Subscribe:

Saturday, December 31, 2011

Maamuzi ya kamati ya utendaji ya CUF - Taifa




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama Cha Wananchi (CUF) imefanya kikao chake cha kawaida cha siku mbili mjini Zanzibar tarehe 30 – 31 Desemba, 2011 chini ya Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad.

Pamoja na kujadili ajenda kadhaa za kawaida kuhusiana na mambo ya utendaji katika Chama, Kamati ya Utendaji ya Taifa pia ilipata nafasi ya kupokea taarifa ya kina kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chama kutoka kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama kupitia Kamati yake Ndogo ya Nidhamu na Maadili. Taarifa hiyo ilijikita zaidi katika njama zinazoendeshwa na wanachama 14 wakiongozwa na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed zenye mwelekeo wa kutaka kukivuruga Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna hoja za msingi na ushahidi wa kutosha dhidi ya wanachama hao 14 unaoonesha kuhusika kwao na njama hizo. Wanachama hao ni:

1. Hamad Rashid Mohamed2. Doyo Hassan Doyo
3. Shoka Khamis Juma
4. Juma Said Saanani
5. Yasin Mrotwa
6. Mohamed Albadawi
7. Mohamed Masaga
8. Doni Waziri
9. Yusuf Mungiro
10. Nanjase
11. Ahmed Issa
12. Tamim Omar
13. Amir Kirungi
14. Ayubu Kimangale

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kifungu cha 63 kinachozungumzia Wajibu wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, kifungu cha 63 (1) (d) kinafafanua wajibu huo kuwa ni “kulinda na kuendeleza heshima ya Chama na Serikali zote halali za nchi.” Kifungu cha 63 (1) (j) kinaelezea wajibu mwengine kuwa ni “kuwachukulia hatua za nidhamu viongozi na wanachama wanaoshutumiwa kwa makosa mbali mbali kwa kufuata masharti ya Katiba hii na kanuni zitakazotungwa mara kwa mara kwa mujibu wa katiba hii.”

Kwa kuzingatia hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna haja ya kutumia uwezo iliopewa chini ya kifungu cha 62 (1) cha Katiba ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ili kutafakari hali hiyo, kusikiliza tuhuma zinazowakabili wanachama hao, kuwapa nafasi ya kuwasiliza na kujitetea na kisha kuchukua hatua kama litakavyoona inafaa.

Kikao hicho cha Baraza kuu la Uongozi la Taifa kitafanyika Zanzibar, tarehe 04/01/2012 katika ukumbi wa hoteli ya Mazson.

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawaomba wanachama na wapenzi wote wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na kutoa nafasi kwa vikao vya Chama kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama.


HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa na;

JULIUS MTATIRO,
NAIBU KATIBU MKUU (TANZANIA BARA),
KATIBU WA KAMATI YA UTENDAJI TA TAIFA (CUF NATIONAL CENTRAL COMMITTEE).
31 Disemba 2011,
ZANZIBAR.
Reactions::

basi la mtei express lapata ajali

             Taarifa ambazo mjengwablog haiwezi kuzidhibitisha peke yake zinasema kuwa basi la mtei express(pichani) linalotoka manyara kuja Arusha limepata ajali.hatuna taarifa kwa sasa kuhusu vifo au majeruhi.tutawafahamisha kwa usahihi taarifa rasmi zitakapotufikia
Reactions::

waziri mkuu atembelea waathirika wa mafuriko dar

  Vijana wakipika ugali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Dar es salaam walioweka kambi kwenye shule ya sekondari ya Benjamin jijini Dar es salaam wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowatembelea Desemba 31, 2011.
           Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es salaam kwenye shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa wakati alipowatembelea Desemba 31, 2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Reactions::

Salaam Za Mwaka Mpya Kutoka Bagamoyo!





Ndugu zangu,

Nianze kwanza kwa kuwatakia heri na fanaka za mwaka mpya wa 2012.

Ewe ndugu mwanakijiji wa blogu hii ya Mjengwa, leo tunaumaliza mwaka wa 2011. Hivyo basi, kesho ni siku nyingine tena inayotujia.Ni mwaka mpya. Hivyo,  nawe kama utakuwa umejaaliwa siha ya kuyasoma haya. Mshukuru Mungu wako kwa kukujalia hilo.

Katika dunia hii, mwanadamu unaweza kuandaa juu ya nini kifanyike siku ya kifo chako. Lakini, mwanadamu usifikiri sana kuhusu siku yako ya kufa, maana,hujui ni siku gani, lakini  itafika siku utakufa, iwe mchana au usiku.

Utakufa ndani ya siku. Ndani ya saa 24. Ndio, utakufa ndani ya mwaka wenye siku 365. Na mauti yakikufika, basi, huna tena utakaloweza kulifanya. Hali yako ya umauti itaachwa kwa wanadamu wenzako. Hivyo, mwanadamu kaa uumize kichwa kufikiri siku unayoishi, na zijazo kama utaishi. Fikiri sasa juu ya utakayoyafanya kwa mwaka huu wa 2012.

Fikiri pia utakayowaachia nyuma  wanadamu wenzako. Yale ambayo utapenda ukumbukwe nayo pale watakapotaja jina lako. Maana, si kweli kuwa yote tuyafanyao sasa, mema na mabaya, yatapotea na umauti wetu.

Jiulize; Je, mwaka mpya una maana gani kwangu?

Ndio,  nami nimejiuliza swali hilo. Nimetafakari  juu ya siku na maana yake kwetu wanadamu. Juu ya mwaka na maana yake kwa mwanadamu.

Najiuliza; siku inakuja au inakwenda? Na mwaka je? Fikra zangu zimenielekeza kwenye kuamini,  kuwa wenye kudhani kuwa siku  na miaka inakwenda wanakosea. Maana, siku  na haziendi wala hazigandi. Siku zinakuja. Vivyo hivyo kwa mwaka. Miaka haendi wala haigandi. Miaka inakuja.

Na usihangaike sana  kujiuliza; leo ni siku gani? Lililo muhimu ni kuiona siku. Unaweza hata kuamua uipe siku jina jingine badala ya  Jumapili kama ilivyo siku ya leo.

Basi, ewe mwanadamu mwenzangu, kama zawadi,  ipokee kwa mikono miwili siku hiyo iliyokujia. Ipokee kwa furaha na si kwa manung’uniko. Mshukuru na mwombe Mungu wako akuongoze katika kuitafuta busara na hekima ya kuitumia vema siku hiyo iliyokujia.

 Akuongoze kutenda yalo mema na yenye wingi wa uadilifu.  Yale yatakayokuwa na manufaa kwako na kwa wanadamu wenzako. Hivyo basi, kwa jamii unayoishi. Kwa Nchi yako. Usiwe ni mtu mwenye tamaa. Usiwe mbinafsi na mwenye tamaa ya mamlaka.

Na ndugu zangu Wakristo na hata wengine wasio Wakristo wanakitambua kisa cha Essau na Yakobo. Na tafsiri zaweza kuwa nyingi; hii ni ya kwangu. Tunasoma, kuwa Essau na Yakobo walikuwa ni wana wa Isaka.

Essau alikuwa ni mkubwa akifuatiwa na Yakobo. Essau Yule alikuwa ni mwindaji. Naye Yakobo alikuwa akipenda sana kushiriki shughuli za mapishi jikoni akiwa na mama yake.


Biblia inasema, kuwa siku moja Essau alikwenda katika mawindo yake. Alirudi mikono mitupu, hakupata kitoweo. Aliporudi nyumbali Essau alikuwa ni mwenye njaa kali, kwani, aliwinda siku nzima mwituni pasipo kula.

Nyumbani alimkuta Yakobo akiwa amepika dengu. Essau alimuomba Jakobo ampatie bakuli la dengu ili ale na kutuliza njaa yake.

Yakobo alimwambia kaka yake Essau; ” Kama unataka bakuli la dengu, basi, ukubali kuwa mdogo kwangu.” Yaani, Essau akubali kuwa, kuanzia siku hiyo, yeye Yakobo ahesabike kuwa mkubwa (mzaliwa wa kwanza) wa Isaka baba yao, na Essau awe ni mzaliwa wa pili.

Kwa vile Essau alikuwa na njaa sana, alikubali kuwa mdogo kwa Yakobo. Ndipo akapewa bakuli la dengu amalize njaa yake. Naam, tunaona, kuwa njaa ilimfanya Essau auze haki yake ya uzaliwa wa kwanza.


Na ya akina Essau na Yakobo tunayaona sasa. Kuna hata wanaouza haki za Wananchi kwa sababu ya njaa zao. Na wengine si kwamba wana njaa kali hivyo. Ni wenye njaa ya kutaka shibe kama ya mbwa mwitu. Ni watu wenye kuendekeza tamaa.

Na akina Yakobo wa sasa wenye bakuli la dengu baadhi yao ndio hao wanaoitwa wafanyabiashara. Masharti yao ya kutoa bakuli la dengu ni pamoja na kusamehewa kodi au kupewa upendeleo katika kupata tenda mbali mbali. Wamefikia hata kutoa masharti ya kutuchagulia viongozi wetu.

Na nguvu hizo tumewapa wenyewe kwa baadhi yetu kuendekeza njaa na kutaka shibe za mbwa mwitu. Na wenye bakuli la dengu wa siku hizi, hawakupi bakuli la dengu likajaa. Kwamba ule ukashiba. La, watakupa dengu kiduchu ili urudi tena kuomba bakuli lingine. Uwe tegemezi kwao.

Ndugu zangu,

Kuna wengi mlio kwenye jiko lenye giza huku mkiwa na njaa kali. Mnachohitaji kwanza ni ukombozi wa kifikra . Ukombozi huo utawapelekea kwenye kuepuka kufa na njaa. Kuepuka kuwa watumwa kwenye nchi yenu mliyozaliwa. Kwenye ardhi ya mababu zenu. Anzeni sasa kuuwasha moto. Moto huo utawapa pia mwanga kwenye jiko hilo lenye giza nene.

E nendeni mkayatafute majani makavu. Kisha muyaweke katikati ya mafiga. Tieni moto kiberiti muyawashe. Yakishawaka, anzeni taratibu kuweka vijiti na vibanzi vikavu juu yake. Na vitakaposhika moto, endeleeni kuweka kuni kubwa huku mkipulizia.

Moto utakaowaka hapo hautazimika kirahisi. Utawapa shibe ya boga au muhogo. Utawapa mwanga pia. Ni mwanga wa ukombozi wa kifikra na kiuchumi.  Heri ya Mwaka Mpya kwenu nyote.

Maggid Mjengwa,
Bagamoyo
Desemba 31, 2011
Reactions::

Babu Wa Loliondo Janga La Kitaifa 2011


“Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote”,ni wimbo unaovutia ni wimbo unaelezea wasifu wetu wasifu wa nchi yetu Tanzania kweli jina lako ni tamu tulalapo tunakuota wewe, Ndoto wakati mwingine uashiria kitu kijacho !

Naam ndugu zangu Watanzania,
tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka nchi yetu imekumbwa na majanga kadhaa likiwepo hili la mafuriko napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote waliofikwa na mafuriko najua Mungu atasimama upande wao, janga hili ni muendelezo wa majanga mengi yaliyoikuta Tanzania yetu tunayoiota tutalalapo,,Ambikile Mwaisapile  maarufu kama babu wa loliondo  ni moja ya majanga hayo .

 Inayodaiwa kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeonyesha  madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu ilikuwa ni mradi, na kwa kweli kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa.

Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi mabaya, na ni sugu. Ndio, miongoni mwetu kuna wenye kusumbuliwa na maradhi ya unafiki. Nitatoa mfano  nilipata  kukaa na wasomi wawili, tena wana digrii zao. Tukazungumzia ya Babu wa Loliondo.

Mimi na wasomi wale tulikuwa na misimamo ya kufanana, tulipinga upotoshaji unaoendelea katika jamii kuwa Babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapile , anatibu ukimwi, kansa, kisukari na mengineyo. Na kwa vile wote tumekwenda shule, hoja kuu ilikuwa hii; kuwa hadi sasa hakuna hata wagonjwa watatu wa ukimwi waliothibitishwa kitaalamu kuwa wamepona ukimwi kwa dawa ya Babu. Badala yake, kuna wengi wamekufa baada ya kuacha kutumia madawa waliyoelekezwa na madaktari watalaamu waliosomea tiba.

Wakati tukiendelea kuzungumza, mara akatokea mheshimiwa fulani, naye akaingia moja kwa moja kwenye mjadala. Alimtetea Babu na kusisitiza kuwa Babu ni lulu ya taifa, lazima aenziwe. Wasomi wale afadhali wangekaa kimya, hapana, walianza kumuunga mkono mheshimiwa kwa hoja nyepesi.
Hawakuwa wapumbavu, walijifanya tu wapumbavu wakiniacha mimi nikipambana peke yangu kuziponda hoja za mheshimiwa yule. Kwa kiasi fulani, niliogopa kuona hulka hii ya wasomi wetu. Wasomi ambao, kwa unafiki, wanashindwa kutetea na kusimamia katika hoja zao za msingi. Na hii, bila shaka, ni moja ya majibu ya swali la kwa nini Tanzania ni masikini?

Hakika, ya Babu wa Loliondo ni aibu yetu kitaifa. Katika karne hii ya 21 nchi yetu inatumia raslimali zake kufanya promosheni ya ndoto ya Mtanzania mmoja kati ya Watanzania milioni 42! Ndio, tunafanya promosheni ya jambo lisilo na uthibitisho wa kisayansi. Si tuliona, haikupita siku bila kusikia habari za Babu wa Loliondo?

Kwa sasa, tunaweza kabisa kusema, kuwa habari za huduma za Babu wa Loliondo zilitangazwa na kuufikia umma kuliko habari za Wizara yeyote ile katika Serikali ya Awamu ya Nne. Babu wa Loliondo si mchezo bwana, alikuwa na ‘maafisa habari wake’ wanaowafunika hata maafisa habari wa Wizara za Serikali.

Na katika mzaha huu wa mambo ya msingi kitaifa, tuna maelfu kwa maelfu ya Watanzania wanaotaabika na hata baadhi kufa kwa kuamini kuwa Loliondo kuna tiba, na iko Loliondo tu! , kuna Watanzania walioweka rehani mavuno yao ya mwaka mzima ili wapate nauli ya kwenda kwa Babu. Si wameambiwa, kuwa hata mawaziri wanapanga foleni ya kwenda kupata kikombe cha Babu!
Na wakishapata kikombe wanapiga picha ya ukumbusho, au labda ya kisiasa. Asubuhi yake ’maafisa habari’ wa Babu wameshatundika picha ya waziri ukurasa wa kwanza gazetini! Jimboni kwa mheshimiwa wapiga kura wake watamwona au kusikia kuwa Mheshimiwa naye anaumwa kama sisi, na amepata kikombe cha Babu!

Kikombe cha Babu ni abrakadabra, nilipata kuandika hilo. Na Watanzania, baadhi, kwa hiyari yetu, tumekubali kujifanya, wajinga na hivyo kuwapumbaza wengi wengine. Kwanini? Tulitafute jibu kwa kufikiri kwa bidii.

Hebu jiulize; wakati Shirika la Afya Duniani (WHO), Juni mwaka huu, liliadhimisha miaka 30 ya mapambano dhidi ya ukimwi, je, Tanzania, kama nchi, tulikuwa na banda la maonyesho likielezea ugunduzi wa tiba ya ukimwi iliyotokana na ndoto ya Babu?!

Labda ndio maana, magazeti yetu ya lugha ya Kiingereza hayakufanya sana promosheni ya tiba ya Babu. Maana, kama habari za Babu zingepewa uzito kama ilivyo kwenye magazeti yetu ya lugha ya Kiswahili, basi, wana jumuiya ya Kimataifa, wakiwamo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, huenda wangeshindwa kuamini wanachokisoma.

Maana, wawakilishi wa mashirika kama PSI na FHI yenye miradi ya kupambana na ukimwi nchini na mengineyo wangejiuliza; nini hasa wanachokifanya katika nchi yetu. Na pengine wameshatafsiriwa tunachooandika juu ya Babu kwa Kiswahili chetu!

Si ajabu basi, Ubalozi wa Marekani ulikuja na tamko lake Mei 5 mwaka huu. Wamarekani hawa, kwa kuwaonea huruma Watanzania, wameshauri watu wanaotumia tiba mbadala wasiache kutumia dawa walizopewa na madakatri na vile vile waendelee kujikinga na maambukizi.

Na wakaweka msisitizo kuwa, kuacha kutumia dawa hizo za madaktari watalaamu kunafanya dawa hizo zinapotumiwa tena kushindwa kufanya kazi ipasavyo (drug resistance). Na ajabu ya habari ya tamko lile la Wamarekani ilichapishwa katika gazeti moja tu kwa lugha ya Kiingereza - The Citizen, jina la gazeti hilo lina maana ya Mwananchi; ingawa wananchi wengi hawakupata habari hiyo kwa lugha yao!

Kwa hakika, hatuhitaji kuambiwa na Wamarekani juu ya ukweli huu na wajibu wetu. Huu ni wakati kwa wizara inayohusika kufanya jitihada za dhati kutoa tamko litakaloweka bayana kuwa tiba inayodaiwa kutolewa na Babu bado haijathibitika kitalaamu kama inaponya maradhi sugu kama vile ukimwi, kansa na kisukari.

Wakati utafiti huo ukiendelea, umma ukumbushwe kuwa, dawa zinazotambulika kitalaamu kwa sasa ni zile zinazotolewa na madaktari wetu watalaamu. Kwamba wanaokwenda kwa Babu wana ruhusa ya kufanya hivyo, lakini, kikombe cha Babu kinaweza kunywewa pamoja na dawa za hospitalini.
Tufanye hivyo sasa, na ujumbe huo usambazwe kwa nguvu zote na maafisa wa habari wa wizara husika. Ndio, maofisa habari wa Wizara ya Afya nao washindane na ‘maafisa habari’ wa kujitolea wa Babu wa Loliondo!

Watanzania tunapita kwenye kipindi kigumu sana. Na huu ni wakati wa kutafakari kwa kina. Na nimepata kumwuliza jamaa yangu swali hili; mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani angetamka kuwa, angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri?

Haya ya kwa ‘Babu wa Loliondo’ ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, unahitaji mwanga.

Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu wakaoteshwa na Mungu juu ya dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndio, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa kiserikali.

Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo; maana, watakuwa wameufanyia utafiti. Nahitimisha.

Niwatakieni Heri ya Mwaka Mpya.
Maggid Mjengwa.

Reactions::

CCM ZANZIBAR WAFANYA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU

Rais wa zanzibar Mohamed Shein, Amani Karume(rais mstaafu) na Vuai Ali Vuai katika kikao hicho kilichofanyika Kisiwandui Unguja


Baadhi ya wajumbe
Picha na Ramadhan Othman IKULU YA ZANZIBAR
Reactions::

BALOZI SEFUE AAPISHWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI MPYA LEO

         Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo (kushoto) akimkabidhi nyaraka za serikali maalum kwa kuapishiwa na Biblia, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ili kuanza kuapishwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salam leo
      Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo
                    Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Reactions::

UBABE HUU MADEREVA WA MAGARI ACHENI

Reactions::

MWENZIO AKINYOLEWA .......

Reactions::

KIPANYA HUYU!

Reactions::

MAGAZETINI LEO





Reactions::

MEZA YA MAGAZETI LEO


Reactions::

Kauli Ya Ehud Barak Si Tu Ya Kuupuzwa, Bali...

Ndugu zangu,

Nimefuatilia michango ya waliotangulia. Nami mtazamo wangu ni huu; Kauli ya Ehud Barak si tu ya kupuuzwa. Bali, Tanzania , kama taifa, iliweke wazi hilila upuuzi wa Barak  kwa Serikali ya Israel na kwa njia za Kidiplomasia ili Israel kama nchi ielewe upuuzi uliotamkwa na Waziri wake. 

Ni kauli ya dharau kubwa kutoka kwa waziri wa taifa ambalo lingeweza kuwa jirani zetu  kama League of Nations ingeendelea na hoja ya kuwatafutia Waisrael  waliokuwa wakitangatanga duniani ardhi ya kujishikiza  baada ya Vita Kuu ya Dunia. Uganda ilikuwa tayari kutoa sehemu ya ardhi ya nchi yake kuwasitiri Wayahudi.

Kwa kutambua ukweli huu wa kihistoria na kauli hiyo ya Barak. Hivyo basi,Tanzania iitake  Israel  ituombe radhi. Kinyume cha hapo, Tanzania ina uwezo  wa kupambana na kushinda  kwenye vita vya Kidiplomasia dhidi ya Israel. Na nia na sababu za kufanya hivyo tutakuwa tunazo. Ndipo hapo ndipo Israel itatambua kuwa Tanzania is  relevant.

 
Nawasilisha.
 
Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.
Desemba 31, 2011
Reactions::

RAIS KIKWETE AKIWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI MSTAAFU NA MPYA

  Rais Jakaya Kikwete akiongea na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Mh Philemon Luhanjo (kulia) na Katibu Mkuu kiongozi mteule Balozi Ombeni Sefue ofisini kwake Ikulu Dar es salaam Ijumaa usiku mara baada ya kufanya uteuzi huo
Picha na IKULU
Reactions::

Boko Haram washambulia msikiti Nigeria

 Boko Haram wameelekeza mashambulizi misikitini
Mlipuko mkubwa umetokea karibu na msikiti katika mji wa Maiduguri, kaskazini mwa Nigeria, ambapo watu kadhaa wameripotiwa kuuwawa.
Walioshuhudia wanasema wameona miili ya watu wanne waliouwawa.
Msemaji wa jeshi la Nigeria akizungumza na BBC amelaumu kundi la Kiislamu la Boko Haram kwa shambulizi hilo.
Kundi hilo ambalo limekuwa likitaka kulazimisha kuwepo utawala wa sharia nchini Nigeria, limeendesha mashambulizi kadhaa, zaidi kaskazini mashariki mwa nchi.
Limekiri kufanya mashambulizi kadhaa siku ya krisimasi yaliyolenga makanisa, na yaliyouwa watu wasiopungua 42.
Kundi la Boko Haram katika siku zilizopita pia limeshafanya mashambulizi dhidi ya mashirika ya kimataifa, na pia dhidi ya viongozi wa Kiislamu wa madhehebu yanayolipinga.
Msemaji wa Jeshi alisema lilikuwa shambulizi baya lakini hakueleza idadi ya watu walioathirika.
Maelfu ya watu wametoroka makwao mjini Maiduguri na miji mingine iliyoshambuliwa na Boko Haram.
Siku ya Alhamisi Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan aliwaita wakuu wa jeshi kwenye mkutano kujadili namna ya kukabiliana na tishio la Boko Haram.
Viongozi wa Chad na Cameroon, ambazo ziko karibu na Maiduguri wameripotiwa kufanya mazungumzo kuhusu namna wanavyoweza kusaidia kuzuia kuenea kwa ghasia zinazosababishwa na kundi hilo ndani ya mipaka yao.
Kundi hilo, ambalo shina lake ni mjini Maiduguri, mwaka huu lilifanya mashambulizi ya kujitoa muhanga kwenye makao makuu ya umoja wa mataifa na makao makuu ya Jeshi la Polisi katika mji mkuu Abuja.
Pia lilihusika na mashambulizi kadhaa ya mabomu katika mji wa Jos , kati kati mwa Nigeria, katika mkesha wa Krisimasi mwaka 2012, na vile vile mashambulizi kwenye kituo cha kijeshi mjini Abuja katika mkesha wa mwaka mpya 2011.
Source:BBC
Reactions::

ttcl watoa misaada mafuriko dar

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (katikati) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kulia) wakimkabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ilala Bw. Mwasabite Elioth kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko.(picha na TTCL)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (katikati) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kulia) wakimkabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ilala Bw. Mwasabite Elioth kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko
Baadhi ya Maofisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL wakiwa katika piocha ya pamoja na watoto yatima baada ya kuwapa vyakula mbalimbali kwa msimu huu wa sikukuuu.(picha na TTCL)
Reactions::

Halima nae Ngahyoma.(shairi)

Mola twakushukuru, kwahii yako rehema,

Mola wewe ni nuru, Mja wetu wa Karima

Mola umetunusuru, kwa nyingi dhahama.

Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.



Mola upe amani Halima, dada yetu maridhawa

Mola umpumzishe daima, mtangazaji wa dawa,

Mola ulimpa rehema, mpirani alikuwa muruwa,

Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.



Ulipomwita Ngahyoma, hakusita kuitika,

Leo katuacha nyuma, nyumbani na Afirika,

Sikioni bado vuma, utangazaji wake hakika,

Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.



Pole wanahabari, Tanzania na dunia,

Msijione wahatari, Mola anapowachagua,

Tujipange misitari, ibadani kuwaombea,

Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.



Kazi ya mola timilifu, daima haina makosa,

Tuwahifadhi nadhifu, tusamehe waliokosa,

Mavazi yawe ya sufu, tuwavishe wao sasa,

Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.



Wanalia wanafamilia, Wahalima na Ngahyoma,

Wahariri wanawalilia, hakika imewachoma,

TBC na BBC walia, wapendwa wametuhama,

Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.



Majonzi yamenifika, Mroki nagugumia,

Moyo imenishtuka, habari ziliponifikia,

Hakika tutawakumbuka, Halima na Ngahyoma,



Kaditama natamatia, Mroki nawakimbia,

Mola atawakumbatia, wafiwa nawaambia,

Hakika nitawafuatia, Mola ataponiambia,

Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.



Mroki Mroki “Father Kidevu”

mrokim@gmail.com

0755373999/0717002303

UKONGA-DAR ES SALAAM
Reactions::

Ideas For New Years Resolutions

 Body and Health
1. Eat more fruits and vegetables everyday. Make it a goal to add at least three
2. Join a health club and go at least 3 times a week
3. Build muscle. Remember, each pound of muscle burns an extra 40 calories a day while at rest!
4. Get regular doctors visits, exams, and physicals
5. Stop smoking, or smoke less
6. Take the stairs instead of the elevator, park further away
7. Get at least 8 hours of sleep each night
8. Limit your sugar and fatty food intake
Family and Relationships
1. Be a more attentive parent, spouse, or friend
2. Spend more time with your loved ones
3. Make people laugh
4. Be more supportive of your childrens dreams
5. Bond with a family member that you don't see often
6. Have family night at least once a week
7. Have date night with your partner or spouse at least once a week
Career, Education, and Finance
1. Save 10% of your income (or whatever percent is good for your financial situation)
2. But less needless stuff
3. Devise a savings plan so that you can buy something important
4. Save money by doing things yourself rather than hiring someone
5. Create a budget and stick to it
6. Vow to learn at least one new thing each day
7. Further your education
8. Improve your business or career status
9. Make a new career or educational move
10. Redevote yourself to your career
Fun
1. Take a few vacations and weekend trips
2. Take up a new hobby
3. Start a club or organization
4. Meditate
5. Volunteer or donate to a charity or good cause
6. Take time for yourself
7. Smile more often (it really is contagious)
8. Have spa days
Misc.
1. Keep your car, office, and home cleaner
2. Swear/curse less
3. Finish something you started
4. Start a garden
5. Drive safer
6. Watch less television
7. Set goals, put them in writing, and go for it!

Article Source: http://EzineArticles.com/3488979
Reactions::

VODACOM YAWAKUMBUKA MAREHEMU BI MCHUKA NA NGAHYOMA




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Vodacom yatoa pole vifo vya wanahabari Marehemu Halima Mchuka
na John Ngahyoma.

Dar es salaam Disemba 30, 2011. Kampuni ya simu ya mawasiliano
ya Vodacom imepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za vifo vya
wanahabari nguli nchini Bi. Halima Mchuka na Bw. John Ngahyoma.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, wanahabari hao wamefariki kwa siku
tofauti akianza Halima juzi na baadae Ngahyoma aliyefariki asubuhi ya leo
wote jijini Dar es salaam.

“Tunatoa mkono wa pole kwa familia za marehemu, waajiri wao na kipekee
familia ya wanahabari nchini kwa kuondokewa na wapendwa wetu ambao
walikuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa tasnia ya habari na utangazaji
nchini.”Alisema Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania
Bi. Mwamvita Makamba

Marehemu Bi. Halima Mchuka alikuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji
Tanzania – TBC na Marehemu Bw. John Ngahyoma hadi umauti unamkuta
alikuwa ni mwanahabari wa Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC Ofisi ya
Tanzania.

Marehemu wote wawili watakumbukwa kwa jinsi ambavyo walikuwa mahiri
katika tasnia ya habari na utangazaji kwamba mchango wao utaendelea
kuwa chachu hasa kwa vizazi vijavyo vya wanahabari chipukizi nchini.

“Tutamkumbuka sana Marehemu Halima ambae rekodi zinaonyesha kuwa ni
mtangazaji wa kwanza mwanamke kutangaza mpira. Marehemu Ngahyoma
kwa upande wake ni sehemu ya watangazaji wa awali kabisa wa televisheni
Tanzania Bara mwanzoni mwa miaka ya tisini”Alisema Mwamvita.

Mwamvita amesema kampuni ya Vodacom daima ina thamini na kuheshimu
mchango wa wanahabari katika maendeleo ya taifa na ushamirishaji ustawi
wa jamii

Mungu azilaze roho za Marehemu Bi Halima Mchuka na Bw. John
Ngahyoma mahali pema peponi - Amen
Reactions::

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika hospitali ya Hydom ya kukagua miradi ya maendeleo 30/12/2011

  .mbele Mganga Mkuu wa Hospitali ya Hydom akimuongoza Mkuu wa mkoa wa Manyara(Mh.Elaston Mbwilo ) kumuonyesha miradi mbalimbali ya maendeleo katika Hospitali maalum ya HYDOM
                    Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Hydom bw. Emanuel akitoa maelekezo mbalimbali juu mradi wa ujenzi wa jengo la kinamama ,wa kwanza kushoto  ni Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh.Anatory Choya  akiteta jambo  na Mkuu wa Mkoa
                                      .Kutoka kulia muuguzi mkuu ndugu Emanuel akitoa maelezo juu ya ujenzi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya Hydom ,anayefuata kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa hospitali Dr.Naaman 
Na Sunday Morab
Reactions::

Tunauaga mwaka 2011 bila mafanikio katika michezo


LEO ni siku ya mwisho wa mwaka 2011. Siku hii inatukumbusha nini tulifanya mwaka huu kabla ya kuanza mwaka 2012.Tunafahamu katika mwaka huu wa 2011 tulipata mafanikio kidogo sana katika michezo hali ambayo imekuwa ikijitokeza kila mwaka na Tanzania tumekuwa tukichukilia hali hiyo kama hali ya kawaida.

Tunasema hivyo kwa sababu ya kutofanyia kazi mapungufu yanayojitokeza kila mwaka ambayo ndio kiini cha sekta ya michezo kushindwa kufanikiwa.

Kamwe hatutaweza kuendelea katika michezo kama hatutakubali kufanyia kazi chanzo cha matatizo yanayokwanza kupatikana kwa mafanikio katika michezo kwa jumla.Athari kubwa ya kudumaa kwa michezo nchini imeshawateka mashabiki na wapenzi wa michezo hasa soka ambao wamehamishia ushabiki wao nchi za Ulaya hasa England na Hispania.

Hatufurahii hata kidogo uzembe uliopo katika kusimamia michezo nchini hali inayosababisha kupata wanamichezo wenye viwango vya chini na kupata mafanikio duni katika mashindano ya kimataifa.

Ukiangalia ushiriki wa wanamichezo wetu mwaka huu katika mashindano ya kimataifa utagundua kwa kiasi kikubwa tulifanya vibaya.Bado vichwa vya habari kama  "ngumi watembeza bakuli","Udhamini wakwamisha ligi ya kikapu","Soka yapoteza dira", na vingine vingi vya aina hiyo vilikuwa ni 'ujumbe' uliotawala vyombo vya habari mwaka huu.

Vichwa vya habari kadhaa vinaonyesha picha jinsi michezo yetu ilivyokuwa katika mwaka huu, ambapo kesho tunaanza mwaka mpya huku ikitarajiwa kwa kiasi kikubwa hali hiyo ya vichwa vya habari vya kusikitisha kuhusu michezo yetu kuendelea kutawala.

Mara nyingi wachambuzi wa habari za michezo katika gazeti hili wamekuwa wakizungumzia umuhimu wa uboreshwaji wa sera yetu ya michezo, uboreshwaji wa miundombinu ya michezo (shule maalum za michezo na viwanja), uwekezaji katika michezo na wanamichezo kuandaliwa.

Lakini, mwaka unamalizika bila mabadiliko yoyote katika mambo hayo wakati sehemu yoyote utakayokwenda ulimwenguni, hawezi kuikimbia michezo.Ni wale tu wasiojua faida za michezo ndio watakaothubutu kujitenga nayo.

Wakati mwingine tunafikiria kwamba viongozi wa michezo wameingia madarakani bila kuwa na uzoefu na mambo ya michezo na kwa sababu hiyo siku zote wamekuwa wakitanguliza maslahi binafisi mbele.

Inashangaza mwaka huu kupita Tanzania ikiambulia medali moja ya Shaba pamoja na kushiriki michezo mbalimbali ya kimataifa kama  soka kwa wanawake, Netiboli, Ngumi, Riadha, Paralimpiki na Judo na bado viongozi wake wamekaa kimya.

Pia haiwezekani kuona mwaka huu tumeshiriki katika mashindano ya Jumuiya ya Madola, mashindano ya dunia ya riadha na kutoka bila medali halafu halafu viongozi wa michezo wakae kimya na sisi tukae kimya.

Vilevile haiwezekani kukubali tushiriki bila mafanikio mashindano ya Chalenji ya kikapu, mashindano ya Kanda ya Tano Afrika ya kikapu, mashindano ya Kombe la Kagame katika soka, mashindano ya Ligi ya Mabingwa, mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, tutolewe katika kuwania kufuzu kushiriki fainali za Mataifa 2012, halafu viongozi waone hali hiyo ni kawaida.

Lazima tuelewe mamilioni ya watu duniani wanategemea michezo kuendesha maisha yao, ambapo bila wanasiasa au serikali kuisapoti michezo nchini au makampuni kujitokeza na kuwekeza kwenye michezo, viongozi wa michezo kutimiza wajibu wao na wananchi kukubali kusaidia na kufanikisha, hatuwezi kuona mabadiliko.

Ni wazi tunatakiwa tukubali wachezaji nyota katika mchezo wowote huandaliwa, lakini kwetu mwaka unakwisha tukiwa hatuna dira wala mikakati ya mwaka 2011.

Ukweli ni kwamba ni lazima tujipange na kutekeleza kwa vitendo mikakati yote iliyoainishwa kama kichocheo cha kukuza michezo nchini. Tutakuwa tunadanganya umma wa wapenda michezo iwapo hatutakuwa tayari kufanya mageuzi. 
Source:Mwananchi
Reactions::

SIASA 2011:Ilikuwa vita ya Chadema, CCM (gazeti mwananchi)

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa

 MWAKA 2011 unamalizika leo na kuacha kumbukumbu ambazo ni vigumu kusahaulika katika medani za siasa nchini, huku baadhi ya vigogo wa kisiasa wakiweka historia kutokana na kukumbwa na matukio ya aina yake.
Katika miezi 12 iliyopita, Taifa limepita katika misukosuko mingi ya kisiasa iliyoanzia Januari 5, pale maadamano ya Chadema yaliyofanyika mjini Arusha yaliposababisha vifo vya watu wanne.

Hilo ni miongoni mwa matukio mengi ya kisiasa ambayo yalikuwa na sura ya mvutano baina ya vyama vya CCM na Chadema, ambavyo hivi sasa vinatoa mwelekeo wa siasa za nchi.

Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano hayo, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta Jenerali Saidi Mwema ambaye awali alipiga marufuku maandamano hayo kwa madai ya kuwepo uwezekano wa kutokea vurugu.Soma habari yote www.mwananchi.co.tz

Reactions::

Kumekucha Udzungwa!

Reactions::

Kaa Chonjo; Udzungwa Express!


Reactions::

Friday, December 30, 2011

' Mwenyekiti' Wenu Niko Bagamoyo!


 Ndugu zangu,
Nimeingia leo jioni nikiwa na makamanda wangu na mama yao. Usiku tumetembea kwa miguu kutoka tulikofikia hadi Soko Kuu. Hapo tulipata mlo mwanana wa usiku ulioandaliwa na Bibi Lishe. Yaani, wali wa nazi na maharage ya nazi. Na kisamvu juu. Vyote vya moto. Bei? Shilingi elfu moja na mia mbili kwa sahani.Tafsiri yake? Maisha bado ni magumu sana kwa mtu wa kawaida. Kwa bei hiyo bibi yangu yule hawezi kutengeneza faida kubwa kwa kazi ngumu anayoifanya. Vinginevyo? Bagamoyo inakua na bado ni tulivu.
Usiku mwema.
Maggid,
Bagamoyo.
Reactions::

Mrithi wa Luhanjo ni Balozi Sefue


 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Ombeni Yohana Sefue kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Balozi Sefue anachukua nafasi inayoachwa wazi na Bwana Phillemon Luhanjo ambaye anahitimisha mkataba wake wa utumishi wa umma kesho, Jumamosi, Desemba 31, 2011.

Kabla ya uteuzi wake, Balozi Sefue alikuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Kabla ya hapo, Balozi Sefue alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada tokea Oktoba 2005.

Balozi Sefue ataapishwa kesho, Jumamosi, Desemba 31, 2011 saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Reactions::

Wadau Vipi Hapo Tukitumia Majina Kama Haya Kwenye Nyumba Za kufikia Wageni(Wenyeji) Tanzania Bila......Itawezekana tu

Reactions::

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUJIUZULU KWA KIBANDA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI, NA MICHEZO
Simu: 022 - 2123947
022 - 2123931
E-mail: km@hum.go.tz
Website: www.hum.go.tz.
Holland House,
Mtaa wa Samora,
S.L.P. 8031,
DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUJIUZURU KWA BW. ABSALOM KIBANDA KAMA MJUMBE WA KAMATI YA
TAIFA YA MCHAKATO WA KUPATA VAZI LA TAIFA

Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea kwa masikitiko taarifa
iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free
Media Bw. Absalom Kibanda ya kujitoa kwenye Kamati ya Taifa ya kukamilisha
mchakato wa kupata vazi la Taifa, Wizara haina pingamizi na uamuzi wake huo.

Wizara imesikitishwa na sehemu ya tamko lake kudai kuwa namnukuu,

“Nimelazimika kufikia uamuzi huu, baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba
mchakato mzima uliohusisha sakata langu kama Mhariri Mtendaji kuhojiwa na
kufunguliwa mashitaka na Polisi na hatimaye kufikishwa kwangu Mahakamani
usingeweza kufikiwa pasipo kuishirikisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo inayoongozwa na Waziri Nchimbi”, mwisho wa nukuu.

Kwa taarifa hii Wizara inapenda kuutarifu umma kuwa Habari hiyo ni uzushi usio
na mashiko wenye nia ya kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya Wizara na wadau
wa Habari nchini.

Kwa mujibu wa majukumu ya Wizara, si sehemu ya kazi za wizara hii
kushauri, kuchunguza au kuandaa tuhuma za makosa ya jinai. Ni vema iwe
wazi kuwa Wizara hii, viongozi , watendaji, na watumishi wake hawajashiriki,
hawajashirikishwa na hawajajishirikisha na hawajashauri wala kushauriwa juu ya
tuhuma na mashitaka dhidi ya Bw. Kibanda.

Wizara inavisihi vyombo vya Habari kuendelea kuzingatia weledi, mila na desturi
zetu katika kutekeleza majukumu yake.

Imetolewa na,

Msemaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Tarehe 29/12/2011.
Reactions::

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TBC HALIMA MCHUKA LEO

                Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa TBC marehemu Halima Mchuka leo jijini Dar es salaam katika makaburi ya Msasani.
                    Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiwekwa katika makao ya kudumu katika makaburi ya Msasani leo jijini Dar es salaam.
                       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu umezikwa leo katika makaburi ya Msasani jijini Dar es salaam.
                    Baadhi ya ndugu na watoto wa marehemu  wakiuombea dua mwili wa marehemu Halima Mchuka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Na Aron Msigwa MAELEZO
Reactions::

JOHN NGAHYOMA WA BBC AFARIKI DUNIA



Tumepata taarifa kwamba Mwandishi wa Habari mkongwe nchini ambaye alikuwa akifanya kazi na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), John Ngahyoma amefariki dunia leo asubuhi.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tabata, karibu na nyumbani kwa Marehemu Danny Mwakiteleko. Mwenye taarifa zaidi atufahamishe.

Tunaitakia moyo wa subira na Mungu awafariji wanafamilia wa Ngahyoma katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.

RIP John Ngahyoma, umetangulia na wengine tutafuata.
Reactions::