We have 179 guests and no members online

Simu

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amesifu juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.

Posted On Saturday, 02 December 2017 13:27

Waziri Mkuu  Kassimu Majaliwa, amesema kuna haja ya kuangalia upya mfumo wa elimu ya juu nchini, ili kuuboresha uweze kusaidia kutayarisha haraka rasilimali watu walioelimika  zaidi, watakaoliwezesha  taifa kuwa na maendeleo na kufikia uchumi wa kati,ifikapo mwaka 2025.

Posted On Saturday, 02 December 2017 13:26

Wanaume nchini wamesisitizwa kuwa kipaumbele katika kupima Maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) ili kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na vita dhidi ya maambukizo ya ukimwi.

Posted On Saturday, 02 December 2017 13:22

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati),  Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke (wa pili kulia), Mwakilishi wa masuala ya Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China Bw. Lin Zhiyong (wa pili kushoto) pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya pande hizo kuhusu Biashara, uwekezaji na ushirikiano, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Posted On Friday, 01 December 2017 03:40

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina sambamba na kuchukulia hatua kali za kisheria, kwa watakao bainika kuhusika na uvunjifu wa haki za binadamu katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa marudio wa Novemba 26, 2017 uliofanyika katika kata 43.

Posted On Friday, 01 December 2017 03:38

Zikiwa zimebaki siku mbili tu kufanyika kwa mbio za Kigamboni Marathon kwa mwaka 2017, tayari viongozi mbalimbali wa mashirika na taasisi za Kiserikali na binafsi wamethibitisha kushiriki mbio hizo ambazo pia zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka na kisha mbio hizo kufanyika hiyo Desemba 2, katika viunga vya Mji wa Kigamboni.

Posted On Friday, 01 December 2017 03:36

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umepata hati safi katika taarifa ya hesabu zake za fedha katika kipindi cha mwaka 2015-2016 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.Katika taarifa hiyo mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 (mwaka wa kwanza tangu kuaza kufanya kazi zake), thamani ya Mfuko ilifikia shilingi bilioni 65.68 na mfanikio haya yaliweza kufikiwa kutokana na ubunifu na ushirikiano mkubwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko na Bodi ya Udhamini, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Mfuko huo, Bw.Bezil Kwala, aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko huo unaoingia siku yake ya pili na  a mwisho kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha, wakati akiwasilisha taarifa hiyo ya fedha leo Novemba 30, 2017. 

Posted On Friday, 01 December 2017 03:32

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Coca Cola Afrika Mashariki Bw. Ahmed Rady. Tukio hilo limefanyika  ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Posted On Friday, 01 December 2017 03:29

media

Wanajeshi wa Sudan Kusini

Posted On Thursday, 30 November 2017 06:13

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe aliongoza kikao cha wadau kujadili mradi wa maji katika halmashauri za Mkoa wa Simiyu. Tayari tahmini ya mazingira imekamilika na kazi ya upembuzi yakinifu ipo katika hatua za mwisho na zabuni imepangwa kutangazwa mwezi Januari 2018 baada ya kukamilika kwa zabuni, Ujenzi wa Mradi unakadiriwa kuchukua miezi 24.

Posted On Thursday, 30 November 2017 06:11

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 5000 kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na nyumba za askari katika eneo la Matevesi ambapo kuna mradi wa Safari City umbali wa kilomita 12 kutoka katikati ya mji wa Arusha.

Posted On Thursday, 30 November 2017 06:09

Image result for PROF. LIPUMBA

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Mwenyekiti wa Chama cha CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake, katika kesi ya RITA kuhusu Bodi ya Wadhamini.

Posted On Thursday, 30 November 2017 06:02

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kumkamata Wakala wa Kampuni ya Wallmark anayefahamika kwa jina la Samwel pamoja na Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Bahman kutoka Kampuni ya NAS, kwa kosa la kutaka kutoa Bandarini magari makubwa 44 aina ya Semi tela bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Posted On Thursday, 30 November 2017 06:00

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Novemba, 2017 amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Posted On Thursday, 30 November 2017 05:56
Page 4 of 2084

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart