We have 525 guests and no members online

Matangazo Mapya

We provide the full IT solutions including web design, web development ...

G1

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kulia ni Mfamasia Sehemu Elimu, Habari na Takwimu Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Amani Masami.

G2

Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)(P.T)

Kenya yateketeza marundo ya pembe za tembo

Published in Jamii

Rais wa Kenya Jumamosi (30.04.2016) amechoma maelfu ya pembe za ndovu na faru na kuteketeza mrundiko wa pembe hizo na kutuma ujumbe mkali kwamba biashara ya viungo vya wanyama haina budi kukomeshwa.

Moshi ulitanda wakati mrundiko wa pembe hizo ukiteketea katika mbuga ya wanyama ukingoni mwa mji mkuu wa Nairobi na kuangamiza tani 105 za pembe kutoka takriban wanyama 8,000 ambao ni uchomaji mkubwa sana wa aina yake.

Rais Uhuru Kenyatta amepuuzilia mbali hoja za wale walioitaka Kenya ambayo ilichoma pembe zake za kwanza hapo mwaka 1989 badala yaake ingeziliuza pembe hizo ambazo zinakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 150.

Alisema kabla ya kutia moto rundo la kwanza la pembe hizo kati karibu ya marundo kumi na mbili kwamba "Kenya inatowa ujumbe kwamba kwa sisi pembe haina thamani venginevyo inakuwepo kwa tembo wenyewe."

Kenya yataka marufuku ya pembe(P.T)

Read more...

Jumba lililoanguka

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaka kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba ilioanguka mjini Nairobi na kuwaua watu saba.

Kenyatta aliyezuru mkasa wa tukio hilo pia amewataka wakaazi wa nyumba zilizopo karibu na eneo hilo kuondoka wa kuwa nyumba hizo zimethibitishwa kutokuwa salama.

Maafisa wa Kaunti ya Nairobi wamethbitisha kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeorodheshwa miongoni mwa majumba yaliotarajiwa kuvunjwa kwa kuwa haikuafikia viwango vya nyumba ya kuishi watu wengi.

Rais Uhuru Kenyatta

Juhudi za uokoaji zinaendelea lakini zimetatizwa na mvua kubwa inayoendelea mbali na uwezo wa kufikia eneo hilo.

Jeshi la Kenya linaloongoza juhudi hizo za uokozi limelazimika kutumia mikono na misumeno ya kielektroniki kuchimba chini ya vifusi kwa kuwa vifaa vinavyohitajika katika zoezi hilo haviwezi kuingia katika eneo hilo.BBC

????????????????????????????????????

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo

Na. Immaculate Makilika-MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana amezindua kampeni ya usafi ya mkoa iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Kampeni  ya usafi ya  siku 90 inayobeba kauli mbiu “usijifanye mstaarabu kuwa mstaarabu” itaanza leo (1/5/2016)  kwa lengo la  kuboresha hali ya usafi  katika  mitaa mbalimbali pamoja na  jiji la Dar es salaam kwa ujumla,  ambapo itasaidia kuzuia magonjwa ya mlipuko, na wakazi wa jiji hilo wamehamasishwa kushiriki kufanya usafi katika mitaa yao pamoja na maeneo mbalimbali na baadae washindi  kupatiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 100 kwa mitaa miwili itakayokuwa imeshinda, ambapo pia  Mkuu huyo wa mkoa aligawa vifaa vya usafi kwa wenyeviti wa mitaa kutoka wilaya zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke.

Bw. Makonda amesema kuanzia sasa wakazi wa jiji la Dar es salaam watafanya usafi katika mitaa na maeneo yao  kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi, na baada ya siku 90 washindi wawili, ambapo  mtaa utakaokuwa msafi na wenye makazi yaliyo katika mpangilio mzuri utapata zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 50 na mtaa utakaokuwa msafi lakini hauna makazi yaliyo katika mpangilio mzuri nao utapata fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 50, vilevile  mtaa utakaoongoza kwa uchafu utatangazwa ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wake kueleza namna ambavyo ameshindwa  kusimamia usafi katika eneo lake.

“Mganga Mkuu wa Mkoa atafanya ukaguzi na kutangaza  vigezo vya washindi baada ya siku 90, tangu kuanza kwa kampeni hii, tunataka kuona mabadiliko na watu lazima washiriki kwa usafi na kuyapaka rangi  majengo yao. Suala la usafi si la Serikali pekee ni letu sote” alisema Makonda.

Aidha, ameagiza wamiliki wa vyombo vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es Salaam hasa daladala kuwa na vifaa vya kutupia taka katika vyombo vyao na kuanzia mei 2, atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa kampuni, taasisi na watu mbalimbali kuunga mkono zoezi hilo kwa kutoa misaada mbalimbali ikiemo kuhamasisha wananchi juu ya suala hili. Pia amewapongeza wakazi wa mkoa huo kwa kushiriki kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni ya usafi na  kuzipongeza  kampuni za Clouds Media group, Azam na redio ya EFM kwa michango yao katika kufanikisha kampeni hiyo ya usafi kwa mkoa wa Dar es salaam.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi, amewasisitiza wakazi wa  mkoa  wa Dar es salaam kufanya zoezi la usafi kuwa endelevu kwa kuwa wananchi wenyewe ndio wazalishaji wakubwa wa uchafu hivyo ni lazima wahahikishe wanauondoa.

Naye, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Bw. Mustafa Mkama, amesema wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaunga mkono kampeni hii na kuitaka jamii kwa ujumla ibadilike kwa kufanya usafi na Serikali nayo ihakikishe inaweka vyombo vya kuhifadhia taka  katika maeneo mbalimbali, sambamba na kuendelea kuelimisha wananchi umuhimu wa kuwa na  mazingira safi.

Uzinduzi wa kampeni ya usafi ya mkoa  wa Dar es Salaam ulitanguliwa na maandamano ya Mkuu wa Mkoa, viongozi mbalimbali wa dini na vyama vya siasa, wasanii mbalimbali akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul maarufu kama Diamond platnamz pamoja na wakazi wa mkoa huo, ambayo yalianza   katika wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni  na kuishia katika viwanja vya Leaders.

Ikumbukwe  kuwa 9 desemba 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe  Magufuli alihairisha shamrashamra za sherehe za Muungano na kufanya usafi, huku akiwataka watanzania wote kushiki kufanya usafi katika maeneo yao na kuagiza kuwa zoezi la kufanya usafi kuwa endelevu nchi nzima. (P.T)

HAK1

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu toka Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Chitralekha Massey akiwapiga msasa baadhi ya waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.

HAK2

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. James Jesse akitoa mada mbele ya waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.

HAK3

Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Salma Ally Hassan (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.

HAK4

Wadau wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja na Waaandishi wa Habari waliohudhuria mafunzo ya siku moja ya warsha kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

Na Benedict Liwenga.

Asasi za Kiraia pamoja na Taasisi za kutetea haki za binadamu nchini zimewaasa Waandishi wa Habari nchini kujikita katika kuhabarisha umma kuhusiana na masuala ya haki za binadamu ikiwemo mauaji ya watu wenye ualbino, mauaji ya vikongwe, ukatili dhidi ya watoto, pamoja na adhabu ya vifo.

Rai hiyo imetolewa leo na Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Salma Ally Hassan wakati wa Warsha ya siku moja iliyofanyika mkoani Morogoro yenye lengo la kuwajengea uelewa Wanahabri kuhusu Mpango wa Kimataifa wa kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR).

Bi. Salma ameeleza kuwa kutokana na tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini, vyombo vya habari havinabudi kuwa na uelewa mkubwa kuhusu umuhimu wa kuziongelea haki za binadamu kwani jamii imekuwa haizitambui baadhi ya haki hizo na kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo vya uvunjifu wa amani yakiwemo matukio ya mauaji ya watu wenye ualbino, vikongwe pamoja na ukatili kwa watoto.

Ameongeza kuwa, baadhi ya watu nchini wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi kwa kuua watu ambapo watu wenye kuyasemea hayo ni Vyombo vya Habari lengo likiwa ni kukemea kuendelea kwa vitendo hivyo.

“Uvunjaji wa haki za binadamu unafanywa na watu katika jamii, kwa mfano, mauaji ya Watu wenye Ualbino, mauaji ya vikongwe, pale sio Serikali inakua imevunja haki za binadamu, bali ni watu katika jamii”, alisema Bi. Salma.

Kwa upande wake Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bi. Chitralekha Massey ameeleza kuwa, ni vema Tanzania ikakubalina na mapendekezo yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu yanayoendana na Dunia kwa ajili ya ulinzi wa haki hizo.

“Sisi kama Umoja wa Mataifa tunapenda kuona Tanzania inafanya uamuzi utakaosaidia kuboreshwa kwa haki za binadamu nchini kwani ni wakati sasa wa jamii kusema kwa uwazi kuwa mapendekezo hayo yatakuwa yenye manufaa kwao”, alisema Massey.

Aidha, katika warsha hiyo, vyombo vya habari, jamii pamoja na Serikali wanajukumu la kulinda haki za binadamu na kuendelea kukemea matukio yanayovunja amani katika jamii.

Tarehe 9 Mei, 2016 Tanzania inatarajiwa kufanyiwa tathmini ya pili juu ya hali ya haki za binadamu nchini na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ambapo tayari Asasi za Kiraia na Watetezi wa haki za binadamu wamekwisha wasilisha mapendekezo yao kwa Wawakilishi wa nchi wanachama wa umoja huo.(P.T)

wa1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

wa3

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

wa2

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) (P.T)

Neno Fupi La Usiku: Vipofu Na Wenye Kuona..

Published in Jamii

blind-cane

Ndugu zangu,

Duniani hapa kimsingi wanadamu wamegawanyika katika makundi mawili; vipofu na wenye kuona. Naliona hilo ninapowatafakari wanadamu kwa kuyasoma mawazo ya wanafalsafa Plato na Confucius.

Katika kuliangalia hilo tukubaliane, kuwa kuna miongoni mwetu wenye kuishi bila kufikiri. Na baadhi wanafikiri tu, lakini, hawawezi kuziweka fikra zao kwenye mpangilio na kimatendo. Ni hao wenye kuishi bila kufikiri ndio wenye kuzihangaisha fikra hata za watu wa aina yangu, bila shaka, ukiwamo wewe msomaji .

Hawa ni watu wasiotabirika. Ndio hawa, ukikutana nao asubuhi na mkakubaliana jambo, yumkini, mkikutana tena jioni, basi, yale makubaliano ya asubuhi hayapo tena, na pengine mtu huyo ameshasahau mlikubaliana nini!

Hawa ni watu wasiojitambua na hawajui kuwa hawajitambui. Hilo la pili ni tatizo kubwa zaidi. Hawajui walikotoka, hawajui walipo wala wanakokwenda. Ndio dhana ya upofu inayozungumzwa hapa.

Yumkini, watu hawa wamejifunika vilemba vya ujinga.

Ni Neno Fupi La Usiku.(P.T)

Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya.

Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava .

Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko.

Sehemu ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko.

Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.(P.T)

Read more...

UZINDUZI WA MASHINDANO YA UMISSETA MKOANI MWANZA

Published in Jamii

1

Mkuu wa mkoa wa Mwanza.John Mongella akipokelewa na viongozi na wadau wa michezo alipowasili uwanja wa CCM Kirumba kuzindua mashindano ya COPA UMISSETA

2

Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Hamis Maulidi akizungumza wakati wa hafla hiyo.

3

Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa(BMT), Mohamed Kiganja akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo.

6

 Meneja masoko wa wa kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola Kanda ya Ziwa, Marco Masaka akizungumza katika uzinduzi huo.(P.T)

Read more...

Ambaye Hakuvaa Suti Na Tai Ndiye Mwenyekiti Wenu..!

Published in Jamii

Ndugu zangu,

Novemba mwaka jana nilifika ' Nchi Wapenda Suti Na Tai'. Ni Malawi.Nchi Ya Wapenda Kuvaa Suti Na Tai..!
Ni Malawi.
Jamaa kutoka Zambia alinishukuru sana nilipoingia mkutanoni na style yangu ya mashati, maana naye hakuwa na suti na tai. Alidhani angekuwa peke yake! Akasema;
" Thus why I love Tanzanians, they are so simple!"
Maggid,
Iringa.(P.T)

BASATA KUADHIMISHA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ

Published in Jamii

New Picture

National Arts Council BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Elimu na Sayansi (UNESCO) litaungana na wasanii mbalimbali nchini na wadau wa Sanaa kuazimisha siku ya muziki wa Jazz duniani ambayo kwa mara ya kwanza itaazimishwa nchini Mei 2, 2016.

Maazimisho hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii wa muziki wa jazz hususan Band maarufu ya Das Jazz yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ofisi za BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Sambamba na burudani hizo, kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wadau wa muziki huu wa jazz ambazo zitalenga kuamsha ari, thamani na ufahamu wa muziki huu maarufu duniani miongoni mwa wasanii nchini.

Wawasilishaji wa mada hizo pamoja na mada zao kwenye mabano ni pamoja na John Kitime (Matumizi ya neno Jazz), Carola Kinasha (Uhusiano kati ya Elimu ya Muziki na Jazz) na Kurwigira Mareges (Historia ya Muziki wa Jazz) na Masoud Masoud (Ujue Muziki wa Jazz)

Mbali na burudani na mada hizo kuhusu muziki huo wa Jazz kutakuwa na wageni waalikwa kutoka kwenye balozi na vituo vya Utamaduni vya nchi mbalimbali zilizopo hapa Tanzania

BASATA linatoa wito kwa wasanii na wadau wa muziki huu wa jazz kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya ambayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka sambamba na mataifa mengine duniani.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza

Katibu Mtendaji – BASATA (P.T)

New Picture

Ndugu zetu pamoja na Marafiki zetu, wakati huu tukiendelea kuomboleza msiba wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ushiriki wenu wa hali na mali katika kuandaa safari yake ya mwisho.Katika kumuenzi na kukumbuka urafiki wake wa kipekee, Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam inawaalika na kuwakaribisha katika kusanyiko la kumuenzi jioni ya leo 30 April 2016 kuanzia saa 11 jioni pale Triple 7 (@777). Kusanyiko hili ni mahsusi kwa mambo mawili makubwa, moja likiwa ni kukumbuka na kuenzi maisha yake katikati yetu na pili kupashana habari za kuhitimisha maandalizi ya Safari ya kumuweka katika nyumba yake ya Milele.

Naomba tujumuike wote na tunaamini hata huko aliko atafurahi tunapomkumbuka.

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe

Imetolewa na Dr. George Longopa KNY Kamati ya Maandalizi ya Dar ES SALAAM (P.T)

UCHUKUZI SC YAWA YA TATU, KIPA ADAKA PENATI 3

Published in Jamii

MO1

Kipa Willium Barton wa Uchukuzi SC akikaa tayari kupangua penati ya kipa mwenzake wa Tanesco Hashim Yahya. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2.

MO2

Abubakar Mwamachi (9) wa Uchukuzi SC akikokota mpira huku mlinzi wa Tanesco Juma Rajabu akiwa ameshika ardhini.(P.T)

Read more...

She visited Karibu Tanzania Association and Ilula Development College a month and a half ago..
Maggid,
Iringa.(P.T)

Oh! Oh! The Guardian, today.

Published in Jamii

Renatusi Njohole akiwa katika picha ya pamoja na kaka yake

 Benchi la ufundi la Yanga Bwn. Gerry Mshana(kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Nico Njohole siku ya Alhamisi Dallas, Texas. Nico na Renatus wamekuja maalum kuhudhuria mkutano wa DICOTA na kuchezea Simba kwenye mtanange wa watani wa jadi.

  Kutoka kushoto ni Gerry Mshana, Mary Maswanya (dada mkubwa wa Nico na Renatus), Renatus, Nico na Rais wa DICOTA, Ndaga Mwakabuka walipopata picha ya kumbukumbu. 

 Rais wa DICOTA Bwn. Ndaga Mwakabuta akiwa katika picha ya pamoja Nico na Renatus

 Kutoka kushoto ni Jerry, Nico, Ndaga Mwakabuta, Renatus, na Gerry Mshana wakiwa kwenye picha ya pamoja(P.T)

Oh! Oh! Mwenyekiti Wenu Na Ugeni...

Published in Jamii

Ni kwenye ofisi zetu za Karibu Tanzania Association, Iringa, majuma matatu yaliyopita. Wajumbe wangu Adam Lington na Agripina zamani akiwa na TGNP nao walikuwemo kwenye msafara uliokuja. Pichani wakipata maelezo ya shughuli za KTA kutoka kwa mwenzangu Grasiano Myinga, Mratibu wa Miradi, KTA.
Maggid.(P.T)

Kim

Kim alipatikana na makosa ya kufanya ujasusi

Raia wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.

Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.

Kim aliwasilishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi.

Mwezi Machi, mwanafunzi mwingine Mmarekani alifungwa jela miaka 15 kwa kujaribu kuiba bango la propaganda.

Alipatikana na makosa ya "uhalifu dhidi ya dola”.

Mhubiri wa Canada afungwa maisha Korea Kaskazini

Waziri auawa kwa kusinzia mbele ya rais

Kim amefungwa jela katika kipindi ambacho uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi nyingine za Magharibi umedorora.

Majuzi, Pyongyang imefanya msururu wa majaribio ya kurusha makombora baada ya kufanyia majaribio bomu ya nyuklia mwezi Januari, majaribio yote yakivunja vikwazo zilivyowekwa na UN.

Pyongyang ilijaribu kurusha makombora mawili ya masafa ya wastani Alhamisi lakini yalilipuka na kuanguka baharini muda mfupi baada ya kurushwa.

Hatua hiyo ilipelekea kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.BBC

SU1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam jana April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendejana baina ya Tanzania na Urusi.

SU2

SU4

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam jana April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendejana baina ya Tanzania na Urusi.

SU5

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam jana April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendejana baina ya Tanzania na Urusi.(P.T)

Read more...

Staffan di Mistura amesema ataitisha duru nyingine ya mazungumzo ya kutafuta amani Syria mwezi ujao lakini amezitaka Marekani na Urusi kuhakikisha makubaliano ya kusitisha mapigano yanazingatiwa.

Di Mistura ameyasema hayo baada ya kuwa na kikao na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuliarifu kuhusu duru ya hivi karibuni ya mazungumzo ya kutafuta amani Syria.

Mjumbe huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema mazungumzo hayo yalipiga hatua licha ya kuongezeka kwa ghasia nchini Syria ambazo zinatishia kufikiwa makubaliano ya kuvimaliza vita vya Syria.

Di Mistura ameitaka Marekani ambayo inayaunga mkono makundi kadhaa ya waasi nchini Syria na Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa utawala wa Rais wa Syria Bashar al Assad kuitisha mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri wa nchi zenye nguvu zaidi duniani kujadili namna ya kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kabla ya mazungumzo ya kutafuta amani kuendelea.

Mapigano yamezidi Syria

Tangazo hilo linakuja huku majeshi ya serikali ya Syria yakiishambulia hospitali na maeneo ya makaazi ya watu katika mji wa Aleppo na kusababisha vifo vya takriban watu 20 wakiwemo watoto wawili.

Daktari pekee wa kuwatibu watoto katika mji huo wa Aleppo ambao unadhibitiwa na waasi pia ameuawa katika mashambulizi hayo ya angani yaliyofanywa hapo jana.

Katika mashambulizi mengine mashariki na magharibi mwa mji huo mapema hapo jana watu 16 waliuawa wakiwemo raia watano.

Di Mistura amesema pande zote zilizoshiriki mazungumzo ya Geneva sasa zanatambua haja ya kuwepo serikali ya mpito Syria ambayo itakuwa na jukumu la kuandika katiba mpya hata kama kuna tofauti kubwa kuhusu muundo wa serikali hiyo.

Di Mistura ameongeza kuwa kuna uelewa mzuri kuwa kipindi cha mpito kinapaswa kusimamiwa na serikali mpya ya kuaminika na inayojumuisha kila upande ambayo itachukua mahala pa serikali ya sasa.

Hata hivyo mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria amekataa kuzungumzia suali kuu ambalo limekuwa kikwazo cha mazungumzo kusonga mbele nalo ni hatma ya Rais Assad.

Je Assad ataachia madaraka?

Upande wa upinzani umesiistiza kuwa Assad hawezi kuwa sehemu ya serikali mpya ya mpito na sharti akubalie kuachia madaraka kama sehemu ya makubaliano. Upinzani unaoungwa mkono na Saudi Arabia na nchi za magharibi, ulijiondoa rasmi kutoka kwenye mazungumzo wiki hii ukipinga kuongezeka kwa ghasia.

Upande wa serikali nao umesema Assad hawezi kuwa mojawapo ya ajenda ya mazungumzo ya kutafuta amani.

Hapo jana Urusi iliutaka Umoja wa Mataifa kuliweka kundi la wapiganaji la Jaish al Islam katika orodha ya makundi ya kigaidi kwa madai lina mafungamano na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Dola la Kiislamu IS na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda.

Mazungumzo ya kutafuta amani yamekuwa yakilenga kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 270,000 na kuwaaacha mamilioni ya Wasyria bila ya makaazi.(P.T)

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Wanakijiji

BLOG SHABIHANA