We have 277 guests and no members online

Mjengwa Blog

Mjengwa Blog

I am a writer, photographer, social entrepreneur, political analyst and a teacher- facilitator.

Website URL: http://www.mjengwablog.com

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo. Anayeshuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mapango

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/2017-2020/2021 unalenga kuboresha maisha ya Watanzania wengi kwa kuhakikisha Sekta zinazoajiri watu wengi na walio masikini zinakuwa kwa kasi. 

Akizindua Mpango huo leo (Jumanne, Juni 7, 2016) katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itahakikisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Uvuvi na Mifugo zinakua kwa kasi ya kuridhisha ili kuongeza fursa za ajira na kupunguza umasikini. Amesema utekelezaji wa Mpango huo ambao umefungamanisha maendeleo ya viwanda na maendeleo ya watu na unatazamiwa kujibu changamoto ya umasikini Tanzania. 

Waziri Mkuu amesema katika Mpango huo kuna maeneo mbalimbali ya vipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango huo ni miradi mikubwa kama ya chuma cha Liganga, kufufua shirika la Ndege, Makaa ya Mawe Mchuchuma, ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha standard Gauge ambayo matokeo yake yanatarajiwa kuwa kichocheo cha utekelezaji wa miradi mingine. 

“Tunatarajia ifikapo mwaka 2025 tuwe tumejenga nchi ambayo ina maisha bora, yenye amani, umoja na utawala bora, jamii inayojifunza na iliyoelimika, yenye uwezo wa kuzalisha na kuwa na ukuaji wa uchumi endelevu na wenye ushindani,” amesema. 

Waziri Mkuu Majaliwa amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ukuaji huo wa uchumi unakuwa shirikishi zaidi katika utekelezaji wa Mpango huu na kwamba uendelezaji wa viwanda ndio utakaoleta mafanikio makubwa karika mwelekeo huo. 

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema jumla ya viwanda 39 kati ya 106 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambavyo vilikuwa vya vinazalisha bidhaa za chuma, ngozi, korosho zana za kilimo, sabuni na mafuta ya kupikia wamevifunga na kutoviendeleza. 

Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kwa Msajili wa Hazina itaendelea na zoezi la kuvirejesha viwanda hivyo Serikalini ili waangalie utaratibu mwingine ulio bora wa kuviendeleza kwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo. 

Amesema Mpango huo ambao utajikita zaidi katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na vile vilivyobinafsishwa ili kuongeza fursa za ajira na kipato kwa wananchi wengi. 

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano ambao utahitimishwa Juni 30, 2016 Serikali ilifanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara za lami na madaraja ya Kigamboni, Maligisu Nagoo, Mbutu na Ruhekei. Pia ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542), ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi katika maeneo ya Madimba na Songosongo, ujenzi wa vituo vya kupokelea gesi vya Somanga-Fungu na Kinyerezi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati akizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango kitabu cha mpango huo.(P.T)

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa (Nduli), Bi.Hanna Kibupile akitoa taarifa ya utendaji wa kiwanja hicho kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara alipokikagua.

Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Mkoani Iringa Bw. Haji Musa Usantu akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipokagua Mamlaka hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Mwenye Kofia) akitazama moja ya kifaa kinachopima hali ya hewa ya udongo alipokagua kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa.Kulia ni Meneja wa (TMA) Mkoani humo Bw. Haji Musa Usantu.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa (Nduli), Bi. Hanna Kibupile alipokikagua.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (katikati) huku Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa (Nduli), Bi. Hanna Kibupile alifuatilia.(P.T)

Waimbaji wa Abba

Wanachama wanne wa bendi ya Abba wameonekana wakiwa pamoja nchini Sweden na kuwashangaza mashabiki kwa kuimba pamoja.

Nyota hao walikusanyika siku ya Jumapili katika warsha moja ya kibinafsi, kuadhimisha ushirikiano wa miaka 50 kati ya watunzi wa nyimbo Bjorn Ulvaeus na Benny Andersson.

Wakati wa warsha hiyo, Agnetha Faltskog na Anni-Frid Lyngstad waliimba wimbo "The Way Old Friends Do".

Baadaye Ulvaeus na Andersson walijiunga nao wakati walipokaribia kumaliza wimbo huo na kuwa ndiyo mara ya kwanza bendi hiyo kukutana na kuimba tangu miaka 30 iliyopita.

Wakati ilishuhudia mafanikio makubwa, bendi hiyo iliponea kuvunjika kwa ndoa kati ya Ulvaeus na Faltskog pamoja na Lyngstad na Andersson.BBC

Mtaalamu wa Teknolojia ya mtambo unaotoa chumvi na baadhi ya madini yasiyotakiwa kwenye maji Ronny Graul kutoka Kampuni ya TRUNZ ya Uswisi akikinga maji yaliyokwisha chujwa kutoka katika moja ya mitambo ya kisasa inayotumika kusafishia maji, wanaomtazama ni baadhi ya wataalamu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji waliohudhuria mafunzo ya matumizi ya mtambo huo yaliyofanyika Juni 6,2016 Jijini Dar es Salaam.

Mtaalamu wa Teknolojia ya mtambo unaotoa chumvi na baadhi ya madini yasiyotakiwa kwenye maji Ronny Graul kutoka Kampuni ya TRUNZ ya Uswisi akionyesha jinsi mtambo huo unavyofanya kazi, wanaomtazama ni baadhi ya wataalamu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji waliohudhuria mafunzo ya matumizi ya mtambo huo yaliyofanyika Juni 6,2016 Jijini Dar es Salaam.

Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imepewa mafunzo na Kampuni ya TRUNZ kutoka Uswisi juu ya mitambo inayosafisha maji yenye chumvi na madini yasiyotakiwa katika maji ili kusaidia ongezeko la upatikanaji wa maji safi na salama nchini.

Mafunzo hayo yametolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Teknolojia kutoka katika Kampuni hiyo, Ronny Graul ambaye ameelezea na kuonyesha jinsi mitambo hiyo inavyosafisha maji yenye chumvi au madini yasiyotakiwa hadi kuwa safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

“Mitambo hii inatumia nguvu ya jua na umeme kidogo sana lakini inafanya kazi kubwa ya kusafisha maji yenye chumvi na madini ambayo hayahitajiki katika maji yakiwemo madini ya floride, chuma,zinki, shaba pamoja na naitreti na kuyaacha maji yakiwa safi na salama katika viwango vinavyohitajika na Shirika la Afya Duniani (WHO)”,alisema Graul.

Mtaalamu huyo ameongeza kuwa mitambo hiyo inapatikana kiurahisi na ina uwezo mkubwa wa kusafisha maji hasa kwa maeneo yenye visima vya maji yenye chumvi pamoja na madini yasiyotakiwa ambapo kwa Tanzania maeneo yaliyokithiri kwa kuwa na maji yenye chumvi nyingi ni Mtwara,Singida, Dar es Salaam na Pwani.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Maji Mjini wa wizara hiyo, Muhandisi Mary Mbowe alisema kuwa lengo la Wizara kuomba mafunzo hayo ni kufahamu namna gani mitambo hiyo inavyofanya kazi ili kama itakidhi vigezo iweze kununuliwa na kupelekwa katika maeneo sugu yenye maji ya chumvi hivyo, kusaidia Watanzania wengi kupata maji safi na salama.

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi wa Ubora wa Maji Philip Chacha pamoja na wataalamu wengine wa ubora wa maji kutoka wizarani hapo wamesema kuwa wamejidhihirisha kwa ubora wa mitambo hiyo na jinsi ilivyo na uwezo mkubwa wa kusafisha maji kwa kwa muda mfupi hivyo, itaweza kuokoa maisha ya Watanzania hasa waishio vijijini kwani wataepuka magonjwa yanayosababishwa na maji yasiyo safi na salama.

Mitambo hiyo imeundwa na mitambo miwili inayofanya kazi kwa pamoja ambapo mtambo wa kwanza unajulikana kwa jina la AQUIFIER 200 unaotumika kuondoa chumvi na madini yasiyotakiwa katika maji na mtambo wa pili unaitwa SURVIVOR 300 ambao unachuja maji na kuyaacha yakiwa safi na salama kwa kunywa bila kuchemsha wala kutia dawa ya kusafishia.(P.T)

nec

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani Kobwey wakikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 12 kwa Rais John Magufuli.

Fedha hizo zimeokolewa katika fedha zilizopangwa kutumika na Tume ya Uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015.(P.T)

????????????????????????????????????

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni wakifanya ishara ya uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula na (kulia) ni Mkurugenzi wa VETA, Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko.

????????????????????????????????????

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni wakifanya ishara ya uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana.

????????????????????????????????????

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mkuu wa Chuo cha VETA – Kipawa, Mhandisi Lucius Luteganya, Mkurugenzi wa VETA, Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni na Mkurugenzi Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula.

·         Mfumo wa kwanza wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao Tanzania

·         Kuleta ufarahisi na gharama nafuu

·         Mafunzo kupatikana kupitia application maalum

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA  imeshirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kuanzisha application mpya ijulikanayo kama “VSOMO”  yaani VETA SOMO, ili kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia simu za mkononi . Kuanzishwa kwa VSOMO itasaidia kupanua wigo wa mpango wa Airtel FURSA na kuwafikia vijana wengi zaidi nchini.(P.T)

Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Wanakijiji

BLOG SHABIHANA