We have 200 guests and no members online

Mjengwa Blog

Mjengwa Blog

I am a writer, photographer, social entrepreneur, political analyst and a teacher- facilitator.

Website URL: http://www.mjengwablog.com

Ägypten Proteste für Demokratie 2013 Tote

Maandamano ya 2013 nchini Misri, watu 200 waliuwawa na wengine 4,500 kujeruhiwa katika uwanja wa Rab'a Al-Adaweya

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuacha mara moja mauzo ya silaha kwa Misri kutokana rekodi za ukiukaji wa haki za binaadamu kwa kuwa zinachochea mauwaji.

Katika taarifa mpya ya Amnesty inaeleza takribani nusu ya mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yamekiuka hatua ya usimamishaji wa kupeleka silaha nchini Misri na hivyo kusababisha hatari mbaya ya wimbi la mauwaji holela, watu kutoweshwa na mateso.

Mmoja wa maafisi wa Amnesty, Magdalena Mughrabi amesema ukandamizaji unaofanywa na vikosi vya ulinzi vya ndani vya taifa hilo umeendelea kuwa mkubwa, na hakuna uwajibikaji wowote kufuatia matatizo hayo.

Tuhuma kwa rais al-Sisi

Kwa ujumla ripoti yenyewe inamtuhumu rais Abdel Fattah al-Sisi kwa kuongoza nchi kimabavu na kwa ukandamizaji tangu kumuondoa madarakani mtangulizi wake, rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi mwaka 2013.

Amnesty, imesema mataifa 12 kati ya mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya yasalia kuwa wasambazaji wakubwa wa silaha na vifaa vingine vya matumizi kwa ajili ya polisi. Shirika hilo vilevile limesema hatua hiyo inakiuka makubaliono ya kusitisha kuipa silaha Misri ya umoja huo ambayo yaliridhiwa muda mfupi baada ya mauwaji ya mamia ya waanamanaji katika kile kilichoonekana kama matumizi makubwa kabisa ya nguvu kwa waandamanaji katika matukio ya Agosti 2013 nchini Misri.

Amnesty yenye makao yake makuu mjini London, Uingereza inasema hatua hiyo inaweza kufutiliwa mbali pamoja na kutokuwa na ufanisi.

Uidhinishwaji wa leseni za vifaa vya kijeshi

Kwa mwaka 2014 pekee, mataifa ya Umoja wa Ulaya yameidhinisha leseni 290 za vifaa vya kijeshi kwa Misri, vyenye gharama ya zaidi ya euro bilioni sita. Vifaa ambavyo mataifa hayo yaliviwasilisha kwa usafiri wa meli nchini humo ni pamoja na silaha ndogo ndogo, risasi, magari ya silaha, helkopta za kijeshi, silaha nzito na teknolojia ya ulinzi.

Pamoja na Marekani mataifa ya Ulaya yanayotajwa katika ripoti ambayo makampuni yake yanaingiza vifaa vya ulinzi ni pamoja nchini Misri ni pamoja na Uingereza, Ujerumani na Italia. Aidha taarifa hiyo imeyataja mataifa mengine kama Bulgaria, Cyprus, Jamhuri ya Czech, Ufaransa, Hungary, Poland, Romania, Slovakia na Uhispania.

Brian Wood, mkuu wa udhibiti wa silaha na haki za binaadamu wa Amnesty amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kusimamisha mara moja usafirishaji wake aina zozote za silaha na vifaa ambavyo vinatumiwa na Misri kufanya ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Hata hivyo kufuatia lawama hizo mataifa ya Umoja wa Ulaya na Marekani yamesema yataendelea na bisahara yao ya silaha kwa Misri kwa kuwa ni mshirika wao madhubuti katika kanda hiyo tete.DW

Inspekta wa polisi Kenya Kimaiyo

Polisi nchini Kenya inaendelea na msako wa kuutia mbaroni mtandao wa kundi la wapiganaji la ISIS ambalo linataka kukita mizizi yake nchini Kenya kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio kuwa na hatia. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi .

Kauli hiyo imetolewa baada ya polisi nchini Kenya kuwatia mbaroni watu wawili wanaoshukiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la wapiganaji la ISIS.

Kwa mujibu wa polisi, kukamatwa kwa wawili hao ambao ni Mwangolo Mgutu na Abubakar Jillo Mohammed kumezuia mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa yakipangwa kwa kutumia vilipuzi na silaha nyingine katika mji wa Nairobi na Mombasa.

Mbali na kukamatwa kwa washukiwa hao wawili, polisi pia imepata vitu mbalimbali katika nyumba ya Kiguzo Mwangolo kama vile misumari, betri, waya na mbolea ambazo inadaiwa zingetumika kutungezea bomu la nyumbani.

Polisi imeendelea kusema, katika uchunguzi wake wa mwanzo, imebaini kuwa Kiguzo na Abubakar ni miongoni mwa waandishi wa makala iliyokuwa inasambaa kupitia mtandao ambao ilikuwa ikielezea kuwepo kwa kundi la Jahba katika eneo la Afrika Mashariki ambalo limetangaza kumuunga mkono kiongozi wa ISIS Abubakr Al-Baghdadi.BBC

TC3

Kaimu Mkurugenzi Mamlakaya Mawasiliano Tanzania(TCRA)Mhandishi James Kilaba. 

Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika sekta ya mawasiliano  hadi kufikia kuwa kwenye kundi la  nchi zilizoendelea kimawasiliano Duniani.

Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania takribani milioni 39 wana laini za simu za kiganjani pamoja na watumiaji wa intaneti takribani milioni 20 ambapo miaka ya nyuma idadi ya laini za simu za kiganjani zilikuwa 2,963,737.

Haya ni maendeleo makubwa yanayoifanya Tanzania kuwa nchi bora kwa upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba alisikika akisema kwamba,”Ukuaji wa kasi wa sekta ya mawasiliano nchini umechangia sio tu katika kuboresha maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi bali unachangia sana katika kuinua pato la Taifa”.

Ukuaji huu umetokana na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za mawasiliano.

Kama wasemavyo wahenga kuwa ya Kaisari tumpe Kaisari basi sifa zote ziwaendee Mamlaka ya

 

Mawasiliano Tanzania kwa kazi nzuri wanazozifanya.

TCRA wana jukumu la kusimamia shughuli  hizo zote wakishirikiana na wadau wa mawasiliano nchini katika kusimamia na kuzitekeleza kwa makini sera,sheria na kanuni hizo ili kuwezesha kupatikana kwa huduma za mawasiliano nchini kote kwa kushawishi uwekezaji ,kusimamia vizuri ushindani pamoja na kutoa fursa sawa kwa watoa huduma.

TCRA inaendelea kuhakikisha kuwa rasilimali adimu zikiwemo za masafa na namba za simu zinatumika kwa makini ili kukidhi mahitaji ya Taifa na maendeleo ikiwa ni kutekeleza lengo la Serikali la kuwawezesha wananchi wote kupata habari na kuhakikisha hawaachwi nyuma katika maendeleo ndani ya karne hii ya utandawazi.

Huduma hizi za mitandao pia zimegawanyika kutokana na kutofautiana kwa mahitaji ya wananchi. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,  huduma za mitandao ni kama ifuatavyo; Intaneti, Benki Mtandao, Elimu Mtandao, Matibabu Mtandao,Biashara Mtandao, Malipo Mtandao pamoja na Mawasiliano Mtandao.

Huduma hizi zimekuwa zikirahisisha mambo mengi hasa ya kikazi na ya kijamii,ukiangalia kwa sasa ofisi zote za umma na za binafsi wanatumia huduma za mitandao katika kufanya shughuli zao zote za kiofisi kama njia salama ya kuhifadhi data zao.

Kwa ofisi za  Serikalini wameipa huduma hii jina la Serikali Mtandao (E-Government) ambapo watumishi wa umma wanashauriwa kutumia mtandao huu ili kuhakikisha kazi zote za ofisi zinafanyika katika hali ya usalama na usiri mkubwa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Mllao anasisitiza umuhimu wa watumishi wa Umma kupata mafunzo ya huduma za mitandao ili kuepuka matatizo yanayotokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wakuteleza majukumu yao.

“Tumegundua kwamba watumishi wanahitaji muongozo juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, hivyo tunashkuru sana uongozi wa TCRA kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wetu,”alisema Bi.Nuru wakati wa mafunzo ya watumishi kuhusu masuala ya mawasiliano.

Kwa upande mwingine, jamii inatumia huduma za mitandao kwa ajili ya mawasiliano kupitia intanenti ambapo kama tulivyosema hapo awali jumla ya wananchi milioni 20 wanatumia huduma za intanenti ambazo zinahusisha matumizi ya mitandao ya kijamii kama ya facebook, instagramu,WhatsApp, Forums, Linkedin pamoja na barua pepe katika kuwasiliana kati ya mtu mmoja na mwingine.

Matumizi hayo ya mitandao ya kijamii pia ni muhimu kwa wananchi kwa kuwa inatumika kama njia rahisi katika kupashana habari kwa haraka na kufanya dunia kuonekana kama kijiji kwani watu hupata habari za masafa ya mbali kwa haraka.

Kama tunavyojua “Kizuri hakikosi kasoro”, japokua matumizi ya huduma za mitandao yana faida nyingi lakini kuna baadhi ya madhara hutokea kama mitandao hiyo ikitumiwa vibaya.

Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy anasema kuwa ongezeko la watumiaji wa huduma za mawasiliano linaenda sambamba na ongezeko la vifaa mbalimbali vinavyowezesha mawasiliano hayo kufanyika.

“Miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na simu za kiganjani,vifaa vya mawasiliano ya kiganjani (tablets), kompyuta pamoja na modemu, kadri idadi ya watu na vifaa vya mawasiliano vinavyoongezeka ndivyo matumizi mabaya ya mitandao yanazidi kuibuka,”anasema Mungy.

Kuna baadhi ya wananchi ambao tunaweza kusema hawana maadili ya kutosha ambao wanatumia vibaya huduma hizi za mitandao kwa ajili ya kujinufaisha kwa njia zisizo za halali pamoja na kuupotosha umma kwa kutuma vitu ambavyo viko  kinyume na maadili ya mtanzania.

Matumizi mabaya ya mitandao yanapelekea kuwepo kwa madhara kama ya mauaji, wizi, ukiukwaji wa maadili, ugomvi na kutokuelewana katika jamii zetu.

Ili kuzuia madhara haya ni lazima kila mmoja azingatie matumizi sahihi ya huduma za mitandao. Mamlaka inayosimamia Huduma za Mawasiliano nchini imeelezea baadhi ya mambo muhimu ambayo yatasaidia kuimarisha usalama pindi utumiapo huduma hizo.

Unatakiwa kutotumia nywila (password) moja kujiunga kwenye mtandao zaidi ya mmoja wala kuweka nywila ambazo mambo yako binafsi ambayo yanajulikana kwa watu wengi ili kuzuia mtu mwingine asipate urahisi wa kubuni kuingia katika mtandao wa mtu mwingine.

Unashauriwa kubadilisha nywila mara kwa mara pamoja na kutengeneza nywila ambayo ina muunganiko wa namba na herufi ili isiwe rahisi mtu mwingine kuibuni pia nywila ni siri yako hushauriwi kumpa mtu mwingine yoyote.

Aidha, hutakiwi kuiandika sehemu yoyote kwa ajili ya kumbukumbu wala kukubali au kujibu barua pepe zinazotoka kwa watu usiowajua kwa kuwa wanaweza kutumia kama njia ya kufahamu  nywila yako.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania inawasisitiza wananchi kujifunza njia bora za kutumia mawasiliano hususani matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ili iweze kuwanufaisha na kuendelea kukuza uchumi wa nchi kuliko kuitumia vibaya hatimaye ikaleta madhara ambayo yatasababisha matatizo kwa mtu binafsi au Taifa kwa ujumla.

Watanzania tunatakiwa kubadilika kulingana na hali halisi ya maendeleo ya nchi yetu ambapo kwa sasa teknolojia ya huduma za mitandao inazidi kukua kwa kasi hivyo kurahisisha zaidi huduma muhimu.

Huduma hizi za mitandao ni kwa ajili ya wananchi wote, hatutakiwi kuziacha  zitupite kushoto.(P.T)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

TZ

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Nchini (CRB) kesho tarehe 26 Mei, 2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa mwaka wa mashauriano na wadau wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi unatarajiwa kuhudhuriwa na  zaidi ya Makandarasi na wadau wa Sekta ya Ujenzi wapatao 1000 na utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26 Mei, 2016 hadi tarehe 27 Mei 20l6.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Juhudi za Makusudi za Kukuza Uwezo wa Makandarasi Wazalendo kwa Maendeleo Endelevu ya Kiuchumi; Changamoto na Mustakabali Wake’.

Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau wa Bodi ya Usajili Makandarasi na Sekta ya Ujenzi ili kujadili changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kuwajengea uwezo Makandarasi Wazalendo.

Imetolewa; Eng. Joseph M. Nyamhanga

Katibu Mkuu (Ujenzi)

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

25 Mei, 2016 (P.T)

Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Wanakijiji

BLOG SHABIHANA