We have 343 guests and no members online

×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

Related image

Chanzo, VOA Swahili.

Tarehe 4 mwezi Ferbuari  ni siku ya saratani duniani ambapo kila mwaka inatoa fursa ya kuongeza uwelevu wa saratani na kushawishi njia za kuizuia, kuitambua na matibabu. Katika eneo la utambuzi, watafiti katika chuo kikuu cha Johns Hopkins kwenye kitengo cha Kimmel Cancer kilichopo Baltimore, Maryland wamefanya utafiti wa upimaji damu ambao unasaidia kutambua aina nane tofauti za saratani. Saratani ni ugonjwa wa pili wa juu unaosababisha kifo duniani kote, na watu wengi hawatambui kuwa wana maradhi hayo mpaka pale dalili zinapojitokeza. Hili linaweza kubadilika kwa kupima damu ambayo hujulikana kama CancerSEEK.

Posted On Monday, 05 February 2018 07:12

Tokeo la picha la KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA CHUO CHA MUHIMBILI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii jinsia na watoto, Dk Mpoki Ulisubisya, amefanya ziara kwenye Chuo Kikuu cha Tiba ya Afya Shirikishi, Muhimbili University of Health Allied Science (MUHAS) ambapo mbali na mambo mengine, amezungumzia kuhusu mikakati ya serikali katika kuongeza wataalamu wa afya ili kuboresha huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hospitali nyingine nchi nzima.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 10:05

Tunayofuraha kuwataarifu wana Dudumizi na jamii kwa ujumla kuwa, baada ya kukaa jikoni kwa muda mrefu, tunatarajia kuzindua programu yetu ya mauzo, inayojulikana kama Michongo App.  Application hii ya Michongo inakuwezesha kuuza na kununua bidhaa mbalimbali zilizopo kwenye punguzo.

 Michongo inajitofautisha na programu nyingi za mauzo ya online kwa sababu kuu zifuatao;

1. Michongo inauza bidhaakwa bei ambayo hauwezi kuipata sokoni. Inamaana, Michongo imeshabageni bei kwa ajili yako.

2. Michongo inatumia programu rafiki ya Affiliate kuwezesha watu kuingiza kipato kwa kila linki wanayosambaza kwa marafiki zao na rafiki akanunua bidhaa. Hii inamaanisha, Michongo ni agent wa timu ya sales itakayokufanyia kazi. Kwa mtindo huu, unaweza kupunguza gharama za kutangaza biashara yako hadi nusu kwa sababu hakuna gharama yoyote kwa kutangaza kwenye Michongo, pia kuna mamilioni ya watu watakuwa busy kusambaza link za bidhaa yako. Hii itawawezesha wajasiriamali wadogo wengi kuingia sokoni na kutengeneza ajira zaidi na zaidi, kama malengo ya Rais wetu (kuongeza ajira).

Posted On Tuesday, 20 September 2016 05:34

Uhusiano kati ya Tanzania ni moja kati ya mahusiano ya muda mrefu, mahusiano haya yameanza tangu enzi  za Baba wa Taifa na wakati huo wachina hawakuwa na nguvu au uwezo mkubwa kama walivyo sasa. Mahusiano haya yamedumu kwa miongo bila kutetereka. Na kwa wachina huwa wanatuita, marafiki wazuri (好朋友). Tumekuwa tukishirikiana na China kiuchumi, kijamii, kiulinzi na kadha wakadha.

 Katika miaka ya karibuni, nchi ya China imekuwa ikiendelea kwa kasi na hatimaye hata kuwa nchi ya pili kwa uchumi duniani. Ukuaji huu wa Uchumi umepelekea China kujitanua zaidi kibiashara. Leo hii, bidhaa nyingi muhimu ama zinatoka China ama zimetengenezwa China. Pia, makampuni mengi ya kichina yamekuwa yakimiminika Tanzania kutafuta nafasi za kibiashara.

 Katika dunia ya leo, Website ni eneo muhimu na la lazima kwa wafanya biashara makini. Website iliyotengenezwa kwa kuzingatia tamaduni na tabia mtandao za eneo husika ndiyo itakayopelekea matokeo thabiti. Na Dudumizi ikiwa kampuni ya wazawa, imeamua kujikita kwenye kuhakikisha inawawezesha wafanya biashara wa kichina waliopo Tanzania kupata Website zilizotengenezwa kutumika na jamii husika.

Katika kufanikisha ufanyaji biashara kati ya nchi mbili, sasa Website ya Dudumizi itapatikana katika lugha ya Kichina. Timu ya Dudumizi ina wataalamu wenye uelewa wa kina juu ya lugha, teknolojia na tamaduni za Kichina kuwezesha kuwa chaguo sahihi kwa biashara yako. Mlengwa mkuu ni Kampuni za Kichina zinazotaka kuwafikia wazawa na kampuni za wazawa zinazotaka kuwafikia wachiina. Dudumizi inaweza kuwa nyenzo thabiti kufikia malengo yako.

Kupata Website yako, bofya hapa

Posted On Thursday, 28 April 2016 11:23

Matumizi ya email za kampuni (Corporate Business Email Address) ni moja ya njia rahisi kabisa ya kutangaza biashara yako kwa wateja. Mfano, miaka sita iliyopita nilinunua mashine ya kutotolesha vifaranga kutoka China na mawasiliano mengi tulifanya kwa kutumia email. Juzi mmoja wa watu wangu wa karibu alitaka kununua machine, alitumiwa quotation nyingi tu, aliponionesha,kulikuwa na emails 13. Kati ya hizo, 3 zilikuwa zenye domain za kampuni 2 Yahoo 5 Gamil 3 QQ. Kupitia email hizo,niiliweza kubaini moja wapo ya hizi email zilizotumia domain za kampuni (Corporate Business Email Address) ni wale walionuzia mashine ambayo inatumika hadi leo. Hivyo, ilikuwa rahisi kwangu kuwabaini na kupelekea kumshauri afanye nao kazi.

Kitu ambacho nilikuwa ninajiuliza sana, inawezekana vipi mtu akatuma taarifa za kampuni kwa kutumia email za gmail? Utamuhakikishia vipi mteja kama anadili na kampuni na si mtu binafsi (mfanyakazi wa ndani ya kampuni aliyeamua kuifanya hiyo kazi mwenyewe)?

Matumizi ya emails za bure siyo tu yanakuondolea uthamani (Value), bali kunaweza kukukimbizia wateja wengi. Pia, kumbuka kuwa, si lazima uwe na website ili uwe na email ya kampuni. Unachotakiwa ni kuwa na jina la website na ukanunua bando la email. Dudumizi tunayo huduma ya email kwa kampuni (Business Emails).Huduma hizi zote zinapatikana kwenye website yetu ya Hosting https://Dudumizi.net

Posted On Monday, 18 April 2016 10:11

Tayari umeshamaliza kusajili kampuni Brela na sasa unajiandaa kukamilisha taratibu za kupata TIN kutoka TRA na hatimaye leseni ya biashara ili kuanza rasmi biashara yako. Umeshikwa na shauku kubwa kusubiria siku kuu ambayo utakata keki kuashiria ufunguaji rasmi wa biashara yako. Lakini, Dudumizi inapenda kukukumbusha kuna kitu umekisahau kwenye orodha ya shughuli za kufanya, nacho ni usajili wa .co.tz domain.

Kumbuka, si lazima uwe na Website ndiyo usajili Domain, usajili wa domain unatakiwa kufanyika mapema ili kulinda jina lako hata kama haujaanza kulitumia. Sajili domain hapa.

Historia ya majina ya Website:

Kabla ya mwaka 1984 ambayo University of Wisconsin technicians walitengeneza seva za majina ya website(Name Server), hakukuwa na majina ya Website, watu walitumia namba tu, mfano, kama unataka kutembelea Website ya Dudumizi, ulitakiwa kuandika https://198.207.55.196. Hebu fikiria tungekwa tunaiandikaje kwenye Business card?

Mwaka 1985, majina ya Website kwa kutumia .com, .net na .org yalianza kutumika na watu kuanza kuachana na namba. Kwa kulitambua hilo, kwa tanzania, mchakato ulianza mwaka 1995 na hatimaye, TCRA iliuna tzNIC kama msimamizi mkuu wa .tz domaiin, na hatimaye, mwaka 2009, tzNIC ilianza rasmi kumanage majina ya .tz domain kupitia kwa mawakala wake, Dudumizi ikiwa mmoja wao.

Ingawa wapo watu wenye shauku ya kumiliki domain ya .co.tz lakini, kuna maswali au utata unaozunguka kichwani, hivyo, makala hii itasaidia kutatua maswali yanayoweza kujitokeza kuhusu .tz domain.

Posted On Friday, 01 April 2016 12:17

Moja ya vitu ambayo wengi wetu tumekuwa tukidhani ni kuwa, Website ikishatengenezwa, basi itaishi milele bila kufanyiwa mabadiliko yoyote ya kimfumo. Katika dunia ya leo, Website ni moja kati ya nyenzo thabiti kwa biashara. Hivyo, taarifa, muundo na hata sababu ya kuwa na Website inatakiwa iwe inaangaliwa na kuboreshwa kwa wakati.

Kwa mfano, kwa miaka ya hivi karibuni, tumeona jinsi matumizi ya simu za mkononi yalivyoongezeka, hivyo ni lazima ujiulize kama Website yako inao uwezo wa kuwahudumia wateja hawa wanaotumia simu kutembelea Website. Website ni lazima iende sambamba na mabadiliko hayo. Kitu cha kuzingatia ni kuwa, si lazima ubadili muonekano wa Website ili iweze kuendana na matakwa hayo.

 

Posted On Wednesday, 13 January 2016 13:12

Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya Dkt. Mohd Dahoma akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Wizara ya Afya juu tahadhari ya ukonjwa wa Kipindupindu hivyo amewashauri wananchi kununua chakula kilicho hifadhiwa vizuri ama chakula kimoto na kujiepusha kutumia juice zinazotengenezwa kienyeji. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar .

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya vyakula na vinywaji katika viwanja vya sikuu inayoanza kesho kutokana na tishio la maradhi ya kuharisha na kutapika ambayo yameanza kujitokeza katika nchi jirani.(VICTOR)

Posted On Thursday, 24 September 2015 08:49

Ile kaul iiliyowahi kutolewa miaka ya tisini na rais wa awamu ya pili ndugu Ally Hassan Mwinyi kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu sasa uwenda ikawa historia kwa taifa letu.

Ujasili huu nilionao wa kusema kuwa uwenda kauli hiyo itakuwa historia ni kutokana na kiwango kilicho onyeshwa na timu yetu ya taifa katika mechi ya kuwania kufuzu AFCON mwaka 2017 uko Gabon dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.

Kama ilivyo ada kabla ya mchezo huo kulikuwa na maneno ya hapana pale kutoka kwa wadau wa soka wa hapa nchini kwa kila mmoja kusema lake.

Wapo waliosema Stars itabeba kapu la magoli kutoka kwa Nigeria lakini wengine walisema Stars ina nafasi ya kusahihisha makosa yake ya awali.

Ikumbukwe katika mechi yake ya kwanza Stars ilicheza ugenini na kulazwa kwa bao 3-0 kutoka kwa Misri.

Posted On Wednesday, 09 September 2015 13:52

Kwa Mujibu wa Meneja Chapa ambaye pia ni Ambasador wa Mavazi Store bwana  Steve Seducter   mfumo huu wa kisasa umelenga  Kuondoa kero ya kutafuta bidhaa mbalimbali zinazohusiana na Urembo pamoja na Mavazi, pia kuwaokolea muda wateja  kwa kuunganisha  maduka Mengi zaidi kupitia tovuti hii ya www.mavazi.co.tz. Mtu yeyote mwenye simu ya kiganjani au kupitia katika kompyuta yake ataweza kutembelea Tovuti hii na kuona biashara zilizosajiliwa pamoja na Bidhaaa wanazouza. Hii itamuwezesha kuchagua  na kuwasiliana na duka husika Moja kwa moja alipo (Delivery).

Muonekano wa Tovuti ya MavaziStore  (www.mavazi.co.tz) Pamoja na mengine Mtafiti wa Masoko na ukuaji wa biashara Bwana Fred Crich  alifafanua kwamba  kwa Sasa ConnectMoja Technologies imejikita kusaidia ukuaji wa biashara mbalimbali za kitanzania, na kuhakikisha kwamba Maendeleo yanayotokea katika Dunia hasa kupitia teknolojia yanaipa Manufaa pia jamii yetu ya Kitanzania.

Crich ameongeza kwamba  Kwa Kampuni inatoa Ofa kwa wamiliki wa maduka kutangaza katika Tovuti hii Bure kwa Mwezi Mmoja  ili kuwafikia zaidi wateja walio wengi. Ili Kutangaza Nasi Tembelea  http://mavazi.co.tz/advertise/ au Wasiliana nasi kwa Simu   0777880007  au 0714215 600  : Office:  Oysterbay – Dar free Market Mall (GL14) Imetolewa na  Kitengo Cha Masoko – ConnectMoja Technologies Limited

www.connectmoja.co.tz   | info@connectmoja.co.tz

Posted On Tuesday, 08 September 2015 21:33

fastjet_2409696b

fastjet, the low-cost pan-African airline, has increased the number of flights on its growing international and domestic network from Dar es Salaam’s Julius Nyerere International Airport, Tanzania, in response to strong passenger demand.

fastjet now offers daily flights on its international routes from Dar es Salaam to Johannesburg, Harare and Lusaka, providing passengers with increased and more convenient travel options at affordable fares.

It has also doubled its flight frequency on the newly launched Dar es Salaam – Lilongwe route from two to four flights per week, which follows not long after the first flight took off between the two cities on 29 July 2015. fastjet’s Dar es Salaam and Kilimanjaro to Entebbe routes remain at three times weekly schedules.

Domestically, the airline will now offer up to five daily flights from Dar es Salaam to Mwanza, up to four daily flights linking Dar es Salaam and Kilimanjaro, two daily flights from Dar es Salaam to Mbeya, and daily flights between Kilimanjaro and Mwanza.

The new schedule will commence on 1 September 2015 for the Johannesburg flights and mid-September for all other flights from Dar es Salaam. Tickets for the additional flights are on sale already, with international fares starting from as little as US$50 one-way, and domestic fares for as little as US$20, excluding airport and government taxes.

“We have always promised to increase the frequency on our routes as and when our customers demand it,” says Richard Bodin, Chief Commercial Officer of fastjet. “The increased frequencies emphasize our commitment to growing our network across Africa, making air travel easy, safe and affordable.”

The increased flight schedule is made possible by the introduction of additional aircraft into the Tanzanian fleet later this month, making the fleet a total of four A319 aircraft.

“We really are thrilled at the positive reception that fastjet has enjoyed across Africa,” said Bodin. “With our low-cost fares, fastjet is making air travel more accessible than ever before, with many of our passengers being first time flyers who would otherwise not have been able to afford to travel by air.”

Posted On Tuesday, 08 September 2015 03:38

Ndugu zangu,
Hatupaswi kutenda tu yale nafsi zetu yanataka. Wakati mwingine tuwe na subira na kusikiliza wayatakayo wengine.
Kama leo nataka watu wanifuate kwa njia ya uhuru kabisa, na kwa maendeleo yao, basi, sipaswi kuwafukuza.
Nitaendelea kujitahidi kuandika maneno yenye kutujenga kwenye misingi ya kimaadili. Na wakati nwingine nayafanya yawe mafupi ili kujenga hamu ya kujua zaidi.
Kujenga kiu ya kusoma zaidi. Maana, naamini, kuwa vitabu vimebeba maarifa mengi ya dunia.
Tusome.
Ni Neno Fupi La Usiku.
Maggid.

Posted On Sunday, 06 September 2015 22:01
Page 1 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji