| Makada wa chama waliohudhuria mkutano huo.Picha zote na Victor Makinda |
Sunday, July 31, 2011
Mgao Wa Umeme, Wataalamu Wasikilizwe; Asema Mbatia
Kamati Maalumu Ya Wanafunzi Wa Chuo Cha Ustawi Wa Jamii. Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Msemaji wa Kamati Maalumu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Boniface Benezeth, akisoma taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), leo mchana jijini Dar es Salaam, kuhusu mgomo wa wanafunzi wa chuo hicho uliofanyika hivi karibuni. Picha na Victor Makinda KAMATI MAALUMU YA WANAFUNZI WA TAASISI YA USTAWI WA JAMII TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Ndugu Wanahabari, JULAI 21, 2011, Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) ilisitisha masomo (kufunga chuo) kwa muda usiojulikana kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni mgomo usio halali wa wahadhiri. Hali hii ya kufunga chuo (kusitisha masomo) imekuwa na madhara makubwa kwa wanafunzi (wanachuo) ikiwa ni pamoja na wengi kukosa malazi na hata wengine kushindwa kujikimu kimaisha huku wengine muda wao wa ruhusa kazini ukimalizika. Kutokana na hali hiyo, baada ya tangazo la kusitisha masomo kutolewa na Kaimu Mkuu wa Taasisi, Mlwande Madihi mbele ya Mkutano Mkuu wa Wanafunzi ikiwa yapata saa 11:15 jioni, wanafunzi wote wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii katika Mkutano huo wakiongozwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (ISWOSO) walikubaliana na kuunda Kamati Maalumu ya Dharura kwenda Dodoma kuwasilisha kilio cha wanafunzi kwa Serikali na hasa ikizingatiwa kuwa kutokana na vikao vya Bunge la 10 kuendelea, wakiamini kuwa viongozi hao wa Serikali (Mawaziri na Manaibu Waziri) watapatikana kirahisi hukohuko. JULAI 24, 2011 (Jumapili), Kamati ilifika Dodoma na ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Chrisant Mutatina; Makamu Mwenyekiti Mariam Saad na Katibu Kitamogwa Safari. Ikiwa Dodoma, ilikutana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na kisha ikakutana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya. Siku iliyofuata Kamati hiyo ikiwa na wajumbe 10 ilikaribishwa katika Kikao cha Bunge na soma zaidi http://www.kwanzajamii.com |
| Reactions:: |
JK Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya CCM
| Reactions:: |
Soko Kuu Lateketea Kampala
Rais Wa Zanzibar Asoma Risala Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani
| Reactions:: |
Wanafunzi Darasa La Saba Wauza Kuni Kulipia Gharama Za Mitihani
| Reactions:: |
Denmark Na Korea Kusini Zaisaidia Tanzania 592 Bilion
| Reactions:: |
Alfajiri Ya Leo Tunaruka Kurudi Nyumbani Kwenye Ndege Wetu!
Mimi, makamanda wangu na mama yao. Kama kila kitu kitakwenda sawa, basi, saa tano usiku wa leo Jumapili tutakuwa Dar. Ama kweli, nyumbani ni nyumbani. Nimewakumbuka sana ndugu, jamaa na marafiki. Nimewakumbuka ndege wa nyumbani pia. Iringa ninakoishi, kila alfajiri huamshwa na sauti za kuvutia za ndege wa porini. Mara moja moja bundi hulia pia. Pichani ni siku Mrisho Mpoto aliponitembelea nyumbani kwangu Iringa. Kamanda wangu hakuchelewa kutoa burudani ya muziki kwa kupiga gitaa lake. Naam, nimefurahia sana vekesheni yangu ya Ulaya. Ahsanteni sana wote ambao, kwa namna moja ama nyingine, mmenikarimu ' Mwenyekiti' wenu nilipokuwa hapa Sweden. Panapo majaliwa nitarudi tena, sijui lini. Kila la kheir kwenu nyote!
| Reactions:: |
Saturday, July 30, 2011
Bilioni 30 Zatengwa Na Serikali Kwa Ajili Ya Mradi Wa Maji Wilayani Masasi
| Reactions:: |
Bajeti Ya Marekani Imekwama
| Reactions:: |
Naibu Spika Atunikiwa CPA London
| Tuzo yenyewe kama inavyoonekana. |
| Reactions:: |
Ya Madini Na Nishati Ni Kioja Kingine! ( Makala, Raia Mwema)
Na Maggid Mjengwa,
PTOLEMY, mwanafalsafa wa Kiyunani alipata kuandika: ”Ex Africa simper aliquid novi". Maana yake: "Kila kukicha kitazuka kioja kingine Afrika."
Naandika makala haya nikiwa nchini Sweden. Katika kufuatilia yanayoandikwa na kusemwa na wanahabari wa Sweden kutuhusu sisi, basi, nimekutana na kashfa ambayo kimsingi ni kioja chenye kutuhusu.
Hapa Sweden kuna Shirika la Misaada limeishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.
Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey, inavuna gesi ya Songosongo nchini Tanzania; huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli , TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid, iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.
Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 10. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabini na tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.
Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi uliotamalaki unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Unatuacha tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.
Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na mkataba wa kifisadi usiotanguliza maslahi ya Taifa. Taarifa hii niliweka mtandaoni majuma mawili yaliyopita na hakika wengi wameshiriki kuitolea maoni yao.
Ni jambo la faraja na kutia moyo kuwa hata waheshimiwa wabunge, bila kujali itikadi zao za vyama, wameanza kuamka na kuwa wakali kutetea rasilimali zetu. Na hakika, huu ni wakati wa waheshimimiwa wabunge wetu kumweka kikaangoni Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na Waziri Ngeleja atwambie ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii, na hivyo basi kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.
Naamini kuwa nchi yetu ni nchi tajiri sana, lakini wananchi wake wengi wamo katika lindi la umasikini unaotokana na ufisadi wa wachache tuliowapa dhamana za uongozi.
Haiyumkini mtu mwenye akili zake na anayeipenda nchi yake akakubali kuingia mkataba wa miaka 25, kwa maana ya robo karne, na kampuni ya kigeni kuruhusu wageni hao wavune gesi yetu asilia iliyo kwenye visima vyetu kule Songo Songo.
Na kioja katika mkataba huo ni mgeni mwekezaji anayevuna gesi yetu tunakubali asitozwe kodi kwa faida anayopata kwa kutuuzia umeme unaotokana na gesi ya kwetu wenyewe! Kwa mwanadamu, ni heri uwe mwendawazimu kuliko kuwa limbukeni. Watanzania tumefanywa kuwa malimbukeni.
Na majuzi hapa tumemsikia Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo, akimtuhumu Bungeni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kwa kutumia Shiolingi bilioni moja kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge. Nacho ni kioja kingine kwa wizara ya serikali kutumia fedha kuwahonga wawakilishi wa wananchi ili bajeti ipite, na wawakilishi hao wakapokea hongo hiyo.
Ni jambo jema kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufikia busara ya kuondoa bungeni hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini. Na itakaporudi tena bungeni, ni wakati wa wabunge wetu kusimammia maslahi ya umma na kuibana Wizara kufafanua baadhi ya mikataba yenye kashfa kama huu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli, TANESCO na kampuni ya Pan African Energy.
Na kauli ifuatayo ya Mbunge wa Nzega, Mheshimiwa Hamisi Kingwangwalah inatia matumaini kuwa bado tuna wabunge walio tayari kupambana kutetea maslahi ya umma.
Mbunge Kingwangwalah aliyasema haya bungeni:
"Nataka nianze kwa kusema siungi mkono hoja ya kupitishwa kwa bajeti hii na nawaomba wabunge wenzangu msipitishe bajeti hii kwa sababu tupo gizani". Mbali na tatizo la umeme, alitaja sababu nyingine za kutaka bajeti hiyo isipitishwe kuwa ni mikataba mibovu ya sekta ya madini na nishati ambayo imesababisha rasilimali za nchi kuibwa na wageni huku Watanzania walio wengi wakiendelea kuogelea kwenye umasikini.
Mbunge Kingwangwala anasema: "Waliosababisha hayo wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua. Wengine wapo hapa bungeni na wengine wako serikalini. Hii ni mikataba kandamizi. Watu hao wapo kwenye 'system' (mfumo wa Serikali). Nchi inauzwa, wachache wanashibisha matumbo yao. Watu hawa wamelifikisha taifa kwenye mazingira haya ya kifisadi kwa sababu ya kutumia nafasi zao kujinufaisha na kuweka kando maslahi ya umma wa Watanzania...Hawa watu kama hawafikirii kwa matumbo wanafikiria kwa kutumia 'spinal cord' (uti wa mgongo) badala ya ubongo."
Mbunge huyo akaongeza kusema; “ Watendaji walioliingiza taifa kwenye mikataba hiyo mibovu wanapokwenda kuisaini wanajali kile watakachopata ili kufanikisha malengo yao binafsi kama vile kujenga majumba ya kifahari. Wanaruhusu ardhi ya Watanzania kuuzwa nao wanafaidi kwa kwenda kujenga Mbezi Beach (Dar es Salaam),"
Akaongeza kusema: “Miongoni mwa mikataba ya kifisadi ni kati ya Pan African na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusiana na uzalishaji na usafirishaji wa gesi asilia.” Mwisho wa kumnukuu.

Ndio, kuna baadhi ya viongozi wetu wameigeuza nchi yetu kuwa Banana Republic. Katika Banana Republic, wanasiasa wachache hutumia siasa kufanya biashara na uchumi wa nchi. Wako tayari kuuza rasilimali za nchi kwa faida yao.
Watanzania tuna lazima ya kukataa kugeuzwa malimbukeni na kuruhusu nchi yetu kuwa Banana Republic’- Jamhuri ya Migomba. Nahitimisha.
| Reactions:: |
Tanzania: Ni Vigumu Kutimiza Matumaini Ya Vijana Katika Dunia Ya Utandawazi
MAELEZO YA PICHA:
Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue akizungumza wakati wa Mkutano wa Kilele wa Vijana uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ukiwashirikisha vijana kutoka mataifa mbalimbali, mawaziri wanaohusika na masuala ya Vijana na Taasisi za kijamii. Akizungumza mbele ya wajumbe wa mkutano huo, Balozi Sefue amesema Utandawazi na matumizi ya vyombo vya habari vya kijamii ( Social Media) siyo tu kumewafanya vijana kuwa katika kijiji kimoja lakini pia vijana wamekuwa na matumaini na mwamko mkubwa kisiasa, kijamii, kiuchumi na kitamaduni na kwamba kasi waliyonayo vijana hivi sasa inashindana na kasi ya serikali nyingi katika kuwatimizia mahitaji yao zikiwamo ajira.
Na Mwandishi Maalum
New York
Imeelezwa kwamba baadhi ya nchi zitashindwa kutekeleza kwa kasi matarajio na matumaini makubwa waliyonayo vijana.
Matarajio na matumaini hayo ni yale yanayoletwa na utandawazi na matumizi mkubwa ya vyombo vya habari vya kijamii.
Tahadhari hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue.Alikuwa akizungumza katika Mkutano wa kilele wa Vijana uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Amesema utandawazi ambao unaendeshwa na teknolojia unawafanya vijana kuwa katika kijiji kimoja cha kimataifa. Na kuwajengea ufahamu mkubwa wa wapi walipo au wapi wanatakiwa kwenda.
Balozi Sefue akaeleza , Utandawazi huo umewajengea vijana matumaini makubwa ya kisiasa, kiuchumi , kiutamaduni na kijamii.“ Lakini, baadhi ya matarajio hayo hayawezi kutekelezwa na serikali nyingi kupitia raslimali zilizonazo au sera zilizopo na kwa kasi wanayoitaka vijana”.
“ kwa maneno mengine, ingawa Utandawazi unawapa matarajio kwa vijana wetu, lakini siku zote utandawazi huohuo hautoi nyenzo sahihi za kuwapatia uwezo na fursa vijana ya kutimiza ndoto zao”.akasisitiza Balozi Sefue
Akatahadharisha kuwa kutotimizwa kwa ndoto hizo za vijana, kunaweza kusababisha madhara makubwa. Madhara ambayo yanaweza kuvuka mipaka ya nchi.
Kwa hiyo akasema, ni muhimu kuunga mkono juhudi za serikali za kitaifa na kikanda, za kuujenga uutandawazi wa haki utakao wawezesha vijana siyo tu kuwa na matumaini bali pia kuwa na fursa ya kumiliki mali.
Kuhusu matumizi ya vyombo vya habari vya kijamii ambayo vijana wengi wanajitanabaisha navyo, Balozi Sefue amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, ingawa vyombo hivyo ni nyezo muhimu katika kuleta mabadiliko chanya. Kwa bahati mbaya vyombo hivyo kama havitatumia ipasavyho vinaweza pia kuleta matokeo mabaya.
Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UM, akabainisha kuwa serikali yake inaamini kwamba vijana siyo tu viongozi wa kesho, kwani wanaweza kuwa viongozi wa leo na kutoa mchango mkubwa wa kulijenga taifa lao kwa kushirikiana na wazee wao.
Akasema kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wa vijana katika ujenzi wa nchi yao, ndio maana serikali ya Tanzania imepitisha sera zinazo wawezesha vijana wa kike na kiume kupata nafasi za uongozi katika vyombo vya utoaji wa maamuzi likiwamo Bunge.
Mkutano huo ambao ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, uliwashirikisha mawaziri wanaohusika na masuala ya vijana kutoka nchi wanachama wa UM. Pamoja na mambo mengine ulijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana duniani kote na namna ya kuzitafutia ufumbuzi.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani. Pamoja na wawakilishi kutoka taasisi zisizo za kiserikali. Na ulitoa na maazimio mbalimbali yakiwamo ya kubuni mbinu mbadala za kushughulikia matatizo ya vijana zikiwamo ajira.
| Reactions:: |
Hamkulijua Hili; ' Mwenyekiti' Wenu Anapenda Ukoko!
Jana nilialikwa mlo wa mchana mji wa Gavle hapa Sweden. Nilikaribishwa wali kwa choroko ama chooko kama wanavyoita wengine. Basi, mwenyeji wangu akanipakulia wali. Nikamwomba anikwangulie na ukoko.
| Reactions:: |
Friday, July 29, 2011
JK Akikagua.....
1. Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ubanguaji unaofanywa na wakulima wadogo katika kijiji cha Kitama,Wilayani Tandahimba wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.
2. Rais dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua korosho iliyosindikwa kwa mashine katika kiwanda cha Rift Valey Foods, wilayani Tandahimba. ( Picha: Freddy Maro)
| Reactions:: |
JK Ziarani Newala, Tandahimba Na Nanyumbu
1. Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika ghala jipya za mazao wilayani Tandahimba.
2. Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua chanzo cha Maji ya mradi wa Makonde Water Supply katika bonde la Kitangari wilayani, Newala, mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.
3. Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwete na kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dr.Zulkarnain Ikaji wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi Zahanati ya Sengenya, iliyopo wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara jana.
4. Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dr.Zulkarnain Ikaji akimwonesha Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete gari la kubebea wagonjwa aina ya bajaj litakalotumika katika Zahanati ya Sengenya wilayani Nanyumbu jana (Picha; Freddy Maro)
| Reactions:: |
Dr Salim Ahamed Salim Azindua Maadhimisho Miaka 50 YaKumbukumbu Ya Mwalimu Nyerere
| Reactions:: |
CCM Kilimanjaro Wawajulia Hali Majeruhi Wa Ajali
| Magari yaliyopata ajali. |
| Reactions:: |
Ludacris Atinga Viwanja Vya Jangwani Sekondari
| Wanafunzi wa Jangwani sekondari |
| Ludacris (katikati) akiwa na wasanii wa Bongo Fleva wa hapa nyumbani, leo jioni katika viwanja vya shule ya sekondari ya Jangwan. (Picha na mpigapicha wa mjengwablog) |
| Reactions:: |
Jeshi La Polisi Tanzania: Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
| Reactions:: |
Awamu Ya JK Kwenye Televisheni Ya Sweden; Tafsiri Yangu
Ndugu zangu,
Katika miezi ya karibuni, nchi yetu Tanzania, katika hali isiyo ya kawaidia kwenye media ya nchi za Magharibi, mara kadhaa imezungumzwa katika sura chanya kwenye vyombo vya habari vya nchi ya Sweden ikiwamo televisheni yao ya taifa.
Huko nyuma nimepata kukaa Sweden kwa miaka kumi na miwili; 1992-2004 sura ya Tanzania iliyokuwa ikionyeshwa kwenye media ni kuwa ni moja ya nchi masikini Afrika na inayotegemea misaada ikiwamo misaada kutoka nchi ya Sweden tangu miaka ya 1970. Ni kama mtoto anayenyonyeshwa kila anapolia njaa.
Lakini, katika mfululizo wa vipindi vya Televisheni “ Det Nya Afrika"-ikiwa na maana ya ' Afrika Mpya' vilivyoonyeshwa mapema mwaka huu kwenye televisheni ya taifa ya Sweden, mwandishi Erica Bjorstrom alitembelea Tanzania mara kadhaa. Mwandishi huyu anaitaja Tanzania kuwa mfano mzuri wa nchi iliyoanza kusimama na kuinuka kiuchumi. Unaweza kuona moja ya vipindi hivi kwa lugha ya Kisweden ukitembelea; Tanzania: Välståndet växer - Rapport | SVT Play
Kwa mujibu wa mwandishi huyu, uchumi wa Tanzania ni moja ya uchumi unaokua kwa kasi kubwa barani Afrika. Kwamba uchumi wa Tanzania unakua na hali za maisha ya watu zimeanza kuwa bora. Inasemwa , kutokana na kukua huko kwa uchumi na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na kodi,Tanzania imeanza hata kufikiria kutoa malipo ya pensheni kwa wasio katika mfumo rasmi wa ajira kwa mfano wakulima.
Mwandishi huyu anatoa sababu mbili zinazopelekea Tanzania kuinuka kiuchumi; Mosi,Tanzania imetoka kwenye mfumo wa chama kimoja na kuingia kwenye vyama vingi, pili, kuwepo kwa mfumo wa soko huria na kuruhusu watu kuendesha shughuli za viwanda na biashara.
Mwandishi huyo wa televisheni anatoa mfano wa moja ya viwanda vya kampuni ya Azam; ni kiwanda cha kusindindika matunda. Kwamba kinachangia kuinua uchumi wa nchi kwa kutoa ajira, kununua mazao ya wakulima na hata kuchangia uchumi wa Sweden kwa vile kampuni ya vifaa vya viwandani ya Sweden, ABB inauza vifaa na vipuri vya viwandani kwa kampuni hiyo ya Azam.
Katika moja ya vipindi hivyo vya televishen mwandishi huyu Erica Bjostrom anaongea na gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu . Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anatoa picha ya Tanzania iliyojizatiti kuinua uchumi wake kwa kujenga uchumi unaotegemea sekta nyingi.
Pia mwandishi huyo anamhoji Balozi wa Sweden nchini Tanzania , Bw. Lennarth Hjalmaker ambaye anakubali kuwa uchumi wa Tanzania unakua na kuwa Sweden, kama nchi, imeanza kujipanga kubadili aina ya misaada inayotoa kwa Tanzania. Sweden sasa inafikiria zaidi katika kuisaidia Tanzania katika maeneo ya biashara na viwanda.
Hayo ni machache tu katika mengi mazuri ambayo Tanzania na hususan utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete umepambwa nayo na mmoja wa nchi wafadhili wakubwa wa Tanzania tangu tupate uhuru, Sweden. Ni sifa ambazo nilikutana nazo kutoka kwa baadhi ya raia wa Sweden tangu siku ya kwanza nilipotua Sweden yapata majuma sita yaliyopita.
Ni mtazamo huo chanya wa kimaendeleo ya kiuchumi kwa Tanzania kutoka kwa watu wa kawaida wa Sweden ndio ulionifanya nipekue mtandaoni kuona ni nini hasa kilichoripotiwa na vyombo vya habari vya Sweden juu ya Tanzania.
Tafsiri yangu;
Vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kuathiri mitazamo ya watu . Kazi ile ya mwandishi Erica Bjostrom imechangia kuifanya Tanzania, machoni mwa watu wa Sweden kuwa ni nchi yenye kuleta matumaini ya kuwa mfano wa taifa la Kiafrika linalopiga hatua kutoka hali ya ukale na kuingia kwenye kuwa taifa la kisasa zaidi. Mara nyingi, hilo la mwisho ndilo lenye kuiletea nchi na watu wake heshima zaidi.
Na taifa la kisasa ni lile lenye kuheshimu misingi ya utawala bora ikiwamo kuamini katika demokrasia ya mazungumzo na si ya virungu . Taifa la kisasa ni taifa lenye kuruhusu uwazi zaidi na si kuruhusu usiri hata kwenye masuala ya msingi yenye maslahi kwa umma. Mfano hapa ni uwepo wa mikataba ya siri. Ni mikataba yenye kuhusu rasilimali za wananchi kufanywa kuwa jambo la siri.
Ndio, taifa la kisasa lazima liachane na ubaguzi wa kisiasa. Tanzania, tangu awamu ya kwanza imeendesha siasa za kibaguzi ikiwa na maana kuwabagua wale wote wenye fikra tofauti na kuwapiga mihuri ya wasaliti, wapinzani na majina mengineyo. Na tunayoyavuna leo ikiwamo ufisadi uliotamalaki unaolitafuna taifa ni matunda ya ubaguzi wa kisiasa ambao mbegu zake zimepandwa miaka 50 iliyopita.
Tumekuwa ni watu wa hovyo hovyo. Watu tusiotanguliza maslahi ya taifa bali ya chama, na hakika si ya chama, bali maslahi binafsi na ya kimakundi. Ni watu wa hovyo hovyo tunaotanguliza udini na ukabila badala ya utaifa.
Kwenye makala ya ’ Neno la Leo’ niliyoandika usiku wa kuamkia leo nimesimulia kisa cha Mfalme Ihsani kwenye nchi ya bahari ya giza.
Ndio, popote panapotokea maendeleo makubwa na ya haraka, basi, hutokea pia mabadiliko yenye kuyakwaza na kuyavunja maendeleo hayo. Ni mambo yenye kusababishwa na ubinafsi, chuki, husuda, fitina, wivu na siku hizi kuna neno mizengwe pia. Yote hayo ndio haswa ’ Magamba’ tuliyo nayo Watanzania. Hayo si magamba ya chama cha siasa tu. Ni magamba ya kitaifa.Kuyavua hayo sharti ukokwe moto ili kuipasha moto kwanza miili yetu!
Tufanye nini?
Umefika wakati sasa kwa Chama na Serikali iliyopo madarakani ijenge ujasiri wa kukubali kuwa Tanzania ni muhimu zaidi kuliko Chama cha siasa au watu mmoja mmoja. Kiandae mazingira yasiyokuwa na mizengwe ya kuandaa Katiba itakayowatoa Watanzania walio wengi kwenye umasikini wa kudhalilisha unaotokana na ubaguzi wa kisiasa. Maana, nchi yetu ni nchi tajiri sana ila watu wake ndio masikini kutokana na maovu ya wachache tuliowapa dhamana ya kutuongoza.
Ona Finland . Haka ni ka- nchi kadogo sana katika dunia hii. Lakini ni moja ya nchi tajiri sana na ambazo Tanzania kama nchi, viongozi wake hupita huko kutembeza bakuli la ’ Saidia Masikini!’.
Ndugu zangu,
Ka- nchi ka Finland kale uchumi wake ulianza kwa kutegemea miti ya mbao nyepesi. Hawana miti ya mpingo wala misonobali. Lakini kwa vile hawaendekezi ubaguzi wa kisiasa na kuwa wanatanguliza maslahi ya nchi yao, wameweza kujenga miundo mbinu imara ikiwamo ya hata akilini kwa maana ya elimu.
Sisi Watanzania tuna miti ya mipingo, dhahabu, almasi, gesi asilia, uranium, makaa ya mawe, Tanzanite,mito, maziwa, bahari, mbuga za wanyama na mengine mengi. Lakini bado tunaona hata fahari kujitambulisha kuwa; ” Sisi ni nchi masikini bwana!”
Na tuna viongozi wanaosimama hadharani na kutamka kuwa ni vizuri tukabaki na mfumo wa chama kimoja. Vyama vingi vitatuletea vita!”
Na kiongozi mwingine katika kuendekeza ubaguzi wake wa kisiasa anatamka hadharani; ” Ukitaka biashara yako ikuendee vizuri njoo CCM!”
Ni fikra kama hizi za ukale ndizo zitakazomfanya mwandishi Erica Bjostrom na wengine wa dunia hii kurudi tena Tanzania na kuripoti habari ya nchi ya Tanzania iliyoonyesha dalili za kusimama na kukimbia, kuwa sasa inaangamia tena kwa machafuko ya kisiasa na watu kuuana. Na sababu kubwa itakuwa ni ubaguzi wa kisiasa wenye kujenga misingi ya hila katika chaguzi.
Naam, wahenga walinena; ngoma ikivuma sana hupasuka. Ndio maana ya kusema; Pavumapo palile, si kazi kudamirika!
Maggid
Sweden,
Ijumaa, Julai 29, 2011

Subscribe to:
Posts (Atom)