We have 75 guests and no members online

Maji
×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 648

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 647

779 4597316803710 307443258 n b3a98

Shati linafuliwa, linapigwa pasi, linawekwa sandukuni. Linasubiri mkesha mwingine wa Mwaka Mpya. Kwanini uhangaike kununua mashati ya sikukuu ya mwaka mpya kila mwaka wakati unaweza kuwa nalo moja hata kwa miaka mitano, kama mimi!

Posted On Tuesday, 01 January 2013 06:59
IMG-20130101-00103 b30a3
Posted On Tuesday, 01 January 2013 06:03
100 4441 18b90
Mafinga hapa,gari imebuma
Posted On Tuesday, 01 January 2013 04:47

100 4613 e2246

Kijijini Madibira, juma la juzi

Posted On Tuesday, 01 January 2013 04:36

banda cdb62

Na: George Njogopa

SIKU chache baada ya viongozi wa dini wa madhehebu ya Kikristo nchini Malawi na Tanzania kuwasiliana kwa lengo la kutaka wajadili mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo mbili, Serikali ya Tanzania imezuia mjadala huo, Mwananchi imeelezwa.

Viongozi hao wa dini, Baraza la Wakristo Tanzania (TCC) na Baraza la Wakristo Malawi (MCC) walitangaza kujiingiza kwenye mgogoro huo wakitaka washirikishwe kama wasuluhishaji  katika kile walichoeleza kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu bila suluhu yoyote.Hata hivyo Serikali ya Tanzania imepinga wazo la viongozi hao kwa maelezo kuwa suala la mzozo huo limefikishwa kwa mpatanishi maalumu ambaye amekubaliwa na pande zote mbili.

Posted On Tuesday, 01 January 2013 04:12
IMG-20130101-00111 c1a95
Posted On Tuesday, 01 January 2013 03:57

MANISPAA ya Kinondoni  imeahidi  kuongeza nguvu katika kushughulikia masula ya migogoro ya ardhi , huku pia ikiwataka wananchi kutoa ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya watu wote wanaokwenda kinyume na utaratibu uliopo.Akizungumza na jiji Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus Fwema alisisitiza kuwa katika  kukabiliana na migogoro hiyo, uongozi wa manispaa umekuwa ukichukua hatua za haraka kuhakikisha  viongozi na watendaji wanaojihusisha na migogoro na kashfa za ardhi wanachukuliwa hatua mara moja.

Posted On Tuesday, 01 January 2013 04:06
kp31122012 475ec
Posted On Tuesday, 01 January 2013 03:57

100 4640 8c2c1

Na:  Hussein Semdoe, Handeni

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amebainisha kuwa, wilaya zaidi ya 45 nchini ziko hoi kwa ukosefu wa  chakula, sababu ikielezwa kuwa ni kukithiri kwa ukame.Waziri huyo amewaonya wafanyabiashara kuwa na utu kwa kuacha kuwaumiza wananchi kwa kupandisha bei ya chakula.

Akihutubia wananchi katika vijiji mbalimbali vya Kata za Kwamsisi, Kwasunga na Kwaluguru, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Dk Kigoda alisema kuwa, wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya kati ya 45 nchini, zinazokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, kutokana na eneo hilo kukumbwa na ukame mkali, hivyo kusababisha baadhi ya wakazi wake kula mboga za majani.

Kufuatia upungufu huo wa chakula, kumesababisha mfumko mkubwa wa bei ya mahindi na unga wa sembe kuwa juu, ambapo, Handeni gunia moja la kilo 100 za mahindi limefikia kuuzwa kati ya Sh90,000 hadi Sh100,000, kiwango ambacho hakijawahi kutokea wilayani humo.

Dk Kigoda ambaye pia ni Mbunge wa Handeni, alikutana na changamoto kubwa ya wananchi kumlilia chakula cha msaada ama kinachoweza kuuzwa kwa bei nafuu vijijini, wakidai wengi wao wanakula mlo mmoja kwa siku au kukosa kabisa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwamsisi, Athumani Mwagahazi, alimweleza waziri huyo kuwa, wananchi wengi katika eneo hilo sasa wanaishi kwa kula maembe ya kuchemsha pamoja na majani ya mchunga.

Akizungumzia hali hiyo Dk Kigoda aliwaeleza wananchi hao kwamba, Serikali inatarajia kusambaza chakula kinachotarajiwa kuuzwa kati ya Sh700 hadi Sh850 kwa Mkoa wa Tanga, ambao unatarajiwa kuwafikia wananchi wiki hii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Hassan Mwachibuzi, alisema kwamba wanatarajia kupata tani 150 za unga wiki hii, utakaouzwa Sh750 na 900 kwa kilo moja vijijini katika Mkoa wa Tanga.

Mwachibuzi alisema bei hizo zinatofautiana kutokana na gharama za usafirishaji kutoka Jijini Dar es Salaam na maeneo ya mkoa huo, akisema kwa wilaya ya Handeni ambayo ndiyo iliyopo karibu na jiji hilo, kitauzwa na wafanyabiashara kwa bei ya Sh750.

Posted On Tuesday, 01 January 2013 03:46

2013-Wallpaper-HD-10 e3cc7

Kwa jamii ya ndugu zangu wahaya,kila mwaka huwa unapewa jina lake.sifahamu hasa historia ya jambo hili,ila ninajua tangu uhuru kila mwaka unalo jina.ni jukumu la wahaya kutufafanulia nini maana ya mwaka kupewa jina.huu mwaka mpya 2013 unaitwa WEBANGE.haya mwenye kujua tafsiri na atuambie maana.

Posted On Monday, 31 December 2012 21:45

546436 4592685127921 1518475066 n 0e58d

Mkesha ukimalizika linarudi sandukuni. Lina miaka mitano sasa!

Posted On Monday, 31 December 2012 21:54

Photo: Salamu Za Mwaka Mpya Kutoka Mjengwablog!
Ndugu zangu, 
Imekuwa ni utamaduni wangu kutuma salamu za Mwaka Mpya kwa wanakijiji wa Mjengwablog, marafiki zangu kwenye FB na wengine walio ndani na nje ya mitandao ya kijamii.
 Nimefanya hivyo tangu mwaka 2006 ilipoanzishwa Mjengwablog. Na mwaka huu naendeleza utamaduni huo. Nina mambo makubwa mawili kwenye salamu za mwaka huu, lakini, nitaanza salamu hizi kwa kukumbushua ahadi muhimu ya Mwana –TANU; kwamba; 
 ” Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa manufaa ya wote”. 
 Ndugu zangu, 
Siku kama ya leo miaka 30 iliyopita nilikuwa ndani ya garimoshi la Tazara nikielekea Dar kutokea kijijini kwetu Nyeregete. 
Nikiwa Nyeregete kwenye likizo ndefu ya kusubiri matokeo ya Kidato cha Nne, zilinifikia taarifa kuwa nahitajika haraka Dar es salaam kwenda kufanya maandalizi ya kuanza Kidato cha Kwanza shule ya Sekondari Tambaza. Masomo yetu pale Tambaza yalianza Januari 13, 1983. 
 Siku kama ya leo miaka 30 iliyopita nilivuka kwa kuogelea korongo la Lihamile ili kuifikia Rujewa na hatimaye stesheni ya Tazara kule Ihanga. Korongo hilo lilijaa maji ya mvua ya masika yaliyokuwa yakipita kwa kasi. 
Hakukuwa na daraja. Baadae likajengwa daraja la magogo wakati wa kipindi cha Ubunge wa Kanali Mstaafu, Edmund Mjengwa. Daraja hilo sasa limeoza. Halipitiki. Ahadi nyingi zimetolewa kulijenga upya. Zimebaki kuwa ahadi. Ni daraja muhimu kiuchumi na kijamii kwa watu wa Nyeregete na wengine wengi wenye kulitumia. Ni kero kubwa kwa wananchi wa Nyeregete. 
Nimeongea na baadhi ya viongozi wa Nyeregete. Na nimewaambia, kuwa tushirikiane kuhakikisha, kuwa mwaka 2013 daraja hizo linajengwa hata kama ni kwa nguvu za wananchi. Tayari tumeshafanya utafiti na kuona inawezekana likajengwa kwa kiwango cha zege na chini ya shilingi milioni 20. 
Hivyo basi, mwaka 2013 nitashirikiana na wananchi wa Nyeregete na wengine wote watakaokuwa tayari kusaidia kuhakikisha tunapitisha harambee ya kujenga daraja hilo. Miaka 30 baada ya mimi kuvuka Lihamile kwa kuogelea itakuwa ni aibu kubwa kuwaona tena wananchi wa Nyeregete na wengine wakivuka korongo hilo kwa kuogelea. Ni nini basi maana ya kwenda shule?
 Ndugu zangu, 
Maji ni kero kubwa kwa wananchi wengi wa Bonde la Usangu, Mbarali Mbeya. 
Badala tu ya kuilalamikia na kuisubiri Serikali iwasaidie wananchi kutatua kero ya maji, mwaka 2013 nimeazimia nitashirikiana na wanakijiji wa vijiji vya Magwalisi na Lihamile wilayani Mbarali ili tuweze kuchangisha fedha za kuchimba visima vya pampu kimoja katika kila kijiji husika. 
Nitashiriki kuchangisha sehemu ya fedha zinazohitajika kugharamia visima hivyo kwa kupanda Mlima Kilimanjaro, kitu ambacho nimependa nikifanye katika maisha yangu lakini sijapata bahati ya kufanya. 
Ndugu zangu, 
Hayo ni mawili makubwa niliyotaka kuyasema kupitia salamu za mwaka mpya wa 2013. 
Ni matumaini yangu, Desemba 31, 2013 Mungu atanijalia uhai na kurudi tena hapa kutoa tena salamu za mwaka mpya huku hayo mawili yakiwa tayari yameshafanyiwa kazi kwa nguvu za pamoja, ikiwamo ushirikiano wenu. Nawatakia Heri na Fanaka Za Mwaka Mpya wa 2013. 
Maggid Mjengwa, 
 Morogoro
 0788 111 765Ndugu zangu,

0788 111 765

Posted On Monday, 31 December 2012 21:53
528470 4592618566257 1000354567 n fdea8
 
Pichani ni leo alasiri.
 
Posted On Monday, 31 December 2012 21:52

06 99466

Ndugu zangu, 
Imekuwa ni utamaduni wangu kutuma salamu za Mwaka Mpya kwa wanakijiji wa Mjengwablog, marafiki zangu kwenye FB na wengine walio ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

 Nimefanya hivyo tangu mwaka 2006 ilipoanzishwa Mjengwablog. Na mwaka huu naendeleza utamaduni huo. Nina mambo makubwa mawili kwenye salamu za mwaka huu, lakini, nitaanza salamu hizi kwa kukumbushua ahadi muhimu ya Mwana –TANU; kwamba;  ” Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa manufaa ya wote”.  Ndugu zangu, 

Posted On Monday, 31 December 2012 21:24
 Na : Nuzulack DausenJESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametoroka.Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977.“Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:

Posted On Monday, 31 December 2012 21:23

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli