Kuna watembeleaji 313  wapo online

Mjengwa Blog

Mjengwa Blog

I am a writer, photographer, social entrepreneur, political analyst and a teacher- facilitator.

Website URL: http://www.mjengwablog.com

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), Hawa Ghasia jana aliongoza mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Moshi Chang'a yaliyofanyika katika makaburi ya Mtwivila, Kihesa Iringa.

Akizungumza katika mazishi hayo, Ghasia alisema Chang'a alikuwa mchapakazi na kuwa hata yalipofanyika mabadiliko ya maeneo ya kazi kutoka wilaya moja kwenda nyingine, hakuwahi kulalamika tofauti na ma-DC wengine.

Alitoa pole kwa familia ya marehemu, wananchi wa wilaya aliyokuwa akiiongoza kwa kuondokewa na mchapakazi huyo.

Ghasia aliwataka wananchi wakati wote kuwa tayari kwa kifo na kutenda mema kwa watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa na kidini, kama alivyokuwa Chang'a.(Martha Magessa)

TUKO KWENYE MASHINDANO (J M)

askofu-gervas-nyaisonga_039a6.jpg

Askofu wa  Katoliki Jimbo la Dodoma Mhashamu Gervas Nyaisonga

 KANISA Katoliki leo wanaendesha ibada maalumu bungeni mjini Dodoma kuombea Bunge Maalumu la Katiba.

Ibada hiyo ya kuombea bunge maalumu inaongozwa na Askofu wa Jimbo la Dodoma, Gervas Nyaisonga katika kanisa lililopo bungeni.

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia Suluhu Hassan alitoa taarifa hiyo jana baada ya shughuli za bunge.

Aliwataka Wakristo kujitokeza kwenye ibada hiyo ya misa inayofanyika saa 7 mchana.(Martha Magessa)

CHANZO:HABARILEO

Takriban watu 63 wamefariki baada ya treni iliyokuwa imebeba abiria kupoteza mwelekeo Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Msemaji wa serikali Lambert Mende alisema kuwa polisi wanahofia kuwa idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka. Pia alisema kuwa polisi watafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali.

Ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la Kamina katika mkoa wenye utajiri wa madini wa Katanga.

Treni hiyo ilikuwa imebeba idadi kubwa ya watu kupindukia wengine wakiwa wameketi juu ya treni yenyewe.

Waziri wa mambo ya ndani katika mkoa huo Jean Marie Dikanga Kazadi, aliambia BBC kuwadereva wa treni hiyo alikuwa anaiendesha kwa kasi .

Watu 80 walijeruhiwa vibaya huku wengine saba wakiwa bado wamekwama ndani ya treni vifusi.

Treni ilianguka Jumanne asubuhi lakini waokozi waliweza tu kuwasili nyakati za jioni.

Sehemu kubwa ya njia ya reli ya DRC, imesalia katika hali yake tangu enzi za ukoloni na ni nadra kufanyiwa ukarabati.

Treni hiyo ilianguka wakati dereva alipokuwa anajaribu kupunguza kasi.

chanzo BBC

(J M)

 

20140423_072521_78c54.jpg

Barabara ya uhuru kuanzia katika shule ya Benjamini Mkapa mpaka Kariakoo kama inavyoonekana katika picha leo asubuhi kwani magari yanashindwa kupita kabisa na kuamua kupitia mtaa wa Agrey na kutokea  Mtaa wa Msimbazi. Picha na (Awadh Ibrahim)

Ndugu Zangu,

TUMEKUWA tukitamka; Ukistaajabia ya Mussa , utayaona ya Filauni! Si wengi wenye kuyajua ya Mussa ni yepi na ya Filauni pia.

Kuna simulizi niliyopata kuipokea. Kuwa alipata kutokea bwana mmoja. Yeye na mkewe walisubiri kwa miaka mingi kupata mtoto. Ikafika siku mkewe akatunga mimba. Na katikati ya kuilea mimba hiyo, bwana yule akapata safari. Naam, akasafiri kwenda mbali. Nyumbani kamwacha mkewe mjamzito.

Huku nyuma mke akapata maumivu. Mganga akamwambia; ili mimba isalimike, basi, ni sharti ale maini ya mbuzi, na afanye hivyo kila anapopata mimba.

Nyumbani hakukuwa na mbuzi wa kuchinja. Mama yule akaenda kwa ndugu wa mumewe mwenye zizi la mbuzi. Akamweleza shida yake.

Bwana yule mfuga mbuzi akakataa katakata. Kuwa hawezi kuchinja mbuzi wake kwa ajili ya kupata maini ya tiba tu. Mama mjamzito akarudi nyumbani akiwa mnyonge. Na mimba ile ikaharibika.

Mume aliporudi akasimuliwa na mkewe. Hakuamini masikio yake. Iweje nduguye amfanyie hivyo? Alijiuliza. Akafunga safari mpaka kwa Mussa, kwenda kuomba ushauri.

Alipofika kwa Mussa akasimulia kisa chake. Mussa alimsikiliza kwa makini. Na kwa vile aliombwa kutoa ushauri, basi, Mussa akamwambia; " Hayo yameshatokea, msamehe nduguyo!"

Bwana yule akaushangaa sana ushauri wa Mussa. Kwamba amsamehe tu mtu aliyesababisha mimba ya mkewe iharibike! Basi, akafunga safari hadi kwa Filauni , alikwenda huko kupata ushauri wake. Filauni naye akasikiliza kwa makini kisa chote.

Na kwa vile aliombwa kutoa ushauri, basi, akatamka; " E bwana ee, mimi naona umsamehe tu nduguyo!"

Bwana yule akaupinga ushauri ule. Akamtaka Filauni aje na ushauri ulio na busara zaidi. Basi, kwa vile Filauni aliombwa aje na ushauri tofauti na wa mwanzo, naye akatamka;

" Basi, mimi naona ni vema ukamkabidhi mkeo kwa nduguyo aliyekataa kumchinja mbuzi ili maini ya tiba yapatikane. Na akae na mkeo hadi atakapompa mimba. Na kwa vile mimba itakuwa ya kwake, basi, nduguyo atalazimika kumchinja mbuzi ili ipatikane tiba. Na mtoto akizaliwa, we nenda kamchukue mkeo na mtoto!"

Naam, ndio hayo ya kustaajabia ya Mussa na kuyaona ya Filauni! Na siye tuliokulia pwani mtu akikwambia; " Acha Ufilauni!" Basi, ujue amekasirika.

Ndio, na hata katika jamii yetu, na hususan kwenye fikra zetu, kuna mahali ambapo akina Mussa Na Filauni wamechangia katika kutufikisha tulipo sasa. Na hili nitalijadili zaidi huko twendako.

Maana, kama nilivyoandika jana, kuwa mara nyingi, kama wanadamu, makosa tuyafanyao hutokana na makosa ya wengine. Tunachofanya ni kuyarudia makosa.

Na je, unafanyaje pale kipofu anapokuvamia na kukusababishia maumivu makali? Jibu; Utakasirika kwa sababu ya maumivu uliyoyapata. Hiyo ni hali ya kibinadamu.

Lakini, ukiamua kulipiza kisasi, kwa wewe kujitoboa macho na kumvamia kipofu, basi, hapo utakuwa umetenda lisilo na busara. Na hilo ni Neno la Leo.Tafakari!

Maggid Mjengwa.
Iringa.(P.T)

Je ni lazima mwanamke anayekwenda kujiburudisha katika kibanda cha kuvutia Shisha aambatane na mwanamume ambaye ni maharamu wake au jamaa wake ambaye hawezi kumuoa awe mlinzi wake?

Majadala huu umekuwa ukigonga vichwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Saidi Arabia.

Mjadala ulianza baada ya picha ya mkahawa mmoja kuwekwa kwenye Twitter.

Mkahawa huo unawaruhusu tu wanawake walioambatana na mlinzi kuingia ndani na kuvuta Shisha.

Bila mlinzi wako basi huwezi kuruhusiwa kuingia kwenye kibanda hicho.

Msichana akivuta shisha hahitaji ulinzi,'' amesema mkereketwa mmoja

Shisha, ambayo pia inaitwa Hookah, huvutwa na wanaume sawa na wanawake katika nchi za kiarabu.

Ni mrija ulio kwenye kifaa kirefu hivi ambacho hutumiwa kuvuta Tumbaku ambayo imewekwa ladha ya matunda na huvutwa hasa na watu wanapojiburudisha. (J M)

kp22042014 bdfe1

Hudugu Ng'amilo.

warioba f9d5b

Na Hudugu Ng'amilo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameuliza maswali saba ya msingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.

Jaji Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba.

Akizungumza kwa ukali, Jaji Warioba alisema: "Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?

"Sheria inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha Muungano."

Katika swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa Serikali ya Muungano ya sasa siyo ya Muungano, ni ya Tanganyika.

Katika swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi ambao waliieleza tume hiyo kuwa Katiba imevunjwa na madaraka ya rais yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.

"Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba katika swali lake la nne.

Katika swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikali tatu kwa sababu yeye pamoja na (Joseph Butiku) walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.

Pia, aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake wanageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Katika swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

Alisema badala ya kujadili hoja za msingi, wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu (akiwamo na yeye), kitendo ambacho alisema si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi.

Katika uzinduzi huo walikuwepo baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ambao ni Dk Hamisi Kigwangalla aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Julius Mtatiro, Maria Sarungi na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole.

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Dudumizi

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

Maoni ya Wanakijiji

Zilizosomwa Zaidi

BLOG SHABIHANA