Friday, September 30, 2011
Mlaki, Stellan Na Omar
Theophilius Mlaki, MC na Mshauri wa masuala ya ICT . Wengine ni Stellan Arvidsson and Omar Mzee from kutoka Ubalozi wa Sweden, Dar es Salaam. Wote wanaudhuria mkutano wa SADCkuhusu Elimu ya Watu Wazima na Elimu Masafa unaofanyika Ubungo Plaza asubuhi hii.
| Reactions:: |
Picha Ya Masafa!
A distance photo! Mkutano wa SADC, Elimu ya Watu Wazima kwa njia ya masafa. Ubungo Plaza, asubuhi hii.
| Reactions:: |
Kulia Kwa Mwenyekiti Ni Mke Wa Mwenyekiti!
Wa kwanza kushoto ni Stellan Arvidssson, anahusika na elimu ubalozi wa Sweden. Na wa mwisho kulia ni mama Mgweno, Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto nayehusika na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi. Pichani ni kwenye mkutano wa SADC kuhusu elimu ya Watu Wazima na hususan elimu masafa. Mkutano unatarajiwa kuanza punde tu.
| Reactions:: |
Mama Mgweno Na Omar Mzee
Mama Mgweno, Mkurugenzi Msaidizi, Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi, Wizara Ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Na Watoto. Kulia ni Omar Mzee anahusika na masuala ya ICT ubalozi wa Sweden, Dar es Salaam. Wote wanaudhuria Mkutano wa SADC kuhusiana na Elimu ya Watu Wazima hususan kuhusu Masafa unaotarajiwa kuanza punde hapa Ubungo Plaza. Mkutano utafunguliwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba Na Sheria.
| Reactions:: |
Makamu Wa Rais Akutana Na Waziri Wa Maendeleo Na Ushirikiano Wa Kimataifa Wa Sweden
1. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo jijini Stockholm Sweden hivi karibuni. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
2. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha yenye Taswara ya mjini wa Zanzibar, Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati Makamu alipofika Ofisini kwa waziri huyo jijini Stockholm Sweden kwa mazungumzo hivi karibuni. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
3. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akichangia katika kongamano la lililoandaliwa na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, kuhusu nafasi ya uhusiano wa Tanzania na Sweden, lililofanyika jijini Stockholm Sweden majuzi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
| Reactions:: |
DUCE: IMPORTANT NOTICE TO FIRST YEAR STUDENTS 2011/2012
DAR ES SALAAM UNIVERSITY
COLLEGE OF EDUCATION
A Constituent College of the University of Dar es Salaam
Tel 022-2850978
Fax 022-2850852
E-mail:
dpacademic@duce.ac.tz
OFFICE OF THE DEPUTY PRINCIPAL
ACADEMIC
IMPORTANT NOTICE TO FIRST YEAR STUDENTS 2011/2012
The Dar es salaam University College of Education (DUCE) is pleased to inform all first year
students admitted into various undergraduate degree programmes offered at the College for 2011/2012
academic year the following:
• Report at the College on Saturday 1st October, 2011 ready for Orientation Week. The college is
located at Chang’ombe in Temeke Municipality, along Taifa Road, adjacent to National Stadium.
Pay TUITION FEE and DIRECT UNIVERSITYCOSTS before being allowed to register and
access College facilities. All students under Higher Education Students Loans Board (HESLB) are
required to pay their tuition fees corresponding to the amount remained after the allocation made by
the Loans Board. For more information on allocated amount visit www.heslb.go.tz
FEE STRUCTURE FOR 2011/2012 ACADEMIC YEAR
Fees Payable by Students
Degree Programme
Faculty
Tuition Fee
Tanzanians (T.shs)
Foreigners (USD)
Bachelor of Arts with Faculty of Humanities & 1,000,000/=
2,100.00
Education
Social Sciences
Bachelor of Education in Faculty of Education
Arts
Bachelor of Science with Faculty of Science
1,300,000/=
2,700.00
Education
Bachelor of Education in Faculty of Education
Science
N.B: In addition to the payment of tuition fees, all students are required to pay direct university costs
amounting to Tshs 77,400/= covering the following:
Direct University Costs (Payable to the University)
Cost Item
Tanzanians (Tshs)
Medical Capitation
50,400
Registration fee
5,000
Examination Fee
12,000
Identity Card
5,000
Student’s Union Fee
5,000
Total
77,400
Payment of Tuition Fees and Direct University Costs should be made through the National Bank
of Commerce (NBC), Account Number 071101000196 and original bank pay–in slip should be
submitted to the bursar’s office for issuance of receipts. Those who have National Health Insurance
Fund (NHIF) cards should not pay medical capitation fee.
• DUCE has limited accommodation facilities. Therefore, priority will be given to female students
from up country and students with disabilities. Students are urged to find their own accommodation
outside the College campus, where rooms can be available for about Tshs 30,000 and above per
month.
• DUCE charges Tshs120,000/= as accommodation cost per year which can be paid in two
installments of Tshs 60,000/= at the start of each semester.
No student will be registered unless he/she brings original bank pay-in-slip as an evidence of fee
payment as well as Original Certificates which supported his/her application (result slips will not be
accepted)
Students need to have enough funds to cater for stationery, books, meals and accommodation while
waiting for loans from Higher Education Students Loans Board.
• On the arrival day, students are advised to avoid carrying heavy luggage so as to minimize
inconveniences.
• Joining instructions can be collected at the College from the date of this announcement to 1st
October, 2011 from 10:00 am – 3:30 pm.
• In case of any inquiry do not hesitate to contact the office of the Deputy Principal Academic
through:
Tell: 255222850978
Mobile: 0714 127 108 or 0784 504 158
E-mail: dpacademic@duce.ac.tz or eliawonyi@hotmail.com.
Website: www.duce.ac.tz
Foreigners (USD)
125.00
100 .00
120.00
5.00
5.00
355.00
Issued by the office of Deputy Principal Academic
Prof. E.T. Mallya
| Reactions:: |
CCM Yanendelea Na Kampeni Igunga
2. Mgombea Ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu akihutubia umati wa wananchi katika kijiji cha Igoweko, jana.
NA BASHIR NKOROMO, IGUNGA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wananchi wa jimbo la Igunga mkoani Tabora kumchagua mgombea wake Dk. Dalaly Kafumu utekelezaji wa mipango ya kuendeleza jimbo hilo usikwame.
Wameambiwa mgombea wa CCM litakuwa chaguo sahihi kwao kwa sababu ndiye atakayeweza kusimamia mipango ya maendeleo iliyokwisha ratibiwa, tofauti na kuchagua mbunge wa upinzani ambaye atatumia muda mwingi kulalamika badala ya kusimamia maendeleo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni za CCM iliyofanyika katika Kata za Nanga na Ziba, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alisema, unalazima wa kumchagua mgombea wa CCM unatokana na sababu nyingi za msingi.
Lusinde alisema, baadhi ya sababu hizo ni kwamba uchaguzi mdogo hautabadilisha serikali ya sasa wala ilani inayotekelezwa ambayo ni ya CCM kwa kuwa ilani na serikali inayotekeleza kwa sasa ni ya CCM kwa kuwa ndiyo ilipewa ridhaa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana baada ya kuipa ushindi CCM kwa kura nyingi za urais na wabunge.
"Jamani mtu mwenye akili kama nguo yake nyeusi ikitoboka atatia kiraka cha rangi ile ile nyeusi au nyingine?, kwa vyovyote hawezi kuweka rangi tofauti na nyeusi kwa kuwa ndiyo rangi ya nguo yake, hivyo kwa kuwa mgombea aliyeondoka alikuwa wa CCM hakuna sababu ya kuweka wa upinzani", alisema Lusinde.
Akimnadi mgombea wa CCM, Dk. Kafumu, Lusinde alisema, ni mgombea mahiri ambaye akilinganishwa na wagombea wa vyama vingine kama CHADEMA na CUF hawawezi kumfikia tangu katika uwezo kielimu na hata uadilifu.
Akiomba kura kwa wananchi, Dk. Kafumu aliwaomba wananchi wa Igunga wana-CCM, wapenzi wa CCM, na wale wa vyama vya upinzani na wasio na vyama kumchagua yeye kwa kuwa anao uhakika kwa asilimia mia moja kwamba ataweza kuibadilisha Igunga kimaendeleo.
"Hapa tunachotafuta kwa kweli si ushindani wa vyama, tunatafuta maendeleo na kwa minajili ya maendeleo nichagueni mimi hata bila kujali itikadi za vyama vyenu kwa kuwa ninao uwezo mkubwa wa kusimamia na kuharakisha upatikanaji maendeleo hapa Igunga", alisema Dk. Kafumu.
Aliwataka wananchi wa Igunga hasa vijana kuachana na siasa za chuki akisema kwamba kufanya hivyo hakutaleta manufaa yoyote zaidi ya maafa baada ya uchagfuzi jambo ambalo litasababisha wana Igunga kubaki wanauguza majeraha ya magomvi wakati waliowashawishi kuvunja amani yao wakiwa wameshaondoka kurejea kwao.
"Tahafadhalini sana vijana, jitahidini kusikiliza sera na kutafuta kwa makini mgombea atakayewaletea maendeleo hapa Igunga ambaye ni mimi, msiwe na haja ya kupigana na kuumizana kwa ajili ya uchaguzi ila uchaguzi uwe sababu ya ninyi kushikamana zaidi" alisema.
Mgombea huyo alianza kampeni zake kwa helkopta tangu juzi ilipowasili na jana peke yake alitarajiwa kufanya mikutano 30 katika maeneo na kata mbalimbali jimboni hapa.
Uchaguzi mdogo jimbo la Igunga umepanagwa kufanyika Jumapili wiki hii, baada ya kampeni za muda takribani mwezi mzima ambazo zitazifikia kikomo Jumamosi wiki hii.
| Reactions:: |
Good News For All Who Own Or Plan Buying American Vehicles In East Africa!
or all who own or plan buying American Vehicles; we want to let you know that we got your back on spare parts and accessories related with your vehicles. We are working with largest auto parts suppliers the United States: new, Used and aftermarket. We are here to help you if you need to buy: vehicles or Spare parts. We here to save you, have peace of mind and enjoying American Pie. For enquires and price quotes do not hesitate to contact us:
Besigwa Njilomo:
East Africa Manager
American Pie Automotive Supply, LLP.
Email: Bnjilomo@gmail.com
Skype: americanpie360
| Reactions:: |
Thursday, September 29, 2011
Leo Nilikuwa Na Safari Ngumu Na Mafungu Hayakuwezekana!
Pichani ni Mikumi, leo mchana.
Ndugu zangu,
Nimeingia Dar usiku huu nikitokea Iringa. Nimechoka sana kwa safari ngumu. Nilipofika katikati ya mbuga ya Mikumi alasiri ya leo, basi, mvua kubwa ilinyesha. Na udereva ukawa mgumu pia. Njia nzima ilikuwa na mvua mpaka ndani ya Morogoro. Pale Mdaula nikapata pancha tairi ya nyuma. Usiombe kubadilisha tairi kwenye mvua. Kesho nikiwa hapa Dar nitaudhuria mkutano wa kimataifa wa siku 2 juu ya elimu ya watu wazima na hususan elimu masafa. Kwa mujibu wa ratiba Rais Jakaya Kikwete
atafungua mkutano huo.
Maggid,
Dar es Salaam
| Reactions:: |
Makamu Wa Rais Dr Bilal Akiwa Sweden
Baa La Njaa Somalia: Michango Yenu Imewasilishwa UNICEF Juma La Jana
Septemba 22, 2011. Jumla hiyo inayoonekana kwenye risiti ya benki. Kwa bahati mbaya karani wa benki alishindwa kuingiza senti 78. Niliweza pia kufika ofisi za Unicef Dar es Salaam na kukabidhi risiti ya michango yenu.
Tunawashukuru nyote mliojitolea kuokoa maisha ya watoto wa Somalia walio kwenye baa la njaa.
Maggid Mjengwa,
Mratibu wa Michango.
| Reactions:: |
Baa La Njaa Somalia: Orodha Ya Mwisho Ya Waliopata Nafasi Ya Kujitolea
Orodha:
1. Anonymous 100,000
2. Anonymous 100,000
3.Edwin Namnauka 15,000
4. Dennis Tagalile 20,000
5.Batamwa Rwamugila 5,000
6.Joyce Mpangile 5,000
7. Humphrey Mutakyawa 10,000
8. Dr. Bukaza Chachage 10, 000
9. Fidelis Msigwa 10,000
10.Sagisto Amon 24,500
11.Omari Mzirai 10,000
12. Anonymous 10,000
13. J. J Dickson 34,750
14. Priscula Mushi 30,000
15. David Kafulila 160,000
16. Salum Maleta 10,000
17. Zitto Kabwe 250,000
18. Ephraem Madembwe 10,000
19. Sarafina Hossa 10,000
20. Fullshangweblog 20,000
21. Chibiriti 20,000
22.Joseph Rwezahura 5,000
23. Joseph Ludovic 5,000
24.Godwin Mbwiga 21,000
25.Wenge Swill 5,000
26.Brown Mwashimaha 5,000
27. Mrisho Mpoto (Mjomba) 50,000
28. Ausy Francis 15,000
29. Sigisto Simba 29,750,00
30. Anonymous 155,622, 78
31. Anonymous 20,000
31. Anonymous 20,000
32. Hamisi Omari 10,000
33. Nelson Bisigoro 15,000
34. Eileen M. Kihula 30,000
35. Anonymous 10,000
36. Mariam Salim Milinga 15,000
37. Anonymous 50,000
37. Anonymous 50,000
38. Halifa Mjengwa 75,000
39. Abbakari Jumanne 100,000
40. Anonymous 16,000
40. Anonymous 16,000
41. Ally Masoud 10,000
42. Anonymous 15,000
43. Frank Mwaisumbe 12,000
44. Stephen Chang'a 27,000
45. Peter Msigwa 50,000
46. Sebastian Nambi 7,000
47. Kristeen Chachage 50,000
48. Anonymous 40,000
49. Anonymous 150,000
50. Mary S 50,000
51. Jumbe Abdalah 90,000
52. Malick Malick 20,000
Jumla iliyokusanywa mpaka kufikia saa sita usiku Septemba 11, 2011 ni; 2,017,622, 78 (Shilingi Milioni Mbili, kumi na saba elfu , mia sita na ishirini na mbili na senti sabini na nane )
Wahenga walinena; kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
Wenu,
Maggid Mjengwa
| Reactions:: |
Baa La Njaa Somalia: Salaam Za Shukran Kutoka Kwa Mwenzetu Naima Besta
Pichani: Naima Abdallah Besta
Wapendwa wanakijiji wenzangu wa Mjengwablog,
Wapendwa wanakijiji wenzangu wa Mjengwablog,
Ninatoa shukrani zangu za dhati kabisa kutoka ndani ya nafsi yangu kwa kuitikia kwenu wito wangu na wa Mwenyekiti wetu bwana Mjengwa uliotuwezesha kuchangisha kiasi cha pesa kilichopatikana. Pia ninamshukuru Mwenyezi mungu kwa kutuwezesha sisi kuwakumbuka wenzetu wenye shida.
Baada ya kutoa shukrani,
napenda kusema kuwa nimepata faraja kubwa sana kwa kujitokeza kwenu kuchangia watoto wa Somalia. Mimi kama mzazi nilipoona picha zinazoonyesha hali halisi huko Somalia na kaskazini mwa Kenya, nilifadhaika sana. Na nililia sana nilipoona kwenye TV mama aliyefiwa na watoto 4 ndani ya masaa 24 akiwa anapapasa kaburi la mwanae.
Kwa kweli kama mzazi nilisikia uchungu sana kwani kila mzazi matarajio yake ni kuwaona watoto wake wakiwa na afya njema, wakicheza kwa furaha na kukua kuwa watu wazima, lakini sio huo mtihani uliompata huyo mama na wamama wengine wa Somalia waliowaacha watoto wao pembeni mwa barabara.
Hivyo nikajitazama mimi kama mwanadamu nakujiuliza mimi kiumbe dhaifu lakini Mwenyezi Mungu ameniruzuku kwa rehma zake nyingi sina budi kufanya jambo lolote ambalo litasaidia kuokoa maisha ya watoto wa Somalia.
Waswahili walisema haba na haba hujaza kibaba, hicho mlichochangia si haba kinaweza kununua chakula cha kuokoa maisha ya watoto zaidi ya 30 kwa kuwapatia chakula cha kutibu utapiamlo mkali unaohatarisha maisha yao.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu awape ulinzi wake nyinyi pamoja na familia zenu, na aendelee kuwaruzuku rizki zisizo ukomo na muendelee na moyo huo huo wa kuthamini wanadamu wengine.
Ahsanteni sana na mbarikiwe wote.
Naima Abdallah Besta
| Reactions:: |
Tamko La Madereva Wa Malori Kwa Serikali
WALAKA KUTOKA KWA MADEREVA WA MAROLI
Sisi madereva wa magari makubwa tunapenda kuchukua nafasi hii kuipa taadhali serikali yetu kwamba, pamoja na mgomo ambao ulitokea siku za karibuni, mji mdogo wa tunduma kwa ushawishi wa madereva wachache kwa kuzusha chama cha madereva wa maroli kisicho na usajili , kuna uwezekano wa luzuka mgomo mwingine kama tahadhari haitachukuliwa.
Kwanza kabisa hicho kinachoitwa chama cha madereva wa maroli hakipo, ni madereva wachache tu ambao wamejaribu kutumia ushawishi wao kuanzisha hii mgomo isiyofuata utaratibu kwa maslahi yao
Kundi hili ndilo liliosababisha madhara makubwa wakati ule wa mgomo. Sisi madereva tunapenda kuwahakikishia waajiri wetu kwamba wengi wetu tulingia katika mkumbo huu kwa kulazimishwa, na kutishwa maana kama tungeonyesha ukaidi kulikuwa na uwezekano wa kudhuliwa na mfano mdogo ni pale serikali ilipoamua kutoa ulinzi kwa wale madereva ambao walikuwa tayare kusitisha mgomo na kuondoka tulipewa vitishompaka vya kuhatarisha maisha yetu. Wao ndio walikuwa wanatoa ushawishi wa kutishia kuchoma matairi barabarani na baya zaidi wakaliteka gari linapakia gesi maalum kutoka Zambia na kumnyanang”mya funguo dereva kisha kuziba barabara kwa kutumia gari hilo na funguo ( switch wakazificha na kutoa tahadhali atakae thubutu kupita watalipua gari hilo.
Tumeamua kutoa maoni yetu kwa nia njema kabisa ya kulinda mahusiano yetu na waajiri wtu. Maana mgomo ule tunaweza kusema kwamba wengi wetu tumepakwa matoe bila ridhaa yetu. Katika kazi hii ya udereva baadhi yetu tumekwenda shule na tuna ufahamu wa kutosha kuhusu masharti ya ajira. Mgomo ule upo katika sura mbili sio moja kama baadhi ya vyombo vya habari vinvyotaka kupotosha.Madai ya madereva kwa waajiri wao ukiangalia kwa undani si mengi, madai kwa waajiri tunaweza kusema moja ni mikataba ya ajira na mishahara. Yanayoihusu serikali ni mengi kidogo nayo ni usumbufu wa trafiki barabarani , kero za mizani na mengine mengi ambayo yamo katika wara uliotumwa kwa waziri mkuu.
Tunapendekeza kwamba jambo hili lisiingizwe kwenye siasa na kuonekana ni la upande mmoja tu wa madereva na wajiri wao hapana. Ni pande zote mbili sura inayojionyesha hapa ni kama vile kutuchonganisha sisi na waajiri wetu kama ni madai yafanywe kwa utaratibu ambao utahusisha pande husika.
Mgomo huu ulishawishiwa kufanywa nchi nzima lakini sababu ulikuwa ni maslahi ya wachache haukufanikiwa kwa sababu wengi wetu tulilazimishwa na kutishiwa maisha yetu. Tukija kwenye suala la ajira , ni wazi kwamba ajira hufanywa kwa mapatano kwa maana ya mshara na posho na marupurupu mengine haingii akilini dereva agome kazi kwa madai ya nyongeza ya mshahara maana kama hajaridhika unakwenda kutafuta ajira mahali pengine si kugoma.Tunaomba serikali itulinde kattika mpango huu haramu ambao lengu ni kuwanufaisha wachache kwa maslahi yao maana kauli yeti ni kwamba sisi hatulazimishwi kufanya kazi na wajiiri wetu bila mapatano.
Isitumike siasa kuonyesha ni jamo la madereva na wajiri . kama kuna madai yafanywe kwa njia ya utaratibu baina ya serikali na vyombo vya dola tusibughuziwe na hawa wachache wanaotaka mgomo kwa manufaa yao binafsi
Aksante.
| Reactions:: |
Wednesday, September 28, 2011
Vyuo Visivyokidhi Vigezo Kufungwa
Na Elisante John, Singida
Septemba 28,2011.
WIZARA ya afya na ustawi wa jamii kwa kushirikiana na baraza la wauguzi,imeahidi kuvifunga vyuo vya afya visivyosajiliwa, ili kulinda ubora wa kiwango cha utoaji wa huduma ya afya nchini.
Hayo yameelezwa leo mjini hapa na waziri wa afya na maendeleo ya jamii Hadji Mponda,katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na muuguzi mkuu wa serikali Clavery Mpandana,kwenye mkutano mkuu wa 39 wa chama cha wauguzi nchini(TANNA).
Mponda alisema kuwa, vyuo hivyo vimekuwa vikitoa wataalamu wasiokidhi vigezo vilivyowekwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii, hali inayorudisha nyuma jitihada za serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini.
Kutokana na hali hiyo, Mponda alisema serikali kwa kushirikiana na chama cha wakunga itavifungia vyuo hivyo, ili kulinda kiwango cha utoaji wa huduma za afya nchini.
Aidha kanali Mponda, pia amewataka wauguzi na waganga wakuu wa wilaya kuhakikisha wanafikisha fedha za vifaa kwenye vituo vya kutolea tiba, zitumike kwa kazi iliyokusudiwa.
Kwa upande wake Rais wa chama hicho kanali Ntuly Mwambingu ameiomba serikali kurejesha mfumo wa elimu wa zamani vyuoni, ili kusomea taaluma ya uuguzi iwe miaka minne, badala ya miwili inayotumika sasa.
Awali, ombi hilo lilitolewa na chama cha TANNA, katika mkutano huo unaohudhuriwa na wauguzi zaidi ya 700 kutoka mikoa yote nchini, na wageni mbalimbali kutoka mataifa ya jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADEC).
Hata hivyo baadhi ya wauguzi wameiomba serikali kuzikabili kikamilifu changamoto mbalimbali zinawazowakabili wauguzi,ili kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya afya.
Walisema ni vyema zaidi serikali ikayatatua matatizo yao kwa uwazi na ukweli, badala ya kuwataka wauguzi watumie akili zao katika kukabiliana nayo, hali inayoweza kuchochea vitendo vya rushwa kwa wanaowahudumia.
MAELEZO YA PICHA YA 1 WAUGUZI WAKIWA PICHA YA PAMOJA:Mgeni rasmi muuguzi mkuu wa serikali Clavery Mpandana (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini kwenye mkutano 39 wa chama cha wauguzi nchini(TANNA) unaofanyika mjini Singida, mwenye kanzu mbele ni askofu wa jimbo katoliki la Singida.
MAELEZO YA PICHA YA PILI:BAADHI YA WASHIRIKI WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI NA PICHA YA NNE NI MGENI RASMI AKIFUNGUA MKUTANO HUO.
MAELEZO YA PICHA YA NNE:MAANDAMANO YA WAUGUZI YAKIANZIA HOSIPTALI YA MKOA SINGIDA KWENDA JUKWAA LA MABULA, TAYARI KWA AJILI YA UFUNGUZI WA MKUTANO HUO WA SIKU TATU UNAOFANYIKA MJINI SINGIDA(Picha na Elisante John).
| Reactions:: |
Helikopta Ya CHADEMA Yatikisa Igunga ( MWANANCHI)
MBILI ZA CCM ZASHINDWA KUTUA ZABAKI KIA, YA CUF KUPASUA ANGA LEO
Waandishi Wetu, Igunga
WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilitikisa anga la Igunga baada ya kuanza kutumia helikopta kufanya kampeni zake, zile mbili za wapinzani wao, CCM zikishindwa kuwasili jimboni humo na kubaki Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na sababu za kiufundi.Wakati Chadema ikipasua anga na mbili za CCM zikibaki KIA, helikopta ya Chama cha Wananchi (CUF) nayo imeshindwa kutua Igunga jana na sasa inatarajiwa hapa leo.
Helikopta ya Chadema ilianza kuonekana katika anga la Igunga saa 10:40 jioni ikiwa na maandishi makubwa ya chama hicho na rangi ya bluu.Ujio wa helikopta hiyo ulivuta kwa muda idadi kubwa ya wananchi waliokuwa kwenye Viwanja vya Sabasaba wakisubiri ujio wa helikopta mbili za CCM, ambazo awali, ilielezwa kuwa zingewasili saa 8:00 mchana.
Baadaye ilielezwa kwamba helikopta hizo za CCM zingetua Igunga saa 11:30 jioni zikiwa na makada wa chama hicho akiwamo Katibu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
Hata hivyo, ilipofika saa 12:00 jioni, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akitumia gari la matangazo la Bendi ya muziki ya ToT Plus alitangaza kwamba helikopta hizo zisingeweza kutua Igunga kutokana na sababu za kiufundi.
Alisema zilichelewa kupata vibali kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kwamba baada ya kutua KIA ilishauriwa kuwa ni vyema zilale hapo.
Alisema kama helikopta hizo zingeondoka KIA jana jioni na kufika hapa usiku wakati tayari kungekuwa na giza kitu ambacho kisingekuwa kizuri kiusalama. Alisema helikopta hizo sasa zitawasili leo saa 4:00 asubuhi.
Matumizi hayo ya helikopta yanawafanya wananchi wa Igunga kushuhudia kampeni nzito na za aina yake tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa vyama hivyo mwaka 1994 na Rostam Aziz kushinda.Jimbo hilo lenye wapiga kura 170,000 katika vijiji 96, halijawahi kushuhudia kampeni nzito kiasi hicho zinazohanikizwa na magari yenye vifaa vya kisasa vya muziki.
Habari kutoka ndani ya CCM, zinaeleza kuwa katika kujihakikishia kura katika kipindi hiki cha lala salama, chama hicho kitawatumia makada wake, Makamba na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wanaoelezwa kuwa na ushawishi mkubwa.
Kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM anatarajiwa kurudi tena hapa keshokutwa.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye aliwasili hapa jana kuongeza nguvu kwa viongozi wa chama hicho ambacho idadi kubwa ya wabunge wake wameweka kambi hapa.
Helikopta ya CUF
Kwa upande wake, CUF kinatarajiwa kuanza kutumia helikopta yake kuanzia leo huku Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Juma Duni Haji akitarajiwa kufunga pazia la kampeni za chama hicho ambazo, awali zilitarajiwa kufungwa na Katibu Mkuu wake ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad.
Akizungumzia na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema kampeni hizo sasa zitafungwa na Haji anayetarajia kuwasili wakati wowote katika kipindi hiki cha mwisho wa kampeni.Mtatiro alisema tayari wabunge wa chama hicho akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar) Ismail Jussa wanaendelea na kampeni jimboni humo.
CCM, Chadema vyatuhumiana
Kiwewe cha uchaguzi huo kimezidi kutesa vyama vya CCM na Chadema, baada ya kuendelea kutuhumiana huku chama tawala kikidai kunasa kile ilichokiita mpango wa siri wa wapinzani wake hao wa kujitangazia ushindi kabla Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kufanya hivyo.
Chadema nacho kimekituhumu CCM kwamba kimeandaa mpango wa kupeleka wapigakura mamluki kutoka katika baadhi ya mikoa ukiwamo Dar es Salaam.
Jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wassira aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba Chadema kimepanga mpango huo wenye lengo la kuwaandaa wanachama wake waone wameibiwa kura pindi CCM kitakapotangazwa mshindi.“Tunazo taarifa za uhakika kuwa wamepanga kutumia magari ya matangazo kutangaza kuwa Chadema imeshinda, hata kabla ya kura kuhesabiwa ili wapate leseni ya kuanzisha vurugu,” alisema Wassira.
Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), alisema tayari CCM wameviarifu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuchukua hatua na pia kuwaelimisha na kuwasihi wananchi kutoingia katika mtego huo.
“Lengo ni kuwaharibu vijana kisaikolojia kwamba yakitangazwa matokeo tofauti waone wamechakachuliwa kura zao na CCM. Tunawasihi Chadema na wanachama wao watulie wakati wananyolewa,” alisema Wassira.
Wassira alisema wanakusudia kutumia mikutano ya hadhara ya kampeni iliyobakia wiki hii ya lala salama, kuwaeleza wananchi juu ya mpango huo wa Chadema ambao alidai hauwatakii mema wananchi wa Igunga.
Hata hivyo, Mratibu wa Kampeni za Chadema Igunga, Mwita Waitara alikanusha vikali madai hayo akisema hawana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa wananchi wameshafanya uamuzi wa kuikataa CCM.“Wassira anafahamu utaratibu wa kutangaza matokeo ulivyo kwamba Chadema hatuna uwezo huo. Hivi kama tulikuwa na uwezo huo kulikuwa na sababu gani ya kufanya kampeni na kuteua hadi mawakala?,” alihoji.
Alikishutumu CCM akidai kuwa kina mpango wa kuingiza watu 1,050 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Singida na Shinyanga ili watumie shahada bandia kukipigia kura chama hicho tawala.Waitara alidai kuwa watu 500 watatoka Dar es Salaam, 300 Singida na 250 Shinyanga lakini akasisitiza kuwa Chadema kina mtandao mpana na kitahakikisha kinazuia mpango huo usifanikiwe.
Chagonja atua Igunga
Kamishina wa Polisi anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja jana aliwasili hapa na kusema polisi watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuanzisha vurugu.“Nasema vurugu sasa basi na ninaonya yeyote atakayejaribu kutuchokoza tutakabiliana naye kwa nguvu zote… wananchi waende kwa uhuru vituoni kupiga kura,” alisema.
Kwa upande wake, Naibu Kamishina wa Polisi anayeratibu usalama Igunga, Isaya Mngulu amesema polisi wamefungua vituo tisa kwa ajili ya kukabiliana na matukio ya vurugu yatakayojitokeza.
Alisema vituo hivyo vina vifaa vyote vya kisasa yakiwamo mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha na kwamba vikosi vimejizatiti kukabiliana na hali yoyote ya vurugu itakayojitokeza.
Alivitaja vituo hivyo kuwa vipo katika maeneo ya Simbo, Mwisi, Nkinga, Sungwisi, Ziba, Mwanshimba na Itumba na kwamba kila kituo kina polisi wa kutosha wenye uzoefu wa kukabiliana na kila aina ya vurugu.
Katika kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa amani na usalama, askari mgambo 325, Magereza wanane na polisi 94 watatumika katika kusimamia zoezi la upigaji kura katika vituo vyote 427.
Maandalizi yakamilika
Msimamizi wa Uchaguzi Igunga, Protas Magayane alisema jana kwamba vifaa vyote kwa ajili ya upigaji kura vipo tayari na vitaanza kusambazwa katika vituo vyote Jumamosi.
Magayane alisema orodha ya wapiga kura itabandikwa vituo kesho Alhamisi na kuwataka wale wote waliojiandikisha waende kuhakikisha majina yao na kufahamu vituo watakavyotumia kupiga kura.
Alisema wasimamizi wa vituo vya uchaguzi wapatao 427 waliapishwa jana na kwamba NEC itafanya kikao na viongozi wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo ili kuwekana sawa.
CUF nayo yapata homa
CUF nacho kimetoa shutuma mbalimbali dhidi ya CCM ikiwamo ya kuingiza makontena ya sukari wilayani Igunga kwa lengo la kugawa kwa wananchi kama njia ya kurubuni wananchi wakipigie kura.
Tuhuma nyingine za CUF kwa CCM ni kuwa kinatarajia kuingiza kundi la makomandoo waliomaliza mafunzo na semina katika Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwatisha wapiga kura siku za mwisho za kampeni na uchaguzi.
Tuhuma hizo zilitolewa jana Mtatiro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema tayari chama hicho kimepata taarifa za kuaminika kuwa kuna makontena yanayotarajia kusafirishwa kutoka Mara kwenda Igunga kwa ajili ya kugawanywa kwa wapiga kura. Bila kutaja kiasi alisema zinatarajiwa kuingia Septemba 29.
“Hii ni rushwa, haiwezekani kipindi hiki cha uchaguzi Serikali ya CCM kuleta kontena za sukari... tunataka Igunga ipate mbunge halali atakayechaguliwa na wananchi na sisi tumejipanga kuzuia jaribio hilo,” alisema Mtatiro.
Pia alidai kwamba chama hicho kimepanga kugawa chakula cha msaada nyumba kwa nyumba siku moja kabla ya kupiga kura na kwamba mpango huo umekamilika na magari yameandaliwa kufanya kazi hiyo Septemba 31 na Oktoba Mosi.
Akijibu tuhuma hizo Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba alikanusha na kusema wapinzani wao hao wana maralia ya uchaguzi.
Nchemba alisema kambi inayodaiwa ilifanyika siku nyingi na shughuli zake ziliisha... “Kambi tulishamaliza na sasa hakuna kinachoendelea, CCM hatuna mpango wa kuingiza vijana katika mji huu kutoka nje kwa ajili ya uchaguzi.”
Kuhusu chakula alisema Serikali imekuwa ikigawa chakula cha msaada katika maeneo mbalimbali yenye njaa na ilianza kufanya kazi hiyo kabla ya uchaguzi.
“Wanasema tunataka kugawa chakula Septemba 31 na Oktoba Mosi hapa Igunga? Siyo kweli kama tunafanya hivyo kwa ajili ya uchaguzi. Serikali inagawa chakula cha msaada katika maeneo yote ya njaa ikiwamo Igunga” alisema Nchemba.Chanzo: Mwananchi.

Kuhusu TBC1: Mwenyekiti Wenu Nakiri Mapungufu
Ndugu zangu,
Juzi hapa nilitoa maoni yangu kuhusu nilichokiona kwenye TBC1 kuhusu coverage ya Igunga. Niliamini kuwa yalikuwa ni mapungufu ya TBC1 kumwonyesha mgombea wa UPDP akimwaga sera zake katika hali niliyoiona mimi kuwa ni ya ulevi.
Nimeyatafakari kwa kina maoni ya wengi wenu na hata kukubaliana nanyi, kuwa mgombea wa UPDP, katika hali yeyote iwayo, alikuwa na haki ya kurushwa hewani, na kuwa TBC1 wametimiza wajibu wao wa kutuhabarisha na kutusaidia katika kazi yetu ya kuchambua. Natumia fursa hii kumwomba radhi mgombea ubunge wa UPDP na TBC1 niliowalaumu kwa kazi yao waliyoifanya.
Na jana usiku TBC1 walifanya coverage bora kuliko zote kuhusiana na Igunga. Ilikuwa well balanced na kuonekana ya kiweledi zaidi. Hivyo ndivyo tunavyotaka iwe, maana TBC1 ni chombo cha umma.
Maana, kilichoonekana juzi kwa mgombea wa UPDP kinaweza pia kutafsiriwa kuwa ni dhihaka kwa demokrasia tunayotaka kuijenga maana hakukuwa na analysis yeyote baada ya mheshimiwa yule kumwaga sera zake ambazo nyingi zilikuwa ni mambo ya kusadikika.
Siku njema kwenu nyote.
Maggid,
Iringa.
Chini hapa ni background ya mjadala huu:
Ndugu zangu,
Kuna miongoni mwetu kila ifikapo saa mbili usiku tunaacha shughuli nyingine na kufungulia TBC1 kuangalia habari. Leo kulikuwa na ' kioja' cha habari kutoka Igunga. Tukaonyeshwa mgombea ubunge wa UPDP.
Ilikuwa ni kama kuangalia Ze Comedy. Na mgombea huyo alipewa muda mwingi hewani. Yumkini alikuwa amepiga kinywaji kwa jinsi alivyokuwa akiropoka. Najiuliza, hivi wahariri hawakuona kioja kile?
TBC1 bado inaheshimika sana. Kurudia mara kwa mara makosa kama tuliyoyaona leo kutaipunguzia TBC1 heshima yake. Ni angalizo tu.
Maggid
Iringa. 12 comments:
- Anonymous at: Mon Sep 26, 11:44:00 PM EAT said...
- Inawezekana TBC1 nao wameona kile ni kioja, ndio maana wakaona wawaonyeshe.Pia inawezekana wamefanya makusudi kuwaonyesha uyo mkombea wa UPDP, ili wenye mawazo mafupi wafikiri kwamba kumbe wagombea wa upinzani ni wahuni, ukichukulia tayari wananchi washalishwa sumu kwamba CHADEMA na CUF ni wafanya fujo. So mwananchi haiyejua chochote lazima aamini kwamba mgombea wa CCM ndio best choice. Naamini kabisa TBC1 hawakuonesha kwa bahati mbaya ni uendelezaji wa kampeni za CCM.Tafakari.
- Anonymous at: Tue Sep 27, 12:08:00 AM EAT said...
- Kaka Mjengwa, wanaoleta habari wanatakiwa watuletee hivyo hivyo ilivyo,sasa kama jamaa alikuwa amelewa wao wanatakiwa wamtoe hivyohivyo alivyo na wapiga kura wajue wamchague nani.
- { Jiniaaz! Popkorn } at: Tue Sep 27, 12:26:00 AM EAT said...
- wee magidi, wenzio ndo wanafurahia, ili wananchi waone kuwa upinzani ni pumba. ikitokea mpinzani kamimina nondo za uhakika na zenye uhai katika kampeni hawezi kuwekwa kwa jinsi hiyo kwa hiyo tivii stesheni ya ccm. lazima wataediti kiaina hivi hiyo ndo tanzania yetu ya leo chini ya ccm
- Anonymous at: Tue Sep 27, 12:31:00 AM EAT said...
- Wewe Majjid acha ukoloni mambo leo. Unapomwita mgombe Ubunge "mlevi" humtendei haki. Hata kama hakukufurahisha wewe kama Mjengwa ana haki ya kuonyeshwa kwenye chombo cha habari kama mtanzania. Ni mlipa kodi na katika uhuru wa vyombo vya habari anaruhusiwa. Sidhani kama alimtukana mtu!! Kama hakumtukana mtu basi hajavunja sheria na anayohaki ya kuonyeshwa kwenye chombo cha habari. Nadhani ifikie mahali tusibadilishe mitazamo yetu binafsi kuwa ndiyo mtazamo wa umma. Huo unaitwa ukoloni mambo leo. Hata kama utaibania comment yangu lakini messege sent! Mdau wa Netherlands
- Anonymous at: Tue Sep 27, 12:33:00 AM EAT said...
- Kwa hiyo ulitaka kila siku waonyeshe CCM, CHADEMA na CUFU ndiyo watu mrizike kuwa wamefanya coverage? Wala huna haki ya kulaumu chombo cha habari. Ni haki yake ya msingi kufanya corage habari aina yoyote ili mradi jamii inatakiwa ifahamu. Kama wasingemrusha huyo jamaa tungejuaje kuwa kuna mtu kama yule Tanzania? Ulitaka chombo gani sasa kituonyeshe hiyo taarifa?
- Anonymous at: Tue Sep 27, 07:02:00 AM EAT said...
- Sasa wewe kaka Mjengwa unataka waonyeshe kila kitu unachopenda wewe.....TBC wanayo haki ya kurusha habari yeyote wanayoipenda.
- Anonymous at: Tue Sep 27, 08:54:00 AM EAT said...
- Mjengwa Asante sana kwa hilo, kinachoniuzi mimi ni kuwanyima airtime vyama venye nguvu na kuonyesha CCM tu kila wakati na muda mwingine kuonyesha upinzani hasa panapokuwa na tatizo kama mahakamani etc, sijawahi kuona mkutano wa kampeni wa CDM wala CUF kwenye TBC1 kwa kweli nashindwa kuelewa siasa za TZ na vyombo vya habari vya serikali, sijui tutafika lini huko tuendako.
- Anonymous at: Tue Sep 27, 09:24:00 AM EAT said...
- Mwenyekiti Maggid, Mimi naona TBC 1 walikuwa sahihi kumuonyesha mgombea wa UPDP...wewe umewalaumu kwa kuwa unafikiri yule kijana alikuwa amelewa,labda unachukia pombe kwa kuwa hunywi. Lakini mimi nilivutiwa kwanza na tangazo kwamba mgombea wa UPDP anaanza kampeni zikiwa zimebaki siku tano uchaguzi kufanyika.Kwa hiyo nilikaa kitako nione sera,nione mkakati wao wa kuwapata wapiga kura katika dakika za lala salama. Nikaja kuambulia kituko..kwanza alianza kwa kusema hakuna kurudi nyuma..samaki huwa hana reverse..yeye anasonga mbele. TBC 1 walifanya vizuri kuonyesha hicho kipande kwa muda unaoridhisha kwa sababu ukiacha upande wa umakini alionao binadamu pia kuna upande wa kutokuwa makini,ni vizuri kuitazama shilingi pande zote mbili. Pia hii ni nchi ya demokrasia ingawa bado tunakua lkn naamini kila mtu anatakiwa kuheshimiwa na kusikilizwa. Kilichonifurahisha zaidi ni kwamba pamoja na changamoto za ugumu wa maisha tulizonazo watanzania bado hatujasahau kuwa umakini unahitajika katika kuikomboa nchi yetu...na hili lilidhihirishwa na kijana aliyemuuliza mgombea ubunge kirefu cha UPDP maana alimbaini sio mtu makini. Aluta continua
- Anonymous at: Tue Sep 27, 11:01:00 AM EAT said...
- Na utashangaa mwisho wa siku anapata kura, maana anao wapenzi wake wanaomsapoti kupitia chama chake. Na pia hana tofauti na wagombea wa vyama vingine ambao walichokifanya mpaka sasa ni kuonyeshana ubabe na fujo tu kwani nao hawana sera vile vile. So give a guy a break, labda wasi wasi ni kuwa atapunguza kura za jamaa?
- Anonymous at: Tue Sep 27, 12:46:00 PM EAT said...
- jamani mwenyekiti sasa unatushangaza sie ambao hatuko mrengo wowote,kwani tunatakiwa kuona yote yanayojiri huko igunga,kama tume ya uchaguzi inamtambua yule mgombea kwa nini tbc1 wasionyeshe kampeni zake?? wee baki na mrengo wako! napita tu hapa mwenyekiti.
- Anonymous at: Tue Sep 27, 01:00:00 PM EAT said...
- Mimi kura yangu nampatia mgombea wa UPDP. Mwenyekiti unapomwita mgombea wangu mlevi inabidi uniombe radhi!! Huwezi kulazimisha itikadi zako za CHADEMA wote tuwe CHADEMA. Haiwezekani bwana, kila mmoja ana uhuru wa kuchagua chama anachokitaka ili mradi havunji sheria. UPDP imesajiliwa kihalali na tume ya uchaguzi ya taifa inakitambua kama chama halali. Sasa mgombea wake unapomwita mlevi ni kosa la kupelekwa mahakamani!! Angalia sana Majjid! You are doing wrong to force your ideology to be the community ideology! That is absolutely wrong!! Everybody has a freedom of choice and the media is not restricted to the so called CHADEMA, CCM, CUF, etc. Remember that TBC1 is not a private organization but rather a public good. So every member of the society has the right to have his story broad-casted by TBC1. So what is wrong? Had it been is Mjengwa blog, then you would have said that "huyu mlevi, hivyo sina interest naye" Lakini hiki ni chombo cha umma wa watanzania. Acha hizo Mwenyekiti!!
- Anonymous at: Tue Sep 27, 04:00:00 PM EAT said...
- Mjengwa hayo maoni waliotoa wenzangu ndo inajibu swali la taaluma ya habari ni nini? Nakubalia kabisa na TBC1 kuwa walichofanya ni sahihi. Hakukuwa na haja ya kuchakachua. Kama mgombea ni mlevi atabaki kuwa mlevi tu
| Reactions:: |
Subscribe to:
Posts (Atom)