German ambassador to Tanzania Hon. Klause – Peter Brandes in a deep conversation with the Speaker of The National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda(MP) during his courtesy call to Hon. Makinda’s Office. Ambassador Brandes said German is interesting in strengthening its relation with its Parliament of the Federal Republic of Germany(The German Bundestag)and their counterparts in Tanzania, The National Assembly(Bunge)
Wednesday, November 30, 2011
Ubwa Salum Ajifua Kumkabili Mustafa Dotto Desemba 25
Bondia Ubwa Salum (Mwenye bukta ya bluu) na Omari Bayi wakioneshana umwamba wa kutupa masubwi wakati wa Mazoezi ya Kambi ya Ilala Dar es salaam jana Ubwa anajiandaa na mpambano wake na Mustafa Doto Desemba 25 mwaka huu.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
| Reactions:: |
Waziri Mkuu Asisitiza Kuwa Wawekezaji Sio Lazima Watoke Nje
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amesema suala la uwekezaji hapa nchini haliwalengi watu wa nje tu bali hata wa ndani wanaweza kuwekeza hata kama ni kwa kiwango kidogo. Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumatatu, Novemba 29, 2011) wakati akizungumza na wakazi wa mikoa ya Rukwa, Ruvuma na mkoa tarajiwa wa Katavi katika chakula cha jioni ambacho aliwaandalia kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wakazi hao zaidi ya 100 walikuwa wamealikwa kuja jijini Dar es Salaam kushiriki tamasha la Utamaduni la mikoa ya Rukwa na mkoa tarajiwa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tamasha hilo lilifanyika Novemba 25-27, 2011, katika kijiji cha Makumbusho jiini Dar es Salaam.
Akifafanua kuhusu uwekezaji Waziri Mkuu alisema yeye alipochukua mkopo waliopatiwa wabunge wa sh. milioni 90, hakuona haja ya kununua gari bali aliamua kuwekeza katika ujenzi wa nyumba ya kulala wageni kijijini kwao, Kibaoni wilayani Mpanda. “Nilichukua mkopo mwingine benki ya NMB na kuamua kujenga vyumba 24 pale kijijini kwetu. Kama ningetaka ningechukua mafundi wazuri kutoka Kariakoo, (Dar es Salaam) lakini niliamua kutumia mafundi wa kijijini ili kutokana na zile fedha nao pia waweze kununua bati na kuezeka katika nyumba zao, jambo ambalo limewezekana,” alisema. “Ujenzi wa vyumba 24 karibu unakamilika, … kiasi kingine cha fedha nililima shamba la mahindi na nikafanikiwa kuvuna magunia 380,” aliongeza. Waziri Mkuu anasema aliamua kuuza magunia 300 kati ya hayo aliyovuna na kupata sh. milioni 11 ambazo aliziwekeza tena katika mradi wa ufugaji nyuki kijijini kwao na Dodoma. “Nina mizinga 250 kule Dodoma na Kibaoni (kijijini kwao) nina mizinga 600, kila mzinga unauzwa sh. 50,000/- na kila mmoja una uwezo wa kutoa lita 10 za asali. Bei ya asali hapa mjini ni sh. 10,000/- kwa hiyo katika kila mzinga unaweza kupata sh. 100,000/-,” alisema.

Alisema suala la uwekezaji ni muhimu na haliepukiki na kumtaja Mbunge wa Mpanda Mjini, Bw. Said Arfi ambaye alikuwepo katika hafla hiyo kwamba ni miongoni mwa wawekezaji wadogo kwani ana ekari 200 za mahindi na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Kanali Antonio Mzurikwao kuwa naye ana ekari 100 za mahindi. “Hawa nao ni wawekezaji lakini tunawaita wawekezaji wadogo,” alisema. Akifafanua kuhusu uwekezaji, Waziri Mkuu alisema nchi zote zilizoendelea zilifaulu kufiki hatua hiyo kwa kupunguza idadi ya wakulima wadogo na kuongeza idadi wa wakulima wakubwa. “Mkiona wakulima wadogo ni wengi mjue kuwa bado hamjapunguza umaskini,” aliongeza. Alisema Taifa bado linakabiliwa na changamoto ya kupunguza umaskini kwa kuhahakikisha kwamba kuna uzalishaji wa chakula cha kutosha ili watu kwanza washibe lakini pia akaongeza kusema kwamba inabidi uzalishaji uwe na tija ili wakulima wapate mazao mengi na kujiongezea kipato. Akitoa shukrani katika hafla hiyo, Mbunge wa Mpanda Mjini, Bw. Said Arfi aliwashukuru wajumbe wa Kamati za maandalizi katika mikoa ya Dar es Salaam na Rukwa kwa maandalizi mazuri hadi wakafanikisha tamasha la utamaduni wa mikoa hiyo miwili.
| Reactions:: |
Jerry Muro Na Wenzake Waachiwa Huru
Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Aliyekuwa Mtangazaji wa TBC1, Jerry Muro na wenzake 2, wameachiwa huru leo na hakimu Frank Mosha wa mahakama ya kisutu baada ya kuwaona hawana hatia na makosa waliyoshitakiwa nayo. Jerry na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matatu ya Kula njama ya kutenda kosa, kuomba rushwa na kujifanya maafisa wa Takukuru, madai ambayo yametupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
| Reactions:: |
Makamu Wa Rais Aiwakilisha Tanzania Kwenye Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi Za Afrika Mashariki
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania, nchini Burundi, Dkt. James Mwasi, baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliliana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Jan Ping, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akiwa katika Ukumbi wa Golf, wakati akimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifunga rasmi Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, kwenye Ukumbi wa Golf, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza (katikati) na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Jan Ping, wakisimama kwa heshima wakati ukipigwa wimbo maalum wa Afrika baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga rasmi Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilish Tanzania katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika mjini Bujumbura, Burundi Novemba 29 - 30, 2011. Makamu wa Rais alifika mjini hapa jana ambapo aliwakuta Mawaziri kadhaa wa Tanzania waliotangulia kuhudhuria mikutano ya ngazi za Mawaziri wakiongozwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Manaibu Waziri Deo Mfutakamba, Lazaro Nyalandu na Adam Malima.
Katika mikutano ya awali katika ngazi ya Mawaziri, Tanzania ilijumuika na nchi nyingine za ukanda huu kutazama namna ya kusaini Protokali ya Ulinzi wa pamoja, protokali inayotaka nchi wanachama wa Jumuiya hii kushirikiana kijeshi pale inapokubalika ama inapoonekana kufaa baada ya nchi mwanachama kuwa katika hatari ya vita.
Hata hivyo mjadala huu ulikuwa ni mkali huku Tanzania ikitaka protokali hii isainiwe mara tu pale itakapokuwa na kipengele kinachobainisha kuwa, nchi wanachama watatakiwa kushirikiana ama kusaidiana baada ya kila nchi mwanachama kupima aina ya hatari na mchango wa hatari hiyo kwa nchi mshiriki ambaye ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pia, mkutano huu ulikuwa na kazi ya kupitisha maelekezo ya wataalam yanayolenga kuongeza kasi ya kuundwa kwa shirikisho la Afrika Mashariki. Msimamo wa Tanzania katika agenda hii ni kuwa zoezi hili halijafikia muda muafaka na kwamba kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanyika kabla ya Jumuiya hii kuunda shirikisho.
Hata hivyo nchi nyingine za Afrika Mashariki zimekuwa zikishirikiana kwa lengo la kuongeza kasi na kuishinikiza Tanzania kukubali kuundwa kwa shirikisho, jambo ambalo linapingana na taratibu na kanuni za Jumuiya hii, zinazotokana maamuzi yote yafanyike kwa makubaliano yanayotoka kwa wananchi wa jumuiya hii na kwa kila taifa husika. Kwa mujibu wa ujumbe wa Tanzania, suala la shirikisho lilipingwa katika kamati ya Wangwe na hadi wakati Tume hiyo ilipokusanya maoni, hadi sasa hakujawa na tofauti ya mtazamo.
Tanzania inahitaji kufanyika kwanza maafikiano katika soko la pamoja na mataifa ya jumuiya hii kutazama namna yatakavyoweza kunufaika kabla ya kukimbilia ushirikiano wa kisiasa ambao kama utakimbiliwa bila mazingira kujengwa, ni rahisi kwa jumuiya hii kuvunjika kama ilivyowahi kufanyika huko nyuma.
Makamu wa Rais pia alikuwa na kazi ya kufunga mkutano wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukijadili mahusiano na uendelezaji wa Ukanda za Ziwa Tanganyika ambapo katika mkutano huo, alifafanua namna Tanzania inavyoshiriki kwa ukamilifu kuunganisha mikoa yake na nchi za mipakani hasa katika ujenzi wa barabara za lami, na namna ushirikiano kati ya nchi za SADC, EAC na COMESA unavyolenga kukuza biashara sambmba na uchumi kwa nchi wanachama.
Makamu wa Rais anarejea nyumbani kesho Desemba Mosi ambapo atakuwa na kazi ya ufunguzi wa barabara jijini Dar es Salaam Desemba pili, 2011.
Imetolewa na: Idara ya Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
Novemba 30, 2011
| Reactions:: |
Watu 34 Iringa Walazwa Kwa Kunywa Togwa Yenye Sumu
Watu waliokunywa togwa wakati wa sherehe wakiwa wamelazwa hospital wakipatiwa matibabu.
WATU 34 wa kijiji cha mtitu wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ikiwemo familia moja ya watu sita wamenusurika kifo na kulazwa katika hospital teule ya wilaya ya Iringa (Hospital ya Ipamba) baada ya kunywa togwa katika sherehe ya kipaimara inayosadikika kuwa na sumu. Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika kijiji hicho cha Mtitu wilaya ya Kilolo wakati watu hao walipofika kusherekea sherehe ya kipaimara cha mtoto Hotmary Mpogole na kupewa kinywaji hicho cha asili kilichotengenezwa kwa unga wa nafaka ya mahindi (togwa). Akielezea juu ya tukio mhanga wa tukio hilo Geofrey Chavala alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na rafiki yake wakati akitokea msibani kuwa waelekee katika nyumba hiyo kwa ajili ya kula wali wa sherehe na baada ya kufika walipewa chakula hicho na baada ya hapo walipewa togwa kama kisushio . Hata hivyo alisema wakati akiendelea kunywa alibaini radha tofauti na ile ambayo amepata kuizoea kwa kinywaji kama hicho na hivyo kuonyesha kusitasita katika kuendelea kunywa japo alijitahidi kunywa hadi anamaliza lita moja peke yake.
Alisema baada ya kumaliza hali ya hewa tumboni ilibadilika na kujikuta akianza kutapika na kuhara damu hali iliyopelekea kurudi nyumbani na baada ya kufika huo alikutana na bibi yake na kuelezwa kuwa kama amekunywa togwa wenzake wanakusanywa kwa ajili ya kwenda Hospital ndipo alipoungana na wenzake hao. Fedelika Chaula (40) ambaye ni mzazi wa watoto waliokuwa wakifanyiwa sherehe hiyo ya Kipaimara alisema kuwa aliandaa sherehe hiyo kwa ajili ya kuwapongeza watoto wake wawili na kuandaa togwa hiyo kwa ajili ya kunywaji kwa watu walioalikwa katika sherehe hiyo. Hata hivyo alisema kuwa mahindi yaliyotumika kwa ajili ya kuandaa togwa hiyo ni mahindi ambayo wamekuwa wakiyatumia siku zote kwa ajili ya chakula na kuwa anashangazwa na kutumia nafaka hiyo kwa kutengeneza togwa na kupatwa na madhara hayo.
Alisema kuwa watoto wake wanne wamelazwa katika hospital hiyo pamoja na yeye mwenyewe kwa kunywa togwa hiyo . Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mtitu Beatus Kivamba akielezea tukio hilo alisema kuwa awali alikutana na watu wawili wakitoka katika sherehe hiyo huku wakitapika na kuraha kutona na kunywa togwa hiyo na baada ya kuwasiliana na muunguzi wa kituo cha afya Mtitu ndipo alipomthibitishia kupokea wagonjwa zaidi wa tukio hilo . Alisema kutokana na tukio hilo alilazimika kuomba msaada kwa gari kwa Paroko wa Mtitu ambaye alitoa usafiri wa Lori na kuwachukua wagonjwa wote 34 na kuwafikisha katika Hospital hiyo ya Ipamba kwa matibabu. Muuguzi mkuu wa Hospital hiyo ya Ipamba Sr. Julieta Mzena aliwataja waliofikishwa hospital hapo na kulazwa kuwa ni pamoja na watoto zaidi ya watano ambao ni wanafunzi na watu wazima wanaume na wanawake.
Aliwataja wahanga hao ambao wamelazwa kuwa ni pamoja na Yudita Ndongoro , Onolata Mhangara, Otineli Mpogole, Sekela Mbilingi, Jafarini Mhulila, Faines Mhulila, Agineli Luvinga, Sofia Mhulila, KIlelia CHongolo, Frolida Mgaya, Geofrey Chawala, Vero Kasuga, Meshack Chaula, Nemia Chaula, Baraka Kivale, Edison Kivale, MUstaphar Mhulila, na Gelion Mpogole. Wengine ni Chelelina Chongolo , Raheli Mgogolo ,Kanisia Chongolo, Diana Chongolo , Chadeta Mlimakizi, Zaina Mpagama, Bile Mtono , Setty Kilave, Nesta Mwofuga,Manwela Mhagala ,Federika Chaula na mtoto Hotmery Mpogole mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi mtitu ambaye ndiye alikuwa ameandaliwa sherehe hiyo ya kipaimara. Alisema kuwa hali za wagonjwa hao zinaendelea vizuri na kuwa tatizo lao inaonekana kula chakula chenye sumu. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla alisema kuwa yupo nje ya ofisi na kikazi na kuwa bado hajapata tarifa na kuahidi kufuatilia zaidi.

Taifa Stars Yainy'uka Djibouti 3 - 0
Mlinzi wa Stars, Shomari Kapombeakichuana na nahodha wa Djibouti
Mohamed Kadar wakati wa mpambano wa TUSKER CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP kwenye uwanja wa Taifa Stars ilishinda bao 3-0. Mabao ya timu hiyo yalifungwa na Thomas
Ulimwengu, Mwinyi Kazimoto na Yusuf Rashid.

PICHA NA MOHAMED MAMBO
| Reactions:: |
Pima- Maji Ya Mjengwablog: Watano Hawa Wanaogelea Kwenye Kina Kirefu!
Ni kwenye Pima- maji ya Mjengwablog. Halima Mdee ameawaacha mbali wenzake. Watano waliovuka hatua ya kwanza ni Halima Mdee, Regia Mtema, Raya Ibrahim, Zainab Kawawa na Esther Bulaya. Watano hawa watapambanishwa na watano kutoka kundi la wabunge vijana. Tayari kuna majina yaliyopendekezwa na watembeleaji wa Mjengwablog. Majina hayo ni yafuatayo: 1.JANUARY MAKAMBA CCM 2.JOHN MNYIKA CDM 3DAVID KAFULILA NCCR 4 ISMAIL JUSSA LADHU CUF 5 DR.HAMIS KIGWANGALA CCM 6 ZITTO KABWE CDM 7 FELIX MKOSAMALI NCCR 8 SELEMANI MASELE CCM 9 GODBLESS LEMA CDM 10.MOSES MACHALI NCCR Hatua hii ikikamilika tutaingia katika kitakachoitwa; Mjengwablog Young Leadership Awards. HNi jitihada za blogu hii kumpata mwanasiasa bora wa mwaka kutoka kundi la wabunge vijana. Chini hapa ni matokeo yalivyokuwa katika hatua iliyopita; Vicky Kamata | 17 (3%) |
Raya Ibrahim | 28 (5%) |
Sabrina Sungura | 9 (1%) |
Halima Mdee | 395 (72%) |
Regia Mtema | 32 (5%) |
Lucy Mayenga | 11 (2%) |
Zainab Kawawa | 19 (3%) |
Cathrine Magige | 7 (1%) |
Ratchel Mashishanga | 5 (0%) |
Esther Bulaya | 21 (3%) |
Votes so far: 544
Poll closed
| Reactions:: |
Tanzania Responsible Business Network
Founding members of the Tanzania Responsible Business Network (TRBN) in a group photo soon after the official launch held at the Hyatt Regency, the Kilimanjaro on Monday 28th November 2011.
| Reactions:: |
TMTV a.k.a Tanzania Music Television 24/7 Non Stop
Link www.tmtv.co.tz Downlod microsoft Silverlight itajitokeza ktk screen,kama haijafunguka yenyewe.
Email. info@tmtv.co.tz
| Reactions:: |
Ngoma Africa Band Kuvamia Munchen Jumamosi Disemba 3
FFU wa Ngoma Africa Band kutoa burudani ya kukata na Mundu
Watanzania wanaoishi Ujerumani ! na Full Shangwe ya Miaka 50 ya Uhuru ! Kuanzia München hadi Berlin Chereko !Chereko! Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi ! 10-12-2011 Berlin!
Watanzania wanaoishi Ujerumani ! na Full Shangwe ya Miaka 50 ya Uhuru ! Kuanzia München hadi Berlin Chereko !Chereko! Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi ! 10-12-2011 Berlin!
Watanzania waishio Ujerumani wameanza shamra shamra za kusherekea miaka 50 ya uhuru
wa Tanzania bara, kwa kasi kubwa inayotingisha kila kona,sherehe hizo zinaanzia mjini
München siku ya 3 Dec 2011 ambapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za
Tanzania,mavazi,na mdahalo rasmi na usiku kutakuwa na muziki wa Ngoma Africa Band
katika mtaa wa Siebold Str,11 ndipo penye ukumbi.
Kuanzia 9 hadi 10-Dec-2011 mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio
mji mkuu wa Ujerumani,kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi
wa UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) siku ya jumamosi 10-12-2011,umoja
huo unawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani,ulitiliwa nguvu na balozi Mh.Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Bw.Mfundo Peter Mfundo(mwenyekiti) na
Bi.Tullalumba Mloge (katibu),utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9 mchana hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU,watatumbuiza na muziki wao,mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin,
UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU !
sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com

Pima-Maji Ya Mjengwablog: Watano Hawa Wamezamishwa!
Kura zao hazikutosha kuingia kwenye tano bora kati ya washiriki kumi waliopendekezwa na watembeleaji wa Mjengwablog. Waliozamishwa ni waheshimiwa Cathrine Magige, Vicky Kamata, Sabrina Sungura, Rachel Mashishanga na Lucy Mayenga. Angalia matokeo ya Pima- Maji hiyo hapo juu kulia.
| Reactions:: |
Tuesday, November 29, 2011
JK Asaini Muswaada Wa Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao
kilichopita cha Bunge. Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na
Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010. Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na
mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria
hiyo.Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye
maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru
kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu
| Reactions:: |
Mjengwablog Iko Kwenye Ukarabati: Je, Mnaonaje Juu Ya Mwonekano Huu Mpya?
Ndugu zangu,
Tunakaribisha maoni yenu wakati tukiendelea na kazi ya ukarabati .
Maggid,
Iringa.
| Reactions:: |
Uzinduzi Wa Programu Ya Miundo Mbinu Ya Masomo Utengenezaji Thamani Na Huduma Za Kifedha Vijijini
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizindua Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na baadhi ya viongozi waliohudhuria katika uzinduzi wa Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar
Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Programu ya Miundo mbinu ya Makomo, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd hayupo pichani katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Na Hamad Hija –.Maelezo Zanzibar
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amesema kuwa utekelezaji wa Programu ya Miundo mbinu ya masoko, Uongezaji thamani na Huduma za kifedha vijijini utasaidia sana kusukuma mbele maendeleo ya wakulima wafugaji pamoja na wavuvi wanaoishi vijijini. Balozi Seif ameyasema hayo huko katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani mjini Zanzibar wakati akizindua programu ya miundombinu masoko na uongezaji thamani na huduma za kifedha Vijijini kwa upande wa Zanzibar.
Alisema kwamba mpango huo wa utelekelezaji wa mifumo ya masoko kwa upande wa Tanzania Bara umeweza kuwanufaisha walengwa na kuongeza bei ya mazao yao kwa wastani wa mara mbili zaidi ya kile ambacho wakulima walikuwa wakikipata hapo awali. Aidha amekumbusha kuwa kutokana na mafanikio yaliyopatikana kupitia mpango huo Serikali ikishirikiana na washirika wa maendeleo kama vile IFAD,ADB na ACRA ilionelea kuwa ni vyema mafanikio hayo kuenezwa na kupelekwa kwa wananchi walio wengi kupitia mpango huo ikiwemo vijiji vya Zanzibar. Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikichukuwa hatua mbali mbali katika kuimarisha miundo mbinu ya umwagiliaji maji, kuongeza ruzuku ya pembejeo na utekelezaji wa programu mbali mbali za kuendeleza kilimo uvuvi na ufugaji kwa lengo la kupunguza umasikini na kuongeza kipato cha wakulima. Balozi Seif Ali Idd amefahamisha kuwa sekta ya kilimo ni muhimu sana kwa vile imekuwa ikitowa ajira kwa zaidi ya asilimia 70 na kuchangia asilimia 50 ya chakula katika Nchi yetu.
Aidha Balozi amesema kuwa hatuwa ya kuzindua programu hii ni hatua moja wapo ya kupunguza umasikini na kujitosheleza kwa chakula ambapo hiyo ndio sera ya maendeleo inayolenga maendeleo endelevu na kuongeza kipato kupitia kazi za wajasiriamali nchini. Naye Mratibu wa Programu hiyo Khalfan Masuod Saleh amesma kuwa uzinduzi huo ambao umefanywa hivi leo ni mpango ambao unagharamiwa kwa pamoja na Serikali ya Muungano ya Tanzania ambapo kwa upande wa Serikali ya Muungano imetoa Dola za kimarekani Milion 9.6, Mfuko wa kimataifa wa Maendeo ya Kilimo (IFAD) umetoa Dola Milion 90.6 . Aidha Bank ya Kimaendeleo ya Afrika (ADB) imetoa Dola za kimarekani 62.9 ambapo kwa upande wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani ya Afrika (ACRA) imechangia kwenye mfuko huo jumla ya dola za kimarekani 6.9
Akizungumzia mpango huo mratibu huyo amesema kuwa lengo kuu la mpango huo ni kwa ajili ya wanawake ambapo itajenga uwezo kwa wakulima na kuwaunganisha na masoko ili kuhakika suala lao la masoko nchini linapatiwa ufumbuzi. Khalfan amesema kuwa Programu hiyo itawajengea uwezo wakulima ili wapate taarifa mbali mbali zinazohusiana na shughuli zao kwa kuwaunganisha na makampuni mbali mbali. Ameongeza kuwa mpango huo unategemewa kuwa wa muda wa miaka sita kwa kuwa utaendeshwa Tanzania nzima na unategemewa kufikia kaya laki tano vijijini.
Amesema lengo kuu la mpango huu ni kuongeza kipato cha uhakika wa chakula vijijini kwa njia endelevu hususani kuboresha miundo mbinu ya masoko ili kuwajengea uwezo wananchi waishio vijijini. Programu hiyo pia itawawezesha wakulima kuyafikia masoko na kuongeza thamani ya mazao yao ya kilimo pamoja na kupanuwa wigo wa huduma za kifedha vijijini.
| Reactions:: |
JK Aagana Na Balozi Wa Denmark Anaemaliza Muda Wake Nchini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Denmark aliyemaliza muda wake wa kazi nchini Bw. Bjarne Henneberg Sorensen Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2011.
Picha na IKULU
Picha na IKULU
| Reactions:: |
Lowassa; "Mungu Yupo Na Mimi Nitayashinda Majaribu"
Askofu Mkuu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kati Mch, Eliufoo Sima akitoa mahubiri katika kanisa hilo usharika wa Amani Sabasaba mjini Singida wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ulioendeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa.
Askofu wa KKKT Mchungaji Eliufoo Sima akipokea kiasi cha shilingi milioni 10 taslimu kutoka kwa Mhe.Lowasa kama mchango wake katika kufanikisha harambee ya ujenzi wa kanisa hilo.
Picha Na Hillary Shoo
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe.Edward Lowasa amesema kuwa pamoja na kusemwa maneno mengi sana kwenye vyombo vya habari juu yake lakini anamwami mungu kuwa anampigania kila kukicha.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoani Singida Hillary Shoo anaripoti kuwa Lowasa ameyasema hayo leo mjini Singida wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT usharika wa Amani sabasaba mjini Singida. “Wale wanaofuatilia siasa za nchi yetu kuna maneno mengi saana lakini bwana ni mwema na mwaminifu hatimae tumeshinda”.Alisema. Alisema mara baada ya taarifa hizo siku moja akiwa nyumbani kwake na mkewe huku wakiangalia TV na kutaka kujua magazeti yanasemaje asubuhi kulikuwa na maneno mengi yaliyosemwa ya hovyo hovyo juu yake mengine walishindwa kuyasoma.
“Lakini mke wangu alienda chumba cha pili na kuchukua biblia na kunifungulia maneno ya bibilia kitabu cha Isaya 41:10, usiogope kwa maana mimi niko pamoja nawe tusifadhaike kwa maana mimi ni mungu wako nitakutia nguvu naam nitakusaidia, naam nitakushika mkono wa kuume wa haki yangu.” Alisema na kuongeza kwa maneno hayo niliendelea sana lakini baba askofu nisamehe nichukue hadhara hii kuwashukuru watu wengi sana walioniombea na hatimae kufika hapa nilipo. “Wapo waislamu na mashekhe walifanya dua kwa niaba yangu, nawashukuru sana, pia wapo wakristo walioniombea nao nawashukuru sana, mapadri, mashemasi na watawa, wachungaji na wainjilisti wa madhehebu yote, kwaya bmbalimbali na waimbaji wa nyimbo za injili, wanamaombi wote, wanamtandao wao wa ajabu una nguvu kweli kweli na maaskofu wa makanisa yote ya kikristo pia nawashukuru sana.” Alisema Lowasa.
Aidha Mhe Lowasa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli alisema kuwa maneno mengi ya kisiasa yalisemwa juu yake lakini kimsingi hayakuwa ya kweli ya ukweli na siasa zinazoendelea kwa sasa ni za kuchafuana. Pia Lowasa alinukuu maandiko mengine ambayo aliyasoma kutoka kitabu kitakatifu cha Warumi ambayo aliyasoma mwenyewe. “ Lakini ikiwa roho yake yeye aliyemfufua yesu katika wafu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu hataihuisha miili yemu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake anakaa ndani yenu” alinukuu Lowasa.Aidha alisema kutokana na misukosuko ya kisiasa ambayo amekumbana nayo amekuwa akimwona mungu akimtetea na utetezi huo ameupata kutoka kwa mungu, kutokana na maombi ya watakatifu kutoka dini mbalimbali ambao wako pamoja.
Wale wote ambao wamaamini kuwa nafanya kazi kwa kusimamia haki ya mungu na kazi zote kwa ujumla waliniombea usiku na mchana na kwa hilo mungu kawasikia na kanifanya kuendelea tofauti na uchafu ambao mimekuwa nikibambikizwa na siasa za kuchafuana. Hata hivyo Lowasa alidai kuwa kama kiongozi hana mungu ndani yake hawezi kuhimili mikiki ya kisiasa kwani kinachotakiwa ni kumwomba mungu ili aweze kutetea kazi zinazofanywa na mtu mwenye haki. “Nimekuja kwenye harambee sio kupiga maneno ya kisiasa, nilimwambia baba askofu tuna utamaduni wa kualikwa haramabee nyingi sana , lakini kabla ya kukubali unauliza kwamba hao unaoshiriki nao wamefanya nini, nyie mmefanya kazi kubwa sana nawashukuru na nafurahi kwenye harambee hii.” Alisistiza na kuongeza.
“Kwa sababu ni njia mojawapo ya kuthibitisha kwamba wananchi wanaweza kufanya mambo yao kwani kanisa kama hili miaka ya nyuma lingeweza kujengwa na wafadhili wa nje lakini leo limejengwa na wananchi wenyewe. Mapema askofu mkuu wa KKKT Dayosisi ya kati Mchungaji,Eliufoo Sima anaamini utulivu wa viongozi wa nchi hii ni dhahiri kwamba Taifa hili kwa jinsi ya utamaduni na mapokeo yake , na mambo magumu yanayotokea siku hadi siku, litafanikiwa kutengeneza njia thabiti ya mafanikio ya watu wake. Askofu Sima alisema kumekuwepo na madai mengi kuwa nchi yetu ni maskini lakini angependa viongozi kuyashughulikia kwa umakini mkubwa ili kuondoa manung’uniko miongoni mwao ili yasiharibu tabia njema ya baadhi yao. Hataa hivyo Askofu Sima alimwagia sifa Mhe.Lowasa na kusema kuwa ni tofauti na viongozi wengine ambao unaweza kuwatafuta kwenye simu kwa muda mwingi na wakawa hawapatikani.
“Kwa kweli wewe ni kiongozi wa pekee,tofauti na wengine,unaweza ukmtafuta kwenye simu hata mara tano na hapatikani, lakini wewe kila ninapokupigia unapokea simu yangu,na hata katika harembee hii nilipokupigia nikakuomba uje Singida ukasema upo njiani unaenda Dodoma,”. “Lakini na mimi nikakwambia nipo njiani naenda Morogoro,ukasema basi tukutane njiani,mtu mkubwa kama wewe kukutana njiani hiyo ni ajabu.”alisema Askofu. Katika harambee hiyo Mhe.Lowasa amechangia kiasi cha shilingi milioni kumi ambapo makusanyo yote yaliyopatikana katika ujenzi wa kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Amani zilipatikana zaidi ya shilingi milioni 138. Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini liliko Kanisa hilo Mohammed Dewji (MO) alichangia shilingi milioni 10, Mfanya biashara maarufu hapa nchini aliyemtaja kwa jina moja tu la Patel amechangia mabati ya kuezekea kanisa hilo yenye thamani ya shilingi milioni 50. Kanisa hilo la usharika wa amani linatarajiwa kukamilika mapema hapo mwakani kwa gharama ya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 480.
| Reactions:: |
Kanisa Katoliki Jimbo La Bukoba
Kanisa kuu la Bikira Maria Mama Wa Huruma (Mater Misericordia) la kanisa katoliki jimbo la Bukoba mjini(Cathedral). likimalizika Marehemu Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa atazikwa hapa akihamishwa kutoka kashozi alikozikwa kwa muda tangu mwaka 1997.Ujenzi unatarajiwa kumalizika hivi karibuni.
Hili ni jengo la ghorofa mbili ofisi za kanisa hilo katoliki pembezoni mwa kanisa lenyewe. ndipo ofisini kwa aliyekuwa askofu msaidizi wa jimbo la Dar es salaam aliyehamishiwa huku bukoba,askofu msaidizi Methodius Kilaini.
Na Mdau wa Mjengwablog, Bukoba
| Reactions:: |
Sokoni Bukoba Leo
Dagaa.kilo moja sh.5000
Hawa ni samaki aina ya Kamongo.hawana mifupa hawa. huyu mmoja ni sh. 12,000.Samaki aina ya sangara.mmoja ni sh.3000. wanasema kutokana na viwanda vya samaki hapa (Vickfish) sangara ni adimu na wanaopatikana ni wadogowadogo tu ila bei kali.
Duka la vifaa vya nyumbani sokoni bukoba
Sokoni Bukoba mjini leo. ndizi zina bei kubwa sasa hata hapa bukoba. mkungu mmoja ni sh.15,000.Na mdau wa Mjengwablog, Bukoba
| Reactions:: |
Subscribe to:
Posts (Atom)