Kuna watembeleaji 576  wapo online

LIVE - Kwanza Jamii radio

Magazeti ya Leo

Kwa habari na mambo ya kijamii, siasa, biashara, uchumi, michezo nk, sikiliza LIVE kwanza Radio.

 

 

Matangazo Mapya

Azania Bank Limited is the first indigenous private bank, formerly kno ...

Magazeti Leo Jumapili

Published in Jamii

Mwenyekiti Wenu Kinamtosha Hiki..!

Published in Jamii

1_5244f.jpg


Ugali kwa tembele, uyoga kwa mbali, nyanya chungu, nyanya maji, bamia na pilipili shamba..
Usiku Mwema.

Soko Kuu Iringa Leo Jioni..

Published in Jamii

1_8aa8e.jpg

Mgeni Siku Ya Kwanza..!

Published in Jamii

1_fceba.jpg


Jacqueline Muro kwenye studio za Kwanza Jamii. Kulia ni mwenyeji wake, Victor Simon wa Kwanza Jamii Radio/Mjengwablog.com

MBUNGE JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA

Published in Jamii

11018982_10204955727345677_8410184730571474681_n_9e63e.jpg

John Komba Nilimwona Kwa Mara Ya Kwanza Mwaka 1981..

Ndugu zangu,

Nimepokea kwa masikitiko habari za kifo cha ghafla cha msanii mhamasishaji John Komba.

Nilikuwa kijana mdogo sana nilipomwona kwa mara ya kwanza John Komba akitumbuiza ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa mwaka 1981.

Nilimwona John Komba na kikundi chake cha Kwaya ya JKT Mgulani. Alikuwa kijana mwembamba. Alikuwa mwanzoni kabisa mwa nyota yake kuanza kung'aa kuwarithi wasanii wahamasishaji wa tangu enzi za TANU, akina Mzee Makongoro na Chalamila.

Hata kwa masikio ya utotoni, nilimwona John Komba mwenye nyota itakayong'aa zaidi. Tungo zake zilivutia, sauti yake pia.

Bila shaka, John Komba ni msanii aliyekisaidia sana Chama Cha Mapinduzi katika kueneza jumbe zake.

Mfano, miaka ile ya 80, CCM, kwenye moja ya mikutano mikuu ya CCM, vijana waliombwa na chama chao kujitokeza kwenye kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za wilayani.

Ni John Komba aliyeufikisha ujumbe huo vema kabisa kwa tungo ambayo bado naikumbuka, aliimba:
" Vijana wanaombwa, waende wilayani, kwenye vikao vya chama vya utendaji wilaya".

Kwa bara la Afrika, ilipata kutokea, miaka ile ya 80, kwa kikao cha OAU kuvunjika. John Komba akaimba kwa masikitiko:

" Haijatokea hata siku moja, kikao OAU kikaja vunjika!" kisha kuziasa nchi kuendelea kiimarisha OAU.

Hakika, kuna wa kizazi changu, ambao tumekua tukizisikiliza, kuhamasika na kujifunza kwa tungo za John Komba.
Tutakukumbuka, John Komba.

Maggid Mjengwa,
Iringa.

TANZIA MBUNGE JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA

Published in Jamii

komba_61a05.jpg

Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.

Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.

"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu.

Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.

Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.

Eatv imewatafuta Afisa habari wa Ofisi ya Bunge ndugu Owen Mwandumbya, Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Elimu kwa umma bwana Jesse Mwakasyuka na katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila bila mafanikio kwa kuwa hawakupokea simu.

WAVAMIZI NA WAMILIKI WA ardhi KUKIONA...

Published in Jamii

Ardhi_-_1_22a27.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Alphayo Kidata (kulia) bakitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu linaloendelea katika Manispaa ya Kinondoni jana jijini la Dar es salaam.Kulia ni Muhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Baraka Mkuya

Ardhi_-_2_1c6b6.jpg

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bw. Alphayo Kidata (hayupo pichani) alipokuwa akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa kwa wananchi waliovamia maeneo yanayomilikiwa kisheria na watu wengine katika manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es salaam

Ardhi_-_3a_9af2b.jpg

Moja ya ukuta uliojengwa kinyume cha sheria katika eneo lisiloruhusiwa eneo la Tegeta ukibomolewa jana.

Ardhi_-_4_2e1c3.jpg

Baadhi ya wananchi katika manispaa ya Kinondoni wakiondoa bidhaa zo katika maduka eneo la Tegeta Machakani kupisha zoezi la bomoa bomoa kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.

Ardhi_-_5_d1456.jpg

Fundi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) akiendelea na zoezi la kukata umeme eneo la Mikocheni B kufuatia zoezi la bomoa bomoa lililokuwa likiendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Manispaa ya Kinondoni, jana jijini Dar es salaam.

Ardhi_-_6_24728.jpg

Tingatinga likiendelea kubomoa maduka eneo la Tegeta Machakani kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.

Ardhi_-_7_1_9a4f0.jpg

Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi wakati wa zoezi la bomoa bomoa maeneo ya wazi na yale yaliyochukuliwa kinyume cha sheria kutoka kwa wananchi wanaoyamiliki kihalali eneo la Mikocheni na Tegeta jijini Dar es salaam.

WAVAMIZI NA WAMILIKI WA ARDHI KINYUME CHA SHERIA JIJINI DAR KUKIONA, KUKUMBWA NA BOMOA BOMOA.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO, Dar es salaam.

28/2/2015. Dar es salaam.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa itaendelea na zoezi la kuvunja nyumba zilizojengwa katika maeneo ya wazi na yale yaliyochukuliwa kwa nguvu kinyume cha sheria kutoka kwa wananchi wanaoyamiliki kihalali katika maeneo mbalimbali nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Alphayo Kidata alipokuwa akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu linaloendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini la Dar es salaam.

Alisema kuwa wizara imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambao maeneo yao yamevamiwa na watu wengine kinyume cha sheria ambayo wao wanayoyamiliki kihalali.

Alieleza kuwa kutumia kanuni na taratibu zinazosimamia umiliki na matumizi ya ardhi nchini wizara hiyo itaendelea kuchukua hatua na kuyabaini maeneo yote yenye migogoro inayosababishwa na baadhi ya wananchi wasio na nyaraka halali za umiliki kisheria kuingia kwenye viwanja vya wananchi.

"Sisi kama wizara tumekubaliana kuwa zoezi hili litakuwa endelevu, wale wote waliovamia maeneo ambayo sio yao yakiwemo maeneo ya wajane na kujenga majengo yao Serikali itayabomoa kwa nguvu hata kama wamejenga maghorofa na Hoteli" Amesisitiza.

Alisema kwa muda mrefu pamekuwa na wimbi kubwa la migogoro ya ardhi inayosababishwa na tabia ya wananchi wasio na nyaraka kisheria kuingia kwenye viwanja vya watu wengine wenye hati za kumiliki ardhi kihalali na kuviendeleza kiuvamizi pasipokuwa na vibali vyovyote vya ujenzi.

Bw. Kidata alibainisha kuwa vitendo wanavyofanya wananchi hao ni kosa la jinai na kinyume cha sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu namba 175(1) kinachozuia mwananchi yeyote kuingia na kuendeleza kwenye ardhi asiyoimiliki kisheria.

Alisisitiza kuwa hakuna raia yeyote wa Tanzania aliye juu ya sheria hivyo watanzania bila kujali hali walizo nazo wanao wajibu wa kutii na kufuata sheria za nchi zinazosimamia sekta ya ardhi na kuongeza kuwa Serikali haitamvumilia yeyote atakayeendesha vitendo vya kuhujumu maeneo ya wazi, kujenga kuta katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuvamia maeneo ya hidhadhi ya Bahari.

Kwa upande wake Muhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya ambaye zoezi hilo lilifanyika katika manispaa anayoisimamia ameeleza kuwa awamu ya tatu ya zoezi la bomoa bomoa katika manispaa hiyo limehusisha ubomoaji wa kuta, majengo na maduka katika maeneo ya tofauti ya kata Mikocheni B na Tegeta.

Aliongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maenedeleo kwa kushirikiana na manispaa ya Kinondoni na vyombo vya ulinzi na usalama itaendelea na zoezi hilo ili kusimamia sheria za nchi kutokana na baadhi ya wananchi kwa makusudi kuendesha vitendo vya hujuma na vurugu miongoni mwa jamii.

"Kwa upande wetu kama manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara na vyombo vya ulinzi na usalama, tutalifanya zoezi hili kuwa endelevu ili tuweze kuondoa kabisa migogoro ya ardhi katika manispaa yetu" Alisisitiza.

MWISHO.

Mafuriko yawaua watu 14 Madagascar

Published in Jamii

Watu 14 wameuawa kwenye mafuriko nchini Madagascar ambapo pia wengine 20,000 wamelazimika kuhama makwao.

Mafuriko hayo yaliukumba mji mkuu Antananarivo na maeneo yaliyo karibu.

Utawala unasema kuwa mvua nyingi siku zijazo huenda ikasababisha madhara zaidi.

Mvua kubwa imenyesha nchini humo kwa takriban wiki mbili.

Mwezi uliopita kimbunga Chedza kiliwaua watu 80 nchini Madagascar. CHANZO: BBC

Van Gaal:Man U haina mshambuliaji mzuri

Published in Michezo

Kilabu ya Manchester United haiwezi kushinda taji la ligi kwa kuwa haina mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga mabao 20 kwa msimu.

Meneja Luois Van Gaal amesema kuwa mshambuliaji mwenye mabao mengi katika klabu hiyo ni Van Persie mwenye mabao 10 pekee ikilinganishwa na Diego Costa na Sergio Aguerro ambao wamefunga mabao 17 kila mmoja wao.

''Ni kweli'',alisema Van Gaal.

''Robin van Persie hawezi kukataa,Falcao naye hawezi kupinga na Rooney hachezi katika safu ya mashambulizi.

MKufunzi huyo wa Old Trafford amekuwa akikosolewa kwa kumchezesha Wayne Rooney katika kiungo cha kati,huku Radamel Falcao akipewa fursa chache kwa madai kwamba hayuko shwari.

Van Gaal alisema:''Kwa sasa hatuna mshambuliaji ambaye anaweza kufunga mabao 20''.CHANZO:BBC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR

Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkuruenzi huyo nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR

Read more...

 

 Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  mjumbe wa TBN Mkala Fundikira,  Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIMS, Shafiq Mpanja wa AIM, Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na mjumbe wa TBN Khadija Kalili.

Katika mkutano huo TBN imesema kesho Jumamosi jioni Bloggers takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers.

 Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.

 Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.

Read more...

Dkt. Fenella akutana na Wasanii Nchini

Published in Jamii

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimueleza jambo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis Michael wakati wa mkutano na wasanii uliofanyika katika ukumbi wa uwanja mpya wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko akiongea na wasanii nchini na kuwaeleza kuhusu umuhimu wa sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika masuala ya kitaifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya, Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo.

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na wasanii nchini na kuwaasa wasanii kuielimisha na kuhamasisha Jamii kuhusu Katiba Inayopendekezwa kupitia kazi mbalimbali za sanaa, wakati wa mkutano na wasanii nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Read more...

Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akifungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini.

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza jambo na Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila kabla ya kuanza kwa mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam.

Read more...

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

tangazahapa_copy_7ab8d.jpg

Maoni ya Wanakijiji

Zilizosomwa Zaidi

BLOG SHABIHANA