We have 190 guests and no members online

Simu

 

Mudde-injury-2

Watazamaji 7,412 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Toto Africans lililochezwa jana (Machi 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 42,508,000. Mechi hiyo namba 135

Posted On Sunday, 10 March 2013 14:59

 

07Mkuu wa Wilaya ya Mfia Sauda Mtondoo akimkabidhi  Prudence Nyombi zawadi ya King’amuzi cha Star timu baada ya kujishindia kutokana na kujibu swali aliloulizwa juu ya matumizi ya Mawasiliano, wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika Wilayani Mafia.katikati ni Mkurugenzi wa Watumiaji na Watoa Huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema akishuhudia.

Posted On Sunday, 10 March 2013 14:51

162

NA BASHIR NKOROMO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana anaondoka nchini leo Machi 10, 2013, kwenda Jamhuri wa Watu wa China kwa ziara ya kikazi ya siku kumi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) cha nchi hiyo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro  amesema leo kwamba katika ziara hiyo Kinana atakuwa na msafara wa  watu 14, ambao baadhi yao ni Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM, Makatibu wakuu wa Jumuia za Chama na Wenyeviti wa Chama wa mikoa.

 

Posted On Sunday, 10 March 2013 11:02

No comments

martina

Na Mwandishi wetu

………………………………………………..
KAMPUNI ya  Advanced security Limited imeingia  makubaliano na bingwa wa dunia wa mchezo wa Kareti,  Profesa Maurizio Martina wa Italia kwa ajili ya kutengeneza filamu mbalimbali pamoja na ile inayopinga mauaji ya walemavu wa ngozi, albino na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.
Makubaliano hayo yalifanyika jana kwenye hotel ya JB Delmonte na filamu hiyo itaanza kurekodiwa ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na kukamilika kwa miezi mitatu.

Posted On Sunday, 10 March 2013 10:59

photo d67bd

Bomba mbili hapa

Posted On Sunday, 10 March 2013 10:53

Photo: Tukumbushane Neno; Falsafa Ya Mtungi..
Ndugu zangu,
Asubuhi moja nikiwa kwenye mchakamchaka ( jogging)  nilimsikia mchungaji wa kanisa akiwatamkia waumini wake; 
“ Angalieni upepo, nguvu ya upepo. Duniani upepo unaweza kutingisha miti, ukavunja matawi na hata ukaangusha miti….!” Sikusimama nikasikiliza alichotaka kusema Mchungaji yule juu ya upepo na nguvu zake. Lakini, nami nikaanza kutafakari na kujiuliza; Matatizo yetu wanadamu na hasa sisi Watanzania ni nini? 
Nikafikiri, kuwa mara nyingi Watanzania hatutaki kuyajua matatizo yetu. Tunataka kuyajua ya wenzetu. Na tukiyajua yetu, hatutaki kuyaweka wazi. Tu mahodari wa kusiliba matatizo yetu. Nje hayaonekani, yamesilibiwa, lakini, ndani hali iko vile vile. 
Tuliokaa vijijini tunajua, kuwa nyumba ya kijijini haijakamilika bila kuwa na mtungi. Afrika hakuna tu siri ya mtungi, kuna falsafa ya mtungi pia. Ninapoingia kwenye nyumba kijijini huangalia kwanza ulipo mtungi. 
Kwenye mtungi yawezekana ndimo yalimo maji ya kunywa. Na ukiinamia mtungi wa maji, usiaangalie sana, chota maji yako, kunywa. Lakini, mtungi pia hutumika kuhifadhia vyakula; iwe unga au maharage. Mara nyingi mtungi huwekwa kwenye kona ya chumba. Na mtungi ukikaa sana, basi, siku ukiinuliwa, huacha alama.
 Na unafanyaje basi mtungi wa maji unapoonyesha kuwa na nyufa, kuwa maji yameanza kuvuja? Kuna mawili; la kwanza si la busara sana. Ni jawabu la muda mfupi, la pili ni la busara zaidi, ni suluhisho la muda mrefu. 
Afrika mtungi wenye nyufa unaweza kuzibwa kwa kusaga vipande vya mtungi wa zamani, kisha ukachanganya na nta. Baada ya hapo utasiliba kwenye nyufa za mtungi. Hiyo ni njia ya kwanza, ni suluhisho la muda mfupi.
Maana, tabu inakuja, siku mtungi utakapohitajika kuchemshia ‘ komba’- togwa la pombe. Basi, kwenye moto mkali wa kuni nyufa zile, pamoja na kusilibwa na nta, hazitahimili nguvu ya moto. Mtungi utamegeka vipande vipande. ‘ Komba’, ama togwa la pombe litamwagika. 
Naam, dawa ya mtungi wenye nyufa si kusiliba kwa nta, ni kufinyanga mtungi mpya, basi. Na jamii yetu imekuwa ni kama ya ‘ Super- glo’, ile gundi inayoaminiwa inaweza kusiliba , ama kuunga chochote kile. Kila jambo tunakimbilia kuitafuta ‘ Super-glo’. Kama nta, Super-glo nayo haihimili kwa muda mrefu joto la moto, au hata la jua. 
Wanadamu tuwe na ujasiri wa kuyatambua matatizo yetu kama yalivyo. Tusiwe wepesi wa kukimbilia ‘ kusiliba’ kwa nta au super-glo. Mengine ni ya kuyafanyia mabadiliko ya jumla. 
Natamani nikutane na Mchungaji yule wa Kanisa, aniambie, kuwa kwake alikuwa na maana gani aliposema kuwa upepo ni tatizo. Tafakari. 
Maggid Mjengwa, 
Iringa. 
0788 111 765
<a href=
Ndugu zangu,
Asubuhi moja nikiwa kwenye mchakamchaka ( jogging) nilimsikia mchungaji wa kanisa akiwatamkia waumini wake;

“ Angalieni upepo, nguvu ya upepo. Duniani upepo unaweza kutingisha miti, ukavunja matawi na hata ukaangusha miti….!” Sikusimama nikasikiliza alichotaka kusema Mchungaji yule juu ya upepo na nguvu zake. Lakini, nami nikaanza kutafakari na kujiuliza; Matatizo yetu wanadamu na hasa sisi Watanzania ni nini? 

Posted On Sunday, 10 March 2013 06:32

l 001 63ed9

Posted On Sunday, 10 March 2013 05:18

Photo: Good Morning Africa, Good Morning The World!
Kibwe village, Morogoro, this morning.

 Good Morning Africa, Good Morning The World!
Kibwe village, Morogoro, yesterday morning.

Posted On Sunday, 10 March 2013 04:01

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, . Picha na OMR.

 

Posted On Sunday, 10 March 2013 03:54

oxoxox e4b07

TGNP kwa kushirikiana na wanaharakati wa masuala ya haki  na usawa wa Kijinsia, haki za Binadamu, Demokrasia, Utawala bora na Maendeleo  wameungana na wanaharakati wengine duniani katika kusherehekea na kutafakari maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ili kuwezesha jamii kutambua mchango wa wanawake  kisiasa, kijamii na kiuchumi na matokeo ya harakati zao, changamoto zinazowakabili wanawake na kuendelea kutafakari mbinu za kuboresha kwa kipindi cha baadae.

Posted On Saturday, 09 March 2013 18:37

 IMG_6109

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akizungumza na wananchi
wa Machui Wilaya ya Kati Unguja,baada ya kuangalia maendeleo ya hatua
za mwanzo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa tangi la maji safi,akiwa katika
ziara ya Mkoa wa \Kusini Unguja jana,(kulia)Waziri wa
Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati,Ramadhan Abdalla Shaaban,[Picha na
Ramadhan Othman Ikulu.]

 

Posted On Saturday, 09 March 2013 18:30

04 07c23

Kikundi cha Tarab cha Bigstaa kikisubiri kutumbuiza katika kilele cha siku ya wanawake Duniani,huko Kijito Upele Fuoni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

05 4548f

Posted On Saturday, 09 March 2013 15:13

Morogoro, leo mchana huu. Darasa lina mchanganyiko wa vijana na wazee. Limechangamka.

Posted On Saturday, 09 March 2013 13:39

DSC_0225

Katibu wa Jumuiya ya FaweZanzibar Dkt.Mwatima Abdalla akizungumza na wazee na wanafunzi kabla ya kuwakabidhi msada wa fedha zilizotolewa na Al-Amana ya Dubai kupitia Jumuiya ya FaweZanzibar.

 

 

Posted On Saturday, 09 March 2013 13:32
martha-karua-campaigns d989f
 
I and my Running mate Hon. Lotodo, wish to formally congratulate Hon. Uhuru Kenyatta, the President Elect of the Republic of Kenya together with his running mate Hon william Ruto. Kenyans have spoken and we respect their decision. We had pledged to abide by the results of the electoral process and hereby keep that promise to Kenyans. We wish the incoming government well and urge them to uphold the constitution. We are embarking on a great moment in history and We have been honored to be a part of this historic election and the transition into the new dispensation. To my family, my mother and my father my supportive siblings and my extended family- thank you for your
Posted On Saturday, 09 March 2013 09:33

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart