We have 323 guests and no members online

Global Education Link

Niliyoyaona Muhimbili Jana Usiku Yamenitia Simanzi ....

muhimbili ec810Ndugu zangu,
Jana usiku nilifika Wodi ya Sewa Haji pale Muhimbili kumwona ndugu yangu aliyepata ajali.

Hakukuwa na ruhusa ya kuingia wodini kwa vile ni usiku. Baada ya kujieleza kwa mlinzi akanielewa. Nikaruhusiwa kuingia, maana, mgonjwa alinihusu sana na kesho nisingeweza kumwona.Nilipoingia kwenye corridor za wodi niliingiwa na simanzi kuwaona wagonjwa waliolala pembezoni mwa korido, wengine wakiugulia maumivu.

Picha iliyonijia haraka ni kama vile nchi yetu imeingia kwenye vita ambavyo hatukujiandaa, na kwamba ninaowaona ni majeruhi wa vita waliokosa vitanda.

Kuna tatizo kubwa, maana Muhimbili ndio ilipaswa kuwa Hospitali kubwa ya Rufaa hapa nchini. Unajiuliza, kama Muhimbili hali ni kama hii, je hali ikoje kwenye hospitali za wilaya?

Nimerudi nilikofikia nikiwa hata hamu ya chakula imeniishia. Nawafirikiria wagonjwa wale wa kando kando ya korido za wodi watakavyopitisha usiku huu wakiwa wamelala chini, wenye maumivu na hata vyandarua hawana.

Na kuna wenye kufikiri , eti , wawekezaji wavune gesi yetu, na kama shukrani, watujengee kule Kilwa hospitali ya hadhi ya Appolo kule India. Kwamba ije iwahudumie Marais na waheshimiwa wengine!

Wenye kufikiri hivyo wanasahau kuwa tuna Muhimbili yenye kuhitaji kurejeshewa hadhi yake ya Muhimbili ya enzi hizo. Inawezekana.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.

HEADER

Mangiangane
+1Mangiangane2013-01-22 11:20#1
Mwenyekiti,
umesema mara nyingi kuwa Nchi hii ina matatizo ya msingi mengi. ukaenda mbali zaidi kuyataja na hata kushauri ni hatua gani za haraka zichukuliwe. naamini kabisa wanaofanya maamuzi hapa nchini hupitia kwenye blog yako zaidi ya mara moja kwa siku na huwa wanayaona maoni na mawazo yako. huwa najiuliza hivi huwa wanasoma blog yako kutafuta huko riwaya au nini? maana hakuna anaeyapa uzito stahili.
Mnukuu
Mangiangane
+1Mangiangane2013-01-22 11:29#2
juzi gazeti la Mwananchi liliandika habari ya hali mbaya ya huduma katika hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro. hakuna hata mhusika mmoja aliyejitokeza kueleza angalau kuna mikakati gani ya kuboresha miundombinu kwenye hospitali hiyo. hali hiyo ya Mawenzi ni kielelezo cha hali mbaya iliyopo kwenye hospitali zote za serikali nchini. fedha zetu zinagawiwa kwa vyama vya siasa visivyo na tija na kuendelea kuweka maisha ya watanzania rehani. hali ni ya kukatisha tamaa na nahisi tunahitaji wawekezaji wawekeze kwenye akili za viongozi wetu zaidi kuliko kwenye miundombinu.
hivi tumepewa vichwa vyenye ubongo kwa ajili ya kuupamba mwili?
tutafakari kwa pamoja.
Asante Mwenyekiti kwa kuliweka hili wazi.
Mnukuu
MULA
+1MULA2013-01-22 11:52#3
Ndugu Mjengwa, ukistaajabu ya Musa...Hakika Muhimbili ni yetu LAKINI...Kama uliona udogo wa vitanda vile na fikiria kwa mgonjwa aliyezidiwa anapojaribu kugeuka. Pembezoni hayana chuma cha kuzuia. Kwa uchungu mno huwezi kuamini nilikuta mgonjwa wangu ameanguka chini mpaka asubuhi hakubebwa na kuwekwa kitandani. Hakika aliishia kupata maumivu makali hatimaye alifariki hata hivyo. HII NDIYO NATIONAL HOSPITAL
Mnukuu
Grace
+1Grace2013-01-22 11:59#4
Kaka hii ni Tanzania au umesahau? Ungeenda labour ward hapo Muhimbili ndio ungezimia kabisa.....wama ma wanakufa kimya kimya.......hak una huduma yoyote. Wanmasiasa wetu hawana muda na sisi akina yakhe ndugu yangu, Wao wakiumwa wanatibiwa ulaya. Na kama hauna pesa unakufa rafiki yangu. Hii ndiyo bongo. Nadhani labda 2015 tutapata watu wa tofauti, labda. Hospitali za wilayani usiombee, hazifai...dakta ri mwenyewe mmoja, akienda kula wodini mnaugulia mpaka audi! Lakini ndio nchi yetu!
Mnukuu
Mwafrika Halisi
0Mwafrika Halisi2013-01-22 12:14#5
Nukuu ya alichoandika MULA:
Ndugu Mjengwa, ukistaajabu ya Musa...Hakika Muhimbili ni yetu LAKINI...Kama uliona udogo wa vitanda vile na fikiria kwa mgonjwa aliyezidiwa anapojaribu kugeuka. Pembezoni hayana chuma cha kuzuia. Kwa uchungu mno huwezi kuamini nilikuta mgonjwa wangu ameanguka chini mpaka asubuhi hakubebwa na kuwekwa kitandani. Hakika aliishia kupata maumivu makali hatimaye alifariki hata hivyo. HII NDIYO NATIONAL HOSPITAL

Pole sana Mula, hii habari imenisikitisha mno mno mno, ni uchungu uliokithiri. Hawa wanasiasa na viongozi inabidi kuwabana kwenye kutibiwa nje ya nchi ili waweze kuona machungu na umuhimu wa kuboresha huduma za afya. Je kwenye katiba mpya tumekaribisha maoni ya Madktari wasomi ambao si wanasiasa kwani kuna madaktari wengi ambao nao ni wana siasa.
Niliwahi kusema kuwa tatizo la Watanzania ni Watanzania wenyewe, kwani kuna mengi mno yanatokea ale Muhimbili yanayosikitisha mno.
Mnukuu
ibrahim
0ibrahim2013-01-22 12:58#6
Miye pia nilisikitika niliposoma makala ya mwenyekiti kuhusu Muhimbili.Kilic honitia huzuni ni kwamba, "shida hii bado ipo tu" kwani miaka hamsini iliyopita nilipoanza kazi hapo palikuwa na matatizo kama hayo, tukiwalaza wagonjwa kwenye sakafu. I was going to pray for help,but I thought of President Obamas speech recently from this parable...

A CARTER was driving a wagon along a country lane, when the wheels sank down deep into a rut. The rustic driver, stupefied and aghast, stood looking at the wagon, and did nothing but utter loud cries to Hercules to come and help him. Hercules, it is said, appeared and thus addressed him: "Put your shoulders to the wheels, my man. Goad on your bullocks, and never more pray to me for help, until you have done your best to help yourself, or depend upon it you will henceforth pray in vain."
Basi, ninachotaka kusema ni sisi wananchi, hasa wale waliojaliwa mabavu wajitolee kuondoa tatizo hili.
Mnukuu
MWEWWE
0MWEWWE2013-01-22 12:59#7
Muhimbili imeakarabatiwa majengo tu, hakuna kitu kule watu wanalala chini na kuna watu wanasema liwalo na liwe
Mnukuu
Bahati
+2Bahati2013-01-22 14:41#8
Ndo hiyo bongoland utashangaa bajeti yote inaenda kwenye kujenga ofisi, kununua vx, safari za kujenga uwezo/uzoefu ( sasa sijui toka wasafiri huo uzoefu hawajaupata) yaani ni aibu hela yote inaenda kwenye matumizi badala ya maendeleo. Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo.
Mnukuu
Mgoha
0Mgoha2013-01-22 15:09#9
Unashangaa nini? hii ndio mara yako ya kwanza kwenda muhimbili? hiyo hali ipo muda mrefu sana wewe ndio unaona sasa..........s i muhimbili tu ni all over the country. Then kwa taarifa hii utakuwa umempa wakati mgumu mlinzi wa zamu kwa sababu yeye alikusaidia tu.
Mnukuu
YAKOWAZI
-1YAKOWAZI2013-01-22 16:02#10
nani atajali muhimbili wakati tuliowapa dhamana wao huenda apolo india ama kweli tutajiju 2015
Mnukuu
Mcc
+1Mcc2013-01-23 17:02#11
Unashangaa nini? Mwandishi mkubwa kama wewe ulikuwa haujui hali ya Muhimbili? Mbona ulikuwa unachangia kwenye mgogoro kati ya madakitari na serikali? Tatizo ni hospitali za Apollo.
Mnukuu
Guest
+1Guest2013-01-28 15:43#12
Hali ya huduma za Afya Tanzania zinasikitisha kama ulivyoona muhimbili.Na hospitali zingine zipo hivyo.Madaktari na Wauguzi hawana jinsi.Serikali ndio hiyo.Madaktari wakilalamika inaonekana wanadai Maslahi yao na sio kuboreshwa kwa huduma yaani vifaa na vitendea kazi.Mwisho wa siku Viongozi wa madaktari wanatekwa na kunyamazishwa kwa kipigo na wengine kutishiwa kufukuzwa kazi.
HII NDIO TANZANIA NCHI YENYE AMANI."tutafaka ri na tuchukue hatua"
Mnukuu
Guest
0Guest2013-01-29 13:00#13
Hii ndio TANZANIA. Nakumbuka wakati fulani baba yangu akiwa mgonjwa taabani daktari akamwambia kaka yangu eti hakuna chumba cha kulaza wagonjwa hivyo aende giest house kwa kua nyumbani kwetu ni kijijini. Kaka angu akasema nimemtoa nyumbani nimelete hapa hosptali kwani hulo guest kuna huduma? wakasema kama uda dola 300 kuna kitanda cha private, ambapo kuna matibabu ya haraka. Najiuliza hivi ni Watz wangapi wanaweza kutoa dola 300 kwa kushtukiza?? kama hawana ndio hivyo, walale chini au guest. Lakini ndio nchi hii inavuna dhahabu ikiwa nchi ya nne Afrika,inavuna gesi ya Songosongo na sasa ina mpango wa kusafirisha gesi toka Mtwara kwenda Dar ili wajengewe hosptali ya Apollo. Aibu sana.
Mnukuu
Guest
0Guest2013-01-29 18:21#14
Jamani tupinge sera ya Jk kujenga hospitali zingine, Rekebisha zilizoko mbona kote kubaya sasa nenda KCMC utashangaa lakini who cares! Madaktari waligoma wananchi wakalaumu hawana ubinadamu mbona wangesikilizwa mambo yangebadilika hawakuwa wanadai mishahara jamani walitaka mfumo ubadilisha ila watu wakakuza mishahara.
Mnukuu
Guest
0Guest2013-01-30 09:31#15
tujiandae sasa nchi imeshauzwa hii.
Mnukuu
Guest
0Guest2013-02-04 13:20#16
Shida ya mtu mweusi sio langi ni ubinafsi,nchi yetu ilipaswa kuvuka jambo hilo,Haya uhuru unakuja kesho
Mnukuu
Guest
0Guest2013-02-25 16:49#17
serikali lazima ifahamu kuwa HEALTH OF THE PEOPLE IS THE SUPREME LAW OF THE LAND.BILA AFYA HAKUNA TAIFA ....SASA TUANGALIE AFYA KWANZA SIO KUZINDUA BARABARA NA MADARAJA ILI HALI WATU WANAPOTEA
Mnukuu

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Wanakijiji

BLOG SHABIHANA