We have 71 guests and no members online

Tatizo La Ben...!

Posted On Saturday, 12 August 2017 20:01 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: one or more people, eyeglasses and closeupNdugu zangu, 

Nimesoma mahali juzi , kuwa Kiongozi wa Chama cha siasa ametaka Rais aliye madarakani sasa aombewe asiwe na maneno makali.

Imenikumbusha Ben Mkapa. Huenda ni ukweli, kuwa Watanzania huwa hawapendi kuambiwa kwa maneno makali hata kama wanachoambiwa ni ukweli. 

Tofauti ya viongozi aina ya Jakaya Kikwete na Mzee Mwinyi, Mkapa huwa hawezi kurembaremba maneno. 

Ben Mkapa ni mwanadiplomasia, lakini, wakati mwingine diplomasia yake ni ya Ki-gun boat fulani. Ni ile ya kutanguliza makombora kumtisha aliye mbele yake...na Mkapa mwenyewe akibanwa anaweza kuwa mkali kama mbogo.

Akihojiwa na Tim Sebastian kwenye ' Hard Talk' 2001 kuhusiana na machafuko ya Zanzibar, Mkapa hakupenda maswali ya Tim ( Huenda aliona ni ya kipumbavu!).

Nilimwona kwenye tv Mkapa akionyesha hasira, na Tim Sebastian akamuuliza;

" Mr President, are you angry?"
Ben Mkapa akajibu; 
" Yes, I am" huku akizidi kuonyesha amekasirika...

Mjadala uendelee..

Read 69 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli