We have 738 guests and no members online

Magazeti ya Leo

Matangazo Mapya

We provide the full IT solutions including web design, web development ...

Kilichomuua Deo Filikunjombe

Published in Jamii

Uchunguzi wa awali kuhusu ajali ya chopa iliyogharimu maisha ya aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wenzake watatu, unaonyesha ilitokana na hitilafu ya injini,

Katika ajali hiyo iliyotokea Oktoba 16 kwenye pori la Selous, mbali ya Filikunjombe, rubani wa chopa hiyo, Kapteni William Silaa na wengine wawili waliokuwamo ndani ya chombo hicho kilichokuwa na namba za usajili 5Y-DKK na namba za utengenezwaji 7027 Eucereuil, pia walifariki dunia.

Filikunjombe alikodi chopa hiyo kutoka kampuni ya ndege ya Sun Drew inayomilikiwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka na ilikuwa inafanyiwa ukarabati na kampuni ya Laid Loris.

Baada ya ajali hiyo Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa ushirikiano na Wizara ya Uchukuzi waliita timu ya wachunguzi wa ndege kutoka Ufaransa ambayo ilitua nchini Oktoba 20. Timu hiyo ya watu wanne ilijumuisha mtu mmoja kutoka kampuni ya Airbus Industries ya Marseilles ambao ni watengenezaji wa chopa hiyo; mtu mmoja kutoka kampuni ya Turbo Meca, waliotengeneza injini; na watu wawili kutoka BEA, kitengo cha uchunguzi wa ndege kutoka Serikali ya Ufaransa.

Timu hiyo ilibaini hitilafu hiyo, ikibainisha kuwa baada ya injini kufeli, chopa hiyo ilianza kushuka hadi ikaanguka na kulipuka. Sababu za kulipuka kwake zimetajwa na wachunguzi hao kuwa ni madumu matano ya mafuta ya ujazo wa lita 20 yaliyokuwa ndani ya chopa hiyo.

Mchunguzi Mkuu wa Ajali za Ndege wa Wizara ya Uchukuzi, Omar Mhina aliiambia Mwananchi kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa injini.

“Katika uchunguzi wa awali, tulichukua injini na kugundua kuwa ilipata hitilafu. Hiyo ndiyo lugha ya kwanza tunayoweza kusema wakati tukisubiri uchunguzi mwingine,” alisema Mhina katika mahojiano na Mwananchi.

Mhina alisema wameshaichukua injini kutoka pori hilo la Selous na kwamba wanatarajia kuipeleka kwa watengenezaji wake kwa ajili ya kufunguliwa na kujua kiini cha kufeli kwa injini hiyo.

Alisema waliwasiliana na wamiliki wa chopa hiyo nchini Kenya, lakini hawajapata ushirikiano wa kuridhisha mpaka sasa. Lakini Mwananchi ilizungumza na opereta mkuu wa chopa hiyo wa Kenya, na rubani wa kampuni ya Sun Drew, Kapteni Charles Wachira ambaye alisema TCAA hawajawasiliana na Mamlaka ya Anga ya Kenya (KCAA) kwa ajili ya uchunguzi wa ajali hiyo.

“Mimi ni kapteni wa ndege lakini siwezi kufanya lolote kama sijapata baraka kutoka TCAA na KCAA. Wao ndio walitakiwa wawasiliane kwanza kabla ya sisi Sun Drew kuchukua hatua zozote, ni suala baina ya serikali na serikali,” alisema Wachira.

Kapteni huyo amesema akipata ruhusa kutoka KCAA atakuja nchini kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha ajali ya chopa hiyo.

Read more...

2308960_UltraWide

MAKIPA
Joe Hart (Man City)

Gianluigi Buffon (Juventus)

Manuel Neuer (Bayern)

Denys Bokyo (Dnipro)

MABEKI
David Alaba (Bayern)

Jerome Boateng (Bayern)

Dani Alves (Barcelona)

Javier Mascherano (Barcelona)

Gerard Pique (Barcelona)

Giorgio Chiellini (Juventus)

Leonardo Bonucci (Juventus)

David Luiz (PSG)

Thiago Silva (PSG)

Diego Godin (Atletico Madrid)

Sergio Ramos (Real Madrid)

Ricardo Rodriguez (Wolfsburg)

VIUNGO
James Rodrigues (Real Madrid)

Paul Pogba (Juventus)

Claudio Marchisio(Juventus)

Arturo Vidal(Bayern)

Marco Verratti (PSG)

Hakan Calhanoglu (Bayer Leverkusen)

Andres Iniesta (Barcelona)

Kevin De Bruyne (Man City)

Ivan Rakitic (Barcelona)

Eden Hazard (Chelsea)

Grzegorz Krychowiak (Sevilla)

Yevhen Konoplyanka (Sevilla)

WASHAMBULIAJI
Sergio Aguero (Man City)

Alexis Sanchez (Arsenal)

Gareth Bale (Real Madrid)

Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Thomas Muller (Bayern)

Robert Lewandowski (Bayern Munich)

Lionel Messi (Barcelona)

Luis Suarez (Barcelona)

Neymar (Barcelona)

Zlatan Ibrahimovic (PSG)

Antoine Griezmann (Atletico Madrid)

Alvaro Morata (Juventus)

Majina ya wachezaji hayo yamejuisha vilabu 13 kutoka kwenye ligi 6 tofauti na wachezaji 12 kati ya hao 40 wamewahi kuwepo katika kikosi hicho cha mwaka kwa miaka iliyopita.

Upigaji wa kura unafanyika katika mtandao wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA na kura zinatarajiwa kupigwa hadi Januari, 5 mwaka 2016 na kikosi kutangazwa Januari 8.

KLABU BINGWA ULAYA: Matokeo

Published in Michezo

blj

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea hapo jana Jumanne kwa michezo 8 katika viwanja tofauti tofauti na haya ndiyo matokeo ya michezo hiyo

Ratiba ya michezo ya leo jumanne Novemba 24 katika ligi ya mabingwa Ulaya UEFA

GROUP: E

BATE Borisov 1 – 1 Bayer Leverkusen

Barcelona 6 – 1 Roma

GROUP: F

Arsenal 3 – 0 Dinamo Zagreb

Bayern Munich 4 – 0 Olympiakos

GROUP: G

Porto 0 – 2 Dynamo Kyiv

Maccabi Tel Aviv 0 – 4 Chelsea

GROUP: H

Zenit St. Petersburg 2 – 0 Valencia

Lyon 1 – 2 Gent

Ratiba ya michezo ya leo Jumatano katika ligi ya mabingwa Ulaya UEFA

GROUP: A

Shakhtar Donetsk – Real Madrid 22:45 EAT

Malmo – Paris Saint German 22:45 EAT

GROUP: B

Manchester United – PSV 22:45 EAT

CSKA Moscow – Wolfsburg 20:00 EAT

GROUP: C

Astana – Benfica 18:00 EAT

Atletico Madrid – Galatasaray 22:45 EAT

GROUP: D

Juventus – Manchester City 22:45 EAT

Borussia Moenchegladbach – Sevilla 22:45 EAT

IMG-20151125-WA0024

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akisalimiana na Papa Francis wakati alipowasili mapema leo Novemba 25 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

papa11

Papa Francis ameanza ziara yake Afrika kwa kuhimiza umoja, uwazi, kuwathamini vijana na kuyatunza mazingira.Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliwasili Nairobi mwendo wa saa kumi unusu jioni na kukaribishwa kwa shangwe na viongozi wa kisiasa na kidini uwanja wa ndege.Baada ya kuwasili, alielekea Ikulu ambako alipanda mti kisha kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kabla ya kutoa hotuba yake ya kwanza.Akimkaribisha kutoa hotuba, Rais Kenyatta, alieleza umuhimu wa ziara ya kiongozi huyo wa kidini, akimkumbusha kwamba kesho ni siku ya mapumziko na siku ya kitaifa ya maombi Kenya.

 

Aliposimama kuhutubu, Papa Francis alishukuru sana kwa alivyopokelewa kabla ya kuanza mara moja kusisitiza kuhusu umuhimu wa umoja na utangamano Afrika. Pia, alikariri umuhimu wa kuwa na uwazi na usawa akisema ndiyo njia bora ya kumaliza mizozo.Kadhalika, alisisitiza nafasi muhimu ya vijana kwa taifa.“Taifa lenu pia lina vijana wengi. Siki hizi nitakazokuwa hapa, nasubiri sana kukutana na wengi wao, kuzungumza nao na kuwapa matumaini katika ndoto zao za siku za usoni.” Alisema.“Vijana ndio rasilimali yenye thamani zaidi kwa taifa. Kuwalinda, kuwekeza katika vijana, na kuwasaidia, ndiyo njia bora zaidi ya kuhakikisha siku njema za usoni zenye kufuata busara na maadili ya kiroho ya wazee wetu, maadili ambayo ndiyo nguzo ya jamii.”

Read more...

Kwa wazazi tufahamu watoto wetu tunawatia moyo sana tunapochukua muda kuona wanayofanya hata kwenye michezo..
Maggid,
Iringa.(P.T)

Kwa wazazi tufahamu watoto wetu tunawatia moyo sana tunapochukua muda kuona wanayofanya hata kwenye michezo..
Maggid,
Iringa.(P.T)

Papa Francis awasili Kenya

Published in Jamii

Papa Francis ashuka kutoka kwenye ndege.

Alakiwa kwa shangwe na nderemo. Amsalimia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Papa Francis amewasili Kenya katika ziara yake ya kwanza ya kihistoria barani Afrika bara linalokabiliwa na changamoto za kiusalama. Mamilioni wanatarajiwa kuhudhuria misa Nairobi.(P.T)

Read more...

Kala Jeremiah sasa kuwa wa kimataifa

Published in Burudani

KALLAJEREMIAH1

Staa wa muziki wa hip hop nchini, Kala Jeremiah.

Sweetbert lukonge, Dar es Salaam
STAA wa muziki wa hip hop nchini, Kala Jeremiah, ameamua kupanua wigo wa muziki wake baada ya kuanza harakati za kuhakikisha anatusua kimataifa.

Hatua hiyo inatokana na changamoto nyingi ambazo amekuwa akikumbana nazo kutoka kwa mashabiki wake ambao wamekuwa wakimsisitiza kufanya hivyo.

Kala ambaye ni zao la Bongo Star Search (BSS) aliiambia Mikito Jumatano kuwa kabla ya mwaka huu kumalizika lazima aikate kiu hiyo kwa kutoa ngoma na kichupa kikali ambacho kitachezwa kwenye runinga za kimataifa.

“Hivi sasa nipo katika harakati za kutoa wimbo mpya utakaoambatana na video kali itakayokuwa na viwango vya kimataifa ili niweze kukata kiu ya mashabiki wangu.

“Kwa sasa siwezi kuweka wazi jina la ngoma hiyo ila nina matumaini kuwa utafanya vizuri, pia video yake nitaifanyia hapa hapa nchini kwa viwango vya kimataifa, namuomba Mungu anijalie uzima ili niweze kutimiza mapema ndoto yangu hiyo,” alisema Jeremiah ambaye alitambulishwa zaidi kupitia Ngoma ya Wimbo wa Taifa aliyofanya na Nakaaya.(P.T)

Oh! Oh!

Published in Jamii

Hapa Kazi Tu..!

Published in Jamii

Iringa, jana mchana.(P.T)

WANAHARAKATI WA TANZANIA WANATOA WITO KWA JAMII

Published in Jamii

  Eda Malick kutoka Tanzania Women and Children Welfare center akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

 Afande Christina Onyango, Afisa wa Polisi, mkoa wa kipolisi Ilala akielezea namna ambavyo dawati la jinsia wamejipanga kufikisha ujumbe wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.(P.T)

Read more...

Kipindupindu chapungua DAR

Published in Jamii

Na Jacquiline Mrisho- maelezo

Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam imepungua kufikia wagonjwa kumi na mbili (12) kwa mkoa mzima, huku wilaya ya Temeke ikiwa na wagonjwa saba,Kinondoni wagonjwa wanne na Ilala ikiwa na mgonjwa mmoja

Haya yamezungumzwa na Mratibu wa Magonjwa ya kuambukiza wa Jiji la Dar es salaam Bw. Alex Mkamba ofisini kwake leo akielezea jinsi gani mkoa umefanikisha kupambana na kipindupindu kwa kuzingatia usafi katika jiji.

Ameongeza kuwa katika kufanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu wametoa mafunzo juu ya mbinu shirikishi ya namna ya kujikinga na kipindupindu kwa watendaji wa mitaa na pia imewahimiza kukagua maeneo yao na kuwapa kibali cha kufunga maeneo ya biashara au maeneo yatoayo huduma za chakula yasiyozingatia usafi.

Akielezea kuhusu huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam mratibu huyo amesema jiji lina dawa za kutosha za kuhudumia wagojwa ipasavyo kwa kuwapatia huduma bora zaidi kuendana na kasi ya maambukizi yaliyopo.

“ hata leo Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa dawa za kusafishia maji (Water Guard) maboksi 45 kwa kila wilaya” Mkamba alifafanua.

Aidha alisema serikali imejipanga katika kudhibiti maambukizi mapya kwa kuwapima wagonjwa kabla na baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini na aliwashauri wananchi kubadili tabia kwa kuhakikisha usafi unafanyika pia kuchemsha maji na kuufanya usafi kuwa ni tabia yao ya kila siku.

Mpaka sasa jumla ya watu 55 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam.(P.T)

 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) , Jumanne Sajini baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya TAMISEMI jijini Dar es salaam kuzungumza na watumishi Novemba 24, 2015.

 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam kuzungumza na wafanyakazi Novemba 24, 2015.

 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam Novemba 24, 2015. 

 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es slaam baada ya kuzungumza nao Novemba 24, 2015.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)

Read more...

Mbunge kingu aeleza sababu ya kukataa posho za bunge

Published in Jamii

3.Elibariki Kingu akitoa ufafanuzi wa jambo mara baada ya kuulizwa maswali kutoka kwa wanahabari.

Elibariki Kingu akitoa ufafanuzi wa jambo mara baada ya kuulizwa maswali kutoka kwa wanahabari.

1. Kutoka kushoto ni aliyekuwa Mgombea wa Jimbo hilo la Singida Magharibi baada ya kushindwa kura za maoni na kumuunga mkono, Hamis Ngila, Elibariki Kingu na Gerard Lukas.

Kutoka kushoto ni Hamisi Ngila, aliyekuwa mpinzani wa Kingu katika kura za maoni ndani ya CCM, Elibariki Kingu na Gerard Lukas.

4.Elibariki akisoma taarifa yake aliyokuwa ameiandaa kwa wanahabari.

Elibariki akisoma taarifa yake aliyokuwa ameiandaa kwa wanahabari.

2.Wanahabri wakichukua tukio.

Wanahabari wakichukua tukio.

MBUNGE wa Singida Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu amesema sababu za kuandika barua kwa Katibu wa Bunge kusimamisha posho zake zote za vikao ’sitting allowance’ ni kutaka fedha hizo kupelekwa kwenye mfuko wa jimbo lake kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.(P.T)

Read more...

Tunisia: watu wasiopungua 14 wauawa katika mashambulizi

Published in Jamii

VIkosi vya usalama vya Tunisia, Machi 19 jijini Tunis.

Na RFI

Watu wasiopungua 14 wameuawa Jumanne hii Novemba 24 katika mlipuko dhidi ya basi la usalama wa rais katikati mwa mji wa Tunis, msemaji wa Ikulu ya rais amesema, akithibitisha kuwa ni "shambulizi ".

"Watu kumi na wanne wamepoteza maisha na 11 wamejeruhiwa" katika mlipuko ambao umetokea Jumanne hii alasiri karibu na moja ya meneo makuu ya mji mkuu, Moez Sinaoui, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Ninathibitisha mlipuko ndani ya basi la usalama wa rais kuwa ni shambulizi", ameongeza msemaji wa Ikulu ya rais nchini Tunisia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Walid Louguini, awali alibaini kwenye kanda ya kwanza ya runinga ya serikali kuwa watu 11 walipoteza maisha.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa la AFP ameweza kuona sehemu moja ya basi ikiteketea kwa moto karibu na mtaa wa Mohamed wa 5, karibu na eneo lililofungwa. Magari mengi ya wagonjwa, maafisa wa Zima moto na vikosi vya usalama walikua katika eneo la tukio, kwa mujibu wa chanzo hicho. Watu wengi machozi yalikua yakiwatiririka.

"Maafisa wengi ambao walikua ndani ya basi wamefariki", chanzo cha usalama kilio kwenye eneo la tukio kimesema.

Wizara ya mambo ndani haikuweza kutaja ni watu wa ngapi ambao walikua ndani ya basi hilo.

Tunisia ilikabiliwa na mashambulizi kadhaa ya kijihadi mwaka jana, ambapo mashambulizi mawili dhidi ya makavazi ya Bardo mjini Tunis mwezi Machi na dhidi ya hoteli moja karibu na mji wa Sousse mwishoni mwa mwezi Juni, yaliwaua watu 60.(P.T)

NATO yaikinga kifua Uturuki

Published in Jamii

Jumuia ya kujihami ya nchi za magharibi NATO imesema inasimama pamoja na Uturuki baada ya kuitungua ndege ya kivita ya Urusi.

Akizungumza baada ya mkutano wa dharura ulioitishwa na Uturuki, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema tathmini ya tukio hilo inaonyesha kuwa ndege ya kivita ya Urusi iliruka katika anga ya Uturuki.

Huku kukiwa na hali ya wasiwasi, Stoltenberge ametaka kuwepo na hali ya utulivu kutoka pande zote.

Amesema taarifa walizozipokea kutoka nchi washirika, zinaenda sambamba na maelezo ya Uturuki ya tukio hilo.

"Ushirikiano tulioupata kutoka kwa washirika mbalimbali kwa leo unathibitisha taarifa tuliyoipata kutoka Uturuki."

Hata hivyo, Moscow bado wanasisitiza kwamba, ndege hiyo ilikuwa katika anga ya Syria, na kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa anga ya Uturuki.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kila mtu sharti aheshimu haki ya nchi yake ya kulinda mipaka yake.

Rais Obama pia ameitetea haki ya Uturuki ya kulinda anga yake.

Kwa upande wake, msemaji wa jeshi la Urusi, Jenerali Sergey Rudskoi, amesema angalau rubani mmoja kati ya wawili wa ndege hiyo iliyoangushwa na Uturuki siku ya Jumanne amefariki kutokana na moto uliokuwepo chini baada ya kutoka katika ndege hiyo.

Mpaka sasa hakijulikani kilichomsibu rubani mwengine.BBC

Tumetoka Mbali: 'Old Boy': Nyeregete, 1988!

Published in Jamii

Pichani niko na Mwalimu Mkuu, Nyeregete Primary School, 1988!
Ni Marehemu Mwalimu Ngwandu, pichani katikati. Hakuwahi kunifundisha, isipokuwa tulikutana nilipokuwa likizo kijijini kwetu Nyeregete, Mbarali, Mbeya. Hivyo, kwa namna moja au nyingine alikuwa mwalimu wangu.
Maggid,
Iringa.(P.T)

Kibuyu...!

Published in Jamii

Angalizo; Wajumbe Mnaruhusiwa Kujadili Kibuyu Alichobeba Mwenyekiti, Lakini, Si Mwanadada Aliyesimama Na Mwenyekiti...!
Pichani ni kijijini kwetu Nyeregete.

Maggid,
Iringa.(P.T)

Sababu za uharibifu wa vivuko zatajwa

Published in Jamii

Na Jovina Bujulu

Uchafuzi wa mazingira katika vituo vya vivuko , utegaji wa nyavu katika njia za vivuko na kukauka kwa maji na kujaa mchanga kwenye njia za vivuko ni sababu zinazochangia kuharibika kwa vivuko nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Ukodishaji mitambo na Huduma za Vivuko kutoka wakala wa Ufundi wa umeme Tanzania Mhandisi Japhet Maselle.

Aidha, alitaja sababu za uharibifu wa vivuko hivyo kuwa ni pamoja na baadhi ya abiria kutofuata taratibu za vivuko na wananchi kutumia mitumbwi ambayo si salama kuvukia hasa maeneo ya magogoni Dar es salaam na Pangani Tanga .

“Utegaji wa nyavu husababisha kunasa kwenye mifumo ya kuendeshea vivuko, na takataka kuingia kwenye mitambo ya kuendeshea vivuko ambapo husababisha athari katika mitambo hiyo” alisema ndugu Maselle.

Katika kukabiliana na matatizo hayo, TAMESA imeendelea kutoa elimu kwa watu wanaochafua mazingira na maeneo ya vivuko kutangaza taratibu za vivuko ndani ya vivuko na kuboresha huduma za vivuko na kuongeza maeneo yenye uhitaji.

Wakala wa ufundi na Umeme Tanzania (TAMESA) ilianzishwa kwa sheria ya wakala namba 30 ya mwaka 1997 ikiwa na lengo la kutoa huduma katika Nyanja za uhandisi mitambo, umeme na uendeshaji wa vivuko .

Kwa sasa kuna vivuko 28 vinavyofanya kazi katika vituo 19 Nchini, baadhi ya vivuko hivyo ni Mv Msungwi,Mv sabasaba, Mv Sengerema,Mv mwanza, Mv ukara , Mv Nyerere na Mv Temesa.(P.T)

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu ambayo inaadhimishwa kwa kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

 

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa TACAIDS Dkt. Jerome Kamwela akiwaonesha waandishi wa Habari Bango lenye Takwimu za Hali ya Maambukizi ya VVU nchini Tanzania.

Wito umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba 1 ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Ameeleza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo za Utoaji wa Elimu ya Afya na Upimaji wa hiari wa VVU katika maeneo mbalimbali kote nchini kupitia vituo vitakavyowekwa, Kufungua kituo cha maarifa cha udhibiti UKIMWI eneo la Manyoni mkoani Singida ambayo ni njia kuu kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi za Jirani za Burundi na Rwanda.

Ameongeza kuwa Tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendesha mikutano ya kitaalam kuhusu UKIMWI, Zoezi la upimaji wa hiari wa VVU kwa wananchi, Kupokea tamko litakalotolewa na Baraza la Watu wanaoishi na VVU pamoja na Uzinduzi wa taarifa ya tathmini ya Sheria zinazotumika zinazohitaji kurekebishwa zinazozuia malengo ya sifuri 3.

Aidha Tume itapokea taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU duniani itakayotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuhusu dunia na mapambano dhidi ya VVU.

Dkt. Fatma amefafanua kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pamoja na mambo mengine atazindua Mfuko wa UKIMWI ambao utakuwa chachu ya kupunguza maambukizi ya VVU nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathmini kuhusu UKIMWI wa TACAIDS Dkt.Jerome Kamwela amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 kimepungua na kufikia asilimia 5.3 huku mikoa ya nyanda za juu kusini ya Njombe, Iringa na Mbeya ikiongoza kwa kuwa na maambukizi zaidi na mikoa ya Manyara, Tanga na Lindi ikiwa na maambukizi ya chini ya asilimia mbili.

Dkt. Kamwela amesema kuwa maambukizi ya VVU ni mengi hasa kwa kundi la watu wenye umri wa miaka 19-24 huku makundi ya wanaojidunga, wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, wanawake wanaofanya biashara ya ngono yakiendelea kuwa katika hatari ya kuathiriwa zaidi na maambukizi ya VVU.(P.T)

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

Maoni ya Wanakijiji

BLOG SHABIHANA