We have 132 guests and no members online

Simu

 

President Uhuru Kenyatta gestures to supporters as he leaves the last Jubilee Party campaign rally ahead of the August 8th election in Nakuru, Kenya

Rais Kenyatta ta matumaini ya kuchaguliwa tena

Utulivu unashuhudiwa nchini Kenya baada ya kampeni kali wakati nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa siku ya Jumanne.

Miaka 10 iliyopita zilishuhudiwa ghasia mbaya nchini humo ambazo hakuna mtu angependa zirudie tena.

Posted On Monday, 07 August 2017 06:04

PICHA ONE

Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo

Posted On Monday, 07 August 2017 06:02

IMG_6028

Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Deodatus Alexander akimkabidhi kitambulisho chake Bw. Abrahman Mohamed Mussa, akiwa miongoni mwa wananchi waliokamilisha taratibu za Usajili na kukabidhiwa Vitambulisho vyao wakati wa maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo Lindi.

Posted On Monday, 07 August 2017 05:58

01

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiwasili Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) Tunguu kufungua kambi ya matibabu ya macho ya siku tano inayosimamiwa na madaktari kutoka Chuo Kikuu cha Lahore Pakistan na madaktari wazalendo, (kulia) Mkuu wa Chuo cha ZU Dkt. Mustafa Rashashi.

Posted On Monday, 07 August 2017 05:56

IMGL8852

Mshauri wa Bunge wa Mambo ya Sheria, Ndg. Everyne Shibandiko (kushoto) akitoa maelezo kuhusu Chimbuko la Bunge pale wageni Mbali mbali walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzunguni Mjini Dodoma.

Posted On Monday, 07 August 2017 05:55

unnamed

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi tawi la NMB Ikungi.

Posted On Monday, 07 August 2017 05:51

Image may contain: 1 person, smiling, outdoor and food

Shida wenye kuitumia hawasemi kuwa ni picha ya Mwenyekiti!

 

Posted On Monday, 07 August 2017 05:12

Image may contain: 1 person, standing and text

 

Posted On Monday, 07 August 2017 05:10

Image may contain: 3 people, people smiling, people eating, people sitting, table and foodNdugu zangu,

Pichani tulipokaribishwa kwa Mama Chonya, Wilolesi, jana mchana. Mama Chonya amekuwa mwalimu wa hesabu na Sayansi kwa watoto wetu wote. Kwa wote wanne hakuna aliyefeli somo la hesabu na Sayansi.

Maggid

Posted On Monday, 07 August 2017 05:08

Image may contain: 2 people, people sitting, tree, outdoor and natureNdugu wa kwenye mapambano. 
Pichani nikiwa na ndugu yangu, Dr Bukaza Chachage. 
Kambi hii ilipigwa kando ya mto ruaha, iringa.

Maggid,

Iringa.

 

Posted On Monday, 07 August 2017 05:04

Image may contain: 1 person, eyeglasses, sunglasses and closeupNdugu zangu, 

Hata kama hana mdomo wa chuchunge, Ben Mkapa amekuwa na kauli za moja kwa moja. Mkapa hana kawaida ya kumung'unya maneno.

Kama anakuona wewe mjinga na mpumbavu atakwambia kuwa wewe ni mjinga na mpumbavu!

Akiwa Waziri wa Habari na Utangazaji, na huku yeye mwenyewe akiwa mwanahabari na aliyewahi kuwa Mhariri wa Gazeti la Serikali, Ben Mkapa asubuhi moja ya Desemba 5, 1992 alialikwa kwenye Semina ya kuadhimisha miaka 30 ya gazeti la Chama, Uhuru.

Haikuchukua muda, kwenye hotuba yake Mkapa akawavaa wanahabari kwa kuwaambia waache kuandika habari za hotuba za viongozi, badala yake waandike habari za wananchi na maoni ya wananchi.

Kama haikutosha, Ben Mkapa akawarushia Wanahabari wale ukumbini kombora lingine kwa kuwaambia waache tabia ya kupokea bahasha.

Siku tatu baadae, wanahabari wakajipanga kujibu mapigo ya Waziri wao wa habari, Ben Mkapa. Ni kupitia Tanzania Journalists Association ( TAJA).

Daily News la Desemba 9, 1992, Siku ya Uhuru, likaripoti kuwa Wanahabari kupitia TAJA wamesikitishwa na alichokisema Waziri Mkapa, na kwamba walitaka ufafanuzi wa kauli yake kutoka kwa Mkapa mwenyewe.

Mpaka hii leo, sikuwahi kusoma mahali popote ufafanuzi wa Ben Mkapa kwa wanahabari.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
 
 
Posted On Monday, 07 August 2017 05:02

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing, child, wedding and outdoor

Image may contain: one or more people, people standing and outdoor

 

Ndugu zangu,

Kuna wajumbe wameona picha hiyo ya kulia na kuuliza watoto hao ni akina nani?

Anayeonekana pichani anaitwa Ipelanya Kulwa, wa kwanza kushoto kwenye picha ya pili. Pichani ni Harare, Zimbabwe, Desemba, 1989.

Ipelanya alikuwa mdogo sana wakati huo, labda miaka 9 au 10. Mapema mwaka 2014 niliiweka picha hiyo kwenye mjengwablog na ukurasa huu wa fb. Sikujua kama Ipelanya ni mjumbe wangu, naye akajitambua kwenye picha hiyo.

Akanipigia simu. Alishangaa sana kuiona picha yake ya utotoni. Hakuwa hata na kumbukumbu kuwa nilipata kutembea nae kwa miguu mitaa ya Harare akiwa na mtoto mwenzake.

Na mimi niliiweka picha hiyo bila kuwa na kumbukumbu ya majina ya watoto hao. Na bado ningependa kujua huyo mtoto wa pili ni nani, na yuko wapi sasa. Ipelanya atusaidie.

Ipelanya aliponipigia simu alitaka kujua zaidi ya wakati huo. Nakumbuka Baba yake alikuwa Mtaalamu wa mawasilino ya simu. Wakati huo, Zimbabwe iliomba wataalamu wa maeneo mbali mbali kutoka Tanzania.

Na hakika, Zimbabwe ilikuwa nchi changa sana.Ilikuwa na miaka 6 tu ya Uhuru. Na mimi nilikuwa ndio kwanza nimemaliza Form Four pale Tambaza Sekondari.

Tangu enzi nikiwa shuleni , nilipenda sana kufuatilia masuala ya harakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika. Nilifika Lusaka pia, Zambia. Hapo kulikuwa na Makao Makuu ya ANC.

Nikiwa Zimbabwe sikuishia Harare tu, nilifika maeneo ya vijijini pia. Nilifika Nyanga, Mberengwa, jirani na mpaka wa Msumbiji, na hata Bulawayo.

Nikiwa Nyanga niliona nini maana ya jamii zilizokuwa zikiishi katika mifumo ya kibaguzi. Mji unakuwa na sehemu mbili; ya Wazungu na Weupe. Kwenye Township ndiko walikoishi Makabwela.

Kwenye moja ya kijiji nilichokaa kwa siku kadhaa kule Mberengwa, jirani na Msumbiji, nilisikia simulizi nyingi za wapiganaji wa Renamo waliokuwa wakivuka mpaka na kufika hata kwenye vijiji hivyo vya mpakani kuiba vyakula vya wenyeji.

Kwenye Maktaba yangu bado nina picha kadhaa za wakati huo. Moja nimepiga nje ya nyumba ya familia ya Ipelanya Harare, picha inaonyesha nikiwa na dada yake Ipelanya.

Dada wa Ipelanya alikuwa mrembo haswa. Kijana Ipelanya ameniambia dada yao amebaki Zimbabwe na ameolewa huko, miaka yenda mbio kweli!

Hongera Ipelanya kwa kufunga ndoa! Ni imani yangu, kuwa ndoa hiyo imeshadumu kwa miaka mitano sasa.

Na inastahili hongera ya mwenyekiti. Kule Zimbabwe wanasema Makorokoto!
Maggid,
Iringa.

Posted On Sunday, 06 August 2017 19:17

Image may contain: 5 people, people smiling, people standing, shoes and childAmeniambia mpiga picha; " Baba Olle ngoja nichuchumae. Nikisimama nao nitatokea mfupi wakati niliwapokea shuleni wakiwa wadogooo!"

Posted On Sunday, 06 August 2017 19:16

Image may contain: 4 people, people sitting, shoes and indoorNdugu zangu, 
Anaitwa Mama Chonya, watoto wetu wote wamepitia mikononi mwake kwenye masomo ya sayansi na mathematics, Iringa International School.
Olle na John wamekuja na zawadi kwa mwalimu wao ambaye sasa ni mstaafu. Gustav na Manfred wanachukua nafasi hii kumuaga rasmi mwalimu wao. Wanakwenda masomoni Sweden wiki ijayo.
Maggid.

Posted On Sunday, 06 August 2017 19:14
Page 9 of 2023

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart