We have 895 guests and no members online

  • DALADALA YAGONGA MTEMBEA KWA MIGUU IRINGA
    DALADALA YAGONGA MTEMBEA KWA MIGUU IRINGA

    DALADALA iliyosababisha ajaliilitelekezwa na derev…

Magazeti ya Leo

Matangazo Mapya

We provide the full IT solutions including web design, web development ...

Ndugu zangu,

Pichani ni kijijini Kwembe, nje ya Dar es Salaam. Ni zamani kidogo, anaonekana Balozi, Profesa Joram Biswalo akinionyesha ilikoishia mipaka ya eneo lake. Profesa ana eneo kubwa! Na Profesa amewahi kuwa Balozi wetu Brazil. Amerudi nyumbani akitokea Ethiopia, kama Balozi.

Na mwanadamu usione aibu ya kwapa unapoonyesha eneo lako. Maana, kuna kisa cha Chifu wa Kifipa kule Lyamba lya Mfipa.

Wazungu walipoingia eneo lake hawakutaka ugomvi na Chifu. Wakamwomba Chifu awaonyeshe mipaka ya eneo lake na litakalobaki litakuwa ni eneo la Wazungu.

Basi, Chifu yule aliona aibu kuonyesha kwapa lake. Hivyo, wakati akionyesha eneo lake hakunyanyua mkono ukanyoka. Akaishia kukuunja kunja.

Alipozinduka Chifu akajikuta amebaki na kieneo kidogo wakati Wazungu wamechukua eneo kubwa ikiwamo milima ya Lyamba lya Mfipa!

Maggid,
Iringa.(P.T)

Siku likitua Iringa nahofia kamba zitapanda bei madukani! Si mnatujua Wanyalukolo...!

Maggid,
Iringa.(P.T)

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi ameimbia RFI Kiswahili kuwa, viongozi wa kisiasa kutoka serikali na upinzani wamekubaliana uchaguzi Mkuu kurudiwa tena.

Hata hivyo, Makamu huyo wa pili amedokeza kuwa hadi sasa haijaafikiwa ikiwa tume ya sasa ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Jecha Salim aliyefuta matokeo hayo itakubaliwa kusimamia uchaguzi mpya.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameeeleza kuwa rais Ali Mohamed Shein anaendelea kuwa uongozini kikatiba.Wananchi wa Zanzibar wanasubiri uamuzi wa viongozi wa kisiasa kuhusu mvutano huu wa kisiasa katka visiwa hivyo.

IMECHOTWA NA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

LEICESTER KUITWANGA TENA MAN 5?

Published in Michezo

LEICESTER-MANUNITED

MSIMU uliopita, Manchester United waliongoza 3-1 huko King Power Stadium na kujikuta wakitandikwa 5-3 na Leicester City katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Septemba 21, 2014 na Jumamosi Timu hizi zinakutana Uwanja huo huo.

Safari hii, Leicester City, ndio Vinara wa Ligi Kuu England, wakiwa Pointi 1 mbele ya Man United iliyo Nafasi ya Pili.

Mwaka Jana, Straika wa Leicester, Jamie Vardy, alifunga Bao lake la kwanza kwenye Ligi na kutengeneza zote 4 walipoifunga Man United 5-3, na safari hi indie anaongoza kuwa Mfungaji Bora wa Ligi.

Safari hii, Leicester wapo chini ya Kocha Claudio Ranieri ambae mara ya mwisho alifukuzwa akiwa Kocha wa Greece baada ya Nchi hiyo kufungwa na Vibonde wa Ulaya Faroe Islands.(VICTOR)

Read more...

Hii Si Sawa Kabisa..!

Published in Jamii

Nionavyo, taasisi za Serikali kutumia fedha za umma kupongeza magazetini na kwenye runinga badala ya kubana matumizi si jambo la tija.

Rais ameshachaguliwa na kuapishwa, pongezi za jumla zimeshatolewa. Sasa ni kufanya kazi tu kuijenga nchi.

Hatuwezi kuendelea kwa kutumia fedha za umma kutuma salamu za pongezi magazetini mwezi mzima.

Na likija baraza jipya iwe hivyo hivyo, hatutafika. Sekta binafsi iachwe itumie fedha kwa jambo hilo. Hao ndio wa kutunisha mfuko wa hazina, lakini si kwa taasisi za serikali.
Wajumbe mna maoni gani?
Maggid,
Iringa.(P.T)

Nilijionea kwa karibu shida ya maji kijijini hapo. Ni mwaka 2012.

Maggid(P.T)

Urusi kushirikiana kupambana na IS

Published in Jamii

Rais wa Urusi Vladmir Putin na mwenziye wa Ufaransa Francois Hollande

Urusi imesema iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State.

Rais Vladmir Putin amemwambia mweziye wa Ufaransa Francois Hollande, kuwa shambulio dhidi ya ndege ya abiria ya Urusi na lile lililotokea mjini Paris, ambayo yote kundi la Islamic State limekiri kuhusika, kumefanya nchi hizo kuungana dhidi ya adui wao huyo.

Rais huyo wa Ufaransa yupo nchini Urusi kama sehemu ya kujaribu kutafuta muungano kuweza kuwadhibiti wapiganaji wa Islamic state nchini Syria.BBC

Ndugu zangu,

Jumamosi moja ya Mwezi Mei mwaka 2008 nilikuwa kijijini Chala, Namanyere, Mpanda mkoani Rukwa.
Siku hiyo nilishuhudia moja ya harusi simple kabisa kupata kuziona.

Bwana na Bibi Harusi walikwenda kanisani kwa miguu huku wakisindikizwa na ndugu,jamaa na marafiki. Shughuli ya kanisani ilipomalizika, msafara wa Bwana na Bibi Harusi ukaelekea nyumbani kwa Bwana Harusi. Huko ndiko ilikoandaliwa shughuli ya kunawa mikono na kunywa pia.

Nyimbo ziliiimbwa, watu wakacheza kwa furaha. Kwenye msafara hakukuwa hata na mkokoteni wa kusukumwa na punda. Wote walitembea kwa miguu. Nami nilijiunga na msafara ili nipate picha ya Bwana na Bi Harusi kwa karibu.

Lakini, kadri tulivyokuwa tukitembea, ndipo kukawa na mkanganyiko wa nani haswa ni Bi Harusi! Maana, nilipokuwa nikiangalia kwenye kamera yangu, niliwaona wanawake watatu waliokuwa wakibadilishana katika kutembea kando ya Bwana Harusi Je, unaweza kumtambua Bi Harusi hapo pichani?

Maggid,
Iringa.(P.T)

mo

Msomaji na mdau wa mtandao wako wa habari www.modewjiblog.com unakupa nafasi wewe kumuuliza maswali/swali lolote lile Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL Group, Mohammed Dewji. Maswali yote yatajibiwa na kutolewa ufafanuzi wa kina. Tutakuwa na mahojiano naye karibuni. Asanteni sana.

Utaratibu wa kumuuliza maswali ni kwa kukomenti kwenye post hii kisanduku cha maoni, Zingatia Kanuni na sheria ikiwemo kutotumia lugha zisizo rasmi.

Pia waweza kutoa maoni yako kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ukiwemo ukurasa wa Mohammed Dewji : https://www.facebook.com/mohammeddewjitz/

au Ukurasa wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) : https://www.facebook.com/MeTLGroup/photos (P.T)

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga ili kujionea hali halisi jinsi huduma zinavyotolewa kwa wananchi siku moja tu baada ya muuguzi wa kituo hicho kukamatwa kwa tuhuma ya kuiba dawa za serikali.Pichani ni mkuu wa wilaya Josephine Matiro na katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga wakiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa wakiwa wamepigwa butwaa baada ya kuona chumba kimesheheni dawa wakati mara kwa mara wananchi wamekuwa wakiambiwa hakuna dawa badala yake wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya watu binafsi mtaani-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Hapa ni ndani ya ofisi ya mganga mkuu/msimamizi wa kituo hicho ambapo mkuu wa wilaya akiwa ameambatana na maafisa wengine wa manispaa ya Shinyanga amekutana na uongozi wa kituo hicho pamoja na wananchi waliomkamata muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila akituhumiwa kuiba dawa za serikali.Kulia ni Rashid Shaban akimweleza mkuu huyo wa wilaya jinsi walivyofanikisha kufichua wizi huo

Wa pili kutoka kulia ni msimamizi wa kituo cha afya Kambarage Dkt Nassoro Yahya akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga kuhusu suala la upungufu wa dawa katika kituo chake ambapo alisema kituo kina upungufu wa dawa na walishatoa taarifa panapohusika siku nyingi zilizopita.Hata hivyo maelezo yake yalipingana na yale ya kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana Raphael(mwenye suti pichani) aliyedai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna tatizo la upungufu wa dawa bali dawa pekee ambayo haipo ni ile ya Antibiotic.(P.T)

Read more...

NH9

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Novemba 26, 2015 Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mauzo ya nyumba katika mradi mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam (kulia) Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah.

NH2

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiwaonesha waandishi wa habari michoro ya ramani ya mradi wa nyumba ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam.

NH3

Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza kwa umakini, Bw. Nehemia Kyando Mchechu.(P.T)

Read more...

Niger: Boko Haram yaua wanakijiji 18 Gogone

Published in Jamii

Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015.

Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015.

Na RFI

Shambulio jingine la kigaidi limetokea Kusini-Mashariki mwa Niger, karibu na mpaka na Nigeria. Shambulio hilo linahusishwa wanajihadi wa kundi la Islamic State, kundi la kiislamu la Afrika Magharibi, linalojulikana kama Boko Haram.

Wanakijiji kumi na nane wameuawa, wengi wamejeruhiwa na zaidi ya nyumba mia moja zimechomwa moto.

Mashambulizi ya Gogone yalidumu karibu masaa mawili Jumatano Novemba 25. Yalitekelezwa na idadi kubwa ya wapiganaji wa Boko Haram. Nyumba sabini zilichomwa moto, Meya wa Bosso aliyetembelea kijiji hicho, amesema. Mamadou Bako amesema kuwa watoto wawili waliteketea kwa moto, watu kumi na mmoja wamejeruhiwa, wanne wako katika hali mbaya.

Wanakijiji walijihami kwa pinde na mishale dhidi ya wapiganaji wenye bunduki aina ya Kalashnikov, amesema mkuu wa mkoa, ambaye alitembelea eneo hilo. Hasara ni kubwa, Abdou Kaza amehuzunika.

Wapiganaji waliondoka katika kijiji cha Gogone kwa mguu, kijiji ambacho kinapatikana kilomita kumi na tano kutoka mji wa Bosso, lakini hasa mita kumi kutoka Mto Yobe, ambao unagawa mpaka wa asili kati ya Niger na Nigeria. Watu waliojeruhiwa walisafirishwa katika mji wa Diffa.

Bunge mwezi uliopita liliongeza muda wa hali ya hatari katika jimbo hilo la Kusini-Mashariki mwa Niger ambapo kundi la Boko Haram limezidisha mashambulizi yanayoendelea kusababisha vifo vya watu wengi. Mwezi uliopita wapiganaji hao waliwachinjwa wanakijiji kumi na mmoja katika kijiji kilio karibu na mji wa Diffa.(P.T)

Papa Francis atahadharisha

Published in Jamii

Papa Francis amesema ni jambo la aibu kama viongozi wa dunia hawatafikia muafaka juu ya namna ya kupambana joto duniani.

Akizungumza katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kiongozi huyo wa Kanisa katoliki duniani amesema maslahi ya watu fulani hayapaswi kuruhusiwa kutawala ndani ya manufaa ya wote.

Kabla ya kuzungumzia hayo Papa Francis alikutana na viongozi wa dini ili kujadili umuhimu wa mazungumzo, na kuwa na misa za wazi kabla kukutana na umati wa maelfu ya waumini katika mji mkuu wa Kenya.

Katika ziara yake barani Afrika,kiongozi mkuu huyo wa kanisa katoliki anategemea kuelekea nchini Uganda leo na kuimalizia Jamhuri ya Afrika ya Kati novemba 30..BBC

Magazeti ya Leo Ijumaa

Published in Jamii

SAID KUBENEA AWATEMBELEA WANANCHI WAKE KUWASHUKURU

Published in Jamii

 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiongea na wananchi Stendi ya Mabasi ya Ubungo Dar es Salaam leo, kuwashukuru kwa kumchagua na kujua changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo jana alitembelea Soko la Ndizi la Mabibo, Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano  na kumpa pole ya sh. milioni 1.1 Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mus'ab kilicho chomwa moto na kuunguza magodoro 30.

 Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.

 Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo

 Mbunge Kubenea akisalimiana na wananchi katika soko hilo.(P.T)

Read more...

Na Joseph Ishengoma, MAELEZO

26/11/2015

Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka kesho (tarehe 27.11.2015) anatarajia kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda.

Baba Mtakatifu Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda kesho kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati.

Hii ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kutembelea Bara la Afrika tangu alipoliongoza Kanisa Katoliki mwaka 2013.

Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC) nchini Padre Raymond Saba amesema Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi hizo.

“Tulipata mwaliko kutoka Kenya na Uganda, lakini tumeangalia nafasi yetu na jinsi ya kushiriki katika ziara hii. Hatukuweza kutuma mwakilishi Kenya, lakini Askofu Ruzoka ataiwakilisha TEC Uganda,” amesema.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, jana mabasi mawili ya waumini wa dini ya Kikristo yaliondoka mjini Mwanza kuelekea Namugongo, Uganda ambapo Baba Mtakatifu atakapofanyia ibada.

Eneo la Namugongo ndipo Mfalme Kabaka Mwanga II alipowachoma na kuwaua mashahidi 22 wa Uganda waliofia dini katika karne ya 18.

“Natoa wito kwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini, wafuatilie na kusikiliza kwa makini ujumbe wa Baba Mtakatifu aliouleta katika Barani Afrika kwa sababu unagusa moja kwa moja amani na ushirikiano miongoni mwa jamii,” amesema.

Kwa mujibu wa Padre Saba, Baba Mtakatifu hufanya ziara kufuatia mwaliko wa kanisa na serikali ya mahali husika au tukio la kimataifa linalohusiana na imani Katoliki.

Amesema, “Kanisa pekee yake haliwezi kufanikisha ziara ya Baba Mtakatifu. Ndio maana alipofika Kenya alipokelewa na Rais Uhuru Kenyatta na hata alipokuwa Marekani alipokelewa na Rais Baraka Obama ingawa sio rahisi kwa kiongozi wa Marekani kumpokea mgeni uwanja wa ndege.”

Ziara ya Baba mtakatifu nchini Marekani ilipangwa kabla hajawa kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki. Ziara hiyo ilitokana na kongamano la kimataifa la familia lililofanyika mjini Filadelphia.

Papa Francis anatarajia kuhudhulia kongamano la vijana ulimwenguni nchini Poland mwaka 2016.(P.T)

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wananchi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kuwataka kuwa wamoja na kujiandaa na maendekleo katika jimbo lake.

 Na kusema sasa makundi basi iliobaki ni Kazi Tu kwa maendeleo ya Wananchi wa Jimbo hilo na kusema yeye ni Mbunge wa Wananchi wa Chumbuni wote 

Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa hafla ya kuwashukuru.(P.T)

Read more...

Wahamiaji haramu wakamatwa Tabata Segerea

Published in Jamii

Na Shamimu Nyaki-Maelezo

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wahamiaji haramu 105 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa wanasafirishwa kwenda nchi nyingine za Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Kamishna Suleiman Kova amesema wahamiaji hao ambao wote ni wanaume wamekamatwa kutokana na ushirikiano wa wasamaria wema wanaoshi eneo hilo la Tabata Segerea.

Ameongeza kuwa wahamiaji hao waliingia nchini ya usimamizi wa mwanamke mmoja anaeitwa Zainabu Umwiza (25) anaesemekana ni raia wa nchi ya Burundi ambae anajihusisha na biashara hiyo ya usafirishaji haramu wa binadamu ambao ni kosa la jinai tayari kuwapeleka nchi nyingine na hivyo amemuomba ajisalimishe

“ Bi Zainabu Umwiza mwenye asili ya Burundi tunamwomba ajisalimishe maana yeye ni mfanyabiashara wa usafirishaji wa binaadamu kutoka nchi za Afrika kwenda Ulaya” kamanda Kova alisisitiza.

Aidha kamanda Kova ameeleza kuwa polisi walifanya upekuzi katika nyumba ya mwanamke huyo ndipo walipowakuta wahamiaji hao ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, usafirishaji wa binadamu kutoka Afrika kwenda bara la Ulaya unaofanywa na mwanamke huyo, ambao hufanyika kwa malipo ya Dolla 1000 kwa mtu mmoja.

Kamanda Kova ameongeza kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa kujua kwamba wana kibali chochote cha kuingia nchini waligunduliwa kuwa hawana na kueleza kuwa waliingia kupitia njia za panya na mbinu nyingine ambazo bado zinachunguzwa na kwamba wamewajulisha idara ya Uhamiaji na watashirikiana nao katika upelelezi ili hatimaye sheria ichukue mkondo wake.

Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kundoa na kuzuia tatizo la wahamiaji haramu ambao wamekua tishio katika usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.(P.T)

Sawa Sawa Kabisa...!

Published in Jamii

VITENDO VYA UKATILI KWA WAANDISHI WA HABARI

Published in Jamii

IMG_2832

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimiana na Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi alipowasili katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel.

Na Rabi Hume, Modewjiblog

Serikali mpya ya awamu ya tano iliyochini ya rais Dr. John Magufuli, imeahidi kushirikiana na mashirika na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakipambana kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa salama na kufanya kazi zao kwa uhuru bili kuingiliwa ufanyaji wa kazi zao na mtu yoyote.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Prof. Gabriel amesema serikali ya awamu ya tano ipo tayari kushirikiana na mashirika na wadau mbalimbali ambao wapo kuwasaidia waandishi wa habari ili haki zao ziweze kutekelezwa kutokana na kuwepo kwa uvunjaji wa haki za wanahabari.

Amesema wanatambua kuwepo kwa changamoto hizo kwa waandishi wa habari na kwa serikali ya awamu ya tano itahakikisha kushirikiana na mashirika na wadau ili kutetea haki za wanahabari kwa kuwa na uhuru katika utendaji wa kazi zao bila kuingiliwa na mtu.

“Naahidi kuanzia sasa serikali itakuwa ikishirikiana nanyi kusaidia kuhakikisha kunakuwa na uhuru wa vyombo vya habari, nchi yetu kwa sasa haina sababu ya kuacha kuungana na ninyi kutokomeza vitendo hivyo kwa wanahabari, serikali ni mpya na tutalitekeleza jambo hilo kila tumaposhirikishwa kuhusu vitendo vibaya kwa wanahabari,” amesema Prof. Gabriel.

IMG_2843

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua.

Aidha Katibu Mkuu huyo amewata waandishi wa habari kuwa pamoja na usaidizi ambao wizara imeamua kujitoa kuwasaidia pia wanapaswa kuandika habari zenye weledi na zilizo sahihi kwani kumekuwepo na kundi kubwa la waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiandika habari ambazo hazina uhakika wala weledi na hivyo kuupotosha umma kwa habari wanazoandika ila kuanzia sasa wanabidi kubadilika kwa kuandika habari ambazo zitakuwa na fadia kwa jamii inayowazunguka.

Kwa upande wa UNESCO, kupitia kwa Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues, amesema kumekuwepo na vitendo vingi ambavyo sio vya kibinadamu ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na wao wameamua kujitoa kuhakikisha wanatokomeza vitendo hivyo.

Amesema kama jamii ikiungana kwa pamoja kutokomeza vitendo hivyo inawezekana kwani kutokuwepo uhuru wa waandishi wa habari katika utendaji wao wa kazi kunapelekea jamii kukosa baadhi ya taarifa muhimu ambazo kama kukipatikana uhuru wa habari kutawapa fursa wanahabari wa kuzitoa taarifa hizo.(P.T)

Read more...

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

Maoni ya Wanakijiji

BLOG SHABIHANA