Kuna watembeleaji 462  wapo online

Mjengwa Blog

Mjengwa Blog

I am a writer, photographer, social entrepreneur, political analyst and a teacher- facilitator.

Website URL: http://www.mjengwablog.com

Henry Mdimu (katikati anayezungumza) akitoa ufafanuzi wa namna ya kutoa elimu juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi 'Albino' huku kushoto akiwa ni Mratibu wa Fedha na Udhamini wa Imetosha, Monica Joseph na Masoud Kipanya ambaye naye ni mmoja wa wakilishi wa Imetosha.

Mwakilishi wa Tanzania Bloggers Network, Joakhim Mushi (kushoto) akielezea namna ya kuweza kusambaza taarifa ya kupinga ukatili dhidi ya mauaji ya Albino kupitia vyombo vya habari.

Bango lenye ujumbe wa Imetosha.(P.T)

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amekutana na Viongozi wa Chama cha Watu wenye Albino Tanzania na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuongeza nguvu ili kumaliza tatizo la amauaji ya dhidi ya Albino.

"Mauaji haya yanaisikitisha Serikali na kuifedhehesha sana, msidhani hatufanyi lolote, tunafanya juhudi kubwa na mbalimbali lakini imefikia wakati tuongeze juhudi hizo"alisema Rais.

Katika kikao hicho viongozi wa watu wenye Albino nchini wamesoma risala ambayo imetoa kilio chao na mapendekezo yao kwa serikali na hatimaye ikaafikiwa kuwa na haja ya kuunda kamati ya pamoja ambayo itajumuisha Serikali, viongozi wa watu wenye Albino, viongozi wa waganga wa jadi na wadau wote wakuu katika suala hili ili kupata mapendekezo na mkakati wa pamoja ambao hatimaye mauaji haya kukomeshwa kabisa nchini Tanzania.BBC

Mkoa wa Katanga, kusini mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambao kunaripotiwa mlipuko wa kipindipindu.

Na RFI

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umesababisha vifo vya watu 32 na wengine 1,500 wameambukizwa.

Takwimu hizi zimetolewa na Umoja wa Mataifa ambao unasema kwa kipindi cha miezi miwili sasa, kipindupindu kimeendelea kusababisha maafa hasa Kusini mwa jimbo la Katanga.

Msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Misaada ya Kibinadamu, Sylvestre Ntumba,amesema majuma saba ya kwanza mwaka huu yalishuhudia idadi kubwa ya watu wakiambukizwa ugonjwa huo.(P.T)

Ndugu zangu,

Nimesikiliza muda huu muziki wa Kiafrika kwenye http://mjengwablog.com.Ni muziki wa rhumba. Nyimbo zimenikumbusha picha yangu hii ya kwenye maktaba yangu. Ni vijana wa enzi hizo walipokuwa wakidensi.

Na Afrika mwanamme kwenye densi ndiye kwa heshima humwomba mwanamke waingie ukumbini kudensi.

Na raha ya muziki ndio hiyo, mwanamke kaweka kando viatu!

Hiyo ndio Chakachua Origino!

Ni Neno Fupi La Leo.

Maggid,
Dar es Salaam.(P.T)

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda wilaya za Igunga,Nzega Uyui mpaka Tabora.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.Kulia kwake ni Mbunge wa Tabora Mjini Alhaji Ismail Aden Rage na kushoto ni Mbunge wa Igalula Mhandisi Athumani Mfutakamba.

Mbunge wa Tabora Mjini Alhaji Ismail Aden Rage, akizungumzia mradi huo unaotarajia kunufaisha vijiji 68 na watu karibu watu 385,280 katika maeneo yanayozunguka mradi huo.(P.T)

Wengi wavutiwa na hotuba zake

Wampongeza kwa namna anavyokiimarisha Chama Cha Mapinduzi na msimamo wake wa kutaka Viongozi kuwa karibu na wananchi

 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Kibakwe,jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoa wa Dodoma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe na kuwataka wana CCM kuchagua viongozi wanaowataka na kusema wilaya au mkoa hawataka jina la mtu yeyote aliyechaguliwa na wananchi.(P.T)

Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa tarehe 04 Machi, 2015 Wilayani Kahama mafuriko makubwa yalitokea na kuathiri wakazi wa kata ya Mwakata katika vijiji vya Mwakata, Numbi na Mwaguguma. Kutokana na mafuriko yaliyotokea tathmini ya awali inaonesha kuwa watu 42 wamepoteza maisha, watu 82 wamejeruhiwa na watu wanaokadiriwa kufikia 574 wameathirika. Jumla ya nyumba 137 zimeathirika kwa viwango mbalimbali.

Serikali imechukua hatua za haraka kwa kushirikiana na wananchi kuwafikia na kuwanusuru waathirika wa mafuriko hayo waliokuwa wamezingirwa na mafuriko. Aidha vimeanzishwa vituo vya muda kuwahifadhi wananchi hao kwenye Shule.

Serikali imepeleka misaada ya kibinadamu kama ifuatavyo;

i. Chakula tani 20. Maharage tani 5, Mafuta ya kupikia lita 1,126 na Sukari tani 1.3

ii. Vifaa vya matumizi ya ndani ambayo vinajumuisha blanketi 650, ndoo 82 za lita 20, ndoo 82 za lita 10 ; Vifaa vya kupikia seti 82 na madumu 82

Kwa kuwa bado Serikali inalo jukumu kubwa la kuwawezesha waathirika kurejea katika maisha yao ya kawaida; inapenda kuwatangazia wale wote wanaoguswa na maafa haya kuwa Serikali inaendelea kupokea misaada mbalimbali ambayo inahitajika kwa waathirika.

Mahitaji haya ni pamoja na sare za shule; daftari za wanafunzi; mavazi ya kike na kiume; na chakula. Aidha kwa kuzingatia kuwa waathirika hawa wamepoteza mali na fedha katika maafa haya; misaada ya vifaa vya ujenzi (sementi, mabati, mbao, n.k.) inahitajika sana.

Utaratibu wa kupokea misaada hiyo kwa walio Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha misaada hiyo Idara ya Kuratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu au kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga_ Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Serikali itaendelea kuwasaidia Waathirika dhidi ya Changamoto zinazoweza kujitokeza hususani za kiafya zinazosababishwa na uchafuzi wa vyanzo vya maji na mazingira. Elimu juu ya ujenzi wa nyumba bora na makazi maeneo salama itaendelea kutolewa.

al1_a0cae.jpg

Rais Kikwete akisalimiana na ​Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 alipowakaribisha ili kusikiliza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​

al5_b7648.jpg

Rais Kikwete akiongea na ​Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 alipowakaribisha ili kusikiliza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

al3_93de8.jpg

Dr Possy akimsomea Rais Kikwete Mapendekezo ya ​ Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania juu ya namna ya kupambana na kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​.

Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Azam Tv Bw. Tido Muhando akizungumza wa waandishi wa habari

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji msaidizi wa Azam

Tv Bw Tido Muhando amesema kituo hicho kitakacho zinduliwa kesho na Rais wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete  hapo kesho kitakuwa cha kwanza kwa ubora Tanzania na Afrika mashariki. Picha na (Awadh Ibrahim wa Mjengwa Blog/Kwanza Jamii Radio)

Kwenye nchi ya Kusadikika hakuna uhaba wa maajabu.
Kwenye moja ya bodaboda za Kusadikika imeandikwa nyuma; " Mjini Usije Na Jembe". Mie niliyefika mjini jana nikitokea Uhambingeto ujumbe umenifikia.

Lakini, ajabu ya Wasadikika, hata wa mijini, ni kuwa kila mtu ana jembe lake!
Mwingine kwenye meza ya magazeti atalalamika kuwa hakuna habari ya maana. Ni kwa kuwa tu magazeti hayana habari zenye kumhusu ' jembe lake' .

Ajabu ya Msadikika unaweza kubishana nae sana juu ya jambo. Na ukimuuliza kwanini anang'ania hoja anayoshindwa kuipa nyama ikaeleweka, basi, atakujibu, kasema fulani; " Yule ni jembe langu bwana!"
Kwamba anashindwa kuelewa, kuwa si kila jembe lina makali ya kudumu. Na majembe mengine ni butu, na hayanoleki tena.

Raia makini ni yule anayesoma na kusikiliza ya wengine, lakini, mwenye kukaa chini na kutafakari. Kuchanganya na akili zake ili kujenga uelewa.
Bahati mbaya, Wasadikika wengi ni wavivu wa kuifanya kazi hiyo. Wasadikika huamini sana wanayoambiwa na wenzao akina Sadiki. Na wengine wamewapa hata vyeo; Ni majembe!
Maggid,
Dar es Salaam.(P.T)

Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

tangazahapa_copy_7ab8d.jpg

Maoni ya Wanakijiji

Zilizosomwa Zaidi

BLOG SHABIHANA