor Makinda |
| Reactions:: |
Jengeni Tabia Ya Kuandika Wosia Wenu Mkiwa Hai, Asema Sitta
| Reactions:: |
Aliyekuwa Rais Wa Zambia Chiluba Azikwa
| Reactions:: |
Subscribe to:
Posts (Atom)