Subscribe:

Thursday, February 02, 2012

Hata Kaburini, Mwalimu Bado Anatusikitikia

( Pichani Mwalimu akiwa Mbeya mwaka 1963. Wengine ni Kaunda na Kawawa. Picha ya maktaba yangu)
Reactions::

14 comments:

Anonymous said...

Mjengwa wala hujakosea, kwa hali ya sasa ya serikali yetu. Nyerere huko halipo analia sana. Mfano issue ya Posho za wabunge,Inakuaje serikali moja chama kimoja lakini inatofautiana kauli? Rais anasema vile, msaidizi aliyemteua yeye mwenyewe(waziri mkuu) anasema vingine. Spika wa bunge anasema posho tushaanza kulipana siku nyingi. Je wanaweza kulipana bila Ofisi ya Raisi kubaliki? Je aliyesema kwamba rais amesharidhaia(Pinda),je alikua mwongo? Je nae Pinda anaridhika kurukwa kimanga na ofisi ya rais?Kama rais hakumwagiza pinda inatakiwa hamtimue kazi.

Pili CCM inasema hakijaridhia posho, lakini ni wabunge wake ndio wako mstari wa mbele kudai hizo posho, je kinashindwa vipi kuwachukulia hatua, au inawaogopa?Nahisi hapa kuna sarakasi zinapigwa huku watu wakiendelea kula posho mpya. Huku wananchi wakifa kwa kukosa huduma mzuri za afya.

Anonymous said...

nyerere ndio alikua ovyo kbs ktk miaka 25 yake ya utawala

Anonymous said...

Picha hii ilipopigwa uchumi wa Tanzania ulikuwa sawa na wa Korea Kusini na Singapore, lakini thanks to 'Baba wa Taifa' leo Tanzania imezama katika lindi la umaskini wa kutisha huku kukiwa hakuna dalili yoyote kama itaweza kujikwamua hivi karibuni.

Anonymous said...

ma anon wa mwisho nyote mnayajua mambo kweli hii nchi huyo ndo kaiangamiza kakuta watu walikuwa wanauza mazao yao wanasomesha watoto yeye akasema eti ukabila kumbe ilitakiwa na wengine waige huo mfano,hakuna lolotea analo tulilia yeye alijitengenezea mazingira ya kuishi vyema na kuabudiwa halafu alikuwa mkabila vilevile ndio maana wakuu wa majeshi wengi wanatoka mkoa wa mara kula bure kulala bure

Anonymous said...

Kambarage was our very own Kim Jong-il.

Jaribu said...

Naona wanafunzi wa shule za kata mmeamka. Tanzania ilikuwa sawa na Korea Kusini au Singapore, my foot! Here is another nugget. Mwanzoni wa karne ya kumi na tisa, uchumi wa Tanzania ulikuwa sawa na Marekani kwa sababu Industrial Revolution ilianza Uingereza. I suppose na hiyo tumlaumu Nyerere kwa kufanya Marekani ituache mbali.

Toka Nyerere aache madaraka mpaka leo imepita miaka 26 na wengine mnaopayuka hapa mlikuwa hata hamjazaliwa. Lakini ndio Nyerere amewafanya wavivu, wazembe, wezi wala rushwa mnaowapigia kura viongozi vilaza, wavivu, wazembe, wezi na wala rushwa. Nyie endeleeni kucheza bao na snookers huku mnalaumu marehemu kwa mapungufu yenu. Labda baada ya miaka mia tano mtakuwa sawa na Korea Kusini, assuming nao watakuwa wanacheza bao na snookers wakati wakiwasubiri.

Anonymous said...

Wadau, msinielewe vibaya. Nilimpenda sana na bado ninamuheshimu sana Baba wa taifa. Lakini naona angelitusikitikia Watanzania wakati tulipokuwa tunasoma kati ya 1982 na 1985 wakati tulikuwa tunaamshwa saa 11 asubuhi kwenda kupanga foleni ya unga, sukari, mafuta ya kupikia na sabuni. Ikifika saa 12 kasorobo asubuhi unaambiwa kila kitu kimekwisha. Sitaki kuongea kuhusu kina James Mapalala (wa kijijini kwetu)na watu wengine waliotiwa kizuizini bila kufikishwa mahakamani ambao hawakusikitikiwa. Najua watu wengi wanaosoma blog hii walizaliwa baada ya 1985, kwa hivyo kuna haja ya wao kujua historia ya nchi yetu ili wajue kuwa Mwalimu (kama vile Kinjeketile) alikuwa ni binaadamu mwenye nia nzuri sana na mazuri mengi lakini pia na mapungufu yake.

Anonymous said...

nyinyi wadau sisi wengine tumesoma enzi za mwlm lakini naye alichemsha haiwezakani binadamu nyote mlingane ila kwa wale watakao kuwa mbele ndo watawavuta wa nyuma kama mipango imewekwa vizuri

Anonymous said...

Matatizo yote yanayotukumba Watanzania wakati huu mizizi yake iko katika utawala wa kidikteta wa Nyerere, period.

Anonymous said...

Mwenyekiti, huwa napatwa na hasira kali sana kila nikiona picha ya Nyerere humu, na hakuna kinachonikera kama kumbukumbu ya mateso makubwa tuliopata kutokana na his reckless and foolish military adventurism in Uganda. Huduma za jamii zilikufa kutokana na fedha nyingi kutumika katika kufanikisha obsession yake ya kumng'oa Idi Amin na hatimaye kuikalia Uganda kwa miaka kadhaa. Tanzania will go down in history as the poorest country to have occupied another country. Hizi ndizo 'fikra sahihi za Baba wa Taifa'.

Jaribu said...

Hamna lolote, matatizo yanayokumba Watanzania mizizi yake iko katika watawala vilaza waliomrithi Nyerere. Mbona wakoloni walitawala Tanzania toka enzi za Wajerumani mpaka Waingereza walipoondoka ilikuwa zaidi ya utawala wa Waingereza ilikuwa zaidi ya miaka 25 ya Nyerere? Je Watanzania ni wachapa kazi kama Wajerumani au Waingereza? Hardly.

Nyerere was no saint, lakini hao wakina Dowans are much worse.

Anonymous said...

Hapa we should not compare Nyerere with anybody. Tunachotakiwa kufanya ni kumpima as an individual.

Jiniaaz! Popkorn said...

This is nothing but sheer propaganda by the current ruling party and givt. leadership. Due to their incompetence of the highest degree they have absolutely failed to rescue the economy and social services of our motherland. In person, I give some credit to Mzee Rukhsa - he did his best, to tell the truth!

These thugs have now decided to hide all their shortcomings behind the back of the late Nyerere.

Ok, let's say, yes it is Nyerere, ... so what?? Yees, you know the mistake - go on and correct it for you are at the disposal of all resources and state machineries required to run a country. Wake up and act, youuuu 'makatibu kata'. Identifying a problem and pointing a finger to a defunct person doesn't sort it out. You vied for running the government in order to fullfill your promises of alleviating poverty in the country. Now that your dreams are far from reality, and realising that problems are outbalancing your capabilities - you are busy looking for reasons for sympathy.

No one will listen to your excuses! And let the public realise how incompetent you are, kudaaadek! What a government!! Shame on you! Only in Bongo the state hates its leaders with positive ideas.

I salute you Jaribu, what you said nothing but truth!!!

Jiniaaz! Popkorn

Jaribu said...

Thanks, Jiniaz. With our ruling "geniuses", they only thing they can run is their mouths, not a country.

Post a Comment