We have 126 guests and no members online

Simu

Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Posted On Saturday, 12 August 2017 14:09

Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki akizungumza katika mkutano na wananchi katika kata ya Mabilioni wilayani Same.

Posted On Saturday, 12 August 2017 14:06

Image may contain: 1 person, standing, bicycle and outdoor

Image may contain: 2 people, outdoor

Image may contain: 1 person, bicycle, plant and outdoor

 

Ndugu zangu,

Ah! Julius Nyerere naye aliendesha baiskeli ya Swala. Ya Mwenyekiti wenu ni Swala pia, ingawa imechakaa kidogo!

Ndio, Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Hakuwa na makuu. Viongozi wake walimuiga pia, na raia nao.

Mwalimu alitembea kwa miguu, alipanda baiskeli, na hapo pichani akiwa Mafia, alipanda Land Rover ya Halmashauri.

Na duniani hapa hakuna miujiza katika kuyafikia mafanikio. Hakuna njia za mkato pia. Ni sharti tufanye kazi kwa bidii. Tusiwe ni watu wenye kutanguliza tamaa na hata kuwadhulumu wengine.

Tuyaishi maisha ya kadiri. Ni kwa kuyafanya yale yaliyo ndani ya uwezo wetu.

Maana, ni wachache duniani walioweza kufanya miujiza kama tunayoambiwa kwenye vitabu vya dini; Bwana Yesu yu miongoni mwa wachache hao. Tunasoma, kuwa Mafalisayo walimshangaa Yesu na mafanikio yake. Wakatamka;

“ Hivi ni Yesu huyu huyu mwana wa Joseph fundi Seremala!”

Naam, mwanadamu usitazame tu alipofikia sasa mwanadamu mwenzako kwenye safari yake. Jitahidi uangalie mwanzo wa safari yake. Alikotokea. Ndipo hapo utayapata ya kujifunza.

Ona mfano huu, Papa Francis wa Kanisa Katoliki amefikia kiwango cha juu cha mafanikio kwenye ngazi ya kanisa. Ni rahisi kumwangalia hapo alipo, lakini ni muhimu kuiangalia safari yake ilipoanzia.

Tunasoma leo, kuwa Papa Francis ni mtu wa kadiri. Muda wote wa uhai wake amejitahidi kuishi maisha ya kadiri. Papa si mtu wa makuu. Na kule Vatican wanashangazwa hata na mavazi yake yasio gharama kubwa, ikiwamo viatu pia.

Hapa kwetu Tanzania Julius Nyerere ni mfano wa viongozi walioishi maisha ya kadiri.

Ndio maana ya kusema, kuwa Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Ni mfano wa kuigwa.

Naam, kajitulize kwako kasuku...!

Tutakukumbuka.
https://www.youtube.com/watch?v=58aDscENUp4

Maggid Mjengwa,
Iringa

Posted On Saturday, 12 August 2017 11:29

Image may contain: one or more people and text-Je, kama mheshimiwa angekuwa mwanamme ingekuwa habari?
- Nilishangaa Mheshimiwa huyu hakwenda Mahakamani kulishtaki gazeti na kudai fidia ya kuingiliwa faragha yake.

Wajumbe mna maoni gani?

Jambo hili lilitokea mwaka 2013.

Tafadhali, tusijadili kwa kutaja majina ya wahusika. 

Maggid, 

Iringa.
 
 
Posted On Saturday, 12 August 2017 11:26

Image may contain: text

Kwa taarifa zaidi na kujiandikisha, tembelea..http://tzdiaspora.org/

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:43

media

Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto baada ya kupokea vyeti vya ushindi Agosti 11 2017

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:39

media

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anapongza uamuzi wa Vladimir Putin kuisaidia Marekani kuokoa fedha ilizokua ikitumia kwa afisi zake nchini Urusi.

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:38

Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela akifanya mahojiano na mwandishi wa kituo cha Televisheni cha ITV, Henry Mabumo mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha Kitabu “Women Creating Wealth” wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwaendeleza Wanawake Afrika (WAA) iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo linasimamiwa na Taasisi ya Graca Machel.(Picha zote na Thebeauty.co.tz)

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:33

ch1

Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete leo amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la Chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya Bagamoyo. Hapa picha mbalimbali zikionyesha Mbunge huyo akigawa vifaa vya michezo kwa viongozi mbalimbali wa vilabu vya mpira katika jimbo hilo.

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:32

 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC (left) accompanied by Tanzania’s High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro and Ambassador Celestine Mushy, Director of  Multilateral Cooperation in the Ministry of Foreign Affairs and Regional Affairs head to the plane ready to take off  for their one day trip of  Zanzibar

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:29

DSC_4497

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na  Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima na Uongozi wa Sirika la Bima  Zanzibar  katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji wa Sirika hilo , [Picha na Ikulu.] 11 /08/2017.

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:28

DG9TAeSXgAABjK-

Posted On Saturday, 12 August 2017 05:26

Image may contain: one or more people and people sitting

Image may contain: 1 person, smiling, standing

 

Ndugu zangu,

Pichani ni Msanii Mrisho Mpoto. Kulia ni msanii Manju Msita na Dada Mija Sayi. Ni mmoja wa bloga maarufu wa enzi hizo.

Mrisho tulifahamiana miaka mingi kabla hajawa na umaarufu. Siku hiyo pichani tulikuwa pamoja kwenye harusi ya Manju Msita na Dada Mija Sayi. Ni mwaka 2009. Na hapo picha ya kwanza tukiwa kanisani. Bila shaka hapo Mrisho anatafakari juu ya tungo zake!

Ni moja ya harusi ninayoikumbuka. Ilifana sana. Ilikuwa na utofauti kwa kila kitu.

Mrisho Mpoto aliposimama ukumbini kughani shairi, wengi walimshangaa. Hakukuwa na mazoea ya watu kughani shairi harusini.

Alipomaliza Mrisho alirudi nyuma ya jukwaa. Kule nikaenda kumpongeza. Aliponiona alianza kucheka sana. Akajiangusha sakafuni akiendelea kucheka!

Kicheko kinaambukiza, nami nikaanza kucheka! Sikufikia kujiangusha chini maana sikujua hasa Mrisho alikuwa anacheka nini, bali alinichekesha kwa jinsi alivyokuwa akicheka!

Maggid,

Iringa.

Posted On Friday, 11 August 2017 20:05

Image may contain: 6 people, people smiling, people sitting and indoorPichani tukiwa na rafiki yetu Mary Kisinga na binti zake, Tracy na Diana. Mary anafanya kazina Umoja wa Mataifa, Damascus.
PS: Kwa Mwenyekiti hakuna ukame wa majani ya chai, atakaye aje!
Maggid,
Iringa.

Posted On Friday, 11 August 2017 20:03

Image may contain: 1 personNdugu zangu, 

Tume ya Uchaguzi Kenya imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa Urais.

Nitumie fursa hii kumpongeza Uhuru Kenyatta na Wananchi wa Kenya kwa kufanya uchaguzi kwa amani na kuwa watulivu mpaka kutangazwa kwa matokeo. Ni ushindi kwa Wakenya wote.

Nini tafsiri ya ushindi wa Uhuru Kenyatta?

Tafsiri moja kuu ni kuwa Wananchi wa Kenya wameamua. 

Ni imani ya wengi wetu, kuwa Raila Odinga atakayakubali matokeo haya ili kupisha maisha ya kisiasa yaendelee na ujenzi wa Kenya uendelee.

Kwetu watu wa Afrika Mashariki kila nchi ina umuhimu katika umoja wetu. Uchaguzi umepita, na sasa mataifa yetu haya na viongozi wake wazingatie kudumisha udugu wetu na waangalie mbele kwa manufaa ya watu wa Afrika Mashariki. 

Hongera Uhuru Kenyatta!

Maggid, 

Iringa.

Posted On Friday, 11 August 2017 19:55
Page 5 of 2023

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart