We have 75 guests and no members online

Bongo Hapo Zamani: Balozi Victoria Richard Mwakasege..

Posted On Saturday, 12 August 2017 19:44 Written by
Rate this item
(0 votes)

No automatic alt text available.

 Ndugu zangu, 

Nilikutana mara ya kwanza na Victoria Mwakasege akiwa Afisa wa Ubalozi kijana kwenye Ubalozi wetu, Stockholm, Sweden. Ni mwaka 1994.

Victoria alionekana tangu hapo, akiwa na malengo ya kufika mbali kama mwanadiplomasia. Hakuwa mrasimu, muda wote alikuwa tayari kushirikiana na Watanzania wa diaspora lakini alikuwa kiungo muhimu kwa Serikali yetu na nchi ya Sweden. 

Victoria alikubali na kuhudhuria mialiko mingi ya jumuiya ya Watanzania Sweden lakini hata jumuiya za watu wa Sweden wenye mashirikiano na Tanzania, mfano wa jumuiya hii ni SVETAN ikiwa na maana ya SWEDEN NA TANZANIA.

Victoria alipata uelewa mkubwa wa nchi za Scandinavia. Baadae alihamishiwa Maputo. 

Mara ya mwisho kukutana nae ni mwaka 2016 akiwa Kaimu Balozi wetu Burundi. Niliweza pia kufanya mahojiano naye kwenye kipindi cha ' Nyumbani Na Diaspora'. 

Pembeni, Victoria aliweza kunipa elimu kubwa juu ya mgogoro wa Burundi na jinsi nchi yetu ilivyo na ushawishi mkubwa kwenye nchi za Maziwa Makuu. 

Mara ya mwisho Victoria alikuwa Balozi wetu Malawi. 

( Picha hii ni ya 1994, Stockholm, Sweden. Iko kwenye maktaba ya mjengwablog.com)

Maggid , 

Iringa.

Read 78 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli