We have 172 guests and no members online

BUGU

Katibu  wa Bunge ambaye pia ni msimamizi wa Uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Thomas Kashililah  akizungumza na wawakilishi mbalimbali wa Vyama vya Siasa kuhusu uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashiriki. Wa kwanza kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Posted On Monday, 20 March 2017 16:11

IMG_1744

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amevitaka vyama vya Siasa nchini kuhakikisha kuwa Katiba na Kanuni za Vyama vya Siasa zinaheshimiwa na kufuatwa katika utendaji wa kila siku wa chama cha siasa ili kuepuka migogoro na migongano ndani ya vyama. Hayo ameyabainisha kwenye barua yenye Kumb. Na. HA.322/362/01/103 aliyoiandikia vyama vya siasa mapema jana.

“Nimeona ni vyema nitumie fursa hii kuviasa Vyama vya Siasa kuhusu hali hii, kwani hali hii ya kufanya mambo kiholela pasipo kufuata Katiba na Kanuni kama itaachwa iendelee hivi ndani ya vyama kwa hakika italeta migogoro na mipasuko mikubwa ndani ya Vyama vya Siasa husika”

“Wakati huu ambapo nchi yetu inasubiri marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, nimeandikiwa barua na pia kupata nakala za barua kutoka kwa baadhi ya Vyama vya Siasa kuhusu migongano ya wanachama na viongozi au viongozi wenyewe kwa wenyewe kuhusu suala la kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar,“ alisema Jaji Mutungi.

Barua hiyo ilibainisha kuwa suala hilo la migongano limejitokeza pia kwa wingi kwenye Vyombo vya Habari, ambapo wanachama na viongozi au viongozi wenyewe kwa wenyewe wametofautiana na kupingana hadharani.

Jaji Mutungi amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 3(1) ya kanuni za Usajili wa Vyama vya Siasa za mwaka 1992 (GN.No. 111) Vyama vya Siasa vinaposajiliwa vinapaswa kuwasilisha Katiba na Kanuni zake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

“Ikumbukwe kwamba, suala la msingi hapa ni kwamba,sharti la kuwepo kwa Katiba na Kanuni katika chama, kimsingi ni mwendelezo wa kukuza na kudumisha dhana ya kuendesha Vyama kitaasisi kulingana na mwongozo uliokubalika na kuasisiwa kichama kwa mfumo wa Katiba na Kanuni za chama na si kuendesha chama kiholela kama inavyoelekea kuota mizizi kwa baadhi ya Vyama vya Siasa hivi sasa.”ameongeza Jaji Mutungi

Jaji Mutungi amevisihi Vyama vyote vya Siasa, kuhakikisha kwamba matamko ya chama hususan yahusuyo msimamo wa chama kuhusu jambo zito la kisera, kitaifa n.k., mathalan kama lilivyo la uchaguzi huu wa Zanzibar basi yatolewe rasmi na mtu mwenye mamlaka ya kuongea kwa niaba ya chama. Na endapo kuna mwananchama au kiongozi ambaye ataenda kinyume achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo na chama husika kwa kuzingatia katiba na kanuni zake ili kuepusha sitofahamu inayokuwa imejitokeza katika jamii.

“Ni vyema misimamo kama hiyo ya chama itokane pia na vikao halali vya chama na siyo matakwa ya kiongozi mmoja au mwanachama mmoja au wachache. Vinginevyo kama tutapeleka na kufanya uendeshaji wa vyama kiholela tutachangia kuwachanganya wananchi na kupoteza kabisa imani na heshima ya Jamii iliyokuwa imeanza kujengeka kwa Vyama vya Siasa,” amesisitiza Jaji Mutungi

Aidha vyama vvya Siasa vimeaswa kuchua hatua ya haraka iwezekanavyo kwa mwanachama au kiongozi wa chama anayefanya mawasiliano ama kutoa matamko bila idhini ya mamlaka na pia vyama vimeonywa kutowajengea wananchi tashwira ya kwamba kuna makundi yanagombania madaraka na kuendeleza maslahi binafsi kwa sababu jambo hilo linashusha hadhi ya vyama vya Siasa nchini.(P.T)

Posted On Wednesday, 17 February 2016 04:23

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amejiuzulu wadhifa huo . Bwana Fabius ambae pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Rais wa Baraza la Katiba la Ufaransa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius

Maafisa wa serikali nchini Ufaransa wamethibitisha leo kwamba Waziri Fabius amejiuzulu wadhifa wake na kwa maana hiyo ameamua kujiondoa kwenye siasa za mstari wa mbele baada ya kuwamo katika medani hiyo kwa miaka zaidi ya 30.

Bwana Fabius alionekana akiwapungia watu wakati alipokuwa anatoka kuhuduhuruia kikao chake cha mwisho cha baraza la mawaziri leo asubuhi. Mwenyewe amethibitisha kwamba amejiuzulu wadhifa wake, hatua itakayosababisha kufanyika mabadiliko ya baraza la mawaziri baadae mnamo wiki hii.(VICTOR)

Posted On Wednesday, 10 February 2016 22:18

Trump

Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Bernie Sanders wamepata ushindi katika mchujo wa jimbo la New Hampshire.

Seneta wa Vermont Bernie Sanders, aliyemshinda Hillary Clinton, amesema ushindi wake unaonesha watu wanataka “mabadiliko kamili”.

Bw Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala.

Maafisa wa jimbo walikadiria kwamba watu wengi wangejitokeza kushiriki kura za mchujo huo wa New Hampshire.

Gavana wa Ohio John Kasich alimaliza wa pili katika chama cha Republican, mbele ya gavana wa Florida Jeb Bush, Texas Seneta Ted Cruz na Seneta wa Florida Marco Rubio wote ambao wanang’ang’ania nafasi ya tatu.(VICTOR)

Posted On Wednesday, 10 February 2016 12:34

IMGS2886

Rais Dkt. John Magufuli akisalimiana na Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CC, Abdulrahman Kinana (katikati baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida kuhudhuria sherehe za miaka 39 ya CCM Februari 6, 2016.

IMGS2901

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida kuhudhuria  sherehe za miaka 39 ya CCM Febbruari  6, 2016.

IMGS3157

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakya Kikwete na Rais John Magufuli wakiwa wamekalia moja kati ya madwati 1,000 yaliyotolewana CCM mkoa wa Singidaili yagawiwe kwa shule za mkoa huo ikiwa ni moja ya hatua za kutatua tatizo la madawati nchini. Walikuwa katika sherehe za miaka 39 ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6,2016. Watatu kushoto ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majliwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMGS2965 copy

Rais Joh Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Rachel Mashishanga ambaye alirejea CCM katika sherehe za Miaka 39 ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6, 2016.

IMGS2977

Rais John Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Viti Maalum CHADEMA , Cristawaja  Mtinda ambaye alitangaza kurejea CCM katika sherehe za miaka 39 ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6, 2016.(P.T)

Posted On Saturday, 06 February 2016 21:01

1

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi  Februari 6 mwaka huu kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mkoani humo, wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na mkuu wa wilaya ya Singida mjini Mh. Said Amanzi. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”

(PICHA NA JOHN BUKUKU – FULLSHANGWE-SINGIDA)

2

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi  Februari 6 mwaka huu mkoani humo, kushoto ni Mh. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

4

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na akina mama mbalimbali waliojitokeza kumpokea wakati alipowasili mjini Singida jana.

5

Akina mama na wana CCM mbalimbali wakiimba nyimbo za kumlaki Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili mkoani Singida jana. (P.T)

Posted On Thursday, 04 February 2016 04:09

Trump

Seneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa uchaguzi wa mgombea wa uchaguzi wa Republican katika jimbo la Iowa, Marekani.

Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.

Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa dalili zinaonyesha kwamba atakuwa wa pili.

Seneta wa Florida Marco Rubio anaonekana kufanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na huenda akamaliza nambari tatu.

Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.(VICTOR)

Posted On Tuesday, 02 February 2016 05:30

DW Reihe What America do you want Bernie Sanders' America

Wagombea wanaowania uteuzi wa vyama vya Republican na Democratic wamewahimiza wapiga kura wa jimbo la Iowa katika dakika za lala salama kabla kufanyika uchaguzi wa kwanza wa awali.

USA Wahlkampf Demokraten Präsidentschaftskandidaten TV-Debatte

Hillary Clinton (kushoto) na Bernie Sanders

Kufikia leo jioni wagombea wanaowania uteuzi wa vyama vya Republican na Democratic katika uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 2016 watajua kama muda wao, jitihada zao na fedha walizotumia katika kampeni zao zimefaulu kwa kuwavutia wapigaji kura wengi, jambo litakalozipa msukumo kampeni zao wakati kinyang'anyiro kitakapohamia jimbo la New Hampshire.

Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton wanaongoza katika kura za maoni lakini hawana idadi kubwa ya kutosha kuwahakikishia ushindi wa wazi katika uchaguzi wa awali wa vyama vyao hivi leo.

Je Marco Rubio wa Republican pengine ataungwa mkono na kukifanya kinyang'anyiro cha Warepulican kuwa cha watu watatu, yaani Donald Trump na mhafidhina Ted Cruz? Na je msoshalisti wa chama cha Democratic aliyejitangaza mwenyewe, Bernie Sanders, atafaulu kuyageuza mapinduzi yake ya kisiasa kuwa kura za kutosha kumpiku Hillary Clinton anayejaribu kushinda uteuzi wa chama kwa mara ya pili?

Kampeni za wagombea wote hawa zinakabiliwa na mtihani kwa mara ya kwanza - watu wazuri wa Iowa.(VICTOR)

Posted On Tuesday, 02 February 2016 05:20

mutungi

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe.Jaji Francis Mutungi ameviasa Vyama vya Siasa kushiriki chaguzi zinazotangazwa na tume za uchaguzi nchini ikiwemo uchaguzi wa Machi 20, mwaka 2016 uliotangzwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa kwa vyama hivyo leo na kusainiwa na Jaji Mutungi ilieleza kwamba, kimsingi Sheria ya Vyama Vya Siasa Sura ya 258 inasisitiza vyama vya siasa kushiriki katika chaguzi zote zinazotangazwa na tume za uchaguzi ili kufikia malengo yake ya kushika dola.

“Katika nchi kidemokrasia na kwa chama cha siasa kinachoamini misingi ya kidemorasia ya vyama vingi vya siasa, hakuna njia mbadala kwa chama cha siasa kufikia malengo yake zaidi ya kushiriki uchaguzi.

“Ni wajibu wa kila chama cha siasa nchini kama wakala wa kukuza demokrasia, utawala wa sheria na amani ya nchi, kuwa wa kwanza kutii matamko ya kisheria yanayotolewa na mamlaka husika . Kama kuna chama cha siasa hakiridhiki au kimekwazwa kwa njia moja au nyingine na suala lolote kuhusu masuala ya uchaguzi, njia stahiki na inayonyesha ukomavu wa kisiasa si kuhamasisha kugomea uchaguzi, bali ni vema kikafuata utaratibu uliowekwa katika sheria za uchaguzi,” alisema Jaji Mutungi.(VICTOR)

Posted On Tuesday, 26 January 2016 20:23


1. Magufuli ateua Makatibu Wakuu
Hii ni habari inayochukua nafasi ya kwanza kwa mujibu wa mtandao wa mjengwablog.com. Inahusu Serikali na utawala wa nchi. Baada ya kukamilisha zoezi la kuteua mawaziri wake, hatua hii ya pili ya kuteua Makatibu Wakuu nayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kutokana na umuhimu wake inapozungumziwa ufanisi katika utendaji wa shughuli za Serikali.
Kimsingi, kwa kiasi kikubwa Makatibu Wakuu ndio Serikali yenyewe. Nchi inaweza kwenda bila Mawaziri, lakini, ni vigumu kwa nchi kwenda bila Makatibu Wakuu.

