Subscribe:

Monday, October 31, 2011

Mjomba Mrisho Mpoto Kupamba Uzinduzi Wa Gazeti La Kwanza Jamii Iringa

Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr . Christine Ishengoma. Pichani ni Mrisho Mpoto akiwa na Simon Mkina, Mhariri Mtendaji wa Kwanza Jamii leo jioni. Gazeti la Kwanza Jamii linatoka pia katika Mkoa wa Njombe.
Reactions::

Mafuriko Ya Unguja

Reactions::

F,Maro, Atetea Ushoga

Baadhi ya mashoga,Dar es salaam


Kumekuwa na Mijadala kuhusu ushoga kwa kipindi kirefu ndani ya Jamiiyetu na katika siku za karibuni mijadala hiyo imeamia kwenye mitandaojamii kama huu na muelekeo wa wachangiaji wengi ni kwa wenyewekutokutambua ushoga kama upo na nisehemu ya tamaduni zetu kwa miaka mingi .
Mimi pia niliwahi kuwa hivi kipindi cha nyuma sikukubaliana na hali
hii lakini hali hii kwa mara ya kwanza nilikutana nayo shule ya msingi
nikiwa Dar na Nairobi Kenya , nikakumbana nayo mpaka vyuoni na sehemu
za kazi na zaidi nilikuja kukumbana nayo kwenye mitandao kama hii .
Kwenye mitandao kama hii haswa wanapatikana kwenye Facebook kwa wingi
tu , kwenye chatroom mbalimbali haswa wale watu wanaotafuta marafiki
ambapo utamjua kama ni shoga baadaye sana .
Mashoga ni sehemu ya jamii yetu tumekuwa nayo kwa kipindi kirefu na
wengi wamekuwa wakijificha lakini wamekuja wazi kutokana na hii
mitandao jamii pamoja na NGOS za kuwatetea na mabaraza mengine ya
maongezi .

Mtu kuwa shoga sio kwamba ametaka mwenyewe hapana , wengine wamezaliwa
hivyo , wengine wameingia kwenye mkumbo huo mashuleni na vyuoni haswa
yale mashule ya bweni wengine wamefundishwa kwenye nyumba za ibada ,
wengine na ndugu zao majumbani na makazini .

Kwangu mimi naona hili sio tatizo , ni tatizo endapo tutashindwa
kuwatambua watu hawa na kuwafanya sehemu ya jamii yetu kwamba
wanastahili haki zote kama binadamu wengine na pengine zaidi kutokana
na hali zao za kihisia na jinsi wanavyobaguliwa .

Sina nia ya kutangaza vita dhidi ya wale wanaopinga ushoga na usagaji hapana , hapa ni kufungua uwanja wa majadiliano na kuthamini uwepo wa
mashoga na wasagaji katika jamii zetu katika ujenzi wa uchumi wetu na
jamii yetu lazima tukubaliane nalo .
Kwa sasa ni kuanza kubuni njia za kusaidia kundi hili la kijamii yaani
mashoga na wasagaji ambapo kwa muda mrefu wamekuwa wahanga wa
unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi wa aina mbalimbali na kwa njia hiyo
wamekuwa wakiathirika sana na magonjwa ya zinaa na kuendelea kujificha
bila kupata msaada wowote .
Ndugu zangu na wanajukwaa wenzangu , kesho ni siku ya ukimwi duniani ,
tuangalie kundi hili la jamii , tuone jinsi gani tunavyoweza
kulisaidia kwa hali na mali , tukubali ushoga tukubali mabadiliko nasi
tubadilike
Na F.Maro

Ndugu, salaam. wakati wengi wenu mkilalamikia alichofanya Cameroon,kuhusu kutaka nchi zetu ziruhusu ushoga, ndugu Maro ambaye nadhani ni mmatumbi mwenzetu, anaandika kutetea ushoga. tunaruhusu makusudi maoni yake ili yasaidie kuimarisha mjadala kuhusu jambo hili katika jamii yetu.

Msaidizi wa Mwenyekiti, Mjengwablog
Reactions::

Waraka Wa Godbless Lema Kabla Ya Kwenda Jela




JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.



Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu.
Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.
Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi.
Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi.
Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!
Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.
NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.
Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.

Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.

Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.
Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.
Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.
Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU.

Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011.
Reactions::

Misaada Hii Jamani! Tuweni Makini


David Cameron has threatened to withhold UK aid from governments that do not reform legislation banning homosexuality.
The UK prime minister said he raised the issue with some of the states involved at the Commonwealth Heads of Government Meeting in Perth, Australia.
Human rights reform in the Commonwealth was one issue that leaders failed to reach agreement on at the summit.
Mr Cameron says those receiving UK aid should "adhere to proper human rights".
Ending the bans on homosexuality was one of the recommendations of an internal report into the future relevance of the Commonwealth.
Mr Cameron's threat applies only to one type of bilateral aid known as general budget support, and would not reduce the overall amount of aid to any one country.
Malawi has already had some of its budget support suspended over concerns about its attitude to gay rights. Concerns have also been raised with the governments of Uganda and Ghana.

British empire
Mr Cameron told BBC One's Andrew Marr Show that "British aid should have more strings attached".
But he conceded that countries could not change immediately, and cautioned that there would be a "journey".
"This is an issue where we are pushing for movement, we are prepared to put some money behind what we believe. But I'm afraid that you can't expect countries to change overnight.
"Britain is one of the premier aid givers in the world. We want to see countries that receive our aid adhering to proper human rights.: http://www.bbc.co.uk/news/uk-15511081
Reactions::

Blandina Nyoni Afunga Kongamano La Wanahabari La Bima Ya Afya Morogoro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni (kushoto) akihutubia alipokuwa akifunga kongamano la wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu taarifa za tafiti za upatikanaji wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika mjini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni (kushoto) akizungumza na wanahabari baada ya kufunga kongamano la wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu taarifa za tafiti zaupatikanaji wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika mjini Morogoro
Baadhi ya washiriki wakiwa katika kongamano hilo mjini Moro.
Na Richard Mwaikenda
Reactions::

Madiwani Wa CCM Wamlalamik​ia Meya Wao.....

Diwani wa kata Mungumaji Hassan Mkata akiongea kwenye baraza la madiwani, Manispaa ya Singida, kuhusiana na maamuzi mbalimbali yanayoafikiwa na baraza hilo, lakini hayatekelezwi.
Diwani wa kata ya Utemini Bartazar Kimario akiongea kwa hisia kali katika baraza hilo, kulalamikia maamuzi mbalimbali yanayotolewa na baraza hilo, lakini hayatekelewi hali aliyotishia kutoka kwenye kikao hicho.hata hivyo alibaki baada ya mawazo yake kukubaika
Madiwani wakifuatilia hoja kupitia katika makablasha yao
.:Meya wa manispaa Singida Shekhe Salum Mahami akifungua baraza hilo, kulia ni mkurugenzi wa mniapsaa Yona Maki


MADIWANI wa manispaa ya Singida wamemlalamikia Meya shekhe Salumu Mahami, wakidai hayatendea haki maamuzi ya baraza hilo na hiyo inaweza klutoa nafasi kwa wapinzani, siku za usoni.

Baadhi ya madiwani waliotoa shutuma hizo ni Hassan Mkata (Mungumaji), Shaaban Sattu(Unyambwa), Baltazar Kimario(Utemini) na Moses Ikaku(Unyamikumbi).
“Meya lazima sasa tusome nyakati, umekuwa kama kinyonga, unabadilika badilika rangi kutokana na eneo unalokuwa….mnaifichaficha nini, mkurugenzi naye tunaweza kumtoa nje ili tumjadili, tukiona amekosea tutaamua hapa hapa,”alisisitiza Mkata.
Baraza la madiwani, manispaa ya Singida lina jumla wajumbe 21, wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee, wakiwemo wawakilishi kata 14, viti maalumu watano na wabunge wawili.
                                                                             Na Elisante John
Reactions::

In The Everlasting Loving Memory Of

Mwl. Zephaniah E. R. N. Memba: Our beloved father

It seems like yesterday but it’s already six years since you departed from us to join our father in Heaven.  You are still vivid and real in our hearts and minds.  Although physically you are not with us, spiritually you are in our hearts daily.  Indeed you were a special gift to us from GOD. We thank the Almighty GOD for the time you spent with us. We miss you great but we always take courage and hope in the verse you left with us from Romans 8: 31 “If GOD Be For US, Who Can Be against Us?”

You are deeply missed and remembered by your wife, Mama Ukende P Memba, Your children, Joyce, Albert, Rhoda, Imani, Flora and Peter, in-laws, Maria Makalla Memba, William Stephen Kotta, Johnson Nyingi, and grandchildren, Joshua, Milan David, Nkambujah Romeo, Rodney Ngadumka, Ukende Ronia, Rowan Tyalambula, Ukende Rondelle, Rochelle and Ukende Ashley.
Reactions::

Wakazi Wa Misugusugu Kibaha Mkoani Pwani Wakikata Chuma Chakavu Katika Mabaki Ya Basi La Deluxe

 Wakazi wa Misugusugu Kibaha mkoani Pwani katika Barabara ya Morogoro wakikata chuma chakavu katika mabaki ya basi la Deluxe ambalo lilipinduka na kuwaka moto na kupoteza maisha ya watu.
Picha na Yusuf Badi
Reactions::

Kampuni Ya Panasonic Yafanya Mambo Tabora

Wataalamu wa Kampuni ya Panasonic wakiwa katika Uwanja wa ndege wa Tabora  wakirejea kutoka katika Kijiji cha Mbola, wilaya ya Uyui, mkoani Tabora walikokwenda kukabidhi kontena la kisasa lenye vifaa vya umeme wa jua kwa ajili ya wanakijiji  wa kijiji hicho, umeme ambao utasaidia wananchi kuona matukio mbalimbali kupitia televisheni na kuhifadhi dawa za hospitali. Mkuu wa Mkoa, Fatuma Mwassa ndiye aliyepokea kontena hilo. Jumla y ash. Milioni 350 zimetumika katika mradi huo. Mbola imeteuliwa kama kijiji cha mfano cha millennia.
Picha na Mohamed Mambo.
Reactions::

Wema Wamponza

Fundi radio katika eneo la Tulivu Klabu katika Manispaa ya Iringa akiwa anavuja damu baada ya kuambulia kipigo wakati akiamua ugomvi uliozuka kazini kwake
Fundi radio huyo akielezea tukio lilivyotokea kwa baadhi ya wananchi jana
                         Na francisgodwineblog 
Reactions::

Matukio Safari Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel Kuelekia Fainali Za Mrembo Wa Dunia

Miss Vodacom Tanzia 2011 Salha Israel  aliye vaa Nguo za Njano katika Mazoezi  ya nguvu kabisa wakati wa maandalizi ya shindano la Miss World Tanzania
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa pili kutoka kulia akiwa Edinburgh Castle hivi karibuni katika safari ya kuelekea katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia  
     Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Pili kutoka kulia akiwa anapiga Chiazi  na wenzake .. katika safari  ya kuelekea kumtafuta Mrembo wa Dunia. 
                                                       Na Fredy Njenje
Reactions::

Francis Miyayusho Amtwanga Mbwana Matumla Na Kunyakua Ubingwa Wa UBO

Bingwa mpya wa UB0 uzito wa bantum Francis Miyeyusho akifurahia ushindi, alipokuwa akivalishwa mkanda wa ubingwa na mlezi wa mchezo wa ngumi nchini kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova. Mpambanohuo ulifanyika hapo jana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Miyeyusho aliibuka Mshindi baada ya kumpiga bingwa wa zamani wa UBO Mbwana Matumla.
Picha kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com
Reactions::

Mkurugenzi Mwendeshaji Wa Benki Ya Uwekezaji Tanzania Atembelea Mabanda ya Wizara Ya Fedha

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Uwekezaji Tanzania(Tanzania  Investment Benk-TIB) Peter Noni (kushoto) akipata maelezo  kutoka Afisa  Msaidizi Huduma na Elimu kwa walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) Simon Massawe juu ya utaratibu wa misamaha ya ushuru wa magari na  pikipiki (jana) jijini Dar esalaam wakati alipotemblea maonyesho ya  Wizara ya Fedha ya miaka 50 ya uhuru katika viwanja vya Mnazi mmoja. 
    Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO-Dar es salaam
Reactions::

Waziri Mkuu Achangisha Sh. Milioni 111.6 Katika Sadaka Ya Mavuno Oysterbay

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyesha simu  ya Bw. Leonard Kapinga (kulia) ambayea liitoa ili inadiwe katika  harambee ya siku ya mavunokwenye kanisa la Mtakatifu Petro Mjini Dar es  salaam Oktoba 30, 2011.Simu hiyo iligombolewa na waliohudhuria kwenye  harambee hiyo na kurudishwa kwa mwenyewe gharama ya sh. 522,000/.  Kushoto ni Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Petro,Padri  Joseph Mosha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


SIMU ya Nokia aina ya NOKIA 2600 ya Bw. Leonard Kapinga (37) mkazi wa Msasani jana mchana (Jumapili, Oktoba 30, 2011) ambayo kwa kawaida huuzwa kwa sh. 60,000/-hadi 65,000/- ilikuwa kivutio cha pekee katika michango ya mavuno kwa jimbo katika parokia ya Mt. Petro jijini Dar es Salaam ambapo ilichangiwa sh. 522,000/- ili ikombolewe kwa sababu mwenye nayo hakuwa na fedha za kuchagia harambee hiyo.
     Bw. Kapinga ambaye hajui thamani ya simu yake kwa sababu alipewa zawadi na mama mmoja ambaye ni muumini mwenzake, alifikia hatua hiyo baada ya kuguswa na mahubiri kuhusu kumtolea Mungu sadaka ambayo inaumiza moyo wa muumini. Aliamua kutoa laini ya simu (simcard) na kumkabidhi Waziri Mkuu kama mchango wake lakini Waziri Mkuu akaamua kuwaomba watu wamchangie ili Kapinga arudishiwe simu yake.
     Ibada ya mavuno kwa Kanisa la Mt. Petro lililoko Oysterbay jijini Dar es Salaam, ilifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mbuyuni na kufuatiwa na harambee hiyo ambayo ilichangisha jumla ya sh. milioni 111. 65 zikiwa ni fedha taslimu na ahadi. Lengo lilikuwa ni kufikisha sh. milioni 100/-.
     Akiwashukuru wote waliojitolea, Waziri mkuu alisema ameguswa na moyo wa kijana Leonard kwa sababu ametoa kama ambavo mafundisho ya leo yalihimiza. Vilevile alisema ameguswa na wazee wastaafu ambao wamejitokeza kwa wingi na kuchangia kila mmoja kwa kiasi chake. Wengi waliofika ni Majaji wastaafu, maafisa wa Serikali wastaafu na watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).  
  “Wote mliotoa michango Mungu awabariki, kijana mwenye simu iliyokusanya sh. 522,000/- ametusaidia sana, sababu mchango tumepata na simu yake amebaki nayo… wazee wangu wastaafu mmenitia moyo kwamba kustaafu siyo kwisha… mmejitoa mno na Mungu awabariki,” alisema.
     Alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi waendelee kusisitiza umuhimu wa maadili ya kiroho na kimwili. “Hivi ni kwa nini mtu umuue mlemavu wa ngozi kwa kisingizio kuwa kiungo cha mwili wake kitakuongezea utajiri? Yule ni mwanadamu kama wewe, ana haki ya kuishi kama ilivyo kwa sisi wengine,” alisisitiza.
     Alionya kuhusu mauaji hayo ambayo yameibuka upya na katika mwezi huu tayari watoto wawili wamekatwa viungo vyao. Alisema mwaka 2008, watu 42 wenye ulemavu wa ngozi waliuawa kutokana na imani hizo potofu.
     Waziri Mkuu pia alionya Watanzania kuenzi amani iliyopo nchini kwani yanayoendelea katika nchi za jirani yanatisha na si ya kuomba yatokee kwa Watanzania. “Tuangalie yanayotokea Libya, si mambo mazuri hata kidogo. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kuwa kifo cha Gaddafi si sahihi hata kidogo, ni bora angekamatwa akashtakiwa kuliko watu kujiamulia kutoa roho ya mtu mwingine hivihivi. Watanzania tuombeane tusifike huko,” alisisitiza.
     Mapema, akitoa mahubiri katika ibada hiyo, Padre Paul Haule aliwaonya waumini kuacha tabia ya kumpa Mungu mabaki au sadaka zenye ulemavu na kuwataka watoe kwa moyo wote ili Mungu azidi kuwabariki.     Akifafanua somo kutoka Kitabu cha Malaki sura ya tatu, Padre Haule alisema Mungu hapendi masazo, anataka kupewa kilicho bora na ndiyo maana aliwauliza wana wa Israeli: “Mnaninyima hata kilicho changu?”
     Alisema ukombozi wa wanadamu uliofanywa na Bwana Yesu pale msalabani haukuwa wa lelemama bali ilikuwa ni sadaka ngumu iliyokuwa na uchungu. “Sadaka lazima ikuume mwamini na hata Bwana Yesu alilia pale msalabani sababu ya maumivu”.
     Akifafanua kuhusu matumizi ya sadaka ya Injili, Padre Haule alisema inatumiwa kusomesha wanafunzi 43 wanaosoma katika Seminari Kuu za hapa nchini na pia kueneza Injili vijijini.
     Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mavuno, Dk. Adelhem Meru alisema Parokia hiyo imekwishakusanya sh. milioni 37.4/- kutoka kwa waamini na katika kanda tisa za Parokia hiyo.
Reactions::

Blogu Ya 8020 Fashion Yatimiza Miaka 5 Ya Utendaji Wake

Shamimu Mwasha mmiliki wa 8020 Fashion akimlisha keki mgeni rami Mh  Angela Kairuki wakati wa hafla ya blogu hiyo kutimiza miaka 5 ya utendaji wake wa kazi.
Mmiliki wa Blogu ya mavazi ya 8020 Fashions Shamimu Mwasha kushoto  aka Shamimu Zeze pamoja na mgeni rasmi Mbunge wa CCM viti maalum Dar es salaam Agela Kairuki wakizundua nembo ya mavazi ya B2A itakayomilikiwa na Shamimu, wakati wa hafla ya kutimiza miaka 5 ya mtandao wa 8020 Fashions iliyofanyika kwenye ukumbi wa Daimond Jubilee jijini Dar es salaam leo mchana.
Tukio hilo limedhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa kusaidia wanawake  MMWEI na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers kupitia kinywaji chake kikali cha Baileys
hamimu Mwasha mmiliki wa 8020 Fashion na mgeni rasmi Mh Angela Kairuki wakiangalia mavazi ya nguo zilizobuniwa kwa kutumia nembo ya mavazi ya B2A kama wanavyoonekana
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakijimwaga stejini kucheza muziki kama wanavyoonekana katika picha.
Joseline Kamuhanda kushoto na Grace Lyon  kutoka Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania , Mwamvita Makamba kulia akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa MMWEI Vodacom Tanzania Mwamvua Mlangwa katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi Mh.  Angela Kairuki  akitoa hotuba yake katika hafla ya miaka 5 ya blogu ya 8020 Fashion iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Shamimu Mwasha mmiliki wa 8020 Fashion akizungumza katika hafla hiyo wakati alipokuwa akikaribisha wageni mbalimbali.
Picha na fullshangwe.blogspot.com
Reactions::

Hoja Yangu; Lay Man Ni Nani?

Madaktari wakifanya upasuaji mkubwa. Huwaita wote wasio na taaluma ya udaktari LAY MEN
Wanasheria wakiwa mahakamani. nao huwaita wote wasio wanasheria, LAY MEN
Mapadre na watu wa wakfu.huitwa wenye daraja, na wote wasio na daraja takatifu huitwa LAY MEN.


Wadau nimeshangazwa na madai a makundi haya kwenye jamii.ukitoa maoni kwenye masuala ya kisheria wakati wewe siyo mwansheria, unaitwa Lay man na wenye fani yao.madaktari nao huwaita wasio madktari kuwa ni lay men, kadhalika na mapadre na watu wenye wakfu huwaita waamini wasio na wakfu lay men.sasa mimi najiuliza, LAY MAN ni nani? na kwa nini hizi profession tatu pekee ndizo zinaita wengine lay men. karibu tujadili
Na Mdau wa Mjengwablog
Reactions::

Kambi Hii!


Jana Jumapili, tulipiga kambi kwa kutwa nzima pale River Valley kijijini Lundamatwe. Ni kando kando ya mto Ruaha umbali wa kilomita 18 kutoka Iringa Mjini.  Pichani ni rafiki yangu Dr Bukaza Chachage. Tulikuwa na familia zetu na za rafiki wengine. Huko Lundamatwe kutwa nzima sikuwa hewani, hivyo basi, mbali kabisa na simu na laptop. Nimerudi nyumbani usiku na kufurahia kazi nzuri inayofanywa na msaidizi wa mwenyekiti wenu hapa kijijini.
Reactions::

Sunday, October 30, 2011

Profesa Mwandosya Mambo Yake Safi!

Nipashe, Jumapili.
Reactions::

Na Babu Naye Ni Janga!

Gazeti Mtanzania, leo Jumapili.
Reactions::

Kipanya Huyu!

Reactions::

Duniani Kuna Mambo!

Reactions::

Lema (MB) CHADEMA, Aongea Na Vyombo Vya Habari

Godbless Lema

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Nawasalimu nyote.
Nimewaita kutoa taarifa juu ya kilichotokea juzi tarehe 28/10 /2011 baada ya kuhairishwa shauri la kesi ya uchaguzi iliyoko mahakamani dhidi yangu .
Tarehe 27/10/2011 kesi hii ilihahirishwa na Judge A . Mujuluzi kwani usikilizaji wake usingewezekana kwa kuangalia idadi ya watu walivyokuwa wamejaa pale mahakamani ,maagizo yalitoka kwamba shauri litakalofuata mahakama iwe imetayarisha vipaza sauti kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.
Lakini kwa bahati mbaya jambo hilo halikuwezekana kabisa kwa sababu ambazo baadaye Mh. Judge alizitolea ufafanuzi mzuri na mawakil wa pande zote wakakubaliana kuendelea na shauri hilo bila vipaza sauti lakini kwa ahadi kuwa mpango huo unatekelezwa haraka na wakati mwingine wa kesi itakapokuja mahakami utaratibu huo utakuwa umekamilika.
Jambo la kushangaza siku hiyo wakati nafika mahakamani nilikuta polisi wengi sana na wamevaa nguo zinazoashiria tayari wako kwa mapambano na watu wakizuiwa kabisa kuingia mahakamani kuanzia geti kubwa na polisi walikuwa wanajaribu kuhoji kila mtu kuwa anakwenda kusikiliza shauri gani na kama mtu angejibu ni shauri la kesi ya uchaguzi basi halikuwa haruhusiwi kuingia mahakamani kuanzia geti la mwanzo wa mahakama.
Nilikata dhambi hii na uonevu huu kwa wapiga kura wangu nilimfuata OCD Bwana Zuberi Mwombeji kuongea naye juu ya jambo hili la kuzuia watu* na alikataa kabisa na kusema* “ hao watu wanaenda wapi kwani kesi inawahusu ? na yeyote atakaye vuka* hawa polisi hapa hatakuwa chambo na kuniambia kuwa hata watu wakija maelfu na maelfu mahakamani* lazima kesi hii initie kidole “ ( Zuberi) , tulibishana huku* nikijaribu kutetea utu wangu na mamlaka yangu kama Mbunge* , ikawa zogo mahakamani muda *mrefu bila mafanikio *mpaka nilipomuomba wakili wangu aingilie kati kisheria ndipo watu waliporuhusiwa kwenda kusikiliza kesi .
Baadaye baada ya kesi* nilikuta wananchi waliokuwa nje ya chumba cha mahakama *wakiwa na hasira huku wakilalamika na kwani kwa mara nyingine tena OCD Zuberi alikuwa amewaita tena wananchi PANYA na akiamuru polisi wa ngazi ya chini* kwa kusema “sogezeni hao *PANYA nyuma”
Lugha hii ni mbaya* haikubaliki hata kidogo, niliongea na wanachi na na kukemea lugha hii kwa hasira *baadaye nilielekea ofisini kwangu kwa miguu huku nikisindikizwa na polisi na watu wengi waliokuwa mahakamani *na baadhi *ya watu niliomba tukutane nao ofisini kwangu wengi wakiwa ni viongozi wa matawi na vijana naotarajia kuwa mashaidi katika kesi ya uchaguzi *, niliongea nao ofisini kwangu nikawaaga* nikaondoka* na wachache niliwaacha ofisini kwangu na Katibu wangu na baadhi ya wageni wengine, baada ya muda nilipigiwa simu kuwa polisi wameingia ofisini kwangu na kukamata watu wote , nilimpigia simu Kaimu RPC kumueleza suala hili na* yeye alisema ni bora nifike ofisini kwake tuongee jambo hili , nilipofika nilimueleza jinsi OCD anavyoendelea kufanya kazi kibabe, kwa shuruti za siasa na bila busara na kuhumiza watu bila sababu , alinisikiliza kwa muda usiopungua saa nzima na baadae nikifikiri nimeeleweka* ghafla niliwekwa chini ya ulizi na kuambiwa nitoe maelezo na kushitakiwa kwa kosa la kuongea watu nje kabisa ya viwanja* vya Mahakamani na ofisini kwangu .
Ninafahamu mipango yote ya siri na wazi iliyokusudiwa kwangu na wafuasi wangu , ndio maana sishangai kwamba vyama vingine vinaweza kufanya mikutano na maandamano bila kibali na kuchungwa na polisi na yeye OCD* na polisi walipohojiwa na waandishi wa habari juu ya jambo hilo UVCCM kufanya mkutano na maandamano bila kibali,, Polisi walisema wanataarifa na wametoa onyo kwa viongozi waliohusika.
Lakini mimi *Mbunge nimekatazwa hata kutembea kwa miguu kutoka mahakamani na ni *lazima nipande gari hata kama nataka kutembea kwa miguu na hata kuongea na Wananchi mahakamani na ofisi kwangu ni kufanya mkutano bila kibali ? Jambo hili limenisikitisha sana lakini moyo wangu huko imara kwani naamini kila matatizo yanayotokana na kupigani haki au usawa* matatizo hayo mara nyingi huwa ni mpango wa Mungu juu ya kusudi Fulani.
Kesi *ya uchaguzi bado inaendelea, nilichaguliwa kwa kupata kura zaidi ya elfu 56. Wakija takribani asilimia kumi tu ya walionichagua ni watu zaidi ya 5,600. Watu hawa wakija kusikiliza kesi na baada ya kesi* wakaamua kuondoka kwa kuelekea mjini na sehemu mbali mbali* , je kundi hili la watu wataondokaje mahakamani ili msongamano huu usiitwe maandamano ? Hatuhitaji nguvu kubwa ya jeshi la polisi kutawanya watu wanaotoka mahakamani tunahitaji ulinzi wao na busara zao ili watu wasambae kwa amani *“ kwani kusudi la mkusanyiko huu hautokani na nia mbaya bali ni kesi ya uchaguzi ambayo hauwezi kushanga kwanini kuna watu wengi mahakamani.
Matukio mengi ya uhalifu Tanzania huwa yatokei kukiwepo na msongamano *wa watu tu bali yanatokea tu pale penye dhamira ya uovu bila hata msongamano , mara nyingi tunasikia taarifa za mabenki kuibiwa , watu kuvamiwa katika nyumba zao usiku na kuchomwa visu na kuporwa mali zao mambo haya huwa yanafanyika tena msongamano wa watu ukiwa usingizini, sio kweli kuwa kila msongamano wa watu ni maandamano au ishara ya vita na uovu ndio maana sokoni na sehemu za ibada huwa hakuna polisi wanaolinda kuepusha msongamano kwani kusudi la msongamano huo unajulikana maudhui yake. Haitoshi kutembea kwa miguu idadi kubwa ya watu kuita maandamano. *Maandamo yanatafsiri pana sana.
Hakuna shaka ni siasa ambayo iko wazi juu ya kilichotokea* tahere 28/10/2011* kwani sio mara ya kwanza kutoka mahakamani kwa miguu na kuja ofisi kwangu *kwani tarehe 21/10/2011 tulitoka mahakamani kuelekea Ngarenaro kwa miguu tena kupitia* njia ya polisi , mbona siku hiyo kutembea huko hakuitwa maandamano ? ama kwa vile OCD hakuwepo ? *.
Ninatoa wito kwa serikali na viongozi wa jeshi la polisi sio afya hata kidogo mwakilishi wa wananchi *kama mimi kuwa na uhusiano mbaya na Jeshi la polisi *kwa sababu ya mtu mmoja.
Ndugu wananchi na wanahabari Wakati Fulani huko Nyuma *OCD *alituma kwa katibu wetu wa Mkoa Meseji kuwa mimi Mbunge nimeandaa mpango wa kumteka mtoto wa OCD *na kumuua , Mimi pamoja na Mkiti wetu wa Taifa Mh Mbowe *tulienda kumuona RPC* na viongozi wengine kujadili na RPC alihaidi na kuona umuhimu wa kukaa pamoja na kujaribu kutafuta uhusiano mwema na suluhu jambo ambalo halikuwezekana mpaka leo kwa sababu pengine za msingi.


Sasa najiuliza nikiwa nimevamiwa usiku au nahitaji polisi kwa msaada wowote ule , je nitakuwa na ujasiri gani wakumuita OCD kwa msaada , kwangu mimi hofu niliyonayo dhidi yake kama kiongozi wa polisi ni kubwa kuliko kukutana na majambazi usiku* , hata hivyo” LETS GO, LETS GOD”
*Lakini kutafakari kwangu historia mara kwa mara* inatia moyo kwamba hakuna harakati ambazo hazikuitwa ukorofi ,uvunjaji wa sheria , uhaini, na ukiukwaji wa taratibu , niweke wazi *kwamba nitapinga ukandamizaji wowote ule mbele ya yoyote Yule mwenye silaha yoyote ile na mwenye magereza yenye mateso makali* kuliko jehanamu bila woga , na sheria yeyote inayokiuka misingi ya *


Kwa kweli nimejiandaa hata kupokea mauti* japo najua Mungu anapenda niishi muda mrefu ili kutimiza kusudi lake ,* sitarudi nyuma *katika harakati hizi* za kupinga uonevu , dhuluma na ukandamizaji wa haki za binadamu nasubiri kwa hamu sana kuona mikakati yote iliyopangwa kinyume nami na wafuasi wote wanaopinga uonevu. Hata hivyo Nimeiandaa* familia yangu *kuwa tiyari wakati wowote kwa jambo lolote na kwa taarifa yoyote dhidi ya ukweli tunaoupigania.
Ndugu wanahabari **kila mara huwa nawaambia wananchi kuwa dhambi mbaya kuliko zote Duniani ni UOGA. Lazima watambue kuwa *wengine watateswa ,wengine watauwawa lakini wengine watafurahia haki na uhuru kamili tunaoupigania* hata kama hatutakuwepo kwa sababu tu wengine walipitia mateso mbali mbali. Mimi natambua kuwa faida ya kuishi* sio kuishi vizuri tu wewe na familia yako bali ni wewe kuwa sehemu ya mabadilikio ya watu wanaokuzunguka , katika kupigani UTU , HAKI ,* ustawi mzuri wa Jamii. Na kila mtu anayemuogopa Mwenyezi* Mungu ataishi kufanya hivyo kama* Mahatma Gadhi alivyopata kusema* “The best way to find yourself is to loose yourself in the service of others”*
Godbless Jonathan Lema (MB)
30/10/2011
Reactions::

NBC,Waisaidia DUCE Milioni 10

Mshauri wa habari wa benki ya NBC, ndugu Redemptus Masanja akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10 kwa Prof. Bavo Nyichomba(kulia) akishuhudiwa na makamu mkuu wa chuo kikuu kishiriki cha elimu DUCE,Mh. Prof.Salome Misana(wa pili kulia).mwingine ni meneja mahusiano wa NBC,Robi Matiko-Simba.tukio hilo ni msaada wa kujenga maabara ya shule ya sekondari Chang'ombe iliyo chini ya DUCE.
Picha na Francis Nyoni
Reactions::

Rais Kikwete Ahutubia Siku Ya Kilele Ya Mkutano Wa CHOGM

Rais Mh.Jakaya Kikwete Akizungumza Mwishoni Mwa mkutano wa Perth.katikati ni waziri mkuu wa Australia Ndg,Julia Gillard, na kushoto ni katibu mkuu wa nchi za jumuiya ya madola Bwana Kamalesh Sharma, ambaye amechaguliwa kuendelea na wadhifa huo.
Picha na Fred Maro
Reactions::

Pinda Achangisha Zaidi Ya Milioni 100, St.Peters,Dar

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto baada ya kuongoza harambee ya siku ya mavuno kwenye kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es saalaa, Oktoba 30,2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiwa katika picha ya pamoja na watoto waliochangia katika harambee ya siku ya mavuno ya kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam Oktoba 30,2011. Kushoto kwake ni paroko wa kanisa hilo,Padri Joseph Mosha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Reactions::

Serengeti Breweries Wazindua Kinywaji Kikali Aina Ya Baileys

Mkurugenzi wa Masoko Serengeti Breweriers Akizungumza katika uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers Ephraim Mafuru kulia akiwa na Meneja Masoko Kampuni hiyo Emillian Rwejuna wakizunguza na wageni walikwa katika hafla hiyo
Kunre Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kampuni ya bia ya Serengeti alikuwa nji mmoja wa wageni waliotoa zawadi kwa washindi wa chupa za mvinyo wa kinwaji cha Baileys
Mkurugenzi wa masoko wa vinywaji vikali kampuni ya EABL Angelique Libese akizungumza wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha Baileys uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam jana , ambapo wadau na wageni waalikwa mbalimbali walijitokeza katika uzinduzi huo, Baileys ni kinywaji kitakachosambazwa na kuuzwa na kampuni ya boa ya Serengeti Breweries
Kutoka Fullshangweblog

Reactions::

Ukweli Kuhusu Hali Ya Mh. Ztto Kabwe


 29 Oktoba 2011

Ndugu zangu,
 
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).
 
Mwanzo
 
Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.
Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.
Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.
 
Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.
 
Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.
Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).
Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.
 
Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.
Hali kubadilika
 
Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajuliha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.
Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!
Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.
 
Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.
Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.
 
Hali kuwa Mbaya
Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.
Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.
Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.
Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.
Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).
Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.
Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

Sijafa
Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

Shukran
Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.
Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.
Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri
Ndugu yenu
Zitto

Chanzo jamiiforums.com
Reactions::