We have 133 guests and no members online

Simu

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing and suitNdugu zangu,

Mume wa Anna Tibaijuka aliitwa Wilson Tibaijuka.

Wilson alikuwa rafiki yangu wakati akiwakilisha nchi yetu kama balozi Sweden, Norway, Denmark na Finland. Nami nilikuwa nikiishi Sweden.

Wilson alikuwa Balozi kijana, makini na aliyekwenda na wakati. Sikushangaa hakuona shida mkewe kujiingiza kwenye uanaharakati na hata kupambana na dola wakati Wilson ni Balozi.

Wilson alihakikisha napata telex zote zinazotumwa balozi zetu nje kutokea Foreign Affairs Dar.
Mara nyingi alitaka nisome na tujadili.

Angekuwa hai leo, naamini Wilson angekuwa mwanadiplomasia mahiri na mwenye uzoefu mwingi wa kusaidia taifa.

R.I. P Wilson.
Maggid,
Iringa.

 

Posted On Sunday, 06 August 2017 14:05

Image may contain: 1 person, smiling, crowd and outdoor

Image may contain: one or more people

 

Tuliokuwepo tunakumbuka. Ambao hamkuwepo historia ni mwalimu mzuri. Tusome historia yetu.

Maggid.

Posted On Sunday, 06 August 2017 14:03

No automatic alt text available.

Image may contain: one or more people, people standing and outdoor

 

Ndugu zangu,

Hiyo ni passport yangu ya tangu enzi hizo. Picha ya pili nikiwa Harare 1988. Nilifika tena Harare 1996 na gamba hilo pichani.

Kaka yangu wa tangu Tambaza Boys, Hassan Chikusa, yeye alivuta gamba mwaka huo huo wa 1992, na alipasua mpaka Jo, Berg. Ana kesi ya Jamhuri ya kujibu!
Maggid,
Iringa.

Posted On Sunday, 06 August 2017 14:00

No automatic alt text available.Ndugu zangu,

Hati hii ya kusafiria nilikabidhiwa Juni, 1992. Kabla ya hapo nilishakuwa nimesafiri kwa hati ya muda kwenda Harare, Zimbabwe, 1988.
Hati hiyo hapo juu iko kwenye maktaba yangu.

Tumetoka Mbali.

Maggid,
Iringa.
 
 
Posted On Sunday, 06 August 2017 13:57

Ndugu zangu,

Anayenisimanga Nyeregete asubuhi, jioni nitasikia, popote nilipo. 
Karibu kila mwanakijiji Nyeregete ana mahusiano na ukoo wa Mjengwa.

Pichani nikiwa na wazee wa kijijini Nyeregete, 1992. 
Maggid,
Iringa.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:34

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:31

media

Wafuasi wa vyama vya siasa nchini Kenya wakishangilia kwenye moja ya mikutano.

Kampeni za kuwania kiti cha urais nchini Kenya zimetamatika rasmi siku ya Jumamosi Agosti 5 kwa wagombea wa kiti hicho kumaliza kampeni zao wakiwataka wananchi wa wachague kuhudumu katika Serikali ijayo.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:26

Image result for bomba la mafuta tanga

Na: Judith Mhina – MAELEZO

Hakika historia imejirudia, mkoa wa Tanga ni kati ya mikoa mashuhuri nchini Tanzania kabla ya uhuru wa Tanganyika katika kupigania uhuru, kwa kuwa ni mkoa uliokuwa na wasomi wengi kuliko mikoa mingine wakati huo.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:23

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Serikali wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akikabidhi sehemu ya jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) zilizotolewa na NMB kuchangia Tamasha la Usalama barabarani linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:20

L1

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) Romanus Mwang’ingo akielezea jambo mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhadisi Gerson Lwenge (wa pili kushoto) wakati wa ziara yake ya kugagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ugawaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani jana.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:19

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisoma na kupata maelezo mbalimbali kuhusu ufanisi katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:16

IMG_5071

Meneja wa Mradi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha, Julius Lenguyana (kulia) akimuongoza Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) alipowasili chuoni hapo kuangalia utekelezaji wa mradi wa ufadhili wa wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake kwa miaka mitano katika Chuo hicho.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:14

DSC_0443

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey W. Zambiakipewa Maelezo na Afisa Vipimo juu ya Mizani ya iliyoundwa na Watanzania.

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:13

1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.

3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pongezi na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga

Posted On Sunday, 06 August 2017 04:11
Page 10 of 2023

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart