Subscribe:

Wednesday, August 31, 2011

Makamanda Walipotua Rujewa Kwa Bibi Mama Abdul!



Reactions::

Mjomba Hanifa Huyu!

Leo kashiriki kikamilifu kuniandalia mjombawe na timu yangu mlo mwanana wa Eid  pale Rujewa kabla hatujaelekea kijijini kwetu Nyeregete. Ahsante sana!
Reactions::

Hapa Inaandaliwa Nguna Ya Eid!

Nyumbani kwa dada mama Hanifa, Rujewa, leo mchana.
Reactions::

Dada Zangu Hawa!

Mama Hadija kushoto na Mama Hanifa. Rujewa,  Binti wa sahangazi mama Abdul. Waliniandalia pilau ya nguvu mimi na timu yangu mchana wa leo. Mlo wa jioni ni kijijini Nyeregete. Nyeregete kuna  digidigi wengi. Ni watamu kwa kuwachoma!
Reactions::

Swala Ya Idd al Fitr Leo Msikiti Wa Kichangani Magomeni Jijini Dar es Salaam




Picha zote na Victor Makinda

Reactions::

Swala Ya Iddi Zanzibar


Picha 1: Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein akiwahutubia viongozi na wananchi hawapo pichani kwenye ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar baada ya kumalizika kwa mfungo wa ramadhani.

Picha 2: Naibu Mufti wa Zanzibar Sheikh Swaleh Omary Kaab akimkaribisha Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuhutubia baraza la Iddi lililofanyika kwenye ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar.

Picha 3: Umati katika swala ya Iddi kwenye uwanja wa Maisara

Picha 4: Umati katika swala ya Iddi kwenye uwanja wa Maisara

Picha zote: Yusuf Simai, Maelezo Zanzibar



Reactions::

JK Ashiriki Swala Ya Iddi Msikiti Wa Kichangani,Magomeni Mapipa DSM


Picha 1: Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Picha 2: Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Iddi katika msikiti wa kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam leo asubuhi

Picha 3: Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa Iddi baadhi ya waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Picha zote: Freddy Maro







Reactions::

TTCL Yatoa Zawadi Za Idi Kwa Wazee Wasiojiweza Na Watoto Yatima Kilimanjaro




Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Said Amir Said aliyevaa suti akikabidhi zawadi za siku kuu ya Idi kwa wazee wasiojiweza na watoto yatima mkoani Kilimanjaro. Picha: Issa Michuzi
Reactions::

Nakwenda Kula Eid Kwetu Kijijini!

Nyeregete, Mbarali Mbeya. Makamanda wangu na mama yao niko nao njiani.
Reactions::

EID MUBARAK!

Kwenu nyote!
Reactions::

Jana Tumeuona Mwezi Iringa!


Reactions::

Baa La Njaa Somalia; Orodha Ya Waliochangia Na Jumla Iliyopatikana Hadi Sasa....

Watoto Wanne Wanakufa, Familia Moja; Tunafanya Nini?
Mwenzetu Bi. Naima Abdalah Besta amekuja na wazo la kuwachangia ndugu zetu wa Somalia na hususan watoto wanaokufa njaa kila siku. Na mchango wako waweza kuwa hata wa shilingi elfu moja. Na hapa ni taarifa ya michango hadi sasa;
1. Anonymous 100,000
2. Anonymous 100,000
3.Edwin Namnauka 15,000
4. Dennis Tagalile 20,000
5.Batamwa Rwamugila 5,000
6.Joyce Mpangile 5,000
7. Humphrey Mutakyawa 10,000
8. Dr. Bukaza Chachage 10, 000
9. Fidelis Msigwa 10,000
10.Sagisto Amon 24,500
11.Omari Mzirai 10,000
12. Anonymous 10,000
13. J. J Dickson 34,750
14. Priscula Mushi 30,000
15. David Kafulila 160,000
16. Salum Maleta 10,000
17. Zitto Kabwe 250,000
18. Ephraem Madembwe 10,000
19. Sarafina Hossa 10,000
20. Fullshangweblog 20,000
21. Chibiriti 20,000
22.Joseph Rwezahura 5,000
23. Joseph Ludovic 5,000
24.Godwin Mbwiga 21,000
25.Wenge Swill 5,000
26.Brown Mwashimaha 5,000
27. Mrisho Mpoto (Mjomba) 50,000
28. Ausy Francis 15,000
29. Sigisto Simba 29,750,00
30. Anonymous 155,622, 78
31. Anonymous  20,000 
32.  Hamisi Omari 10,000
33. Nelson Bisigoro 15,000
34.  Eileen M. Kihula  30,000
35.  Anonymous      10,000
36.  Mariam Salim Milinga 15,000
37. Anonymous             50,000 
38. Halifa Mjengwa       75,000
39. Abbakari Jumanne  100,000
40. Anonymous                  16,000

Jumla iliyopatikana hadi sasa ni; 1,496,622, 78 (Shilingi Milioni Moja, laki nne  na tisini na sita , mia sita na ishirini na mbili na senti sabini na nane )

Bado tunaendelea kukusanya michango yenu...
Na hapa ni taarifa husika; Zaidi ya watu milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa katika nchi 3 za Afrika Mashariki. Watoto zaidi ya milioni mbili wako katika hali mbaya. Watoto laki 5 wamekumbwa na utapia mlo mbaya unaohatarisha maisha yao. Kati yao watoto zaidi ya 10 hufa kila siku.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani, shirika hilo linahitaji Dola za Kimarekani milioni themanini hadi kufikia mwisho wa mwaka huu ili liweze kufanikisha kazi ya kuokoa maisha ya ndugu zetu wa Somalia na hususan watoto.

Tulio tayari tusaidie kwa kuchangia kwa ajili ya watoto hao waliokumbwa na janga la njaa huko Somalia. Michango hiyo itakapopatikana itapelekwa moja kwa moja Red Cross Dar es Salaam ili baadae iwafikie walengwa.


Changia kwa kutuma kwa M-PESA 0754 678 252 Au TIGO PESA; 0712 95 61 31, ZAP 0788 111 765 ( Maggid Mjengwa) Au NMB- PESA-FASTA- 0754 678 252 ( Ukituma kwa NMB- PESA-FASTA unijulishe kwa ujumbe ili nipate nr ya simu ya mtumaji ambaye atakuwa na namba za siri za kutolea pesa)

Au ukitaka unaweza pia kutuma moja kwa moja kwenye Account Number:

01j2070759000 ( CRDB, Iringa) Jina, Maggid j. Mjengwa

Anayechangia kwa njia ya benki anijulishe kwa email au sms.
Au kwa Western Union, Maggid Mjengwa, Iringa. ( Atumaye anijulishe pia)


Namna nyingine rahisi ya kuchangia? Wasiliana na;


mjengwamaggid@gmail.com au sms; +255 754 678 252, Plus 255 712 95 61 31
Utapata maelezo ya njia rahisi ya kutuma mchango wako.

Mwisho wa kukusanya michango ni Septemba 11, 2011. Baada ya hapo tutaweka orodha ya majina na kiasi kilichochangwa kwenye Mjengwablog (http://mjengwa.blogspot.com/) na iwapo hutataka jina lako liwemo kwenye orodha, basi, utatambulika kama 'anonimous'.

Wahenga walinena; kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.

Wenu,

Maggid Mjengwa

Mratibu wa Michango
Reactions::

Anayetaka Kufaidi Mpunga Wa Eid; Aende Kwa Babu!

Pilau, biriani na ubwabwa bwelele, na  utasukumia na ' kikombe orijino' cha Babu. Wengine wote walikunywa juisi!
Reactions::

Hivi Kwa Ngeleja Hakuna Chenji Iliyobaki?!

Na watani zangu Wasukuma hawana dogo. Nasikia Ngeleja shughuli ya Jairo Wizarani aliifungia safari- Dodoma- Dar. Si kulikuwa na vya kuchoma!
Reactions::

Basi La Champion Laua Watu Nane Dodoma

  AJALI za barabarani zimezidi kutikisa nchi baada ya jana, basi la Kampuni ya Champion kupinduka na kuua watu nane papo hapo Mkoani Dodoma.Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea mnamo saa 8:00 mchana, katika kijiji cha Nala wakati basi hilo likitoka Mwanza kuelekea jijini Dar es Salaam na kwamba, majeruhi 53 wamelazwa katika hospitali ya mkoa Dodoma.

Eneo hilo la ajali ni kilomita 15 kutoka Dodoma mjini na Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zelothe Stephen amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, lakini akasema, uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo unaendelea.

Hata hivyo, kamanda Stephen alisema taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zinaeleza chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye alishindwa kulimudu gari hilo baada ya kukutana na tuta ghafla.

Kwa upande wa mashuhuda hao, walisema chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mwendo huo kasi na wakati dereva alipokutana na tuta ghafla tairi la mbele la basi hilo lilipasuka na ndipo lilipopoteza mwelekeo.


Taarifa hizo zilifafanua kwamba, baada ya basi hilo kupasuka tairi moja la mbele na kupoteza mwelekeo tairi lake jingine la mbele pia lilipasuka ndipo likapinduka matairi juu bodi chini.

Mwandishi aliyefika muda mfupi baada ya ajali, alishuhudia baadhi ya miili ikitolewa na baadhi ya marehemu walifariki kutokana na kukosa hewa kutokana na basi hilo kuwafunika wakati matairi yakiwa juu.


Katika tukio hilo, juhudi za kutoa miili ya marehemu katika basi hilo pamoja na majeruhi zilifanyika kwa takriban saa tatu tangu kutokea ajali hiyo hadi mnamo saa 11: 35 jioni.

Katika siku za karibuni nchi imeshuhudia ikitikiswa na ajali za barabarani huku Mkoa wa  Morogoro ukiwa umeandamwa zaidi kuanzia ile ya wasanii wa kundi la Five Stars, kati ya lori la Mohamed Enterprises (MeTL) na basi la Hood ambayo magari yote yaliteketea kwa moto. Chanzo:Gazeti Mwananchi. Picha ya Mtandao

Reactions::

Tendwa,Mkuchika Nao Watofautiana Vikali *Ni Kuhusu Madiwani Waliofukuzwa CHADEMA



WATENDAJI wa juu ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete wamezidi kutofautiana vikali na
kutoa misimamo inayokinzana, safari hii ikiwa ni zamu ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Bw. George Mkuchika kuhusu sakata la madiwani wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama mkoani Arusha.

Wakati Bw. Mkuchika akiruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote, Bw. Tendwa ameshangazwa na uamuzi huo na kusema kuwa serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama.


Akizungumza na gazeti hili jana, Bw.Tendwa alisema kuwa alishangazwa na uamuzi huo wa Bw. Mkuchika na kusema kuwa Bunge au diwani akiishafukuzwa uanachama ndio kikomo cha uongozi na ili kurudishia uongozi ni lazima hoja itenguliwe na mahakama.


"Serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama, haiwezekani hata kidogo, na kama mtu siyo mwanachama hawezi kuwa na wadhifa wa kubunge au diwani ni nafasi za siasa," alisisitiza.


Bw. Tendwa alitofautiana na Bw. Mkuchika kwa uamuzi wake wa kuandika barua kwa Meya wa Manispaa ya Arusha Bw. Gaudence Lyimo kuhusu hatima ya madiwani ya kutaka waendelee  kuhudhuria vikao vyote vya baraza  na kulipwa stahili zote hadi mahakama itakapotoa uamuzi.


Alisema kuwa yeye mpaka sasa haamini kama kweli Bw. Mkuchika ameamuru madiwani hao waendelee na kuhudhuria vikao vyote vya baraza huku wakiwa wamevuliwa uanachama na kwamba ameingilia uhuru wa mahakama.


"Huwezi kutengua lolote la mahakama, kwa kuwa kufanya hivyo utakuwa umeingilia uhuru wa mahakama," alisema.


Alisema kuwa hata Meya wa Arusha alitakiwa kuangalia sheria zinasemaje badala ya kukubali kupelekwapelekwa, kwa kuwa kesi hiyo iko mahakamani walichotakiwa kusubiri ni uamuzi wa mahakama pekee, ambao ndio yenye mamlaka ya kuwarejeshea uanachama au la.


Hivi karibuni, Bw. Mkuchika alidaiwa kukiuka Katiba ya nchi kutokana na kuandika barua ya kuruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote.


Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya kuahirishwa kwa kesi ya viongozi wa chama hicho katika Mahakama Kuu Mwanasheria, Bw. Method Kimomogolo alitoa kauli hiyo baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibrod Slaa kuonyesha nakala ya barua iliyotoka kwa Bw. MKuchika yenye kumb Na. HA 23/235/01/16 ya Agosti 23 mwaka huu iliyotumwa kwa Meya wa Manispaa ya Arusha, Bw. Lyimo kuhusu hatima ya madiwani hao.


Nakala ya barua hiyo ambayo ilibeba kichwa cha habari kisemacho: "Kuvuliwa uanachama hivyo kukosa sifa ya kuwa diwani huku mwisho wa barua hiyo ikisema kuwa 'kutokana na na madiwani hao watano kufungua kesi na kuiomba mahakama kuwarejesha uanachama wataendelea kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili yote hadi mahakama itakapotoa uamuzi'.


Bw. Kimomogolo alisema maamuzi yaliyofikiwa na Bw. MKuchika yalikiuka Katiba ya Muungano kwa vile mtu anayehitaji kugombea uongozi katika nafasi yoyote ni lazima awe na dhamana ya chama.


Alisema kuwa vipengele vingine vinaweka bayana kuwa katika suala la urais, ubunge na udiwani utakoma pindi chama kilichomwekea dhamana kitaondoa dhamana yake na kusema kwa kuwa tayari CHADEMA ilikwishaindoa dhamana kwa madiwani hao sasa hawana sifa.


Bw. Kimomogolo alisema kuwa inashangaza kuona serikali iliyopinga mgombea binafsi mahakamani na kushinda kesi, inakuja kuwatambua madiwani ambao mdhamini wao wamekwishawafukuza ambaye ni CHADEMA.


"Kwenye kesi aliyofungua Mchungaji Christopher Mtikila, ambapo mahakama imeamua hakuna mgombea binafsi, hivyo maamuzi yanayofanywa na madiwani hao kwenye kwenye vikao vya baraza nayo ni batili na posho wanazopokea ni wizi na anayewapa atawajibika kuzilipa,"alisema.


Naye Dkt. Slaa alisema kuwa alishangazwa na maamuzi hayo kwa kuwa madiwani hao walikwishavuliwa uanachama na kupelekea kukimbilia mahakamani ili kurejeshewa uanachama wao hivyo iwapo waziri ataendelea kuwatambua wakati chama hicho kiliondoa dhamana ni kukiuka taratibu za sheria.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Bw. Estomii Chang'a alikiri kuipata barua hiyo na kwamba anachokitekeleza ni maamuzi hayo yaliyotoka ngazi za juu.


Madiwani waliofukuzwa CHADEMA baada ya kukaidi maamuzi ya Kamati Kuu yaliyowataka kujivua nyadhifa walizopata kupitia muafaka walioingia bila baraka za chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya Bw. Estomii Mallah (Kimandoli),Bw. Charles Mpanda (Kaloleni),Bw. Ruben Ngowi (Themi) na Bibi. Rehema Mohamed (Viti Maalum).Chanzo, Gazeti Majira




Reactions::

Majeshi Ya Gaddafi Yatakiwa Kusalimu Amri

Viongozi wa waasi wa Libya wamewapa majeshi yanayomwuunga mkono Kanali Gaddafi mpaka Jumamosi kusalimu amri au kukabiliana na majeshi.
Mustafa Abdul Jalil, anayeongoza Baraza la Mpito la Taifa (NTC), alisema onyo hilo limeelekezwa kwa wanaomtii Kanali Muammar Gaddafi waliopo mji alipozaliwa wa Sirte na katika miji mengine.
Tangazo hilo limetolewa baada ya mke wa Kanali Gaddafi na watoto wake watatu kukimbilia nchi jirani ya Algeria.
Algeria imejitetea kwa hatua hiyo waliochukua, huku waasi wakiita " kitendo cha kiburi".
Mpaka sasa mahala alipo Kanali Gaddafi haijulikani.
Wakati huo huo huo huko Libya, waasi wanajaribu kupambana na wanaomtii Gaddafi, na kujiandaa kusogea Sirte.BBC
Reactions::

Tuesday, August 30, 2011

Sherehe Ya Siku Ya Kuzaliwa Ya Mtoto Iman Pinto

Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akikata keki tayari kumlisha mwanawe Imani

Mtoto wa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto, Imani Pinto, akikata keki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka minne ya kuzaliwa kwake, mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam.

Reactions::

Beach Soccer World Cup Revenna, Italy

AsalamAlkum,
Eid Mubarak,
hali yako ndugu yangu, nakutumia picha ya team yangu ya Oman ya Beach
tukiwa katika mji wa Revenna, tayari kwa mashindano ya kombe la Dunia la
mpira wa Ufukweni linalo anza tarehe 01/9/2011.
mechi yetu ya kwanza itakua ya ufunguzi na timu ya Argentina siku ya ufunguzi
tarehe 1/9.
nakua nakupa matokeo au pia unaweza kupata kwenye www.beachsoccerworldwide.com
Nakutakia Eid njema na familia yako.
Talib Hilal

Reactions::

Benki Ya NMB Tawi La Ludewa Lawamani

Wananchi wa jimbo la Ludewa ambao ni wateja wa benki ya NMB tawi la Ludewa wametinga nyumba kwa mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe, wakitaka awasaidie kuishtaki benki hiyo kwa madai ya upotevu wa fedha zao katika mazingira tata.
Agnesi Mapunda ni mtumishi wa Halmashauri ya Ludewa idara ya ardhi ambaye ni mteja wa benki hiyo mwenye akanti namba 6012400590 NMB tawi la Ludewa ambaye alidai kuwa akaunti yake ilikuwa na fedha zaidi ya shilingi milioni 1 ila mwezi wa sita alikuta akaunti hiyo ikiwa na salio la shilingi 144,000 pekee na baada ya kuuliza aliambiwa fedha zake zimetolewa kwa huduma ya pesa fasta na NMB Mobel huduma ambayo kwa upande wake hajawahi kuitumia toka awe mteja wa benki hiyo.
Hata hivyo alisema baada ya kuhoji sana ndipo benki hiyo ilipoamua kuchunguza suala hilo na kubaini majina ya watu waliohamisha fedha hizo na kuwa hadi sasa suala hilo lipo polisi linafanyiwa kazi.
Huku baadhi ya wateja wakienda benki hapo na polisi kutaka kufunga akaunti zao na kuhama uteja na benki hiyo .
Walisema kuwa wakati mwingine baada ya kufika na kulalamika katika benki hiyo na kuambiwa wafike baada ya siku mbili ama tatu na kukuta akaunti zao zinapesa kama walivyoziacha .
Mbunge wa jimbo hilo amekili kupokea malalamiko hayo na tayari amewasiliana na meneja wa kanda na meneja wa tawi la benki hiyo ili kutolea ufafanuzi suala hilo.
Hata hivyo alisema kuwa majibu ambayo ameelezwa na viongozi hao  inawezekana fedha hizo zinachnukuliwa na jamaa wa wateja hao ambao wamekuwa wakiwapa namba zao za siri bila kujua ama kwa kujua ama ni kampuni ya simu ambayo inashughulika na huduma hiyo .
Pia alisema kuwa ameshangazwa na ushirikiano mdogo wa wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Ludewa kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa wateja wao wenye matatizo hayo kwa kuwataka waende polisi kufikisha malalamiko yao huku wakijua wazi kuwa wateja hao wameingia mkataba na benki ya sio polisi .
Hata hivyo meneja wa NMB tawi la Ludewa alipotafutwa kwa simu alisema kuwa hana mamlaka ya kulizungumzia suala hilo na kuwa uongozi wa juu wa benki hiyo ndio unaweza kuzungumzia suala hilo. Imeandikwa na Francis Godwin, kutoka Iringa.

Reactions::

Hii Ndio Chakachua Orijino!


Haichuji, haichachi, we acha tu!
Reactions::

Precision Air Services LMT Imeanzisha Safari Za Ndege Kwenda Nchini Afrika Kusini

Mkurugenzi na ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Ndege la Precision Air Services LMT,  Alfonse Kioko, (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsk jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanzishwaji kwa huduma mpya ya ndege za kampuni hiyo kwenda nchini Afrika Kusini,  iliyoanza kutolewa na shirika hilo hivi karibuni. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Ubora na Usalama, Bwana Allen na kulia ni Kulia ni Mkurugenzi wa biashara Phil Mwakitawa.  Picha na Victor Makinda.

Reactions::

Jumuiya Ya Waislamu Wa-Tanzania Waishio Marekani Wamfuturisha Balozi Mwanaidi Maajar

Mgeni rasmi katika futari ya pamoja akitoa hutuba fupi ya kuwa pongeza na kuwashukuru viongozi pamoja na wana Jumuiya ya kiislamu Tanzanian Muslim Community Washngton DC, na kutoa hotuba fupi ya kuhamasisha Watanzania waliokuwepo hapa Marekani kujumuika na kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa Nchi yetu Tanzania.

Mgeni rasmi Balozi Mwanaidi Maajar akiwa na waumini katika futari iliyoandaliwa na jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community, kwenye ukumbi wa Hillandale Local Park, New Hampshire Avenue, Silver Spring Maryland Nchini Marekani.

Waumini wakipata futari ilioandaliwa na jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community Washngton DC

Waumini wa jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community wakiwa katika futari

Reactions::

Wasuni Waswali Swala Ya Idd al Fitr Leo

Waumini wa Kiislamu wa dhehebu la Suni,wakiingia katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya swala ya Idd al Fitr.


Waumini wa dini ya Kiislamu wa dhehebu la Suni, wakiswali swala ya Idd al Fitr leo asubuhi katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam.  Wakati Wasuni wameadhimisha sikukuu ya Idd al Fitr leo, kesho Waislamu wengine wataadhimisha sikuukuu hiyo.  Hii....INAKANGANYA kidogo.. Kwenu wanazuoni wa Kiislamu.  Picha zote na Victor Makinda

Reactions::

Dr. Dalaly Peter Kafumu Ndiye Mgombea Ubunge Jimbo La Igunga Kwa Tiketi Ya CCM

Dr. Dalaly Peter Kafumu. 'Daima Mbele'


Reactions::

Baa La Njaa Somalia; Orodha Ya Waliochangia Na Jumla Iliyopatikana Hadi Sasa....


Watoto Wanne Wanakufa, Familia Moja; Tunafanya Nini?
Mwenzetu Bi. Naima Abdalah Besta amekuja na wazo la kuwachangia ndugu zetu wa Somalia na hususan watoto wanaokufa njaa kila siku. Na mchango wako waweza kuwa hata wa shilingi elfu moja. Na hapa ni taarifa ya michango hadi sasa;
1. Anonymous 100,000
2. Anonymous 100,000
3.Edwin Namnauka 15,000
4. Dennis Tagalile 20,000
5.Batamwa Rwamugila 5,000
6.Joyce Mpangile 5,000
7. Humphrey Mutakyawa 10,000
8. Dr. Bukaza Chachage 10, 000
9. Fidelis Msigwa 10,000
10.Sagisto Amon 24,500
11.Omari Mzirai 10,000
12. Anonymous 10,000
13. J. J Dickson 34,750
14. Priscula Mushi 30,000
15. David Kafulila 160,000
16. Salum Maleta 10,000
17. Zitto Kabwe 250,000
18. Ephraem Madembwe 10,000
19. Sarafina Hossa 10,000
20. Fullshangweblog 20,000
21. Chibiriti 20,000
22.Joseph Rwezahura 5,000
23. Joseph Ludovic 5,000
24.Godwin Mbwiga 21,000
25.Wenge Swill 5,000
26.Brown Mwashimaha 5,000
27. Mrisho Mpoto (Mjomba) 50,000
28. Ausy Francis 15,000
29. Sigisto Simba 29,750,00
30. Anonymous 155,622, 78
31. Anonymous  20,000 
32.  Hamisi Omari 10,000
33. Nelson Bisigoro 15,000
34.  Eileen M. Kihula  30,000
35.  Anonymous      10,000
36.  Mariam Salim Milinga 15,000
37. Anonymous             50,000 
38. Halifa Mjengwa       75,000
39. Abbakari Jumanne  100,000
40. Anonymous                  16,000

Jumla iliyopatikana hadi sasa ni; 1,496,622, 78 (Shilingi Milioni Moja, laki nne  na tisini na sita , mia sita na ishirini na mbili na senti sabini na nane )

Bado tunaendelea kukusanya michango yenu...
Na hapa ni taarifa husika; Zaidi ya watu milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa katika nchi 3 za Afrika Mashariki. Watoto zaidi ya milioni mbili wako katika hali mbaya. Watoto laki 5 wamekumbwa na utapia mlo mbaya unaohatarisha maisha yao. Kati yao watoto zaidi ya 10 hufa kila siku.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani, shirika hilo linahitaji Dola za Kimarekani milioni themanini hadi kufikia mwisho wa mwaka huu ili liweze kufanikisha kazi ya kuokoa maisha ya ndugu zetu wa Somalia na hususan watoto.

Tulio tayari tusaidie kwa kuchangia kwa ajili ya watoto hao waliokumbwa na janga la njaa huko Somalia. Michango hiyo itakapopatikana itapelekwa moja kwa moja Red Cross Dar es Salaam ili baadae iwafikie walengwa.


Changia kwa kutuma kwa M-PESA 0754 678 252 Au TIGO PESA; 0712 95 61 31, ZAP 0788 111 765 ( Maggid Mjengwa) Au NMB- PESA-FASTA- 0754 678 252 ( Ukituma kwa NMB- PESA-FASTA unijulishe kwa ujumbe ili nipate nr ya simu ya mtumaji ambaye atakuwa na namba za siri za kutolea pesa)

Au ukitaka unaweza pia kutuma moja kwa moja kwenye Account Number:

01j2070759000 ( CRDB, Iringa) Jina, Maggid j. Mjengwa

Anayechangia kwa njia ya benki anijulishe kwa email au sms.
Au kwa Western Union, Maggid Mjengwa, Iringa. ( Atumaye anijulishe pia)


Namna nyingine rahisi ya kuchangia? Wasiliana na;


mjengwamaggid@gmail.com au sms; +255 754 678 252, Plus 255 712 95 61 31
Utapata maelezo ya njia rahisi ya kutuma mchango wako.

Mwisho wa kukusanya michango ni Septemba 11, 2011. Baada ya hapo tutaweka orodha ya majina na kiasi kilichochangwa kwenye Mjengwablog (http://mjengwa.blogspot.com/) na iwapo hutataka jina lako liwemo kwenye orodha, basi, utatambulika kama 'anonimous'.

Wahenga walinena; kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.

Wenu,

Maggid Mjengwa

Mratibu wa Michango
Reactions::

Hii Imekaaje?

Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana amemwita ofisini kwake Balozi wa Libya nchini Prof.  Ahmed Al Ash'hab. Kisa? Ubalozi huo umebadilisha bendera ya Libya, kuondoa iliyokuwa ikitumika enzi za Gaddafi na kuweka inayotumiwa sasa nchini Libya. Ubalozi huo unaambiwa umefanya hivyo  bila kufuata utaratibu. Je, hii imekaaje? Picha na Tagie Mwakawago wa Mambo ya Nje.
Reactions::

Tanzanian Muslim Community In Washington DC Metro, Inakutakia....

IDD MUBARAK



Uongozi wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC Metro(TAMCO) unawatakia wote IDDI MUBARAK.


Pia mnakaribiswa katika sherehe za Aidil Fitr za Pamoja zitakazo fanyika at:

Hillandale PAB - Hillandale Local Park:
10615 New Hampshire Avenue,
Silver Spring,
MD 20903

SAT. 09/03/11

Starting at 3.00PM

Uongozi

TAMCO
Reactions::

Biafra Jogging And Sports Club!

Pichani ni Kinondoni Biafra miaka ya 80

BIAFRA JOGGING & SPORTS CLUB – 90 DEGREE PUB KINONDONI


RATIBA YA HAFLA YA KUJUMUIKA PAMOJA NA WATOTO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD MOSI, UKUMBI WA 90 DEGREES PUB KINONDONI - AGOSTI, 2011

MUDA
TUKIO
MUHUSIKA
07:00 – 08:00
Wadau wote kuwasili klabuni na maandalizi ya kuanza kukimbia
Katibu Msaidizi Biafra Jogging
08:00 – 09:00
Uzinduzi wa mbio
M/Kiti S/M na M/Kiti Biafra Jogging
09:00 – 09:30
Chai kwa watoto
Meneja 90° Pub, Sarah, Emmy
09:30 – 10:30
Kuwasili uwanjani na kuanza michezo mbalimbali
William John, Selemani Hamis
10:30 – 11:00
Kurudi klabuni na kuwasili kwa mgni rasmi
Katibu Biafra Jogging
11:30 – 11:45
Kusomwa Risala ya watoto
Katibu, mwakilishi tok Boko
11:45 – 12:30
Burudani ya nyimbo na maigizo toka kwa watoto
Katibu Biafra Jogging, watoto
12:30 – 12:45
Risala na maelezo mafupi ya klabu
Mkurugenzi 90°Pub, viongozi klabu rafiki
12:45 – 01:00
Maneno machache toka kwa mgeni rasmi (kujibu risala)
Mgeni Rasmi
01:00 – 01:45
Mashindano mbalimbali ya watoto (chemsha bongo, kucheza, n.k.)
Katibu, Mkurugenzi 90° Pub, watoto
01:45 – 02:45
Chakula cha mchana na burudani
Meneja 90°, Happy Mdeka, Sarah, Riddy Sound
02:45 – 03:00
Burudani na maandalizi ya zawadi
Happy Mdeka, Mkurugenzi 90°, Makamu M/kiti
03:00 – 03:30
Kugawa zawadi kwa watoto walioshiriki mashindano
Mgeni Rasmi, Makamu M/Kiti, Mkurugenzi 90°
03:30 – 04:00
Burudani ya muziki kwa watoto
Ritchie - Riddy Sound “in the house”
04:00 – 04:30
Watoto kuondoka
Henry Maseko, Robert Kabugi, Makamu M/Kiti

KARIBU SANA, JUMUIKA PAMOJA NA WATOTO KWA UPENDO, FURAHA NA MATUMAINI
Reactions::

Zawadi Ya Eid Toka Kwa Mwanablogu Nova Kambota

Natoa wazo “ukweli mchungu ila una manufaa” sasa naomba nitofautiane na watanzania wenzangu kuelekea siku kuu ya Idd Elfitri, mimi sitatoa mbuzi, sitatoa mchele wala soda, bali natoa zawadi itakayoishi milele kuanzia kwa watoto wetu mpaka wazee wetu, Idd Mubarak watanzania wenzangu “NAOMBA TUJENGE UTAMADUNI WA KUPENDA KUJISOMEA DAIMA”
Nova Kambota
Reactions::

Monday, August 29, 2011

JK Aongoza Kikao cha Kamati Kuu Ya CCM Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya Halmashuri kuu ya CCM kilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo (Picha na Freddy Maro)

Reactions::

Tanzania Yakiri Gaddafi Kuangushwa

TANZANIA imekiri utawala wa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, kuangushwa huku ubalozi wa nchi hiyo nchini, ukipandisha bendera ya waasi.Kuangushwa
kwa utawala wa Kanali Gaddafi, kumethibitishwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

"Kimsingi utawala wa miongo minne wa kiongozi wa Libya Kanali Ghaddafi umeanguka kutokana waasi hao wanasaidiwa na mataifa ya magharibi kuteka na kudhibiti miji mingi ukiwemo Mji Mkuu wa Tripoli," alisema Bw. Membe na kuongeza kuwa mapigano bado yanaendelea ndani ya nchi hiyo.


Alisema Tanzania na Umoja wa Afrika (AU) zinasisitiza mazungumzo ya amani ili kufikia makubaliano. Aliongeza kuwa Tanzania  imekuwa ikifanya hivyo kutafuta suluhu la   migogoro mingi kwenye nchi nyingi za Afrika.


Alisema mgogoro wa Libya una sura ya koo mbalimbali kupingana, hivyo si rahisi kuutambua utawala wa waasi ambao bado haujawa na mfumo unaoeleweka.


"Unapozungumzia serikali si kikundi kinasimama na kusema ni utawala, hapana serikali ni lazima iwe mfumo unaokubalika wa Mahakama, Bunge na Utawala,  sisi tunataka wafikie hapo kwa faida ya Walibya," alisema Bw. Membe.


Alisema pamoja na nchi nyingi kutambua Baraza la Waasi, Tanzania haitafanya hivyo hadi hapo taratibu muhimu zitakapofuatwa kwa manufaa ya pande zote zinazohusika katika mgogoro huo.


Aliongeza kuwa awali AU ilionya hatua ya kuwaunga mkono waasi, lakini Balaza Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kudhibiti matumizi ya anga ya Libya, kwa nia ya kulinda usalama wa raia dhidi ya mashambulizi ya vikosi vya serikali, lakini baadhi ya mataifa ya magharibi yalitafsiri vibaya azimio hilo, kwa kutumia nafasi hiyo kushambulia utawala uliopo madarakani.


Alipoulizwa kuhusu hatua ya ubalozi wa Libya nchini kupandisha bendera ya waasi, Bw. Membe alisema Libya kama nchi ina haki ya kufanya jambo ndani ya ubalozi, bila kuathiri uhusiano wa kimataifa.


Alisema sehemu ile (ubalozini) kwa mujibu wa sheria za kimataifa ni ardhi ya nchi nyingine na kuwataka Walibya waliopo nchini kuwa watulivu katika kipindi hiki.


Bw. Membe pia alizungumzia tatizo  la njaa kwenye nchi ya Somaria na kuelezea kuwa ni janga la kutisha linalohitaji msaada wa haraka.


Alisema Tanzania inashiriki  kuhakikisha msaada wa chakula unapelekwa haraka kuokoa maisha ya binadamu.Alisema Tanzania itatoa kiasi cha dola za Marekani 200,000 kusaidia wananchi wa nchi hiyo.


Alisema ili kuunga mkono juhudi za jumuiya za kimataifa za kuokoa maisha ya Wasomaria wanaokufa kwa njaa, Tanzania imetoa msaada wa tani 300 za chakula na pia itauza kwa bei ndogo chakula cha akiba tani 11,000 kwa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) ili kisaidie kunusuru watu zaidi ya milioni 12 wanaokabiliwa na njaa.Chanzo, Gazeti Majira

>

 


 
Reactions::