Tumeona, Rais Magufuli amefanya uteuzi uliosheheni wachapa kazi. Na katika maeneo yenye kuhusiana na kupambana na uhalifu ikiwamo ujangili, Rais ameteua Makatibu Wakuu wenye weledi pia kwenye masuala ya kijeshi.
Ni safu ya Makatibu Wakuu yenye kuonyesha dhamira ya kusonga mbele kiuchumi. Angalizo ni kwa kutorudi kwenye mazoea ya baadhi ya wanasiasa kuingilia majukumu ya Makatibu Wakuu katika utendaji wa kazi zao. Wakati yawezekana Waziri au Naibu Waziri wake wakawa ni wenye majimbo, Katibu Mkuu hana jimbo. Jimbo lake ni Tanzania. Anapaswa kuelekeza rasilimali za nchi kwa kuangalia maslahi ya nchi na si ya mwanasiasa na jimbo lake la uchaguzi.

Hatua iliyobaki muhimu ni uteuzi wa Wakurugenzi wa Idara mbalimbali ikiwamo taasisi na mashirika ya umma. Katika wakati tulio nao, ingelikuwa vema tukayapa mgongo mazoea ya uteuzi, badala yake Serikali kuajiri Wakurugenzi kwa kutangaza nafasi za kazi. Na Katibu Mkuu wa Wizara hapa angepaswa kuwa mshiriki mkuu katika zoezi la kuchambua waombaji wenye sifa stahiki katika kujaza nafasi za Wakurugenzi na ambao kimsingi, ndio watakaomsaidia Katibu Mkuu katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

2.Kashfa yazikumba MCC, Symbion

Hii ni habari inayochukua nafasi ya pili kwa ukubwa. Wakati MCC inaweka masharti magumu kwa nchi masikini kama Tanzania katika kutoa misaada yake ya maendeleo, imeripotiwa, hata MCC na symbion nao wamo katika kashfa ya ndani katika utendaji wa kazi zao. 

 

3. Serikali lawamani kuchelewesha pembejeo
Imeripotiwa kutoka Nachingwea, kuwa wakati msimu wa kilimo umeshawadia, wakulima bado hawajapatiwa ruzuku ya pembejeo za kilimo ikiwamo mbolea. Tafsiri ya habari hii ni kuwa, kama hali hii ya Nachingwea iko mahali pengine nchini, basi, tusije tukashangaa itakapokuja habari kuwa wananchi Nachingwea na kwingineko wamekumbwa na njaa. Ni wakati wa Waziri Mwigulu Nchemba kufanya ziara ya ' kushtukiza' kwa wenye wajibu wa kuwafikishia wakulima pembejeo.

Posted On Thursday, 31 December 2015 06:18

Kaimu Mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma Ismail Jussa.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile.

Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Baada ya kuipitia taarifa ya CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo, CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya yafuatayo:

1. Taarifa yenyewe haionekani kama imeandaliwa na watu makini wala haioneshi kama walioitoa wanajua nini kilichopo. Hilo liko wazi kutokana na taarifa yenyewe kuwa na maudhui yanayopingana ambayo yamekuja kukorogwa zaidi na maelezo yaliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar mbele ya waandishi wa habari na kuoneshwa katika vituo kadhaa vya televisheni:

(a) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini papo hapo inaeleza kwamba kikao kimeridhia mazungumzo yanayoendelea Ikulu Zanzibar. Taarifa haisemi iwapo maamuzi ya vikao vya mazungumzo hayatakuwa na suala la kurudiwa uchaguzi, upi ni mwelekeo wa CCM.

(b) Taarifa inazungumzia uchaguzi wa marudio lakini papo hapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anasema CCM haina imani na Tume ya Uchaguzi iliyopo na kwa hivyo uchaguzi huo wa marudio lazima ufanyike chini ya Tume mpya. Baada ya hapo hasemi Tume iliyopo ambayo muda wa utumishi wa Makamishna wake unalindwa kikatiba itaondolewa vipi na Tume mpya itapatikana vipi.

(c) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini Katibu wa itikadi na Uenezi anasema hata usiporudiwa ndani ya siku 90, bado Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais.

Nukta hizi tatu ambazo haziwezi zote kusimama kwa pamoja bila ya kupingana moja dhidi ya nyingine zinaonesha tu ni kwa kiasi gani viongozi wa CCM Zanzibar wamepoteza mwelekeo na hawana uhakika wa nini kitatokea katika kuondokana na mgogoro huu wa kutengenezwa.

2. Taarifa ya CCM haiwasaidii wanachama wa CCM wala wananchi wa Zanzibar kwa kuwapa matumaini ya kumalizika kwa mgogoro wa kutengenezwa wa uchaguzi wa Zanzibar na badala yake inaonekana imelenga kuwachanganya zaidi wananchi kwa maelezo yanayopingana.

3. Taarifa inaonyesha ni jinsi gani CCM kilivyopoteza mvuto kwa kujiweka mbali na wananchi. Taarifa hiyo inapongeza eti kuwepo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakati wananchi wa Zanzibar, bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, siyo tu wanumia kutokana na sera mbovu za CCM lakini sasa wanazidi kuteketea na maisha yao kuwa magumu zaidi kutokana na fadhaa (tension) na taharuki iliyopo katika nchi kutokana na kutokuwepo kwa Serikali yenye ridhaa yao.

Harakati za maisha zimeathirika sana huku bidhaa vikiwemo vyakula vikipanda bei. Viongozi wa CCM hawaonekani kujali hali hii mradi wao yao yanawaendea. Tabia hii ya CCM kutowajali wananchi wanyonge wa nchi hii ndiyo iliyopelekea wananchi kukiadhibu chama hicho katika uchaguzi mkuu na kupelekea mgombea wake wa Urais wa Zanzibar na wagombea Uwakilishi kushindwa vibaya kwa tofauti ya zaidi ya kura 25,831.(P.T)

Posted On Tuesday, 29 December 2015 15:53


.. Wanaosema Zanzibar haina Rais hawayajui mazonge ya Zanzibar, Kama Ingelikuwa Hivyo, Hata Mie Mwenyekiti Wetu Nisingetia Mguu Zanzibar...

Ndugu zangu,

Na nimepata kuandika hapa, ni vema tukakumbushana, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri.

Wakati fulani mwaka 1984, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar walikutana pale Kisiwandui Imagechini ya Alhaj Aboud Jumbe, aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa JMT.

Ndani ya kikao kile walikuwamo wanasiasa wa aina ya Ramadhan Haji Fakhi, huyu alikuwa Waziri Kiongozi, alikuwamo pia Hamad Rashid, Hamis Shabaan Mloo, na Seif Sharif Hamad.

Wajumbe walizungumza jasho likiwatoka juu ya hali isiyo sawa kwenye Muungano yakiwemo madai kuwa Zanzibar haikuwa hata na fursa ya kukopa nje ya nchi kwa vile imo ndani ya Muungano.

Ikajengwa hoja ya Serikali Tatu. Wajumbe wote wakaafiki. Ikafika siku ya kuwasilisha hoja Dodoma.

Ajabu ya jambo lile, Julius Nyerere, alionekana kulijua hilo mapema sana. Alhaj Jumbe mkutanoni Dodoma akawa na wakati mgumu.

Wenzake wote akiwamo Seif Sharif Hamad waliikana hoja isipokuwa Ramadhan Haji Fakhi, Waziri Kiongozi.

Inasemwa, Julius Nyerere alimuuliza Ramadhan Haji Fakhi;
" Moja jumlisha moja ni ngapi?"
Jibu: " Tatu!"

Inasemwa pia, Julius Nyerere aliwachekesha wajumbe alipohoji ni shule gani aliyesoma Ramadhan Haji Fakhi yenye kufundisha hesabu kwa namna hiyo!

Hatma ya kikao kile cha Dodoma ni Alhaj Jumbe kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama ikiwamo kuachia Urais wa zanzibar. Ramadhan Haji Fakhi pia akunusurika, alikwenda na maji.

Ali Hassan Mwinyi akafanywa kuwa Rais wa Zanzibar na Seif Sharif Hamad akawa Waziri Kiongozi.

Mwaka mmoja na nusu baadae, mwaka 1985, Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano na akawa Rais kwa kuchaguliwa na Wananchi.

Inasemwa, kwa vile Ali Hassan Mwinyi alipata fursa hiyo, basi, Seif Sharif Hamad alitumaini angekuwa Rais wa Zanzibar.

Hapana, CCM ikamteua Idrissa Abdul Wakil kugombea nafasi ya Rais wa Zanzibar. Seif Sharif Hamad akawa ameukosa Urais na akafanywa kuwa Waziri Kiongozi. Kukawa na minong'ono ya Seif kulalamika chini chini.

Ikafika wakati kukawa na ' Hali ya Hewa ya kisiasa Iliyochafuka Visiwani'. Nilikuwa mwanafunzi pale Tambaza Sekondari. Ilinong'onwa mjini kuwa Rais wa Zanzibar, Abdul Wakil, kutokana na hali ya hewa kuchafuka, akawa anafanya kazi Unguja na anarudi kulala Dar es Salaam.

Siku moja wakati nikitoka shule na kupita maeneo ya Upanga kuelekea kituo cha mabasi cha Palm Beach, kwenye moja ya nyumba za eneo hilo, nikamwona kwa macho yangu Rais wa Zanzibar, Idrissa Abdul Wakil. Nikafahamu baadae, kuwa aliishi kwenye moja ya nyumba za eneo hilo.

Mwaka 1988, akina Seif Sharif Hamad , Hamad Rashid na wenzao, walitaka hoja ya Serikali Tatu ipelekwe tena Dodoma. Safari hii Idrissa Abdul Wakil aliipinga kutokana na uzoefu wa 1984.

Seif Sharif Hamad naye akaishia kupokonywa kadi yake ya uanachama CCM. Vuguvugu la mageuzi ya kisiasa duniani likaanza kwenye kipindi hicho. Lilitokea Ulaya Mashariki.

Ndipo akina Seif Sharif Hamad wakapata fursa ya kuanzisha KAMAHURU. Na baadae CUF ikaja pia. Na ndoto ya Seif Sharif Hamad ikabaki hai, ndoto ya siku moja kuwa Rais wa Visiwa vya Zanzibar.

Mwaka huu wa 2015, Seif Sharif Hamad amerusha tena karata yake. Anaweka rekodi, ya kuwa mgombea mkongwe kushinda wote, na mwenye uzoefu wa kugombea Urais kwa zaidi ya miaka 20. Kuna tunachojifunza.

Ndugu zangu Wajumbe,

Nimejaribu kukumbuka hayo. Nakaribisha maoni yenu pia...

Maggid,
Jambiani, Zanzibar.

MAONI YA WADAU KWENYE FB..

Lameck Mavipya · 3 mutual friends
Dah.....yataisha tu!
Like · Reply · 12 hrs
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · Friends with Ismail Jussa and 4 others
Haya tumeyaona na kuyatolea maoni siku nyingi.
Tulitaraji ungekikemea na kusikitishwa na yaliotokea ya ukwiukwaji wa katiba na Sheria ambayo yamesababisha haya leo. Unakwenda kutueleza ya miaka ya thamanini wakati haya ya leo ni makubwa kuliko haya.
U...See More
Like · Reply · 5 · 11 hrs
Abihud Greepherson
Abihud Greepherson · 13 mutual friends
Huyu majid ni mnazi wa ccm. Hoja zake nyingi ni za kinafiki
Like · Reply · 10 hrs
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · Friends with Freddy Macha and 4 others
Na yaangalie hayo uyaitayo mazonge ya Zanzibar yameanzia wapi?
Nitakuambia yalipoanzia, yalianza Tokea siku ya mtu yule ... Soma zaidi kwa kubofya hapo chini...

Posted On Sunday, 27 December 2015 02:51
Page 1 of 114

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart