We have 310 guests and no members online

Bongo Hapo Zamani: Rais Wa Jamhuri Hakuwa Na Makuu..!

Posted On Saturday, 12 August 2017 11:29 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: 1 person, standing, bicycle and outdoor

Image may contain: 2 people, outdoor

Image may contain: 1 person, bicycle, plant and outdoor

 

Ndugu zangu,

Ah! Julius Nyerere naye aliendesha baiskeli ya Swala. Ya Mwenyekiti wenu ni Swala pia, ingawa imechakaa kidogo!

Ndio, Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Hakuwa na makuu. Viongozi wake walimuiga pia, na raia nao.

Mwalimu alitembea kwa miguu, alipanda baiskeli, na hapo pichani akiwa Mafia, alipanda Land Rover ya Halmashauri.

Na duniani hapa hakuna miujiza katika kuyafikia mafanikio. Hakuna njia za mkato pia. Ni sharti tufanye kazi kwa bidii. Tusiwe ni watu wenye kutanguliza tamaa na hata kuwadhulumu wengine.

Tuyaishi maisha ya kadiri. Ni kwa kuyafanya yale yaliyo ndani ya uwezo wetu.

Maana, ni wachache duniani walioweza kufanya miujiza kama tunayoambiwa kwenye vitabu vya dini; Bwana Yesu yu miongoni mwa wachache hao. Tunasoma, kuwa Mafalisayo walimshangaa Yesu na mafanikio yake. Wakatamka;

“ Hivi ni Yesu huyu huyu mwana wa Joseph fundi Seremala!”

Naam, mwanadamu usitazame tu alipofikia sasa mwanadamu mwenzako kwenye safari yake. Jitahidi uangalie mwanzo wa safari yake. Alikotokea. Ndipo hapo utayapata ya kujifunza.

Ona mfano huu, Papa Francis wa Kanisa Katoliki amefikia kiwango cha juu cha mafanikio kwenye ngazi ya kanisa. Ni rahisi kumwangalia hapo alipo, lakini ni muhimu kuiangalia safari yake ilipoanzia.

Tunasoma leo, kuwa Papa Francis ni mtu wa kadiri. Muda wote wa uhai wake amejitahidi kuishi maisha ya kadiri. Papa si mtu wa makuu. Na kule Vatican wanashangazwa hata na mavazi yake yasio gharama kubwa, ikiwamo viatu pia.

Hapa kwetu Tanzania Julius Nyerere ni mfano wa viongozi walioishi maisha ya kadiri.

Ndio maana ya kusema, kuwa Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Ni mfano wa kuigwa.

Naam, kajitulize kwako kasuku...!

Tutakukumbuka.
https://www.youtube.com/watch?v=58aDscENUp4

Maggid Mjengwa,
Iringa

Read 47 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji