We have 338 guests and no members online

Znateli
Tokeo la picha la nasa supporters
Wafuasi wa NASA wameanza kuwasili katika viwanja vya Uhuru Park tayari majira ya saa 11 alfajiri kusubiri tukio la kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa rais wa jamhuri ya Kenya.  

Msemaji mkuu wa NASA Bw. Norman Magaya amesema zoezi la kuapishwa kwa Odinga litamalizika majira ya saa 7 mchana.

Posted On Tuesday, 30 January 2018 06:54
Tokeo la picha la nasa supporters busea

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na gazeti la Daily Nation la nchini humo zinasema mabasi yaliyokamatwa yalikuwa ni miongoni mwa mabasi sita yaliyoondoka Mombasa kuelekea Nairobi, ambayo yaliwabeba wafuasi wa NASA kwenda Nairobi kushudia tukio la kuapishwa kwa Raila Odinga na Kalonzo Musyoka.

Posted On Tuesday, 30 January 2018 06:32

Tokeo la picha la ETTIOPIA STRIKES

Wakati mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Afrika AU, ukiendelea mjini Addis Ababa Ethiopia chini ya mwenyekiti wa Umoja huo Paul Kagame, kwa upande mwingine Maandamano yameripotiwa na vyombo vya habari nchini humo ambapo watu kadhaa wameripotiwa kuuwawa katika ghasia hizo zilizofanyika kaskazini mwa nchi hiyo.

Posted On Monday, 29 January 2018 14:04

   Picha inayohusiana

Kiongozi wa mungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Jamhuri ya Kenya Jumanne ya tarehe 30 January. Kuapishwa huko kunatokana na upinzani nchini Kenya kutokukubaliana na ushindi wa rais Uhuru Kenyatta aliyechaguliwa mwishoni mwa mwaka uliopita, ingawa upinzani haukushiriki duru ya pili ya uchaguzi baada ya matokeo ya uchaguzi wa awali kukataliwa na mahakama.

Posted On Monday, 29 January 2018 13:22

Kwa mara ya kwanza tangu kurejea nchini Tanzania, balozi mteule Dkt Wilbroad Slaa amekutana na kufanya mazungumzo na rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao na Rais, Dkt Slaa amesema ameamua kukubali kufanya kazi na Rais baada ya kuridhika na kazi kubwa inayofanywa na Rais kwa wananchi.

Posted On Monday, 29 January 2018 13:04

Tokeo la picha la fire break in langata nairobi

Watu wanne wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya moto uliotokea usiku wa kuamkia leo January 29 katika mtaa wa Kijiji eneo la Langata-Nairobi, huku wengine wakiripotiwa kukesha baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa moto.

Kwa mujibu wa Maafisa wa serikali nchini humo, nyumba 6,000 makazi ya watu karibu 14,000 ziliharibiwa na moto huo.

Posted On Monday, 29 January 2018 12:06

Picha inayohusiana

Waziri wa mifugo na uvuvu Luhaga Mpina amesema uvuvi haramu ni moja kati ya majanga yanayomaliza rasilimali za wananchi ambazo zingetumika kufanya shughuli nyingine kama uwasomesha watoto.

Posted On Monday, 29 January 2018 04:50

media

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress na kiongozi wa Palestina pia wamehotubia mkutano huo. Wakati mkutano huo, rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi yake inawaheshimu Waafrika, na hivi karibuni itatuma mjumbe wake katika bara hilo.

Posted On Sunday, 28 January 2018 22:09

Meli iliyokuwa na manusura (L) na meli ya uokozi katika bahari ya Pacific. Januari. 28, 2018.

Kikosi cha anga cha New Zealand kimewagundua Jumla ya watu sita akiwemo mtoto mmoja, waliokutwa wakiwa hawajitambui baada ya kuelea kwenye maji zaidi ya wiki moja katika boti ndogo ya mbao katika bahari ya Pacific.

Posted On Sunday, 28 January 2018 22:03

Tokeo la picha la RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA JAJI KISANGA

Tokeo la picha la RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA JAJI KISANGA

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Bi.Mama Janeth Magufuli, wameyaongoza mamia ya waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Jaji mstaafu Robert Kisanga ambaye alifariki Dunia mwezi January 23 mwaka huu.

Posted On Sunday, 28 January 2018 16:08

Picha inayohusiana

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewasimamisha kazi Afisa mifugo wa wilaya ya karatu, mtendaji wa kijiji na Afisa mifugo wa kijiji. Gambo amechukua hatua hiyo baada ya watendaji hao kushindwa kusimamia vizuri zoezi kupiga chapa mifugo ambalo pia ni la kitaifa, na kuagiza katibu tawala wa mkoa kuwaandikia barua ya kuwaonya mkurugenzi na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu

Posted On Sunday, 28 January 2018 15:34

Deutschland | Polizei löst Kurden-Demo in Köln

Chanzo, DW.

Jeshi la Polisi nchini Ujerumani limewatawanya  waandamanaji takribani 15,000 wa kikurdi waliokuwa wamebeba mabango yanayoonesha  nembo  za  chama  cha  wafanyakazi wa  Kikurdi PKK, zilizopigwa marufuku  nchini  humo.

Posted On Sunday, 28 January 2018 12:59

Tokeo la picha la igp simon siro

Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Simon Siro amesema jeshi la polisi limefanikiwa kuimarisha amani nchini kwa kuwakamata wahalifu huku baadhi yao wakikimbilia nje ya nchi hasa Msumbiji. IGP Siro alipokuwa akiongea na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam, kuwajulisha hali ya utulivu iliyopo imechangiwa na mahusiano na uhirikiano ulioonyeshwa hasa kipindi cha changamoto kubwa kwenye maeneo ya Kibiti na Ikwilili.

Posted On Sunday, 28 January 2018 03:42

Tokeo la picha la juma nyosoMkurugenzi wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema sakata la Juma Nyoso kumpiga shabiki wanaliacha chini kamati ya nidhamu ambayo mpaka sasa bado inaendelea na uchunguzi ili kutolea uamuzi wa mwisho.

Posted On Sunday, 28 January 2018 03:34

Tokeo la picha la Deadly blast rocks Kabul

Watu 95 wamepoteza maisha na wengine 158 kujeruhiwa katika shambulio la kubwa la kigaidi katika mji mkuu wa Afghanistan -Kabul.

Kundi la kigaidi la Taliban limehusishwa kutekeleza shambulio hilo ambalo ni la tatu kutokea katika kipindi cha muda wa siku saba zilizopita.

Posted On Saturday, 27 January 2018 16:48
Page 8 of 2110

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji