We have 244 guests and no members online

Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakutana na wadau wa Sekta ya Filamu kujadili kuhusu Sera ya Filamu

Posted On Tuesday, 21 February 2017 16:05 Written by
Rate this item
(0 votes)

NAP1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao

NAP2

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.

NAP3

Mtayarishaji na msambazaji wa filamu nchini Bibi. Rose Urio akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.

NAP4

Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitolea ufafanuzi maoni yaliyotolewa wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.

NAP5

Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.

NAP6

Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu wakisikiliza hoja zilizokua zikiendelea kutolewa wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.

NAP7

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wanne kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya filamu walioshiriki katika kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura, watano kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao

Picha na: Genofeva Matemu WHUSM

Read 441 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji